Chromium na Google Chrome hutumia kundi moja la sera. Tafadhali kumbuka kwamba hati hii inaweza kujumuisha sera ambazo zinalenga matoleo ambayo hayajatolewa (kwa mfano kipengele cha "Linalotumika kwenye' kinarejelea toleo la Google Chrome) ambalo halijatolewa na kwamba sera kama hizo zinaweza kubadilishwa au kuondolewa bila taarifa, na hakuna uhakika wowote kuhusu vipengele vyake vya usalama na faragha.
Sera hizi zinalenga kutumiwa hasa kwa kuweka mipangilio ya matukio ya Google Chrome ya ndani ya shirika lako. Matumizi ya sera hizi nje ya shirika lako (kwa mfano, katika programu inayosambazwa kwa umma) yanachukuliwa kuwa programu hasidi na yanaweza kuainishwa kama programu hasidi na Google na wauzaji wa kingavirusi.
Si lazima uweke mipangilio ya programu hizi kwa njia ya kawaida! Violezo vilivyo rahisi kutumia vya Windows, Mac na Linux vinaweza kupakuliwa kutoka https://www.chromium.org/administrators/policy-templates.
Njia inayopendekezwa ya kuweka mipangilio ya sera kwenye Windows ni kupitia GPO, ingawa kuweka sera kupitia usajili bado kunatumika kwa matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®.
| Jina la Sera | Maelezo |
| Google Cast | |
| EnableMediaRouter | Washa Google Cast |
| ShowCastIconInToolbar | Onyesha aikoni ya upau wa vidhibiti ya Google Cast |
| Hifadhi ya Google | |
| DriveDisabled | Huzima Hifadhi ya Google katika programu ya Faili za Google Chrome OS |
| DriveDisabledOverCellular | Zima huduma ya Hifadhi ya Google kupitia miunganisho ya mitandao ya simu katika programu ya Faili za Google Chrome OS |
| Kidhibiti cha nenosiri | |
| PasswordManagerEnabled | Washa kipengele cha kuhifadhi manenosiri kwenye kidhibiti cha nenosiri |
| Kitoaji chaguomsingi cha utafutaji | |
| DefaultSearchProviderEnabled | Wezesha kitoaji chaguomsingi cha utafutaji |
| DefaultSearchProviderName | Kitoaji chaguomsingi cha utafutaji |
| DefaultSearchProviderKeyword | Nenomsingi la mtoa huduma chaguomsingi wa utafutaji |
| DefaultSearchProviderSearchURL | Mtoaji wa utafutaji chaguomsingi wa URL ya utafutaji |
| DefaultSearchProviderSuggestURL | Mtoa huduma chaguomsingi wa utafutaji anapendekeza URL |
| DefaultSearchProviderIconURL | Aikoni ya mtoaji wa utafutaji chaguomsingi |
| DefaultSearchProviderEncodings | Usimbaji wa kitoaji chaguomsingi cha utafutaji |
| DefaultSearchProviderAlternateURLs | Orodha ya URL mbadala za mtoa huduma chaguomsingi wa utafutaji. |
| DefaultSearchProviderImageURL | Kigezo kinachotoa kipengele cha kutafuta kwa picha kwa mtoa huduma wa utafutaji chaguomsingi |
| DefaultSearchProviderNewTabURL | Mtoa huduma ya utafutaji chaguomsingi ya URL ya ukurasa wa kichupo kipya |
| DefaultSearchProviderSearchURLPostParams | Vigezo vya URL ya utafutaji inayotumia POST |
| DefaultSearchProviderSuggestURLPostParams | Vigezo vya URL ya kupendekeza inayotumia POST |
| DefaultSearchProviderImageURLPostParams | Vigezo vya URL ya picha inayotumia POST |
| Kuchapisha | |
| PrintingEnabled | Wezesha uchapishaji |
| CloudPrintProxyEnabled | Wezesha proksi ya Google Cloud Print |
| PrintingAllowedColorModes | Dhibiti hali ya uchapishaji wa rangi |
| PrintingAllowedDuplexModes | Dhibiti hali ya uchapishaji kwenye pande mbili |
| PrintingColorDefault | Hali chaguomsingi ya uchapishaji wa rangi |
| PrintingDuplexDefault | Hali chaguomsingi ya uchapishaji kwenye pande mbili |
| CloudPrintSubmitEnabled | Wezesha uwasilishaji wa nyaraka kwenye Google Cloud Print |
| DisablePrintPreview | Lemaza Uhakiki wa Uchapishaji |
| PrintHeaderFooter | Chapisha Vichwa na Vijachini |
| DefaultPrinterSelection | Sheria za kuchagua printa chaguomsingi |
| NativePrinters | Uchapishaji Asilia |
| NativePrintersBulkConfiguration | Faili za mipangilio ya printa ya biashara |
| NativePrintersBulkAccessMode | Sera ya kufikia mipangilio ya printa |
| NativePrintersBulkBlacklist | Printa za biashara zisizotumia sera |
| NativePrintersBulkWhitelist | Printa za biashara zinazotumia sera |
| DeviceNativePrinters | Faili za mipangilio ya printa ya biashara kwenye vifaa |
| DeviceNativePrintersAccessMode | Sera ya kufikia mipangilio ya printa za vifaa. |
| DeviceNativePrintersBlacklist | Printa za biashara zisizotumia sera |
| DeviceNativePrintersWhitelist | Printa za biashara zinazotumia sera |
| PrintPreviewUseSystemDefaultPrinter | Tumia Printa Chaguomsingi ya Mfumo kama Chaguomsingi |
| Kufungua kwa haraka | |
| QuickUnlockModeWhitelist | Mipangilio imeruhusu hali za kufungua haraka |
| QuickUnlockTimeout | Weka mara ambazo mtumiaji anatakiwa kuweka nenosiri ili atumie kipengele cha kufungua haraka. |
| PinUnlockMinimumLength | Weka kima cha chini cha urefu wa PIN ya skrini iliyofungwa |
| PinUnlockMaximumLength | Weka kima cha juu cha urefu wa PIN ya kufunga skrini |
| PinUnlockWeakPinsAllowed | Ruhusu watumiaji waweke PIN ambazo si thabiti zitumike kama PIN ya skrini iliyofungwa |
| Kufunguka, Ukurasa wa kwanza na ukurasa wa Kichupo Kipya | |
| ShowHomeButton | Onyesha kitufe cha Mwazo kwenye upauzana |
| HomepageLocation | Sanidi URL ya ukurasa wa kwanza |
| HomepageIsNewTabPage | Tumia Ukurasa Mpya wa Kichupo kama ukurasa wa kwanza |
| NewTabPageLocation | Weka URL ya ukurasa wa Kichupo Kipya |
| RestoreOnStartup | Kitendo kwa kuanza |
| RestoreOnStartupURLs | URL za kufunguliwa unapooanza |
| Kuripoti mtumiaji na kifaa | |
| ReportDeviceVersionInfo | Ripoti OS na toleo la programu dhibiti |
| ReportDeviceBootMode | Ripoti modi ya kuwasha kifaa |
| ReportDeviceUsers | Ripoti watumiaji wa kifaa |
| ReportDeviceActivityTimes | Ripoti muda wa shughuli za kifaa |
| ReportDeviceNetworkInterfaces | Ripoti violesura vya mtandao wa kifaa |
| ReportDeviceHardwareStatus | Ripoti hali ya maunzi |
| ReportDeviceSessionStatus | Ripoti taarifa kuhusu vipindi vya skrini nzima vinavyoendelea |
| ReportDeviceBoardStatus | Ripoti hali ya ubao |
| ReportDevicePowerStatus | Ripoti hali ya nishati |
| ReportDeviceStorageStatus | Ripoti hali ya hifadhi |
| ReportUploadFrequency | Idadi ya upakiaji wa ripoti ya hali ya kifaa |
| ReportArcStatusEnabled | Ripoti maelezo kuhusu hali ya Android |
| HeartbeatEnabled | Tuma vifurushi vya mtandao kwenye seva ya udhibiti ili kufuatilia hali ya mtandao |
| HeartbeatFrequency | Idadi ya kufuatilia vifurushi vya mtandao |
| LogUploadEnabled | Tuma kumbukumbu za mfumo kwenye seva ya udhibiti |
| DeviceMetricsReportingEnabled | Wezesha kuripoti kwa metriki |
| Kuwasha na kuzima | |
| DeviceLoginScreenPowerManagement | Udhibiti wa nishati kwenye skrini ya kuingia |
| UptimeLimit | Wekea kifaa vizuizi vya muda wa kuwaka kwa kuzima na kuwasha kiotomatiki |
| DeviceRebootOnShutdown | Uwashaji tena kiotomatiki baada ya kuzima kifaa |
| Legacy Browser Support | |
| AlternativeBrowserPath | Kivinjari mbadala cha kufunguka katika tovuti zilizowekewa mipangilio. |
| AlternativeBrowserParameters | Vipengee vya mstari wa amri kwenye kivinjari mbadala. |
| BrowserSwitcherChromePath | Njia ya kufikia Chrome kwa ajili ya kubadili kutoka kivinjari mbadala. |
| BrowserSwitcherChromeParameters | Vipengee vya mstari wa amri vya kubadili kutoka kivinjari mbadala. |
| BrowserSwitcherDelay | Chelewesha kabla ya kufungua katika kivinjari mbadala (milisekunde) |
| BrowserSwitcherEnabled | Washa kipengele cha Uwezo wa Kutumia Kivinjari Kilichopitwa na Wakati. |
| BrowserSwitcherExternalSitelistUrl | URL ya faili ya XML ambayo inajumuisha URL za kupakia katika kivinjari mbadala. |
| BrowserSwitcherKeepLastChromeTab | Acha kichupo cha mwisho kikiwa kimefunguliwa katika Chrome. |
| BrowserSwitcherUrlList | Tovuti zinazofunguka katika kivinjari mbadala |
| BrowserSwitcherUrlGreylist | Tovuti ambazo hazipaswi kusababisha kubadilishwa kwa kivinjari. |
| BrowserSwitcherUseIeSitelist | Tumia sera ya SiteList ya Internet Explorer ili upate Uwezo wa Kutumia Kivinjari Kilichopitwa na Wakati. |
| Metadata ya Linux | |
| VirtualMachinesAllowed | Ruhusu vifaa vitumie mashine pepe vinavyotumia Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome |
| CrostiniAllowed | Mtumiaji anaweza kutumia Crostini |
| DeviceUnaffiliatedCrostiniAllowed | Ruhusu watumiaji wasio washirika watumie Crostini |
| CrostiniExportImportUIAllowed | Mtumiaji anaweza kutuma au kuhamisha metadata za Crostini kupitia Kiolesura |
| Mipangilio ya Android | |
| ArcEnabled | Washa kipengele cha ARC |
| UnaffiliatedArcAllowed | Ruhusu watumiaji wasio washirika kutumia ARC |
| ArcPolicy | Weka mipangilio ya ARC |
| ArcAppInstallEventLoggingEnabled | Rekodi matukio ya usakinishaji wa programu za Android |
| ArcBackupRestoreServiceEnabled | Dhibiti huduma ya Android ya kuhifadhi nakala na kurejesha |
| ArcGoogleLocationServicesEnabled | Dhibiti huduma za mahali za Google kwenye Android |
| ArcCertificatesSyncMode | Weka upatikanaji wa cheti kwa programu za ARC |
| Mipangilio ya Faili za Kushiriki katika Mtandao | |
| NetworkFileSharesAllowed | Hudhibiti Faili za Kushiriki katika Mtandao kwa ajili ya upatikanaji wa ChromeOS |
| NetBiosShareDiscoveryEnabled | Hudhibiti ugunduzi wa Faili ya Kushiriki kwenye Mtandao kupitia NetBIOS |
| NTLMShareAuthenticationEnabled | Hudhibiti kuwashwa kwa NTLM kuwa itifaki ya kuthibitisha katika vipengee vya kupachika SMB |
| NetworkFileSharesPreconfiguredShares | Orodha ya faili za kushiriki mtandaoni zilizowekewa mipangilio mapema. |
| Mipangilio ya Kuvinjari Salama | |
| SafeBrowsingEnabled | Wezesha Kuvinjari Salama |
| SafeBrowsingExtendedReportingEnabled | Washa Kipengele cha Kuripoti kwa Upana Kuvinjari Salama |
| SafeBrowsingExtendedReportingOptInAllowed | Ruhusu watumiaji kuchagua kuingia katika kuripoti Kuvinjari Salama kulikopanuliwa |
| SafeBrowsingWhitelistDomains | Weka mipangilio ya orodha ya vikoa ambavyo kipengele cha Kuvinjari Salama hakisababishi onyo. |
| PasswordProtectionWarningTrigger | Kisababishi cha ilani ya ulinzi wa nenosiri |
| PasswordProtectionLoginURLs | Weka mipangilio ya orodha ya URL za kuingia katika akaunti ya biashara ambapo huduma za ulinzi wa nenosiri zinapaswa kunasa alama bainifu za nenosiri. |
| PasswordProtectionChangePasswordURL | Weka mipangilio ya URL ya kubadilisha nenosiri. |
| Mipangilio ya Maudhui | |
| DefaultCookiesSetting | Mpangilio wa vidakuzi chaguomsingi |
| DefaultImagesSetting | Mpangilio chaguomsingi wa picha |
| DefaultJavaScriptSetting | Mpangilio chaguomsingi wa JavaScript |
| DefaultPluginsSetting | Mipangilio chaguomsingi ya Flash |
| DefaultPopupsSetting | Mpangilio chaguomsingi za ibukizi |
| DefaultNotificationsSetting | Mpangilio wa arifa chaguomsingi |
| DefaultGeolocationSetting | Mpangilio chaguomsingi wa eneo la kijiografia |
| DefaultMediaStreamSetting | Mpangilio chaguomsingi wa mkondomedia |
| DefaultWebBluetoothGuardSetting | Dhibiti matumizi ya API ya Bluetooth ya Wavuti |
| DefaultWebUsbGuardSetting | Dhibiti matumizi ya API ya WebUSB |
| AutoSelectCertificateForUrls | Chagua kiotomatiki vyeti vya mteja vya tovuti hizi |
| CookiesAllowedForUrls | Ruhusu vidakuzi kwenye tovuti hizi |
| CookiesBlockedForUrls | Zuia vidakuzi katika tovuti hizi |
| CookiesSessionOnlyForUrls | Dhibiti vidakuzi visilinganishe URL kwa kipindi cha sasa |
| ImagesAllowedForUrls | Ruhusu picha katika tovuti hizi |
| ImagesBlockedForUrls | Zuia picha katika tovuti hizi |
| JavaScriptAllowedForUrls | Ruhusu JavaScript kwenye tovuti hizi |
| JavaScriptBlockedForUrls | Zuia JavaScript kwenye tovuti hizi |
| PluginsAllowedForUrls | Ruhusu programu jalizi ya Flash itumike kwenye tovuti hizi |
| PluginsBlockedForUrls | Zuia programu jalizi ya Flash kwenye tovuti hizi |
| PopupsAllowedForUrls | Ruhusu ibukizi kwenye tovuti hizi |
| RegisteredProtocolHandlers | Sajili vishikilizi vya itifaki |
| PopupsBlockedForUrls | Zuia madirisha ibukizi kwenye tovuti hizi |
| NotificationsAllowedForUrls | Ruhusu arifa katika tovuti hizi |
| NotificationsBlockedForUrls | Zuia arifa katika tovuti hizi |
| WebUsbAllowDevicesForUrls | Zipe tovuti hizi ruhusa kiotomatiki kuunganisha kwenye vifaa vya USB vilivyo na vitambulisho mahususi vya bidhaa na muuzaji. |
| WebUsbAskForUrls | Ruhusu WebUSB kwenye tovuti hizi |
| WebUsbBlockedForUrls | Zuia WebUSB kwenye tovuti hizi |
| Mipangilio ya Programu ya Skrini Nzima | |
| DeviceLocalAccounts | Akaunti za kifaa cha karibu nawe |
| DeviceLocalAccountAutoLoginId | Kuingia kiotomatiki katika akaunti iliyo kwenye kifaa |
| DeviceLocalAccountAutoLoginDelay | Kipima muda cha kuingia kiotomatiki katika akaunti iliyo kwenye kifaa |
| DeviceLocalAccountAutoLoginBailoutEnabled | Washa njia ya mkato ya kibodi ya usaidizi wa kuingia otomatiki |
| DeviceLocalAccountPromptForNetworkWhenOffline | Washa ombi la usanidi wa mtandao inapokuwa nje ya mtandao |
| AllowKioskAppControlChromeVersion | Ruhusu kipengele kilichofunguliwa kiotomatiki bila chochote kuchelewesha programu inayotumia skrini nzima kudhibiti toleo la Google Chrome OS |
| Mipangilio ya kudhibiti Microsoft® Active Directory® | |
| DeviceMachinePasswordChangeRate | Kasi ya kubadilisha nenosiri kwenye mashine |
| DeviceUserPolicyLoopbackProcessingMode | Hali ya uchakataji unaojirudia wa sera ya mtumiaji |
| DeviceKerberosEncryptionTypes | Aina za usimbaji wa Kerberos zinazoruhusiwa |
| DeviceGpoCacheLifetime | Akiba ya GPO ya siku zote |
| DeviceAuthDataCacheLifetime | Muda wa kutumia akiba ya data ya uthibitishaji |
| Mipangilio ya kuingia katika akaunti | |
| DeviceGuestModeEnabled | Wezesha modi ya wageni |
| DeviceUserWhitelist | Ingia kwenye orodha ya kutoa idhini ya mtumiaji |
| DeviceAllowNewUsers | Ruhusu uundaji wa akaunti mpya za mtumiaji |
| DeviceLoginScreenDomainAutoComplete | Washa kipengee cha jina la kikoa cha kukamilisha kiotomatiki wakati wa mtumiaji kuingia katika akaunti |
| DeviceShowUserNamesOnSignin | Onyesha majina ya watumiaji kwenye skrini ya kuingia |
| DeviceWallpaperImage | Picha ya mandhari ya kifaa |
| DeviceEphemeralUsersEnabled | Futa data ya mtumiaji unapoondoka |
| LoginAuthenticationBehavior | Weka mipangilio ya tabia ya kithibitishaji cha kuingia katika akaunti |
| DeviceTransferSAMLCookies | Hamisha vidakuzi vya SAML IdP wakati wa kuingia katika akaunti |
| LoginVideoCaptureAllowedUrls | URL zitakazopewa idhini ya kufikia vifaa vya kurekodi video kwenye kurasa za kuingia katika SAML |
| DeviceLoginScreenExtensions | Weka orodha ya programu zilizosakinishwa kwenye skrini ya kuingia katika akaunti |
| DeviceLoginScreenLocales | Lugha ya skrini ya kuingia katika kifaa |
| DeviceLoginScreenInputMethods | Miundo ya kibodi ya skrini ya kuingia katika kifaa |
| DeviceSecondFactorAuthentication | Hali ya uthibitishaji wa hatua mbili iliyowekwa |
| DeviceLoginScreenIsolateOrigins | Washa Utengaji wa Tovuti katika sehemu zilizobainishwa |
| DeviceLoginScreenSitePerProcess | Washa kipengele cha Utengaji wa Tovuti katika kila tovuti |
| DeviceLoginScreenAutoSelectCertificateForUrls | Chagua kiotomatiki vyeti vya mteja vya tovuti hizi kwenye skrini ya kuingia katika akaunti |
| Mipangilio ya kusasisha kifaa | |
| ChromeOsReleaseChannel | Kituo cha Kutoa |
| ChromeOsReleaseChannelDelegated | Watumiaji wanaweza kuweka mipangilio ya kituo cha matoleo ya Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome |
| DeviceAutoUpdateDisabled | Zima kipengele cha Kusasisha Kiotomatiki |
| DeviceAutoUpdateP2PEnabled | Usasishaji kiotomatiki wa P2P umewashwa |
| DeviceAutoUpdateTimeRestrictions | Sasisha Masharti ya Wakati |
| DeviceTargetVersionPrefix | Toleo Lengwa la Kusasisha Otomatiki |
| DeviceUpdateStagingSchedule | Ratiba ya kuanzisha mchakato wa kutumia sasisho jipya |
| DeviceUpdateScatterFactor | Sasisha kiotomatiki kipengee cha kutawanya |
| DeviceUpdateAllowedConnectionTypes | Aina za miunganisho zinazoruhusiwa kwa visasisho |
| DeviceUpdateHttpDownloadsEnabled | Ruhusu vipakuliwa vya kusasisha kiotomatiki kupitia HTTP |
| RebootAfterUpdate | Zima na uwashe tena otomatiki baada ya kusasisha |
| MinimumRequiredChromeVersion | Weka mipangilio ya msingi inayoruhusiwa ya toleo la Chrome kwenye kifaa. |
| DeviceRollbackToTargetVersion | Rejea kwenye toleo lengwa |
| DeviceRollbackAllowedMilestones | Idadi ya matukio ya urejeshaji inaruhusiwa |
| DeviceQuickFixBuildToken | Huwapa watumiaji Muundo wa Kurekebisha kwa Haraka. |
| Mipangilio ya mtandao | |
| DeviceOpenNetworkConfiguration | Usanidi wa mtandao wa kiwango cha kifaa |
| DeviceDataRoamingEnabled | Wezesha utumiaji wa data nje ya mtandao wako wa kawaida |
| NetworkThrottlingEnabled | Washa kipengele cha kudhibiti kipimo data cha mtandao |
| DeviceHostnameTemplate | Kiolezo cha jina la mpangishaji wa mtandao wa kifaa |
| DeviceWiFiFastTransitionEnabled | Washa Ubadilishaji Haraka wa Vigezo vya Muunganisho wa 802.11r |
| DeviceWiFiAllowed | Washa Wi-Fi |
| DeviceDockMacAddressSource | Chanzo cha anwani ya MAC wakati imeambatishwa |
| Mipangilio ya ufikiaji | |
| ShowAccessibilityOptionsInSystemTrayMenu | Onyesha chaguo za ufikiaji katika menyu ya trei ya mfumo |
| LargeCursorEnabled | Washa kiteuzi kikubwa |
| SpokenFeedbackEnabled | Wezesha maoni yaliyozungumzwa |
| HighContrastEnabled | Wezesha modi ya juu ya kulinganua |
| VirtualKeyboardEnabled | Washa kibodi ya skrini |
| KeyboardDefaultToFunctionKeys | Vitufe vya media huelekeza kwenye vitufe vya vitendo kwa chaguomsingi |
| ScreenMagnifierType | Weka aina ya kikuza skrini |
| DeviceLoginScreenDefaultLargeCursorEnabled | Weka hali chaguomsingi ya kiteuzi kikubwa kwenye skrini ya kuingia katika akaunti |
| DeviceLoginScreenDefaultSpokenFeedbackEnabled | Weka hali chaguomsingi ya maoni yanayotamkwa kwenye skrini ya kuingia katika akaunti |
| DeviceLoginScreenDefaultHighContrastEnabled | Weka hali chaguomsingi ya hali ya juu ya utofautishaji kwenye skrini ya kuingia katika akaunti |
| DeviceLoginScreenDefaultVirtualKeyboardEnabled | Weka hali chaguomsingi ya kibodi ya skrini kwenye skrini ya kuingia katika akaunti |
| DeviceLoginScreenDefaultScreenMagnifierType | Weka aina ya kikuza skrini cha msingi kama kimewashwa kwenye skrini ya kuingia katika skrini |
| Mratibu wa Google | |
| VoiceInteractionContextEnabled | "Ruhusu programu ya Mratibu wa Google ifikie maudhui ya skrini" |
| VoiceInteractionHotwordEnabled | Ruhusu programu ya Mratibu wa Google isikilize kifungu cha kuwasha sauti |
| Nyingine | |
| UsbDetachableWhitelist | Orodha ya vifaa vya USB vinavyoweza kutenganishwa vilivyoidhinishwa |
| DeviceAllowBluetooth | Ruhusu Bluetooth kwenye kifaa |
| TPMFirmwareUpdateSettings | Weka mipangilio ya shughuli za kusasisha programu dhibiti ya TPM |
| DevicePolicyRefreshRate | Onyesha upya kiwango cha Sera ya Kifaa |
| DeviceBlockDevmode | Zuia hali ya wasanidi programu |
| DeviceAllowRedeemChromeOsRegistrationOffers | Ruhusu watumiaji kukomboa matoleo kupitia Usajili wa Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome |
| DeviceQuirksDownloadEnabled | Washa kipengele cha hoja za Seva ya Quirks ya wasifu wa maunzi |
| ExtensionCacheSize | Weka ukubwa wa akiba inayoruhusiwa ya Programu na Viendelezi (katika baiti) |
| DeviceOffHours | Vipindi vya saa zisizo za kazi ambapo sera za kifaa zilizobainishwa hutolewa |
| Onyesho | |
| DeviceDisplayResolution | Weka mipangilio ya ubora wa onyesho na kigezo cha kipimo |
| DisplayRotationDefault | Weka mzunguko chaguomsingi wa onyesho, unaotumika kila unapowashwa tena |
| PluginVm | |
| PluginVmAllowed | Ruhusu vifaa vitumie PluginVm kwenyeGoogle Chrome OS |
| PluginVmLicenseKey | Ufunguo wa leseni ya PluginVm |
| PluginVmImage | Picha ya PluginVm |
| Seva ya proksi | |
| ProxyMode | Chagua jinsi ya kubainisha mipangilio ya seva mbadala |
| ProxyServerMode | Chagua jinsi ya kubainisha mipangilio ya seva mbadala |
| ProxyServer | Anwani au URL ya seva ya proksi |
| ProxyPacUrl | URL hadi proksi ya faili ya .pac |
| ProxyBypassList | Kanuni za ukwepaji proksi |
| Tarehe na wakati | |
| SystemTimezone | Saa za eneo: |
| SystemTimezoneAutomaticDetection | Weka mbinu ya ugunduzi wa saa za eneo kiotomatiki |
| SystemUse24HourClock | Tumia saa ya saa 24 kwa chaguomsingi |
| Ufikiaji wa mbali | |
| RemoteAccessHostClientDomain | Weka mipangilio ya jina la kikoa linalohitajika kwa ajili ya seva teja za ufikiaji wa mbali |
| RemoteAccessHostClientDomainList | Weka mipangilio ya majina ya vikoa yanayohitajika kwa ajili ya viteja vya kufikiwa kwa mbali |
| RemoteAccessHostFirewallTraversal | Inawezesha kutamba kwa ngome kutoka katika ufikivu wa mpangishaji wa mbali |
| RemoteAccessHostDomain | Sanidi jina la kikoa linalohitajika kwa wapangishaji wa ufikivu wa mbali |
| RemoteAccessHostDomainList | Weka mipangilio ya majina ya kikoa yanayohitajika kwa ajili ya seva pangishi wa uwezo wa kufikia kwa mbali |
| RemoteAccessHostTalkGadgetPrefix | Sanidi kiambishi awali cha TalkGadget kwa ufikiaji wa wapangishaji wa mbali |
| RemoteAccessHostRequireCurtain | Wezesha uzuiaji wa wapangishaji wa ufikiaji mbali. |
| RemoteAccessHostAllowClientPairing | Washa au zima uthibitishaji usiotumia PIN kwa seva pangishi za uwezo wa kufikia kwa mbali |
| RemoteAccessHostAllowGnubbyAuth | Ruhusu kipengele cha uthibitishaji wa gnubby kwa seva pangishi za uwezo wa kufikia kwa mbali |
| RemoteAccessHostAllowRelayedConnection | Washa matumizi ya seva za relei kwa mpangishi wa ufikiaji wa mbali |
| RemoteAccessHostUdpPortRange | Zuia masafa ya lango la UDP yaliyotumiwa na mpangishi wa ufikiaji wa mbali |
| RemoteAccessHostMatchUsername | Washa kipengele kinachohitaji kuwa jina la mtumiaji wa ndani na mmiliki wa seva pangishi yenye uwezo wa kufikia kwa mbali vilingane |
| RemoteAccessHostTokenUrl | URL ambapo seva teja za ufikiaji wa mbali zinapaswa kupata tokeni za uthibitishaji |
| RemoteAccessHostTokenValidationUrl | URL ya kuidhinisha tokeni ya kuthibitisha seva teja ya ufikiaji wa mbali |
| RemoteAccessHostTokenValidationCertificateIssuer | Cheti cha seva teja cha kuunganisha kwenye RemoteAccessHostTokenValidationUrl |
| RemoteAccessHostAllowUiAccessForRemoteAssistance | Ruhusu watumiaji wa mbali kutumia madirisha yaliyoinuliwa katika vipindi vya usaidizi wa mbali |
| RemoteAccessHostAllowFileTransfer | Ruhusu watumiaji walio na idhini ya kufikia kwa mbali kuhamisha au kuhamishia faili kwenye seva pangishi |
| Ujumbe wa Asili | |
| NativeMessagingBlacklist | Sanidi orodha ya wasioidhinishwa ya ujumbe asili |
| NativeMessagingWhitelist | Sanidi orodha ya walioidhinishwa ya ujumbe asili |
| NativeMessagingUserLevelHosts | Ruhusu seva za Ujumbe wa Mfumo wa ngazi ya watumiaji (unaosakinishwa bila idhini ya msimamizi) |
| Usimamizi wa nishati | |
| ScreenDimDelayAC | Ufifili wa skrini unachelewesha wakati wa kuendesha kwa nishati ya AC |
| ScreenOffDelayAC | Kuchelewa kwa kuzima skirini wakati nishati ya AC inapotumika |
| ScreenLockDelayAC | Ufungaji wa skrini unachelewa wakati nishati ya AC inapotimika |
| IdleWarningDelayAC | Onyo ya kuchelewa wakati wa kutokuwa na shughuli wakati wa kuendesha kwa nishati ya AC |
| IdleDelayAC | Kutokuwa na shughuli kunachelewesha wakati wa kuendesha kwenye nishati ya AC |
| ScreenDimDelayBattery | Ufifili wa skrini unachelewa wakati wa kuendesha kwa nishati ya betri |
| ScreenOffDelayBattery | Kuzimika kwa skrini kunachelewa wakati wa kuendesha kwa nishati ya betri |
| ScreenLockDelayBattery | Ufungaji wa skrini unachelewa wakati wa kuendesha kwa nishati ya betri |
| IdleWarningDelayBattery | Onyo ya kuchelewa wakati wa kutokuwa na shughuli wakati wa kuendesha kwa nishati ya betri |
| IdleDelayBattery | Kutokuwa na shughuli kunachelewesha wakati wa kuendesha kwa nishati ya betri |
| IdleAction | Hatua ya kuchukua wakati ucheleweshaji wa kutokuwa na shughuli unapofikiwa |
| IdleActionAC | Kitendo cha kuchukua ucheleweshwaji wa kutulia unapofikiwa wakati inaendeshwa kutumia nishati ya AC |
| IdleActionBattery | Kitendo cha kuchukua wakati ucheleweshaji wa kutofanya kitu umefikiwa ikiendeshwa kutumia nishati ya betri |
| LidCloseAction | Hatua ya kuchukua mtumiaji anapofunga mfuniko |
| PowerManagementUsesAudioActivity | Bainisha iwapo shughuli za sauti zinaathiri udhibiti wa nishati |
| PowerManagementUsesVideoActivity | Bainisha iwapo shughuli za video zinaathiri udhibiti wa nishati |
| PresentationScreenDimDelayScale | Asilimia ya kupima kuchelewesha kwa mwanga wa skrini katika modi ya wasilisho |
| AllowWakeLocks | Ruhusu wake lock |
| AllowScreenWakeLocks | Ruhusu makufuli ya kuwasha skrini |
| UserActivityScreenDimDelayScale | Asilimia ambayo mwangaza wa skrini utaongezwa uchelewaji iwapo mtumiaji anaanza kutumia baada ya kupunguza mwangaza |
| WaitForInitialUserActivity | Subiri shughuli ya kwanza ya mtumiaji |
| PowerManagementIdleSettings | Mipangilio ya kusimamia nishati mtumiaji anapokuwa hafanyi kitu |
| ScreenLockDelays | Ucheleweshaji wa kufunga sjrini |
| PowerSmartDimEnabled | Ruhusu muundo mahiri wa kufifiliza mwangaza kuendelea hadi wakati mwangaza wa skrini utakuwa hafifu |
| ScreenBrightnessPercent | Asilimia ya ung'avu wa skrini |
| DevicePowerPeakShiftBatteryThreshold | Weka kipengele kinachopunguza matumizi ya betri kwa kubadilisha mfumo kuendeshwa kwenye nguvu za betri katika asilimia |
| DevicePowerPeakShiftDayConfig | Weka mipangilio ya mchana ya kipengele kinachopunguza matumizi ya betri kwa kubadilisha mfumo kuendeshwa kwenye nguvu za betri |
| DevicePowerPeakShiftEnabled | Washa kipengele kinachopunguza matumizi ya betri kwa kubadilisha mfumo kuendeshwa kwenye nguvu za betri |
| DeviceBootOnAcEnabled | Washa nishati ya AC ya kuwasha kifaa (nishati inayobadilikabadilika). |
| DeviceAdvancedBatteryChargeModeEnabled | Washa hali ya kuchaji betri kwa kina |
| DeviceAdvancedBatteryChargeModeDayConfig | Weka mipangilio ya hali ya siku ya kuchaji betri kwa kina |
| DeviceBatteryChargeMode | Hali ya kuchaji betri |
| DeviceBatteryChargeCustomStartCharging | Weka mapendeleo ya muda wa kuanza kuchaji betri katika asilimia |
| DeviceBatteryChargeCustomStopCharging | Weka mipangilio ya kusimamisha mchakato wa kuchaji betri katika asilimia |
| DeviceUsbPowerShareEnabled | Ruhusu hali ya kushiriki nishati kwa kutumia USB |
| Uthibitishaji wa HTTP | |
| AuthSchemes | Mipango inayohimiliwa ya uthibitishaji |
| DisableAuthNegotiateCnameLookup | Lemaza kidokezo cha CNAME unapohawilisha uthibitishaji wa Kerberos |
| EnableAuthNegotiatePort | Jumuisha lango lisiyo wastani katika Kerberos SPN |
| AuthServerWhitelist | Orodha ya kuidhinisha ya seva ya uthibitishaji |
| AuthNegotiateDelegateWhitelist | Orodha iliyoidhinishwa ya ukaumu wa seva ya Kerberos |
| AuthNegotiateDelegateByKdcPolicy | Tumia sera ya KDC kutoa kitambulisho. |
| GSSAPILibraryName | Jina la maktaba ya GSSAPI |
| AuthAndroidNegotiateAccountType | Aina ya Akaunti kwa uthibitishaji wa HTTP Negotiate |
| AllowCrossOriginAuthPrompt | Vishtuo vya Cross-origin HTTP Basic Auth |
| NtlmV2Enabled | Washa uthibitishaji wa NTLMv2 |
| Uthibitishaji wa Mbali | |
| AttestationEnabledForDevice | Washa usahihishaji wa mbali wa kifaa |
| AttestationEnabledForUser | Washa usahihishaji wa mbali kwa mtumiaji |
| AttestationExtensionWhitelist | Viendelezi vinaruhusiwa kutumia API ya usahihishaji wa mbali |
| AttestationForContentProtectionEnabled | Washa matumizi ya usahihishaji wa mbali wa kulinda maudhui ya kifaa |
| Viendelezi | |
| ExtensionInstallBlacklist | Sanidi orodha inayotiliwa shaka ya usakinishaji wa kiendelezi |
| ExtensionInstallWhitelist | Sanidi orodha iliyoidhinishwa ya usakinishaji kiendelezi |
| ExtensionInstallForcelist | Sanidi orodha ya programu na viendelezi vilivyosakinishwa kwa nguvu |
| ExtensionInstallSources | Sanidi viendelezi, programu, na vyanzo vya kusakinisha hati |
| ExtensionAllowedTypes | Sanidi aina za programu/viendelezi zinazoruhusiwa |
| ExtensionAllowInsecureUpdates | Ruhusu algoriti zisizo salama katika ukaguzi wa mabadiliko ya data kwenye masasisho na usakinishaji wa viendelezi |
| ExtensionSettings | Mipangilio ya kudhibiti viendelezi |
| Wilco DTC | |
| DeviceWilcoDtcAllowed | Huruhusu kidhibiti cha uchunguzi na upimaji cha WILCO |
| DeviceWilcoDtcConfiguration | Kuweka mipangilio ya Wilco DTC |
| AbusiveExperienceInterventionEnforce | Kuingilia Kati ili Kuzuia Matumizi Yanayopotosha |
| AdsSettingForIntrusiveAdsSites | Mipangilio ya matangazo kwa tovuti zilizo na matangazo yanayokatiza matumizi |
| AllowDeletingBrowserHistory | Washa ufutaji wa historia ya upakuaji na kivinjari |
| AllowDinosaurEasterEgg | Ruhusu Mchezo Fiche wa Dinosau |
| AllowFileSelectionDialogs | Ruhusu ubatilishaji wa vidadisi vya uchaguzi wa faili |
| AllowOutdatedPlugins | Ruhusu kuendesha programu jalizi ambazo zimepitwa na wakati. |
| AllowPopupsDuringPageUnload | Huruhusu ukurasa kuonyesha madirisha ibukizi wakati wa kuondoa |
| AllowScreenLock | Ruhusu kufunga skrini |
| AllowedDomainsForApps | Bainisha vikoa vinavyoruhusiwa kufikia G Suite |
| AllowedInputMethods | Weka mipangilio ya mbinu za kuingiza data zinazoruhusiwa katika kipindi cha mtumiaji |
| AllowedLanguages | Weka mipangilio ya lugha zinazoruhusiwa katika kipindi cha mtumiaji |
| AlternateErrorPagesEnabled | Wezesha kurasa badala za hitilafu |
| AlwaysOpenPdfExternally | Fungulia faili za PDF nje kila wakati |
| ApplicationLocaleValue | Lugha ya programu |
| AudioCaptureAllowed | Ruhusu au upinge kurekodi sauti |
| AudioCaptureAllowedUrls | URL ambazo zitapewa ufikiaji wa vifaa vya kunasa sauti bila ushawishi |
| AudioOutputAllowed | Ruhusu kucheza sauti |
| AutoFillEnabled | Washa uwezo wa Kujaza kitomatiki |
| AutofillAddressEnabled | Washa kipengele cha Kujaza Kiotomatiki kwa anwani |
| AutofillCreditCardEnabled | Washa kipengele cha Jaza Kiotomatiki kwa kadi za mikopo |
| AutoplayAllowed | Ruhusu maudhui yacheze kiotomatiki |
| AutoplayWhitelist | Ruhusu maudhui yacheze kiotomatiki kwenye orodha ya ruwaza za URL zilizoidhinishwa |
| BackgroundModeEnabled | Endelea kuendesha programu za mandharinyuma wakati Google Chrome imefungwa |
| BlockThirdPartyCookies | Zuia vidakuzi vya wengine |
| BookmarkBarEnabled | Wezesha Upau wa Alamisho |
| BrowserAddPersonEnabled | Washa kipengele cha kuongeza wasifu katika kidhibiti cha mtumiaji |
| BrowserGuestModeEnabled | Washa matumizi ya wageni katika kivinjari |
| BrowserNetworkTimeQueriesEnabled | Ruhusu hoja kwenye huduma ya wakati ya Google |
| BrowserSignin | Mipangilio ya kuingia katika akaunti ya kivinjari |
| BuiltInDnsClientEnabled | Tumia DNS teja ya kijenzi cha ndani |
| CaptivePortalAuthenticationIgnoresProxy | Uthibitishaji wa ukurasa wavuti hupuuza seva mbadala |
| CertificateManagementAllowed | Huruhusu watumiaji kudhibiti vyeti vilivyosakinishwa. |
| CertificateTransparencyEnforcementDisabledForCas | Zima utekelezaji wa Uwazi wa Cheti katika orodha ya hashi za subjectPublicKeyInfo |
| CertificateTransparencyEnforcementDisabledForLegacyCas | Zima utekelezaji wa Uwazi wa Cheti katika orodha ya Mamlaka ya Vyeti Vilivyopitwa na Wakati |
| CertificateTransparencyEnforcementDisabledForUrls | Zima utekelezaji wa Uwazi wa Cheti kwa orodha ya URL |
| ChromeCleanupEnabled | Washa Kipengele cha Kusafisha Chrome kwenye Windows |
| ChromeCleanupReportingEnabled | Hudhibiti jinsi Kipengele cha Kusafisha Chrome huripoti data kwa Google |
| ChromeOsLockOnIdleSuspend | Wawezesha kufunga wakati kifaa kinapokuwa hakifanyi kitu au kimesimamishwa |
| ChromeOsMultiProfileUserBehavior | Dhibiti tabia ya mtumiaji katika kipindi cha wasifu nyingi |
| CloudManagementEnrollmentMandatory | Washa ujumuishaji wa lazima katika usimamizi wa wingu |
| CloudManagementEnrollmentToken | Tokeni ya ujumuishaji wa sera ya wingu kwenye eneo-kazi |
| CloudPolicyOverridesPlatformPolicy | Sera ya wingu ya Google Chrome inabatilisha sera ya Mfumo. |
| ComponentUpdatesEnabled | Ruhusu masasisho ya vipengele katika Google Chrome |
| ContextualSearchEnabled | Washa kipengele cha Gusa ili Utafute |
| ContextualSuggestionsEnabled | Washa mapendekezo ya muktadha wa kurasa za wavuti husika |
| DataCompressionProxyEnabled | Washa kipengee cha proksi cha upunguzaji wa data |
| DefaultBrowserSettingEnabled | Weka Google Chrome kama Kivinjari Chaguomsingi |
| DefaultDownloadDirectory | Weka saraka chaguomsingi ya kupakua |
| DeveloperToolsAvailability | Dhibiti mahali ambapo Zana za Wasanidi Programu zinaweza kutumika |
| DeveloperToolsDisabled | Lemaza Zana za Wasanidi Programu |
| DeviceLocalAccountManagedSessionEnabled | Ruhusu vipindi vinavyodhibitiwa kwenye kifaa |
| DeviceRebootOnUserSignout | Lazimisha kifaa kiwake tena mtumiaji anapoondoka katika akaunti |
| DeviceScheduledUpdateCheck | Weka ratiba maalum ili kuangalia masasisho |
| Disable3DAPIs | Lemaza uhimili wa API za michoro ya 3D |
| DisableSafeBrowsingProceedAnyway | Lemaza kuendelea kutoka kwenye ukurasa wa ilani ya Kuvinjari Salama |
| DisableScreenshots | Zima upigaji picha za skrini |
| DisabledPlugins | Bainisha orodha ya programu jalizi zilizolemazwa |
| DisabledPluginsExceptions | Bainisha orodha ya programu jalizi ambayo mtumiaji anaweza kuwezesha au kulemaza |
| DisabledSchemes | Lemaza mipango ya itifaki ya URL |
| DiskCacheDir | Weka saraka ya akiba ya diski |
| DiskCacheSize | Weka ukubwa wa akiba ya diski katika baiti |
| DownloadDirectory | Weka saraka ya kupakua |
| DownloadRestrictions | Weka vikwazo vya upakuaji |
| EasyUnlockAllowed | Huruhusu Smart Lock itumiwe |
| EcryptfsMigrationStrategy | Mkakati wa uhamishaji wa ecryptfs |
| EditBookmarksEnabled | Washa au uzime kipengele cha kubadilisha alamisho |
| EnableDeprecatedWebPlatformFeatures | Washa vipengele vilivyoacha kuendesha huduma vya mbinu ya wavuti kwa muda mfupi |
| EnableOnlineRevocationChecks | Washa ukaguzi wa OCSP/CRL mtandaoni |
| EnableSymantecLegacyInfrastructure | Ruhusu uaminifu wa Muundomsingi wa PKI ya Zamani ya Symantec Corporation |
| EnableSyncConsent | Washa kipengele cha kuonyesha Idhini ya Usawazishaji wakati wa kuingia katika akaunti |
| EnabledPlugins | Bainisha orodha ya programu jalizi zilizowezeshwa |
| EnterpriseHardwarePlatformAPIEnabled | Huruhusu viendelezi vinavyodhibitiwa kutumia API ya Enterprise Hardware Platform |
| ExternalStorageDisabled | Lemaza uangikaji wa hifadhi ya nje |
| ExternalStorageReadOnly | Ainisha vifaa vya hifadhi ya nje kuwa vya kusoma tu |
| ForceBrowserSignin | Washa kulazimisha kuingia katika akaunti ya Google Chrome |
| ForceEphemeralProfiles | Mfumo wa Muda Mfupi |
| ForceGoogleSafeSearch | Lazimisha Google SafeSearch |
| ForceMaximizeOnFirstRun | Tanua dirisha la kwanza la kivinjari unapofungua mara ya kwanza |
| ForceNetworkInProcess | Lazimisha msimbo wa mtandao kutekelezwa katika mchakato wa kivinjari |
| ForceSafeSearch | Lazimisha SafeSearch |
| ForceYouTubeRestrict | Lazimisha Kiwango cha chini cha Hali yenye Mipaka kwenye YouTube |
| ForceYouTubeSafetyMode | Lazimisha Hali Salama ya YouTube |
| FullscreenAllowed | Ruhusu hali ya skrini nzima |
| HardwareAccelerationModeEnabled | Tumia uongezaji kasi wa maunzi wakati unapatikana |
| HideWebStoreIcon | Ficha duka la wavuti kwenye ukurasa mpya wa kichupo na kifungua programu cha Chrome |
| Http09OnNonDefaultPortsEnabled | Washa matumizi ya HTTP/0.9 kwenye milango isiyo chaguomsingi |
| ImportAutofillFormData | Leta data ya fomu ya kujaza otomatiki kutoka kwenye kivinjari chaguomsingi wakati wa uendeshaji wa kwanza |
| ImportBookmarks | Ingiza alamisho kutoka kivinjari chaguomsingi wakati wa uendeshaji wa kwanza |
| ImportHistory | Leta historia ya kivinjari kutoka kwenye kivinjari chaguomsingi wakati wa uendeshaji wa kwanza |
| ImportHomepage | Leta ukurasa wa mwanzo kutoka kwenye kivinjari chaguomsingi kwenye uendeshaji wa kwanza |
| ImportSavedPasswords | Leta manenosiri yaliyohifadhiwa kutoka kwenye kivinjari chaguomsingi kwenye uendeshaji wa kwanza |
| ImportSearchEngine | Leta injini za utafutaji kutoka kwenye kivinjari chaguomsingi wakati wa uendeshaji wa kwanza |
| IncognitoEnabled | Washa hali Fiche |
| IncognitoModeAvailability | Upatikanaji wa hali fiche |
| InstantTetheringAllowed | Ruhusu matumizi ya Usambazaji wa Mtandao Papo Hapo. |
| IsolateOrigins | Washa Utengaji wa Tovuti katika sehemu zilizobainishwa |
| IsolateOriginsAndroid | Washa sera ya Utengaji wa Tovuti katika vyanzo vilivyobainishwa kwenye vifaa vya Android |
| JavascriptEnabled | Wezesha JavaScript |
| KeyPermissions | Ruhusa za Funguo |
| MachineLevelUserCloudPolicyEnrollmentToken | Tokeni ya ujumuishaji wa sera ya wingu kwenye eneo-kazi |
| ManagedBookmarks | Alamisho Zinazosimamiwa |
| MaxConnectionsPerProxy | Kiwango cha juu kabisa cha miunganisho ya wakati mmoja kwenye seva ya proksi |
| MaxInvalidationFetchDelay | Upeo wa juu wa ucheleweshaji wa kuleta baada ya kutothibitisha sera |
| MediaCacheSize | Weka ukubwa wa akiba ya diski ya media katika vipimo vya baiti |
| MediaRouterCastAllowAllIPs | Ruhusu Google Cast iunganishwe na Vifaa vinavyotuma maudhui kwenye anwani zote za IP. |
| MetricsReportingEnabled | Wezesha kuripoti kwa matumizi na data zinazohusu mvurugiko |
| NTPContentSuggestionsEnabled | Onyesha mapendekezo ya maudhui kwenye ukurasa wa Kichupo Kipya |
| NetworkPredictionOptions | Wezesha ubashiri wa mtandao |
| NoteTakingAppsLockScreenWhitelist | Toa idhini kwa programu za kuandika madokezo zinazoruhusiwa kwenye skrini iliyofungwa ya Google Chrome OS |
| OpenNetworkConfiguration | Usanidi mtandao wa kiwango cha mtumiaji |
| OverrideSecurityRestrictionsOnInsecureOrigin | Mitindo ya vyanzo au ya majina ya seva pangishi ambako vizuizi vya vyanzo visivyo salama havipaswi kutumika |
| ParentAccessCodeConfig | Mipangilio ya Msimbo wa Kufikia wa Mzazi |
| PinnedLauncherApps | Orodha ya programu zilizobanwa ili kuonekana kwenye kizunduzi |
| PolicyListMultipleSourceMergeList | Ruhusu uunganishaji wa sera za orodha kutoka vyanzo tofauti |
| PolicyRefreshRate | Kiwango cha kuonyesha upya kwa sera ya mtumiaji |
| PromotionalTabsEnabled | Ruhusu kuonyeshwa kwa maudhui ya matangazo katika kichupo chote |
| PromptForDownloadLocation | Uliza mahali pa kuhifadhi kila faili kabla ya kuipakua. |
| ProxySettings | Mipangilio ya proksi |
| QuicAllowed | Ruhusu itifaki ya QUIC |
| RelaunchNotification | Imwarifu mtumiaji kwamba anashauriwa au anatakiwa afungue upya kivinjari au azime kisha awashe kifaa |
| RelaunchNotificationPeriod | Weka kipindi cha arifa za usasishaji |
| ReportCrostiniUsageEnabled | Ripoti maelezo kuhusu matumizi ya programu za Linux |
| RequireOnlineRevocationChecksForLocalAnchors | Inahitaji ukaguzi wa OCSP/CRL wa funguo za mfumo zinazoaminika |
| RestrictAccountsToPatterns | Dhibiti akaunti ambazo zinaonekana kwenye Google Chrome |
| RestrictSigninToPattern | Dhibiti aina za akaunti za Google zinazoruhusiwa kuwekwa kuwa akaunti za msingi za kivinjari katika Google Chrome |
| RoamingProfileLocation | Weka saraka ya wasifu isiyo ya kawaida |
| RoamingProfileSupportEnabled | Washa uundaji wa nakala za urandaji za data ya wasifu wa Google Chrome |
| RunAllFlashInAllowMode | Panua mipangilio ya maudhui ya Flash kujumuisha maudhui yote |
| SAMLOfflineSigninTimeLimit | Weka kikomo cha muda ambao mtumiaji aliyethibitishwa kupitia SAML anaweza kuingia katika akunti nje ya mtandaoni |
| SSLErrorOverrideAllowed | Ruhusu kuendelea kutoka kwenye ukurasa wa onyo wa SSL |
| SSLVersionMin | Toleo la chini la SSL limewashwa |
| SafeBrowsingForTrustedSourcesEnabled | Washa kipengele cha Kuvinjari Salama katika vyanzo vinavyoaminika |
| SafeSitesFilterBehavior | Dhibiti uchujaji wa maudhui ya watu wazima katika SafeSites. |
| SavingBrowserHistoryDisabled | Lemaza kuhifadhi historia ya kivinjari |
| SchedulerConfiguration | Chagua mipangilio ya kiweka ratiba ya majukumu |
| SearchSuggestEnabled | Wezesha mapendekezo ya utafutaji |
| SecondaryGoogleAccountSigninAllowed | Ruhusu Kuingia katika Akaunt Nyingi katika Kivinjari |
| SecurityKeyPermitAttestation | URL/vikoa vinaruhusu ufikiaji uliothibitishwa wa kiotomatiki wa moja kwa moja kwa kutumia Ufunguo wa Usalama |
| SessionLengthLimit | Dhibiti muda wa kipindi cha mtumiaji |
| SessionLocales | Weka lugha zinazopendekezwa kwa kipindi kinachodhibitiwa |
| ShelfAutoHideBehavior | Dhibiti kujificha kitomatiki kwa rafu |
| ShowAppsShortcutInBookmarkBar | Onyesha njia ya mkato katika sehemu ya alamisho |
| ShowLogoutButtonInTray | Ongeza kitufe cha kuondoka kwenye chano la mfumo |
| SignedHTTPExchangeEnabled | Ruhusu utumiaji wa Kubadilisha HTTP Iliyoambatishwa Cheti (SXG) |
| SigninAllowed | Ruhusu kuingia katika akaunti ya Google Chrome |
| SitePerProcess | Washa kipengele cha Utengaji wa Tovuti katika kila tovuti |
| SitePerProcessAndroid | Washa kipengele cha Utengaji wa Tovuti katika kila tovuti |
| SmartLockSigninAllowed | Huruhusu utumiaji wa Kuingia katika Akaunti kupitia Smart Lock. |
| SmsMessagesAllowed | Ruhusu Ujumbe wa SMS kusawazishwa kutoka simu hadi Chromebook. |
| SpellCheckServiceEnabled | Wezesha au lemaza huduma ya wavuti ya ukaguzi tahajia |
| SpellcheckEnabled | Washa kikagua tahajia |
| SpellcheckLanguage | Lazimisha kuwasha sera ya kikagua tahajia |
| SpellcheckLanguageBlacklist | Lazimisha kuzima sera ya kikagua tahajia katika lugha |
| SuppressUnsupportedOSWarning | Kandamiza onyo la Mfumo wa Uendeshaji usiotumika |
| SyncDisabled | Lemaza usawazishaji wa data iliyna Google |
| TabLifecyclesEnabled | Huwasha au kuzima muda wa matumizi ya kichupo |
| TaskManagerEndProcessEnabled | Washa kipengele cha kutamatisha shughuli katika Kidhibiti cha Shughuli kwenye Chrome |
| TermsOfServiceURL | Weka Sheria na Masharti kwa akaunti ya kifaa cha karibu nawe |
| ThirdPartyBlockingEnabled | Washa kipengele cha kuzuia uingizaji unaofanywa na programu za kampuni nyingine |
| TouchVirtualKeyboardEnabled | Wezesha kibodi isiyobayana |
| TranslateEnabled | Wezesha Tafsiri |
| URLBlacklist | Zuia ufikivu kwenye orodha za URL |
| URLWhitelist | Ruhusu ufikiaji kwenye orodha ya URL |
| UnifiedDesktopEnabledByDefault | Fanya Eneo-kazi Lililounganishwa lipatikane na uwashe kwa chaguomsingi |
| UnsafelyTreatInsecureOriginAsSecure | Mitindo ya vyanzo au ya majina ya seva pangishi ambako vizuizi vya vyanzo visivyo salama havipaswi kutumika |
| UrlKeyedAnonymizedDataCollectionEnabled | Washa kipengele cha ukusanyaji wa faragha wa data ukitumia ufunguo wa URL |
| UsageTimeLimit | Kikomo cha Muda |
| UserAvatarImage | Picha ya ishara ya mtumiaji |
| UserDataDir | Weka saraka ya data ya mtumiaji |
| UserDisplayName | Weka jina la onyesho kwa ajili ya akaunti za kifaa cha karibu |
| VideoCaptureAllowed | Ruhusu au ukatae kurekodi video |
| VideoCaptureAllowedUrls | URL ambazo zitapewa ufikiaji wa vifaa vya kunasa video bila ushawishi |
| VpnConfigAllowed | Mruhusu mtumiaji kudhibiti miunganisho ya VPN |
| WPADQuickCheckEnabled | Washa uboreshaji wa WPAD |
| WallpaperImage | Picha ya mandhari |
| WebAppInstallForceList | Weka mipangilio ya orodha ya Programu za Wavuti zilizosakinishwa kwa lazima |
| WebDriverOverridesIncompatiblePolicies | Ruhusu WebDriver Ifute Sera Ambazo Hazioani |
| WebRtcEventLogCollectionAllowed | Ruhusu ukusanyaji wa kumbukumbu za matukio ya WebRTC kutoka huduma za Google |
| WebRtcUdpPortRange | Dhibiti masafa ya milango ya ndani ya UDP inayotumiwa na WebRTC |
| WelcomePageOnOSUpgradeEnabled | Washa kipengee cha kuonyesha ukurasa wa kukaribisha unapofungua kivinjari kwa mara ya kwanza baada ya kusasisha Mfumo wa Uendeshaji |
Ikiwa sera hii imewekwa kuwa ndivyo au haijawekwa, Google Cast itawashwa na watumiaji wataweza kuifungua kwenye menyu ya programu, menyu za ukurasa, vidhibiti vya maudhui kwenye tovuti zinazoweza kutumia Google Cast na (ikiwa imeonyeshwa) aikoni ya upau wa vidhibiti vya Google Cast.
