KITABU eba ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daud, mwana wa Ibrahimu. Ibrahimu alimzaa Isaak; Isaak akamzaa Yakob; Yakob akamzaa Yuda na ndugu zake; Yuda na Tamar wakamzaa Parez na Zara; Parez akamzaa Esrom; Esrom akamzaa Aram; Aram akamzaa Aminadab; Aminadab akamzaa Nahashon; Nahashon akamzaa Salmon; Salmon na Rahab wakamzaa Boaz; Boaz na Ruth wakamzaa Obed; Obed akamzaa Yese; Yese akamzaa mfalme Daud. Mfalme Daud na mke wa Uria wakamzaa Suleman; Suleman akamzaa Rehoboam; Rehoboam akamzaa Abia; Abia akamzaa Asa; Asa akamzaa Yehoshafat; Yehoshafat akamzaa Yoram; Yoram akamzaa Uzia; Uzia akamzaa Yotham; Yotham akamzaa Ahaz; Ahaz akamzaa Hezekia; Hezekia akamzaa Manasse; Manasse akamzaa Amon; Amon akamzaa Yosia; Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa uhamisho wa Babel. Na haada ya uhamisho ule wa Babel, Yekonia akamzaa Shealtiel; Shealtiel akamzaa Zerubbabel; Zerubbabel akamzaa Ahihud; Ahihud akamzaa Eliakim; Eliakim akamzaa Azor; Azor akamzaa Sadok; Sadok akamzaa Ahim; Ahim akamzaa Eliud; Eliud akamzaa Eleazar; Eleazar akamzaa Mattan; Mattan akamzaa Yakob; Yakob akamzaa Yusuf mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwae Kristo. Bassi vizazi vyote tangu Ibrahimu hatta Daud vizazi kumi na vine; na tangu Daud hatta uhamisho ule wa Babel vizazi kumi na vine; na tangu uhamisho ule wa Babel hatta Kristo vizazi kumi na vine. Na kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipoposwa na Yusuf, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Nae Yusuf, mumewe, kwa kuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. Alipokuwa akifikiri haya, malaika wa Bwana akamtokea katika udoto, akisema, Yusuf, mwana wa Daud, usikhofu kumchukua Mariamu mke wako, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Nae atazaa mtoto mwanamume, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, ndiye atakaewaokoa watu wake na dhambi zao. Haya yote yamekuwa, illi litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akinena, Angalia, mwanamke bikira atachukua mimba, nae atazaa mwana, Na watamwita jina lake Immanuel; tafsiri yake, Mungu kati yetu. Yusuf alipoamka katika usingizi, akatenda kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe; asimjue kamwe hatta alipomzaa mwanawe wa kifungua mimba; akainwita jina lake YESU. ALIPOZALIWA Yesu katika Bethlehemu ya Yahudi zamani za mfalme Herode, majusi wa mashariki walifika Yerusalemi, wakinena, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyola yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudu. Mfalme Herode aliposikia haya, akafadhaika, na Yerusalemi pia pamoja nae. Akakusanya makuhani wakuu wote na waandishi wa watu, akatafuta khabari kwao, Kristo azaliwa wapi? Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Yahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, Na wewe Bethlehemu wa inchi ya Yuda, Huwi mdogo kamwe katika majumbe ya Yuda: Kwa kuwa kwako atatoka liwali Atakaewachunga watu wangu Israeli. Kisha Herode akawaita majusi kwa faragha, akapata kwao hakika ya muda ile nyota ilipoonekana. Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkahoji sana mambo ya mtoto; mkiisha kumwona, nileteeni khabari, illi nami nije nimsujudie. Nao waliposikia maneno ya mfalme wakashika njia; na tazama ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hatta ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto. Walipoiona ile nyota, wakafurahi furaha kuliwa mno. Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mama yake, wakaanguka wakasujudu; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tumi, dhahabu, uvumba, na manemane. Nao wakiisha kuonywa katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine. Na hawo walipokwisha kwenda zao, malaika wu Bwami akamtokea Yusuf katika ndoto, akiuena, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukakae huko mpaka nikuambiapo; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize. Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake hatta Misri; akawa huko mpaka alipokufa Herode: illi litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nalimwita mwaua wangu. Bassi Herode, akiona ya kuwa amedhihakiwa na majusi, akaghadhabika sana, akatuma watu kuwaua watoto wote wanawaume waliokuwa Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wa miaka miwili na waliopungua, kwa muda aliouhakiki kwa majusi. Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na kulalama, na maombolezo, Rahel akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, maana hawako. Hatta alipofariki Herode, malaika wa Bwana akamtokea Yusuf katika ndoto huko Misri, akinena, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ushike njia kwenda inchi ya Israeli: kwa maana wamekufa walioilafuta roho ya mtoto. Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake, akatika inchi ya Israeli. Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki Yahudi mahali pa Herode baba yake, akaogopa kwenda huko; akaonywa katika ndoto, akaenda zake hatta pande za Galilaya, akaenda, akakaa mji uliokwitwa Nazareti: illi litimie neno lililonenwa na manabii, Atakwitwa Mnazorayo. SIKU zile akaondokea Yohana Mbatizaji akikhubiri katika jangwa ya Yahudi, akinena, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti yake apigae mbin jangwani, Itengenezeni njia ya Bwana, Nyosheni mapito yake. Yohana mwenyewe alikuwa na mavazi yake ya singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. Ndipo wakamwendea Yerusalemi, na Yahudi yote, na inchi zote za kando za Yordani; wakabatizwa nae mtoni Yordani, wakiziungama dhambi zao. Hatta akiona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, akawaambia, Uzao wa nyoka, nani aliyewaonya mkimbie ghadhabu ijayo? Zaeni bassi matunda yaipasayo toba; msiwaze moyoni kwamba, Tuna baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni ya kwamba Mungu anaweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto. Nalo shoka limekwisha kuwekwa penye shina la miti; bassi killa mti usiozaa matunda mazuri unakatwa na kutupwa motoni. Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Pepeto lake li mkononi mwake, nae ataitakasa sana sakafu yake; atakusanya nganu yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika. Ndipo Yesu akafika hatta Yordani kwa Yohana kutoka Galilaya illi abatizwe nae. Lakini Yohana alikuwa akimzuia, akinena, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, na wewe waja kwangu? Yesu akajibu, akamwambia, Hayo yaache sasa: kwa kuwa hivi imetupasa kutimiza haki yote. Bassi akamwacha. Nae Yesu alipokwisha kubatizwa marra akapanda kutoka majini: mbingu zikamfunukia, akamwona Roho ya Mungu akishuka kama hua, akija juu yake: na sauti toka mbinguni ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninaependezwa nae. NDIPO Yesu alipopandishwa na Roho hatta jangwani, illi ajaribiwe na Shetani. Akafunga siku arubaini mchana na usiku, baadae akaona njaa. Mjaribu akamjia akasema, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate. Akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, illa kwa killa neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Kisha Shetani akamchukua hatta mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini: kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake: Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Yesu akamwambia. Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. Tena Shetani akamchukua hatta mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fakhari yake, akamwambia, Hizi zote nitakupa, ukianguka kunisujudia. Ndipo Yesu akamwambia, Nenda zako, Shetani: kwa maana imeandikwa, Utamsujudia Bwana Mungu wako, nae peke yake utamwabudu. Kisha Shetani akamwacha; wakaja malaika wakamtumikia. Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, akaenda zake hatta Galilaya; akatoka Nazareti, akaenda, akakaa Kapernaum, ulioko pwani, mipakani mwa Zabulon na Nafthalim: illi litimie neno lililonenwa na Nabii Isaya, akisema, Inchi ya Zabulon na inchi ya Nafthalim, Njia ya bahari ngʼambu ya Yordani, Galilaya ya mataifa, Watu waliokaa gizani Waliona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika inchi na kivuli cha mauti, Mwanga umewazukia. Tokea wakati huo Yesu akaanza kukhubiri, na kusema, Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Nae Yesu akitembea kando ya bahari ya Galilaya, akaona ndugu wawili, Simon aitwae Petro, na Andrea ndugu yake, wakitupa jarife baharini; maana walikuwa wavuvi. Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wii watu. Marra wakaziacha nyavu, wakamfuata. Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili. Yakob wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake, walikuwa katika chombo pamoja na Zebedayo baba yao, wakitengeneza nyavu zao; akawaita. Marra wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata. Yesu akazunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika sunagogi zao, na kuikhubiri injili ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa killi namna katika watu. Khabari zake zikaenea katika Sham yote; wakamletea watu waliokuwa hawawezi, walioshikwa mi maradhi mbali mbali na mateso, nao wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya. Makutano mengi wakamfuata, wakitoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemi, na Yahudi, na ngʼambu ya Yordani. NAE akivaona makutano, akapanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake wakamjia; akafunua kinywa chake, akawafundisha, akinena, Wa kheri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao. Wa kheri wenye huzuni: maana hawo watafarajika. Wa kheri wenye upole: maana hawo watairithi inchi. Wa kheri wenye njaa na kiu ya haki: maana hawo watashiba. Wa kheri wenye rehema: maana hawo watarehemiwa. Wa kheri walio na moyo safi; maana hawo watamwona Mungu. Wa kheri wasuluhishi: maana hawo watakwitwa wana wa Mungu. Wa kheri wateswao kwa ajili ya haki: maana ufalme wa mbinguni ni wao. M kheri ninyi watakapowatukana na kuwatesa na kuwanenea killa neno baya kwa uwongo, kwa ajili yangu. Furahini, shangilieni: kwakuwa thawabu yenu nyingi mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu. Ninyi ni chumvi ya dunia: lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwani ikolee? Haifai tena kabisa, illa kufupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kustirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya kibaba, bali juu ya kibao cha kuwekea taa; nayo yaangaza wote waliomo nyumbani. Vivi hivi nuru yenu iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wakamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin nawaambieni, Mpaka mbingu na inchi zitakapoondoka, yodi moja na nukta moja ya torati haitaondoka, mpaka yote yatimie. Bassi mtu atakaevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha wafu hivi, atakwitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni: bali mtu atakaezitenda na kufundisha, huyu afakwitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Maana nawaambieni, Haki yenu isipozidi kuliko haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Mmesikia watu wa kale walivyoanibiwa, Usiue; na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambiem, Killa amwoneae ndugu yake ghadhabu bila sababu, itampasa hukumu; na mtu akimwambia ndugu yake, Haka, itampasa baraza; na mtu akinena, Mpumbavu, itampasa jebannum ya moto. Bassi ukileta sadaka yako madhbahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madbbahu, nenda zako, kwanza patana na ndugu yako, kisha rudi utoe sadaka yako, Patana na mshtaki wako upesi, wakati uwapo pamoja nae njiani; yule mshtaki asije akakupeleka kwa kadhi, kadhi akakutia mkononi mwa askari, ukatupwa kifungoni. Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hatta uishe kulipa pesa ya mwisho. Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usizini: Bali mimi miwaambieni, Killa mtu atazamae mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini nae moyoni mwake. Jicho lako la kuume likikukosesha, lingʼoe ulitupe mbali nawe: kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehannum. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe: kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee, wala mwili wako mzima usitupwe katika jehannum. Waliambiwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe khati ya talaka; bali mimi nawaambieni, Killa mtu amwachae mkewe, isipokuwa kwa khabari ya asharati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini. Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usifanye zuli, bali mtimizie Bwana nyapo zako; bali mimi nawaambieni, Usiape kabisa; hatta kwa mbingu, kwa maana ndio kiti cha enzi cha Mungu; wala kwa inchi, kwa maana ndio pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemi, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unyele mmoja kuwa mwenpe au mwensi. Bali maneno yenu yawe, Ndio, ndio; Sio, sio: kwa kuwa izidiyo haya yatoka kwa yule mwovu. Mmesikia walivyoambiwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino: bali mimi nawaambieni, Msishindane na mtu mwovu; bali mtu akupigae shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Na mtu atakae kukushtaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho. Na mtu atakaekutumikisha maili moja, nenda nae mbili. Akuombae, mpe; nae atakae kukopa kwako, usimpe kisogo. Mmesikia walivyoambiwa, Mpende jirani yako, na, Mchukie adui yako: bali mimi nawaambieni, Wapendeni adui zenu, wabarikini wanaowalaani, watendeni mema wanaowachukia, waombeeni wanaowatendea ukorofi, na kuwatesa; illi mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni: maana yeye jua lake huwazushia waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Maana mkiwapenda wanaowapendani, mwapata thawabu gani? Hatta watoza ushuru, je, nao hawafanyi yayo hayo? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziyada? Hatta wattoza ushuru, je, nao hawafanyi kama hayo? Bassi mwe ninyi wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. ANGALIENI msitoe sadaka zenu mbele ya watu, kusudi mtazamwe nao: kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Bassi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika sunagogi na njiani, illi watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hatta mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kuume ufanyalo; sadaka yako iwe kwa siri: na Baba yako aonae kwa siri atakujazi kwa dhahiri. Tena usalipo, usiwe kama wanafiki: kwa maana wapenda kusali wakisimama katika sunagogi na katika pembe za njia, illi waonekane na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe usalipo, ingia chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele ya Baba yako aliye kwa siri: na Baba yako aonae kwa siri atakujazi kwa dhahiri. Mkiwa katika kusali, msipayukepayuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Bassi msifanane na hawo; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. Bassi ninyi salini hivi; Baba yetu nliye mbinguni, jina lako takatifu litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki zetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi tunavyowasamehe wadeni wetu. Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu. Kwa kuwa wako ni ufalme, na nguvu, na utukufu, hatta milele. Amin. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe nanyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana: maana hujiumbua nyuso zao, illi waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe nso; illi usionekane na watu kuwa unafunga, bali na Baba yako aliye kwa siri; na Baba yako, aonae kwa siri, atakujazi kwa dhahiri. Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu ziharibupo, na wevi huvunja na kuiba: bali jiwekeeni hazina mbinguni, zisikobaribu nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala kuiba; kwa maana ilipo hazina yenu, ndipo utakapokuwa na moyo wako. Taa ya mwili ni jicho; bassi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini jicho lako likiwa ovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Bassi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza, giza gani hilo! Hakuna mtu awezae kuwatumikia bwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja, na kumpenda wa pili; au atamshika mmoja, na kumtweza wa pili. Hamwezi kumtumikia Mungu na mamona. Kiva sababu hii nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mleni au mnyweni; wala mwili wenu, mvaeni. Maisha je, si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa anga, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni awalisha hawo. Ninyi je! si bora kupita hawo? Yupi katika ninyi awezae kwa kusumbuka kujiongeza kimo chake mkono mmoja? Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini khabari za maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayatendi kazi, wala hayasokoti: lakini nawaambieni, ya kwamba hatta Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama moja la hayo. Lakini Mungu akiyavika hivi majani ya mashamba, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je, hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? Msisumbuke, bassi, mkinena, Tuleni? au, Tunyweni? au, Tuvaeni? Kwa maana haya yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji haya yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake; na haya yote mtazidishiwa. Bassi msisumbukie kesho; kwa kuwa kesho itayasumbukia mambo yake. Watosba kwa siku ubaya wake. MSIHUKUMU, illi msihukumiwe Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa: na kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa. Nawe, ya nini kukitazama kibanzi kilicho katika jicho la ndugu yako, na boriti iliyo katika jicho lako huiangalii? Au utamwambiaje ndugu yako, Niache niondoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! imo boriti ndani ya jicho lako? Mnaflki, iondoe kwanza ile boriti katika jicho lako; ndipo utakapoona