Ikiwa sera hii imewekwa kuwa sivyo, Google Cast itazimwa.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, aikoni ya upau wa vidhibiti vya Google Cast itaonyeshwa kila wakati kwenye upau wa vidhibiti au menyu ya vipengee vya ziada, na watumiaji hawataweza kuiondoa.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo au isipowekwa, watumiaji wataweza kubandika au kuondoa aikoni kupitia menyu yake.
Sera ya "EnableMediaRouter" ikiwekwa kuwa sivyo, basi thamani ya sera hii haitakuwa na athari, na aikoni ya upau wa vidhibiti haitaonyeshwa.
Huzima usawazishaji wa Hifadhi ya Google katika programu ya Faili ya Google Chrome OS unapowekwa kuwa Ndivyo. Kwa hivyo, hakuna data inayopakiwa kwenye Hifadhi ya Google.
Isipowekwa au ikiwekwa kuwa Sivyo, basi watumiaji wataweza kuhamisha faili kwenye Hifadhi ya Google.
Sera hii haizuii mtumiaji kutumia programu ya Hifadhi ya Android Google. Ikiwa unataka kuzuia idhini ya kufikia Hifadhi ya Google, usiruhusu usakinishaji wa programu ya Hifadhi ya Android Google pia.
Huzima usawazishaji wa Hifadhi ya Google katika programu ya Faili ya Google Chrome OS inapotumia muunganisho wa simu ya mkononi inapowekwa kuwa Ndivyo. Kwa hivyo, data inasawazishwa tu kwenye Hifadhi ya Google inapounganishwa kupitia WiFi au Ethaneti.
Isipowekwa au ikiwekwa kuwa Sivyo, basi watumiaji wataweza kuhamisha faili hadi Hifadhi ya Google kupitia miunganisho ya simu za mkononi.
Sera hii haiathiri programu ya Hifadhi ya Android Google. Ikiwa unataka kuzuia matumizi ya Hifadhi ya Google kwenye mitandao ya simu, usiruhusu usakinishaji wa programu ya Hifadhi ya Android Google.
Mipangilio hii ikiwashwa, watumiaji wanaweza kuifanya Google Chrome ikumbuke na kuweka manenosiri kiotomatiki wakati mwingine wanapoingia katika tovuti.
Mipangilio hii ikizimwa, watumiaji hawawezi kuhifadhi manenosiri mapya lakini bado wanaweza kutumia manenosiri ambayo yalihifadhiwa awali.
Sera hii ikiwashwa au kuzimwa, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuibatilisha katika Google Chrome. Sera hii isipowekwa, hatua ya kuhifadhi manenosiri itaruhusiwa (lakini mtumiaji anaweza kuizima).
Sera hii haiathiri programu za Android.
Huwasha matumizi ya kitoaji chaguomsingi cha utafutaji.
Ukiwasha mipangilio hii, utafutaji chaguomsingi hufanywa wakati mtumiaji anaandika maandishi katika sanduku kuu ambalo si URL.
Unaweza kubainisha kitoaji chaguomsingi cha utafutaji kitakachotumika kuweka sera zingine za kitoaji chaguomsingi cha utafutaji. Sehemu hizi zikiachwa bila kuwekwa, mtumiaji anaweza kuchagua kitoaji chaguomsingi.
Ukizima mipangilio hii, hakuna utafutaji unaofanywa wakati mtumiaji anaandika maandishi ambayo si URL katika sanduku kuu.
Ukiwasha au kuzima mipangilio hii, watumiaji hawawezi kubadilisha au kubatilisha mipangilio hii katika Google Chrome.
Iwapo sera hii haijawekwa, kitoaji chaguomsingi cha utafutaji kinawashwa na mtumiaji ataweza kuweka orodha ya vitoaji vya utafutaji.
Sera hii inapatikana kwenye matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®. au matukio ya Windows 10 Pro au Enterprise yaliyojumuishwa katika usimamizi wa kifaa.
Inabainisha jina la mtoaji wa utafutaji chaguo -msingi. Likiachwa tupu au bila kuwekwa, jina la mpangishaji lililobainishwa na URL ya utafutaji litatumiwa.
Sera hii inazingatiwa tu ikiwa sera ya 'DefaultSearchProviderEnabled' itawezeshwa.
Hubainisha neno muhimu, ambalo ni njia mkato inayotumiwa katika SanduKuu kusisimua utafutaji kwa mtoa huduma huyu.
Sera hii ni ya hiari. Ikiwa haijawekwa, hakuna neno muhimu litakaloamilisha mtoa huduma ya utafutaji.
Sera hii inazingatiwa tu ikiwa sera ya 'DefaultSearchProviderEnabled' imewezeshwa.
Hubainisha URL ya mtambo wa kutafuta inayotumika unapofanya utafutaji chaguomsingi. URL inapaswa kuwa na mfuatano wa '{searchTerms}', ambao nafasi yake inachukuliwa wakati wa kuandika hoja ya maneno ambayo mtumiaji anatafuta.
URL ya utafutaji wa Google inaweza kubanishwa kuwa: '{google:baseURL}search?q={searchTerms}&{google:RLZ}{google:originalQueryForSuggestion}{google:assistedQueryStats}{google:searchFieldtrialParameter}{google:searchClient}{google:sourceId}ie={inputEncoding}'.
Lazima chaguo hili liwekwe wakati sera ya 'DefaultSearchProviderEnabled' imewashwa na itazingatiwa tu hali hii ikitimizwa.
Hubainisha URL ya mtambo wa kutafuta uliotumiwa kutoa mapendekezo ya utafutaji. URL sharti iwe na mfuatano '{searchTerms}', ambao nafasi yake itachukuliwa wakati wa kuandika hoja ya maandishi ambayo mtumiaji atakuwa ameweka.
Sera hii ni ya hiari. Ikiwa haijawekwa, hakuna mapendekezo ya URL yatakayotumiwa.
URL ya mapendekezo ya Google inaweza kubainishwa kuwa: '{google:baseURL}complete/search?output=chrome&q={searchTerms}'.
Sera hii inazingatiwa tu ikiwa sera ya 'DefaultSearchProviderEnabled' imewashwa.
Inabainisha aikoni ya URL pendwa ya mtoaji chaguomsingi wa utafutaji.
Sera hii ni ya hiari. Ikiwa haitawekwa, hakuna aikoni itakayokuwepo kwa mtojai wa utafutaji.
Sera hii inafuatiliwa tu ikiwa sera ya 'DefaultSearchProviderEnabled' imewezeshwa.
Inabainisha usimbaji wa vibambo unaohimiliwa na kitoaji cha utafutaji. Usimbaji ni majini ya ukurasa msimbo kama UTF-8, GB2312, na ISO-8859-1. Yanajaribiwa katika mpangilio uliotolewa.
Sera hii ni ya hiari. Ikiwa haijawekwa, chaguomsingi itatumika ambayo nis UTF-8.
Sera hii inaheshimiwa tu ikiwa sera ya 'DefaultSearchProviderEnabled' imewezeshwa.
Hubainisha orodha ya URL mbadala zinazoweza kutumiwa ili kupata taminolijia za utafutaji kutoka kwenye mtambo wa kutafuta. URL zinafaa kuwa na maneno '{searchTerms}', ambayo yatatumika kupata taminolojia za utafutaji.
Sera hii ni ya hiari, Iwapo haijawekwa, hakuna url mbadala zitazotumika kupata hoja za utafutaji.
Sera hii inazingatiwa tu iwapo sera ya 'DefaultSearchProviderEnabled' imewashwa.
Hubainisha URL ya injini tafuti inayotumika kutoa utafutaji kwa picha. Maombi ya utafutaji yatatumwa kwa kutumia mbinu ya GET. Kama sera ya DefaultSearchProviderImageURLPostParams imewekwa basi maombi ya utafutaji kwa picha yatatumia mbinu ya POST badala yake.
Sera hii ni ya hiari. Isipowekwa, hakuna utafutaji kwa picha utakaotumika.
Sera hii itatumika tu endapo sera ya 'DefaultSearchProviderEnabled' imewashwa.
Hubainisha URL ambayo injini ya utafutaji inatumia kutoa ukurasa mpya wa kichupo.
Sera hii ni ya hiari. Kama haitawekwa, hakuna ukurasa mpya wa kichupo utatolewa.
Sera hii inatumika tu kama sera ya 'DefaultSearchProviderEnabled' imewashwa.
Hubainisha vigezo vinavyotumika wakati wa kutafuta URL kwa kutumia POST. Ina vikundi vya jina/thamani vinavyotenganishwa na koma. Kama thamani ni kigezo cha kiolezo, kama {Hoja za utafutaji} katika mfano hapo juu, itabadilishwa na data ya hoja za utafutaji halisi.
Sera hii ni ya hiari. Isipowekwa, ombi la utafutaji litatumwa kutumia mbinu ya GET.
Sera hii inatumika endapo sera ya 'DefaultSearchProviderEnabled' imewashwa.
Hubainisha vigezo vinavyotumika wakati wa kufanya utafutaji kwa mapendekezo kutumia POST. Ina vikundi vya jina/thamani vinavyotenganishwa na koma. Kama thamani ni kigezo cha kiolezo, kama, {Hoja za utafutaji} katika mfano hapo juu, itabadilishwa na data ya hoja za utafutaji halisi.
Sera hii ni ya hiari. Isipowekwa, ombi la utafutaji kwa mapendekezo litatumwa kwa kutumia mbinu ya GET.
Sera hii inatumika tu endapo sera ya 'DefaultSearchProviderEnabled' imewashwa.
Hubainisha vigezo vinavyotumika wakati wa kufanya utafutaji kwa picha kutumia POST. Ina vikundi vya jina/thamani vinavyotenganishwa na koma. Kama thamani ni kigezo cha kiolezo, kama {Kijipicha} katika mfano hapo juu, itabadilishwa na data ya kijipicha cha picha halisi.
Sera hii ni ya hiari. Isipowekwa, ombi la utafutaji kwa picha litatumwa kwa kutumia mbinu ya GET.
Sera hii inatumika tu endapo sera ya 'DefaultSearchProviderEnabled' imewashwa.
Huwasha kuchapisha katika Google Chrome na huzuia watumiaji kubadilisha mpangilio huu.
Iwapo mpangilio huu utawashwa au hautasanidiwa, watumiaji wanaweza kuchapisha.
Iwapo mpangilio huu utazimewa, watumiaji hawawezi kuchapisha kutoka kwenye Google Chrome. Uchapishaji utafungwa katika menyu spana, viendelezi, programu za, n.k. Bado kuna uwezekano wa kuchapisha kutoka kwenye programu jalizi zinazopuuza Google Chrome wakati wa kuchapisha. Kwa mfano, programu fulani za Flash zina chaguo la kuchapisha katika menyu zao za muktadha, ambazo hazisimamiwi na sera hii.
Sera hii haiathiri programu za Android.
Huwezesha Google Chrome kufanya kazi kama proksi kati ya Google Cloud Print na printa zilizotangulia zilizounganishwa kwenye mashine.
Iwapo mpangilio huu utawashwa au hutasanidiwa, watumiaji wanaweza kutumia proksi ya kuchipisha ya wingu ili kuthibitisha akaunti ya Google.
Iwapo mpangilio huu utafungwa, watumiaji hawawezi kuwasha proksi, na mashine haitaruhusiwa kushiriki printa zake na Google Cloud Print.
Inaweka uchapishaji wa rangi pekee, rangi moja nyeupe na nyeusi pekee au kudhibiti hali isiyo na rangi. Sera ambayo haijawekewa mipangilio inachukuliwa kuwa hamna kudhibiti.
Inazuia uchapishaji kwenye pande mbili za kurasa. Sera isipowekwa na kusiwe na mipangilio, hali hizo zitachukuliwa kwamba hakuna kizuizi.
Inabatilisha hali chaguomsingi ya rangi ya kuchapisha. Ikiwa hali haipatikani, sera hii haitazingatiwa.
Inabatilisha hali chaguomsingi ya kuchapisha kwenye pande mbili. Ikiwa hali haipatikani, sera hii haizingatiwi.
Inawezesha Google Chrome kuwasilisha nyaraka kwenye Google Cloud Print ili kuchapishwa. KUMBUKA: Hii inaathiri tu msaada wa Google Cloud Print katika Google Chrome. Haizuii watumiaji kuwasilisha kazi zilizochapishwa kwenye tovuti.
Ikiwa mpangilio huu utawezeshwa au hautasanidiwa, watumiaji wanaweza kuchapisha kwenye Google Cloud Print kutoka kwenye Google Chrome kidadisi cha kuchapisha.
Ikiwa mpangilio huu utalemazwa, watumiaji hawawezi kuchapisha kwenye Google Cloud Print kutoka kwenye Google Chrome kidadisi cha kuchapisha
Onyesha mazungumzo ya kuchapisha ya mfumo badala ya uhakiki wa kuchapisha.
Mpangilio huu unapowashwa, Google Chrome itafungua mazungumzo ya kuchapisha ya mfumo badala ya uhakiki wa kuchapisha wa kijenzi cha ndani mtumiaji anapoomba ukurasa kuchapishwa.
Iwapo sera hii haitawekwamu itawekwa kuwa uongo, amri za kuchapisha zitachochea skrini ya ukakiki ya kuchapisha.
Lazimisha 'vichwa na vijachini' viwashwe au vizimwe kwenye kidirisha cha kuchapisha.
Ikiwa sera haijawekwa, mtumiaji anaweza kuamua iwapo atachapisha vichwa na vijachini.
Ikiwa mipangilio ya sera imwekwa kuwa ya sivyo, 'Vichwa na vijachini' havitachaguliwa kwenye kidirisha cha onyesho la kukagua uchapishaji, na mtumiaji hawezi kuibadilisha.
Ikiwa mipangilio ya sera imewekwa kuwa ya ndivyo, 'Vichwa na vijachini' vitachaguliwa kwenye kidirisha cha onyesho la kukagua uchapishaji, na mtumiaji hawezi kuibadilisha.
Hubatilisha mipangilio ya uteuzi wa printa chaguomsingi ya Google Chrome.
Sera hii hubaini masharti ya kuchagua printa chaguomsingi katika Google Chrome, tendo ambalo hufanyika mara ya kwanza ambapo kipengele cha printa kinatumika katika wasifu.
Sera hii ikiwekwa, Google Chrome itajaribu kutafuta printa inayolingana na sifa zote zilizobainishwa na kuichagua ili iwe printa chaguomsingi. Itachagua printa ya kwanza itakayopata ambayo italingana na sera. Iwapo kuna ulinganifu usio maalum, inaweza kuchagua printa yoyote inayolingana. Hali hii itategemea utaratibu ambao printa zinatambuliwa.
Ikiwa sera hii haijawekwa au haipati printa inayolingana katika muda uliyowekwa, itatumia printa ya PDF iliyotengenezewa ndani ya mfumo kwa chaguomsingi au haitachagua printa yoyote iwapo printa ya PDF haitapatikana.
Thamani inachanganuliwa kama kipengee cha JSON, kwa kutii utaratibu ufuatao: { "type": "object", "properties": { "kind": { "description": "Whether to limit the search of the matching printer to a specific set of printers.", "type": "string", "enum": [ "local", "cloud" ] }, "idPattern": { "description": "Regular expression to match printer id.", "type": "string" }, "namePattern": { "description": "Regular expression to match printer display name.", "type": "string" } } }
Printa zilizounganishwa kwenye Google Cloud Print zinachukuliwa kuwa "cloud", na printa nyinginezo zinaainishwa kama "local". Hatua ya kuacha sehemu inamaanisha kuwa thamani zote zinalingana, kwa mfano, kutobainisha uunganishaji kutasababisha Onyesho la Kuchungulia Printa lianzishe utambuzi wa aina zote za printa za mfumo na za wingu. Ni lazima miundo ya maonyesho ya kawaida ifuate sintaksia ya JavaScript RegExp na viwango vinavyolingana huathiriwa na ukubwa au udogo wa fonti.
Sera hii haiathiri programu za Android.
Huweka mipangilio ya orodha ya printa.
Sera hii huruhusu wasimamizi kutoa mipangilio ya printa kwa watumiaji wake.
display_name na description ziko katika mifuatano wazi ambayo inaweza kubadilishwa ikufae ili kurahisisha kuchagua printa. manufacturer na model hukusaidia kutambulisha printa kulingana na watumiaji wake. Huwakilisha mtengenezaji na muundo wa printa. uri inapaswa kuwa mahali ambapo panafikika kutoka kwenye kiteja cha kompyuta ikiwa ni pamoja na scheme, port na queue. Si lazima uweke uuid. Ikiwekwa, itatumika kusaidia kuondoa nakala za printa za zeroconf.
Ni lazima effective_model ifanane na mojawapo ya mfuatano unaowakilisha printa inayotumika ya Google Chrome OS. Mfuatano huo utatumiwa kutambua na kusakinisha PPD inayofaa kwenye printa. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika https://support.google.com/chrome?p=noncloudprint.
Shughuli ya kuweka mipangilio ya printa hukamilika baada ya kutumia printa mara ya kwanza. PPD hazipakuliwi mpaka printa itumike. Baada ya hapo, PDD zinazotumiwa sana huakibishwa.
Sera hii haiathiri iwapo watumiaji wanaweza kuweka mipangilio kwenye vifaa vya kibinafsi. Imewekwa iwe mbinu ya ziada ya kuweka mipangilio ya printa inayotumiwa na watumiaji mahususi.
Kwa vifaa vinavyodhibitiwa na Saraka Inayotumika, sera hii inatumia upanuzi wa ${MACHINE_NAME[,pos[,count]]} kwenye jina la mashine ya Saraka Inayotumika au kiambishi cha msimbo. Kwa mfano, ikiwa jina la mashine ni CHROMEBOOK, basi herufi 4 zitatumiwa badala ya ${MACHINE_NAME,6,4} kuanzia nafasi ya 6, kwa mfano BOOK. Kumbuka kwamba nafasi hii inatumia sufuri.
Hutoa mipangilio ya printa za biashara.
Sera hii hukuruhusu kuweka mipangilio ya printa kwenye vifaa vya Google Chrome OS. Muundo huu ni sawa na kamusi ya NativePrinters, unaohitaji sehemu ya ziada ya "kitambulisho" au "mwongozo" kwa kila printa kwa ajili ya kutoa idhini au kunyima idhini.
Ukubwa wa faili haupaswi kuzidi MB 5 na ni lazima iwe imesimbwa katika JSON. Inakadiriwa kuwa faili iliyo na takribani printa 21,000 itasimbwa kuwa faili ya MB 5. Hashi ya kriptografia itatumika kuthibitisha hadhi ya upakuaji.
Faili hupakuliwa na kuwekwa katika akiba. Itapakuliwa tena wakati hashi au URL itabadilishwa.
Ikiwa sera hii imewekwa, Google Chrome OS itapakua faili kwa ajili ya mipangilio ya printa na kufanya printa zipatikane kulingana na sera za NativePrintersBulkAccessMode, NativePrintersBulkWhitelist na NativePrintersBulkBlacklist.
Kama utaweka sera hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuifuta.
Sera hii haina athari yoyote iwapo watumiaji wanaweka mipangilio ya printa kwenye vifaa mahususi. Imewekwa iwe mbinu ya ziada ya kuweka mipangilio ya printa inayotumiwa na watumiaji mahususi.
Hudhibiti aina za printa kutoka NativePrintersBulkConfiguration zinazopatikana kwa watumiaji.
Hubainisha sera ya ufikiaji inayotumiwa katika mipangilio ya kina ya printa. Ikiwa AllowAll imechaguliwa, printa zote zitaonyeshwa. Ikiwa BlacklistRestriction imechaguliwa, NativePrintersBulkBlacklist itatumika kudhibiti uwezo wa kufikia printa zilizobainishwa. Ikiwa WhitelistPrintersOnly imechaguliwa, NativePrintersBulkWhitelist itabainisha printa ambazo zitachaguliwa pekee.
Ikiwa sera haijawekwa, AllowAll itaendelea kufuatwa.
Hubainisha printa ambazo mtumiaji hawezi kutumia.
Sera hii hutumika tu ikiwa mipangilio ya BlacklistRestriction imechaguliwa katika NativePrintersBulkAccessMode.
Ikiwa sera hii inatumiwa, printa zote hutolewa kwa mtumiaji isipokuwa vitambulisho vilivyoorodheshwa katika sera hii. Ni lazima vitambulisho vilingane na sehemu za "kitambulisho" au "mwongozo" kwenye faili iliyobainishwa katika NativePrintersBulkConfiguration.
Hubainisha printa ambazo mtumiaji anaweza kutumia.
Sera hii hutumika tu ikiwa mipangilio ya WhitelistPrintersOnly imechaguliwa katika NativePrintersBulkAccessMode.
Ikiwa sera hii inatumiwa, printa zenye vitambulisho vinavyolingana na thamani iliyo katika sera ndizo pekee zitakazopatikana kwa watumiaji. Ni lazima vitambulisho vilingane na sehemu za "kitambulisho" au "mwongozo" kwenye faili iliyobainishwa katika NativePrintersBulkConfiguration.
Hutoa mipangilio ya printa za biashara zilizooanishwa kwenye vifaa.
Sera hii hukuruhusu kuweka mipangilio ya printa kwenye vifaa vya Google Chrome OS. Muundo huu ni sawa na ule wa kamusi ya NativePrinters, unaohitaji sehemu ya ziada ya "kitambulisho" au "mwongozo" kwa kila printa kwa ajili ya kutoa idhini au kunyima idhini.
Ukubwa wa faili haupaswi kuzidi MB 5 na ni lazima iwe imesimbwa katika JSON. Inakadiriwa kuwa faili iliyo na takribani printa 21,000 itasimbwa kuwa faili ya MB 5. Hashi ya kriptografia itatumika kuthibitisha hadhi ya upakuaji.
Faili hupakuliwa na kuwekwa katika akiba. Itapakuliwa tena wakati hashi au URL itabadilishwa.
Ikiwa sera imewekwa, Google Chrome OS itapakua faili kwa ajili ya mipangilio ya printa na kufanya printa zipatikane kulingana na sera za DeviceNativePrintersAccessMode, DeviceNativePrintersWhitelist na DeviceNativePrintersBlacklist.
Sera hii haina athari yoyote iwapo watumiaji wanaweka mipangilio ya printa kwenye vifaa mahususi. Imewekwa iwe mbinu ya ziada ya kuweka mipangilio ya printa inayotumiwa na watumiaji mahususi. Sera hii ni nyongeza ya NativePrintersBulkConfiguration.
Ikiwa sera hii haijawekwa, hakutakuwa na printa za vifaa na sera zingine DeviceNativePrinter* hazitafuatwa.
Hudhibiti aina za printa kutoka DeviceNativePrinters zinazopatikana kwa watumiaji.
Hubainisha sera ya ufikiaji inayotumiwa katika mipangilio ya kina ya printa. Kama AllowAll imechaguliwa, printa zote zitaonyeshwa. Kama BlacklistRestriction imechaguliwa, DeviceNativePrintersBlacklist itatumika kudhibiti uwezo wa kufikia printa zilizobainishwa. Ikiwa WhitelistPrintersOnly imechaguliwa, DeviceNativePrintersWhitelist itabainisha tu printa ambazo zinaweza kuchaguliwa.
Ikiwa sera haijawekwa, AllowAll itaendelea kutumika.
Hubainisha printa ambazo mtumiaji hawezi kutumia.
Sera hii hutumika tu ikiwa mipangilio ya BlacklistRestriction imechaguliwa katika DeviceNativePrintersAccessMode.
Ikiwa sera hii inatumiwa, printa zote hutolewa kwa mtumiaji isipokuwa vitambulisho vilivyoorodheshwa katika sera hii. Ni lazima vitambulisho vilingane na sehemu za "kitambulisho" au "mwongozo" kwenye faili iliyobainishwa katika DeviceNativePrinters.
Hubainisha printa ambazo mtumiaji anaweza kutumia.
Sera hii hutumika tu ikiwa mipangilio ya WhitelistPrintersOnly imechaguliwa katika DeviceNativePrintersAccessMode
Ikiwa sera hii inatumiwa, printa zenye vitambulisho vinavyolingana na thamani iliyo katika sera ndizo pekee zitakazopatikana kwa watumiaji. Ni lazima vitambulisho vilingane na sehemu za "kitambulisho" au "mwongozo" kwenye faili iliyobainishwa katika DeviceNativePrinters.
Mipangilio hii husababisha Google Chrome kutumia printa chaguomsingi ya mfumo kama uteuzi chaguomsingi katika Onyesho la Kuchungulia la Printa badala ya printa iliyotumika hivi majuzi.
Ukiizima mipangilio hii au usipoweka thamani, Onyesho la Kuchungulia la Printa litatumia printa iliyotumika hivi majuzi zaidi kama uteuzi chaguomsingi.
Ukiiwasha mipangilio hii, Onyesho la Kuchungulia la Printa litatumia printa chaguomsingi ya mfumo wa uendeshaji kama uteuzi chaguomsingi.
Orodha iliyoidhinishwa inayodhibiti aina za hali za kufungua haraka ambazo mtumiaji anaweza kuwekea mipangilio na kutumia kufungua skrini iliyofungwa.
Thamani hii ni orodha ya mifuatano; data ya orodha sahihi ni: "zote", "PIN", "ALAMA YA KIDOLE". Ukiongeza "zote" kwenye orodha, inamaanisha kuwa kila hali ya kufungua haraka itapatikana kwa watumiaji, ikijumuisha zile ambazo zitatekelezwa baadaye. Vinginevyo, hali za kufungua haraka zilizopakiwa mapema katika orodha ndizo tu zitapatikana.
Kwa mfano, ili kuruhusu kila hali ya kufungua haraka, tumia ["zote"]. Ili uruhusu kufungua kupitia PIN pekee, tumia ["PIN"]. Ili uruhusu PIN na alama ya kidole, tumia ["PIN", "ALAMA YA KIDOLE"]. Ili uzime hali zote za kufungua haraka, tumia [].
Kwa chaguomsingi, hamna hali za kufungua haraka zinazopatikana katika vifaa vinavyodhibitiwa.
Mipangilio hii inadhibiti idadi ambayo skrini iliyofungwa itaomba nenosiri liwekwe ili uendelee kutumia kipengele cha kufungua haraka. Kila mara skrini iliyofungwa inapowekwa, iwapo nenosiri lililowekwa ni zaidi ya mipangilio hii, kipengele cha kufungua haraka hakitapatikana unapoingia kwenye skrini iliyofungwa. Ikiwa mtumiaji atakuwa kwenye skrini iliyofungwa kwa zaidi ya muda huu, ataombwa nenosiri wakati ujao akiweka nambari ya kuthibitisha ambayo si sahihi, au akiweka tena skrini iliyofungwa, chochote kitakachotokea kwanza.
Mipangilio hii ikiwekwa, watumiaji wanaotumia kipengele cha kufungua skrini haraka wataombwa waweke manenosiri yao kwenye skrini iliyofungwa kutegemea mipangilio hii.
Mipangilio hii isipowekwa, watumiaji wanaotumia kipengele cha kufungua skrini haraka wataombwa waweke manenosiri yao kwenye skrini iliyofungwa kila siku.
Sera hii ikiwekwa, kiwango cha urefu wa chini zaidi wa PIN inayowekwa hutumika. (Kima cha urefu kamili wa chini zaidi wa PIN ni 1 thamani zilizo chini ya 1 huchukuliwa kuwa 1.)
Sera hii isipowekwa, urefu wa chini zaidi wa PIN wa tarakimu 6 hutumika. Huu ndio urefu wa chini zaidi unaopendekezwa.
Sera hii ikiwekwa, kima cha urefu wa PIN inayowekwa huibainishwa. Thamani isiyozidi 0 inamaanisha kwamba hakuna kima cha urefu wa juu zaidi, katika hali hiyo, mtumiaji anaweza kuweka PIN ndefu kadri anavyotaka. Mipangilio hii ikiwa chini ya PinUnlockMinimumLength lakini zaidi ya 0, kima cha urefu wa juu zaidi ni sawa na kima cha urefu wa chini zaidi.
Sera hii isipowekwa, hakuna kima cha juu zaidi cha urefu kinabainishwa.
Ikiwa sivyo, watumiaji hawataweza kuweka PIN ambazo ni dhaifu na rahisi kuzitambua.
Mifano ya PIN dhaifu: PIN zilizo na tarakimu moja tu (1111), PIN ambazo tarakimu zake zinaongezeka kwa 1 (1234), PIN ambazo tarakimu zake zinapungua kwa 1 (4321), na PIN zinazotumika kwa kawaida.
Kwa chaguomsingi, watumiaji watapokea onyo, si arifa ya hitilafu, ikiwa PIN itatambulika kuwa dhaifu.
Inaonyesha kitufe cha Mwanzo kwenye upauzana wa Google Chrome.
Ukiwezesha mpangilio huu, kila mara kitufe cha Mwanzo kinaonyeshwa.
Ukilemaza mpangilio huu, kitufe cha Mwanzo hakionyeshwi tena.
Ukiwezesha au kulemaza mpangilio huu, watumiaji hawawezi kubadilisha au kufuta mpangilio huu kwenye Google Chrome.
Kuacha sera hii kama haijawekwa kutaruhusu mtumiaji kuchagua iwapo ataonyesha kitufe cha mwanzo.
Huweka URL chaguomsingi ya ukurasa wa mwanzo katika Google Chrome na huzuia watumiaji kuibadilisha.
Ukurasa wa mwanzo ni ukurasa unaofunguliwa na kitufe cha ukurasa wa Mwanzo. Kurasa zinazofunguka kifaa kinapowashwa zinadhibitiwa na sera za RestoreOnStartup.
Aina ya ukurasa wa mwanzo inaweza kuwekwa kwenye URL unayobainisha hapa au kuwekwa katika Ukurasa Mpya wa Kichupo. Ukichagua Ukurasa Mpya wa Kichupo, basi sera hii haitatekelezwa.
Ukiwasha mipangilio hii, watumiaji hawawezi kubadilisha URL ya ukurasa wao wa kwanza katika Google Chrome, lakini bado wanaweza kuchagua Ukurasa Mpya wa Kichupo kuwa ukurasa wa kwanza.
Sera hii isipowekwa, itamruhusu mtumiaji kuchagua ukurasa wake wa mwanzo iwapo HomepageIsNewTabPage haijawekwa pia.
URL lazima iwe na mfuatano wa kawaida, k.m "http://example.com" au "https://example.com".
Sera hii inapatikana katika matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®. au matukio ya Windows 10 Pro au Enterprise yaliyojumuishwa katika usimamizi wa kifaa.
Inaweka mipangilio ya aina ya ukurasa wa kwanza chaguomsingi katika Google Chrome na huzuia watumiaji kubadilisha mapendeleo ya ukurasa wa kwanza. Ukurasa wa kwanza unaweza kuwekwa kwenye URL unayobainisha au kuwekwa kwenye Ukurasa wa Kichupo Kipya.
Ukiwasha mipangilio hii, Ukurasa Mpya wa Kichupo hutumika wakati wote kuwa ukurasa wa kwanza na URL ya eneo la ukurasa wa kwanza hupuuzwa.
Ukizima mipangilio hii, ukurasa wa kwanza wa mtumiaji kamwe hautakuwa Ukurasa wa Kichupo Kipya, labda URL yake iwekwe iwe 'chrome://newtab'.
Ukiwasha au kuzima mipangilio hii, watumiaji hawawezi kubadilisha aina yao ya ukurasa wa kwanza katika Google Chrome.
Kuacha sera hii bila kuiweka kutaruhusu mtumiaji kuchagua mwenyewe iwapo ukurasa wa kichupo kipya ni ukurasa wake wa kwanza.
Sera hii inapatikana kwenye matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®. au matukio ya Windows 10 Pro au Enterprise yaliyojumuishwa katika usimamizi wa kifaa.
Huweka mipangilio ya URL chaguomsingi ya ukurasa wa Kichupo Kipya na huzuia watumiaji kuibadilisha.
Ukurasa wa Kichupo Kipya ni ukurasa unaofunguka vichupo vipya vinapofunguliwa (ikiwa ni pamoja na kichupo kilichofunguliwa katika madirisha mapya).
Sera hii haiamui kurasa zinazofunguliwa wakati wa kuanza. Kurasa hizo hudhibitiwa na sera za RestoreOnStartup. Hata hivyo sera hii inaathiri Ukurasa wa Mwanzo ikiwa umewekwa ufungue ukurasa wa Kichupo Kipya na pia ukurasa unaoanza ikiwa umewekwa ufungue ukurasa wa Kichupo Kipya.
Sera isipowekwa au ikiachwa tupu, ukurasa wa kichupo kipya chaguomsingi utatumika.
Sera hii inapatikana kwenye matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®. au matukio ya Windows 10 Pro au Enterprise yaliyojumuishwa katika usimamizi wa kifaa.
Hukuruhusu kubainisha tabia unapoanza.
Ukichagua "Fungua Ukurasa wa Kichupo Kipya" Ukurasa wa Kichupo Kipya utafunguliwa kila wakati unapoanzisha Google Chrome.
Ukichagua "Rejesha upya kipindi cha mwisho", URL ambazo zilikuwa zimefunguliwa wakati wa mwisho Google Chrome ilipofungwa zitafunguliwa upya na kipindi cha kivinjari kitarejeshwa upya jinsi kilivyokuwa. Kuteua chaguo hili kunazima mipangilio mingine ambayo inategemea vipindi au inayotenda vitendo katika kuondoka (kama vile Kufuta data ya kuvinjari unapoondoka au vidakuzi vya kipindi pekee).
Ukichagua 'Fungua orodha ya URL", orodha ya "URL kufunguliwa inapoanza" itafunguka mtumiaji anapoanzisha Google Chrome.
Ukiwasha mipangilio hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuifuta kwenye Google Chrome.
Kuzima mipangilio hii ni sawa na kuiacha kama hujaweka mipangilio. Mtumiaji bado ataweza kuibadilisha katika Google Chrome.
Sera hii inapatikana kwenye matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®. au matukio ya Windows 10 Pro au Enterprise yaliyojumuishwa katika usimamizi wa kifaa.
Ikiwa 'Fungua orodha ya URL' imechaguliwa kama kitendo cha kuanza, hii inakuruhusu kubainisha orodha ya URL zinazofunguliwa. Ikiachwa bila kuwekwa hakuna URL itakayofunguliwa wakati wa kuanza.
Sera hii inafanya kazi tu ikiwa sera ya 'RestoreOnStartup' imewekwa kuwa 'RestoreOnStartupIsURLs'.
Sera hii inapatikana kwenye matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®. au matukio ya Windows 10 Pro au Enterprise yaliyojumuishwa katika usimamizi wa kifaa.
Ripoti toleo la OS na programu dhibiti ya vifaa vilivyosajiliwa.
Ikiwa mpangilio huu hautawekwa au utawekwa kuwa Ukweli, vifaa vilivyosajiliwa vitaripoti toleo la OS na programu dhibiti kila mara. Ikiwa mpangilio huu utawekwa kuwa Uongo, maelezo ya toleo hayataripotiwa.
Sera hii haiathiri uwekaji kumbukumbu wa Android.
Ripoti hali ya ubadilishaji wa kifaa cha dev wakati wa kuwasha.
Ikiwa sera hii itawekwa kuwa uongo, hali ya ubadilishaji wa dev haitaripotiwa.
Sera hii haiathiri uwekaji kumbukumbu wa Android.
Ripoti orodha ya watumiaji wa kifaa ambao waliingia katika akaunti hivi karibuni.
Ikiwa sera imewekwa kuwa uongo, watumiaji hawataripotiwa.
Sera hii haiathiri uwekaji kumbukumbu wa Android.
Ripoti muda wa shughuli za kifaa.
Ikiwa mpangilio huu hautawekwa au utawekwa kuwa Ukweli, vifaa vilivyosajiliwa vitaripoti vipindi vya muda mtumiaji anapotumia kifaa. Ikiwa mpangilio huu utawekwa kuwa Uongo, muda wa shughuli za kifaa hautarekodiwa wala kuripotiwa.
Sera hii haiathiri uwekaji kumbukumbu wa Android.
Ripoti orodha ya violesura vya mtandao vilivyo na aina zao na anwani za maunzi kwenye seva.
Ikiwa sera itawekwa kuwa Uongo, orodha ya violesura haitaripotiwa.
Sera hii haiathiri uwekaji kumbukumbu wa Android.
Ripoti takwimu za maunzi kama vile matumizi ya CPU/RAM.
Sera ikiwekwa kuwa sivyo, takwimu hazitaripotiwa. Ikiwekwa kuwa sivyo au iachwe bila kuwekwa, takwimu zitaripotiwa.
Sera hii haiathiri uwekaji kumbukumbu wa Android.
Ripoti maelezo kuhusu kipindi cha skrini nzima kinachoendelea, kama vile Kitambulisho na toleo la programu.
Sera ikiwekwa kuwa sivyo, maelezo ya kipindi cha skrini nzima hayataripotiwa. Ikiwekwa kuwa ndivyo au ikiachwa bila kuwekwa, maelezo ya kipindi cha skrini nzima yataripotiwa.
Sera hii haiathiri uwekaji kumbukumbu wa Android.
Ripoti takwimu za maunzi za vipengee vya SoC.
Ukiweka sera hii kuwa sivyo, takwimu hazitaripotiwa. Ukiweka sera hii kuwa ndivyo au usipoiweka, takwimu zitaripotiwa
Sera hii haiathiri uwekaji kumbukumbu wa Android.
Ripoti takwimu na vitambulishi vya maunzi vinavyohusiana na nishati.
Ukiweka sera hii kuwa sivyo, takwimu hazitaripotiwa. Ukiweka sera hii kuwa ndivyo au usipoiweka, takwimu zitaripotiwa
Sera hii haiathiri uwekaji kumbukumbu wa Android.
Ripoti takwimu na vitambulishi vya maunzi ya vifaa vya hifadhi.
Ukiweka sera hii kuwa sivyo, takwimu hazitaripotiwa. Ukiweka sera hii kuwa ndivyo au usipoiweka, takwimu zitaripotiwa
Sera hii haiathiri uwekaji kumbukumbu wa Android.
Ni mara ngapi vipakiwa vya hali ya kifaa hutumwa, katika milisekunde.
Sera hii isipowekwa, idadi chaguomsingi ni saa 3. Idadi ya chini inayoruhusiwa ni sekunde 60.
Sera hii haiathiri uwekaji kumbukumbu wa Android.
Maelezo kuhusu hali ya Android yatatumwa kwenye seva.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo au isipowekwa, maelezo ya hali hayataripotiwa. Ikiwekwa kuwa ndivyo, maelezo ya hali yataripotiwa.
Sera hii inatumika tu iwapo programu za Android zimewashwa.
Tuma vifurushi vya mtandao kwenye seva ya udhibiti ili kufuatilia hali ya mtandaoni, ili kuruhusu seva igundue kama kifaa kiko nje ya mtandao.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, ufuatiliaji wa vifurushi vya mtandao (maarufu kama heartbeats) utatumwa. Ikiwekwa kuwa sivyo au isipowekwa, hakuna vifurushi vitakavyotumwa.
Sera hii haiathiri uwekaji kumbukumbu wa Android.
Mara ambazo vifurushi vya mtandao vya ufuatiliaji hutumwa, katika milisekunde.
Sera hii isipowekwa, muda chaguomsingi ni dakika 3. Muda wa chini ni sekunde 30 na muda wa juu ni saa 24 - thamani nje ya masafa haya itaunganishwa kwenye masafa haya.
Sera hii haiathiri uwekaji kumbukumbu wa Android.
Tuma kumbukumbu za mfumo kwenye seva ya udhibiti, ili uruhusu wasimamizi kufuatilia kumbukumbu za mfumo.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, kumbukumbu za mfumo zitatumwa. Ikiwekwa kuwa sivyo au kutowekwa, basi hakuna kumbukumbu za mfumo ambazo zitatumwa.
Sera hii haiathiri uwekaji kumbukumbu wa Android.
Hubainisha ikiwa vipimo vya matumizi na data ya uchunguzi pamoja na ripoti za kuacha kufanya kazi, zitaripotiwa kwa Google.
Ukiweka kuwa ndivyo, Google Chrome OS itaripoti vipimo vya matumizi na data ya uchunguzi.
Ukiweka kuwa sivyo, kipengele cha kuripoti data ya vipimo na uchunguzi kitazimwa.
Kama hujaweka mipangilio ya sera hii, kipengele cha kuripoti vipimo na data ya uchunguzi kitazimwa kwenye vifaa visivyodhibitiwa na kuwashwa kwenye vifaa vinavyodhibitiwa.
Sera hii pia inadhibiti matumizi ya Android na ukusanyaji data ya utatuzi.
Sanidi usimamizi wa nishati kwenye skrini ya kuingia katika akaunti ya Google Chrome OS.
Sera hii hukuruhusu kusanidi jinsi Google Chrome OS hufanya kazi kunapokuwa hakuna shughuli ya mtumiaji kwa muda huku skrini ya kuingia katika akaunti ikiwa inaonyeshwa. Sera hii hudhibiti mipangilio mingi. Kwa vigezo maalum na mfululizo wa thamani, tazama sera zinazolingana ambazo hudhibiti usimamizi wa nishati wakati wa kipindi. Tofauti za pekee zilizoko kwenye sera hizi ni: * Vitendo vya kuchukua wakati haifanyi kitu au kifuniko kimefunikwa haviwezi kuwa kumaliza kipindi * Kitendo chaguomsingi cha kuchukua wakati kifaa hakifanyi kitu kinapoendeshwa kutumia nishati ya AC ni kuzima.
Kama mpangilio usipobainishwa, thamani chaguomsingi inatumika.
Sera hii ikiondolewa, chaguomsingi zitatumika kwa mipangilio yote.
Pima muda wa kuwaka wa kifaa kwa kuratibu kuwasha tena kiotomatiki. Sera hii inapowekwa, inabainisha urefu wa muda wa kuwaka wa kifaa baada ya upi uwashaji tena kiotomatiki utaratibiwa.
Sera hii isipowekwa, muda wa kuwaka wa kifaa hauna kipimo.
Ukiweka sera hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuifuta.
Kuwasha tena kiotomatiki huratibiwa kwa wakati uliochaguliwa lakini kunaweza kucheleweshwa kwenye kifaa hadi saa 24 kama mtumiaji anatumia kifaa kwa sasa.
Kumbuka: Kuwasha tena kiotomatiki kunawashwa wakati skrini ya kuingia katika akaunti inaonyeshwa au kipindi cha programu ya kioski kinaendelea kwa sasa. Hii itabadilika siku zijazo na sera itatumika kila wakati, bila kujali iwapo kipindi cha aina yoyote kinaendelea ua la. Thamani ya sera inapaswa kubainishwa katika sekunde. Thamani huwekwa pamoja ili iwe angalau 3600 (saa moja).
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo au isisanidiwe, Google Chrome OS itamruhusu mtumiaji kuzima kifaa. Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, Google Chrome OS itaanzisha kuwasha tena mtumiaji anapozima kifaa. Google Chrome OS huchukua nafasi ya matukio yote ya vitufe vya kuzima katika kiolesura kwa kutumia vitufe vya kuzima. Mtumiaji akizima kifaa akitumia kitufe cha kuwasha/kuzima, hakitawasha tena kiotomatiki, hata kama sera imewashwa.
Sera hii inadhibiti aina ya amri itakayotumiwa kufungua URL katika kivinjari mbadala.
Usipoweka sera hii, mipangilio mahususi ya mfumo itatumika: Internet Explorer katika Windows au Safari katika Mac OS X. Kwenye Linux, hatua ya kufungua kivinjari mbadala haitatekelezwa iwapo hujaweka sera hii.
Ukiweka sera hii katika mojawapo ya ${ie}, ${firefox}, ${safari} au ${opera}, kivinjari hicho kitafunguka iwapo kimesakinishwa. ${ie} inapatikana tu kwenye Windows na ${safari} inapatikana tu kwenye Windows na Mac OS X.
Wakati umeweka mipangilio ya sera hii katika njia ya faili, faili hiyo itatumika kama faili inayoweza kutekelezwa.
Sera hii inadhibiti vipengee vya mstari wa amri ili kufungua kivinjari mbadala.
Iwapo hujaweka mipangilio ya sera hii, URL pekee ndiyo itapitishwa kama kipengee cha mstari wa amri.
Iwapo umeweka mipangilio ya sera hii kwenye orodha ya mifuatano, kila mfuatano utapitishwa kwenye kivinjari mbadala kama kipengee cha mstari wa amri kivyake. Kwenye Windows, vipengee vinaunganishwa kwa nafasi. Kwenye Mac OS X na Linux, kipengee kinaweza kuwa na nafasi na bado kichukuliwe kama kipengee kimoja.
Iwapo kipengee kina ${url}, nafasi yake inachukuliwa na URL ya ukurasa unaofunguliwa.
Iwapo hamna kipengee ambacho kina ${url}, URL itaambatishwa mwishoni mwa mstari wa amri.
Vigezo vya mazingira hupanuliwa. Kwenye Windows, nafasi ya %ABC% inachukuliwa na thamani ya ABC ya kigezo cha mazingira. Kwenye Mac OS X na Linux, nafasi ya ${ABC} inachukuliwa na thamani ya ABC ya kigezo cha mazingira.
Sera hii hubaini amri ya kutumia ili kufungua URL katika Google Chrome unapobadili kutoka Internet Explorer.
Ikiwa kipengele cha 'Uwezo wa Kutumia Kivinjari Kilichopitwa na Wakati' cha Internet Explorer hakijasakinishwa, sera hii haina athari.
Sera hii ikiachwa bila kuwekwa, Internet Explorer itatambua kiotomatiki njia ya utekelezaji wa Google Chrome' wakati inafungua Google Chrome kutoka Internet Explorer.
Sera hii inapowekwa, itatumiwa kufungua Google Chrome wakati inafungua Google Chrome kutoka Internet Explorer.
Sera hii inaweza kuwekwa kuwa njia ya utekelezaji wa faili au ${chrome} kutambua kiotomatiki sehemu ya usakinishaji kwenye Chrome.
Sera hii inadhibiti vipengee vya mstari wa amri katika Chrome kutoka Internet Explorer.
Ikiwa kipengele cha "Uwezo wa Kutumia Kivinjari Kilichopitwa na Wakati" cha Internet Explorer hakijasakinishwa, sera hii haina athari.
Sera hii isipowekwa, Internet Explore itapitisha tu URL kwenye Chrome kama kipengele cha mstari wa amri.
Sera hii ikiwekwa kuwa orodha ya mifuatano, mifuatano hiyo huunganishwa kwa kutumia nafasi na kupitishwa kwenye Chrome kama vipengele vya mstari wa amri.
Ikiwa kipengee kinajumuisha ${url}, nafasi yake itachukuliwa na URL ya ukurasa utakaofunguka.
Kama hakuna kipengele kinachojumuisha ${url}, URL itawekwa mwishoni mwa mstari wa amri.
Vipengele vya kimazingira hupanuliwa. Kwenye Windows, nafasi ya %ABC% inachukuliwa na thamani ya kipengele cha kimazingira cha ABC.
Sera hii inadhibiti muda unaosubiri kabla ya kufungua kivinjari mbadala katika milisekunde.
Sera hii isipowekwa au ikiwekwa kuwa 0, hatua ya kwenda kwenye URL iliyobainishwa itaifungua katika kivinjari mbadala mara moja.
Sera hii ikiwekwa kuwa nambari, Chrome inaonyesha ujumbe unaodumu milisekunde zilizobainishwa kisha inafungua kivinjari mbadala.
Sera hii inadhibiti ruhusa ya Uwezo wa Kutumia Kivinjari Kilichopitwa na Wakati.
Sera hii isipowekwa au ikiwekwa kuwa 'sivyo', Chrome haitajaribu kufungua URL zilizobainishwa katika kivinjari mbadala.
Sera hii ikiwekwa kuwa 'ndivyo', Chrome itajaribu kufungua baadhi ya URL katika kivinjari mbadala (kama vile Internet Explorer). Mipangilio ya kipengele hiki huwekwa kwa kutumia sera katika kikundi cha Legacy Browser support.
Kipengele hiki kinachukua nafasi ya kiendelezi cha 'Legacy Browser Support'. Mipangilio kutoka kiendelezi italetwa kwenye kipengele hiki, lakini tunapendekeza zaidi utumie sera za Chrome badala yake. Hali hii inahakikisha uoanifu bora zaidi katika siku zijazo.
Sera hii ni URL inayorejelea faili ya XML katika muundo sawa na sera ya Internet Explorer ya SiteList. Sera hii hupakia masharti kutoka faili ya XML, bila kushiriki masharti hayo na Internet Explorer.
Sera inapoachwa bila kuwekwa au isipowekwa kuwa URL sahihi, Google Chrome haiitumii kama chanzo cha sheria za kubadilisha vivinjari.
Sera hii inapowekwa kuwa URL sahihi, Google Chrome inapakua tovuti kutoka URL hiyo na kutumia masharti kuwa kama mipangilio iliyowekwa kwa kutumia sera ya BrowserSwitcherUrlList.
Kwa maelezo zaidi kuhusu sera ya Internet Explorer ya SiteList: https://docs.microsoft.com/internet-explorer/ie11-deploy-guide/what-is-enterprise-mode
Sera hii hubaini iwapo Chrome itafungwa kabisa wakati kichupo cha mwisho kitahamia kwenye kivinjari kingine.
Sera hii isipowekwa au ikiwekwa kuwa 'ndivyo', Chrome itasalia na angalau kichupo kimoja kilichofunguka, baada ya kuhamia kwenye kivinjari mbadala.
Sera hii ikiwekwa kuwa 'sivyo', Chrome itafunga kichupo baada ya kuhamia kwenye kivinjari mbadala hata kama kilikuwa kichupo cha mwisho. Hali hii itasababisha Chrome kufungwa kabisa.
Sera hii inadhibiti orodha ya tovuti zinazofunguliwa katika kivinjari mbadala.
Kumbuka kuwa unaweza pia kuongeza vipengee kwenye orodha hii kupitia sera ya BrowserSwitcherUseIeSitelist na BrowserSwitcherExternalSitelistUrl.
Iwapo hujaweka mipangilio ya sera hii, hamna tovuti zitakazoongezwa kwenye orodha.
Ukiweka mipangilio ya sera hii, kila kipengee kitachukuliwa kama masharti ya kufungua kitu fulani katika kivinjari mbadala. Google Chrome inatumia masharti hayo wakati unachagua iwapo URL inapaswa kufungua katika kivinjari mbadala.
Wakati programu jalizi ya Internet Explorer inapatikana na imewashwa, Internet Explorer itarudi kwenye Google Chrome iwapo masharti hayatalingana.
Iwapo masharti yanakinzana Google Chrome itatumia masharti yaliyo mahususi zaidi.
Sera hii inadhibiti orodha ya tovuti ambazo hazitawahi kusababisha kubadilishwa kwa kivinjari.
Kumbuka kuwa unaweza pia kuongeza vipengee kwenye orodha hii kupitia sera ya BrowserSwitcherUseIeSitelist na BrowserSwitcherExternalSitelistUrl.
Iwapo hujaweka mipangilio ya sera hii, hamna tovuti zinazoongezwa kwenye orodha.
Iwapo umeweka mipangilio ya sera hii, kila kipengee kitashughulikiwa kama masharti, jinsi ilivyo katika sera ya BrowserSwitcherUrlList. Hata hivyo, hali itabadilika: masharti yanayolingana hayatafungua kivinjari mbadala.
Tofauti na BrowserSwitcherUrlList, masharti yanatumika pande zote mbili. Yaani, wakati programu jalizi ya Internet Explorer inapatikana na imewashwa, inabaini pia iwapo Internet Explorer inapaswa kufungua URL hizi katika Google Chrome.
Sera hii inadhibiti iwapo utapakia masharti kutoka sera ya SiteList ya Internet Explorer.
Usipoweka sera hii, au uiweke kuwa Sivyo, Google Chrome haitatumia sera ya SiteList ya Internet Explorer kama chanzo cha masharti ya kubadilisha vivinjari.
Ukiweka sera hii kuwa Ndivyo, Google Chrome itasoma SiteList ya Internet Explorer ili ipate URL ya orodha ya tovuti. Kisha Google Chrome itapakua orodha ya tovuti kutoka URL hiyo, na kutumia masharti hayo jinsi yalivyowekwa kwenye sera ya BrowserSwitcherUrlList.
Kwa maelezo zaidi kuhusu sera ya SiteList ya Internet Explorer fungua: https://docs.microsoft.com/internet-explorer/ie11-deploy-guide/what-is-enterprise-mode
Hukuruhusu udhibiti ikiwa mashine pepe zinaruhusiwa kutumia Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome.
Ikiwa sera imewekwa kuwa Ndivyo, kifaa kinaruhusiwa kutumia mashine pepe. Ikiwa sera imewekwa kuwa Sivyo, kifaa hakitaruhusiwa kutumia mashine pepe. Sera zote tatu, VirtualMachinesAllowed, CrostiniAllowed na DeviceUnaffiliatedCrostiniAllowed inahitaji kuwekwa kuwa ndivyo wakati zinaomba Crostini iruhusiwe kutumika. Sera hii inapobadilishwa kuwa Sivyo, inaanza kutumika kwenye mashine pepe mpya lakini haizimi mashine pepe ambazo tayari zinatumika. Kama sera hii haijawekwa kwenye kifaa kinachodhibitiwa, kifaa hakiruhusiwi kutumia mashine pepe. Vifaa ambavyo havidhibitiwi vinaruhusiwa kutumia mashine pepe.
Washa ili mtumiaji huyu atumie Crostini.
Ikiwa sera imewekwa kuwa sivyo, Crostini haijawashwa ili itumiwe na mtumiaji. Ikiwa sera imewekwa kuwa ndivyo au haijawekwa, Crostini inawashwa ili itumiwe na mtumiaji kama mipangilio mingine inairuhusu. Sera hizi tatu, VirtualMachinesAllowed, CrostiniAllowed na DeviceUnaffiliatedCrostiniAllowed zinahitaji kuwekwa kuwa ndivyo wakati zinaomba Crostini iruhusiwe kutumika. Sera hii ikibadilishwa kuwa sivyo, inatumika kwa metadata mpya inayooanza ya Crostini lakini haizimi metadata ambayo tayari inatumika.
Ikiwa sera imewekwa kuwa sivyo, watumiaji wasiohusishwa hawataruhusiwa kutumia Crostini.
Ikiwa sera hii haijawekwa au imewekwa kuwa ndivyo, watumiaji wote wanaruhusiwa kutumia Crostini kama mipangilio mingine pia inairuhusu. Sera zote tatu, VirtualMachinesAllowed, CrostiniAllowed, na DeviceUnaffiliatedCrostiniAllowed zinahitaji kuwekwa kuwa ndivyo wakati zinaomba Crostini iruhusiwe kutumika. Sera hii ikibadilishwa kuwa sivyo, inatumika kwa metadata mpya inayoanza ya Crostini lakini haizimi metadata ambayo tayari inatumika.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, kiolesura cha kutuma au kuhamisha hakitapatikana kwa watumiaji, hata hivyo bado inawezakana kutumia amri za 'lxc' moja kwa moja kwenye mashine pepe ili kutuma au kupakia picha za metadata.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, kipengee cha ARC kitawashiwa mtumiaji (kutegemea kanuni za mipangilio ya ziada ya sera - kipengee cha ARC bado hakitapatikana ikiwa kipindi cha matumizi ya muda au kipengee cha kuingia katika akaunti nyingi kitawashwa katika kipindi cha sasa cha mtumiaji).
Mipangilio hii ikizimwa au isiposanidiwa, basi watumiaji wa biashara hawawezi kutumia kipengee cha ARC.
Ikiwa sera imewekwa kuwa sivyo, watumiaji wasiohusishwa hawataruhusiwa kutumia ARC.
Ikiwa sera hii imebadilishwa au imewekwa kuwa ndivyo, watumiaiji wote wanaruhusiwa kutumia ARC (ila katika hali ambapo ARC inazimwa kwa kutumia mbinu nyinginezo).
Mabadiliko kwenye sera yatatumika wakati ARC haitekelezwi tu, kwa mfano, mfumo wa uendeshaji wa Chrome unapoanza.
Hubainisha kikundi cha sera zitakazotolewa wakati ARC inatumika. Lazima thamani iwe JSON sahihi.
Sera hii inaweza kutumika kuweka mipangilio ya kubainisha programu za Android ambazo zinasakinishwa kiotomatiki kwenye kifaa:
{ "type": "object", "properties": { "applications": { "type": "array", "items": { "type": "object", "properties": { "packageName": { "description": "Android app identifier, e.g. "com.google.android.gm" for Gmail", "type": "string" }, "installType": { "description": "Specifies how an app is installed. OPTIONAL: The app is not installed automatically, but the user can install it. This is the default if this policy is not specified. PRELOAD: The app is installed automatically, but the user can uninstall it. FORCE_INSTALLED: The app is installed automatically and the user cannot uninstall it. BLOCKED: The app is blocked and cannot be installed. If the app was installed under a previous policy it will be uninstalled.", "type": "string", "enum": [ "OPTIONAL", "PRELOAD", "FORCE_INSTALLED", "BLOCKED" ] }, "defaultPermissionPolicy": { "description": "Policy for granting permission requests to apps. PERMISSION_POLICY_UNSPECIFIED: Policy not specified. If no policy is specified for a permission at any level, then the `PROMPT` behavior is used by default. PROMPT: Prompt the user to grant a permission. GRANT: Automatically grant a permission. DENY: Automatically deny a permission.", "type": "string", "enum": [ "PERMISSION_POLICY_UNSPECIFIED", "PROMPT", "GRANT", "DENY" ] }, "managedConfiguration": { "description": "App-specific JSON configuration object with a set of key-value pairs, e.g. '"managedConfiguration": { "key1": value1, "key2": value2 }'. The keys are defined in the app manifest.", "type": "object" } } } } } }
Ili kubandika programu kwenye kifungua programu, angalia PinnedLauncherApps.
Huruhusu kuripotiwa kwa matukio muhimu wakati wa kusakinisha programu ya Android kwenye Google. Matukio hurekodiwa tu kwa programu ambazo usakinishaji wake unatokana na sera.
Ikiwa sera imewekwa kuwa ndivyo, matukio yatarekodiwa. Ikiwa sera imewekwa kuwa sivyo au haijawekwa, matukio hayatarekodiwa.
Sera hii hudhibiti hali ya awali ya kipengele cha Android cha kuhifadhi na kurejesha nakala.
Mipangilio ya sera hii isipowekwa au ikiwekwa kuwa BackupAndRestoreDisabled, kipengele cha Android cha kuhifadhi na kurejesha nakala kitazimwa kwanza.
Sera hii ikiwekwa kuwa BackupAndRestoreEnabled, kipengele cha Android cha kuhifadhi na kurejesha nakala kitawashwa kwanza.
Sera hii ikiwekwa kuwa BackupAndRestoreUnderUserControl, mtumiaji ataombwa achague iwapo atatumia kipengele cha Android cha kuhifadhi na kurejesha nakala. Ikiwa mtumiaji amewasha kipengele cha kuhifadhi na kurejesha nakala, data ya programu ya Android itapakiwa kwenye seva za kuhifadhi nakala za Android na kurejeshwa kutoka seva hizo baada ya kusakinishwa tena katika programu zinazooana.
Kumbuka kwamba sera hii inadhibiti hali ya kipengele cha Android cha kuhifadhi na kurejesha data wakati wa kuweka mipangilio ya kwanza pekee. Mtumiaji anaweza kufungua mipangilio ya Android baadaye na kuwasha au kuzima kipengele cha Android cha kuhifadhi na kurejesha nakala.
Sera hii hudhibiti hali ya awali ya Huduma za Mahali za Google.
Mipangilio ya sera hii isipowekwa au ikiwekwa kuwa GoogleLocationServicesDisabled, Huduma za Mahali za Google huzimwa kwanza.
Sera hii ikiwekwa kuwa GoogleLocationServicesEnabled, Huduma za Mahali za Google huwashwa kwanza.
Sera hii ikiwekwa kuwa GoogleLocationServicesUnderUserControl, mtumiaji huulizwa ikiwa atatumia Huduma za Mahali za Google. Hali hii itaruhusu programu za Android kutumia huduma kubaini mahali kifaa kilipo. Pia itaruhusu hali ya kuwasilisha data ya mahali uliko kwa Google bila kufichua maelezo yanayoweza kukutambulisha.
Kumbuka kwamba sera hii hudhibiti hali ya Huduma za Mahali za Google wakati wa kuweka mipangilio ya kwanza pekee. Mtumiaji anaweza kufungua mipangilio ya Android baadaye na kuwasha au kuzima Huduma za Mahali za Google.
Kumbuka kwamba sera hii haitumiwi na Huduma za Mahali za Google huzimwa kila wakati sera ya DefaultGeolocationSetting inapowekwa kuwa BlockGeolocation.
Ikiwekwa kuwa SyncDisabled au isiposanidiwa, vyeti vya Google Chrome OS havitakuwepo kwa ajili ya programu za ARC.
Ikiwekwa kuwa CopyCaCerts, vyeti vyote vya CA vilivyosakinishwa kwenye ONC vyenye Web TrustBit vitapatikana kwa ajili ya programu za ARC.
Sera hii inadhibiti iwapo kipengele cha Faili za Kushiriki katika Mtandao kwenye Google Chrome OS kinaruhusiwa kwa mtumiaji.
Iwapo hujaweka mipangilio ya sera hii au umeiweka kuwa Ndiyo, watumiaji wataweza kutumia Faili za Kushiriki katika Mtandao.
Iwapo umeweka sera hii kuwa Sivyo, watumiaji hawataweza kutumia Faili za Kushiriki katika Mtandao.
Sera hii inadhibiti iwapo kipengele cha Faili za Kushiriki kwenye Mtandao cha Google Chrome OS kinapaswa kitumie NetBIOS Name Query Request protocol ili kugundua faili zinazoshirikiwa kwenye mtandao wako. Wakati sera hii imewekwa kuwa Ndivyo, kipengele cha kugundua faili za kushiriki kitatumia itifaki ya NetBIOS Name Query Request protocol ili kugundua faili zinazoshirikiwa kwenye mtandao. Sera hii inapowekwa kuwa Sivyo, kipengele cha kugundua faili za kushiriki hakitatumia itifaki ya NetBIOS Name Query Request protocol ili kugundua faili zinazoshirikiwa kwenye mtandao. Ikiwa sera hii haijawekwa, hali chaguomsingi huzimwa kwa watumiaji wanaosimamiwa kibiashara na kuwashwa kwa watumiaji wasiosimamiwa.
Sera hii inadhibiti iwapo kipengele cha Faili za Kushiriki Mtandaoni katika Google Chrome OS kitatumia NTLM kuthibitisha.
Iwapo sera hii imewekwa kuwa Ndivyo, NTLM itatumika kuthibitisha faili za kushiriki za SMB panapohitajika. Iwapo sera hii imewekwa kuwa Sivyo, kipengele cha kuthibisha cha NTLM kwenye faili za kushiriki za SMB kitazimwa.
Iwapo sera hii haijawekwa, mipangilio chaguomsingi itazimwa kwa watumiaji wanaodhibitiwa na biashara na kitawashwa kwa watumiaji wasiodhibitiwa.
Hubainisha orodha ya faili za kushiriki mtandaoni zilizowekewa mipangilio mapema.
Kila kipengee cha sera kwenye orodha huwa na sehemu mbili: "share_url" na "mode". "share_url" inapaswa kuwa URL ya kipengee cha kushiriki na "mode" inapaswa kuwa "drop_down" au "pre_mount". Hali ya "drop_down" inaashiria kuwa "share_url" itaongezwa kwenye menyu kunjuzi ya kutambua kipengee cha kushiriki. Hali ya "pre_mount" inaashiria kuwa "share_url" itawekwa.
Huwasha kipengele cha Kuvinjari Salama cha Google Chromena huzuia watumiaji kubadilisha mpangilio huu.
Ukiwasha mipangilio hii, kipengele cha Kuvinjari Salama kitatumika kila wakati.
Ukizima mipangilio hii, kipengele cha Kuvinjari Salama hakitatumika kamwe.
Ukiwasha au uzime mipangilio hii, watumiaji hawawezi kubadilisha au kufuta mipangilio ya "Ruhusu ulinzi dhidi ya wizi wa data na programu hasidi" katika Google Chrome.
Ikiwa sera hii haitawekwa, mipangilio hii itawashwa lakini mtumiaji hataweza kuibadilisha.
Angalia https://developers.google.com/safe-browsing ili upate maelezo zaidi kuhusu Kuvinjari Salama.
Sera hii inapatikana kwenye matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®. au matukio ya Windows 10 Pro au Enterprise yaliyojumuishwa katika usimamizi wa kifaa.
Huwasha Kipengele cha Kuripoti kwa Upana Kuvinjari Salama cha Google Chrome na huzuia watumiaji wasibadilishe mipangilio hii.
Kipengele cha Kuripoti kwa Upana hutuma baadhi ya maelezo ya mfumo na maudhui ya ukurasa kwenye seva za Google ili kusaidia kutambua programu na tovuti hatari.
Kama mipangilo imewekwa kuwa ndivyo, basi ripoti zitaundwa na kutumwa wakati wowote zinapohitajika (kwa mfano, wakati ambapo skrini ya usalama inaonyeshwa).
Kama mipangilo imewekwa kuwa sivyo, ripoti hazitawahi kutumwa.
Kama sera imewekwa kuwa ndivyo au sivyo, watumiaji hawataweza kubadilisha mipangilio.
Kama sera hii haijawekwa, mtumiaji ataweza kubadilisha mipangilio na kuamua ikiwa atatuma au hatatuma ripoti.
Angalia https://developers.google.com/safe-browsing ili upate maelezo zaidi kuhusu Kuvinjari Salama.
Mipangilio hii haitumiki tena, tumia SafeBrowsingExtendedReportingEnabled badala yake. Kuwasha au kuzima SafeBrowsingExtendedReportingEnabled ni sawa na kuweka mipangilio ya SafeBrowsingExtendedReportingOptInAllowed kuwa Sivyo.
Kuweka sera hii kuwa sivyo kunazuia watumiaji wasichague kutuma baadhi ya maelezo ya mfumo na maudhui ya ukurasa kwenye seva za Google. Ikiwa mipangilio hii imewekwa kuwa ndivyo au haijawekwa, basi watumiaji wataruhusiwa kutuma baadhi ya maelezo ya mfumo na maudhui ya ukurasa kwenye kipengele cha Kuvinjari Salama ili kusaidia kugundua programu na tovuti hatari.
Angalia https://developers.google.com/safe-browsing ili upate maelezo zaidi kuhusu Kuvinjari Salama.
Weka mipangilio ya orodha ya vikoa ambavyo kipengele cha Kuvinjari Salama kitaamini. Hii inamaanisha: Kipengele cha Kuvinjari Salama hakitakagua nyenzo hatari (kwa mfano, wizi wa data ya binafsi, programu hasidi na programu zisizotakikana) ikiwa URL zake zinalingana na vikoa hivi. Huduma ya ulinzi wa upakuaji katika kipengele cha Kuvinjari Salama haitakagua vipakuliwa vitakavyopangishwa kwenye vikoa hivi. Huduma ya ulinzi wa manenosiri katika kipengele cha Kuvinjari Salama haitakagua utumiaji tena wa manenosiri ikiwa URL ya ukurasa italingana na vikoa hivi.
Mipangilio hii ikiwashwa, basi kipengele cha Kuvinjari Salama kitaamini vikoa hivi. Kama mipangilio hii imezimwa au haijawekwa, basi itatumia ulinzi chaguomsingi wa Kuvinjari Salama katika nyenzo zote. Sera hii inapatikana kwenye matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®. au matukio ya Windows 10 Pro au Enterprise yaliyojumuishwa katika usimamizi wa kifaa.
Inakuruhusu udhibiti utoaji wa onyo la ulinzi wa nenosiri. Kipengele cha ulinzi wa nenosiri huarifu watumiaji wakati wanatumia tena nenosiri linalolindwa kwenye tovuti zinazotiliwa shaka.
Unaweza kutumia sera za 'PasswordProtectionLoginURLs' na 'PasswordProtectionChangePasswordURL' kuweka mipangilio ya nenosiri utakalolinda.
Iwapo mipangilio ya sera hii imewekwa kuwa 'PasswordProtectionWarningOff', hamna onyo la ulinzi wa nenosiri litakaloonyeshwa. Iwapo mipangilio ya sera hii imewekwa kuwa 'PasswordProtectionWarningOnPasswordReuse', onyo la ulinzi wa nenosiri litaonyeshwa wakati mtumiaji anatumia tena nenosiri linalolindwa kwenye tovuti ambayo haijaidhinishwa. Iwapo mipangilio ya sera hii imewekwa kuwa 'PasswordProtectionWarningOnPhishingReuse', onyo la ulinzi wa nenosiri litaonyeshwa wakati mtumiaji anatumia tena nenosiri lake linalolindwa kwenye tovuti inayoiba data binafsi. Iwapo mipangilio ya sera hii haijawekwa, huduma ya ulinzi wa nenosiri italinda tu manenosiri ya Google lakini mtumiaji yule mwingine ataweza kubadilisha mipangilio hii.
Weka mipangilio ya orodha ya URL za kuingia katika akaunti ya biashara (Mifumo ya HTTP na HTTPS pekee). Alama bainifu ya nenosiri itarekodiwa kwenye URL hizi na kutumika katika utambuzi wa kutumia nenosiri tena. Ili Google Chrome irekodi alama bainifu za nenosiri kwa usahihi, tafadhali hakikisha kuwa kurasa za kuingia katika akaunti zinafuata mwongozo kwenye https://www.chromium.org/developers/design-documents/create-amazing-password-forms.
Kama mipangilio hii imewashwa, basi huduma ya ulinzi wa manenosiri itarekodi alama bainifu ya nenosiri kwenye URL hizi kwa madhumuni ya utambuzi wa kutumia nenosiri tena. Ikiwa mipangilio hii imezimwa au haijawekwa, basi huduma ya ulinzi wa manenosiri itarekodi alama bainifu ya nenosiri kwenye https://accounts.google.com. Sera hii inapatikana kwenye matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®. au matukio ya Windows 10 Pro au Enterprise yaliyojumuishwa katika usimamizi wa kifaa.
Weka mipangilio ya URL ya kubadilisha nenosiri (Mifumo ya HTTP na HTTPS pekee). Huduma ya ulinzi wa manenosiri itawaelekeza watumiaji kwenye URL hii ili wabadilishe manenosiri yao baada ya kuona ilani katika kivinjari. Ili Google Chrome iweze kurekodi vizuri alama bainifu ya nenosiri jipya kwenye ukurasa huu wa kubadilisha nenosiri, tafadhali hakikisha kuwa ukurasa wa kubadilisha nenosiri lako unafuata mwongozo ulio kwenye https://www.chromium.org/developers/design-documents/create-amazing-password-forms.
Iwapo umewasha mipangilio hii, inamaanisha kuwa huduma ya ulinzi wa nenosiri itaelekeza watumiaji kwenye URL hii ili wabadilishe nenosiri lao baada ya kuona onyo katika kivinjari. Iwapo mipangilio imezimwa au haijawekwa, inamaanisha kuwa huduma ya ulinzi wa nenosiri itaelekeza watumiaji kwenye https://myaccounts.google.com ili wabadilishe nenosiri lao. Sera hii inapatikana kwenye matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®. au matukio ya Windows 10 Pro au Enterprise yaliyojumuishwa katika usimamizi wa kifaa.
Hukuruhusu kuweka iwapo tovuti zinaruhusiwa kuweka data ya ndani. Kuweka data ya ndani kunaweza kuruhusiwa kwa tovuti zote au kukataliwa kwa tovuti zote.
Sera hii ikiwekwa 'Weka vidakuzi kwa muda wa kipindi' basi vidakuzi vitafutwa kipindi kikifungwa. Kumbuka kwamba ikiwa Google Chrome inatekeleza katika 'hali ya chini chini', huenda kipindi kisifungwe wakati dirisha la mwisho litakapofungwa. Tafadhali angalia sera ya 'BackgroundModeEnabled' kwa maelezo zaidi kuhusu kusanidi tabia hii.
Sera hii ikiachwa bila kuwekwa, kipengee cha 'AllowCookies' kitatumiwa na mtumiaji ataweza kukibadilisha.
Inakuruhusu kuweka iwapo tovuti zinaruhusiwa kuonyesha picha. Kuonyesha picha kunaweza kuwa kwa tovuti zote au kukataliwa kwa tovuti zote.
Ikiwa sera hii itasalia kama haijawekwa, 'AllowImages' itatumiwa na mtumiaji ataweza kuibadilisha.
Kumbuka kuwa hapo awali sera hii iliwashwa kimakosa kwenye Android, lakini kipengele hiki hakijawahi kutumika kikamilifu kwenye Android.
Inakuruhusu kuweka iwapo tovuti zinaruhusiwa kuendesha JavaScript. Kuendesha JavaScript kunaweza kuruhusiwa kwa tovuti zote au kukataliwa kwa tovuti zote.
Ikiwa sera hii itasalia kama haijawekwa, 'AllowJavaScript' itatumiwa na mtumiaji ataweza kuibadilisha.
Hukuruhusu kuweka iwapo tovuti zinaruhusiwa kutekeleza kiotomatiki programu jalizi ya Flash. Kutekeleza programu jalizi ya Flash kiotomatiki kunaweza aidha kuruhusiwa kwa tovuti zote au kukataliwa kwa tovuti zote.
Kubofya ili kucheza kutaruhusu programu jalizi ya Flash kutekelezwa lakini mtumiaji lazima abofye kwenye kishika nafasi ili kuitekeleza.
Uchezaji tena wa kiotomatiki huruhusiwa kwa vikoa vilivyoorodheshwa wazi katika sera ya PluginsAllowedForUrls. Kama ungependa kuwasha uchezaji kiotomatiki wa tovuti zote zingatia kuongeza http://* na https://* kwenye orodha hii.
Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa, mtumiaji ataweza kubadilisha mipangilio hii yeye mwenyewe.
Inakuruhusu kuweka ikiwa tovuti zinaruhusiwa kuonyesha ibukizi. Kuonyesha ibukizi kunaweza kuruhusiwa kwa tovuti zote au kukataliwa kwa tovuti zote.
Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa, 'BlockPopups' itatumiwa na mtumiaji ataweza kuibadilisha.
Inakuruhusu kuweka iwapo tovuti zinaruhusiwa kuonyesha arifa. Kuonyesha arifa za eneo-kazi kunaweza kuruhusiwa kwa chaguomsingi, kukataliwa kwa chaguomsingi au mtumiaji anawewa kuulizwa kila wakati tovuti inayotaka kuonyesha arifa za eneo-kazi.
Ikiwa sera hii itasalia kama haijawekwa, 'AskNotifications' itatumika na mtumiaji ataweza kuibadilisha.
Inaruhusu iwapo tovuti zinaruhusiwa kufuatilia eneo halisi la mtumiaji. Kufuatilia eneo halisi la mtumiaji kunaweza kuruhusiwa kwa chaguomsingi, kukataliwa kwa chaguomsingi au mtumiaji anaweza kuulizwa kila wakati tovuti ambayo inaomba eneo halisi.
Ikiwa sera hii itasalia kama haijawekwa, 'AskGeolocation' itatumika na mtumiaji ataweza kuibadilisha.
Sera hii ikiwekwa kuwa BlockGeolocation, programu za Android haziwezi kufikia maelezo ya mahali. Ukiweka sera hii kuwa thamani nyingine yoyote au uiache bila kuiweka, mtumiaji ataombwa akubali programu ya Android inapotaka kufikia maelezo ya mahali.
Inakuruhusu kuweka ikiwa tovuti zinaruhusiwa kufikia vifaa vya media vya kunasa. Ufikivu wa vifaa vya media vya kunasa unaweza kuruhusiwa kwa chaguomsingi, au mtumiaji anaweza kuulizwa kila wakati tovuti inapotaka kufikia vifaa vya media vya kunasa.
Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa, 'PromptOnAccess' itatumiwa na mtumiaji ataweza kuibadilisha.
Hukuruhusu kuweka ikiwa tovuti zinaruhusiwa kupata idhini ya kufikia vifaa vya karibu vya Bluetooth. Idhini ya kufikia inaweza kuzuiwa kabisa, au mtumiaji anaweza kuulizwa kila wakati tovuti inapotaka kufikia vifaa vya karibu vya Bluetooth.
Sera hii ikiachwa bila kuwekwa, chaguo la '3' litatumiwa, na mtumiaji ataweza kulibadilisha.
Hukuruhusu ubaini ikiwa tovuti zinaruhusiwa kupata idhini ya kufikia vifaa vya USB vilivyounganishwa. Idhini ya ufikiaji inaweza kuzuiwa kabisa, au mtumiaji anaweza kuulizwa kila wakati atoe adhini tovuti inapotaka kufikia vifaa vya USB vilivyounganishwa.
Sera hii inaweza kubatilishwa katika ruwaza mahususi ya URL kupitia sera za 'WebUsbAskForUrls' na 'WebUsbBlockedForUrls'.
Sera hii ikiachwa bila kuwekwa, '3' itatumiwa na mtumiaji ataweza kuibadilisha.
Inakuruhusu kubanisha orodha ya miundo ya url inayobainisha tovuti ambako Google Chrome inafaa kuteua kiotomatiki cheti ya kiteja, ikiwa tovuti itaomba cheti.
Ni lazima thamani iwe mkusanyiko wa kamusi za JSON katika maandishi. Ni lazima kila kamusi iwe na muundo wa { "pattern": "$URL_PATTERN", "filter" : $FILTER }, ambapo $URL_PATTERN ni muundo wa mipangilio ya maudhui. $FILTER hudhibiti vyeti vya kiteja ambako kivinjari kitachagua kiotomatiki. Bila kutegemea kichujio, itachagua tu vyeti ambavyo vitalingana na ombi la cheti kwenye seva. Kwa mfano, ikiwa $FILTER ina muundo wa { "ISSUER": { "CN": "$ISSUER_CN" } }, wa zaidi, itachagua tu ni vyeti vya kiteja ambavyo vitatolewa na cheti chenye CommonName $ISSUER_CN. Ikiwa $FILTER inajumuisha sehemu ya "ISSUER" na "SUBJECT", cheti cha kiteja kinapaswa kutimiza masharti yote mawili ili kichaguliwe. Ikiwa $FILTER inabainisha shirika ("O"), ni lazima cheti kiwe na angalau shirika moja ambalo linalingana na thamani iliyobainishwa ili kichaguliwe. Ikiwa $FILTER inabainisha kitengo cha shirika ("OU"), ni lazima cheti kiwe na angalau kitengo kimoja cha shirika kinacholingana na thamani iliyobainishwa ili kichaguliwe. Ikiwa $FILTER ni kamusi isiyo na kitu {}, uteuzi wa cheti cha kiteja haudhibitiwi kwa njia ya ziada.
Sera hii isipowekwa, hakuna uteuzi wa kiotomatiki utakaofanyika kwenye tovuti yoyote.
Hukuruhusu kuunda orodha ya ruwaza za url inayobainisha tovuti zinazoruhusiwa kuweka vidakuzi.
Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa, thamani chaguomsingi itatumiwa kwa tovuti zote kutoka kwenye sera ya 'DefaultCookiesSetting' endapo itawekwa, au mtumiaji akiweka mipangilio mwenyewe.
Angalia pia sera za 'CookiesBlockedForUrls' na 'CookiesSessionOnlyForUrls'. Kumbuka kuwa hakufai kuwa na ruwaza ya URL inayokinzana kati ya sera hizi tatu - haijabainishwa ni sera ipi inayopewa kipaumbele.
Inakuruhusu kuweka orodha ya ruwaza za url zinayobainisha tovuti zinazoruhusiwa kuweka vidakuzi. Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa, thamani chaguomsingi itatumiwa kwa tovuti zote kutoka kwenye sera ya 'DefaultCookiesSetting' endapo itawekwa, au mtumiaji akiweka mipangilio mwenyewe. Angalia pia sera za 'CookiesAllowedForUrls' na 'CookiesSessionOnlyForUrls'. Kumbuka kuwa hakufai kuwa na ruwaza za URL zinazokinzana kati ya sera hizi tatu - haijabainishwa ni sera ipi inayopewa kipaumbele.
Vidakuzi vilivyowekwa na kurasa zinavyolingana na ruwaza hizi za URL vitatumika tu katika kipindi cha sasa, yaani, vitafutwa unapofunga kivinjari.
Kwa URL ambazo hazijajumuishwa katika ruwaza zilizotajwa hapa, au kwa URL zote ikiwa sera hii haijawekwa, thamani ya jumla ya chaguomsingi itatumika kutoka kwenye sera ya 'DefaultCookiesSetting', ikiwa imewekwa au mipangilio binafsi ya mtumiaji ikiwa haikuwekwa.
Kumbuka kuwa ikiwa Google Chrome inatumika katika 'hali ya chinichini', huenda kipindi kisifungwe wakati kidirisha cha mwisho kitafungwa lakini badala yake kitaendelea kutumika hadi kivinjari kitakapofungwa. Tafadhali angalia sera ya 'BackgroundModeEnabled' kwa maelezo zaidi kuhusu kuweka mipangilio kulingana na sifa hizi.
Angalia sera za 'CookiesAllowedForUrls' na 'CookiesBlockedForUrls' pia. Kumbuka kuwa hakufai kuwa na ruwaza ya URL inayokinzana kati ya sera hizi tatu - haijabainishwa ni sera ipi inayopewa kipaumbele.
Ikiwa sera ya "RestoreOnStartup" imewekwa kuwa rejesha URL kutoka vipindi vya awali sera hii haitazingatiwa na vidakuzi vitawekwa kwenye tovuti hizo bila uwezekano wa kuviondoa.
Inakuruhusu kuweka orodha ya ruwaza za url zinazobainisha tovuti zinazoruhusiwa kuonyesha picha.
Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa, thamani chaguomsingi itatumiwa kwa tovuti zote kutoka kwenye sera ya 'DefaultImageSetting' endapo itawekwa, au mtumiaji akiweka mipangilio mwenyewe.
Kumbuka kuwa hapo awali sera hii iliwashwa kimakosa kwenye Android, lakini kipengele hiki hakijawahi kutumika kikamilifu kwenye Android.
Inakuruhusu kuweka orodha ya ruwaza za url zinazobainisha tovuti zisizoruhusiwa kuonyesha picha. Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa, thamani chaguomsingi itatumiwa kwa tovuti zote kutoka kwenye sera ya 'DefaultImagesSetting' endapo itawekwa, au mtumiaji akiweka mipangilio mwenyewe. Kumbuka kuwa hapo awali sera hii iliwashwa kimakosa kwenye Android, lakini kipengele hiki hakijawahi kutumika kikamilifu kwenye Android.
Inakuruhusu kuweka orodha ya ruwaza za url ambazo zinabainisha tovuti ambazo zinaruhusiwa kuendesha JavaScript.
Ikiwa sera hii itasalia kama haijawekwa thamani yote chaguomsingi itatumiwa kwa tovuti zote kutoka kwenye sera ya 'DefaultJavaScriptSetting' ikiwa imewekwa, au vinginevyo usanidi binafsi wa mtumiaji.
Inakuruhusu kuweka orodha ya ruwaza za url ambazo zinabainisha tovuti ambazo haziruhusiwi kuendesha JavaScript.
Ikiwa sera hii itasalia kama haijawekwa thamani chaguomsingi ya ulimwenguni itatumiwa aidha kutoka kwenye sera ya 'DefaultJavaScriptSetting' ikiwa imewekwa, au vinginevyo usanidi binafsi wa mtumiaji.
Hukuruhusu kuweka orodha ya ruwaza za url inayobainisha tovuti zinazoruhusiwa kutumia programu jalizi ya Flash.
Ikiwa sera hii haitawekwa, thamani chaguomsingi itatumiwa kwa tovuti zote kutoka kwenye sera ya 'DefaultPluginsSetting' endapo itawekwa, au mtumiaji akiweka mipangilio mwenyewe.
Hukuruhusu kuweka orodha ya ruwaza za url inayobainisha tovuti zisizoruhusiwa kutumia programu jalizi ya Flash.
Ikiwa sera hii haitawekwa, thamani chaguomsingi itatumiwa kwa tovuti zote kutoka kwenye sera ya 'DefaultPluginsSetting' endapo itawekwa, au mtumiaji akiweka mipangilio mwenyewe.
Inakuruhusu kuweka orodha ya ruwaza za url ambazo zinabainisha tovuti ambazo zinaruhusiwa kufungua ibukizi.
Ikiwa sera hii itasalia kama haijawekwa thamani yote chaguomsingi itatumiwa kwa tovuti zote kutoka kwenye sera ya 'DefaultPopupsSetting' ikiwa imewekwa, au vinginevyo usanidi binafsi wa mtumiaji.
Hukuruhusu kusajili orodha ya vishikilizi vya itifaki. Hii inaweza kuwa sera iliyopendekezwa pekee. Sifa |protocol| inastahili kuwekwa kuwa mpango kama vile 'mailto' na sifa |url| inastahili kuwekwa kuwa mpangilio wa URL ya programu inayoshikilia mpango. Mpangilio unajumuisha '%s', ambayo ikiwepo itabadilishwa na URL iliyoshikiliwa.
Vishikilizi vya itifaki vilivyosajiliwa na sera vinaunganishwa na vilivyosajiliwa na mtumiaji na vyote viwili vinapatikana kwa matumizi. Mtumiaji anaweza kubatilisha vishikilizi vya itifaki vilivyosakinishwa na sera kwa kusakinisha kishikilizi kipya cha chaguomsingi, lakini hawezi kuondoa kishikilizi cha itifaki kilichosajiliwa na sera.
Vidhibiti vya itifaki vilivyowekwa kupitia sera hii havitumiwi wakati wa kushughulikia utaratibu wa kuratibu wa Android.
Inakuruhusu kuweka orodha ya ruwaza za url zinazobainisha tovuti zisizoruhusiwa kufungua ibukizi.
Ikiwa sera hii itaachwa bila thamani chaguomsingi yote itatumiwa kwa tovuti zote kutoka kwenye sera ya 'DefaultPopupeSetting' ikiwa imewekwa, au vinginevyo usanidi binafsi wa mtumiaji.
Inakuruhusu kuweka orodha ya ruwaza za url ambazo zinabainisha tovuti ambazo zinaruhusiwa kuonyesha arifa.
Ikiwa sera hii itasalia kama haijawekwa thamani yote chaguomsingi itatumiwa kwa tovuti zote kutoka kwenye sera ya 'DefaultNotificationsSetting' ikiwa imewekwa, au vinginevyo usanidi binafsi wa mtumiaji.
Inakuruhusu kuweka orodha ya ruwaza za url ambazo zinabainisha tovuti ambazo haziruhusiwi kuonyesha arifa.
Ikiwa sera hii itasalia kama haijawekwa thamani yote chaguomsingi itatumika kwa tovuti zote kutoka katika sera ya 'DefaultNotificationsSetting' ikiwa imewekwa, au vinginevyo usanidi binafsi wa mtumiaji.
Hukuruhusu kuweka orodha ya urls ambazo zinabainisha tovuti zitakazopewa ruhusa kiotomatiki ya kufikia kifaa cha USB chenye Vitambulisho husika vya muuzaji na bidhaa. Lazima kila kipengee kwenye orodha kijumuishe vifaa na urls ili sera itumike. Kila kipengee kwenye vifaa kinaweza kujumuisha sehemu ya Kitambulisho cha muuzaji na Kitambulisho cha bidhaa. Kitambulisho chochote kisichowekwa kinachukuliwa kuwa herufi wakilishi isiyofuata kanuni moja na kanuni hii ni kwamba kitambulisho cha bidhaa hakiwezi kubainishwa bila kitambulisho cha muuzaji kubainishwa pia. Vinginevyo, sera haitakuwa sahihi na itapuuzwa.
Muundo wa ruhusa za USB hutumia URL ya tovuti inayotuma ombi ("URL inayotuma ombi") na URL ya tovuti maarufu ya fremu ("URL iliyopachikwa") ili kutoa ruhusa kwa URL inayotuma ombi iweze kufikia kifaa cha USB. URL inayotuma ombi inaweza kuwa tofauti na URL iliyopachikwa wakati tovuti inayotuma ombi imepakiwa kwenye iframe. Kwa hivyo, sehemu ya "urls" inaweza kujumuisha hadi mifuatano miwili ya URL inayotenganishwa kwa koma ili kubainisha URL ya kutuma ombi na URL iliyopachikwa mtawalia. Ikiwa URL moja tu imebainishwa, basi ufikiaji wa vifaa vinavyolingana vya USB utatolewa wakati URL ya tovuti inayotuma ombi inalingana na URL hii bila kuzingatia hali ya upachikwaji. Lazima URL kwenye "urls" ziwe URL sahihi, vinginevyo sera hii itapuuzwa.
Sera hii isipowekwa, thamani chaguomsingi ya jumla itatumiwa kwenye tovuti zote, kutoka sera ya 'DefaultWebUsbGuardSetting' ikiwa sera imewekwa au vinginevyo kutoka mipangilio ya binafsi ya mtumiaji.
Ruwaza za URL katika sera hii hazipaswi kukinzana na zile ambazo mipangilio yake huwekwa kupitia WebUsbBlockedForUrls. Kama zinakinzana, sera hii itatumika kwanza kabla ya WebUsbBlockedForUrls na WebUsbAskForUrls.
Hukuruhusu uweke orodha ya ruwaza za url ambayo inabainisha tovuti zinazoruhusiwa kumuuliza mtumiaji atoe ruhusa ya kufikia kifaa cha USB.
Ikiwa sera hii haitawekwa, thamani chaguomsingi itatumiwa kwa tovuti zote kutoka sera ya 'DefaultPluginsSetting' endapo itawekwa. Vinginevyo, itatumia mipangilio ya binafsi ya mtumiaji.
Ruwaza ya URL haipaswi kukinzana na ile ambayo imewekwa kupitia WebUsbAskForUrls. Haijabainishwa ni ipi kati ya sera hizi mbili inayofaa kuanza iwapo URL inafanana na zote mbili.
Hukuruhusu uweke orodha ya ruwaza za url ambayo inabainisha tovuti zinazozuiliwa ili zisimuulize mtumiaji atoe ruhusa ya kufikia kifaa cha USB.
Ikiwa mipangilio ya sera hii haitawekwa, thamani chaguomsingi itatumiwa kwa tovuti zote kutoka sera ya 'DefaultWebUsbGuardSetting' endapo itawekwa. Vinginevyo, itatumia mipangilio ya binafsi ya mtumiaji.
Ruwaza ya URL haipaswi kukinzana na ile ambayo imewekwa kupitia WebUsbAskForUrls. Haijabainishwa ni ipi kati ya sera hizi mbili inayofaa kuanza iwapo URL inafanana na zote mbili.
Hubainisha akaunti za kifaa cha karibu nawe cha kuonyeshwa kwenye skrini ya kuingia.
Kila ingizo la orodha hubainisha kitambulishi, kinachotumiwa ndani kutambua akaunti tofauti za kifaa cha karibu nawe zilizo mbali.
Kuingia kiotomatiki katika akaunti iliyo kwenye kifaa baada ya ucheleweshaji.
Ikiwa sera imewekwa, itaingia kiotomatiki kwenye akaunti katika kipindi kilichobainishwa baada ya kipindi cha muda kupita katika skrini ya kuingia bila mtumiaji kuchukua hatua yoyote. Mipangilio ya akaunti iliyo kwenye kifaa lazima iwe imewekwa tayari (angalia|DeviceLocalAccounts|).
Ikiwa sera hii haijawekwa, haitaingia katika akaunti kiotomatiki.
Ucheleweshaji wa kuingia kiotomatiki katika akaunti ya kifaa.
Ikiwa sera ya |DeviceLocalAccountAutoLoginId| haijawekwa, sera hii haina athari yoyote. Vinginevyo:
Sera hii ikiwekwa, inabainisha kiasi cha muda ambacho kinaweza kupita bila shughuli ya mtumiaji kabla kuingia kiotomatiki katika akaunti ya kifaa inayobainishwa na sera ya |DeviceLocalAccountAutoLoginId|.
Ikiwa sera haitawekwa, muda utakwisha baada ya milisekunde 0.
Sera hii inabainishwa kwa milisekunde.
Washa njia mkato ya kibodi ya usaidizi wa uingiaji otomatiki.
Iwapo sera hii haijawekwa au imewekwa kwenye Ruhusu na akaunti ya ndani ya kifaa imesanidiwa kwa kutochelewa wakati wa kuingia otomatiki, Google Chrome OS itaheshimu njia mkato ya kibodi ya Ctrl+Alt+S kwa kukwepa kuingia otomatiki na kuonyesha skrini ya kuingia.
Iwapo sera hii imewekwa kwenye Uongo, kuingia bila kuchelewa (iwapo kumesanidiwa) hakuwezi kukwepwa.
Washa ombi la usanidi wa mtandao inapokuwa nje ya mtandao.
Sera hii isipowekwa au ikiwekwa kuwa Ndivyo na akaunti ya kifaa ya karibu isanidiwe kwa kuingia kiotomatiki pasipo kuchelewa na kifaa kiwe hakina ufikiaji kwa Intaneti, Google Chrome OS itaonyesha ombi la kusanidi mtandao.
Sera hii ikiwekwa kuwa Sivyo, ujumbe wa hitilafu utaonyeshwa badala ya ombi la kusanidi mtandao.
Ikiwa utaruhusu programu inayotumia skrini nzima kufunguka kiotomatiki bila kuchelewa ili kudhibiti toleo la Google Chrome OS.
Sera hii hudhibiti ikiwa utaruhusu programu inayotumia skrini nzima kufunguka kiotomatiki bila kuchelewa ili kudhibiti toleo la Google Chrome OS kwa kutaja required_platform_version katika faili yake ya maelezo na kuitumia kama kiambishi awali cha toleo la kusasisha kiotomatiki.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, thamani ya ufunguo wa faili ya maelezo ya required_platform_version ya programu inayotumia skrini nzima kufunguka kiotomatiki bila kuchelewa itatumiwa kama kiambishi awali cha toleo la kusasisha kiotomatiki.
Sera hii isipowekwa au ikiwekwa kuwa sivyo, ufunguo wa faili ya maelezo ya required_platform_version utapuuzwa na kipengele cha kusasisha kiotomatiki kuendelea kama kawaida.
Onyo: Unashauriwa kutohawilisha udhibiti wa toleo la Google Chrome OS kwenye programu ya skrini nzima kwa sababu inaweza kuzuia kifaa kupokea masasisho ya programu na marekebisho muhimu ya usalama. Kuhawilisha udhibiti wa toleo la Google Chrome OS kunaweza kuhatarisha hali ya watumiaji.
Ikiwa programu inayotumia skrini nzima ni programu ya Android, haiwezi kudhibiti toleo la Google Chrome OS, hata kama sera hii itawekwa kuwa True.
Hubainisha muda (katika siku) ambayo mteja huchukua ili kubadilisha nenosiri la akaunti ya mashine. Nenosiri huzalishwa bila mpangilio wowote na mteja na halionekani kwa mtumiaji.
Kama ilivyo katika manenosiri ya mtumiaji, ni sharti manenosiri ya mashine yabadilishwe mara kwa mara. Kuzima sera hii au kuweka idadi nyingi ya siku kunaweza kuwa na athari mbaya kwa usalama kwa sababu hali hii huwapa wavamizi wa akaunti muda zaidi wa kupata na kutumia nenosiri la akaunti ya mashine.
Ikiwa sera hii haijawekwa, nenosiri la akaunti ya mashine litabadilishwa baada ya kila siku 30.
Kama sera hii imewekwa kuwa 0, kipengele cha kubadilisha nenosiri la akaunti ya mashine itazimwa.
Kumbuka kwamba manenosiri huenda yakawa ya zamani zaidi kuliko siku zilizobainishwa ikiwa mteja amekuwa nje ya mtandao kwa muda mrefu zaidi.
Hubainisha uwezekano na utaratibu wa kuchakata sera ya mtumiaji kutoka kompyuta ya GPO.
Kama sera imewekwa kuwa 'Chaguomsingi' au kama haijawekwa, sera ya mtumiaji inasomwa tu kutoka GPO ya mtumiaji (GPO za kompyuta hazizingatiwi).
Kama sera imewekwa kuwa 'Unganisha', sera ya mtumiaji katika GPO za mtumiaji zitaunganishwa na sera ya mtumiaji katika GPO za kompyuta (GPO za kompyuta hupendelewa).
Kama sera imewekwa kuwa 'Badilisha', sera ya mtumiaji katika GPO za mtumiaji inabadilishwa na sera ya mtumiaji katika GPO za kompyuta (GPO za mtumiaji hazizingatiwi).
Huweka aina za usimbaji ambazo zinaruhusiwa wakati wa kuomba tiketi za Kerberos kutoka seva ya Microsoft® Active Directory®.
Kama sera imewekwa kuwa 'Zote', aina ya usimbaji wa AES 'aes256-cts-hmac-sha1-96' na' aes128-cts-hmac-sha1-96' na pia aina ya usimbaji wa RC4 wa 'rc4-hmac' zitaruhusiwa. Usimbaji wa AES hupendelewa zaidi ikiwa seva inatumia aina zote mbili za usimbaji. Kumbuka kuwa RC4 si salama na ni sharti seva iwekewe mipangilio upya ikiwezekana ili itumie usimbaji wa AES.
Kama sera imewekwa kuwa 'Thabiti' au haijawekwa, aina za usimbaji wa AES ndizo zitaruhusiwa.
Kama sera imewekwa kuwa 'Iliyopitwa na Wakati', aina ya usimbaji wa RC4 ndio unaruhusiwa pekee. Chaguo hili si salama na linahitajika katika hali maalum pekee.
Pia angalia https://wiki.samba.org/index.php/Samba_4.6_Features_added/changed#Kerberos_client_encryption_types.
Hubainisha muda wa siku zote (katika saa) wa akiba ya Kipengee cha Sera ya Kikundi (GPO). Badala ya kupakua tena Vipengee vya Sera za Kikundi kwa kila sera inayoletwa, mfumo huenda ukatumia tena akiba ya Vipenge vya Sera za Kikundi ikiwa toleo lake halibadiliki. Sera hii inabainisha upeo wa muda ambao akiba ya Vipengee vya Sera za Kikundi inaweza kutumiwa tena kabla ya kupakuliwa tena. Kuwasha tena au kuondoka katika akaunti hufuta akiba.
Sera hii isipowekwa, akiba ya Vipengee vya Sera za Kikundi (GPO) huenda zikatumiwa tena kwa hadi saa 25.
Sera hii ikiwekwa kuwa 0, uwekaji wa akiba ya Vipengee vya Sera za Kikundi (GPO) huzimwa. Kumbuka kwamba hatua hii huongeza utendaji wa seva kwa kuwa Vipengee vya Sera za Kikundi (GPO), hupakuliwa tena kila sera inapoletwa, hata kama hazikubadilika.
Hubainisha muda wa siku zote (katika saa) wa akiba ya data ya uthibitishaji. Akiba inatumiwa kuharakisha kuingia katika akaunti. Inajumuisha data ya jumla (jina la kikundi cha kazi n.k.) kuhusu sehemu zinazohusiana, kwa mfano, sehemu zinazoaminiwa na upande wa mashine. Hakuna data inayombainisha mtumiaji na hakuna data ya sehemu zisizohusiana inayowekewa akiba. Kuwasha kifaa tena hufuta akiba.
Sera isipowekwa, akiba ya data ya uthibitishaji huenda ikatumika tena kwa hadi saa 73.
Sera ikiwekwa kuwa 0, kipengele cha kuweka akiba ya data ya uthibitishaji huzimwa. Hali hii inaweza kupunguza kasi ya kuingia katika akaunti ya watumiaji wanaohusiana kwa kuwa data ya sehemu mahususi huletwa kila unapoingia katika akaunti.
Kumbuka kwamba data ya sehemu huwekwa hata kwa watumiaji wa muda mfupi. Akiba sharti izimwe ikiwa ufuatiliaji wa sehemu za watumiaji wa muda mfupi inapaswa kuzuiwa.
Ikiwa sera hii itawekwa kwenye Ndivyo au haitasanidiwa, Google Chrome OS haitawezesha uingiaji wa mgeni. Uingiaji wa mgeni ni vipindi visivyojulikana vya mtumiaji na havihitaji nenosiri..
Ikiwa sera hii itawekwa kwenye Sivyo, Google Chrome OS haitaruhusu vipindi vya mgeni kuanzishwa.
Hubainisha orodha ya watumiaji ambao wanaruhusiwa kuingia katika akaunti kwenye kifaa. Hoja zinazowekwa ni za muundo wa user@domain, kama vile madmax@managedchrome.com. Ili kuruhusu watumiaji wowote kwenye kikoa, tumia hoja za muundo wa *@domain.
Ikiwa mipangilio ya sera hii haijawekwa, hakuna vizuizi ambavyo watumiaji wanahitaji kuingia katika akaunti yake. Kumbuka kuwa hatua ya kuweka watumiaji wapya bado inahitaji mipangilio ya sera ya DeviceAllowNewUsers kuwekwa ifaavyo.
Sera hii hudhibiti anayeweza kuanzisha kipindi cha Google Chrome OS. Haizuii watumiaji kuingia katika akaunti za ziada za Google kwenye Android. Ikiwa unataka kuzuia hatua hii, weka mipangilio ya sera mahususi ya Android accountTypesWithManagementDisabled kuwa sehemu ya ArcPolicy.
Inadhibiti iwapo Google Chrome OS inaruhusu akaunti mpya za mtumiaji kufunguliwa. Ikiwa sera hii imewekwa kuwa sivyo, watumiaji ambao hawana akaunti hawataweza kuingia katika akaunti.
Ikiwa sera hii imewekwa kuwa ndivyo au haijawekewa mipangilio, akaunti mpya za mtumiaji zitaruhusiwa kufunguliwa mradi tu DeviceUserWhitelist haimzuii mtumiaji kuingia katika akaunti.
Sera hii inabaini iwapo watumiaji wapya wanaweza kuongezwa kwenye Google Chrome OS. Haizuii watumiaji kuingia katika akaunti za ziada za Google ndani ya Android. Ikiwa unataka kuzuia hatua hii, weka mipangilio ya sera mahususi ya Android accountTypesWithManagementDisabled kuwa sehemu ya ArcPolicy.
Ikiwa sera imewekwa kuwa mfuatano usio na kitu au mipangilio isipowekwa, Google Chrome OS haitakuonyesha chaguo la kukamilisha kiotomatiki wakati wa utaratibu wa mtumiaji kuingia katika akaunti. Sera ikiwekwa kuwa mfuatano unaowakilisha jina la kikoa, Google Chrome OS itaonyesha chaguo la kukamilisha kiotomatiki wakati mtumiaji anaingia katika akaunti na kumruhusu mtumiaji kuandika jina la mtumiaji pekee bila kiendelezi cha jina la kikoa. Mtumiaji ataweza kubatilisha kiendelezi hiki cha jina la kikoa. Ikiwa thamani ya sera si kikoa sahihi, sera haitatumika.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo au mipangilio isipowekwa, Google Chrome OS itaonyesha watumiaji waliopo kwenye skrini ya kuingia katika akaunti na kukuruhusu uteue mmoja.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, Google Chrome OS haitaonyesha watumiaji waliopo kwenye skrini ya kuingia katika akaunti. Skrini ya kawaida ya kuingia katika akaunti (inayomdokezea mtumiaji kuweka anwani yake ya barua pepe na nenosiri au simu) au skrini ya ukurasa wenye maelezo yanayomwelekeza mtumiaji kuendelea na uthibitishaji kupitia SAML (kama imewashwa kupitia sera ya LoginAuthenticationBehavior) itaonyeshwa, isipokuwa katika hali ambapo mipangilio ya Kipindi Kilichodhibitiwa imewashwa. Wakati mipangllio ya Kipindi kilichodhibitiwa imewekwa, ni akaunti za kipindi kilichodhibitiwa pekee zitakazoonyeshwa, hali inayokuruhusu kuteua moja. Kumbuka kwamba sera hii haizingatii ikiwa kifaa kinahifadhi au kuondoa data ya ndani ya mtumiaji.
Weka mipangilio ya picha ya mandhari ya kiwango cha kifaa ambayo inaonyeshwa kwenye skrini ya kuingia katika akaunti ikiwa hakuna mtumiaji aliyeingia katika kifaa. Sera inawekwa kwa kubainisha URL ambayo kifaa cha Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome kinaweza kupakua picha ya mandhari na hash ya kriptografia inayotumiwa kuthibitisha kwamba kipakuliwa hakina virusi. Lazima picha iwe ya aina ya faili ya JPEG, ukubwa wake usizidi MB 16. Lazima URL ifikiwe bila uthibitishaji wowote. Picha ya mandhari hupakuliwa na kuakibishwa. Itapakuliwa tena wakati URL au hash inabadilika.
Sera inapaswa kubainishwa kama mfuatano unaoeleza URL na hash katika aina ya faili ya JSON, kwa mfano, { "url": "https://example.com/device_wallpaper.jpg", "hash": "examplewallpaperhash" }
Ikiwa sera ya mandhari ya kifaa itawekwa, kifaa cha Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome kitapakua na kutumia picha ya mandhari kwenye skrini ya kuingia katika akaunti ikiwa hakuna mtumiaji ambaye ameingia katika kifaa. Pindi tu mtumiaji anapoingia katika akaunti, sera ya mandhari ya mtumiaji itaanza kutumika.
Ikiwa sera ya mandhari ya kifaa itaachwa bila kuwekwa, ni sera ya mandhari ya mtumiaji itakayoamua kitu cha kuonyesha ikiwa sera ya mandhari ya mtumiaji itawekwa.
Inathibitisha iwapo Google Chrome OS inaweka data ya akaunti ya karibu baada ya kuondoka. Ikiwa imewekwa kwenye ndivyo, hakuna akaunti za kudumu zinazowekwa kwa Google Chrome OS na data yote kutoka kwenye kipindi cha mtumiaji itatupwa baada ya kuondoka. Ikiwa sera hii imewekwa kuwa sivyo au haijasanidiwa, kifaa kinaweza kuweka data ya mtumiaji wa karibu (iliyosimbwa fiche).
Sera hii ikiwekwa, mtiririko wa uthibitishaji wa kuingia katika akaunti utakuwa katika mojawapo ya njia zifuatazo kulingana na thamani ya mipangilio:
Ikiwekwa kuwa GAIA, kuingia katika akaunti kutafanyika kupitia mtiririko wa kawaida wa uthibitishaji wa GAIA.
Ikiwekwa kuwa SAML_INTERSTITIAL, kuingia katika akaunti kutaonyesha skrini ya ukurasa wenye maelezo yanayomwelekeza mtumiaji kuendelea na uthibitishaji kupitia SAML IdP ya kikoa cha usajili wa kifaa, au kurudi kwenye mtiririko wa kawaida wa kuingia katika akaunti wa GAIA.
Hubainisha iwapo vidakuzi vya kuthibitisha vilivyowekwa na SAML IdP wakati wa kuingia katika akaunti vinapaswa kuhamishiwa kwenye wasifu wa mtumiaji.
Mtumiaji anapothibitisha kupitia SAML IdP anapoingia katika akaunti, vidakuzi vilivyowekwa na IdP kwanza huandikwa kwenye wasifu wa muda mfupi. Vidakuzi hivi vinaweza kuhamishiwa kwenye wasifu wa mtumiaji ili kuendelea na hali ya uthibitishaji.
Sera ikiwekwa kuwa ndivyo, vidakuzi vilivyowekwa na IdP huhamishiwa kwenye wasifu wa mtumiajia kila vinapothibitisha dhidi ya SAML IdP wakati wa kuingia katika akaunti.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo au isipowekwa, vidakuzi vilivyowekwa na IdP huhamishiwa kwenye wasifu wa mtumiaji anapoingia katika kifaa kwa mara ya kwanza pekee.
Sera hii inaathiri watumiaji ambao vikoa vyao vinalingana na kikoa cha usajili wa kifaa pekee. Kwa watumiaji wengine wote, vidakuzi vinavyowekwa na IdP huhamishiwa kwenye wasifu wa mtumiaji anapoingia kwa mara ya kwanza kwenye kifaa chake pekee.
Vidakuzi vilivyohamishiwa kwenye wasifu wa mtumiaji haviwezi kufikiwa na programu za Android.
Michoro katika orodha hii italinganishwa na asili ya usalama wa ombi la URL. Zikilingana, idhini ya kufikia vifaa vya kurekodi video itatolewa kwenye kurasa za kuingia katika SAML. Ikiwa hazilingani, idhini ya kufikia itakataliwa kiotomatiki. Michoro ya herufi wakilishi hairuhusiwi.
Hubainisha orodha ya programu na viendelezi vinavyosakinishwa chinichini kwenye skrini ya kuingia katika akaunti, bila kumhusisha mtumiaji, na ambavyo haviwezi kuondolewa na mtumiaji. Ruhusa zote zinazoombwa na programu zitatolewa kwa njia fiche, bila mtumiaji kuhusishwa, ikiwa ni pamoja na ruhusa zozote za ziada zinazoombwa na matoleo ya baadaye ya programu.
Kumbuka kwamba, kwa sababu za usalama na faragha, huruhusiwi kusakinisha viendelezi kwa kutumia sera hii. Zaidi ya hayo, vifaa vilivyo kwenye Kituo thabiti vitasakinisha tu programu ambazo zinamilikiwa na orodha iliyoidhinishwa kwenye Google Chrome. Vipengee vyovyote ambavyo havitii masharti haya havitazingatiwa.
Ikiwa programu iliyosakinishwa hapo awali kwa lazima itaondolewa kwenye orodha hii, itaondolewa kiotomatiki na Google Chrome.
Kila kipengee cha orodha ya sera ni kifungu ambacho kinajumuisha kitambulisho cha kiendelezi na URL ya "sasisho" inayotenganishwa kwa nukta mkato (;) Kitambulisho cha kiendelezi ni kifungu cha herufi 32 kinachopatikana, kwa mfano kwenye chrome://extensions ikiwa katika hali ya wasanidi programu. URL ya "sasisho" inapaswa kuashiria hati ya XML ya faili ya Maelezo ya Sasisho kama ilivyofafanuliwa katika https://developer.chrome.com/extensions/autoupdate. Kumbuka URL ya "sasisho" iliyowekwa katika sera hii hutumika tu kwa ajili ya usakinishaji wa kwanza, masasisho yanayofuata ya kiendelezi hutumia URL ya sasisho iliyobainishwa kwenye faili ya maelezo ya kiendelezi.
Kwa mfano, gbchcmhmhahfdphkhkmpfmihenigjmpp;https://clients2.google.com/service/update2/crx husakinisha programu ya Chrome Remote Desktop kutoka URL ya "sasisho" la kawaida la Duka la Chrome kwenye Wavuti. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kupangisha viendelezi, angalia: https://developer.chrome.com/extensions/hosting.
Huweka mipangilio ya lugha ambayo inatekelezwa kwenye skrini ya kuingia katika kifaa ya Google Chrome OS.
Sera hii ikiwekwa, skrini ya kuingia katika kifaa itaonyeshwa kila mara kwa lugha iliyowekwa katika thamani ya kwanza (sera imebainishwa kuwa orodha ya uoanifu wa kusambaza). Sera hii isipowekwa au ikiwekwa kwenye orodha tupu, skrini ya kuingia katika kifaa itaonyeshwa kwa lugha ya kipindi cha mtumiaji wa mwisho. Sura hii ikiwekwa kuwa thamani ambayo si lugha sahihi, skrini ya kuingia katika kifaa itaonyeshwa kwa lugha chaguomsingi (ambayo kwa sasa ni Kiingereza cha Marekani).
Huweka mipangilio ya miundo ya kibodi inayoruhusiwa kwenye skrini ya kuingia katika kifaa cha Google Chrome OS.
Sera hii ikiweka kuwa orodha ya vitambulishi vya mbinu ya kuingiza data, mbinu husika za kuingiza data zitapatikana kwenye skrini ya kuingia katika kifaa. Mbinu ya kwanza ya kuingiza data itachaguliwa. Wakati podi ya mtumiaji inapolenga skrini ya kuingia katika kifaa, mbinu ya kuingiza data ya mtumiaji iliyotumiwa mara chache zaidi hivi majuzi itapatikana kando na mbinu za kuingiza data zilizotolewa na sera hiii. Sera hii isipowekwa, mbinu za kuingiza data zilizo kwenye skrini ya kuingia katika kifaa zitatolewa kwenye lugha ambayo imetumiwa kuonyesha skrini ya kuingia katika kifaa. Thamani ambazo si vitambulisho sahihi vya mbinu za kuingiza data zitapuuzwa.
Hubainisha jinsi maunzi salama unayotumia yanaweza kutoa uthibitishaji wa hatua mbili ikiwa yanaweza kukitumia kipengele hiki. Kitufe cha kuwasha/kuzima mashine kinatumika kutambua kuwepo kwa mtumiaji mwenyewe.
Ukichagua 'Imezimwa', hamna uthibitishaji wa hatua mbili utakaotolewa.
Ukichagua 'U2F', uthibitishaji wa hatua mbili uliowekwa utafanya kazi kulingana na kibainishi cha FIDO U2F.
Ukichagua 'U2F_EXTENDED', uthibitishaji wa hatua mbili uliowekwa utatoa utendakazi wa U2F pamoja na baadhi ya viendelezi vya uthibitishaji wa mtu binafsi.
Sera hii inatumika kwenye skrini ya kuingia katika akaunti. Tafadhali angalia pia sera ya IsolateOrigins ambayo inatumika kwenye kipindi cha mtumiaji. Tunapendekeza uweke sera zote mbili ziwe katika thamani sawa. Iwapo thamani hazilingani, huenda ikachelewesha kufungua kipindi cha mtumiaji wakati inatumia thamani iliyobainishwa na sera ya mtumiaji. Iwapo umewasha sera hii, kila chanzo ulichotaja katika orodha inayotenganishwa kwa koma kitatumia mchakato wake. Hatua hii pia itatenga vyanzo vinavyotajwa kwa vijikoa; k.m. hatua ya kubainisha https://example.com/ itasababisha pia https://foo.example.com/ itengwe ili isiwe sehemu ya tovuti ya https://example.com/. Iwapo sera imezimwa, vipengele vyote viwili vya IsolateOrigins na SitePerProcess vitazimwa. Bado watumiaji wataweza kuwasha IsolateOrigins wenyewe, kupitia ripoti za mstari wa amri. Iwapo hujaweka mipangilio ya sera hii, mipangilio ya mfumo chaguomsingi wa utengaji wa tovuti itatumika kwenye skrini ya kuingia katika akaunti.
Sera hii inatumika kwenye skrini ya kuingia katika akaunti. Tafadhali angalia pia sera ya SitePerProcess ambayo inatumika katika kipindi cha mtumiaji. Tunapendekeza uweke sera zote mbili ziwe katika thamani sawa. Ikiwa thamani hazitalingana, huenda ikachelewesha shughuli ya kuweka kipindi cha mtumiaji wakati thamani iliyobainishwa na sera ya mtumiaji inatumika. Huenda utataka kuangalia mipangilio ya sera ya IsolateOrigins ili upate hali bora kati ya hizi mbili, utengaji na athari ndogo kwa watumiaji kwa kutumia IsolateOrigins kwenye orodha ya tovuti ambazo ungependa kutenga. Mipangilio hii, SitePerProcess, inatenga tovuti zote. Iwapo umewasha sera hii, kila tovuti itatumia mchakato wake. Iwapo umezima sera hii, vipengele vya IsolateOrigins na SitePerProcess vitazimwa. Bado watumiaji wataweza kuwasha SitePerProcess wenyewe, kupitia ripoti za mstari wa amri. Iwapo hujaweka mipangilio ya sera, mtumiaji ataweza kubadilisha mipangilio hii.
Inakuruhusu kubainisha orodha ya michoro ya url inayobainsha tovuti ambazo cheti cha mteja kinachaguliwa kiotomatiki kwenye skrini ya kuingia katika akaunti katika fremu inayopangisha mtiririko wa SAML, tovuti ikiomba cheti. Mfano wa matumizi ni kusanidi cheti cha matumizi pana ya kifaa kitakachowasilishwa kwenye SAML IdP.
Thamani lazima iwe mfululizo wa mifuatano ya kamusi za JSON. Kila kamusi lazima iwe na muundo wa { "pattern": "$URL_PATTERN", "filter" : $FILTER }, ambapo $URL_PATTERN ni mfuatano wa mchoro wa mipangilio ya maudhui. $FILTER inadhibiti cheti cha mteja ambacho kivinjari kitachagua kiotomatiki. Haitumii kichujio, ni vyeti ambavyo vinalingana na ombi la cheti cha seva ndivyo vitakavyochaguliwa pekee. Kama $FILTER ina muundo wa { "ISSUER": { "CN": "$ISSUER_CN" } }, vyeti zaidi vya mteja pekee vinavyochaguliwa ndivyo vinapewa cheti chenye jina la kawaida la CommonName $ISSUER_CN. Kama $FILTER kina kamusi tupu{}, uteuzi wa vyeti vya mteja haudhibitiwi zaidi.
Ikiwa sera hii itasalia kama haijawekwa, hakuna uteuzi kiotomatiki utakaofanyika kwa tovuti yoyote.
Hubainisha kituo cha kutoa ambacho kifaa hiki kinastahili kufungiwa kwacho.
Ikiwa sera hii itawekwa kuwa Ndivyo na sera ya ChromeOsReleaseChannel haijabainishwa basi watumiaji wa kikoa cha uandikishaji kitaruhusiwa kubadilisha kituo cha kutoa cha kifaa. Ikiwa sera hii itawekwa kuwa siyo Ndivyo kifaa kitafungwa katika kituo chochote ambapo kilikuwa kimewekwa mwisho.
Kituo kilichoteuliwa na mtumiaji kitafutwa kwa sera ya ChromeOsReleaseChannel, lakini ikiwa kituo cha sera ni thabiti zaidi kuliko kile ambacho kilikuwa kimesakinishwa kwenye kifaa, hivyo basi kituo kitabadili tu baada ya toleo la kituo thabiti zaidi kinachofikia idadi ya juu zaidi ya toleo kuliko lililosakinishwa kwenye kifaa.
Huzima masasisho ya kiotomatiki yanapowekwa kuwa Ndivyo.
Vifaa vya Google Chrome OS hutafuta masasisho kiotomatiki ikiwa mipangilio hii haijawekwa au kuwekwa kuwa Sivyo.
Onyo: Unashauriwa kuwasha kipengele cha masasisho ya kiotomatiki ili watumiaji wapokee masasisho ya programu na marekebisho muhimu. Kuzima kipengele cha masasisho ya kiotomatiki kunaweza kuhatarisha hali ya watumiaji.
Hubainisha iwapo p2p itatumika kwa sasisho za data ya OS. Kama imewekwa kuwa Kweli, vifaa vitashiriki na kujaribu kusasisha data kwenye LAN, hivyo kuna uwezekano wa kupunguza matumizi ya kipimo data cha intaneti na msongamano. Kama sasisho ya data haipo kwenye LAN, kifaa kitarudia kupakua kutoka kwenye seva ya sasisho. Kama imewekwa kuwa Uongo ama haijasanidiwa, p2p haitatumika.
Sera hii hudhibiti vipindi ambapo kifaa cha Google Chrome OShakiruhusiwi kukagua masasisho kiotomatiki. Sera hii inapowekwa katika orodha yenye vipindi fulani vya muda: Vifaa havitaweza kukagua masasisho kiotomatiki katika vipindi vilivyobainishwa. Vifaa ambavyo vinahitaji matoleo ya zamani au vinatumia matoleo yaliyotangulia Google Chrome OS havitaathiriwa na sera hii kutokana na matatizo ya usalama yanayoweza kutokea. Zaidi ya hayo, sera hii haitazuia ukaguzi wa masasisho unaoombwa na watumiaji au wasimamizi. Sera hii isipowekwa au ikikosa kipindi chochote: Hamna ukaguzi wa masasisho ya kiotomatiki utakaozuiliwa na sera hii, lakini unaweza kuzuiliwa na sera zingine. Kipengele hiki kimewashwa tu kwenye vifaa vya Chrome ambavyo vimewekewa mipangilio ya skrini nzima kufunguka kiotomatiki. Vifaa vingine havitazuiwa na sera hii.
Inawezesha toleo lengwa kupokea Masasisho ya Kiotomatiki.
Inabainisha kiambishi awali ambako toleo lengwa la Google Chrome OS linafaa kusasishwa. Ikiwa kifaa kinatumia toleo ambalo ni la kabla ya kiambishi awali kilichobainishwa, kitajisasisha kuwa toleo la sasa lenye kiambishi awali husika. Ikiwa kifaa tayari kipo katika toleo la sasa, athari zinategemea thamani ya DeviceRollbackToTargetVersion. Muundo wa kiambishi awali unafanya kazi kama kijenzi jinsi inavyoonyeshwa katika mifano ifuatayo:
"" (au haijawekwa): sasisha iwe toleo la sasa linalopatikana. "1412.": sasisha iwe toleo lolote dogo la 1412 (kwa mfano. 1412.24.34 au 1412.60.2) "1412.2.": sasisha iwe toleo lolote dogo la 1412.2 (kwa mfano 1412.2.34 au 1412.2.2) "1412.24.34": sasisha iwe toleo hili maalum pekee.
Ilani: Hatupendekezi uweke vikwazo vya toleo kwa kuwa huenda vikazuia watumiaji kupokea masasisho ya programu na kurekebisha hitilafu muhimu za usalama. Huenda hatua ya kudhibiti masasisho katika toleo la kiambishi maalum ikawasababishia watumiaji hatari.
Sera hii hufafanua orodha ya asilimia ambazo zitabaini sehemu ya vifaa vya Google Chrome OS katika OU vitakavyosasishwa kila siku kuanzia siku ambapo sasisho limegunduliwa. Wakati wa kugundua ni wa baadaye ikilinganishwa na wakati ambao sasisho limechapishwa, kwa kuwa inaweza kuwa muda mfupi uliopita baada ya kuchapisha sasisho hadi wakati kifaa kitakapokagua masasisho.
Kila jozi (siku, asilimia) linajumuisha kiasi cha asilimia ya kikundi ambacho kimesasishwa kufikia idadi fulani ya siku kuanzia wakati sasisho limegunduliwa. Kwa mfano, iwapo tuna majozi ya [(4, 40), (10, 70), (15, 100)], inaamanisha kuwa 40% ya kundi inapaswa kuwa imesasishwa siku 4 baada ya kuona sasisho. 70% inapaswa kusasishwa baada ya siku 10 na kadhalika.
Iwapo kuna thamani inayobainishwa katika sera hii, masasisho hayatazingatia sera ya DeviceUpdateScatterFactor na yatafuata sera hii badala yake.
Iwapo orodha hii haina maudhui, mchakato hautaanzishwa na masasisho yatatumika kulingana na sera za vifaa vingine.
Sera hii haitumiki katika swichi za vituo.
Inabainisha idadi ya sekunde ambazo kifaa kinaweza kuamua kuchelewesha upakuaji wake wa sasisho kutoka wakati ambapo usasishaji ulisukumwa kwanza nje katika seva. Kifaa kinaweza kusubiri kijisehemu cha muda huu kwa hali ya muda wa saa na kijisehemu kinachosalia katika hali ya idadi ya ukaguzi wa visasisho. Katika hali yoyote, utawanyishaji umekitwa katika kiwango cha kudumu cha muda ili kifaa kisikwame tena kikisubiri kupakua sasisho kwa muda mrefu.
Aina za miunganisho zinazoruhusiwa kutumia sasisho za Mfumo wa Uendeshaji. Sasisho za Mfumo wa Uendeshaji zinaweza kuweka vichujo vizito kwenye muunganisho kwa sababu ya ukubwa wavyo na huenda vikasababisha gharama ya ziada. Kwa hivyo, haviwashwi kwa chaguomsingi kwa aina za miunganisho zinazoonekana kuwa ghali, zinazojumuisha WiMax, Bluetooth na Simu ya Mkononi kwa wakati huu.
Vitambulisho vinavyotambuliwa vya aina vya muunganisho ni "ethaneti", "wifi", "wimax", "bluetooth" na "simu ya mkononi".
Sasisho za data kiotomatiki kwenye Google Chrome OS zinaweza kupakuliwa kupitia HTTP badala ya HTTPS. Hii huruhusu uakibishaji wa HTTP wazi wa vipakuliwa vya HTTP.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, Google Chrome OS itajaribu kupakua sasisho za data kiotomatiki kupitia HTTP. Sera ikiwekwa kuwa sivyo ama isiwekwe, HTTPS itatumika kupakua sasisho za data kiotomatiki.
Ratibisha kuwasha tena kiotomatiki baada ya sasisho la Google Chrome OS limetumika.
Sera hii inapowekwa kuwa kweli, kuwasha tena kiotomatiki kunaratibiwa wakati sasisho la Google Chrome OS limetumika na kuwasha tena kunahitajika ili kumaliza mchakato wa sasisho. Kuwasha tena kunaratibiwa mara moja lakini kunaweza kucheleweshwa kwenye kifaa hadii saa 24 kama mtumiaji anatumia kifaa kwa sasa.
Sera hii inapowekwa kuwa haitumiki, hakuna kuwasha tena kunakoratibiwa baada ya kutumia sasisho la Google Chrome OS. Mchakato wa sasisho hukamilika mtumiaji anapowasha tena kifaa.
Iwapo utaweka sera hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuifuta.
Kumbuka: Kuwasha tena kiotomatiki huwashwa tu wakati skrini ya kuingia katika akaunti inaonyeshwa au kipindi cha programu ya kioski kinaendelea kwa sasa. Hii itabadilika katika siku zijazo na sera itatumika kila wakati, bila kujali kama kipindi cha aina yoyote kinaendelea au la.
Huweka mipangilio ya mahitaji ya msingi yanayoruhusiwa ya toleo la Google Chrome. Matoleo yaliyo hapa chini yatachukuliwa kuwa hayafai na kifaa hakitaruhusu mtumiaji kuingia katika akaunti kabla ya kusasisha Mfumo wa Uendeshaji. Ikiwa toleo la sasa halitafaa wakati wa kipindi cha mtumiaji, akaunti ya mtumiaji itafungwa kwa lazima.
Ikiwa sera hii haijawekwa, hakuna vizuizi vitakavyotumika na watumiaji wanaweza kuingia katika akaunti bila kujali matoleo ya Google Chrome.
Katika hali hii "Toleo" linaweza kuwa toleo halisi kama vile toleo la '61.0.3163.120' au kiambishi cha toleo, kama vile '61.0'
Hubainisha ikiwa kifaa kitarejeshwa kwenye toleo lililowekwa na DeviceTargetVersionPrefix ikiwa tayari kinatumia toleo la sasa.
Chaguomsingi ni RollbackDisabled
Hubainisha idadi ya chini zaidi ya matukio ya urejesheji wa Google Chrome OS ambayo yanapaswa kuruhusiwa kuanzia kwenye toleo thabiti wakati wowote.
Thamani chaguomsingi ya mteja huwa ni 0 na 4 (kwa takribani nusu ya mwaka) kwa vifaa vilivyojumuishwa katika biashara.
Kuweka sera hiii kunazuia ulinzi wa urejeshaji wa toleo kutumika katika angalau idadi hii ya matukio.
Kuweka sera hii katika thamani ya chini kuna athari ya kudumu kabisa: HUENDA kifaa hakitaweza kutumia tena matoleo ya awali hata baada ya sera kuwekwa upya katika thamani kubwa.
Uwezekano wa urejeshaji halisi huenda ukategemea marekebisho yenye athari kubwa na bodi.
Sera hii hudhibiti ikiwa kifaa kinahitaji au hakihitaji kusasishwa kwenye Muundo wa Urekebishaji wa Haraka.
Thamani ikiwekwa kuwa tokeni inayoambatishwa kwenye Muundo wa Urekebishaji wa Haraka, kifaa kitasasishwa kwenye Muundo wa Urekebishaji wa Haraka unaohusika, ikiwa sasisho halijazuiwa na sera nyingine.
Ikiwa sera hii haijawekwa, au ikiwa thamani yake haijaambatishwa kwenye Muundo wa Urekebishaji wa Haraka, basi kifaa hakitasasishwa kwenye Muundo wa Urekebishaji wa Haraka. Ikiwa kifaa tayari kinatumia Muundo wa Urekebishaji wa Haraka na sera haijawekwa tena au thamani yake haijaambatishwa tena kwenye Muundo wa Urekebishaji, basi kifaa kitasasishwa kwenye muundo wa kawaida ikiwa sasisho halijazuiwa na sera nyingine.
Inaruhusu kusukuma usanidi wa mtandao ili kutumika kwa watumiaji wote wa kifaa cha Google Chrome OS. Usanidi wa mtandao ni mtungo wa JSON ulioumbizwa kama ilivyofafanuliwa na umbizo la Usanidi Huru wa Mtandao ulioelezwa kwenye https://sites.google.com/a/chromium.org/dev/chromium-os/chromiumos-design-docs/open-network-configuration
Programu za Android zinaweza kutumia usanidi wa mtandao na vyeti vya CA vilivyowekwa kupitia sera hii, lakini hazina idhini ya kufikia chaguo za kuweka mipangilio.
Inathibitisha iwapo utumiaji wa data nje ya mtandao wako unapaswa kuwezeshwa kwa kifaa. Ikiwa itawekwa kuwa Ndivyo, utumiaji wa data nje ya mtandao wako unawezeshwa. Ikiwa hautasanidiwa au kuwekwa kuwa siyo Ndivyo, utumiaji wa data nje ya mtandao wako hautapatikana.
Huruhusu kuwashwa na kuzimwa kwa kipengele cha kudhibiti mtandao. Hii inatumika kwa watumiaji wote, na violesura vyote kwenye kifaa. Baada ya kuwekwa, udhibiti utaendelea mpaka sera ibadilike ili kuizima.
Ikiwekwa kuwa sivyo, hakuna udhibiti. Ikiwekwa kuwa ndivyo, mfumo hudhibitiwa ili kufanikisha viwango vya upakiaji na kupakua vilivyowekwa (katika kbits/s).
Hubainisha jina la mpangishaji wa kifaa kinachotumika katika maombi ya DHCP.
Kama sera hii imewekwa kuwa mfuatano ulio na herufi au nambari yoyote, mfuatano huo utatumika kama jina la mpangishaji wa kifaa wakati wa ombi la DHCP.
Mfuatano huu unaweza kujumuisha vigezo ${ASSET_ID}, ${SERIAL_NUM}, ${MAC_ADDR}, ${MACHINE_NAME} ambavyo vinaweza kubadilishwa na thamani kwenye kifaa kabla ya kuvitumia kama jina la mpangishaji. Matokeo ya ubadilishaji sharti yawe na jina sahihi la mpangishaji (kulingana na RFC 1035, sehemu ya 3.1).
Kama sera hii haijawekwa au thamani ya baada ya ubadilishaji si jina sahihi la mpangishaji, jina la mpangishaji halitawekwa katika ombi la DHCP.
Huruhusu kuwasha au kuzima kipengele cha Kubadilisha Haraka. Hali hii inaathiri watumiaji na violesura vyote katika kifaa. Ili utumie kipengele cha Kubadilisha Haraka, unahitaji kuwasha mipangilio hii na kipengee cha ONC kwa kila mtandao. Baada ya kuweka mipangilio hii, kipengele cha Kubadilisha Haraka kitaendelea kuonekana hadi wakati sera itabadilishwa ili kukizima.
Ikiwa sera hii haijawekwa au imewekwa kuwa sivyo, kipengele cha Kubadilisha Haraka hakitumiki. Ikiwa sera imewekwa kuwa ndivyo, kipengele cha Kubadilisha Haraka kinatumika wakati mlango wa mtandao usiotumia waya unaweza kukitumia.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, Google Chrome OS itazima Wi-Fi na watumiaji hawataweza kuiwasha tena. Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo au isipowekwa, watumiaji wataweza kuwasha au kuzima Wi-Fi wapendavyo.
Huweka mipangilio ya anwani ya MAC (udhibiti wa kufikia maudhui) ambayo itatumiwa wakati kituo kimeunganishwa kwenye kifaa.
Wakati kituo kimeunganishwa kwenye baadhi ya miundo ya kifaa, anwani ya MAC ya kituo iliyobainishwa katika kifaa hutumiwa kutambua kifaa kwenye mtandao wa Ethaneti kwa chaguomsingi. Sera hii huruhusu msimamizi kubadilisha chanzo cha anwani ya MAC ikiwa imeambatishwa.
Ikiwa 'DeviceDockMacAddress' imechaguliwa au sera haijawekwa, anwani ya MAC ya kituo iliyobainishwa kwenye kifaa itatumika.
Ikiwa 'DeviceNicMacAddress' imechaguliwa, anwani ya MAC ya NIC (kidhibiti cha kiolesura cha mtandao) ya kifaa itatumiwa.
Ikiwa 'DockNicMacAddress' imechaguliwa, anwani ya NIC MAC ya kituo itatumika.
Mipangilio hii haiwezi kubadilishwa na mtumiaji.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, chaguo za Zana za walio na matatizo ya kuona na kusikia zitaonekana kila wakati katika menyu ya ubao wa aikoni.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, chaguo za Zana za walio na matatizo ya kuona na kusikia hazitawahi kuonekana katika menyu ya ubao wa aikoni.
Ukiweka sera hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuibatilisha.
Sera hii isipowekwa, chaguo za Zana za walio na matatizo ya kuona na kusikia hazitaonekana katika menyu ya ubao wa aikoni, lakini mtumiaji anaweza kufanya chaguo za Zana za walio na matatizo ya kuona na kusikia zionekane kupitia ukurasa wa Mipangilio.
Washa kipengee cha upatikanaji cha kiteuzi kikubwa. Iwapo sera hii imewekwa kuwa kweli, kiteuzi kikubwa kitawashwa kila wakati. Iwapo sera hii imewekwa kuwa haitumiki, kiteuzi kikubwa kitawashwa kila wakati. Iwapo utaweka sera hii, watumiaji hawezi kuibadilisha au kuipuuza. Iwapo sera hii haijawekwa, kiteuzi kikubwa kitazimwa mwanzoni lakini kitawashwa na mtumiaji wakati wowote.
Washa kipengele cha upatikanaji wa maoni yanayotamkwa.
Iwapo sera hii imewekwa kuwa kweli, maoni yanayotamkwa yatakuwa yamewashwa kila wakati.
Iwapo sera itawekwa kuwa haitumiki, maoni yanayotamkwa yatazimwa kila wakati.
Iwapo utaweka sera hii, watumiaji hawezi kuibadilisha au kuipuuza.
Iwapo sera hii haijawekwa, maoni yanayotamkwaa yatazimwa mwanzoni lakini yanaweza kuwashwa na mtumiaji wakati wowote.
Washa kipengee cha upatikanaji cha hali ya juu ya utofutishaji. Kama sera hii imewekwa kuwa kweli, hali ya juu ya utofautishaji itawashwa kila wakati. Kama sera hii imewekwa kuwa haitumiki, hali ya juu ya utofautishaji itazimwa kila wakati. Kama sera hii imewekwa, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuipuuza. Kama sera hii haitawekwa, hali ya juu ya utofautishaji itazimwa mwanzoni lakini inaweza kuwashwa na mtumiaji wakati wowote.
Washa kipengele cha ufikiaji wa kibodi ya skrini.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, kibodi ya skrini itawashwa wakati wote.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, kibodi ya skrini itazimwa wakati wote.
Ukiweka sera hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuibatilisha.
Sera hii isipowekwa, skrini ya kibodi itakuwa imezimwa mwanzoni lakini inaweza kuwashwa na mtumiaji wakati wowote.
Hubadilisha tabia chaguomsingi ya vitufe vya safumlalo ya juu kwenda vitufe vya kukokotoa.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, vitufe vya safumlalo ya juu ya kibodi vitatoa amri za vitufe vya kukokotoa kwa chaguomsingi. Kitufe cha kutafuta lazima kibonyezwe ili kurejesha tabia yake kuwa vitufe vya media.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo au isiwekwe, kibodi itatoa amri za vitufe vya media kwa chaguomsingi na amri za vitufe vya kukokotoa wakati kitufe cha kutafuta kimeshikiliwa.
Ikiwa sera hii imewekwa, inadhibiti aina ya Kikuza Skrini ambacho kimewashwa. Kuweka sera hii kuwa "Hamna" kunazima Kikuza Skrini.
Ukiweka sera hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuibatilisha.
Ikiwa sera hii imeachwa bila kuwekwa, Kikuza Skrini kinazimwa mwanzoni lakini kinaweza kuwashwa na mtumiaji wakati wowote.
Weka hali chaguomsingi ya kipengele cha upatikanaji wa kiteuzi kikubwa kwenye skrini ya kuingia katika akaunti.
Kama sera hii itawekwa kuwa kweli, kiteuzi kikubwa kitawashwa wakati skrini ya kuingia katika akaunti itakapoonyeshwa.
Kama sera hii ni itawekwa kuwa uongo, kiteuzi kikubwa kitazimwa wakati skrini ya kuingia katika akaunti itakapoonyeshwa.
Kama utaweka sera hii, watumiaji wanaweza kuipuuza kwa muda kwa kuwasha au kuzima kiteuzi kikubwa. Hata hivyo, chaguo la mtumiaji halitaendelea na chaguomsingi litarejeshwa tena wakati wowote skrini ya kuingia katika skrini itakapoonyeshwa upya au mtumiaji atakaposalia bila kufanya kitu kwenye skrini ya kuingia katika akaunti kwa dakika moja.
Kama sera hii haijawekwa, kiteuzi kikubwa huzimwa wakati skrini ya kuingia katika akaunti itakapoonyeshwa kwanza. Watumiaji wanaweza kuwasha au kuzima kiteuzi kikubwa wakati wowote na hali yake kwenye skrini ya kuingia katika akaunti inaendelea kati ya watumiaji.
Weka hali ya chaguomsingi ya kipengee cha ufikiaji cha maoni yaliyotamkwa kwenye skrini ya kuingi. Iwapo sera hii imewekwa kuwa kweli, maoni yaliyosemwa yatawashwa skrini ya kuingina katika akaunti itakapoonyeshwa. Iwapo sera hii imewekwa kwa haitumiki, maoni yaliyosemwa yatazimwa skrini ya kuingina katika akaunti itakapoonyeshwa. Ukiweka sera hii, watumiaji wanaweza kuipuuza kwa muda kwa kuwasha au kuzima maoni yaliyotamkwa. Hata hivyo, uchaguzi wa mtumiaji sio wa kuendelea na chaguomsingi hurejeshwa tena wakati wowote skrini ya kuingia katika akaunti inapoonekana upya au mtumiaji anaposalia kama hafanyi kitu kwenye skrini ya kuingia katika akaunti kwa dakika moja. Iwapo sera hii itawachwa bila kuwekwa, maoni yaliyotamkwa yatazimwa skrini ya kuingia katika akaunti itakapoonyeshwa kwanza. Watumiaji wanaweza kuwasha au kuzima maoni yaliyosemwa wakati wowote na hali yake kwenye skrini ya kuingia katika akaunti itakatalia kati ya watumiaji.
Weka hali chaguomsingi ya kipengee cha ufikiaji cha utofautishaji wa juu kwenye skrini ya kuingia katika akaunti. Iwapo sera hii imewekwa kuwa kweli, hali ya juu ya utofautishaji itawashwa wakati skrini ya kuingia katika akaunti itakapoonyeshwa. Iwapo sera hii imewekwa kwa haitumiki, hali ya juu ya utofautishaji itazimwa wakati skrini ya kuingia katika akaunti itakapoonyeshwa. Iwapo utaweka sera hii, watumiaji wanaweza kwa muda kuipuuza kwa kuwasha au kuzima hali ya juu ya utofautishaji. Hata hivyo, chaguo la mtumiaji halitaendelea na chaguomsingi hurejeshwa tena wakati wowote skrini ya kuingia katika akaunto inapoonyeshwa upya au mtumiaji anaposalia bila kufanya kitu kwenye skrini ya kuingia katika akaunti kwa dakika moja. Iwapo sera hii haijawekwa, hali ya juu ya utoafautishaji huzimwa wakati skrini ya kuingia katika akaunti inapoonyeshwa kwanza. Watumiaji wanaweza kuwasha au kuzima hali ya juu ya utofautishaji wakati wowote na hali yake kwenye skrini ya kuingia katika akaunti inaendelea kati ya watumiaji.
Weka hali chaguomsingi ya kipengele cha ufikiaji cha kibodi ya skrini kwenye skrini ya kuingia katika akaunti.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, kibodi ya skrini itawashwa wakati skrini ya kuingia katika akaunti inaonyeshwa.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, kibodi ya skrini itazimwa wakati skrini ya kuingia katika akaunti inaonyeshwa.
Ukiweka sera hii, watumiaji wanaweza kuibatilisha kwa muda kwa kuwasha au kuzima kibodi ya skrini. Hata hivyo, chaguo la watumiaji halidumu na chaguomsingi hurejeshwa kila wakati skrini ya kuingia katika akaunti inapoonyeshwa upya au mtumiaji anapokuwa hafanyi kitu kwenye skrini ya kuingia katika akaunti kwa dakika moja.
Sera hii isipowekwa, kibodi ya skrini inawashwa skrini ya kuingia katika akaunti inapoonyeshwa mara ya kwanza. Watumiaji wanaweza wakazima au kuwasha kibodi ya skrini wakati wowote na hali yake kwenye skrini ya kuingia katika akaunti inadumu kati ya watumiaji.
Weka aina chaguomsingi ya kikuza skrini ambacho kimewashwa kwenye skrini ya kuingia katika akaunti. Kama sera hii itawekwa, itadhibiti aina ya kikuza skrini ambacho kimewashwa wakati skrini ya kuingia katika akaunti itakapoonyeshwa. Kuweka sera kuwa "Hakuna" huzima kikuza skrini.
Kama umeweka sera hii, watumiaji wanaweza kuipuuza kwa muda kwa kuwasha au kuzima kikuza skrini. Hata hivyo, chaguo la mtumiaji haliendelei na chaguomsingi hurejeshwa tena wakati skrini ya kuingia katika akaunti inapoonyeshwa upya au mtumiaji anapobakia bila kufanya kitu kwenye skrini ya kuingia katika akaunti kwa dakika moja.
Kama sera haitawekwa, kikuza skrini kitazimwa wakati skrini ya kuingia katika akaunti itakapoonyeshwa kwanza. Watumiaji wanaweza kuwasha au kuzima kikuza skrini wakati wowote na hali yake kwenye skrini ya kuingia katika akaunti inaendelea kati ya watumiaji.
Sera hii huipa programu ya Mratibu wa Google ruhusa ya kufikia maudhui kwenye skrini na kutuma maelezo kwenye seva. Sera ikiwashwa, programu ya Mratibu wa Google itaruhusiwa kufikia maudhui kwenye skrini. Sera ikizimwa, programu ya Mratibu wa Google haitaruhusiwa kufikia maudhui kwenye skrini. Iwapo sera haijawekwa. watumiaji wanaweza kuamua ikiwa programu ya Mratibu wa Google inaweza kufikia maudhui kwenye skrini au haiwezi.
Sera hii inaipa programu ya Mratibu wa Google ruhusa ya kusikiliza kifungu cha kuwasha sauti.
Ikiwa sera hii imewashwa, programu ya Mratibu wa Google itasikiliza kifungu cha kuwasha sauti. Ikiwa sera hii imezimwa, programu ya Mratibu wa Google haitasikiliza kifungu cha kuwasha sauti. Ikiwa sera hii haijawekwa, Programu ya Mratibu wa Google haitasikiliza kifungu cha kuwasha kifaa.
Hufafanua orodha ya vifaa vya USB vinavyoruhusiwa kutenganishwa kwenye kiendeshaji chake ili vitumiwe kwenye API ya chrome.usb moja kwa moja ndani ya programu ya wavuti. Maingizo ni jozi za Kitambulisho cha Muuzaji cha USB na Kitambulisho cha Bidhaa za kutambua maunzi mahususi.
Ikiwa sera hii haitawekwa, orodha ya vifaa vya USB vinavyoweza kutenganishwa itasalia tupu.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, Google Chrome OS itazima Bluetooth na mtumiaji hawezi kuiwasha tena.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo au isipowekwa, mtumiaji ataweza kuwasha au kuzima Bluetooth apendavyo.
Sera hii ikiwekwa, mtumiaji hawezi kuibadilisha au kuibatilisha.
Baada ya kuwasha Bluetooth, lazima mtumiaji aondoke kisha aingie katika akaunti ili mabadiliko yatekelezwe (hakuna haja ya kufanya hivi wakati wa kuzima Bluetooth).
Huweka mipangilio ya upatikanaji na utendaji wa kipengele cha kusasisha programu dhibiti ya TPM.
Mipangilio mahususi inaweza kubainishwa katika sifa za JSON:
allow-user-initiated-powerwash: Ikiwekwa kuwa true, watumiaji wataweza kusababisha mtiririko wa Powerwash wa kusakinisha sasisho la programu dhibiti ya TPM.
allow-user-initiated-preserve-device-state: Ikiwekwa kuwa true, watumiaji wataweza kuanzisha mtiririko wa sasisho la programu dhibiti ya TPM ambayo inahifadhi hali ya kifaa chote (ikiwa ni pamoja na ujumuishaji katika Enterprise), lakini itapoteza data ya mtumiaji. Mtiririko wa sasisho hili unapatikana kuanzia toleo la 68.
auto-update-mode: Inadhibiti jinsi masasisho ya kiotomatiki ya programu dhibiti ya TPM yanatumika katika programu dhibiti ya TPM inayoweza kuathirika. Mitiririko yote huhifadhi hali ya ndani ya kifaa. Sera hii ikiwekwa kuwa 1 au isipowekwa, masasisho ya programu dhibiti ya TPM hayatatumika. Ikiwekwa kuwa 2, programu dhibiti ya TPM itasasishwa kifaa kitakapowashwa tena baada ya mtumiaji kukubali sasisho. Ikiwekwa kuwa 3, programu dhibiti ya TPM itasasishwa kifaa kitakapowashwa tena. Sera ikiwekwa kuwa 4, programu dhibiti ya TPM itasasishwa baada ya kujumuishwa, kabla ya mtumiaji kuingia katika akaunti. Chaguo hili linapatikana kuanzia toleo la 74.
Sera hii isipowekwa, utendaji wa programu dhibiti ya TPM hautapatikana.
Hubainisha muda kwa kipimo cha milisekunde ambacho huduma ya kudhibiti kifaa ambao huulizwa maelezo ya sera ya kifaa.
Kuweka sera hii kutafuta thamani chaguomsingi ya saa 3. Thamani sahihi za sera hii ziko kuanzia 1800000 (dakika 30) hadi 86400000 (siku 1). Thamani zozote ambazo haziko katika masafa haya zitawekwa katika mpaka husika.
Kuacha sera hii bila kuiweka kutafanya Google Chrome OS itumie thamani chaguomsingi ya saa 3.
Kumbuka kwamba ikiwa mfumo unatumia arifa za sera, ucheleweshwaji wa kuonyesha upya utawekwa kuwa saa 24 (ukipuuza chaguomsingi zote na thamani ya sera hii) kwa sababu inatarajiwa kwamba arifa za sera zitalazimisha kuonyesha upya kiotomatiki wakati wowote ambao sera itabadilika, hivyo kuondoa haja ya kuonyesha upya mara kwa mara.
Zuia hali ya wasanidi programu.
Ikiwa sera hii itawekwa kuwa Ukweli, Google Chrome OS itazuia kifaa kuwaka katika hali ya wasanidi programu. Mfumo utakataa kuwaka na kuonyesha skrini ya hitilafu swichi ya wasanidi programu itakapowashwa.
Ikiwa sera haitawekwa au itawekwa kuwa Uongo, hali ya wasanidi programu itaendelea kupatikana kwa kifaa.
Sera hii hudhibiti hali ya wasanidi programu wa Google Chrome OS pekee. Ikiwa ungependa kuzuia idhini ya kufikia Chaguo za Wasanidi Programu wa Android, unatakiwa kuweka sera ya DeveloperToolsDisabled.
Usimamizi wa IT kwa vifaa vya biashara unaweza kutumia alama hii kudhibiti iwapo itaruhusu watumiaji kukomboa matoleo kupitia Usajili wa Chrome OS.
Iwapo sera hii itawekwa kuwa ndivyo au kuachwa bila kuwekwa, watumiaji wataweza kukomboa matoleo kupitia Usajili wa Chrome OS.
Iwapo sera hii itawekwa kuwa sivyo, mtumiaji hataweza kukomboa matoleo.
Kipengele cha Quirks Server hutoa faili za mipangilio ya maunzi mahususi, kama vile ICC huonyesha wasifu ili kubadilisha vipimo vya skrini.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, kifaa hakitajaribu kuwasiliana na Quirks Server ili kupakua faili za mipangilio.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo au isipowekwa, basi Google Chrome OS itawasiliana na Quirks Server kiotomatiki na kupakua faili za mipangilio, ikiwa zinapatikana, na kuzihifadhi kwenye kifaa. Faili kama hizi huenda, kwa mfano, zikatumika kuboresha hali ya kuonekana kwa skrini zilizoambatishwa.
Programu na Viendelezi vya akiba za Google Chrome OS za kusakinishwa na watumiaji wengi kwenye kifaa kimoja ili kuepuka kuzipakua upya kwa kila mtumiaji. Ikiwa sera hii haijasanidiwa au thamani ni chini ya MB 1, Google Chrome OS itatumia ukubwa wa akiba chaguomsingi.
Akiba hii haitumiwi na programu za Android. Ikiwa watumiaji wengi watasakinisha programu sawa ya Android, itapakuliwa upya kwa kila mtumiaji.
Ikiwa sera ya "OffHours" imewekwa, basi sera za kifaa zilizobainishwa hazitatumika (tumia mipangilio chaguomsingi ya sera hizi) katika vipindi vilivyotajwa. Sera za kifaa huwekwa tena na Chrome kwa kila tukio wakati kipindi cha "OffHours" kinaanza au kukamilika. Watumiaji wataarifiwa na kulazimishwa kuondoka katika akaunti wakati muda wa "OffHours" unakamilika na mipangilio ya kifaa inabadilishwa (kwa mfano, wakati mtumiaji ameingia katika akaunti akitumia akaunti ambayo hairuhusiwi).
Baada ya kuweka sera hii, ubora na kigezo cha kipimo cha kila onyesho kitawekwa kuwa thamani zilizobainishwa. Mipangilio ya onyesho la nje itawekwa kwa maonyesho yote ya nje yaliyounganishwa.
Thamani za "external_width" na "external_height" zinapaswa kubainishwa kwa pikseli. Thamani za "external_scale_percentage" na "internal_scale_percentage" zinapaswa kubainishwa kwa asilimia.
Ikiwa "external_use_native" imewekwa kuwa ndivyo, sera itapuuza thamani za "external_height" na "external_width" na iweke ubora wa maonyesho ya nje kuwa na ubora wa asili.
Ikiwa "external_use_native" imewekwa kuwa sivyo au haijatolewa na "external_height" au "external_width" haujatolewa, sera haitaathiri mipangilio ya onyesho la nje. Ikiwa ubora au kigezo cha kipimo kilichobainishwa hakitumiki kwenye onyesho fulani, sera haitatumika kwenye onyesho hilo.
Ikiwa alama "iliyopendekezwa" imewekwa kuwa ndivyo, huenda watumiaji wakabadilisha ubora na kigezo cha kipimo cha onyesho lolote kupitia ukurasa wa mipangilio baada ya kuingia katika akaunti, lakini mipangilio yao itabatilishwa na thamani ya sera inapowashwa tena. Ikiwa alama "iliyopendekezwa" imewekwa kuwa sivyo au haijawekwa, watumiaji hawataweza kubadilisha mipangilio ya onyesho.
Sera hii ikiwekwa, kila onyesho litazungushwa hadi mkao uliobainishwa kila inapowashwa tena, na mara ya kwanza inapounganishwa baada ya thamani ya sera kubadilika. Watumiaji wanaweza kubadilisha mzunguko wa onyesho kupitia ukurasa wa mipangilio baada ya kuingia katika akaunti, lakini mipangilio yake itabatilishwa na thamani za sera itakapowashwa tena.
Sera hii inatumika kwenye maonyesho ya msingi na ya pili yote.
Sera hii isipowekwa, thamani chaguomsingi ni digrii 0 na mtumiaji yuko huru kuibadilisha. Kwa hivyo, thamani chaguomsingi haitumiwi tena wakati wa kuzima na kuwasha.
Ruhusu kifaa hiki kitumie PluginVm.
Iwapo sera hii imewekwa kuwa sivyo au haijawekwa, PluginVm haitumiwi katika kifaa. Ikiwa sera imewekwa kuwa ndivyo, PluginVm inatumiwa katika kifaa iwapo mipangilio mingine inairuhusu. PluginVmAllowed inatakiwa kuwa 'ndivyo', PluginVmLicenseKey na PluginVmImage iwekwe iliPluginVm iruhusiwe kutumika.
Sera hii inabainisha ufunguo wa leseni ya PluginVm kwenye kifaa hiki
Sera hii inabainisha picha ya PluginVm ya mtumiaji. Sera inawekwa kwa kubainisha URL ambako kifaa kinaweza kupakua picha na upunguzaji wa urefu wa SHA-256 unaotumika kuthibitisha usalama wa kipakuliwa.
Sera inapaswa kubainishwa kama mfuatano unaoelezea URL na upunguzaji wa urefu katika muundo wa JSON.
Hukuruhusu kubainisha seva mbadala inayotumiwa na Google Chrome na kuzuia watumiaji kubadilisha mipangilio ya seva mbadala.
Sera hii hutumika tu ikiwa sera ya ProxySettings haijabainishwa.
Ukichagua kutowahi kutumia seva mbadala na kuunganisha moja kwa moja kila wakati, chaguo zingine zote hazitumiki.
Ukichagua kutumia mipangilio ya seva mbadala ya mfumo, chaguo zingine zote hazitumiki.
Ukichagua kutambua seva mbadala kiotomatiki, chaguo zingine zote hazitumiki.
Ukichagua hali ya seva mbadala isiyobadilishwa, unaweza kubainisha chaguo zaidi katika 'Anwani au URL ya seva mbadala' na 'Orodha ya sheria ambazo hazitumiwi na seva mbadala, iliyotenganishwa kwa koma'. Seva mbadala ya HTTP pekee iliyo na kipaumbele cha kwanza ndiyo inapatikana kwa ajili ya programu za ARC.
Ukichagua kutumia hati ya seva mbadala ya pac, lazima ubainishe URL ya kufikia hati katika 'URL kwenye faili ya seva mbadala ya .pac'.
Kwa mifano ya kina, tembelea: https://www.chromium.org/developers/design-documents/network-settings#TOC-Command-line-options-for-proxy-sett.
Ukiwasha mipangilio hii, Google Chrome na programu za ARC hazitatumia chaguo zote zinazohusiana na seva mbadala zilizobainishwa kwenye mstari wa amri.
Sera hii isipowekwa itaruhusu watumiaji kuchagua mipangilio ya seva mbadala wenyewe.
Huwezi kulazimisha programu za Android zitumie seva mbadala. Sehemu ya mipangilio ya seva mbadala inapatikana kwa programu za Android, ambazo zinaweza kuamua kutii:
Ukichagua kutotumia kamwe seva mbadala, programu za Android zitaarifiwa kwamba hakuna seva mbadala iliyowekwa mipangilio.
Ukichagua kutumia mipangilio ya seva mbadala au seva mbadala ambayo haibadiliki, programu za Android zinapewa anwani ya http na mlango wa seva mbadala.
Ukichagua kugundua seva mbadala kiotomatiki, URL ya hati "http://wpad/wpad.dat" hutolewa kwa programu za Android. Hakuna sehemu nyingine ya itifaki ya kugundua kiotomatiki inayotumiwa.
Ukichagua kutumia hati ya seva mbadala ya a .pac, URL ya hati inatolewa kwa programu za Android.
Sera hii haifanyi kazi, badala yake tumia ProxyMode.
Hukuruhusu kubainisha seva mbadala inayotumiwa na Google Chrome na kuzuia watumiaji kubadilisha mipangilio ya seva mbadala.
Sera hii hutumika tu ikiwa sera ya ProxySettings haijabainishwa.
Ukichagua kutowahi kutumia seva mbadala na kuunganisha moja kwa moja kila wakati, chaguo zingine zote hazitumiki.
Ukichagua kutumia mipangilio ya seva mbadala ya mfumo au kutambua kiotomatiki seva mbadala, chaguo zingine zote hazitumiki.
Ukichagua kuweka mipangilio ya seva mbadala wewe mwenyewe, unaweza kubainisha chaguo zaidi katika 'Anwani au URL ya seva mbadala', 'URL kwenye faili ya .pac' ya seva mbadala' na 'Orodha ya sheria zisizotumika za seva mbadala zilizotenganishwa kwa koma'. Seva mbadala ya HTTP pekee iliyo na kipaumbele cha kwanza ndiyo inapatikana kwa ajili ya programu za ARC.
Kwa mifano ya kina, tembelea: https://www.chromium.org/developers/design-documents/network-settings#TOC-Command-line-options-for-proxy-sett.
Ukiwasha mipangilio hii, Google Chrome haitumii chaguo zinazohusiana na seva mbadala zilizobainishwa kutoka mstari wa amri.
Sera hii isipowekwa itaruhusu watumiaji kuchagua mipangilio ya seva mbadala wenyewe.
Huwezi kulazimisha programu za Android zitumie seva mbadala. Sehemu ya mipangilio ya seva mbadala huwa tayari kwa ajili ya programu za Android, ambazo zinaweza kuchagua kwa hiari kuitii. Angalia sera ya ProxyMode ili upate maelezo zaidi.
Unaweza kubainisha URL ya seva mbadala hapa.
Sera hii itatekelezwa tu ikiwa umechagua mipangilio ya seva mbadala mwenyewe katika 'Chagua jinsi ya kubainisha mipangilio ya seva mbadala' na ikiwa sera ya ProxySettings haijabainishwa.
Hupaswi kuweka sera hii ikiwa umechagua hali nyingine yoyote ya kuweka sera za seva mbadala.
Ili upate chaguo zaidi na mifano ya kina, tembelea: https://www.chromium.org/developers/design-documents/network-settings#TOC-Command-line-options-for-proxy-sett.
Huwezi kulazimisha programu za Android zitumie seva mbadala. Sehemu ya mipangilio ya seva mbadala huwa tayari kwa ajili ya programu za Android, ambazo zinaweza kuchagua kwa hiari kuitii. Angalia sera ya ProxyMode ili upate maelezo zaidi.
Unaweza kubainisha URL kwenye faili ya .pac ya seva mbadala hapa.
Sera hii itatekelezwa tu ikiwa umechagua mipangilio ya seva mbadala mwenyewe katika 'Chagua jinsi ya kubainisha mipangilio ya seva mbadala' na ikiwa sera ya ProxySettings haijabainishwa.
Hupaswi kuweka sera hii ikiwa umechagua hali nyingine yoyote ya kuweka sera za seva mbadala.
Kwa mifano ya kina, tembelea: https://www.chromium.org/developers/design-documents/network-settings#TOC-Command-line-options-for-proxy-sett.
Huwezi kulazimisha programu za Android zitumie seva mbadala. Sehemu ya mipangilio ya seva mbadala huwa tayari kwa ajili ya programu za Android, ambazo zinaweza kuchagua kwa hiari kuitii. Angalia sera ya ProxyMode ili upate maelezo zaidi.
Google Chrome itapuuza seva mbadala yoyote ya orodha ya seva pangishi zilizotolewa hapa.
Sera hii itatekelezwa tu ikiwa umechagua mipangilio ya seva mbadala mwenyewe katika 'Chagua jinsi ya kubainisha mipangilio ya seva mbadala' na ikiwa sera ya ProxySettings haijabainishwa.
Hupaswi kuweka sera hii ikiwa umechagua hali nyingine yoyote ya kuweka sera za seva mbadala.
Kwa mifano ya kina zaidi, tembelea: https://www.chromium.org/developers/design-documents/network-settings#TOC-Command-line-options-for-proxy-sett.
Huwezi kulazimisha programu za Android zitumie seva mbadala. Sehemu ya mipangilio ya seva mbadala huwa tayari kwa ajili ya programu za Android, ambazo zinaweza kuchagua kwa hiari kuitii. Angalia sera ya ProxyMode ili upate maelezo zaidi.
Hubainisha saa za eneo zitakazotumika katika kifaa. Sera hii ikiwekwa, watumiaji wa kifaa hawawezi kubatilisha saa za eneo zilizobainishwa. Thamani isiyo sahihi ikiwekwa, bado sera itatumika katika "GMT" badala yake. Ikiwa mfuatano usio na kitu unawekwa, sera hii haitatumika.
Sera hii isipowekwa, saa za eneo la sasa itaendelea kutumika. Hata hivyo, watumiaji wataweza kubadilisha saa za eneo.
Vifaa vipya huanza kwa kutumia saa za eneo la "Marekani/Pasifiki".
Muundo wa thamani hufuata majina ya saa za maeneo katika "IANA Time Zone Database" (angalia "https://en.wikipedia.org/wiki/Tz_database") Saa nyingi za maeneo zinaweza kurejelewa kwa "continent/large_city" au "ocean/large_city".
Hatua ya kuweka sera hii inazima kabisa chaguo la kubaini saa za eneo kiotomatiki kulingana na eneo kilipo kifaa. Pia hubatilisha sera ya SystemTimezoneAutomaticDetection.
Sera hii ikiwekwa, mtiririko wa kugundua saa za eneo kiotomatiki utakuwa katika mojawapo wa njia zifuatazo kulingana na thamani ya mipangilio:
Ikiwekwa kuwa TimezoneAutomaticDetectionUsersDecide, watumiaji wataweza kudhibiti kipengee cha kugundua saa za eneo kiotomatiki kwa kutumia vidhibiti vya kawaida katika chrome://settings.
Ikiwekwa kuwa TimezoneAutomaticDetectionDisabled, vidhibiti vya kugundua saa za eneo kiotomatiki katika chrome://settings vitazimwa. Kipengele cha kugundua saa za eneo kiotomatiki kitakuwa kimezimwa wakati wote.
Ikiwekwa kuwa TimezoneAutomaticDetectionIPOnly, vidhibiti vya saa za eneo katika chrome://settings vitazimwa. Kipengele cha kugundua saa za eneo kiotomatiki kitakuwa kimewashwa wakati wote. Kipengele cha kugundua saa za eneo kitatumia mbinu ya IP pekee kurekebisha suala la mahali.
Ikiwekwa kuwa TimezoneAutomaticDetectionSendWiFiAccessPoints, vidhibiti vya saa za eneo katika chrome://settings vitazimwa. Kipengele cha kugundua saa za eneo kiotomatiki kitakuwa kimewashwa wakati wote. Orodha ya maeneo ya kufikia WiFi yatatumwa kwenye seva ya API ya Kutambulisha Mahali Kila wakati kwa ugunduzi sahihi wa saa za eneo.
Ikiwekwa kuwa TimezoneAutomaticDetectionSendAllLocationInfo, vidhibiti vya saa za eneo katika chrome://settings vitazimwa. Kipengele cha kugundua saa za eneo kiotomatiki kitakuwa kimewashwa wakati wote. Maelezo ya eneo (kama vile maeneo ya kufikia WiFi, Minara inayoweza Kupokea mtandao, GPS) yatatumwa kwenye seva kwa ugunduzi sahihi wa saa za eneo.
Sera hii isipowekwa, itaonekana kama kwamba TimezoneAutomaticDetectionUsersDecide imewekwa.
Sera ya SystemTimezone ikiwekwa, itabatilisha sera hii. Katika hali hii kipengele cha ungunduzi wa saa za eneo kiotomatiki kitazimwa kabisa.
Hubainisha muundo wa saa ili kutumiwa kwa kifaa.
Sera hii husanidi muundo wa saa ili kutumia kwenye skrini ya kuingia katika akaunti na kama chaguomsingi kwa vipindi vya watumiaji. Bado watumiaji wanaweza kuubatilisha muundo wa saa kwa akaunti yao.
Ikiwa sera itawekwa kuwa kweli, kifaa kitatumia muundo wa saa ya saa 24. Ikiwa sera hii itawekwa kuwa uongo, kifaa kitatumia muundo wa saa ya saa 12.
Ikiwa sera hii haitawekwa, kifaa kitapuuza kuwa muundo wa saa ya saa 24.
Sera hii haitumiki tena. Tafadhali tumia RemoteAccessHostClientDomainList badala yake.
Huweka mipangilio ya majina ya kikoa cha seva pangishi yanayohitajika yatakayolazimishwa kwenye seva ya kufikiwa kwa mbali na huzuia watumiaji kulibadilisha.
Kama mipangilio hii imewashwa, basi wateja kutoka kikoa kimoja kilichobainishwa wanaweza kuunganisha kwenye seva pangishi.
Mipangilio hii ikizimwa au isipowekwa, basi sera chaguomsingi ya aina ya muunganisho hutumika. Kwa usaidizi wa mbali, sera hii huruhusu wateja kutoka kikoa chochote kuunganisha kwenye seva pangishi, wakati wowote inapoweza kufikiwa kwa mbali. Mmiliki wa seva pangishi pekee ndiye anaweza kuunganisha.
Sera hii itabatilisha RemoteAccessHostClientDomain, ikiwa ipo.
Pia angalia RemoteAccessHostDomainList.
Huwasha matumizi ya seva za STUN seva teja za mbali zinapojaribu kutambua muunganisho wa mashini hii.
Ikiwa mpangilio huu utawashwa, basi seva teja za mbali zinaweza kugundua na kuunganisha kwenye mashini hii hata kama zimetenganishwa na ngome.
Ikiwa mpangilio huu utazimwa na miunganisho ya kutoa ya UDP imechujwa na ngome, basi mashini hii itaweza tu kuruhusu miunganisho kutoka kwenye mashini ya seva teja katika mtandao wa karibu.
Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa mpangilio utawashwa.
Sera hii haitumiki tena. Badala yake, tafadhali tumia RemoteAccessHostDomainList.
Huweka mipangilio ya majina yanayotakikana ya vikoa vya seva pangishi, ambayo yatatumika kwenye seva pangishi zinazofikiwa kwa mbali na kuzuia watumiaji wasiyabadilishe.
Mipangilio hii ikiwashwa, inamaanisha kuwa seva pangishi zinaweza kushirikiwa tu kwa kutumia akaunti zilizosajiliwa kwenye mojawapo ya majina ya vikoa yaliyobainishwa.
Mipangilio hii ikizimwa au isipowekwa, inamaanisha kuwa seva pangishi zinaweza kushirikiwa kwa kutumia akaunti yoyote.
Mipangilio hii itabatilisha RemoteAccessHostDomain, ikiwa ipo.
Angalia pia RemoteAccessHostClientDomainList.
Inasanidi kiambishi awali cha TalkGadget ambacho kitatumiwa na mpangishaji wa ufikivu wa mbali na huzuia watumiaji kukibadilisha.
Kikibainishwa, kiambishi hiki awali kinasitishwa kwenye jina la msingi la TalkGadget ili kuunda jina kamili la kikoa la TalkGadget. Jina msingi la kikoa la TalkGadget ni '.talkgadget.google.com'.
Ikiwa mpangilio huu utawezeshwa, basi wapangishaji watatumia jina maalum la kikoa wakati wa kufikia TalkGadget badala ya jina chaguomsingi la kikoa.
Ikiwa mpangilio huu utalemazwa au hautawekwa, basi jina chaguomsingi la kikoa la TalkGadget ('chromoting-host.talkgadget.google.com') litatumiwa kwa wapangishaji wote.
Wateja wa ufikivu wa mbali hawaathiriki kwa mpangilio huu wa sera. Mara kwa mara watatumiwa 'chromoting-client.talkgadget.google.com' ili kufikia TalkGadget.
Inawezesha uzuiaji wa wapangishaji wa ufikivu wa mbali wakati muunganisho unapoendelea.
Ikiwa mpangilio huu utawezeshwa, basi vifaa halisi vya ingizo na towe vitalemazwa wakati muunganisho wa mbali unapoendelea.
Ikiwa mpangilio huu utalemzwa au hautawekwa, basi watumiaji wa karibu na wa mbali wanaweza kuingiliana na seva pangishi inaposhirikiwa.
Mpangilio huu ukiwashwa au usiposanidiwa, basi watumiaji wanaweza kuchagua kuoanisha viteja na mpangishi wakati wa kuunganisha, hivyo kuondoa haja ya kuingiza PIN kila wakati.
Mpangilio huu ukizimwa, basi kipengele hiki hakitapatikana.
Mpangilio huu ukiwashwa, basi maombi ya uthibitisho ya gnubby yatawekwa kama proksi kupitia muunganisho wa mpangishi wa mbali.
Mpangilio huu ukizimwa au usisanidiwe, maombi ya uthibitisho ya gnubby hayatawekwa kama proksi.
Huwasha matumizi ya seva za kutuma wakati viteja vya mbali vinajaribu kutambua muunganisho wa mashine hii.
Mipangilio hii ikiwashwa, basi viteja vya mbali vinaweza kutumia seva za kutuma ili kuunganisha kwenye mashine hii ikiwa muunganisho wa moja kwa moja unakosekana (k.m. kwa sababu ya vizuizi vya kinga mtandao).
Kumbuka kwamba ikiwa sera ya RemoteAccessHostFirewallTraversal imezimwa, sera hii haitatumiwa.
Sera hii ikiachwa bila kuwekwa, mipangilio itawashwa.
Huzuia masafa ya lango la UDP yaliyotumiwa na seva pangishi ya kufikiwa kwa mbali katika mashine hii.
Sera hii ikiachwa bila kuwekwa au ikiwekwa kuwa mfuatano usio na kitu, seva pangishi ya kufikiwa kwa mbali itaruhusiwa kutumia mlango wowote unaopatikana, isipokuwa sera ya RemoteAccessHostFirewallTraversal iwashwe, hali ambapo seva pangishi inayoweza kufikiwa kwa mbali itatumia milango ya UDP katika masafa ya 12400-12409.
Mipangilio hii ikiwashwa, basi seva pangishi inayoweza kufikiwa kwa mbali hulinganisha jina la mtumiaji wa ndani (ambalo linahusishwa na seva pangishi) na jina la akaunti ya Google lililosajiliwa kama mmiliki wa seva pangishi (yaani "johndoe" ikiwa seva pangishi inamilikiwa na akaunti ya Google ya "johndoe@example.com"). Seva pangishi inayoweza kufikiwa kwa mbali haitaanza ikiwa jina la mmiliki wa seva pangishi ni tofauti na jina la mtumiaji wa ndani linalohusishwa na seva pangishi. Sera ya RemoteAccessHostMatchUsername inapaswa kutumiwa pamoja na RemoteAccessHostDomain ili kutekeleza pia akaunti ya Google ya mmiliki wa seva pangishi inayohusishwa na kikoa mahususi (yaani "example.com").
Sera hii ikizimwa au isipowekwa, basi seva pangishi inayoweza kufikiwa kwa mbali inaweza kuhusishwa na mtumiaji yeyote wa ndani.
Sera hii ikiwekwa, seva pangishi inayoweza kufikiwa kwa mbali itahitaji kuthibitisha viteja ili kupata tokeni ya uthibitishaji kutoka URL hii ili kuunganisha. Lazima itumike pamoja na RemoteAccessHostTokenValidationUrl.
Kwa sasa kipengele hiki kimezimwa upande wa seva.
Sera hii ikiwekwa, seva pangishi ya kufikiwa kwa mbali itatumia URL hii ili kuthibitisha tokeni za uthibitishaji kutoka viteja vya kufikiwa kwa mbali ili kukubali miunganisho. Sharti itumike pamoja na RemoteAccessHostTokenUrl.
Kwa sasa kipengele hiki kimezimwa upande wa seva.
Iwapo sera hii imewekwa, seva pangishi itatumia cheti cha kiteja kilicho na jina la kawaida (CN) la kampuni ili kuthibitisha kwenye RemoteAccessHostTokenValidationUrl. Iweke kuwa "*" ili utumie cheti chochote cha kiteja kinachopatikana.
Kwa sasa kipengele hiki kimezimwa upande wa seva.
Mipangilio hii ikiwashwa, seva pangishi ya usaidizi wa mbali itatumiwa katika mchakato kwa ruhusa za uiAccess. Hii itaruhusu watumiaji wa mbali kuwasiliana kwa kutumia madirisha yaliyoinuliwa kwenye eneo-kazi la mtumiaji wa ndani.
Mipangilio hii ikizimwa au isipowekwa, seva pangishi ya usaidizi wa mbali itatumiwa katika muktadha wa mtumiaji na watumiaji wa mbali hawataweza kutumia madirisha yaliyoinuliwa kwenye eneo-kazi.
Hudhibiti uwezo wa mtumiaji aliyeunganishwa kwenye seva pangishi inayoweza kufikiwa kwa mbali kuhamisha faili kati ya kiteja na seva pangishi. Hali hii haitumiki kwenye miunganisho ya usaidizi wa mbali, ambayo haitumii kipengele cha uhamishaji wa faili.
Mipangilio hii ikizimwa, hutaruhusiwa kuhamisha faili. Mipangilio hii ikiwashwa au isipowekwa, utaruhusiwa kuhamisha faili.
Hukuruhusu kubainisha ni wapangishaji wapi wa ujumbe asili ambao hawapaswi kupakiwa.
Thamani ya orodha ya wasioidhinishwa ya '*' inamaanisha kwamba wapangishi wote wa ujumbe asili hawajaidhinishwa isipokuwa kama wamewekwa waziwazi katika orodha ya walioidhinishwa.
Kama sera hii haitawekwa Google Chrome itapakia wapangishi wote waliosakinishwa wa ujumbe asili.
Hukuruhusu kubainisha ni wapangishi wapi wa ujumbe asili wasiowekwa kwenye orodha ya wasioidhinishwa.
Thamani ya orodha ya wasioidhinishwa ya * inamaanisha wapangishi wote wa ujumbe asili hawajapewa idhini na ni wapangishi wa ujumbe asili waliowekwa kwenye orodha iliyoidhinishwa ndio watakaopakiwa pekee.
Kwa chaguomsingi, wapangishi wote wa ujumbe asili wameidhinishwa, lakini iwapo wapangishi wote wa ujumbe asili hawajaidhinishwa na sera, orodha ya walioidhinishwa inaweza kutumiwa kubatilisha sera hiyo.
Huwasha usakinishaji wa seva pangishi za Ujumbe wa Ndani wa kiwango cha mtumiaji.
Mipangilio hii ikiwashwa basi Google Chrome huruhusu matumizi ya seva pangishi za Ujumbe wa Ndani wa kiwango cha mtumiaji.
Ikiwa mipangilio hii imezimwa, basi Google Chrome itatumia tu seva pangishi za Ujumbe wa Ndani wa kiwango cha mtumiaji.
Ikiwa mipangilio hii imeachwa bila kuwekwa, Google Chrome itaruhusu matumizi ya Ujumbe wa Ndani wa kiwango cha mtumiaji.
Hubainisha urefu wa muda bila mchango wa mtumiaji ambapo baadaye skrini hufifilizwa inapoendeshwa kwenye nishati ya betri.
Sera hii inapowekwa kwenye thamani kubwa zaidi ya sufuri, hubainisha urefu wa muda ambao lazima mtumiaji asalie bila shughuli kabla ya Google Chrome OS kufifiliza skrini.
Sera hii inapowekwa kwenye sufuri, Google Chrome OS haififilizi skrini mtumiaji anaposalia bila shughuli.
Sera hii inapokuwa haijawekwa, urefu wa muda wa chaguomsingi unatumiwa.
Sera ya thamani inastahili kubainishwa kwa nukta. Thamani zinabanwa ili kuwa chini ya ucheleweshaji wa kutokuwa na shughuli.
Hubainisha urefu wa muda bila mchango wa mtumiaji ambapo baadaye skrini huzimwa inapoendeshwa kwa nishati ya AC.
Sera hii inapowekwa kwenye thamani kubwa zaidi ya sufuri, hubainisha urefu wa muda ambao lazima mtumiaji asalie bila shughuli kabla ya Google Chrome OS kuzima skrini.
Sera hii inapowekwa kwenye sufuri, Google Chrome OS haizimi skrini mtumiaji anaposalia bila shughuli.
sera hii inapokuwa haijawekwa, urefu wa chaguomsingi hutumiwa.
Sera ya thamani inastahili kubainishwa kwa nukta. Thamani zinabanwa ili kuwa chini ya ucheleweshaji wa kutokuwa na shughuli.
Hubainisha urefu wa muda bila mchango wa mtumiaji ambapo baadaye skrini hufungwa inapoendeshwa kwa nishati ya AC.
Sera hii inapowekwa kwenye thamani kubwa zaidi ya sufuri, hubainisha urefu wa muda ambao lazima mtumiaji asalie bila shughuli kabla ya Google Chrome OS kufunga skrini.
Sera hii inapowekwa kwenye sufuri, Google Chrome OS haifungi skrini mtumiaji anaposalia bila shughuli.
Sera hii inapokuwa haijawekwa, urefu wa chaguomsingi unatumiwa.
Njia iliyopendekezwa ya kufunga skrini isiyo na shughuli ni kuwezesha ufungaji skrini iliyositishwa na kusitisha Google Chrome OS baada ya onyesho liliso na shughuli. Sera hii inastahili kutumiwa tu wakati ambapo ufungaji wa skrini utatokea kwa muda mrefu kuliko kusitisha au usitishaji usio na shughuli hauhitajiki hata kidogo.
Sera ya thamani inastahili kubainishwa kwa nukta. Thamani zinabanwa ili kuwa chini ya ucheleweshaji wa kutokuwa na shughuli.
Inabainisha kipindi ambacho mtumiaji hajatumia programu na baada ya muda huo, kidirisha cha ilani kitaonyeshwa wakati inatumia nishati ya AC.
Sera hii ikiwekwa, inabainisha kipindi ambacho mtumiaji ni sharti awe hajafanya kitu kwenye programu kabla ya Google Chrome OS kuonyesha kidirisha cha ilani kinachomwarifu mtumiaji kwamba hatua ya kutofanya kitu inakaribia kutekelezwa.
Sera hii isipowekwa, hakuna kidirisha cha ilani kitakachoonyeshwa.
Thamani ya sera sharti ibainishwe katika milisekunde. Thamani zinawekwa kuwa chini au sawa na ucheleweshaji wa kukosa kufanya kitu.
Ujumbe wa ilani unaonyeshwa tu ikiwa kitendo cha kutofanya kitu ni kuingia katika akaunti au kuzima.
Hubainisha urefu wa muda bila mchango wa mtumiaji ambao baadaye hatua isiyo na shughuli huchukuliwa inapoendeshwa kwenye nishati ya AC.
Sera hii inapowekwa, hubainisha urefu wa muda ambao lazima mtumiaji asalie bila shughuli kabla ya Google Chrome OS kuchukua hatua ya kutokuwa na shughuli, kinachoweza kusanidiwa tofauti.
Sera hii inapokuwa haijawekwa, urefu wa muda wa chaguomsingi hutumiwa.
Sera ya thamani inastahili kubainishwa kwa nukta.
Hubainisha urefu wa muda bila mchango wa mtumiaji ambapo baadaye skrini hufifilizwa inapoendeshwa kwenye nishati ya betri.
Sera hii inapowekwa kwenye thamani kubwa zaidi ya sufuri, hubainisha urefu wa muda ambao lazima mtumiaji asalie bila shughuli kabla ya Google Chrome OS kufifiliza skrini.
Sera hii inapowekwa kwenye sufuri, Google Chrome OS haififilizi skrini mtumiaji anaposalia bila shughuli.
Sera hii inapokuwa haijawekwa, urefu wa muda wa chaguomsingi unatumiwa.
Sera ya thamani inastahili kubainishwa kwa nukta. Thamani zinabanwa ili kuwa chini ya ucheleweshaji wa kutokuwa na shughuli.
Hubainisha urefu wa muda bila mchango wa mtumiaji ambapo baadaye skrini inazimwa inapoendeshwa kwenye nishati ya betri.
Sera hii inapowekwa kwenye thamani kubwa zaidi ya sufuri, hubainisha urefu wa muda ambao lazima mtumiaji asalie bila shughuli kabla ya Google Chrome OS kuzima skrini.
Sera hii inapowekwa kwenye sufuri, Google Chrome OS haizimi skrini mtumiaji anaposalia bila shughuli.
Sera hii inapokuwa haijawekwa, urefu wa muda wa chaguomsingi unatumiwa.
Sera ya thamani inastahili kubainishwa kwa nukta. Thamani zinabanwa ili kuwa chini ya ucheleweshaji wa kutokuwa na shughuli.
Hubainisha urefu wa muda bila mchango wa mtumiaji ambapo baadaye skrini hufungwa inapoendeshwa kwa nguvu ya betri.
Sera hii inapowekwa katika thamani kubwa zidi ya sufuri, hubainisha urefu wa muda ambao lazima mtumiaji asalie bila shughuli kabla ya Google Chrome OS kufunga skrini.
Sera hii inapowekwa kwenye sufuri, Google Chrome OS haifungi skrini mtumiaji anaposalia bila shughuli.
sera hii inapokuwa haijawekwa, urefu wa chaguomsingi unatumiwa.
Njia inayopendekezwa ya kufunga skrini isiyo na shughuli ni kuwezesha ufungaji skrini iliyositishwa na kusitisha Google Chrome OS baada ya onyesho liliso na shughuli. Sera hii inastahili kutumiwa tu wakati ambapo ufungaji wa skrini utatokea kwa muda mrefu kuliko kusitisha au usitishaji usio na shughuli hauhitajiki hata kidogo.
Sera ya thamani inastahili kubainishwa kwa nukta. Thamani zinabanwa ili kuwa chini ya ucheleweshaji wa kutokuwa na shughuli.
Inabainisha kipindi ambacho mtumiaji hatumii programu na baada ya muda huo kidirisha cha ilani kitaonyeshwa wakati inatumia nishati ya betri.
Sera hii ikiwekwa, inabainisha kipindi ambacho mtumiaji ni sharti awe hajafanya kitu kwenye programu kabla ya Google Chrome OS kuonyesha kidirisha cha ilani kinachomwarifu mtumiaji kwamba hatua ya kutofanya kitu inakaribia kutekelezwa.
Sera hii isipowekwa, hakuna kidirisha cha ilani kitakachoonyeshwa.
Thamani ya sera sharti ibainishwe katika milisekunde. Thamani zinawekwa kuwa chini au sawa na ucheleweshaji wa kukosa kufanya kitu.
Ujumbe wa ilani unaonyeshwa tu ikiwa kitendo cha kutofanya kitu ni kuingia katika akaunti au kuzima.
Hubainisha urefu wa muda bila mchango wa mtumiaji ambapo baadaye skrini hufifilizwa inapoendeshwa kwenye nishati ya betri.
Sera hii inapowekwa, hubainisha urefu wa muda ambao lazima mtumiaji asalie bila shughuli kabla ya Google Chrome OS kuchukua hatua ya kutokuwa na shughuli, inayoweza kusanidiwa tofauti.
Sera hii inapokuwa haijawekwa, urefu wa muda wa chaguomsingi unatumiwa.
Sera ya thamani inastahili kubainishwa kwa nukta.
Kumbuka kwamba sera hii haitumiki na itaondolewa katika siku zijazo.
Sera hii inatoa thamani mbadala ya sera mahususi zaidi za IdleActionAC na IdleActionBattery. Sera hii ikiwekwa, thamani yake inatumika ikiwa sera mahususi zaidi zinazowiana hazijawekwa.
Sera hii isipowekwa, sifa za sera mahususi zaidi haziathiriwi.
Sera hii inapowekwa, hubainisha hatua ambayo Google Chrome OS huchukua wakati mtumiaji anasalia bila shughuli kwa urefu wa muda uliotolewa na ucheleweshaji wa kutokuwa na shughuli, unaoweza kuwekewa mipangilio tofauti.
Sera hii isipowekwa, hatua chaguomsingi huchukuliwa, ambayo ni 'kusimamisha'.
Ikiwa hatua imesimamishwa, Google Chrome OS inaweza kuwekewa mipangilio tofauti ili kufunga au kutofunga skrini kabla ya kusimamisha.
Sera hii inapowekwa, hubainisha hatua ambayo Google Chrome OS huchukua wakati mtumiaji anasalia bila shughuli kwa urefu wa muda uliotolewa na ucheleweshaji wa kutokuwa na shughuli, unaoweza kuwekewa mipangilio tofauti.
Sera hii isipowekwa, hatua chaguomsingi huchukuliwa, ambayo ni 'kusimamisha'.
Ikiwa hatua imesimamishwa, Google Chrome OS inaweza kuwekewa mipangilio tofauti ili kufunga au kutofunga skrini kabla ya kusimamisha.
Sera hii ikiwekwa, itabainisha kitendo ambacho Google Chrome OS itafanya wakati mtumiaji atafunga kifuniko cha kifaa.
Sera hii isipowekwa, hatua chaguomsingi huchukuliwa, ambayo ni 'kusimamisha'.
Ikiwa hatua imesimamishwa, Google Chrome OS inaweza kuwekewa mipangilio tofauti ili kufunga au kutofunga skrini kabla ya kusimamisha.
Ikiwa sera hii imewekwa kuwa Ndivyo au isiwekwe, mtumiaji anaweza kuzingatia kutokuwa na shughuli wakati faili ya sauti inacheza. Hali hii huzuia hali ya kuisha kwa muda wa kutokuwa na shughuli kufikiwa na kitendo cha kutokuwa na shughuli kuchukuliwa. Hata hivyo, hatua za ufifiaji wa mwangaza wa skrini, skrini kuzima na kufunga skrini zitatekelezwa baada ya muda wa kuweka mipangilio kuisha, licha ya shughuli za sauti.
Sera hii ikiwekwa kuwa Sivyo, shughuli ya sauti haizuii mtumiaji kuchukuliwa kuwa hana shughuli.
Sera hii ikiwekwa kuwa Ndivyo au isipowekwa, mtumiaji hachukuliwi kuwa hana shughuli video inapocheza. Hii inazuia kufikia ucheleweshaji wa kutokuwa na shughuli, ufifiaji wa mwangaza wa skrini, ucheleweshaji wa kuzimika kwa skrini na ucheleweshaji wa kufunga kwa skrini na hatua zinazofanana zisitekelezwe.
Sera hii ikiwekwa kuwa Sivyo, shughuli za video hazizuii mtumiaji kuchukuliwa kuwa hana shughuli.
Video inayocheza katika programu za Android haizingatiwi, hata kama sera hii imewekwa kuwa True.
Hubainisha asilimia ambayo ucheleweshaji wa kufifia kwa mwangaza wa skrini hukuzwa iwapo kifaa kipo katika hali ya wasilisho.
Ikiwa sera hii imewekwa, itabainisha asilimia ambayo ucheleweshaji wa kufifia kwa mwangaza wa skrini hukuzwa iwapo kifaa kipo katika hali ya wasilisho. Wakati asilimia ambayo ucheleweshaji wa kufifia kwa mwangaza wa skrini imekuzwa, kipengele cha kuzima skrini, mbinu ya kufunga skrini na kipengele cha kuchelewesha kifaa kisiwe katika hali tuli hubadilishwa ili kudumisha vipindi sawa kutoka ucheleweshaji wa kufifia kwa skrini, jinsi ilivyowekwa katika mipangilio ya awali.
Sera hii isipowekwa, thamani chaguomsingi ya ukuzaji hutumika.
Sera hii hutumika ikiwa tu PowerSmartDimEnabled imezimwa. Vinginevyo, sera hii haitumiki kwa sababu ucheleweshaji wa kufifia kwa mwangaza wa skrini hubainishwa na muundo wa mashine kujifunza.
Ni lazima thamani ya ukuzaji iwe 100% au zaidi. Haturuhusu thamani ambazo zitafanya muda wa ucheleweshaji wa kufifia kwa mwangaza wa skrini katika hali ya wasilisho uwe mfupi kuliko muda wa kawaida wa ucheleweshaji wa kufifia kwa mwangaza wa skrini.
Hubainisha iwapo wake lock zinaruhusiwa. Wake lock zinaweza kuombwa na viendelezi kupitia API ya kiendelezi cha udhibiti wa nishati na programu za ARC.
Iwapo sera hii imewekwa kuwa ndivyo au haijawekwa, wake lock hazitatekelezwa katika udhibiti wa nishati.
Iwapo sera hii imewekwa kuwa sivyo, maombi ya wake lock hayatazingatiwa.
Hubainisha iwapo wake lock za skrini zinaruhusiwa. Wake lock za skrini zinaweza kuombwa na viendelezi kupitia API ya kiendelezi cha udhibiti wa nishati na programu za ARC.
Iwapo sera hii imewekwa kuwa ndivyo au haijawekwa, wake lock za skrini hazitatekelezwa katika udhibiti wa nishati, isipokuwa AllowWakeLocks iwekwe kuwa sivyo.
Iwapo sera hii imewekwa kuwa sivyo, maombi ya wake lock ya skrini yatashushwa hadhi yawe maombi ya wake lock ya mfumo.
Hubainisha asilimia ambayo ucheleweshaji wa kufifia kwa mwangaza wa skrini hukuzwa wakati shughuli za watumiaji zinachunguzwa, mwangaza wa skrini ukiwa umefifia au pindi tu skrini inapozimwa.
Sera hii ikiwekwa, itabainisha asilimia ambayo ucheleweshaji wa kufifia kwa mwangaza wa skrini hukuzwa wakati shughuli za watumiaji zinachunguzwa, mwangaza wa skrini ukiwa umefifia au pindi tu skrini inapozimwa. Wakati ucheleweshaji wa kufifia kwa mwangaza wa skrini umekuzwa, vipengele vya kufunga skrini na kuchelewesha hali tuli hubadilishwa ili kudumisha kipindi sawa kutoka ucheleweshaji wa kufifia kwa mwangaza wa skrini jinsi ilivyowekwa katika mipangilio ya awali.
Sera hii isipowekwa, thamani chaguomsingi ya ukuzaji hutumika.
Sera hii hutumika ikiwa sera ya PowerSmartDimEnabled imezimwa. Vinginevyo, sera hii haitumiki kwa sababu ucheleweshaji wa kufifia kwa mwangaza wa skrini hubainishwa na muundo wa mashine kujifunza.
Ni lazima thamani ya ukuzaji iwe 100% au zaidi.
Hubainisha iwapo ucheleweshaji wa usimamizi wa nishati na kikomo cha urefu wa kipindi lazima tu uanze kutekeleza baada ya kuonekana kwa shughuli ya kwanza ya mtumiaji katika kipindi.
Iwapo sera hii imewekwa kuwa Ndivyo, ucheleweshaji wa usimamizi wa nishati na kikomo cha urefu wa kipindi havianzi kutekeleza mpaka shughuli ya kwanza ya mtumiaji ionekane katika kipindi.
Iwapo sera hii imewekwa kuwaSivyo ama imeachwa bila kuwekwa, ucheleweshaji wa usimamizi wa nishati na kikomo cha urefu wa kipindi huanza kutekeleza mara tu kipindi kinapoanza.
Sera hii hudhibiti mipangilio mingi ya mikakati ya kusimamia nishati mtumiaji anapokosa kufanya kitu.
Kuna hatua za aina nne: * Mwanga wa skrini utafifia iwapo mtumiaji hafanyi kitu katika muda uliobainishwa na |ScreenDim|. * Skrini itazimwa iwapo mtumiaji hafanyi kitu katika muda uliobainishwa na |ScreenOff|. * Kidirisha cha ilani kitaonyeshwa iwapo mtumiaji hafanyi kitu katika muda uliobainishwa na |IdleWarning|, kumwambia mtumiaji kuwa hatua ya kutofanya kitu imekaribia kuchukuliwa ikiwa kitendo cha kutofanya kitu ni kuondoka katika akaunti au kuzima. * Hatua iliyobainishwa na |IdleAction| itachukuliwa iwapo mtumiaji hatafanya kitu katika muda uliobainishwa na |Idle|.
Kwa kila moja ya vitendo vya hapo juu, lazima ucheleweshaji ubainishwe katika milisekunde, na unahitaji kuwekwa katika thamani inayozidi sufuri ili kusababisha kitendo husika. Iwapo ucheleweshaji umewekwa kuwa sufuri, Google Chrome OS haitatekeleza kitendo husika.
Kwa kila moja ya ucheleweshaji wa hapo juu, muda usipowekwa, thamani chaguomsingi itatumika.
Kumbuka kwamba thamani za |ScreenDim| zitawekwa kuwa chini ama sawa na |ScreenOff|, |ScreenOff| na |IdleWarning| zitawekwa kuwa chini au sawa na |Idle|.
|IdleAction| inaweza kuwa moja ya vitendo vinne: * |Suspend| * |Logout| * |Shutdown| * |DoNothing|
Wakati |IdleAction| haijawekwa, hatua chaguomsingi huchukuliwa, ambayo ni kusimamisha.
Pia kuna mipangilio tofauti ya betri na nishati ya AC.
Hubainisha urefu wa muda bila ingizo la mtumiaji ambapo baada ya hapo skrini hufungwa inapoendeshwa kwa nishati ya AC au betri.
Urefu wa muda unapowekwa thamani kubwa kuliko sifuri, inawakilisha urefu wa muda ambao mtumiaji lazima abaki akiwa hafanyi kitu kabla Google Chrome OS skrini kufunga.
Urefu wa muda unapowekwa kuwa sifuri, Google Chrome OS haifungi skrini mtumiaji anapokuwa hafanyi kitu.
Urefu wa muda unapoondolewa, urefu wa muda chaguomsingi hutumika.
Njia iliyopendekezwa ya kufunga skrini ambayo haifanyi kazi ni kuwasha kufunga skrini kwenye kusimamisha na Google Chrome OS kusimamisha baada ya ucheleweshaji wa kutofanya kitu. Sera hii lazima itumike wakati kufunga skrini kunatokea muda kiasi kikubwa kuliko kusimamisha au wakati kusimamisha wakati haifanyi kitu hakutakikani kabisa.
Thamani ya sera inapaswa kubainishwa katika milisekunde. Thamani huwekwa pamoja kuwa chini ya ucheleweshaji wa kutofanya kitu.
Hubainisha ikiwa muundo mahari wa kufifiliza mwangaza unaruhusiwa kupitisha muda hadi wakati mwangaza wa skrini utakuwa hafifu.
Wakati mwangaza wa skrini uko karibu kuwa hafifu, muundo mahiri wa kufifiliza hutathmini ikiwa inafaa kuongeza muda wa kufifiliza mwangaza wa skrini. Ikiwa kipengele mahiri cha kufifiliza mwangaza kinaacha kufifiliza mwangaza wa skrini, kitaongeza muda hadi wakati skrini itafifilizwa. Katika hali hii, kipengele cha kuzima skrini, cha kufunga skrini na cha kuchelewesha kuweka skrini tuli, kitarekebishwa ili kudumisha kipindi sawa kuanzia ucheleweshaji wa kufifilizwa kwa mwangaza wa skrini jinsi ilivyopangwa hapo awali.
Ikiwa sera hii imewekwa kuwa Ndivyo au haijawekwa, kipengele cha muundo mahiri wa kufifiliza mwangaza kitawashwa na kuruhusiwa kupitisha muda hadi wakati mwangaza wa skrini itafifilizwa. Ikiwa sera hii inawekwa kuwa Sivyo, kipengele cha muundo mahiri wa kufifiliza skrini hakitaathiri ufifilizaji wa skrini.
Hubainisha asilimia ya ung'avu wa skrini. Iwapo sera hii imewekwa, ung'avu wa skrini ya mwanzo unabadilishwa uwe thamani ya sera, lakini mtumiaji anaweza kuubadilisha baadaye. Vipengele vya ung'avu wa kiotomatiki huzimwa. Iwapo sera hii haijawekwa, vidhibiti vya skrini ya mtumiaji na vipengele vya ung'avu wa kiotomatiki haviathiriwi. Thamani za sera zinapaswa kubainishwa katika asilimia kati ya 0 na 100.
Weka kipengele kinachopunguza matumizi ya betri kwa kubadilisha mfumo kuendeshwa kwenye nguvu za betri katika asilimia.
Sera hii hutumika tu ikiwa DevicePowerPeakShiftEnabled imewekwa kuwa ndivyo.
Usipoweka sera hii au mipangilio yake, kipengele kinachopunguza matumizi ya betri kwa kubadilisha mfumo kuendeshwa kwenye nguvu za betri kitazimwa kila wakati.
Weka mipangilio ya siku ya kipengele kinachopunguza matumizi ya betri kwa kubadilisha mfumo kuendeshwa kwenye nguvu za betri
Sera hii hutumika tu ikiwa DevicePowerPeakShiftEnabled imewekwa kuwa ndivyo.
Usipoweka sera hii au mipangilio yake, kipengele kinachopunguza matumizi ya betri kwa kubadilisha mfumo kuendeshwa kwenye nguvu za betri kitazimwa kila wakati.
Kumbuka: thamani zinazokubalika za sehemu ya minute katika start_time, end_time na charge_start_time ni 0, 15, 30, 45.
Washa sera ya udhibiti ya kipengele kinachopunguza matumizi ya betri kwa kubadilisha mfumo kuendeshwa kwenye nguvu za betri.
Kipengele Kinachopunguza Matumizi ya Betri kwa Kubadilisha Mfumo Kuendeshwa kwenye Nguvu za Betri ni sera ya kuokoa betri ambayo hupunguza utumiaji wa chaji inayobadilikabadilika wakati betri inatumika zaidi mchana. Kwa kila siku ya wiki unaweza kuweka muda wa kuanza na kumaliza kutumia hali ya Kipengele Kinachopunguza Matumizi ya Betri kwa Kubadilisha Mfumo Kuendeshwa kwenye Nguvu za Betri. Katika kipindi hiki, mfumo utatumia betri hata kama chaji inayobadilikabadilika imewekwa mradi betri haipungui kiwango cha nishati kilichobainishwa. Baada ya muda uliobainishwa kuisha, mfumo utatumia chaji inayobadilikabadilika ikiwekwa lakini haitachaji betri. Mfumo utafanya kazi tena kama kawaida ukitumia chaji inayobadilikabadilika na kuchaji betri tena baada ya Muda Uliobainishwa wa Kuanza wa Kuchaji.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo na DevicePowerPeakShiftBatteryThreshold, DevicePowerPeakShiftDayConfig ziwekwe, kipengele kinachopunguza matumizi ya betri kwa kubadilisha mfumo kuendeshwa kwenye nguvu za betri kitawashwa kila wakati ikiwa kinaweza kinatumika kwenye kifaa hiki.
Sera ikiwekwa kuwa sivyo, kipengele kinachopunguza matumizi ya betri kwa kubadilisha mfumo kuendeshwa kwenye nguvu za betri kitazimwa kila wakati.
Sera hii ikiwekwa, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuibatilisha.
Sera hii isipowekwa, kipengele kinachopunguza matumizi ya betri kwa kubadilisha mfumo kuendeshwa kwenye nguvu za betri kitazima kwanza na hakiwezi kuwashwa na mtumiaji.
Washa sera ya kudhibiti nishati ya AC ya kuwasha kifaa.
Nishati ya AC ya kuwasha kifaa huruhusu mfumo kuwaka kiotomatiki kutoka hali ya IMEZIMWA/Tuli wakati unaingiza kebo ya nishati.
Sera hii ikiwekwa kuwa 'ndiyo' inamaanisha kuwa nishati ya AC ya kuwasha kifaa itawaka kila wakati iwapo inaweza kutumika kwenye kifaa.
Sera hii ikiwekwa kuwa 'sivyo', nishati ya AC ya kuwasha kifaa itazimwa kila wakati.
Sera hii ikiwekwa, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuibatilisha.
Ikiwa sera hii haijawekwa, nishati ya AC ya kuwasha kifaa itazimwa na mtumiaji hataweza kuiwasha.
Ruhusu sera ya kudhibiti nishati ya hali ya kuchaji betri kwa kina.
Hali ya Kuchaji Betri kwa kina huruhusu mtumiaji kuimarisha muda wa kutumia betri. Katika Hali ya Kuchaji kwa Kina, mfumo utatumia algoriti ya kawaida ya kuchaji na mbinu zingine wakati betri haitumiki ili kuimarisha muda wa kutumia betri. Wakati betri inatumika, hali ya kuchaji ya moja kwa moja hutumika. Hali ya kuchaji moja kwa moja huruhusu betri kuchaji kwa haraka zaidi, kwa hivyo, betri hujaa chaji haraka. Kila siku, wakati ambao mfumo unatumika zaidi hubainishwa na muda wa kuanza na kudumu kwa shughuli.
Sera hii ikiwekwa kuwa 'ndivyo' na DeviceAdvancedBatteryChargeModeDayConfig iwekwe, basi hali ya kuchaji kwa kina itaendelea kuwaka kila wakati ikiwa inatumika kwenye kifaa.
Sera hii ikiwekwa kuwa 'sivyo', hali ya kuchaji kwa kina itabaki kuwa imezimwa.
Ukiweka sera hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha wala kuibatilisha.
Sera hii isipowekwa, hali ya kuchaji betri kwa kina huzimwa na haiwezi kuwashwa na mtumiaji.
Weka mipangilio ya mchana ya hali ya kuchaji betri kwa kina.
Sera hii hutumika tu ikiwa DeviceAdvancedBatteryChargeModeEnabled imewekwa kuwa ndivyo.
Mipangilio ya sera hii isipowekwa, hali ya kuchaji betri kwa kina itabaki ikiwa imezimwa kila wakati.
Kumbuka: Ni lazima charge_start_time isipite charge_end_time.
Kumbuka: thamani zinazoruhusiwa za sehemu ya minute ya charge_start_time nacharge_end_time ni 0, 15, 30, 45.
Hubainisha sera ya kudhibiti nishati ya hali ya kuchaji betri.
Dhibiti hali inayobadilika ya kuchaji betri ili kupunguza hali ya betri kuharibika kutokana na kutumika zaidi na uongeze muda wa matumizi ya betri.
Ikiwa hali maalum ya kuchaji betri imechaguliwa basi ni lazima DeviceBatteryChargeCustomStartCharging na DeviceBatteryChargeCustomStopCharging zibainishwe.
Sera hii ikiwekwa, hali ya kuchaji betri itatekelezwa ikiwa inaweza kutumika kwenye kifaa.
Sera hii ikiachwa bila kuwekwa na iwe inaweza kutumika kwenye kifaa, hali ya kawaida ya kuchaji betri itatumika na haitaweza kubadilishwa na mtumiaji.
Kumbuka: DeviceAdvancedBatteryChargeModeEnabled hubatilisha sera hii ikiwa sera ya awali imebainishwa.
Weka mapendeleo ya muda wa kuanza kuchaji betri katika asilimia.
Betri huanza kuchaji inapofikia kiwango maalum cha kuanza kuchaji.
Lazima DeviceBatteryChargeCustomStartCharging iwe chini ya DeviceBatteryChargeCustomStopCharging.
Sera hii hutumika ikiwa tu DeviceBatteryChargeMode imewekwa kuwa sera maalum.
Mipangilio ya sera hii isipowekwa, hali ya kawaida ya kuchaji betri itatumiwa.
Weka mapendeleo ya muda wa kusimamisha kuchaji betri katika asilimia.
Betri huacha kuchaji inapofikia kiwango cha kuacha kuchaji ulichobainisha.
Lazima DeviceBatteryChargeCustomStartCharging iwe chini ya DeviceBatteryChargeCustomStopCharging.
Sera hii hutumika ikiwa tu DeviceBatteryChargeMode imewekwa kuwa sera maalum.
Mipangilio ya sera hii isipowekwa, hali ya kawaida ya kuchaji betri itatumiwa.
Ruhusu sera ya kudhibiti kushiriki nishati kwa kutumia USB.
Vifaa fulani huwa na mlango mahususi wa USB uliowekewa alama ya radi au aikoni ya betri ambayo inaweza kutumika kuchaji vifaa kama vile simu ya mkononi kwa kutumia mfumo wa betri. Sera hii huathiri shughuli ya kuchaji ya mlango huu wakati mfumo uko katika hali tuli na hali za kuzima. Sera hii haiathiri milango mingine ya USB na shughuli ya kuchaji wakati mfumo unatumika.
Mfumo unapotumika, mlango wa USB utatoa nishati kila wakati.
Mfumo ukiwa katika hali tuli, ikiwa sera hii imewekwa kuwa 'ndivyo', basi nishati itatolewa kwenye mlango wa USB wakati kifaa kitachomekwa katika chaja iliyo ukatani au ikiwa kiwango cha betri ni > 50%. Vinginevyo, hakuna nishati itakayotolewa.
Mfumo ukiwa umezimwa, ikiwa sera hii imewekwa kuwa 'ndivyo', basi nishati itatolewa kwenye mlango wa USB wakati kifaa kimechomekwa katika chaja iliyo ukutani. Vinginevyo, hakuna nishati itakayotolewa.
Sera hii ikiachwa bila kuweka, sera inawashwa na haiwezi kuzimwa na mtumiaji.
Hubainisha mipango ya uthibitishaji wa HTTP inayotumia na Google Chrome.
Thamani zinazowezekana ni 'basic', 'digest', 'ntlm' na 'negotiate'. Tenganisha thamani anuwai kwa koma.
Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa, mipango yote minne itatumika.
Inabainisha ikiwa Kerberos SPN ilitengenezwa kulingana na jina la kanuni ya DNS au jina halisi lililoingizwa.
Ukiwezesha mpangilio huu, kidokezo cha CNAME kitaachwa na jina la seva litatumiwa kama lilivyoingizwa.
Ukilemaza mpangilio huu au uuache bila kuuweka, jina la kanuni la seva litathibitishwa kupitia kidokezo cha CNAME.
Inabainisha ikiwa Kerberos SPN zilizotengenezwa zinafaa kujumuisha lango lisilo wastani.
Ukiwezesha mpangilio huu, na lango lisilo wastani (yaani, lango jingine lisilo la 80 au 443) liingizwe, itajumuishwa katika Kerberos SPN iliyotengenezwa.
Ukilemaza mpangilio huu au uuache bila kuwekwa, Kerberos SPN zilizotengenezwa hazitajumuisha lango kwa namna yoyote.
Hubainisha ni seva zipi zinazowekwa katika orodha ya zilizoidhinishwa kwa uthibitishaji uliojumuishwa. Uthibitishaji uliojumuishwa unawashwa tu wakati ambapo Google Chrome inapokea shindano kutoka kwenye proksi au seva iliyo katika orodha hii iliyoruhusiwa.
Seva nyingi tofauti zenye koma. Kadi egemezi (*) zinaruhusiwa.
Ukiacha sera hii bila kuiweka Google Chrome itajaribu kugundua ikiwa seva iko kwenye Intraneti na hapo ndipo itajibu maombi ya IWA pekee. Iwapo seva itagunduliwa kama Intraneti basi maombi ya IWA yatapuuzwa na Google Chrome.
Seva ambazo Google Chrome inaweza kuwekea majukumu.
Tenganisha majina mengi ya seva kwa koma. Herufi wakilishi (*) zinaruhusiwa.
Ukiacha sera hii bila kuiweka Google Chrome haitaweza kuweka majukumu ya vitambulisho vya mtumiaji hata ikiwa seva itagunduliwa kama Intraneti.
Hudhibiti ikiwa uidhinishaji wa sera ya KDC unazingatiwa katika uamuzi wa kutoa tiketi za Kerberos.
Ikiwa sera hii imewekwa kuwa ndivyo, uthibitishaji wa HTTP utazingatia uidhinishaji wa sera ya KDC, kwa mfano, Chrome hutoa tu kitambulisho ikiwa KDC imeweka OK-AS-DELEGATE kwenye tiketi ya huduma. Tafadhali angalia https://tools.ietf.org/html/rfc5896.html ili upate maelezo zaidi. Ni sharti huduma ilingane na sera ya 'AuthNegotiateDelegateWhitelist'.
Ikiwa sera hii haijawekwa au imewekwa kuwa sivyo, sera ya KDC haitazingatiwa kwenye mifumo inayotumika na itazingatia sera ya 'AuthNegotiateDelegateWhitelist' pekee.
Kwenye Windows, sera KDC huzingatiwa kila wakati.
Hubainisha maktaba yapi ya GSSAPI ya kutumia kwa uthibitishaji wa HTTP. Unaweza kuweka tu jina la maktaba, au njia kamili.
Ikiwa hakuna mipangilio iliyotolewa, Google Chrome itaendelea kutumia jina chaguomsingi la maktaba.
Hubainisha aina ya akaunti ya akaunti zinazotolewa na programu ya uthibitishaji wa Android inayotumia uthibitishaji wa HTTP Negotiate (k.m. uthibitishaji wa Kerberos). Maelezo haya yanapaswa kupatikana kutoka kwa muuzaji wa programu ya uthibitishaji. Kwa maelezo zaidi angalia https://goo.gl/hajyfN.
Ikiwa mipangilio haijatolewa, uthibitishaji wa HTTP Negotiate utazimwa kwenye Android.
Hudhibiti iwapo maudhui madogo ya wengine kwenye ukurasa yanaruhusiwa kuibukiza kisanduku kidadisi cha HTTP Basic Auth.
Kwa kawaida hii inalemazwa kama ulinzi wa uhadaaji. Ikiwa sera hii haijawekwa, hii italemazwa na maudhui madogo ya wengine hayataruhusiwa kuibukiza kisanduku kidadisi cha HTTP Basic Auth.
Hudhibiti ikiwa NTLMv2 imewashwa.
Matoleo yote ya hivi majuzi ya seva za Samba na Windows yanatumia NTLMv2. Hali hii inastahili kuzimwa ili matoleo ya awali yaoane pekee na hupunguza usalama wa uthibishaji.
Kama sera hii haijawekwa, sera chaguomsing itakuwa ndivyo na NTLMv2 imewashwa.
Ikiwa ndivyo, ushuhuda wa mbali huruhusiwa kwa ajili ya kifaa na cheti kitazalishwa kiotomatiki na kupakiwa kwenye Seva ya Udhibiti wa Kifaa.
Ikiwa imewekwa kuwa sivyo, au haijawekwa, hakuna cheti kitakachozalishwa na simu kwa API ya kiendelezi cha enterprise.platformKeys zitashindwa.
Ikiwekwa kuwa ndivyo, mtumiaji anaweza kutumia maunzi kwenye vifaa vya Chrome ili kudhibiti kwa umbali utambulisho wake katika CA ya faragha kupitia Enterprise Platform Keys API akitumia chrome.enterprise.platformKeys.challengeUserKey().
Ikiwekwa kuwa sivyo, au isipowekwa, majaribio ya kuwasiliana na API hayatafanikiwa na kutakuwa na msimbo wa hitilafu.
Sera hii hubainisha viendelezi vinavyoruhusiwa kutumia utendaji wa Enterprise Platform Keys API chrome.enterprise.platformKeys.challengeUserKey() kwa uthibitishaji wa mbali. Lazima viendelezi viongezwe kwenye orodha hii ili kutumia API.
Ikiwa kiendelezi hakiko kwenye orodha, au orodha haijawekwa, mawasiliano na API hayatafanikiwa na kutakuwa na msimbo wa hitilafu.
Vifaa vyenye Chrome OS vinaweza kutumia uwezo wa kuthibitisha kutoka mbali (Ufikiaji Uliothibitishwa) kupata cheti kilichotolewa na Chrome OS CA kinachothibitisha kuwa kifaa kimekubaliwa kucheza maudhui yanayolindwa. Utaratibu huu unahusisha kutumia Chrome OS CA maelezo maalum ya kuthibitisha maunzi yanayokitambua kifaa husika.
Kama mipangilio hii si ya kweli, kifaa hakitatumia uwezo wa kuthibitisha kutoka mbali kulinda maudhui na huenda kifaa hakitaweza kucheza maudhui yanayolindwa.
Kama mipangilio hii ni ya kweli, au kama haitawekwa, huenda uwezo wa kuthibitisha kutoka mbali utatumika kulinda maudhui.
Hukuruhusu kubainisha viendelezi ambavyo watumiaji HAWAWEZI kusakinisha. Tutazima viendelezi ambavyo tayari vimesakinishwa ikiwa havijaidhinishwa. Hatutampa mtumiaji uwezo wa kuviwasha. Tutawasha kiotomatiki kiendelezi ambacho kimeidhinishwa ikiwa kilikuwa kimezimwa awali kwa kukosa idhini.
Thamani ya kukosa idhini ya '*' inamaanisha kwamba viendelezi vyote havijaidhinishwa isipokuwa viwe vimebainishwa kwa njia dhahiri kwenye orodha ya viendelezi vilivyoidhinishwa.
Sera hii isipowekwa, mtumiaji bado anaweza kusakinisha kiendelezi chochote katika Google Chrome.
Inakuruhusu kubainisha ni viendelezi gani havihusuiani na orodha kuondoa idhini.
Thamani ya orodha ya kuondoa idhini ya * inamaanisha viendelezi vyote vimeondolewa idhini na watumiaji wanaweza tu kusakinisha viendelezi vilivyoorodheshwa katika orodha ya kutoa idhini.
Kwa chaguomsingi, viendelezi vyote vinatolewa idhini, lakini ikiwa viendelezi vyote vimeondolewa idhini kwa sera, orodha ya kutoa idhini inaweza kutumiwa kuifuta sera hiyo.
Hubainisha orodha ya programu na viendelezi vinavyosakinishwa chinichini, bila kumhusisha mtumiaji, na ambavyo haviwezi kuondolewa au kuzimwa na mtumiaji. Ruhusa zote zinazoombwa na programu au viendelezi zitatolewa kwa njia fiche, bila mtumiaji kuhusishwa ikijumuisha ruhusa zozote za ziada zinazoombwa na matoleo ya baadaye ya programu au kiendelezi. Zaidi ya hayo, ruhusa za API za viendelezi vya enterprise.deviceAttributes na enterprise.platformKeys zinatolewa (API hizi mbili zinapatikana kwenye programu au viendelezi ambavyo havisakinishwi kwa lazima.)
Sera hii inapewa kipaumbele ikiwa kuna sera inayoweza kukinzana ya ExtensionInstallBlacklist. Ikiwa programu au kiendelezi kilichosakinishwa hapo awali kwa lazima kitaondolewa kwenye orodha hii, kitaondolewa kiotomatiki na Google Chrome.
Katika matukio ya Windows ambayo hayajaunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®, usakinishaji wa lazima unatumiwa tu na programu na viendelezi vilivyoorodheshwa katika Duka la Chrome kwenye Wavuti. Kumbuka kuwa msimbo wa kiendelezi chochote unaweza kubadilishwa na mtumiaji kupitia Zana za Wasanidi Programu (hali hii inaweza kuzuia kiendelezi kufanya kazi vizuri). Ikiwa jambo hili litatokea, sera ya DeveloperToolsDisabled inapaswa kuwekwa.
Kila kipengee cha orodha ya sera ni kifungu ambacho kinajumuisha kitambulisho cha kiendelezi na URL ya "sasisho" isiyo ya lazima inayotenganishwa kwa nukta mkato (;). Kitambulisho cha kiendelezi ni kifungu cha herufi 32 kinachopatikana (kwa mfano) kwenye chrome://extensions ikiwa katika hali ya msanidi programu. URL ya "sasisho" , ikiwa imebainishwa, inapaswa kuashiria hati ya XML ya faili ya Maelezo ya Sasisho kama ilivyofafanuliwa katika https://developer.chrome.com/extensions/autoupdate. Kwa chaguomsingi, URL ya sasisho ya Duka la Chrome kwenye Wavuti inatumika (ambayo kwa sasa ni "https://clients2.google.com/service/update2/crx"). Kumbuka kuwa URL ya "sasisho" iliyowekwa kwenye sera hii itatumiwa tu kwenye usanikishaji wa mwanzo; masasisho yanayofuata ya kiendelezi yatatumia URL ya sasisho inayoonyeshwa katika faili ya maelezo ya kiendelezi. Kumbuka pia kuwa hali ya kubainisha URL ya "sasisho" kwa njia bayana ilikuwa lazima katika matoleo ya Google Chrome na mapya zaidi ikiwa ni pamoja na toleo la 67.
Kwa mfano, aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa;https://clients2.google.com/service/update2/crx inasakinisha programu ya aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa kutoka URL ya "sasisho" la kawaida la Duka la Chrome kwenye Wavuti. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kupangisha viendelezi, angalia: https://developer.chrome.com/extensions/hosting.
Ikiwa sera hii haijawekwa, hakuna programu au viendelezi vitakavyosakinishwa kiotomatiki na mtumiaji anaweza kuondoa programu au kiendelezi chochote katika Google Chrome.
Kumbuka kwamba sera hii haitumiki katika hali fiche.
Programu za Android zinaweza kusakinishwa kwa lazima kutoka kwenye Google Admin console kwa kutumia Google Play. Hazitumii sera hii.
Hukuruhusu kubainisha URL ambazo zinaruhusiwa ili kusakinisha viendelezi, programu na mandhari.
Kuanzia toleo la Google Chrome la 21, ni vigumu kusakinisha viendelezi, programu na hati za mtumiaji kutoka nje ya Duka la Chrome kwenye Wavuti. Hapo awali, watumiaji wangebofya kiungo cha kufikia faili ya *.crx na Google Chrome ingewapa fursa ya kusakinisha faili baada ya ilani chache. Baada ya toleo la Google Chrome la 21, faili kama hizi lazima zipakuliwe na kuburutwa kwenye ukurasa wa mipangilio ya Google Chrome. Sera hii huruhusu URL maalum kuwa na mtiririko wa awali na rahisi wa usakinishaji.
Kila kipengee kwenye orodha hii ni mchoro unaolingana na muundo wa kiendelezi (Angalia https://developer.chrome.com/extensions/match_patterns). Watumiaji wataweza kusakinisha kwa urahisi vipengee kutoka URL yoyote inayolingana na kipengee katika orodha hii. Ni lazima eneo la faili ya *.crx na ukurasa ambapo upakuaji ulianzia (kwa mfano, unaoelekeza) liruhusiwe na michoro hii.
ExtensionInstallBlacklist itatumika kwanza kabla ya sera hii. Hii inamaanisha kuwa, kiendelezi kwenye orodha ya zilizozuiwa hakitasakinishwa, hata kama hali hii ikitokea kwenye tovuti iliyo katika orodha hii.
Hudhibiti aina ya programu au viendelezi ambavyo vinaruhusiwa kusakinishwa na hupunguza ufikiaji wa programu inapotumika.
Mipangilio hii inaidhinisha aina ya viendelezi au programu zinazoruhusiwa ambazo zinaweza kusakinishwa katika Google Chrome na seva pangishi ambazo zinaweza kuwasiliana nazo. Thamani ni orodha ya mifuatano ambayo inapaswa kuwa mojawapo ya zifuatazo: "extension", "theme", "user_script", "hosted_app", "legacy_packaged_app", "platform_app". Angalia hati za viendelezi vya Google Chrome ili upate maelezo zaidi kuhusu aina hizi.
Kumbuka kwamba sera hii pia huathiri hali ya viendelezi na programu kusakinishwa kwa lazima kupitia ExtensionInstallForcelist.
Mipangilio hii ikiwekwa, viendelezi au programu ambazo zina aina ambayo haipo kwenye orodha hazitasakinishwa.
Mipangilio hii isipowekwa, hakuna vizuizi vinavyotumika kwenye aina za viendelezi au programu zinazoruhusiwa.
Hali ya kutumia vitambulisho vya viendelezi vilivyotenganishwa kwa koma katika matoleo ya kabla ya toleo la 75 haitumiki na itarukwa. Sehemu iliyosalia ya sera itaendelea kutumika.
Google Chrome huwezesha usakinishaji na usasishaji salama wa viendelezi. Hata hivyo, huenda maudhui ya baadhi ya viendelezi vinavyopangishwa nje ya Duka la Chrome kwenye Wavuti yakalindwa tu kwa kutumia njia isiyo salama ya kuambatisha vyeti au algoriti za kupunguza urefu kama vile SHA1. Sera hii inapozimwa, usakinishaji mpya na masasisho ya viendelezi kama hivyo havitaruhusiwa na Chrome (hadi wasanidi wa viendelezi waunde upya viendelezi vinavyotumia algoriti thabiti). Sera hii ikiwashwa, usakinishaji na masasisho ya viendelezi kama hivi utaruhusiwa.
Sera isipowekwa, hali hii itawashwa kwa chaguomsingi. Kwa kuanzia Google Chrome 75, sera isipowekwa, hali hii itazimwa kwa chaguomsingi.
Kwa kuanzia Google Chrome 77, sera hii haitatumiwa na itachukuliwa kuwa imezimwa.
Huweka mipangilio ya usimamizi wa viendelezi katika Google Chrome. Sera hii hudhibiti mipangilio mingi, ikiwa ni pamoja na mipangilio inayodhibitiwa na sera zozote zilizopo zinazohusiana na viendelezi. Sera hii itabatilisha sera zozote zilizopitwa na wakati ikiwa zote mbili zimewekwa.
Sera hii inaambatisha kitambulisho cha kiendelezi au URL ya sasisho kwenye mipangilio yake. Ikiwa na kitambulisho cha kiendelezi, mipangilio itawekwa kwenye kiendelezi kilichobainishwa pekee. Mipangilio chaguomsingi inaweza kuwekwa kwenye kitambulisho maalum cha "*", ambayo itatumika kwenye viendelezi vyote visivyo na mipangilio maalum katika sera hii. Ikiwa na URL ya sasisho, mipangilio itawekwa kwenye viendelezi vyote vyenye URL mahususi ya sasisho iliyobainishwa katika faili ya maelezo ya kiendelezi hiki, kama ilivyoelezwa katika https://developer.chrome.com/extensions/autoupdate. Kwa matukio ya Windows ambayo hayajaunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®, usakinishaji wa lazima unafanywa tu kwenye programu na viendelezi vilivyoorodheshwa katika Duka la Chrome kwenye Wavuti.
Ili upate maelezo kamili kuhusu mipangilio inayoweza kutumika na muundo wa sera hii, tafadhali tembelea https://www.chromium.org/administrators/policy-list-3/extension-settings-full
Huruhusu msimamizi kudhibiti ikiwa data ya uchunguzi na upimaji sharti ikusanywe, ichakatwe na kuripotiwa na kidhibiti upimaji na uchunguzi (DTC) cha WILCO.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo au ikiachwa bila kuwekwa, DTC itazimwa na haitaweza kukusanya, kuchakata wala kuripoti data ya uchunguzi na upimaji kutoka kifaa hiki. Ikiwa DTC ya WILCO inapatikana kwenye kifaa husika na sera imewekwa kuwa ndivyo, kipengele cha kukusanya, kuchakata na kuripoti data ya uchunguzi na upimaji kitawashwa.
Hutoa mipangilio ya wilco DTC (kidhibiti cha uchunguzi na upimaji).
Sera hii huruhusu kutoa mipangilio ya wilco DTC ambayo inaruhusiwa kutumiwa ikiwa wilco DTC inapatikana kwenye kifaa husika na inaruhusiwa na sera hii. Ukubwa wa mipangilio sharti usizidi MB 1 (baiti 1000000) na sharti usimbwe katika JSON. Wilco DTC inawajibu wa kuishughulikia. Alama ya reli ya kriptografia inatumika kuthibitisha kuaminika kwa kipakuliwa.
Mipangilio inapakuliwa na kuwekwa katika akiba. Itapakuliwa upya wakati URL au alama ya reli inabadilika.
Ukiweka sera hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuibatilisha.
Hukuruhusu kuweka iwapo tovuti zilizo na matumizi yanayopotosha zinapaswa kuzuiwa zisifungue madirisha au vichupo vipya.
Sera hii ikiwekwa kuwa Ndivyo, tovuti zilizo na matumizi yanayopotosha zitazuiwa zisifungue madirisha au vichupo vipya. Hata hivyo, hali hii haitatekelezwa iwapo sera ya SafeBrowsingEnabled imewekwa kuwa Sivyo. Sera hii ikiwekwa kuwa Sivyo, tovuti zilizo na matumizi mabaya zitaruhusiwa kufungua madirisha na vichupo vipya. Sera hii isipowekwa, mipangilio ya Ndivyo itatumika.
Inakuruhusu kubaini ikiwa matangazo yanapaswa kuzuiliwa kwenye tovuti zilizo na matangazo yanayokatiza matumizi. Ikiwa sera hii imewekwa kuwa 2, matangazo yatazuiliwa kwenye tovuti zilizo na matangazo yanayozuia matumizi. Hata hivyo, utendaji huu hautafanyika ikiwa sera ya SafeBrowsingEnabled imewekwa kuwa Sivyo. Ikiwa sera hii imewekwa kuwa 1, matangazo hayatazuiliwa kwenye tovuti zilizo na matangazo yanayokatiza matumizi. Ikiwa sera hii haijawekwa, thamani ya 2 itatumika.
Huwasha ufutaji wa historia ya kivinjari na historia ya upakuaji katika Google Chrome na huzuia watumiaji wasibadilishe mpangilio huu.
Kumbuka kuwa hata na sera hii kuzimwa, historia ya kuvinjari na upakuaji haina uhakika wa kubakishwa: watumiaji wanaweza kubadilisha au kufuta faili za hifadhidata ya historia moja kwa moja, na kivinjari chenyewe kinaweza kupitwa na wakati au kiweke vipengee vyote vya historia kwenye kumbukumbu wakati wowote.
Endapo mpangilio huu utawashwa au usiwekwe, historia ya kuvinjari na upakuaji inaweza kufutwa.
Mpangilio huu ukizimwa, historia ya kuvinjari na upakuaji hauwezi kufutwa.
Ruruhusu watumiaji wacheze mchezo fiche wa dinosau kifaa kinapokuwa nje ya mtandao.
Sera hii ikiwekwa kuwa Sivyo, watumiaji hawataweza kucheza mchezo mchezo fiche wa dinosau kifaa kinapokuwa nje ya mtandao. Mipangilio hii ikiwekwa kuwa Ndivyo, watumiaji wanaruhusiwa kucheza mchezo wa dinosau. Sera hii isipowekwa, watumiaji hawaruhusiwi kucheza mchezo fiche wa dinosau kwenye Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome uliosajiliwa, lakini wanaruhusiwa kuucheza chini ya hali nyingine.
Huruhusu faili zilizo kwenye mashine kufikiwa kwa kuruhusu Google Chrome kuonyesha vidadisi vya uteuzi vya faili.
Ukiwasha mpangilio huu, watumiaji wanaweza kufungua vidadisi vya uteuzi vya faili kama kawaida.
Ukizima mpangilio huu, wakati wowote mtumiaji anapotekeleza kitendo ambacho kinaweza kufanya kidadisi cha uteuzi faili kionyeshwe (kama kuingiza alamisho, kupakia faili, kuhifadhi viungo, n.k.) ujumbe unaonyeshwa badala yake na mtumiaji anachukuliwa kwamba amebofya Ghairi kwenye kidadisi cha uteuzi wa faili.
Ikiwa mpangilio huu haujawekwa, watumiaji wanaweza kufungua kidadisi cha uteuzi faili kama kawaida.
Ukiwasha mipangilio hii, programu jalizi ambazo muda wake umeisha zinatumika kuwa programu jalizi za kawaida.
Ukizima mipangilio hii, programu jalizi ambazo muda wake umeisha hazitatumika na watumiaji hawataombwa ruhusa ya kuzitekeleza.
Ikiwa mipangilio hii haijawekwa, watumiaji wataombwa ruhusa za kutumia programu jalizi ambazo muda wake umeisha.
Sera hii huruhusu msimamizi kubainisha kuwa ukurasa unaweza kuonyesha madirisha ibukizi wakati wa kuondoa.
Sera hii ikiwashwa, kurasa zinaruhusiwa kuonyesha madirisha ibukizi wakati zinaondolewa.
Sera ikizimwa au isipowekwa, kurasa haziruhusiwi kuonyesha madirisha ibukizi wakati zinaondolewa kulingana na maelezo ya msingi (https://html.spec.whatwg.org/#apis-for-creating-and-navigating-browsing-contexts-by-name).
Sera hii itaondolewa katika Chrome 82.
Angalia https://www.chromestatus.com/feature/5989473649164288 .
Ikiwa sera hii imewekwa kuwa ndivyo, watumiaji hawataweza kufunga skrini (utaweza kuondoka katika kipindi cha mtumiaji pekee). Mipangilio hii ikiwekwa kuwa ndivyo au isipowekwa, watumiaji ambao walithibitisha kupitia nenosiri wanaweza kufunga skrini.
Huruhusu kipengele cha kuingia katika akaunti cha Google Chrome kinachodhibitiwa katika G Suite na kuzuia watumiaji wasibadilishe mipangilio hii.
Iwapo utabainisha mipangilio hii, watumiaji wataweza tu kufikia Programu za Google kupitia akaunti kutoka vikoa vilivyobainishwa (kumbuka kuwa ili kuruhusu akaunti za gmail.com/googlemail.com, unapaswa kuongeza "akaunti za watumiaji" (bila manukuu) kwenye orodha ya vikoa).
Mipangilio hii itamzuia mtumiaji asiingie katika akaunti, na asiongeze Akaunti Mbadala kwenye kifaa kinachodhibitiwa ambacho kinahitaji uthibitishaji wa Google, iwapo akaunti hiyo haijajumuishwa katika orodha iliyotajwa awali ya vikoa vinavyoruhusiwa.
Iwapo hutajaza mipangilio hii au hutaiweka, mtumiaji ataweza kufikia G Suite kwa kutumia akaunti yoyote.
Sera hii husababisha kichwa cha X-GoogApps-Allowed-Domains kiwekwe kwenye maombi yote ya HTTP na HTTPS katika vikoa vyote vya google.com, jinsi inavyobainishwa katika https://support.google.com/a/answer/1668854.
Watumiaji hawawezi kubadilisha wala kubatilisha mipangilio hii.
Huweka mipangilio ya miundo wa kibodi ambayo inaruhusiwa katika vipindi vya watumiaji wa Google Chrome OS.
Ikiwa sera hii imewekwa, mtumiaji anaweza tu kuchagua moja ya njia za kuweka data zilizobainishwa na sera hii. Ikiwa sera hii haijawekwa au imewekwa kwenye orodha isiyo na kitu, mtumiaji anaweza kuchagua njia zote zinazotumika za kuweka data. Iwapo njia ya sasa ya kuweka data hairuhusiwi na sera hii, njia hii ya kuweka data itabadilishwa ili kutumia muundo wa kibodi ya maunzi (ikiruhusiwa) au njia ya kwanza ya kuweka data inayoruhusiwa katika orodha hii. Haitazingatia njia zote za kuweka data ambazo hazitumiki au si sahihi, zilizo katika orodha hii.
Huweka mipangilio ya lugha zinazoweza kutumiwa kama lugha zinazopendelewa na Google Chrome OS.
Sera hii ikiwekwa, mtumiaji anaweza kuongeza lugha moja pekee kutoka lugha zilizoorodheshwa katika sera hii kwenye orodha ya lugha zinazopendelewa. Sera hii isipowekwa au ikiwekwa kuwa orodha isiyo na kitu, mtumiaji anaweza kubainisha lugha yoyote anayopendelea. Ikiwa sera hii imewekwa kuwa orodha ya thamani zisizo sahihi, thamani zote zisizo sahihi hazitatumiwa. Kama mtumiaji aliweka lugha kadhaa hapo awali ambazo haziruhusiwi na sera hii kwenye orodha ya lugha zinazopendelewa, lugha hizo zitaondolewa. Ikiwa mtumiaji alikuwa ameweka mipangilio ya Google Chrome OS hapo awali ili ionekane katika mojawapo ya lugha ambazo haziruhusiwi na sera hii, lugha ya kuonyesha itabadilishwa iwe lugha inayoruhusiwa ya kiolesura wakati mtumiaji ataingia tena katika akaunti. Vinginevyo, Google Chrome OS itatumia thamani sahihi ya kwanza inayobainishwa na sera hii, au lugha chaguomsingi (kwa sasa ni kiingereza cha Marekani), ikiwa sera hii inajumuisha tu thamani zisizo sahihi.
Inawezesha matumizi ya kurasa mbadala za hitilafu zilizojengwa katika Google Chrome (kama vile 'ukurasa haukupatikana') na huzuia watumiaji kuubadilisha mpangilio huu.
Ukiwezesha mpangilio huu, kurasa mbadala za hitilafu zinatumiwa.
Ukilemaza mpangilio huu, kurasa mbadala za hitilafu hazitumiwi kamwe.
Ukiwezesha au kuulemaza mpangilio huu, watumiaji hawawezi kuubadilisha au kuufuta mpangilio huu katika Google Chrome.
Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa, hii itawezeshwa lakini mtumiaji ataweza kuibadilisha.
Huzima programu ya ndani ya kusoma PDF katika Google Chrome. Badala yake huichukulia kama kupakuliwa na huruhusu mtumiaji kufungua faili za PDF kwa kutumia programu chaguomsingi.
Sera hii ikiachwa bila kuwekwa au ikizimwa, programu jalizi ya PDF itatumiwa kufungua faili za PDF isipokuwa mtumiaji awe ameizima.
Inasanidi lugha ya programu katika Google Chrome na huzuia watumiaji kubadilisha lugha.
Ukiwezesha mpangilio huu, Google Chrome hutumia lugha iliyobainishwa. Ikiwa lugha iliyosanidiwa haijahimiliwa, 'en-US' inatumiwa badala yake.
Ikiwa mpangilio huu utalemazwa au haujawekwa, Google Chrome hutumia lugha inayopendelewa iliyobainishwa na mtumiaji (ikiwa imesanidiwa), lugha ya mfumo au lugha mbadala 'en-US'.
Sera ikiwashwa au mipangilio isipowekwa (kwa chaguomsingi), mtumiaji atatumiwa kidokezo cha idhini ya kufikia kipengee cha kurekodi sauti isipokuwa kwa URL zilizowekwa mipangilio katika orodha ya AudioCaptureAllowedUrls ambazo zitapewa idhini ya kufikia bila kudokezewa.
Sera hii ikizimwa, mtumiaji hatawahi kudokezewa na kurekodi sauti kutapatikana tu kwa URL zilizowekewa mipangilio katika AudioCaptureAllowedUrls.
Sera hii inaathiri vifaa vyote vya kuingiza sauti wala si maikrofoni iliyojengewa ndani pekee.
Kwa programu za Android, sera hii inaathiri maikrofoni pekee. Sera ikiwekwa kuwa ndivyo, maikrofoni huzimwa sauti kwa programu zote za Android, bila vighairi.
Ruwaza katika orodha hii zitalinganishwa dhidi ya asili ya usalama wa ombi la URL. Zikilingana, idhini ya kufikia vifaa vya kunasa sauti itatolewa bila ombi.
KUMBUKA: Kabla ya toleo la 45, sera hii ilitumika katika Skrini nzima pekee.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, vifaa vya kutoa sauti havitapatikana kwenye kifaa wakati mtumiaji ameingia katika akaunti.
Sera hii inaathiri aina zote za vifaa vya sauti na si tu spika zilizojumuishwa ndani ya kifaa. Vipengele vya sauti vya walio na matatizo ya kuona au kusikia pia vinazuiwa na sera hii. Usiwashe sera hii ikiwa mtumiaji anahitaji kisoma skrini.
Mipangilio hii ikiwekwa kuwa ndivyo au mipangilio isiwekwe, basi watumiaji wanaweza kutumia vifaa vyote vya sauti vinavyotumiwa kwenye kifaa chao.
Sera hii iliacha kuendesha huduma katika M70, badala yake, tafadhali tumia AutofillAddressEnabled na AutofillCreditCardEnabled.
Sera hii huwasha kipengele cha Google Chrome cha Kujaza Kiotomatiki na huruhusu watumiaji kujaza fomu za tovuti kwa kutumia maelezo yaliyohifadhiwa hapo awali kama vile anwani au maelezo ya kadi ya mikopo.
Ukizima mipangilio hii, watumiaji hawataweza kufikia kipengele cha Kujaza Kiotomatiki.
Ukiwasha mipangilo hii au usiweke thamani yoyote, kipengele cha Kujaza Kiotomatiki kitasalia chini ya udhibiti wa mtumiaji. Hali hii itaruhusu watumiaji kupanga wasifu wa kipengele cha Kujaza Kiotomatiki na kuwasha au kuzima kipengele cha Kujaza Kiotomatiki wakati wowote.
Huwasha kipengele cha Kujaza Kiotomatiki cha Google Chrome na kuruhusu watumiaji wajaze kiotomatiki maelezo ya anwani katika fomu za wavuti wakitumia maelezo waliyohifadhi awali.
Iwapo mipangilio hii imezimwa, kipengele cha Kujaza Kiotomatiki hakitawahi kupendekeza wala kujaza maelezo ya anwani. Pia hakitahifadhi maelezo ya ziada ya anwani ambayo huenda mtumiaji atawasilisha anapovinjari wavuti.
Iwapo mipangilio hii imewashwa au haina thamani yoyote, mtumiaji ataweza kudhibiti kipengele cha Kujaza Kiotomatiki kwa anwani kwenye kiolesura.
Huwasha kipengele cha Kujaza Kiotomatiki cha Google Chrome na kuruhusu watumiaji wajaze kiotomatiki maelezo ya kadi ya mikopo katika fomu za wavuti wakitumia maelezo waliyohifadhi awali.
Iwapo mipangilio hii imezimwa, kipengele cha Kujaza Kiotomatiki hakitawahi kupendekeza wala kujaza maelezo ya kadi ya mikopo. Pia hakitaweza kuhifadhi maelezo ya ziada ya kadi ya mikopo ambayo huenda mtumiaji atawasilisha atakapovinjari kwenye wavuti.
Iwapo mipangilio hii imewashwa au haina thamani yoyote, mtumiaji ataweza kudhibiti kipengele cha Kujaza Kiotomatiki katika kadi za mikopo kwenye kiolesura.
Hukuruhusu udhibiti ikiwa video zinaweza kucheza kiotomatiki (bila idhini ya mtumiaji) katika maudhui ya sauti kwenye Google Chrome.
Kama sera imewekwa kuwa Ndivyo, Google Chrome inaruhusiwa kucheza maudhui kiotomatiki. Kama sera imewekwa kuwa Sivyo, Google Chrome hairuhusiwi kucheza maudhui kiotomatiki. Sera ya Orodha Zilizoidhinishwa Kucheza Kiotomatiki inaweza kutumiwa kufuta hali hii katika ruwaza fulani za URL. Kwa chaguomsingi, Google Chrome hairuhusiwi kucheza maudhui kiotomatiki. Sera ya Orodha Zilizoidhinishwa Kucheza Kiotomatiki inaweza kutumiwa kufuta hali hii katika ruwaza fulani za URL.
Kumbuka kwamba kama Google Chrome inatumika na sera hii ibadilike, itatumika tu kwenye vichupo vinavyofunguliwa baada ya hatua hii. Kwa hivyo baadhi ya vichupo huenda vitatumia sera ya awali.
Hudhibiti ruwaza za URL zilizoidhinishwa ambako kipengele cha kucheza kiotomatiki kitawaka kila wakati.
Kama kipengele cha kucheza kiotomatiki kimewashwa basi video zinaweza kucheza kiotomatiki (bila idhini ya mtumiaji) katika maudhui ya sauti kwenye Google Chrome.
Ruwaza sahihi za URL zilizobainishwa ni:
- [*.]domain.tld (inalingana na domain.tld na vikoa vyote vidogo)
- seva pangishi (inalingana na jina sahihi la mpangishaji)
- scheme://host:port (miundo inayotumika: http,https)
- scheme://[*.]domain.tld:port (miundo inayotumika: http,https)
- file://path (Sharti iwe njia kamili na ianze kwa '/')
- a.b.c.d (inalingana na IPv4 ip sawa)
- [a:b:c:d:e:f:g:h] (inalingana na IPv6 ip sawa)
Sera ya Kucheza Kiotomatiki ikiwekwa kuwa Ndivyo basi sera hii haina athari.
Sera ya kucheza Kiotomatiki ikiwekwa kuwa Sivyo basi ruwaza yoyote ya URL iliyowekwa katika sera hii bado itaruhusiwa kucheza.
Kumbuka kuwa kama Google Chrome inafanya kazi na sera hii ibadilike, sera itatumika tu kwenye vichupo viwili vinavyofunguliwa baada ya hatua hii. Kwa hivyo huenda baadhi ya vichupo vitatumia sera ya awali.
Huamua ikiwa machakato wa Google Chrome utaanza wakati wa kuingia katika Mfumo wa Uendeshaji na kuendelea kutekeleza dirisha la mwisho la kivinjari linapofungwa, hivyo kuruhusu programu za chini chini na kipindi cha kuvinjari cha sasa kuendelea, ikiwa ni pamoja na vidakuzi vya kipindi. Mchakato wa chini chini huonyesha aikoni katika treya ya mfumo na unaweza kufungwa kutoka huko wakati wowote.
Sera hii ikiwekwa kuwa Ndivyo, kipengee cha hali ya chinichini huwashwa na hakiwezi kudhibitiwa na mtumiaji katika mipangilio ya kivinjari.
Sera hii ikiwekwa kuwa Sivyo, kipengee cha hali ya chinichini huzimwa na hakiwezi kudhibitiwa na mtumiaji katika mipangilio ya kivinjari.
Sera hii ikiachwa bila kuwekwa, kipengee cha hali ya chinichini huzimwa kwanza na kinaweza kudhibitiwa na mtumiaji katika mipangilio ya kivinjari.
Kuwasha mipangilio hii kunazuia vidakuzi kuwekwa na vipengee vya ukurasa wa wavuti ambavyo havitoki kwenye kikoa kilicho katika sehemu ya anwani ya kivinjari.
Kuzima mipangilio hii kunaruhusu vidakuzi kuwekwa na vipengee vya ukurasa wa wavuti ambavyo havitoki kwenye kikoa kilicho katika sehemu ya anwani ya kivinjari na huzuia watumiaji kubadilisha mipangilio hii.
Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa, vidakuzi vingine vitawashwa lakini mtumiaji ataweza kubadilisha hali hiyo.
Ukiwasha mipangilio hii, Google Chrome itaonyesha sehemu ya alamisho.
Ukizima mipangilio hii, watumiaji hawatawahi kuona sehemu ya alamisho.
Ukiwasha au kuzima mipangilio hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuibatilisha katika Google Chrome.
Mipangilio hii isipowekwa, mtumiaji anaweza kuamua kutumia au kutotumia kipengele hiki.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo au isipowekwa mipangilio, Google Chrome itaruhusu kipengee cha Ongeza Wasifu kutoka kwenye kidhibiti cha mtumiaji.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, Google Chrome haitaruhusu kuunda wasifu mpya kutoka kwenye kidhibiti cha mtumiaji.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo au isisanidiwe, Google Chrome itawasha kipengee cha wageni kuingia katika akaunti. Kuingia katika akaunti kwa wageni ni wasifu wa Google Chrome ambapo madirisha yote yako katika hali fiche.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, Google Chrome haitaruhusu wasifu wa wageni kuanzishwa.
Kuiweka sera hii kuwa sivyo kutasimamisha Google Chrome kutuma hoja mara kwa mara kwenye seva ya Google ili kurejesha muhuri sahihi wa muda. Hoja hizi zitawashwa iwapo sera hii itawekwa kuwa ndivyo au haitawekwa.
Sera hii hudhibiti hali ya kuingia katika akaunti ya kivinjari. Inakusaidia kubainisha kama mtumiaji anaweza kuingia katika akaunti ya Google Chrome kwa kutumia akaunti yake na atumie huduma zinazohusiana kama Usawazishaji wa Chrome.
Ikiwa sera imewekwa kuwa "Zima kuingia katika akaunti ya kivinjari" basi mtumiaji hawezi kuingia katika akaunti ya kivinjari na atumie huduma zinazotegemea akaunti. Katika hali hii vipengele vya kiwango cha kivinjari kama vile Usawazishaji wa Chrome havitatumika na havitapatikana. Kama mtumiaji alikuwa ameingia katika akaunti na sera imewekwa kuwa "Imezimwa" ataondolewa kwenye akaunti wakati unaofuata atakapotekeleza Chrome lakini data yake ya wasifu kwenye kifaa kama vile alamisho, nenosiri n.k. itawekwa salama. Mtumiaji bado ataweza kuingia katika akaunti na atumie huduma za wavuti za Google kama Gmail.
Ikiwa sera imewekwa kuwa "Ruhusu kuingia katika akaunti ya kivinjari," basi mtumiaji anakubaliwa kuingia katika akaunti ya kivinjari na anaingia katika akaunti ya kivinjari kiotomatiki anapoingia katika akaunti ya huduma za wavuti za Google kama Gmail. Kuingia katika akaunti ya kivinjari kuna maana kuwa maelezo ya akaunti ya mtumiaji yatahifadhiwa na kivinjari. Hata hivyo, haina maana kuwa Usawazishaji wa Chrome utawashwa kwa chaguomsingi; lazima mtumiaji achague kuingia ili aweze kutumia kipengele hiki. Kuweka sera hii kutamzuia mtumiaji kuzima mipangilio inayoruhusu kuingia katika akaunti ya kivinjari. Ili kudhibiti upatikanaji wa usawazishaji wa Chrome, tumia sera ya "SyncDisabled".
Ikiwa sera imewekwa kuwa "Lazimisha kuingia katika akaunti ya kivinjari" kidirisha cha kuchagua akaunti huwasilishwa kwa mtumiaji na anapaswa kuchagua na aingie katika akaunti ili kutumia kivinjari. Hii inahakikisha kwamba sera zinazohusishwa na akaunti zinazosimamiwa zimetumika na kutekelezwa. Kwa chaguomsingi hii huwasha kipengele cha Usawazishaji wa Chrome kwenye akaunti, isipokuwa ambapo usawazishaji ulizimwa na msimamizi wa kikoa au kupitia sera ya "SyncDisabled". Thamani chaguomsingi ya BrowserGuestModeEnabled itawekwa kuwa sivyo. Kumbuka kwamba wasifu uliopo ambao haujatumiwa kuingia katika akaunti utafungwa na hautaweza kufikiwa baada ya kuwasha sera hii. Kwa maelezo zaidi, angalia makala ya kituo cha usaidizi: https://support.google.com/chrome/a/answer/7572556.
Ikiwa sera hii haijawekwa basi mtumiaji anaweza kuamua kama anataka kuwasha chaguo la kuingia katika akaunti ya kivinjari na kuitumia anavyopenda.
Hudhibiti iwapo kiteja cha DNS kilichojumuishwa kinatumika katika Google Chrome.
Iwapo sera hii imewekwa kuwa ndivyo, kiteja cha DNS kilichojumuishwa kitatumiwa, iwapo kinapatikana.
Iwapo sera hii imewekwa kuwa sivyo, kiteja cha DNS kilichojumuishwa hakitawahi kutumiwa.
Iwapo sera hii itaachwa bila kuwekwa, kiteja cha DNS kilichojumuishwa kitawashwa kwa chaguomsingi kwenye MacOS, Android (wakati DNS ya Faragha au VPN zimewashwa) na ChromeOS na watumiaji wataweza kubadilisha iwapo kiteja cha DNS kilichojumuishwa kitatumika kwa kuhariri chrome://flags au kubainisha alama ya mstari wa amri.
Sera hii huruhusu Google Chrome OS kutotumia seva yoyote mbadala kwa ajili ya uthibitishaji wa ukurasa wa mwanzo.
Athari za sera hii hutumika tu ikiwa seva mbadala imewekewa mipangilio (kwa mfano, kupitia sera, na mtumiaji katika chrome://settings, au kupitia viendelezi).
Ukiwasha mipangilio hii, uthibitishaji wowote wa kurasa za mwanzo (kwa mfano, kurasa zote za wavuti zinazoanzia ukurasa wa kuingia katika akaunti ya ukurasa wa mwanzo hadi Google Chrome zinatambua muunganisho wa intaneti) zitaonyeshwa kwenye dirisha tofauti zikipuuza mipangilio yote ya sera na vizuizi vya mtumiaji wa sasa.
Ukizima mipangilio hii au usipoiweka, kurasa zozote za uthibitishaji wa ukurasa wa mwanzo zitaonyeshwa katika kichupo cha kivinjari kipya (kawaida), kwa kutumia mipangilio ya seva mbadala ya mtumiaji wa sasa.
Sera hii inabaini iwapo mtumiaji ataweza kupakia au kuondoa vyeti kupitia Kidhibiti cha Vyeti.
Sera hii ikiwekwa kuwa ''Ruhusu watumiaji kudhibiti vyeti vyote'' au isipowekwa, watumiaji wanaweza kudhibiti vyeti.
Sera hii ikiwekwa kuwa ''Ruhusu watumiaji kudhibiti vyeti'', watumiaji wataweza kudhibiti vyeti vya watumiaji lakini si vyeti vinavyotumika kwenye vifaa.
Sera hii ikiwekwa kuwa ''Usiruhusu watumiaji kudhibiti vyeti'', watumiaji hawataweza kudhibiti vyeti, wataweza tu kuviangalia.
Huzima masharti ya kutumia Uwazi wa Vyeti katika orodha hashi za subjectPublicKeyInfo.
Sera hii huruhusu uzimaji wa masharti ya kufichua Uwazi wa Vyeti katika mfululizo wa vyeti vilivyo na vyeti vyenye hashi za subjectPublicKeyInfo. Hali hii inaruhusu vyeti ambavyo havingeaminika, kwa sababu havikufichuliwa kwa umma ipasavyo, viendelee kutumika kwenye Seva pangishi za Kampuni.
Ili kuzima kipengele cha utekelezaji wa Uwazi wa Vyeti wakati sera hii imewekwa, ni lazima mojawapo ya hali hizi zitimizwe: 1. Hashi iwe cheti cha seva cha subjectPublicKeyInfo. 2. Hashi iwe subjectPublicKeyInfo inayoonekana kwenye cheti cha CA katika mfululizo wa vyeti. Cheti hicho cha CA kinabanwa kupitia kiendelezi cha 0000X.509v3 nameConstraints, directoryName nameConstraints moja au zaidi pia zipo katika permittedSubtrees na directoryName ina sifa ya organizationName. 3. Hashi iwe subjectPublicKeyInfo inayoonekana kwenye cheti cha CA katika mfululizo wa vyeti, cheti cha CA kina sifa moja au zaidi ya organizationName kwenye mada ya cheti na cheti cha seva kina idadi sawa ya sifa za organizationName, katika mpangilio sawa na wenye thamani zinazofanana kwenye kila baiti.
Hashi ya subjectPublicKeyInfo inabainishwa kwa kuunganisha jina la algoriti ya hashi, herufi "/" na usimbaji wa Base64 wa algoriti ya hashi iliyotumika kwenye subjectPublicKeyInfo yenye usimbaji wa DER wa cheti kilichobainishwa. Usimbaji huu wa Base64 una muundo sawa na alama bainifu ya SPKI, kama ilivyoelezwa katika RFC 7469, Sehemu ya 2.4. Algoriti za hashi zisizotambulika hupuuzwa. Algoriti ya hashi inayotumika kwa sasa ni "sha256" pekee.
Sera hii isipowekwa, cheti chochote kinachohitaji kufichuliwa kupitia Uwazi wa Cheti kitashughulikiwa kama cheti kisichoaminika kisipofichuliwa kulinganana na sera ya Uwazi wa Cheti.
Huzima masharti yanayotekeleza Uwazi wa cheti katika orodha ya Mamlaka ya Vyeti vilivyopitwa na wakati.
Sera hii huruhusu uzimaji wa masharti ya ufumbuzi wa Uwazi wa Cheti kwa ajili ya misururu ya vyeti vilivyo na vyeti vilivyo na mojawapo ya alama reli iliyobainishwa ya subjectPublicKeyInfo. Hii huruhusu vyeti ambavyo huenda havingeaminika, kwa sababu havikufichuliwa kwa umma ipasavyo, ili viendelee kutumika kwenye seva pangishi za Kampuni.
Ili kuzima kipengele cha kutekeleza Uwazi wa Cheti wakati sera hii imewekwa, ni lazima hashi iwe ya subjectPublicKeyInfo inayoonekana kwenye cheti cha CA kinachotambulika kama Mamlaka ya Cheti Kilichopitwa na wakati (CA). CA iliyopitwa na wakati ni CA ambayo imeaminiwa hadharani kwa chaguomsingi na mfumo moja au zaidi ya uendeshaji unaotumika katika Google Chrome, lakini haiaminiki na Mradi wa Programu huria za Android au Google Chrome OS.
Hashi ya subjectPublicKeyInfo inabainishwa kwa kuunganisha jina la algoriti ya hashi, herufi "/" na programu ya kusimba ya Base64 ya algoriti ya hashi hiyo inayotumika kwenye subjectPublicKeyInfo yenye usimbaji wa DER wa cheti kilichobainishwa. Usimbaji huu wa Base64 una muundo sawa na Alama bainifu ya SPKI, kama ilivyoelezwa kwenye RFC 7469, Sehemu ya 2.4. Algoriti za hashi zisizotambulika zitapuuzwa. Algoriti ya hashi ya kipekee inayotumika kwa wakati huu ni "sha256".
Ikiwa sera hii haijawekwa, cheti chochote kinachotakiwa kufichuliwa kupitia Uwazi wa Cheti kitashughulikiwa kuwa kisichoaminika ikiwa hakitafichuliwa kulingana na sera ya Uwazi wa Cheti.
Huzima utekelezaji wa mahitaji ya Uwazi wa Cheti kwenye URL zilizoorodheshwa.
Sera hii huruhusu vyeti vya majina ya wapangishaji katika URL zilizobainishwa visifichuliwe kupitia Uwazi wa Cheti. Hii huruhusu vyeti visivyoaminika, kwa sababu havikufichuliwa hadharani ipasavyo, viendelee kutumiwa, lakini hufanya ugunduzi wa vyeti vilivyotumiwa vibaya kuwa mgumu kwa wapangishaji hao.
Ruwaza ya URL huundwa kulingana na https://www.chromium.org/administrators/url-blacklist-filter-format. Hata hivyo, kwa sababu vyeti ni sahihi kwa jina maalum la mpangishaji ambayo haitegemei utaratibu, mlango, au njia, ni sehemu ya jina la mpangishaji wa URL ambayo hutumika pekee. Wapangishaji wa herufi wakilishi hawatumiki.
Sera hii isipowekwa, cheti chochote kinachopaswa kuonyeshwa kupitia Uwazi wa Cheti kitachukuliwa kuwa kisichoaminika kama hakitaonyeshwa kulingana na sera ya Uwazi wa Cheti.
Ikiwa sera imezimwa, itazuia Kipengele cha Kusafisha Chrome kisikague mfumo ili kubaini programu zisizotakikana na kuziondoa. Uwezo wa kuanzisha Kipengele cha Kusafisha Chrome kutoka chrome://settings/cleanup umezimwa.
Ikiwa sera imewashwa au haijawekwa, Kipengele cha Kusafisha Chrome hukagua mfumo mara kwa mara ili kubaini programu zisizotakikana na kuziondoa. Ikiwa programu yoyote itapatikana, tutamwuliza mtumiaji ikiwa angependa kuiondoa. Uwezo wa kuanzisha Kipengele cha Kusafisha Chrome kutoka chrome://settings umewashwa.
Sera hii inapatikana kwenye matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®. au matukio ya Windows 10 Pro au Enterprise yaliyojumuishwa katika usimamizi wa kifaa.
Iwapo sera haijawekwa na Kipengele cha Kusafisha Chrome kitambue programu isiyotakikana, kinaweza kuripoti metadata kuhusu ukaguzi kwa Google kulingana na sera zilizowekwa na SafeBrowsingExtendedReportingEnabled. Kisha, Kipengele cha Kusafisha Chrome kitamwuliza mtumiaji iwapo angependa kuondoa programu isiyotakikana. Mtumiaji anaweza kuchagua kushiriki matokeo ya uondoaji na Google ili kusaidia utambuzi wa programu zisizotakikana baadaye. Matokeo haya yana metadata ya faili, viendelezi vilivyosakinishwa kiotomatiki na funguo za sajili kama ilivyobainishwa na Hati ya Faragha ya Chrome.
Iwapo sera imezimwa na Kipengele cha Kusafisha Chrome kitambue programu isiyotakikana, hakitaripoti metadata kuhusu ukaguzi kwa Google, hali itakayobatilisha sera zozote zilizowekwa na SafeBrowsingExtendedReportingEnabled. Kipengele cha Kusafisha Chrome kitamwuliza mtumiaji iwapo angependa kuondoa programu isiyotakikana. Matokeo ya uondoaji hayataripotiwa kwa Google na mtumiaji hatakuwa na chaguo la kufanya hivyo.
Iwapo sera imewashwa na Kipengele cha Kusafisha Chrome kitambue programu isiyotakikana, kinaweza kuripoti metadata kuhusu ukaguzi kwa Google kulingana na sera zilizowekwa na SafeBrowsingExtendedReportingEnabled. Kipengele cha Kusafisha Chrome kitamwuliza mtumiaji iwapo angependa kuondoa programu isiyotakikana. Matokeo ya uondoaji yataripotiwa kwa Google na mtumiaji hatakuwa na chaguo la kuzuia hali hii.
Sera hii inapatikana kwenye matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®. au matukio ya Windows 10 Pro au Enterprise yaliyojumuishwa katika usimamizi wa kifaa.
Washa kipengele cha kufunga wakati vifaa vya Google Chrome OS havifanyi kitu au vikisimamishwa.
Ukiwasha mipangilio hii, watumiaji wataombwa nenosiri ili kufungua kifaa ambacho hakitumiki.
Ukizima mipangilio hii, watumiaji hawataombwa nenosiri ili kufungua kifaa ambacho hakitumiki.
Ukiwasha au kuzima mipangilio hii, watumiaji hawawezi kukibadilisha au kukifuta.
Ikiwa sera hii haitawekwa, mtumiaji anaweza kuchagua kama angependa kuombwa nenosiri ili afungue kifaa au la.
Dhibiti tabia ya mtumiaji katika kipindi cha multiprofile kwenye vifaa vya Google Chrome OS.
Ikiwa sera hii itawekwa kuwa 'MultiProfileUserBehaviorUnrestricted', mtumiaji anaweza kuwa wa kwanza au wa pili katika kipindi cha multiprofile.
Ikiwa sera hii itawekwa kuwa 'MultiProfileUserBehaviorMustBePrimary', mtumiaji anaweza kuwa wa kwanza pekee katika kipindi cha multiprofile.
Ikiwa sera hii itawekwa kuwa 'MultiProfileUserBehaviorNotAllowed', mtumiaji hawezi kushiriki kipindi cha multiprofile.
Ukiweka mpangilio huu, watumiaji hawawezi kuubadilisha au kuufuta.
Ikiwa mpangilio utabadilishwa mtumiaji akiwa ameingia katika kipindi cha multiprofile, watumiaji wote katika kipindi watateuliwa dhidi ya mipangilio yao sambamba. Kipindi kitafungwa ikiwa yeyote kati ya watumiaji haruhusiwi kuwa katika kipindi.
Ikiwa sera itaachwa bila kuwekwa, thamani ya chaguomsingi 'MultiProfileUserBehaviorMustBePrimary' inatumika kwa watumiaji wanaosimamiwa kibiashara na 'MultiProfileUserBehaviorUnrestricted' itatumiwa kwa watumiaji wasiosimamiwa.
Watumiaji wengi wanapoingia katika akaunti, ni mtumiaji wa kwanza pekee anayeweza kutumia programu za Android.
Ikiwa sera hii imewekwa kuwa Ndivyo, ujumuishaji katika udhibiti wa wingu ni wa lazima na huzuia mchakato wa kufungua Chrome ikiwa itashindwa kufunguka.
Ikiwa sera hii haijawekwa au imewekwa kuwa Sivyo, ujumuishaji katika udhibiti wa wingu si wa lazima na hauzuii mchakato wa kufungua Chrome ikiwa itashindwa kufunguka.
Sera hii inatumiwa na mpango wa ujumuishaji wa sera ya wingu katika upeo wa mashine kwenye kompyuta ya mezani na inaweza kuwekwa na Sajili au GPO kwenye Windows, faili ya plist kwenye Mac na faili ya sera ya JSON kwenye Linux.
Kama sera hii imewekwa, Google Chrome itajaribu kujisajili na kutumia sera husika ya wingu katika wasifu zote.
Thamani ya sera hii ni tokeni ya Uandikishaji ambayo inaweza kutolewa kwenye dashibodi ya Msimamizi wa Google.
Ikiwa sera imewekwa kuwa ndivyo, sera ya wingu inapewa kipaumbele iwapo inakinzana na sera ya mfumo. Ikiwa sera imewekwa kuwa sivyo au isipowekwa, sera ya mfumo inapewa kipaumbele ikiwa inakinzana na sera ya wingu.
Sera hii inapatikana tu kama sera ya lazima ya mfumo wa mashine na huathiri tu sera za wingu zinazohusu mashine.
Ikiwa haijawekwa au imewekwa kuwa Ndivyo, masasisho ya vipengele vyote katika Google Chrome huwashwa.
Ikiwekwa kuwa Sivyo, masasisho ya vipengele yatazimwa. Hata hivyo, baadhi ya vipengele havizingatii sera hii: haitazima masasisho ya kipengele chochote ambacho hakina msimbo wa kutekelezwa, au ambacho hakibadilishi zaidi jinsi kivinjari kinavyofanya kazi, au ni muhimu kwa usalama wake. Mifano ya vipengele kama hivyo ni orodha za vyeti vilivyobatilishwa na data ya Kuvinjari Salama. Angalia https://developers.google.com/safe-browsing ili upate maelezo zaidi kuhusu Kuvinjari Salama.
Huwasha kipengele cha Gusa ili Utafute katika mwonekano wa maudhui ya Google Chrome.
Ukiwasha mipangilio hii, kipengele cha Gusa ili Utafute kitapatikana kwa mtumiaji na anaweza kuamua kukiwasha au kukizima.
Ukizima mipangilio hii, kipengele cha Gusa ili Utafute kitazimwa kabisa.
Sera hii ikiachwa bila kuwekwa, ni sawa na kuwashwa, angalia maelezo yaliyo hapo juu.
Iwapo mipangilio imewekwa kuwa ndivyo au haijawekwa, Google Chrome itapendekeza kurasa zinazohusiana na ukurasa huu. Mapendekezo haya yanatafutwa kwa mbali kutoka seva za Google.
Ikiwa mipangilio hii imewekwa kuwa sivyo, haitatafuta wala kuonyesha mapendekezo.
Washa au zima proksi ya kupunguza data na inazuia watumiaji kubadilisha mpangilio huu.
Ukiwasha au kuzima mpangilio huu, watumiaji hawawezi kubadilisha ama kupuuza mpangilio huu.
Kama sera hii imeachwa bila kuwekwa, kipengee cha proksi ya kupunguza data kitapatikana ili mtumiaji achague kama atakitumia au la.
Inaweka mipangilio ya ukaguzi wa kivinjari chaguomsingi kwenye Google Chrome na kuzuia watumiaji kuibadilisha.
Ukiwasha mipangilio hii, Google Chrome itakagua kila wakati itakapoanza kuwaka iwapo ni kivinjari chaguomsingi na kujisajili binafsi kiotomatiki ikiwezekana.
Ukizima mipangilio hii, Google Chrome haitawahi kukagua ikiwa ni kivinjari chaguomsingi na itazima vidhibiti vya mtumiaji vya kuweka mipangilio ya chaguo hili.
Ikiwa mipangilio hii haijawekwa, Google Chrome itaruhusu mtumiaji kudhibiti iwapo ni kivinjari chaguomsingi na iwapo arifa za mtumiaji zitaonyeshwa ikiwa si kivinjari chaguomsingi.
Kumbusho kwa wasimamizi wa Microsoft® Windows: Kitendo cha kuwasha mipangilio hii kitafanya kazi katika mashine zinazotumia Windows 7 pekee. Kwa matoleo ya Windows kuanzia Windows 8, ni sharti utumie faili ya "default application associations" ambayo hufanya Google Chrome kuwa kidhibiti cha itifaki za https na http (na ukipenda, itifaki ya ftp na aina za faili kama vile .html, .htm, .pdf, .svg, .webp, n.k...). Angalia https://support.google.com/chrome?p=make_chrome_default_win ili upate maelezo zaidi.
Husanidi saraka chaguomsingi ambayo Google Chrome itatumia kupakua faili.
Ikiwa utaweka sera hii, itabadilisha saraka chaguomsingi ambayo Google Chrome hupakulia faili. Sera hii si ya lazima, kwa hivyo, mtumiaji ataweza kubadilisha saraka hiyo.
Kama hutaweka sera hii, Google Chrome itatumia saraka chaguomsingi ya kawaida (inayolenga mfumo mahususi).
Ili kupata orodha ya vigezo vinavyoweza kutumika, angalia https://www.chromium.org/administrators/policy-list-3/user-data-directory-variables.
Inakuruhusu udhibiti sehemu ambapo Zana za Wasanidi Programu zinaweza kutumika.
Ikiwa mipangilio ya sera hii imewekwa kuwa 'DeveloperToolsDisallowedForForceInstalledExtensions' (thamani ya 0, ambayo ni thamani chaguomsingi), Zana za Wasanidi Programu na kidhibiti JavaScript, zinaweza kufikiwa kwa jumla, lakini haziwezi kufikiwa katika muktadha wa viendelezi vinavyosakinishwa na sera ya biashara. Ikiwa mipangilio ya sera hii imewekwa kuwa 'DeveloperToolsAllowed' (thamani ya 1), Zana za Wasanidi Programu na kidhibiti JavaScript, zinaweza kufikiwa na kutumiwa katika miktadha yote, ikijumuisha muktadha wa viendelezi vinavyosakinishwa na sera ya biashara. Ikiwa sera hii imewekwa kuwa 'DeveloperToolsDisallowed' (thamani ya 2), Zana za Wasanidi Programu haziwezi kufikiwa na vipengele vya wavuti havitaweza kuchunguzwa tena. Hali hii itazima mikato yoyote ya kibodi na menyu zozote au data ya menyu ya kufungua Zana za Wasanidi Programu au Kidhibiti JavaScript.
Sera hii pia inadhibiti idhini ya kufikia Chaguo za Wasanidi Programu wa Android. Ukiweka sera hii kuwa DeveloperToolsDisallowed' (thamani ya 2), watumiaji hawawezi kufikia Chaguo za Wasanidi Programu. Ukiweka sera hii kuwa thamani nyingine au uiache bila kuiweka, watumiaji wataweza kufikia Chaguo za Wasanidi Programu kwa kugusa mara saba nambari ya muundo katika programu ya mipangilio ya Android.
Sera hii iliacha kutumiwa katika toleo la M68, tafadhali tumia DeveloperToolsAvailability badala yake.
Huzima Zana za Wasanidi Programu na kidhibiti JavaScript.
Ukiwasha mipangilio hii, Zana za Wasanidi Programu haziwezi kufikiwa na vipengele vya tovuti haviwezi kuchunguzwa tena. Njia zozote za mikato ya kibodi na menyu yoyote au ingizo za menyu ya muktadha za kufungua Zana za Wasanidi programu au Kidhibiti JavaScript zitazimwa.
Kuweka chaguo hii ili kuzima au kuliacha bila kuweka huruhusu mtumiaji kutumia Zana za Wasanidi Programu na kidhibiti JavaScript.
Ikiwa kipengele cha DeveloperToolsAvailability kimewashwa, thamani ya sera ya DeveloperToolsDisabled itapuuzwa.
Sera hii pia inadhibiti idhini ya kufikia Chaguo za Wasanidi Programu wa Android. Ukiweka sera hii kuwa ndivyo, watumiaji hawataweza kufikia Chaguo za Wasanidi Programu. Ukiweka sera hii kuwa sivyo au uiache bila kuiweka, watumiaji wataweza kufikia Chaguo za Wasanidi Programu kwa kugonga mara saba kwenye nambari ya muundo katika programu ya mipangilio ya Android.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, kipindi cha mgeni kinachodhibitiwa kitatumika kama ilivyowekwa katika https://support.google.com/chrome/a/answer/3017014 - "Kipindi cha Umma" cha kawaida.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo au isipowekwa, kipindi cha mgeni kinachodhibitiwa kitachukua sifa ya "Kipindi Kinachodhibitiwa" hali ambayo huondoa masharti mengi yanayowekwa katika "Vipindi vya Umma" vya kawaida.
Sera hii ikiwekwa, mtumiaji hawezi kuibadilisha wala kuibatilisha.
Sera hii ikiwekwa kuwa ArcSession, hulazimisha kifaa kuwaka tena mtumiaji akiondoka kwenye akaunti ikiwa Android imefunguka. Sera ikiwekwa kuwa 'Kila Wakati', hulazimisha kifaa kuwaka katika kila tukio la mtumiaji kuondoka kwenye akaunti. Sera isipowekwa, haina athari na hakuna kulazimisha kifaa kuwaka tena mtumiaji akiondoka kwenye akaunti. Hali hii inatumika pia ikiwa sera imewekwa kuwa 'Isiwahi'.
Huruhusu kuweka ratiba maalum ili kuangalia masasisho. Hali hii inaathiri watumiaji na violesura vyote katika kifaa. Baada ya kuwekwa, kifaa kitatafuta masasisho kulingana na ratiba. Ni sharti sera hii iondolewe ili kughairi ukaguzi wowote ulioratibiwa wa masasisho.
Kuwasha mipangilio hii huzuia kurasa za wavuti kufikia sehemu ya kichakataji cha picha (GPU). Hasa, kurasa za wavuti haziwezi kufikia API ya WebGL na programu jalizi haziwezi kutumia API ya Pepper 3D.
Hatua ya kuzima mipangilio hii au kutoiweka inaruhusu kurasa za wavuti kutumia API ya WebGL na programu jalizi kutumia API ya Pepper 3D. Mipangilio chaguomsingi ya kivinjari huenda ikahitaji hoja za mstari wa amri kupitishwa ili kutumia API hizi.
Ikiwa HardwareAccelerationModeEnabled imewekwa kuwa sivyo, Disable3DAPIs haitumiwi na ni sawa na Disable3DAPIs kuwekwa kuwa ndivyo.
Mipangilio ya Kuvinjari Salama inaonyesha ukurasa wa kuonya wakati watumiaji wanavinjari tovuti ambazo zimeripotiwa kuwa hasidi. Kuwasha mipangilio hii kunawazuia watumiaji wasifungue kurasa nyinginezo za tovuti hasidi ila ukurasa wa kuonya.
Sera hii huwazuia watumiaji wasiendelee baada ya maonyo kutoka mipangilio ya Kuvinjari Salama pekee (kwa mfano, programu hasidi na wizi wa data binafsi) wala si katika masuala yanayohusiana na cheti cha SSL kama vile vyeti visivyo sahihi au vyeti ambavyo muda wa kuvitumia umekwisha.
Ikiwa mipangilio hii imezimwa au haijawekwa, basi watumiaji wanaweza kuchagua kufungua tovuti iliyoripotiwa baada ya kuonyeshwa onyo.
Angalia https://developers.google.com/safe-browsing ili upate maelezo zaidi kuhusu mipangilio ya Kuvinjari Salama.
Sera ikiwashwa, picha za skrini haziwezi kupigwa kwa kutumia mikato ya kibodi au APl za kiendelezi.
Sera ikizimwa au isipobainishwa, upigaji picha za skrini unaruhusiwa.
Sera hii haitumiki tena. Tafadhali tumia DefaultPluginsSetting kudhibiti upatikanaji wa programu jalizi ya Flash na AlwaysOpenPdfExternally kubaini ikiwa kitazamaji cha PDF kilichojumuishwa kinapaswa kutumika kufungua faili za PDF.
Hubainisha orodha ya programu jalizi ambazo zimezimwa katika Google Chrome na huzuia watumiaji kubadilisha mipangilio hii.
Herufi wakilishi za '*' na '?' zinaweza kutumiwa kulinganisha mifuatano ya herufi za jumla. '*' inalingana na idadi fulani ya herufi za jumla na '?' inabainisha herufi moja isiyo ya lazima, kwa mfano inalingana na sufuri au herufi moja. Herufi maalum ni '\', kwa hivyo ili ilingane na herufi halisi za '*', '?', au '\', unaweza kuweka '\' mwanzoni mwa herufi hizo.
Ukiwasha mipangilio hii, orodha iliyobainishwa ya programu jalizi haitawahi kutumika katika Google Chrome. Programu jalizi zinatiwa alama kuwa zimezimwa katika sehemu ya 'about:plugins' na watumiaji hawawezi kuziwasha.
Kumbuka kwamba sera hii inaweza kubatilishwa na sera za EnabledPlugins na DisabledPluginsExceptions.
Sera hii isipowekwa, mtumiaji anaweza kutumia programu yoyote jalizi iliyosakinishwa kwenye mfumo isipokuwa katika programu jalizi zilizosimbwa kwenye kiini ambazo hazioani, zilizoishiwa na muda wa kutumia au zilizo hatari.
Sera hii haitumiki tena. Tafadhali tumia DefaultPluginsSetting kudhibiti upatikanaji wa programu jalizi ya Flash na AlwaysOpenPdfExternally kubaini ikiwa kitazamaji cha PDF kilichojumuishwa kinapaswa kutumika kufungua faili za PDF.
Hubainisha orodha ya programu jalizi ambazo mtumiaji anaweza kuwasha au kuzima katika Google Chrome.
Herufi wakilishi '*' na '?' inaweza kutumiwa kulinganisha mifuatano ya herufi za jumla. '*' inalingana na idadi fulani ya herufi za jumla na '?' inabainisha herufi moja isiyo ya lazima, kwa mfano inalingana na sufuri au herufi moja. Herufi maalum ni '\', kwa hivyo ili ilingane na herufi halisi za '*', '?', au '\', unaweza kuweka '\' mwanzoni mwa herufi hizo.
Ukiwasha mipangilio hii, orodha iliyobainishwa ya programu jalizi inaweza kutumika katika Google Chrome. Watumiaji wanaweza kuwasha au kuizima katika sehemu ya 'about:plugins', hata kama programu jalizi inalingana pia na mchoro katika DisabledPlugins. Watumiaji wanaweza kuwasha au kuzima programu jalizi ambazo zinalingana na michoro katika DisabledPlugins, DisabledPluginsExceptions na EnabledPlugins.
Sera inalenga kuruhusu hali iliyo na masharti ya kuondoa idhini huku orodha ya 'DisabledPlugins' ikijumuisha herufi wakilishi kama vile programu jalizi zote zilizozimwa '*' au kuzima programu jalizi zote za Java '*Java*' lakini msimamizi angependa kuwasha toleo fulani kama 'IcedTea Java 2.3'. Matoleo haya mahususi yanaweza kubainishwa katika sera hii.
Kumbuka kwamba haijumuishi jina la programu jalizi na jina la kikundi cha programu jalizi. Kila kikundi cha programu jalizi kinaonyeshwa katika sehemu tofauti katika sehemu ya about:plugins; kila sehemu huwa na programu jalizi moja au zaidi. Kwa mfano, programu jalizi ya "Shockwave Flash" inamilikiwa na kikundi cha "Adobe Flash Player" na majina yote mawili yanafaa kulingana na orodha ya programu ambazo hazijajumuishwa ikiwa programu jalizi inafaa kutengwa kwenye orodha ya programu ambazo haziruhusiwi.
Ikiwa sera hii imeachwa bila kuwekwa, programu yoyote jalizi inayolingana na michoro katika 'DisabledPlugins' itafunguliwa na kuzimwa na mtumiaji hataweza kuiwasha.
Sera hii imeacha kuendesha huduma, tafadhali tumia URL Zilizoondolewa Idhini badala yake. Huzima itifaki za miradi iliyoorodheshwa katika Google Chrome . URL zinazotumia miradi kutoka orodha hii hazitapakia na haziwezi kutembelewa. Iwapo sera hii haitawekwa au orodha ni tupu miradi yote itapatikana katika Google Chrome .
Huweka mipangilio ya saraka ambayo Google Chrome itatumia kuhifadhi faili zilizoakibishwa kwenye diski.
Ukiweka sera hii, Google Chrome itatumia saraka iliyotolewa bila kujali kama mtumiaji amebainisha ripoti ya '--disk-cache-dir' au la. Ili kuepuka kupoteza data au hitilafu zisizotarajiwa, sera hii haipaswi kuwekwa kuwa thamani ya kipeo cha saraka au kwenye saraka iliyotumiwa kwa madhumuni mengine, kwa sababu Google Chrome hudhibiti maudhui yake.
Angalia https://www.chromium.org/administrators/policy-list-3/user-data-directory-variables upate orodha ya aina zinazoweza kutumiwa.
Sera hii isipowekwa saraka ya akiba chaguomsingi itatumiwa na mtumiaji ataweza kuibatilisha kwa amri ya ripoti ya mstari ya '--disk-cache-dir'.
Husanidi ukubwa wa akiba ambao Google Chrome itatumia kwa ajili ya kuhifadhi faili zilizoakibishwa kwenye diski.
Ukiweka sera hii, Google Chrome itatumia ukubwa wa akiba uliotolewa bila kujali kama mtumiaji amebainisha alama ya '- ukubwa wa-diski ya-kuakibisha' au la. Thamani iliyobainishwa katika sera hii sio kikomo kisichoweza kurekebishwa bali ni pendekezo la mfumo wa kuakibisha, thamani yoyote chini ya megabaiti chache ni ndogo mno na itazidishwa hadi kiwango cha chini kinachokubalika.
Iwapo thamani ya sera hii ni 0, ukubwa chaguomsingi wa akiba utatumika lakini mtumiaji hataweza kuibadilisha.
Iwapo sera hii haijawekwa ukubwa chaguomsingi utatumika na mtumiaji ataweza kubatilisha na alama ya - ukubwa wa-diski ya-akiba.
Hupangilia saraka ambayo Google Chrome itatumia kwa kupakua faili.
Ukiweka sera hii, Google Chrome itatumia saraka iliyotolewa bila kujali iwapo mtumiaji amebainisha moja au amewasha alamisho ya kuchochewa kwa eneo la upakuaji kila wakati.
Angalia https://www.chromium.org/administrators/policy-list-3/user-data-directory-variables kwa orodha ya vigezo ambavyo vinaweza kutumiwa.
Ikiwa sera hii itasalia bila kuwekwa saraka chaguomsingi ya upakuaji itatumiwa na mtumiaji ataweza kuibadilisha.
Sera hii haiathiri programu za Android. Programu za Android hutumia saraka chaguomsingi ya vipakuliwa wakati wote na haziwezi kufikia faili zozote zilizopakuliwa na Google Chrome OS katika saraka ya vipakuliwa ambayo si chaguomsingi.
Huweka mipangilio ya aina ya vipakuliwa ambavyo Google Chrome itazuia kabisa, bila kuwaruhusu watumiajai kubatilisha uamuzi huo wa usalama.
Ukiweka sera hii, Google Chrome itazuia aina fulani ya vipakuliwa na haitamruhusu mtumiaji kukwepa onyo za usalama.
Chaguo la 'Zuia vipakuliwa hatari' linapoteuliwa, vipakuliwa vyote vinakubaliwa isipokuwa vile vilivyo na onyo la Kuvinjari Salama.
Chaguo la 'Zuia vipakuliwa ambavyo huenda ni hatari' linapoteuliwa, vipakuliwa vyote vinakubaliwa isipokuwa vile vilivyo na onyo la Kuvinjari Salama kwa vipakuliwa ambavyo huenda si Salama.
Chaguo la 'Zuia vipakuliwa vyote' linapoteuliwa, vipakuliwa vyote vitazuiwa.
Sera hii isipowekwa, (au chaguo la 'Hakuna vizuizi maalum' linapoteuliwa), vipakuliwa vitapitia vizuizi vya kawaida vya usalama kulingana na matokeo ya uchanganuzi wa Kuvinjari Salama.
Kumbuka kuwa vizuizi hivi hutumika kwa vipakuliwa vinavyosababishwa na maudhui kwenye ukurasa wa tovuti pamoja na chaguo la menyu ya 'pakua kiungo...'. Vizuizi hivi havitumiki kwenye vipengele vya kuhifadhi au kupakua vya ukurasa unaoonekana sasa, wala havitumiki kwa kuhifadhi faili katika muundo wa PDF kwenye chaguo za kuchapisha. Angalia https://developers.google.com/safe-browsing ili upate maelezo zaidi kuhusu Kuvinjari salama.
Ukiwasha mipangilio hii, watumiaji wataruhusiwa kutumia Smart Lock ikiwa mahitaji ya kipengele hiki yanatimizwa.
Ukizima mipangilio hii, watumiaji hawataruhusiwa kutumia Smart Lock.
Sera hii ikiachwa bila kuwekwa, hali chaguomsingi hairuhusiwi kwa ajili ya watumiaji wanaodhibitiwa na kampuni na huruhusiwa kwa watumiaji wasiodhibitiwa.
Hubainisha hatua inayopaswa kuchukuliwa wakati saraka ya mtumiaji ya ukurasa wa mwanzo iliundwa kwa kutumia usimbaji wa ecryptfs.
Ukiweka sera hii kuwa 'DisallowArc', programu za Android zitazimwa kwa mtumiaji na haitatekeleza uhamishaji kutoka usimbaji wa ecryptfs kuwa ext4. Programu za Android hazitazuiwa kutumika wakati saraka ya ukurasa wa mwanzo tayari imesimbwa katika ext4.
Ukiweka sera hii kuwa 'Hamisha', saraka za ukurasa wa mwanzo zenye usimbaji wa ecryptfs zitahamishwa kiotomatiki kuwa usimbaji wa ext4 mtumiaji atakapoingia katika akaunti bila kuomba idhini ya mtumiaji.
Ukiweka sera hii kuwa 'Futa', saraka za ukurasa wa mwanzo zilizosimbwa kwa ecryptfs zitafutwa wakati wa kuingia katika akaunti na badala yake, itaunda saraka mpya za ukurasa wa mwanzo zilizosimbwa kwa ext4. Onyo: Hatua hii itaondoa data kwenye kifaa cha mtumiaji.
Ukiweka sera hii kuwa 'MinimalMigrate', saraka za ukurasa wa mwanzo zilizosimbwa kwa ecryptfs zitafutwa wakati wa kuingia katika akaunti na badala yake itaunda saraka mpya za ukurasa wa mwanzo zilizosimbwa kwa ext4. Hata hivyo, itajaribu kuweka tokeni za kuingia katika akaunti ili mtumiaji asihitaji kuingia katika akaunti tena. Onyo: Hatua hii itaondoa data kwenye kifaa cha mtumiaji.
Ukiweka sera hii kuwa chaguo ambalo halitumiki tena ('AskUser' au 'AskForEcryptfsArcUsers'), itachukuliwa kana kwamba ulikuwa umechagua 'Migrate' badala yake.
Sera hii haitumiki kwa watumiaji wa programu za skrini nzima. Sera hii isipowekwa, kifaa kitafanya kazi kama kwamba 'DisallowArc' imechaguliwa.
Ukiwasha mipangilio hii, alamisho zinaweza kuongezwa, kuondolewa au kubadilishwa. Hii ndio hali chaguomsingi wakati sera hii haijawekwa.
Ukizima mipangilio hii, alamisho haziwezi kuongezwa, kuondolewa au kubadilishwa. Alamisho ambazo tayari zilikuwepo bado zinapatikana.
Bainisha orodha ya vipengele vilivyoacha kuendesha huduma vya mbinu ya wavuti ili kuwasha tena kwa muda.
Sera hii inawapa wasimamizi uwezo wa kuwasha tena vipengele vilivyoacha kuendesha huduma vya mbinu ya wavuti kwa muda mfupi. Vipengele vinatambuliwa kwa lebo ya mfuatano na vipengele vinavyolingana na lebo vilivyojumuishwa katika orodha iliyobainishwa na sera hii vitawashwa tena.
Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa, au orodha ikiwa tupu au hailingani na mojawapo ya lebo za mifuatano, vipengele vyote vilivyoacha kuendesha huduma vya mbinu ya wavuti vitasalia vikiwa vimezimwa.
Ingawa sera yenyewe inaweza kutumiwa kwenye mbinu zilizo hapo juu, kipengele inachokiwasha kinaweza kupatikana kwenye mbinu chache. Si vipengele vyote vilivyoacha kuendesha huduma vya Mbinu ya Wavuti vinaweza kuwashwa tena. Vilivyoorodheshwa hapa chini pekee ndivyo vinavyoweza kuwashwa tena kwa muda mfupi, muda huo ni tofauti kwa kila kipengele. Muundo wa jumla wa lebo ya mfuatano utakuwa [DeprecatedFeatureName]_EffectiveUntil[yyyymmdd]. Kama rejeleo, unaweza kupata lengo la yaliyochangia mabadiliko ya kipengele cha Mbinu ya Wavuti https://bit.ly/blinkintents.
Kutokana na sababu kwamba ukaguzi wa ubatilishaji wa mtandaoni unaoshindwa chinichini hautoi usalama bora unaofanya kazi, unazimwa kwa chaguomsingi katika toleo la 19 la Google Chrome na matoleo mapya zaidi. Kwa kuweka sera hii kuwa ndivyo, tabia ya awali inarejeshwa na ukaguzi wa mtandaoni wa OCSP/CRL utatekelezwa.
Ikiwa sera hii haitawekwa, au ikiwekwa kuwa sivyo, basi Google Chrome haitatekeleza ukaguzi wa ubatilishaji wa mtandaoni katika Google Chrome 19 na matoleo mapya zaidi.
Wakati mipangilio hii imewashwa, Google Chrome inaruhusu vyeti vilivyotolewa na huduma ya PKI ya Zamani ya Shirika la Symantec viaminike, ikiwa vitathibitisha na kuunganisha kwenye cheti cha CA kinachotambulika.
Kumbuka kuwa sera hii inategemea mfumo wa uendeshaji ambao bado unatambua vyeti kutoka mfumo wa zamani wa Symantec. Ikiwa sasisho la Mfumo wa Uendeshaji linabadilisha utunzaji wa Mfumo wa Uendeshaji wa vyeti kama hivyo, Sera hii haitatumika. Pia, sera hii inakusudiwa kuwa njia ya muda ya kuipa biashara wakati wa kutosha kuondoka kwenye vyeti vya mfumo wa zamani wa Symantec. Sera hii itaondolewa mnamo au karibu na tarehe 1 Januari 2019.
Ikiwa sera hii haijawekwa, au ikiwekwa kuwa sivyo, inamaanisha kuwa Google Chrome itafuata ratiba ya umma ya kuacha kuendesha huduma iliyotangazwa.
Angalia https://g.co/chrome/symantecpkicerts ili upate maelezo kuhusu kuacha kuendesha huduma.
Sera hii inadhibiti ikiwa Idhini ya Kusawazisha inaweza kuonyeshwa kwa mtumiaji anapoingia katika akaunti kwa mara ya kwanza. Inapaswa kuwekwa kuwa sivyo ikiwa Idhini ya Kusawazisha haitahitajika kwa mtumiaji. Ikiwa imewekwa kuwa sivyo, Idhini ya Kusawazisha haitaonekana. Ikiwa imewekwa kuwa ndivyo au haijawekwa, Idhini ya Kusawazisha inaweza kuonyeshwa.
Sera hii haitumiki tena. Tafadhali tumia DefaultPluginsSetting kudhibiti upatikanaji wa programu jalizi ya Flash na AlwaysOpenPdfExternally kubaini ikiwa kitazamaji cha PDF kilichojumuishwa kinapaswa kutumika kufungua faili za PDF.
Hubainisha orodha ya programu jalizi ambazo zimewashwa katika Google Chrome na huzuia watumiaji kubadilisha mipangilio hii.
Herufi wakilishi za '*' na '?' zinaweza kutumiwa kulinganisha mifuatano ya herufi za jumla. '*' inalingana na idadi fulani ya herufi za jumla na '?' inabainisha herufi moja isiyo ya lazima, kwa mfano inalingana na sufuri au herufi moja. Herufi maalum ni '\', kwa hivyo ili ilingane na herufi halisi za '*', '?', au '\', unaweza kuweka '\' mwanzoni mwa herufi hizo.
Orodha iliyobainishwa ya programu jalizi hutumika kila wakati katika Google Chrome ikiwa zimesakinishwa. Programu jalizi zinatiwa alama kuwa zimewashwa katika sehemu ya 'about:plugins' na watumiaji hawawezi kuzizima.
Kumbuka kwamba sera hii inafuta sera za DisabledPlugins na DisabledPluginsExceptions.
Sera hii ikiachwa bila kuwekwa, mtumiaji anaweza kuzima programu jalizi yoyote iliyosakinishwa kwenye mfumo.
Sera hii ikiruhusiwa, viendelezi vilivyosakinishwa kupitia sera ya biashara huruhusiwa kutumia Enterprise Hardware Platform API.
Sera hii ikizimwa au mipangilio yake isipowekwa, hakuna viendelezi vinavyoruhusiwa kutumia Enterprise Hardware Platform API. Sera hii inatumika pia kwa viendelezi vya sehemu kama vile kiendelezi cha Huduma za Hangout.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, hifadhi ya nje haitapatikana katika kivinjari cha faili.
Sera hii inaathiri aina zote za maudhui ya hifadhi. Kwa mfano: hifadhi za USB ya mwako, diski kuu za nje, kadi ya SD na kadi nyingine za hifadhi, hifadhi ya optiki n.k. Hifadhi ya ndani haiathiriwi, kwa hvyo faili zilizohifadhiwa kwenye folda ya Vipakuliwa bado zinaweza kufikiwa. Hifadhi ya Google pia haiathiriwi na sera hii.
Mipangilio hii ikizimwa au ikiachwa bila kuwekwa, basi watumiaji wanaweza kutumia aina zote za hifadhi ya nje zinazotumika kwenye vifaa vyao.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, watumiaji hawawezi kuandika chochote kwenye vifaa vya hifadhi ya nje.
Mipangilio hii ikiwekwa kuwa sivyo au isipowekwa, basi watumiaji wanaweza kuunda na kurekebisha faili za vifaa vya hifadhi ya nje ambavyo vinaweza kuandikwa.
Sera ya ExternalStorageDisabled huchukua nafasi ya sera hii - ikiwa ExternalStorageDisabled imewekwa kuwa ndivyo, basi idhini zote za kufikia hifadhi ya nje huzimwa na sera hii kupuuzwa.
Kipengele cha kuonyesha upya sera hii kinatumika katika M56 na matoleo ya baadaye.
Sera hii imeacha kuendesha huduma, badala yake jaribu kutumia kipengele cha BrowserSignin.
Kama sera hii imewekwa kuwa ndivyo, mtumiaji anahitaji kuingia katika akaunti ya Google Chrome kwa kutumia wasifu wake kabla ya kutumia kivinjari. Na thamani chaguomsingi ya BrowserGuestModeEnabled itawekwa kuwa sivyo. Kumbuka kuwa wasifu uliopo ambao haujatumiwa kuingia katika akaunti utafungwa na hautaweza kufikiwa baada ya kuwasha sera hii. Kwa maelezo zaidi, angalia makala ya kituo cha usaidizi.
Kama sera hii itawekwa kuwa sivyo au mipangilio haijawekwa, mtumiaji anaweza kutumia kivinjari bila kuingia katika akaunti ya Google Chrome.
Sera hii ikiwekwa kuwa imewashwa hulazimisha wasifu ubadilishwe kuwa kipindi cha matumizi ya muda. Sera hii ikibainishwa kuwa sera ya Mfumo wa Uendeshaji (k.m. GPO kwenye Windows) itatumika katika kila wasifu kwenye mfumo; sera hii ikiwekwa kuwa sera ya Wingu, itatumika kwenye wasifu ulioingia ukitumia akaunti inayosimamiwa pekee.
Katika hali hii, data ya wasifu huchanganuliwa kwenye diski kwa muda wote wa kipindi cha mtumiaji. Vipengele kama vile historia ya kivinjari, viendelezi na data yake, data ya wavuti kama vile vidakuzi na hifadhidata za wavuti hazihifadhiwi baada ya kufunga kivinjari. Hata hivyo, jambo hili halimzuii mtumiaji kupakua data yoyote kwenye diski, kuhifadhi au kuchapisha kurasa.
Ikiwa mtumiaji amewasha kipengele cha kusawazisha, data hii yote itahifadhiwa katika wasifu wake wa kusawazisha kama wasifu wa kawaida. Pia hali fiche inapatikana isipozimwa kabisa na sera.
Sera ikiwekwa kuwa imezimwa au isipowekwa, kuingia katika akaunti husababisha kuwepo kwa wasifu wa kawaida.
Hulazimisha maswali katika Utafutaji wa Wavuti wa Google kufanywa na SafeSearch ikiwa imewashwa na huzuia watumiaji kubadilisha mpangilio huu.
Ukiwasha mpangilio huu, SafeSearch katika Utafutaji wa Google huwa imewashwa wakati wote.
Ukifunga mpangilio huu au usipoweka thamani, SafeSearch katika Utafutaji wa Google haitekelezwi.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, Google Chrome itatumia dirisha lote la kwanza linaloonyeshwa kwenye utekelezaji wa kwanza. Ikiwa sera hii itawekwa kuwa sivyo au mipangilio haitawekwa, uamuzi wa kutumia dirisha lote la kwanza linaloonyeshwa utalingana na ukubwa wa skrini.
Sera hii hulazimisha msimbo wa kuweka mitandao kutekelezwa katika mchakato wa kivinjari.
Sera hii imezimwa kwa chaguomsingi na ikiwashwa, watumiaji hawalindwi dhidi ya matatizo ya usalama baada ya mchakato wa kuweka mitandao kuanza utaratibu wa kuweweka vikwazo.
Sera hii ina lengo la kuzipa biashara fursa ya kuhamia kwenye programu ya watu au kampuni nyingine ambayo haitegemei mvuto wa API za kuweka mtandao. Seva mbadala zinapendekezwa badala ya urekebishaji wa API ya Win32 na LPS.
Ikiwa sera hii haijawekwa, msimbo wa kuweka mItandao huenda hautatekeleza mchakato wa kivinjari kulingana na majaribio ya sehemu ya jaribio la NetworkService.
Sera hii imeacha kuendesha huduma, tafadhali tumia ForceGoogleSafeSearch na ForceYouTubeRestrict badala yake. Sera hii haitumiwi ikiwa sera za ForceGoogleSafeSearch, ForceYouTubeRestrict au sera za (sera iliyoacha kuendesha huduma) ForceYouTubeSafetyMode zimewekwa.
Hulazimisha hoja katika huduma ya Kutafuta kwenye Wavuti ya Google kufanywa na kipengele cha Utafutaji Salama ikiwa kimewashwa na huzuia watumiaji kubadilisha mipangilio hii. Mipangilio hii pia hulazimisha Hali ya Wastani yenye Mipaka kwenye YouTube.
Ukiwasha mipangilio hii, kipengele cha Utafutaji Salama katika huduma ya Tafuta na Google na Hali ya Wastani yenye Mipaka kwenye YouTube hutumika kila wakati.
Ukizima mipangilio hii au usiweke thamani, kipengele cha Utafutaji Salama katika huduma ya Tafuta na Google na Hali ya Wastani yenye Mipaka kwenye YouTube haitumiki.
Hutekeleza kiwango cha chini cha Hali yenye Mipaka kwenye YouTube na huwazuia watumiaji kuchagua hali ambayo haijawekewa mipaka mingi.
Mipangilio hii ikiwekwa kuwa ya Lazima, Hali yenye Mipaka ya Lazima kwenye YouTube inafanya kazi kila wakati.
Mipangilio hii ikiwekwa kuwa ya Wastani, mtumiaji anaweza kuchagua Hali yenye Mipaka ya Wastani pekee na Hali yenye Mipaka ya Lazima kwenye YouTube, lakini hawezi kuzima Hali yenye Mipaka.
Mipangilio hii ikiwekwa kuwa Imezimwa au hakuna thamani iliyowekwa, Hali yenye Mipaka kwenye YouTube haitatekelezwa na Google Chrome. Sera za nje kama vile sera za YouTube bado zinaweza kutekeleza Hali yenye Mipaka.
Sera hii haiathiri progamu ya Android YouTube. Ikiwa Hali ya Usalama kwenye YouTube inapaswa kutekelezwa, kusakinishwa kwa programu ya Android YouTube haipaswi kuruhusiwa.
Sera hii haitumiki tena. Tunakushauri utumie ForceYouTubeRestrict, ambayo inabatilisha sera hii na kuruhusu uboreshaji zaidi.
Hulazimisha Hali ya Wastani ya YouTube yenye Mipaka na kuzuia watumiaji kubadilisha mipangilio hii.
Ikiwa mipangilio hii imewashwa. Hali ya YouTube yenye Mipaka hutumika kwa angalau kiwango cha Wastani.
Mipangilio hii ikizimwa au thamani isipowekwa, Hali ya YouTube yenye Mipaka haitumiki kwenye Google Chrome. Sera za nje kama vile sera za YouTube zinaweza kutekeleza Hali yenye Mipaka.
Sera hii haiathiri progamu ya Android YouTube. Ikiwa Hali ya Usalama kwenye YouTube inapaswa kutekelezwa, kusakinishwa kwa programu ya Android YouTube haipaswi kuruhusiwa.
Sera hii inadhibiti upatikanaji wa hali ya skrini nzima ambayo kiolesura chote cha Google Chrome kimefichwa na ni maudhui ya wavuti tu yanayoonekana.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo ama isipowekwa, mtumiaji, programu na viendelezi vyenye ruhusa vinaweza kuingia katika hali ya skrini nzima.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, mtumiaji ama programu haziwezi kuingia katika hali ya skrini nzima.
Kwenye mifumo yote, isipokuwa Google Chrome OS, skrini nzima haipatikani wakati hali ya skrini nzima imezimwa.
Sera hii haiathiri programu za Android kwa njia yoyote. Zitaweza kuwekwa katika hali ya skrini nzima hata kama sera hii imewekwa kuwa False.
Ikiwa sera hii imewekwa kuwa ndivyo au haijawekwa, kipengele cha kuongeza kasi kwa kutumia maunzi kitawashwa isipokuwa kipengele fulani cha GPU kikose kuruhusiwa.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, kipengele cha kuongeza kasi kwa kutumia maunzi kitazimwa.
Ficha programu ya Duka la Chrome kwenye Wavuti na kiungo cha kijachini kutoka kwenye Ukurasa wa Kichupo Kipya na kifungua programu cha Google Chrome OS.
Sera hii inapowekwa kuwa ndivyo, aikoni hufichwa.
Sera hii inapowekwa kuwa sivyo au isiposanidiwa, aikoni huonekana.
Sera hii huwasha HTTP/0.9 kwenye milango mbali na 80 ya HTTP na 443 ya HTTPS.
Sera huzimwa kwa chaguomsingi, na ikiwashwa, huwaacha watumiaji katika hali ambayo wanaweza kupata matatizo ya usalama https://crbug.com/600352.
Sera hii inadhamiria kuwapa wafanyabiashara nafasi ya kuhamisha seva za sasa kutoka HTTP/0.9, na itaondolewa siku zijazo.
Sera hii isipowekwa, HTTP/0.9 itazimwa kwenye milango ambayo si chaguomsingi.
Sera hii inalazimisha data ya fomu ya kujaza otomatiki kuletwa kutoka kwenye kivinjari chaguomsingi cha awali ikiwa itawashwa. Ikiwashwa, sera hii pia inaathiri kidirisha cha kuleta
Ikizimwa, data ya fomu ya kujaza otomatiki haitaletwa.
Ikiwa haitawekwa, huenda mtumiaji akaombwa kuleta, au huenda uletaji ukafanyika kiotomatiki.
Sera hii ikitekelezwa, hulazimisha alamisho kuingizwa kutoka kivinjari chaguomsingi cha sasa. Ikitekelezwa, sera hii pia itaathiri kidadisi cha kuingiza.
Isipotekelezwa, hakuna alamishi zitakazoingizwa.
Ikiwa hii haitawekwa, huenda mtumiaji akaulizwa aingize alamisho, au huenda zikaingizwa kiotomatiki.
Sera hii inalazimisha historia ya kuvinjari kuletwa kutoka kwenye kivinjari chaguomsingi cha sasa ikiwa imewezeshwa. Ikiwa imewezeshwa, sera hii pia inaathiri kidadisi cha kuleta.
Ikiwa imelemazwa, hakuna historia ya kuvinjari inayoletwa.
Ikiwa haijawekwa, mtumiaji anaweza kuombwa iwapo anataka kuleta, au uletaji unaweza kufanyika kiotomatiki.
Sera hii inalazimisha ukurasa wa kwanza kuingizwa kutoka kwenye kivinjari chaguomsingi cha sasa, kikiwashwa.
Ikilemazwa, ukurasa wa mwanzo hautaletwa.
Ikiwa hautawekwa, huenda mtumiaji akaombwa kuleta, au huenda uletaji ukatendeka kiotomatiki.
Sera hii inalazimisha manaenosiri yaliyohifadhiwa kuletwa kutoka kwenye kivinjari chaguomsingi cha awali ikiwezeshwa. Ikiwezeshwa, sera hii pia inaathiri kidadisi cha kuleta.
Ikilemazwa, manenosiri yaliyohifadhiwa hayataletwa.
Ikiwa haitawekwa, huenda mtumiaji akaombwa kuleta, au huenda uletaji ukatendeka kiotomatiki.
Sera hii inailazimisha mitambo ya kutafuta kuingizwa kutoka kivinjari chaguomsingi cha sasa iwapo itawashwa. Ikiwashwa, sera hii pia itaathiri kidadisi cha kuingiza.
Ikizimwa, mtambo chaguomsingi wa kutafuta hauingizwi.
Ikiwa haitawekwa, mtumiaji anaweza kuomba aingize, au huenda ungizaji ukatendeka kiotomatiki.
Sera hii imepitwa na wakati. Tafadhali, tumia IncognitoModeAvailability badala yake. Huwasha hali fiche katika Google Chrome.
Ikiwa mpangilio huu umewashwa au haujasanidiwa, watumiaji wanaweza kufungua kurasa za wavuti katika hali fiche.
Ikiwa mpangilio huu umezimwa, watumiaji hawawezi kufungua kurasa za wavuti katika hali fiche.
Ikiwa sera hii itawachwa ikiwa haijawekwa, hii itawashwa na mtumiaji ataweza kutumia hali fiche.
Hubainisha iwapo mtumiaji anaweza kufungua kurasa katika hali Fiche kwenye Google Chrome.
Ikiwa hiari ya 'Imewashwa' imechaguliwa au sera haijawekwa, huenda kurasa zikafunguliwa katika hali Fiche.
Ikiwa hiari ya 'Imezimwa' imechaguliwa, huenda kurasa zisifunguliwe katika hali Fiche.
Ikiwa hiari ya 'Imelazimishwa' imechaguliwa, huenda kurasa zikafunguliwa TU katika hali Fiche.
Mipangilio hii ikiwashwa, watumiaji wataruhusiwa kutumia Mtandao wa Kusambazwa Papo Hapo, ambao huruhusu simu yao ya Google kushiriki data ya mtandao wa simu na kifaa chao.
Mipangilio hii ikizimwa, watumiaji hawataruhusiwa kutumia Mtandao wa Kusambazwa Papo Hapo.
Sera hii ikiachwa bila kuwekwa, hali chaguomsingi hairuhusiwi kwa ajili ya watumiaji wanaodhibitiwa na kampuni na huruhusiwa kwa watumiaji wasiodhibitiwa.
Iwapo sera imewashwa, kila chanzo ulichotaja katika orodha inayotenganishwa kwa koma kitatumia mchakato wake. Hatua hii pia itatenga vyanzo vinavyotajwa kwa vikoa; k.m. hatua ya kubainisha https://example.com/ itasababisha pia https://foo.example.com/ itengwe ili isiwe sehemu ya tovuti ya https://example.com/. Ukizima sera hii, vipengele vyote viwili vya IsolateOrigins na SitePerProcess vitazimwa. Bado watumiaji wataweza kuwasha IsolateOrigins wenyewe kupitia ripoti za mstari wa amri. Usipoweka mipangilio ya sera hii, mtumiaji ataweza kubadilisha mipangilio hii. Kwenye Google Chrome OS, tunapendekeza uweke pia sera ya kifaa cha DeviceLoginScreenIsolateOrigins iwe katika thamani ile ile. Iwapo thamani zilizobainishwa na sera zote mbili hazilingani, huenda ikachelewesha kufungua kipindi cha mtumiaji wakati inatumia thamani iliyobainishwa na sera ya mtumiaji.
KUMBUKA: Sera hii haitumiki kwenye Android. Ili uwashe IsolateOrigins kwenye Android, tumia mipangilio ya sera ya IsolateOriginsAndroid.
Iwapo umewasha sera hii, kila chanzo unachobainisha katika orodha inayotenganishwa kwa koma kitatumia mchakato wake. Hatua hii pia itatenga vyanzo vinavyotajwa kwa vijikoa; k.m. hatua ya kubainisha https://example.com/ itasababisha pia https://foo.example.com/ itengwe ili isiwe sehemu ya tovuti ya https://example.com/. Iwapo sera imezimwa, hamna Utengaji wa Tovuti wa moja kwa moja utakaofanyika na majaribio ya sehemu za IsolateOriginsAndroid na SitePerProcessAndroid yatazimwa. Bado watumiaji wataweza kuwasha IsolateOrigins wenyewe, kupitia ripoti ya mstari wa amri. Iwapo hujaweka mipangilio ya sera, mtumiaji ataweza kubadilisha mipangilio hii.
KUMBUKA: Kwenye Android, Utengaji wa Tovuti unatumika kama majaribio. Tutaendelea kuimarisha uwezo wa kutumia huduma hii, lakini kwa sasa huenda ikasababisha matatizo ya utendaji.
KUMBUKA: Sera hii inatumika tu katika Chrome kwenye Android inayotumia tu vifaa vilivyo na RAM inayozidi GB1. Ili utumie sera hii kwenye mifumo isiyo ya Android, tumia IsolateOrigins.
Sera hii imepingwa, tafadhali tumia DefaultJavaScriptSetting badala yake.
Inaweza kutumiwa kulemaza JavaScript kwenye Google Chrome.
Iwapo mpangilio huu umelemazwa, kurasa za wavuti haziwezi kutumia JavaScript na mtumiaji hawezi kubadilisha mpangilio huo.
Iwapo mpangilio huu umezimwa au la, kurasa za wavuti zinaweza kutumia JavaScript lakini mtumiaji anaweza kubadilisha mpangilio huo.
Hutoa idhini ya kufikia vitufe vya shirika vya viendelezi.
Vitufe vinateuliwa kwa matumizi ya shirka ikiwa vitazalishwa kwa kutumia API ya chrome.platformKeys kwenye akaunti inayodhibitiwa. Vitufe vinavyoletwa au kuzalishwa kwa njia nyingine haviteuliwi kwa ajili ya matumizi ya shirika.
Uwezo wa kufikia vitufe vilivyoteuliwa kwa ajili ya matumizi ya shirika unadhibitiwa mahususi na sera hii. Mtumiaji hawezi kutoa idhini wala kuondoa uwezo wa kufikia vitufe vya shirika kuenda au kutoka kwenye viendelezi.
Kwa chaguomsingi kiendelezi hakiwezi kutumia kitufe kilichoteuliwa kwa ajili ya matumizi ya shirika, ambayo ni sawa na kuweka allowCorporateKeyUsage kwenye sivyo kwa kiendelezi hicho.
Ikiwa tu allowCorporateKeyUsage itawekwa kuwa ndivyo kwa kiendelezi, inaweza kutumia mfumo wa kitufe chochote kilichowekewa alama kwa ajili ya matumizi ya shirika kutia sahihi data isiyo na mpangilio. Ruhusa hii inapaswa tu kutolewa kama kiendelezi kinaaminiwa kuweka ufikiaji salama wa kitufe dhidi ya wavamizi.
Programu za Android haziwezi kufikia vitufe vya shirika. Sera hii haiviathiri.
Sera hii haifanyi kazi katika M72. Badala yake, tafadhali tumia CloudManagementEnrollmentToken.
Huweka mipangilio ya orodha ya alamisho zinazodhibitiwa.
Sera hii inajumuisha orodha ya alamisho na kila alamisho ni kamusi yenye funguo za "name" na "url" ambazo zina jina la alamisho na lengo lake. Folda ndogo inaweza kuwekewa mipangilio kwa kufafanua alamisho bila ufunguo wa "url" lakini yenye ufunguo wa ziada wa "children" ambao una orodha ya alamisho kama ilivyofafanuliwa hapo juu (baadhi yazo zinaweza kuwa folda tena). Google Chrome inaweza kurekebisha URL ambazo hazijakamilika kama kwamba ziliwasilishwa kupitia Sanduku kuu, kwa mfano, "google.com" huwa "https://google.com/".
Alamisho hizi zinawekwa katika folda ambayo haiwezi kubadilishwa na mtumiaji (lakini mtumiaji anaweza kuchagua kuificha isionekane kwenye sehemu ya alamisho). Kwa chaguomsingi, jina la folda ni "Alamisho zinazodhibitiwa" lakini linaweza kuwekewa mapendeleo kwa kuongeza kwenye orodha ya alamisho kamusi yenye ufunguo wa "toplevel_name" ulio na jina la folda ambalo ungependa kuwa thamani.
Alamisho zinazodhibitiwa hazisawazishwi kwenye akaunti ya mtumiaji na haziwezi kurekebishwa na viendelezi.
Inabainisha idadi ya juu ya miunganisho sawia katika seva ya proksi.
Seva nyingine za proksi haziwezi kushughulikia idadi kubwa ya miunganisho inayoendana kwa kila mteja na hii inaweza kutatuliwa kwa kuweka sera hii hadi katika thamani ya chini.
Thamani ya sera hii inapaswa kuwa chini ya 100 na kubwa kwa 6 na thamani chaguomsingi ni 32.
Programu nyingine za wavuti zinajulikana kutumia miunganisho mingi kwa GET zinazoning'inia, kwa hivyo kupunguza chini ya 32 kunaweza kusababisha kuning'inia kwa mytando wa kuvinjari ikiwa programu nyingi kama hizo zimefungka. Punguza hadi chini ya chaguomsingi kwa tahadhari yako.
Ikiwa sera hii itasalia kama haijawekwa thamani chaguomsingi itatumika ambayo ni 32.
Hubainisha upeo wa ucheleweshaji katika milisekunde kati ya wakati wa kupokea uthibitishaji wa sera na uletaji wa sera mpya kutoka kwenye huduma ya usimamizi wa kifaa.
Kuweka sera hii kunapuuzia thamani chaguomsingi ya milisekunde 5000. Thamani halali za sera hii ziko kati ya 1000 (sekunde 1) na 300000 (dakika 5 min). Thamani zozote zisizo katika mfululizo huu zitaunganishwa kwenye mpaka husika.
Kuacha sera hii bila kuiweka kutafanya Google Chrome itumie thamani chaguomsingi ya milisekunde 5000.
Husanidi ukubwa wa akiba ambao Google Chrome itatumia kwa ajili ya kuhifadhi faili zilizoakibishwa kwenye diski.
Ukiweka sera hii, Google Chrome itatumia ukubwa wa akiba uliotolewa bila kujali kama mtumiaji amebainisha alama ya '- disk-cache-size' au la. Thamani iliyobainishwa katika sera hii sio kikomo kisichoweza kurekebishwa bali ni pendekezo la mfumo wa Kuakibisha, thamani yoyote chini ya megabaiti chache ni ndogo mno na itazidishwa hadi kiwango cha chini kinachokubalika.
Iwapo thamani ya sera hii ni 0, ukubwa chaguomsingi wa akaiba utatumika lakini mtumiaji hataweza kuibadilisha.
Iwapo sera hii haijawekwa ukubwa chaguomsingi utatumika na mtumiaji ataweza kubatilisha na alama ya- ukubwa wa-diski ya-akiba.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, Google Cast itaunganishwa na Vifaa vinavyotuma maudhui kwenye anwani zote za IP, si anwani za faragha za RFC1918/RFC4193 pekee.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, Google Cast itaunganishwa na Vifaa vinavyotuma maudhui kwenye anwani za faragha za RFC1918/RFC4193 pekee.
Sera hii isipowekwa, Google Cast itaunganishwa na Vifaa vinavyotuma maudhui kwenye anwani za faragha za RFC1918/RFC4193 pekee, isipokuwa kipengele cha CastAllowAllIPs kiwashwe.
Sera ya "EnableMediaRouter" ikiwekwa kuwa sivyo, inamaanisha kuwa thamani ya sera hii haitakuwa na athari yoyote.
Huwasha kuripoti kunakoficha data ya matumizi na data inayohusiana na programu kuacha kufanya kazi kuhusu Google Chrome kwa Google na huzuia watumiaji kubadilisha mipangilio hii.
Ukiwasha mipangilio hii, kuripoti kunakoficha data ya matumizi na data inayohusiana na programu kuacha kufanya kazi hutumwa kwa Google. Ukizima mipangilio hii, maelezo haya hayatatumwa kwa Google. Katika hali zote, watumiaji hawawezi kubadilisha au kufuta mipangilio. Sera hii isipowekwa, mipangilio itakuwa ile ambayo mtumiaji alichagua wakati wa kusakinisha programu au utekelezaji wa kwanza wa programu.
Sera hii inapatikana kwenye matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®. au matukio ya Windows 10 Pro au Enterprise yaliyojumuishwa katika usimamizi wa kifaa. (Kwa ajili ya Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome, angalia DeviceMetricsReportingEnabled.)
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo au isipowekwa, ukurasa wa Kichupo Kipya utaonyesha mapendekezo ya maudhui kulingana na historia ya kuvinjari, mambo yanayovutia, au mahali alipo mtumiaji.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, mapendekezo ya maudhui yanayozalishwa kiotomatiki hayataonyeshwa katika ukurasa wa Kichupo Kipya.
Inawasha kipengele cha ubashiri wa mtandao katika Google Chrome na kuzuia watumiaji wasiweze kubadilisha mipangilio hii.
Hatua hii hudhibiti hali ya kuleta DNS mapema, uunganishaji na utekelezaji awali wa kurasa za wavuti za TCP na SSL.
Ukiweka sera hii, watumiaji hawawezi kubadilisha wala kubatilisha mipangilio hii katika Google Chrome.
Usipoweka sera hii, kipengele cha ubashiri wa mtandao kitawashwa lakini watumiaji wataweza kukibadilisha.
Huzibainisha programu zinazoweza kuwashwa kuwa programu za kuandika madokezo kwenye skrini iliyofungwa ya Google Chrome OS.
Unapoitumia programu ya kuandika vidokezo unayoipendelea kwenye skrini iliyofungwa, kiolesura cha kufungua programu hiyo kitaonekana kwenye skrini iliyofungwa. Unapoifungua programu hiyo, programu itaunda dirisha la programu sehemu ya juu ya skrini iliyofungwa na vipengee vya data (vidokezo) vitaundwa katika skrini iliyofungwa. Programu italeta vidokezo vilivyoundwa kwenye kipindi msingi cha mtumiaji, unapokifungua kipindi. Kwa sasa, unaweza tu kuzitumia programu za Chrome za kuandika vidokezo kwenye skrini iliyofungwa.
Ukiiweka sera, mtumiaji ataruhusiwa kuwasha programu kwenye skrini iliyofungwa iwapo tu Kitambulisho cha kiendelezi kiko kwenye orodha ya thamani ya sera. Ukiiweka sera hii kwenye orodha tupu, kipengele cha kuandika vidokezo kwenye skrini iliyofungwa kitazimwa kabisa. Kumbuka kuwa sera iliyo na Kitambulisho cha programu haimaanishi kuwa mtumiaji anaweza kuwasha programu kuandika vidokezo kwenye skrini iliyofungwa - kwa mfano, kwenye Chrome 61, programu ambazo unaweza kuzitumia zimewekewa vikwazo na mfumo.
Usipoiweka sera, hamna vikwazo vitakavyowekwa kwenye seti ya programu ambazo mtumiaji anaweza kuwasha kwenye skrini iliyofungwa vilivyowekwa na sera.
Inaruhusu kusukuma kwa usanidi wa mtandao kutekelezwa kwa kila mtumiaji katika kifaa cha Google Chrome OS. Usanidi wa mtandao ni mtungo ulioumbizwa wa JSON kama ilivyofasiliwa kwa umbizo la Fungua Usanidi wa Mtandao ilivyofafanuliwa katika https://sites.google.com/a/chromium.org/dev/chromium-os/chromiumos-design-docs/open-network-configuration
Programu za Android zinaweza kutumia usanidi wa mtandao na vyeti vya CA vilivyowekwa kupitia sera hii, lakini hazina idhini ya kufikia chaguo za kuweka mipangilio.
Sera hii inabainisha orodha ya vyanzo (URL) au mitindo ya majina ya seva pangishi (kama vile "*.example.com") ambako vizuizi vya usalama kwenye vyanzo visivyo salama havitatumika.
Nia yake ni kuruhusu mashirika yaweke vyanzo vya kutoa idhini kwenye programu za zamani ambazo haziwezi kutumia TLS au kuweka seva ya majaribio kwa ajili ya usanidi wa tovuti za ndani, ili wasanidi programu waweze kujaribu vipengele vinavyohitaji muktadha salama bila kutumia TLS kwenye seva ya majaribio. Sera hii pia itazuia chanzo kisiwekewa lebo ya "Si Salama" katika sanduku kuu.
Hatua ya kuweka orodha za URL katika sera hii ina athari sawa na kuweka mipanglio ya ripoti ya mstari wa amri '--unsafely-treat-insecure-origin-as-secure' kwenye orodha iliyotenganishwa kwa koma ya URL sawa. Iwapo sera hii imewekwa, itabatilisha ripoti ya mstari wa amri.
Sera hii itabatilisha UnsafelyTreatInsecureOriginAsSecure, ikiwa imewekwa.
Kwa maelezo zaidi kuhusu miktadha salama, angalia https://www.w3.org/TR/secure-contexts/.
Sera hii inaeleza mipangilio inayotumika kuunda na kuthibitisha Msimbo wa Kufikia wa Mzazi.
|current_config| hutumika kila mara kuunda msimbo wa kufikia na inapaswa kutumika kuthibitisha msimbo wa kufikia iwapo tu hauwezi kuthibitishwa na |future_config|. |future_config| ni mpangilio wa msingi unaotumiwa kuthibitisha msimbo wa kufikia. |old_configs| inapaswa kutumika kuthibitisha msimbo wa kufikia iwapo tu hauwezi kuthibitishwa na |future_config| wala |current_config|.
Njia inayotarajiwa ya kutumia sera hii ni kuzungusha kwa hatua mpangilio wa msimbo wa kufikia. Mipangilio mipya huwekwa kwenye |future_config| kila mara na wakati huo huo thamani iliyopo huhamishiwa kwenye |current_config|. Thamani za awali za |current_config| zitahamishiwa kwenye |old_configs| na kuondolewa bada ya mzunguko kukamilika.
Sera hii inatumika kwa mtumiaji mtoto pekee. Sera hii inapowekwa, mipangilio ya Msimbo wa kufikia wa Mzazi inaweza kuthibitishwa kwenye kifaa kinachotumiwa na mtoto. Sera hii isipowekwa, hutaweza kuthibitisha Msimbo wa Kufikia wa Mzazi kwenye kifaa kinachotumiwa na mtoto.
Inaorodhesha vitambuaji vya programu Google Chrome OS huonyesha kama programu zilizobanwa katika upau wa kizinduzi.
Ikiwa sera hii itasanidiwa, uwekaji wa programu ni wa kudumu na hauwezi kubadilishwa na mtumiaji..
Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa, huenda mtumiaji akabadilisha orodha ya programu zilizobanwa katika kizinduzi.
Sera hii inaweza kutumika kubandika programu za Android.
Huruhusu sera zilizochaguliwa kuunganishwa wakati zinatoka kwenye vyanzo tofauti, vilivyo na upeo na viwango sawa.
Ikiwa sera ipo kwenye orodha, katika hali ambapo mgogoro umetokea kati ya vyanzo viwili, ikizingatiwa kwamba vina upeo na viwango sawa, thamani zitaunganishwa katika orodha mpya ya sera.
Ikiwa sera ipo kwenye orodha, katika hali ambapo mgogoro umetokea kati ya vyanzo viwili na pia kati ya upeo na/au viwango tofauti, sera inayopewa kipaumbele cha juu zaidi itatumiwa.
Ikiwa sera haipo kwenye orodha, katika hali ambapo mgogoro umetokea kati ya vyanzo, upeo na/au viwango, sera inayopewa kipaumbele cha juu zaidi itatumiwa.
Hubainisha kipindi kwa kipimo cha milisekunde ambapo huduma ya kudhibiti kifaa huulizwa maelezo ya sera ya mtumiaji
Kuweka sera hii hubatilisha thamani chaguomsingi ya saa 3. Thamani sahihi za sera hii ziko kuanzia 1800000 (dakika 30) hadi 86400000 (siku 1). Thamani zozote ambazo hazipo katika masafa haya zitawekwa katika mpaka husika. Ikiwa mfumo unatumia arifa za sera, ucheleweshwaji wa kuonyesha upya utawekwa kuwa saa 24 kwa sababu unatarajiwa kwamba arifa za sera zitalazimisha kuonyesha upya kiotomatiki wakati wowote ambao sera itabadilika.
Kuacha sera hii bila kuwekwa kutafanya Google Chrome itumie thamani chaguomsingi ya saa 3.
Kumbuka kwamba ikiwa mfumo huu unatumia arifa za sera, ucheleweshwaji wa kuonyesha upya utawekwa kuwa saa 24 (ukipuuza chaguomsingi zote na thamani ya sera hii) kwa sababu inatarajiwa kwamba arifa za sera zitalazimisha kuonyesha upya kiotomatiki wakati wowote ambao sera itabadilika, hivyo kuondoa haja ya kuonyesha upya mara kwa mara.
Hukuruhusu udhibiti uwasilishaji wa matangazo katika kichupo chote na/au maudhui ya elimu katika Google Chrome.
Iwapo hujaweka mipangilio ya sera hii au umeiwasha (iwe ndivyo), Google Chrome inaweza kuonyesha maudhui ya kichupo chote kwa watumiaji ili kutoa maelezo ya bidhaa.
Iwapo umezimwa (imewekwa kuwa sivyo), Google Chrome haitaonyesha maudhui ya kichupo chote kwa watumiaji ili kutoa maelezo ya bidhaa.
Mipangilio hii hudhibiti uwasilishaji wa kurasa za utangulizi ambazo husaidia watumiaji kuingia katika akaunti ya Google Chrome, kuichagua iwe kivinjari chaguomsingi au kuwafahamisha kuhusu vipengele vya bidhaa.
Kama sera hii imewashwa, mtumiaji ataulizwa mahali atakapohifadhi kila faili kabla ya kuipakua. Kama sera imezimwa, upakuaji utaanza moja kwa moja na mtumiaji hataulizwa mahali atakapohifadhi faili. Kama sera haijasanidiwa, mtumiaji ataweza kubadilisha mipangilio hii.
Huweka mipangilio ya seva mbadala ya Google Chrome. Mipangilio hii ya seva mbadala itapatikana kwa ajili ya programu za ARC pia.
Ukiwasha mipangilio hii, Google Chrome na programu za ARC hazitatumia chaguo zote zinazohusiana na seva mbadala zilizobainishwa kutoka mstari wa amri.
Sera hii isipowekwa itaruhusu watumiaji kuchagua mipangilio ya seva mbadala wenyewe.
Ikiwa sera ya ProxySettings imewekwa, itabatilisha sera nyingine zozote mahususi ProxyMode, ProxyPacUrl, ProxyServer, ProxyBypassList na ProxyServerMode.
Sehemu ya ProxyMode hukuruhusu kubainisha seva mbadala inayotumiwa na Google Chrome na huzuia watumiaji kubadilisha mipangilio ya seva mbadala.
Sehemu ya ProxyPacUrl ni URL kwenye ya faili ya .pac ya seva mbadala.
Sehemu ya ProxyServer ni URL ya seva mbadala.
Sehemu ya ProxyBypassList ni orodha ya seva pangishi mbadala ambazo Google Chrome haitatumia.
Sehemu ya ProxyServerMode haitumiki na 'ProxyMode' inatumika badala yake. Hukuruhusu kubainisha seva mbadala inayotumiwa na Google Chrome na huzuia watumiaji kubadilisha mipangilio ya seva mbadala.
Ukichagua thamani ya 'moja kwa moja' kuwa 'ProxyMode', seva mbadala haitawahi kutumiwa na sehemu zingine zote hazitazingatiwa.
Ukichagua thamani ya 'mfumo' kuwa 'ProxyMode', seva mbadala ya mfumo itatumiwa na sehemu nyingine zote hazitazingatiwa.
Ukichagua thamani ya 'tambua kiotomatiki' kuwa 'ProxyMode', sehemu nyingine zote hazitazingatiwa.
Ukichagua thamani ya 'fixed_server' kuwa 'ProxyMode', sehemu za 'ProxyServer' na 'ProxyBypassList' zitatumika.
Ukichagua thamani ya 'pac_script' kuwa 'ProxyMode', sehemu za 'ProxyPacUrl' na 'ProxyBypassList' zitatumika.
Chaguo za kuweka mipangilio ya seva mbadala zinazofuata pekee hupatikana kwa programu za Android. Programu za Android zinaweza kuchagua kutumia seva mbadala. Huwezi kuzilazimisha zitumie seva mbadala.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo au kutowekwa, matumizi ya itifaki ya QUIC katika Google Chrome yanaruhusiwa. Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo matumizi ya itifaki ya QUIC hayaruhusiwi.
Iwaarifu watumiaji kwamba ni sharti Google Chrome ifunguliwe upya au ni sharti wazime kisha wawashe Google Chrome OS ili wakamilishe kuweka sasisho.
Mipanglilio hii ya sera huwasha arifa ili kumwarifu mtumiaji kwamba anashauriwa au anatakiwa afungue upya kivinjari au azime kisha awashe kifaa. Kama sera hii haijawekwa, Google Chrome itamwashiria mtumiai kwamba anahitaji kufungua kivinjari upya kupitia mabadiliko machache kwenye menyu yake ilhali Google Chrome OS itaashiria hali hii kupitia arifa kwenye ubao wa aikoni. Kama imewekwa kuwa 'Inapendekezwa', onyo linalojirudia litaonyeshwa kwa mtumiaji kwamba anashauriwa afungue upya. Mtumiaji anaweza kuondoa onyo hili kwa kuahirisha mchakato wa kufungua upya. Kama imewekwa kuwa 'Inahitajika' onyo linalojirudia litaonyeshwa kwa mtumiaji kuashiria kwamba kivinjari kitafunguliwa upya kwa lazima baada ya kipindi cha onyo kuisha. Kipindi chaguomsingi ni siku saba kwa Google Chrome na siku nne kwa Google Chrome OS, na inaweza kuwekewa mipangilio kupitia ya sera ya RelaunchNotificationPeriod.
Kipindi cha mtumiaji kitarejeshwa baada ya kufunguliwa au kuanzishwa upya.
Hukuruhusu uweke kipindi katika milisekunde, ambapo watumiaji wanaarifiwa kwamba Google Chrome lazima ifunguliwe upya au kifaa cha Google Chrome OS lazima kizimwe kisha kiwashwe ili kukamilisha kuweka sasisho.
Katika kipindi hiki, mtumiaji ataarifiwa mara kwa mara kuhusu haja ya kusasisha. Kwa vifaa vya Google Chrome OS, arifa ya itakayokutaka uzime kisha uwashe kifaa itaonekana katika ubao wa aikoni wakati sasisho litatambuliwa. Kwa vivinjari vya Google Chrome, mabadiliko ya menyu ya programu ya kuashiria kuwa unahitaji kufungua programu upya yanahitajika baada ya thuluthi ya kipindi cha arifa kuisha. Rangi ya arifa hizi itabadilika baada ya thuluthi mbili za kipindi cha kutoa arifa kuisha na itabadilika tena kipindi kamili cha arifa kitakapokwisha. Arifa za ziada zitakazowashwa na sera ya RelaunchNotification zitafuata ratiba ii hii.
Kama hujaweka kipindi, kipindi chaguomsingi cha milisekunde 345600000 (siku nne) itatumika kwa vifaa vya Google Chrome OS na milisekunde 604800000 (wiki moja) itatumika kwa Google Chrome.
Maelezo kuhusu matumizi ya programu za Linux yanatumwa kwenye seva.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo au isipowekwa, hakuna maelezo ya matumizi yanayotumwa. Ikiwekwa kuwa ndivyo, maelezo ya matumizi hutumwa.
Sera hii inatumika tu iwapo programu ya Linux imewashwa.
Mipangilio hii inapowashwa, Google Chrome itakagua ubatilishaji wa vyeti vya seva ambavyo vinathibitisha na vimetiwa sahihi na vyeti vya CA vilivyosakinishwa kwa karibu wakati wote.
Ikiwa Google Chrome haiwezi kupata maelezo ya hali ya ubatilishaji, vyeti kama hivyo vitachukuliwa kuwa vimebatilishwa ('hard-fail').
Sera hii isipowekwa, au ikiwekwa kuwa sivyo, basi Google Chrome itatumia mipangilio iliyopo ya kukagua ubatilishaji wa mtandaoni.
Inajumuisha orodha ya ruwaza ambazo zinatumika kudhibiti kuonekana kwa akaunti katika Google Chrome.
Kila akaunti ya Google kwenye kifaa italinganishwa na ruwaza iliyohifadhiwa katika sera hii ili kubaini kuonekana kwa akaunti katika Google Chrome. Akaunti itaonekana ikiwa jina lake linalingana na ruwaza yoyote kwenye orodha. Vinginevyo, akaunti itafichwa.
Tumia herufi wakilishi ya '*' ili ulinganishe sufuri na vibadala vingine vya herufi. Herufi hiyo maalum ni '\', hivyo basi, ili ulinganishe herufi halisi za '*' au '\', weka '\' mbele yazo.
Kama sera hii haijawekwa, akaunti zote za Google kwenye kifaa zitaonekana katika Google Chrome.
Inajumuisha kilinganishi ambacho kinatumiwa kubainisha aina za akaunti za Google ambazo zinaweza kuwekwa kuwa kivinjari cha akaunti ya msingi katika Google Chrome (yaani akaunti ambayo inachaguliwa wakati wa mchakato wa kuchagua kutekeleza Usawazishaji).
Hitilafu inayofaa itaonyeshwa iwapo mtumiaji atajaribu kuweka akaunti ya msingi ya kivinjari pamoja na jina la mtumiaji ambalo halilingani na mchoro huu.
Iwapo sera hii haijawekwa au haina kitu, inaamanisha kuwa mtumiaji anaweza kuweka akaunti yoyote ya Google iwe akaunti ya msingi ya kivinjari katika Google Chrome.
Huweka mipangilio ya saraka ambayo Google Chrome itatumia kuhifadhi nakala ya kutumia mitandao ya ng'ambo katika wasifu.
Ukiweka mipangilio hii, Google Chrome itatumia saraka unayoweka ili kuhifadhi nakala ya kutumia mitandao ya ng'ambo katika wasifu ikiwa sera ya RoamingProfileSupportEnabled imewashwa. Ikiwa sera ya RoamingProfileSupportEnabled imezimwa au imeachwa bila kuwekwa, thamani iliyohifadhiwa katika sera hii haitumiki.
Angalia https://www.chromium.org/administrators/policy-list-3/user-data-directory-variables ili uone orodha ya vipengee vinavyoweza kutumika.
Sera hii ikiachwa bila kuwekwa, njia chaguomsingi ya wasifu wa kutumia mitandao ya ng'ambo itatumika.
Ukiwasha mipangilio hii, mipangilio iliyohifadhiwa kwenye maelezo ya Google Chrome kama vile alamisho, data ya kujaza kiotomatiki, manenosiri, n.k. pia itahifadhiwa kwenye faili iliyohifadhiwa katika folda ya wasifu wa mtumiaji asiye na mahali palipobainishwa au kwenye mahali palipobainishwa na Msimamizi kupitia sera ya RoamingProfileLocation. Ukiwasha sera hii, usawazishaji kwenye wingu utazimwa.
Sera hii ikizimwa au kuachwa bila kuwekwa, wasifu wa karibu wa kawaida pekee ndio utakaotumiwa.
Sera ya SyncDisabled huzima usawazishaji wote wa data, hivyo kubatilisha RoamingProfileSupportEnabled.
Ikiwa utaweka mipangilio hii, maudhui yote yaliyopachikwa katika Flash kwenye tovuti ambazo zimewekwa kuruhusu Flash katika mipangilio ya maudhui -- na mtumiaji au sera ya biashara -- itatekelezwa, ikijumuisha maudhui kutoka vyanzo vingine au maudhui machache.
Ili kudhibiti aina ya tovuti ambazo zinakubaliwa kutumia Flash, angalia sera za "DefaultPluginsSetting", "PluginsAllowedForUrls", na "PluginsBlockedForUrls".
Ikiwa mipangilio hii imezimwa au haijawekwa, maudhui ya Flash kutoka vyanzo vingine au maudhui machache yanaweza kuzuiwa.
Unapoingia katika akaunti, Google Chrome OS inaweza kuthibitisha dhidi ya seva (mtandaoni) au kutumia nenosiri lililowekwa katika akiba (nje ya mtandao).
Wakati sera hii imewekwa kuwa thamani ya -1, mtumiaji anaweza kuthibitisha nje ya mtandao bila kikomo. Wakati sera hii inawekwa kuwa thamani yoyote nyingine, inabainisha urefu wa muda tangu uthibitishaji wa mwisho wa mtandaoni kisha baadaye mtumiaji atapaswa kutumia uthibitishaji wa mtandaoni tena.
Kuacha sera hii bila kuiweka kutafanya Google Chrome OS itumie wakati chaguomsingi wa kipindi cha juu zaidi cha siku 14 kisha baadaye mtumiaji atapaswa kutumia uthibitishaji wa mtandaoni tena.
Sera hii huathiri watumiaji waliothibitisha kwa kutumia SAML pekee.
Thamani ya sera lazima ibainishwe katika sekunde.
Chrome huonyesha ukurasa wa onyo watumiaji wanapoenda kwenye tovuti ambazo zina hitilafu za SSL. Kwa chaguomsingi au sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, watumiaji wanaruhusiwa kubofya kwenye kurasa hizi za onyo. Kuweka sera kuwa sivyo hakuwaruhusu watumiaji kubofya ukurasa wowote wa onyo.
Ikiwa hujaweka mipangilio ya sera hii inamaanisha kuwa Google Chrome itatumia toleo la chini zaidi katika mipangilio chaguomsingi ambalo ni TLS 1.0.
Vinginevyo, inaweza kuwekwa kuwa mojawapo ya thamani zifuatazo: "tls1", "tls1.1" au "tls1.2". Ikiwekwa, Google Chrome itatumia matoleo ya SSL/TLS yaliyo chini ya toleo lililobainishwa. Haitazingatia thamani ambayo haitambuliki.
Hutambua ikiwa Google Chrome inaweza kuruhusu upakuaji bila ukaguzi wa kipengele cha Kuvinjari Salama wakati unatoka chanzo kinachoaminika.
Sera ikiwekwa kuwa Sivyo, faili zilizopakuliwa hazitatumwa ili zikaguliwe na kipengele cha Kuvinjari Salama wakati zinatoka chanzo kinachoaminika.
Sera isipowekwa (au kuwekwa kuwa Ndivyo), faili zilizopakuliwa zinatumwa ili zikaguliwe na kipengele cha Kuvinjari Salama wakati zinatoka chanzo kinachoaminika.
Kumbuka kwamba vizuizi hivi vinatumika kwenye vipakuliwa vinavyoanzishwa kutoka maudhui ya tovuti na pia chaguo la menyu ya maudhui la 'kiungo cha kupakua...' Vizuizi hivi havitumiki kwenye sehemu ya hifadhi au kupakua ya ukurasa unaonyeshwa kwa sasa wala kutumika katika kuhifadhi kama PDF kutoka chaguo za kuchapisha.
Sera hii inapatikana kwenye matukio ya Windows ambayo yameunganishwa kwenye kikoa cha Microsoft® Active Directory®. au matukio ya Windows 10 Pro au Enterprise yaliyojumuishwa katika usimamizi wa kifaa.
Sera hii hudhibiti utekelezaji wa kichujio cha URL ya SafeSites. Kichujio hiki hutumia API ya Utafutaji Salama wa Google ili kuainisha URL kuwa na maudhui ya ponografia au kukosa maudhui hayo.
Iwapo mipangilio ya sera hii haijawekwa au umeweka "Isichuje tovuti zilizo na maudhui ya watu wazima", tovuti hazitafutwa.
Iwapo sera hii imewekwa kuwa "Ichuje tovuti maarufu zinazoonyesha maudhui ya watu wazima", tovuti zinazoainishwa kuwa za ponografia zitachujwa.
Huzima kipengee cha kuhifadhi historia ya kivinjari katika Google Chrome na kuwazuia watumiaji kubadilisha mipangilio hii.
Mipangilio hii ikiwashwa, historia ya kuvinjari haihifadhiwi. Mipangilio hii pia huzima kipengee cha kusawazisha kichupo.
Sera hii ikizimwa au isipowekwa, historia ya kuvinjari huhifadhiwa.
Huelekeza Google Chrome OS kutumia mipangilio ya kiweka ratiba ya majukumu iliyobainishwa kwa jina mahususi.
Sera hii inaweza kuwekwa kuwa "usitumie" na "tumia", hali ambazo huchagua mipangilio ya kiweka ratiba ya majukumu ambayo imewashwa kwa ajili ya uthabiti na upeo wa juu wa utekelezaji, mtawalia.
Sera hii isipowekwa, mtumiaji anaweza kuweka chaguo lake.
Inawezesha mapendekezo ya utafutaji katika sanduKuu ya Google Chrome na huzuia watumiaji kubadilisha mpangilio huu.
Ukiwasha mpangilio huu, mapendekezo ya utafutaji yanatumiwa.
Ukifunga mpangilio huu, mapendekezo ya utafutaji hayatumiwi kamwe.
Ukiwasha au kufunga mpangilio huu, watumiaji hawawezi kubadilisha au kufuta mpangilio huu katika Google Chrome.
Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa, hii itawezeshwa lakini mtumiaji ataweza kuibadilisha.
Mipangilio hii huruhusu watumiaji kubadili kati ya akaunti za Google katika eneo la maudhui ya dirisha la kivinjari baada ya kuingia katika akaunti wakitumia kifaa chao cha Google Chrome OS.
Kama sera imewekwa kuwa sivyo, watumiaji hawataruhusiwa kuingia katika akaunti tofauti kwenye eneo la maudhui ya kivinjari kisicho na hali fiche.
Kama sera hii haijawekwa au imewekwa kuwa ndivyo, hali chaguomsingi itatumika: utaruhusiwa kuingia katika akaunti tofauti kwenye eneo la maudhui ya kivinjari, isipokuwa katika akaunti za mtoto ambapo itazuiwa katika eneo la maudhui ya kivinjari kisicho na hali fiche.
Katika hali ambapo kuingia katika akaunti tofauti hakuruhusiwa kupitia Hali Fiche, zingatia kuzuia hali hiyo ukitumia sera ya IncognitoModeAvailability.
Kumbuka kwamba watumiaji wataweza kufikia huduma za Google katika hali isiyothibitishwa kwa kuzuia vidakuzi vyao.
Hubainisha URL na vikoa ambavyo hakuna kidokezo kitakachoonyeshwa wakati vyeti vya ufikiaji uliothibitishwa vinaombwa kutoka Funguo za Usalama. Vile vile, ishara itatumwa kwa Funguo za Usalama inayoonyesha ufikiaji uliothibitishwa wa kibinafsi ambao unaweza kutumiwa. Bila hii, watumiaji watadokezewa katika Chrome 65+ wakati tovuti zinaomba ufikiaji uliothibitishwa wa Funguo za Usalama.
URL (kama vile https://example.com/some/path) zitalingana kama U2F appIDs pekee. Vikoa (kama vile example.com) vinalingana kama Vitambulisho vya webauthn RP pekee. Ili kushughulikia API zote mbili za U2F na webauthn za tovuti fulani iliyotolewa, ni sharti URL zote mbili za appID na kikoa ziorodheshwe.
Sera hii ikiwekwa, hubainisha kipindi cha muda ambacho huchukuliwa kisha mtumiaji anaondolewa katika akaunti kiotomatiki; hali inayosimamisha kipindi. Mtumiaji huarifiwa kuhusu muda unaosalia katika kipima muda kinachoonyeshwa kwenye ubao wa aikoni.
Sera hii isipowekwa, muda wa kipindi haupimwi.
Ukiweka sera hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuibatilisha.
Thamani ya sera sharti ibainishwe katika milisekunde. Thamani huwekwa pamoja katika masafa ya sekunde 30 hadi saa 24.
Huweka lugha moja au zaidi zilizopendekezwa kwa kipindi kinachodhibitiwa, hivyo kuwaruhusu watumiaji kuchagua kwa urahisi mojawapo ya lugha hizi.
Mtumiaji anaweza kuchagua lugha na mpangilio wa kibodi kabla ya kuanza kipindi kinachodhibitiwa. Kwa chaguomsingi, lugha zote zinazotumika kwenye Google Chrome OS zimeorodheshwa kwa mpangilio wa alfabeti. Unaweza kutumia sera hii kuhamishia seti ya lugha zilizopendekezwa upande wa juu wa orodha.
Sera hii isipowekwa, kiolesura cha lugha ya sasa kitachaguliwa awali.
Sera hii ikiwekwa, lugha zilizopendekezwa zitahamishiwa upande wa juu wa orodha na zitatenganishwa na lugha nyingine zote. Lugha zinazopendekezwa zitaorodheshwa katika mpangilio ambao zinaonekana katika sera. Lugha ya kwanza iliyopendekezwa itachaguliwa awali.
Ikiwa kuna lugha zaidi ya moja iliyopendekezwa, inachukuliwa kwamba watumiaji wangependa kuchagua kati ya lugha hizi. Uteuzi wa lugha na mpangilio wa kibodi utatolewa kwa kuangaziwa wakati wa kuanza kipindi kinachodhibitiwa. Vinginevyo, inachukuliwa kwamba watumiaji wengi wangependa kutumia lugha hizi zilizochaguliwa awali. Uteuzi wa lugha na mpangilio wa kibodi hautatolewa kwa kuangaziwa wakati wa kuanza kipindi kinachodhibitiwa.
Sera hii inapowekwa na kipengee cha kuingia katika akaunti kiotomatiki kuwashwa (angalia sera za |DeviceLocalAccountAutoLoginId| na |DeviceLocalAccountAutoLoginDelay|), kipindi kinachodhibitiwa kilichoanzishwa kiotomatiki kitatumia lugha ya kwanza iliyopendekezwa na mpangilio wa kibodi maarufu sana unaolingana na lugha hii.
Kila wakati, mpangilio wa kibodi uliochaguliwa awali utakuwa mpangilio maarufu unaolingana na lugha iliyochaguliwa awali.
Sera hii inaweza tu kuwekwa kama ilivyopendekezwa. Unaweza kutumia sera hii kuhamishia seti ya lugha zilizopendekezwa upande wa juu lakini watumiaji wanaruhusiwa kuchagua lugha inayotumika kwenye Google Chrome OS kwa kipindi chao wakati wowote.
Dhibiti kujificha kiotomatiki kwa rafu ya Google Chrome OS.
Iwapo sera hii itawekwa kuwa 'IjificheYenyeweKilaWakati', rafu itajificha kiotomatiki kila wakati.
Iwapo sera hii itawekwa kuwa 'IsiwahiKujifichaYenyewe', rafu haitawahi kujificha kiotomatiki.
Ukiweka sera hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuifuta.
Iwapo sera itaachwa bila kuwekwa, watumiaji wanaweza kuamua iwapo rafu itajificha kiotomatiki.
Huwasha au kuzima njia ya mkato ya programu katika sehemu ya alamisho.
Ikiwa sera hii haitawekwa basi mtumiaji anaweza kuamua kuonyesha au kuficha njia ya mkato ya programu kutoka kwenye menyu ya muktadha ya sehemu ya alamisho.
Ikiwa sera hii itasanidiwa basi mtumiaji hawezi kuibadilisha, na njia ya mkato ya programu kuonyeshwa au kutoonyeshwa kila mara.
Sera ikiwashwa, kitufe kikubwa chekundu cha kuondoka katika akaunti kitaonyeshwa katika ubao wa aikoni kipindi kinapoendelea na ikiwa skrini haijafungwa.
Sera ikizimwa au isipobainishwa, haitaonyesha kitufe kikubwa chekundu cha kuondoka katika akaunti kwenye ubao wa aikoni.
Ruhusu utumiaji wa Kubadilisha HTTP Iliyoambatishwa Cheti (SXG).
Ikiwa sera hii haijawekwa au imewekwa kuwa 'Imewashwa', Google Chrome itakubali maudhui ya wavuti yanayotolewa kama Kubadilisha HTTP Iliyoambatishwa Cheti.
Sera hii ikiwekwa kuwa 'Imezimwa', Kubadilisha HTTP Iliyoambatishwa Cheti hakuwezi kupakiwa.
Sera hii imeacha kuendesha huduma, badala yake jaribu kutumia kipengele cha BrowserSignin.
Humruhusu mtumiaji kuingia katika Google Chrome.
Ukiweka sera hii, unaweza kuweka mipangilio iwapo mtumiaji anaruhusiwa kuingia katika Google Chrome. Kuweka sera hii kuwa 'Sivyo' kutazuia programu na viendelezi ambavyo hutumia API ya chrome.identity visifanye kazi, kwa hivyo unaweza kutumia kipengele cha SyncDisabled badala yake.
Huenda utataka kuangalia mipangilio ya sera ya IsolateOrigins ili upate hali bora kati ya hizi mbili, utengaji na athari ndogo kwa watumiaji, kwa kutumia IsolateOrigins katika orodha ya tovuti unazotaka kutenga. Mipangilio hii, SitePerProcess, inatenga tovuti zote. Iwapo sera imewashwa, kila tovuti itatumia mchakato wake. Ukizima mipangilio hii, vipengele vyote viwili vya IsolateOrigins na SitePerProcess vitazimwa. Bado watumiaji wataweza kuwasha SitePerProcess wenyewe, kupitia ripoti za mstari wa amri. Iwapo hujaweka mipangilio ya sera, mtumiaji ataweza kubadilisha mipangilio hii. Kwenye Google Chrome OS, tunapendekeza uweke pia sera ya kifaa ya DeviceLoginScreenSitePerProcess iwe katika thamani ile ile. Ikiwa thamani hazitalingana, huenda ikachelewesha shughuli ya kuweka kipindi cha mtumiaji wakati thamani iliyobainishwa na sera ya mtumiaji inatumika.
KUMBUKA: Sera hii haitumiki kwenye Android. Ili uwashe SitePerProcess kwenye Android, tumia mipangilio ya sera ya SitePerProcessAndroid.
Tunapendekeza uangalie mipangilio ya sera ya IsolateOriginsAndroid ili upate hali iliyo bora kati ya mbili zilizopo, utengaji na athari ndogo kwa watumiaji kwa kutumia IsolateOrigins kwenye orodha ya tovuti ambazo ungependa kutenga. Mipangilio hii, SitePerProcess, hutenga tovuti zote. Ikiwa sera imewashwa, kila tovuti itatumia mchakato wake. Ikiwa sera imezimwa, hamna dhana ya Utengaji wa Tovuti itakayotumika kwa njia dhahiri na majaribio ya sehemu za IsolateOrigins na SitePerProcess yatazimwa. Bado watumiaji wataweza kuwasha SitePerProcess wenyewe. Ikiwa sera haijawekwa, mtumiaji ataweza kubadilisha mipangilio hii.
KUMBUKA: Kwenye Android, Utengaji wa Tovuti bado unafanyiwa majaribio. Matumizi yataboreshwa baada ya muda lakini kwa sasa yanaweza kusababisha matatizo ya utendaji.
KUMBUKA: Sera hii inatumika tu katika Chrome kwenye vifaa vya Android vyenye zaidi ya GB 1 ya RAM. Ili kutumia sera kwenye mifumo isiyo ya Android, tumia SitePerProcess.
Iwapo mipangilio hii imewashwa, watumiaji wataruhusiwa kuingia katika akaunti zao wakitumia Smart Lock. Hali hii inaruhusu vitendo zaidi kuliko utendaji wa kawaida wa Smart Lock ambao unaruhusu tu watumiaji kufungua skrini zao.
Iwapo mipangilio hii imezimwa, watumiaji hawataruhusiwa kutumia njia ya kuingia katika akaunti kupitia Smart Lock.
Iwapo sera hii haijawekwa, mipangilio chaguomsingi haitaruhusiwa kwa watumiaji wanaodhibitiwa na biashara na itaruhusiwa kwa watumiaji wasiodhibitiwa.
Kama mipangilio hii imewashwa, watumiaji wataruhusiwa kuweka mipangilio kwenye vifaa vyao ili wasawazishe ujumbe wa SMS kati ya simu na Chromebook zao. Kumbuka kwamba ikiwa sera hii itaruhusiwa, ni sharti watumiaji wajijumuishe waziwazi kwenye kipengele hiki kwa kukamilisha utaratibu wa kuweka mipangilio. Pindi utaratibu wa kuweka mipangilio utakamilika, watumiaji wataweza kutuma na kupokea SMS kwenye Chromebook zao.
Ikiwa mipangilio hii imezimwa, watumiaji hawataruhusiwa kuweka mipangilio ya kusawazisha SMS.
Ikiwa sera hii haitawekwa, hali chaguomsingi haitaruhusiwa kwa watumiaji wanaosimamiwa lakini itaruhusiwa kwa watumiaji wasiosimamiwa.
Google Chrome inaweza kutumia huduma ya wavuti ya Google ili kusaidia kutatua hitilafu za tahajia. Ikiwa mpangilio huu umewezeshwa, basi huduma hii inatumika kila mara. Ikiwa mpangilio huu unalemazwa, basi huduma hii haitumiki kamwe.
Ukaguzi tahajia bado unaweza kutekelezwa kwa kutumia kamusi iliyopakuliwa; sera hii inadhibiti tu matumizi ya huduma ya mtandaoni.
Ikiwa mpangilio huu haujasanidiwa basi watumiaji wanaweza kuchagua iwapo huduma ya ukaguzi tahajia unapaswa kutumika au la.
Kama sera hii haijawekwa au imewashwa, mtumiaji anaruhusiwa kutumia kikagua tahajia.
Kama Sera hii imezimwa, mtumiaji haruhusiwi kutumia kikagua tahajia. Sera za SpellcheckLanguage na SpellcheckLanguageBlacklist pia hazitatumiwa wakati sera hii inapozimwa.
Hulazimisha kuwasha sera ya kikagua tahajia katika lugha Lugha ambazo hazijatambuliwa katika orodha hii hazitazingatiwa.
Ukiwasha sera hii, kikagua tahajia kitawashwa kwa ajili ya lugha ulizobainisha, pamoja na lugha ambako mtumiaji amewasha kikagua tahajia.
Usipoweka sera hii, au ukiizima, hakutakuwa na mabadiliko kwenye mapendeleo ya mtumiaji kwenye kikagua tahajia.
Ikiwa sera ya SpellcheckEnabled imezimwa, sera hii haina athari yoyote.
Ikiwa lugha imejumuishwa katika sera hii na sera ya SpellcheckLanguageBlacklist, sera hii inapewa kipaumbele na lugha inayotumia kikagua tahajia huwashwa.
Lugha ambazo zinatumika kwa sasa: Kiafrikana, Kibulgaria, Kikatalani, Kicheki, Kiholanzi, Kigiriki, Kiingereza cha Australia, Kiingereza cha Kanada, Kiingereza cha Uingereza, Kiingereza cha Marekani, Kihispania, Kihispania cha Marekani Kusini, Kihispania cha Argentina, Kihispania cha Uhispania, Kihispania cha Meksiko, Kihispania cha Marekani, Kiestonia, Kiajemi, Kifarosi, Kifaransa, Kiyahudi, Kihindi, Kikoreshia, Kihungari, Kiindonesia, Kiitaliano, Kikorea, Kiluksembagi, Kiflemil, Kibokmali cha Norwe, Kiholanzi, Kipolandi, Kireno cha Brazil, Kireno cha Ulaya, Kiromania, Kirusi, Kislovakia, Kislovenia, Kialbania, Kiserbia, Kiswidi, Kitamili, Kitajiki, Kiturukiri, Kiukreni, Kivietinamu.
Hulazimisha kuzima kikagua tahajia katika lugha. Lugha ambazo hazijatambuliwa katika orodha hii hazitazingatiwa.
Ukiwasha sera hii, kikagua tahajia kitazimwa kwa lugha ulizobainisha. Mtumiaji bado anaweza kuwasha au kuzima kikagua tahajia kwa lugha ambazo hazipo kwenye orodha.
Usipoweka sera hii, au ukiizima, hakutakuwa na mabadiliko kwenye mapendeleo ya mtumiaji kwenye kikagua tahajia.
Ikiwa sera ya SpellcheckEnabled imezimwa, sera hii haina athari yoyote.
Ikiwa lugha imejumuishwa katika sera zote mbili na sera ya SpellcheckLanguage, sera ya SpellcheckLanguage inapewa kipaumbele na kikagua tahajia cha lugha kitawashwa.
Lugha ambazo zinatumika kwa sasa: Kiafrikana, Kibulgaria, Kikatalani, Kicheki, Kiholanzi, Kigiriki, Kiingereza cha Australia, Kiingereza cha Kanada, Kiingereza cha Uingereza, Kiingereza cha Marekani, Kihispania, Kihispania cha Marekani Kusini, Kihispania cha Argentina, Kihispania cha Uhispania, Kihispania cha Meksiko, Kihispania cha Marekani, Kiestonia, Kiajemi, Kifarosi, Kifaransa, Kiyahudi, Kihindi, Kikoreshia, Kihungari, Kiindonesia, Kiitaliano, Kikorea, Kiluksembagi, Kiflemil, Kibokmali cha Norwe, Kiholanzi, Kipolandi, Kireno cha Brazil, Kireno cha Ulaya, Kiromania, Kirusi, Kislovakia, Kislovenia, Kialbania, Kiserbia, Kiswidi, Kitamili, Kitajiki, Kiturukiri, Kiukreni, Kivietinamu.
Hukandamiza onyo linaloonekana Google Chrome inapofanya kazi kwenye kompyuta au mfumo wa uendeshaji ambao hautumiki tena.
Huzima usawazishaji data kwenye Google Chrome kwa kutumia huduma za usawazishaji zilizopangishwa kwenye Google na kuzuia watumiaji kuibadilisha mipangilio hii.
Ukiiwasha mipangilio hii, watumiaji hawataweza kubadilisha wala kubatilisha mipangilio hii kwenye Google Chrome.
Usipoiweka sera hii, mtumiaji atachagua kutumia au kutotumia kipengele cha Usawazishaji wa Google.
Ili kuzima kabisa kipengele cha Usawazishaji wa Google, inapendekezwa uzime huduma ya Usawazishaji wa Google kwenye Google Admin console.
Hupaswi kuiwasha sera hii wakati ambapo sera ya RoamingProfileSupportEnabled imewashwa kwa sababu kipengele hicho kinashiriki utendaji wa huduma sawa. Katika hali kama hii, usawazishaji wa Google utazimwa kabisa.
Kuzima kipengele cha Usawazishaji wa Google kutasababisha kipengele cha Hifadhi Rudufu ya Android na Kurejesha kisifanye kazi vizuri.
Kipengele cha muda wa matumizi ya kichupo hudhibiti CPU na baadaye hifadhi inayohusishwa na vichupo vilivyopo ambavyo havijatumika katika kipindi kirefu, kwa kuanza na kuvizuia, kisha kuvibana na baadaye kuvitupa.
Iwapo sera imewekwa kuwa sivyo, inamaanisha kuwa kipengele cha muda wa matumizi ya kichupo kitazimwa na vichupo vyote vitaendelea kutumika kama kawaida.
Iwapo sera imewekwa kuwa ndivyo au haijabainishwa, inamaanisha kuwa kipengele cha muda wa matumizi ya kichupo kitawashwa.
Ikiwekwa kuwa sivyo, kitufe cha 'Tamatisha mchakato' kitazimwa katika Kidhibiti cha Shughuli kwenye Chrome.
Ikiwekwa kuwa ndivyo au mipangilio isiwekwe, mtumiaji anaweza kutamatisha shughuli katika Kidhibiti cha Shughuli kwenye Chrome.
Huweka Sheria na Masharti ambayo lazima mtumiaji akubali kabla ya kuanzisha kipindi cha akaunti ya kifaa cha karibu nawe.
Sera hii ikiwekwa, Google Chrome OS itapakua Sheria na Masharti na kuyawasilisha kwa mtumiaji kipindi cha akaunti cha kifaa cha karibu nawe kianzapo. mtumiaji ataruhusiwa tu katika kipindi baada ya kukubali Sheria na Masharti.
Iwapo sera hii haitawekwa, sheria na masharti hayataonyeshwa.
Sera itawekwa kwenye URL ambapo Google Chrome OS inaweza kupakua Sheria na masharti. Lazima Sheria na Masharti yawe maandishi matupu, yawe kama maandishi ya kuandika/matupu ya MIME. Markup hairuhusiwi.
Kama sera imewekwa kuwa sivyo, programu ya kampuni nyingine itaruhusiwa kuingiza msimbo inayoweza kutekelezwa katika michakato ya Chrome. Kama sera haijawekwa au imewekwa kuwa ndivyo basi programu ya kampuni nyingine itazuiwa kuingiza msimbo unaoweza kutekelezwa katika michakato ya chrome.
Sera hii inasanidi kuwasha kibodi pepe kama kifaa cha kuingiza data kwenye ChromeOS. Watumiaji hawawezi kuibatilisha sera hii.
Ikiwa sera hii itawekwa kuwa ndivyo, kibodi pepe ya skrini itawashwa wakati wowote.
Ikiwekwa kuwa sivyo, kibodi pepe ya skrini itazimwa wakati wowote.
Ukiweka sera hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuibatilisha. Hata hivyo, watumiaji bado wataweza kuwasha/kuzima kibodi pepe ya skrini ya ufikiaji inayopewa kipaumbele dhidi ya kibodi pepe inayodhibitiwa na sera hii. Angalia sera ya |VirtualKeyboardEnabled| kwa kudhibiti kibodi pepe ya skrini ya ufikiaji.
Ikiwa sera hii itaachwa bila kuwekwa, kibodi ya skrini inazimwa mwanzoni lakini inaweza kuwashwa na mtumiaji wakati wowote. Kanuni za ugunduaji zinaweza pia kutumiwa kuamua wakati wa kuonyesha kibodi.
Inaruhusu huduma iliyojumuishwa ya Google Tafsiri kwenye Google Chrome.
Ukiwasha mipangilio hii, Google Chrome itamwonyesha mtumiaji utendaji wa tafsiri kwa kuonyesha upauzana uliojumuishwa wa kutafsiri (panapohitajika) na chaguo la tafsiri kwenye menyu ya kubofya kulia.
Ukizima mipangilio hii, vipengele vyote vya kutafsiri vilivyojumuishwa vitazima.
Ukizima au kuwasha mipangilio hii, watumiaji hawataweza kubadilisha au kufuta mipangilio hii katika Google Chrome.
Kama mipangilio hii haitawekwa, mtumiaji anaweza kuamua kutumia kipengele hiki au asikitumie.
Sera hii humzuia mtumiaji kupakia kurasa za wavuti kutoka kwenye URL zisizoidhinishwa. Orodha ya URL zisizoidhinishwa hutoa orodha ya ruwaza za URL ambazo hubainisha URL zitakazoondolewa kwenye orodha ya URL zilizoidhinishwa.
Lazima URL iundwe kulingana na https://www.chromium.org/administrators/url-blacklist-filter-format.
Vipengee visivyofuata kanuni vinaweza kufafanuliwa katika sera ya URL zilizoidhinishwa. Sera hizi hazizidi vipengee 1000; vipengee vitakavyofuata vitapuuzwa.
Kumbuka kwamba haipendekezwi kuzuia URL za 'chrome://*' za ndani kwa sababu hatua hii inaweza kusababisha hitilafu zisizotarajiwa.
Kuanzia M73 unaweza kuzuia URL za 'javascript://*'. Hata hivyo, sera inaathiri tu JavaScript iliyoandikwa katika sehemu ya anwani (au kwa mfano, kijialamisho). Kumbuka kwamba URL za JavaScript za ndani ya ukurasa, mradi ni data iliyopakiwa kwa upekee, hazitumii sera hii. Kwa mfano ukizuia ukurasa wa 'example.com/abc', 'example.com' watumiaji bado wataweza kupakia 'example.com/abc' kupitia XMLHTTPRequest.
Sera hii isipowekwa, hakuna URL itakayoondolewa kwenye orodha ya URL zisizoidhinishwa katika kivinjari.
Programu za Android zinaweza kuchagua kwa hiari kutii orodha hii. Huwezi kuzilazimisha kuitii.
Inaruhusu ufikivu kwenye URL zilizoorodheshwa, kama vizuizi katika orodha ya kuondoa idhini ya URL.
Angalia maelezo ya sera ya uzuiaji wa URL ya umbizo la maingizo ya orodha hii.
Sera hii inaweza kutumiwa kufungua vizuizi ili kuondoa vikwazo kwenye orodha zilizozuiwa. Kwa mfano, '*' inaweza kuondolewa idhini ili kuzuia maombi yote, na sera hii inaweza kutumiwa kuruhusu ufikiaji katika orodha chache za URL. Inaweza kutumiwa ili kufungua vizuizi katika mipango fulani, vikoa vidogo, poti, au vijia bainifu.
Kichujio muhimu zaidi kitathibitisha iwapo URL imezuiwa au kuruhusiwa. Orodha ya kuidhinisha inapewa kipau mbele kuliko orodha ya kuondoa idhini.
Sera hii imetengewa tu maingizo 1000; maingizo yanayofuata yatapuuzwa.
Iwapo sera hii haijawekwa hakutakuwa na ruhusa katika orodha ya kuondoa idhini kutoka sera ya 'URLBlacklist'.
Programu za Android zinaweza kuchagua kwa hiari kutii orodha hii. Huwezi kuzilazimisha kuitii.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo, Eneo-kazi Lililounganishwa linaruhusiwa na kuwashwa kwa chaguomsingi, ambapo inaruhusu programu kuonyeshwa katika skrini nyingi kama kwamba ni moja. Mtumiaji anaweza kuzima Eneo-kazi Lililounganishwa kwa maonyesho maalum kwa kuondoa alama katika mipangilio ya onyesho.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo au kutowekwa, Eneo-kazi Lililounganishwa litazimwa. Katika hali hii, mtumiaji hawezi kukiwasha kipengele.
Iliacha kuendesha huduma katika M69. Badala yake, tumia OverrideSecurityRestrictionsOnInsecureOrigin.
Sera hii inabainisha orodha za vyanzo (URL) vitakavyochukuliwa kuwa muktadha salama (kama vile "*.example.com") ambako vizuizi vya usalama kwenye vyanzo visivyo salama havitatumika.
Nia yake ni kuruhusu mashirika yatoe idhini kwa programu za zamani ambazo haziwezi kutumia TLS au kuweka seva ya majaribio kwa ajili ya usanidi wa tovuti za ndani, ili wasanidi programu waweze kujaribu vipengele vinavyohitaji muktadha salama bila kutumia TLS kwenye seva ya majaribio. Sera hii pia inazuia chanzo kuwekewa lebo ya "Si salama" katika sanduku kuu.
Hatua ya kuweka orodha ya URL katika sera hii ina athari sawa na kuweka mipangilio ya ripoti ya mstari wa amri '--unsafely-treat-insecure-origin-as-secure' kwenye orodha iliyotenganishwa kwa koma ya URL sawa. Kama sera imewekwa, itabatilisha ripoti ya mstari wa amri.
Sera hii iliacha kuendesha huduma katika M69 katika OverrideSecurityRestrictionsOnInsecureOrigin. Ikiwa sera zote zimewekwa, OverrideSecurityRestrictionsOnInsecureOrigin itabatilisha sera hii.
Kwa maelezo zaidi kuhusu miktadha salama, angalia https://www.w3.org/TR/secure-contexts/
Washa ukusanyaji wa faragha wa data ukitumia ufunguo wa URL kwenye Google Chrome na uwazuie watumiaji wasiweze kubadilisha mipangilio hii.
Ukusanyaji wa faragha wa data ukitumia ufunguo wa URL hutuma URL za kurasa ambazo mtumiaji anatembelea kwenye Google ili kuboresha utafutaji na kuvinjari.
Ukiruhusu sera hii, kipengele cha ukusanyaji wa faragha wa data ukitumia ufunguo wa URL kitabaki kikiwa kimewashwa kila wakati.
Ukizuia sera hii, kipengele cha ukusanyaji wa faragha wa data ukitumia ufunguo wa URL kitabaki kikiwa kimezimwa kila wakati.
Sera hii isipowekwa, kipengele cha ukusanyaji wa faragha wa data ukitumia ufunguo wa URL kitabaki kikiwa kimewashwa lakini mtumiaji ataweza kukibadilisha.
Hukuruhusu ufunge kipindi cha mtumiaji kulingana na wakati wa mteja au mgawo wa nafasi ya siku hiyo.
|time_window_limit| inabainisha muda wa kila siku ambapo kipindi cha mtumiaji kinapaswa kufungwa. Tunatumia sheria moja tu kwa kila siku ya wiki, kwa hivyo huenda mfuatano wa |entries| ukatofautiana kuanzia 0 hadi 7 katika ukubwa. |starts_at| na |ends_at| ni mwanzo na mwisho wa muda unaoruhusiwa, wakati |ends_at| imepungua zaidi ya |starts_at| ina maana kuwa |time_limit_window| itamalizika siku itakayofuata. |last_updated_millis| ni muhuri wa muda wa UTC unaoonyesha wakati wa mwisho ambapo maelezo haya yalisasishwa, hutumwa kama mfuatano kwa sababu muhuri wa muda hauwezi kutoshea nambari kamili.
|time_usage_limit| inabainisha mgawo wa nafasi ya skrini ya kila siku, kwa hivyo wakati mtumiaji atafikia kiasi hiki, kipindi chake kitafungwa. Kuna kipengee cha kila siku ya wiki na kinapaswa kuwekwa tu iwapo kuna mgawo wa nafasi inayotumika siku hiyo. |usage_quota_mins| ni muda ambao vifaa vinavyodhibitiwa vinaweza kutumia kwa siku na |reset_at| ni wakati ambao nafasi ya matumizi husasishwa. Thamani chaguomsingi ya |reset_at| huwa ni saa sita usiku ({'hour': 0, 'minute': 0}). |last_updated_millis| ni muhuri wa muda wa UTC ambapo maelezo haya yalisasishwa mara ya mwisho, hutumwa kama mfuatano kwa sababu muhuri wa muda hauwezi kutoshea nambari kamili.
|overrides| hutolewa ili kubatilisha kwa muda masharti ya awali. * Iwapo time_window_limit au time_usage_limit haitumiki |LOCK| inaweza kufunga kifaa. * |LOCK| hufunga kipindi cha mtumiaji kwa muda hadi time_window_limit ijayo au time_usage_limit ianze. * |UNLOCK| hufungua kipindi cha mtumiaji kilichofungwa kufikia time_window_limit au time_usage_limit.
|created_time_millis| ni muhuri wa muda wa UTC kwa kazi zinazobatilishwa, hutumwa kama mfuatano kwa sababu muhuri wa muda hauwezi kutoshea katika nambari kamili. Hutumika kubaini ikiwa mabatilisho haya yanapaswa kutekelezwa. Ikiwa kipengee cha kudhibiti wakati wa sasa (kipindi cha matumizi au muda wa matumizi) kimeanza baada ya mabatilisho kufanywa, hayapaswi kutekelezwa. Pia iwapo mabatilisho yalifanywa kabla ya mabadiliko ya mwisho ya time_window_limit au time_usage_window inayotumika, hayapaswi kutekelezwa.
Huenda ikatuma mabatilisho mengi. Itatekeleza mabatilisho sahihi na ya hivi karibuni.
Sera hii inakuruhusu kuweka mipangilio ya picha ya ishara inayowakilisha mtumiaji kwenye skrini ya kuingia katika akaunti. Sera inawekwa kwa kubainisha URL ambayo Google Chrome OS inaweza kupakua picha ya ishara na alama ya reli ya kriptografia inayotumika kuthibitisha kuaminika kwa kipakuliwa. Picha sharti iwe katika muundo wa JPEG, ukubwa wake usizidi kB 512. Ni sharti URL ifikiwe bila uthibitishaji wowote.
Picha ya ishara inapakuliwa na kuwekwa katika akiba. Itapakuliwa upya wakati URL au alama ya reli inabadilika.
Sera sharti ibainishwe kuwa mfuatano ambao unaeleza URL na alama ya reli katika muundo wa JSON, kwa kutii utaratibu ufuatao: { "type": "object", "properties": { "url": { "description": "The URL from which the avatar image can be downloaded.", "type": "string" }, "hash": { "description": "The SHA-256 hash of the avatar image.", "type": "string" } } }
Sera hii ikiwekwa, Google Chrome OS itapakua na kutumia picha ya ishara.
Ukiweka sera hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuibatilisha.
Iwapo sera haijawekwa, watumiaji wataweza kuchagua picha ya ishara inayowawakilisha kwenye skrini ya kuingia katika akaunti.
Huweka mipangilio ya saraka ambayo Google Chrome itatumia kuhifadhi data ya mtumiaji.
Ukiweka sera hii, Google Chrome itatumia saraka iliyotolewa bila kujali iwapo mtumiaji amebainisha ripoti ya '--user-data-dir' au la. Ili kuepuka kupoteza data au hitilafu zisizotarajiwa sera hii haipaswi kuwekwa kuwa thamani ya kipeo cha saraka au saraka iliyotumiwa kwa madhumuni mengine, kwa sababu Google Chrome inadhibiti maudhui yake.
Angalia https://www.chromium.org/administrators/policy-list-3/user-data-directory upate orodha ya aina zinazoweza kutumiwa.
Sera hii isipowekwa njia ya wasifu chaguomsingi itatumiwa na mtumiaji ataweza kuibatilisha kwa amri ya ripoti ya mstari ya '--disk-cache-dir'.
Hudhibiti jina la akaunti Google Chrome OS inayoonekana kwenye skrini ya kuingia kwa ajili ya akaunti ya kifaa cha karibu nawe inayolingana.
Iwapo sera hii itawekwa, skrini ya kuingia itatumia uzi uliobainishwa katika kichaguaji cha kuingia kilicho na picha kwa ajili ya akaunti ya kifaa cha karibu nawe inayolingana.
Iwapo sera itaachwa bila kuwekwa, Google Chrome OS itatumia Kitambulisho cha akaunti ya barua pepe ya akaunti ya kifaa cha karibu nawe kama jina la onyesho kwenye skrini ya kuingia.
Sera hii inaapuzwa kwa akaunti za mtumiaji wa mara kwa mara.
Sera ikiwashwa au mipangilio isipowekwa (iwe chaguomsingi), mtumiaji atatumiwa kidokezo cha idhini ya kufikia vipengee vya kurekodi video isipokuwa kwa URL zilizowekwa katika mipangilio ya orodha ya VideoCaptureAllowedUrls ambazo zitapewa idhini ya kufikia bila kudokeza.
Sera hii ikizimwa, mtumiaji kamwe hatawahi kutumiwa kidokezo na hatua ya kurekodi video itapatikana tu kwa URL zilizowekwa katika mipangilio ya VideoCaptureAllowedUrls.
Sera hii huathiri aina zote za vifaa vya kuingiza video na si tu kamera iliyojengewa ndani ya kifaa.
Michoro katika orodha hii italinganishwa na ya asili ya usalama wa ombi la URL. Ikilingana, idhini ya kufikia vifaa vya kurekodi video itatolewa bila ombi. KUMBUKA: Kabla ya toleo la 45, sera hii ilitumika katika hali ya Skrini nzima pekee.
Ruhusu mtumiaji adhibiti miunganisho ya VPN.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, violesura vyote vya Google Chrome OS ambavyo vingeruhusu mtumiaji kutenganisha au kubadilisha miunganisho ya VPN vitazimwa.
Sera hii isipowekwa au iwekwe kuwa 'ndivyo', watumiaji wanaweza kutenganisha au kubadilisha miunganisho ya VPN kama kawaida.
Ikiwa muunganisho wa VPN unaundwa kupitia programu ya VPN, kiolesura kilicho ndani ya programu hakitaathiriwa na sera hii. Kwa hivyo, mtumiaji bado ataweza kutumia programu kubadilisha muunganisho wa VPN.
Sera hii inafaa kutumiwa pamoja na kipengele cha "VPN iliyowashwa kila wakati", ambacho huruhusu mtumiaji aamue kuweka muunganisho wa VPN wakati wa kuwasha.
Huruhusu kuzima uboreshaji wa WPAD (Ugunduaji Kiotomatiki wa Seva Mbadala kwenye Wavuti) katika Google Chrome.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, uboreshaji wa WPAD utazimwa na kusababisha Google Chrome kusubiri muda mrefu zaidi kwa seva za WPAD zinazotegemea DNS. Sera hii isipowekwa au ikiwashwa, uboreshaji wa WPAD utawashwa.
Kwa kutotogemea ikiwa au jinsi sera hii inavyowekwa, mipangilio ya uboreshaji wa WPAD haiwezi kubadilishwa na watumiaji.
Sera hii inakuruhusu kuweka mipangilio ya picha ya mandhari ambayo inaonyeshwa kwenye eneo-kazi na kwenye mandhari ya skrini ya kuingia katika akaunti ya mtumiaji. Sera inawekwa kwa kubainisha URL ambayo Google Chrome OS inaweza kupakua picha ya mandhari na alama ya reli ya kriptografia iliyotumiwa kuthibitisha uaminifu wa kipakuliwa. Picha lazima iwe katika muundo wa JPEG, ukubwa wa faili yake usizidi MB 16. Ni sharti URL ifikiwe bila uthibitishaji wowote.
Picha ya mandhari inapakuliwa na kuwekwa katika akiba. Itapakuliwa upya wakati URL au alama ya reli inabadilika.
Sera sharti ibainishwe kuwa mfuatano ambao unaeleza URL na alama ya reli katika muundo wa JSON, kwa kutii utaratibu ufuatao: { "type": "object", "properties": { "url": { "description": "The URL from which the wallpaper image can be downloaded.", "type": "string" }, "hash": { "description": "The SHA-256 hash of the wallpaper image.", "type": "string" } } }
Sera hii ikiwekwa, Google Chrome OS itapakua na kutumia picha ya mandhari.
Ukiweka sera hii, watumiaji hawawezi kuibadilisha au kuibatilisha.
Sera ikiachwa bila kuwekwa, mtumiaji anaweza kuchagua picha itakayoonyeshwa kwenye eneo-kazi na kwenye mandhari ya skrini ya kuingia katika akaunti.
Hubainisha orodha ya tovuti zinazosakinishwa chinichini bila kumhusisha mtumiaji na ambazo haziwezi kuondolewa wala kuzimwa na mtumiaji.
Kila kipengee kwenye orodha ya sera ni sehemu yenye kipengele cha lazima: "url" na vipengele vingine viwili visivyo vya lazima: "default_launch_container" na "create_desktop_shortcut". Ni sharti "url" iwe URL ya programu ya wavuti ili isakinishwe, ni sharti "launch_container" iwe aidha "dirisha" au "kichupo" ili kuashiria jinsi Programu ya Wavuti itafunguliwa baada ya kusakinishwa na ni sharti "create_desktop_shortcut" iwekwe kuwa 'ndivyo' ikiwa njia ya mkato ya eneo-kazi inapaswa kuundwa kwenye Linux na Windows. Ikiwa "default_launch_container" haijajumuishwa, programu itafunguka katika kichupo kwa chaguomsingi. Licha ya thamani ya "default_launch_container", watumiaji wanaweza kubadilisha metadata ambamo programu itafunguka. Iwapo "create_desktop_shortcuts" haijajumuishwa, hakuna njia za mkato za eneo-kazi zitakazoundwa.
Sera hii inaruhusu watumiaji wa kipengele cha WebDriver kufuta sera ambazo zinaweza kuathiri utendaji wake.
Kwa sasa, sera hii inazuia sera za SitePerProcess na IsolateOrigins.
Kama sera hii imeruhusiwa, WebDriver itaweza kufuta sera zote ambazo hazioani.
Ikiwa sera imezuiwa au haijawekwa, WebDriver haitaruhusiwa kufuta sera ambazo hazioani.
Kama sera imewekwa kuwa ndivyo, Google Chrome huruhusiwa kukusanya kumbukumbu za matukio ya WebRTC kutoka huduma za Google (kwa mfano, Google Meet) na kupakia kumbukumbu hizo kwenye Google.
Kama sera imewekwa kuwa sivyo au haijawekwa, huenda Google Chrome haitakusanya wala kupakia kumbukumbu hizi.
Kumbukumbu hizi hujumuisha maelezo ya utambuzi ambayo yanasaidia kutatua matatizo ya simu za sauti au video katika Chrome, kama vile wakatI na ukubwa wa vifurushi vya RTP vinavyotumwa na kupokelewa, maoni kuhusu msongamano kwenye mtandao na metadata kuhusu wakati na ubora wa fremu za sauti na video. Kumbukumbu hizi hazijumuishi maudhui ya simu ya sauti wala ya video.
Ukusanyaji wa data hii kwa kutumia Chrome unaweza kuanzishwa tu na huduma za wavuti za Google, kama vile Google Hangouts au Google Meet.
Huenda Google ikahusisha kumbukumbu hizi na kumbukumbu zingine ambazo hukusanywa na huduma ya Google yenyewe kupitia kitambulisho cha kipindi; hali hii inanuia kurahisisha shughuli ya utatuzi.
Sera hii ikiwekwa, masafa ya mlango wa UDP unaotumiwa na WebRTC utatumika kwenye mlango uliobainishwa (sehemu za mwisho zikiwa zimejumuishwa).
Sera hii isipowekwa, au ikiwekwa kwenye mfuatano wazi au masafa ya mlango yasiyo sahihi, WebRTC itaruhusiwa kutumia mlango wowote wa ndani wa UDP.
Sera hii ikiwekwa kuwa ndivyo au mipangilio isipowekwa, kivinjari kitaonyesha upya ukurasa wa kukaribisha kinapofunguliwa mara ya kwanza kufuatia sasisho la Mfumo wa Uendeshaji.
Sera hii ikiwekwa kuwa sivyo, kivinjari hakiruhusiwi kuonyesha upya ukurasa wa mwanzo kufuatia uzinduzi wa kwanza baada ya saisho la Mfumo wa Uendeshaji.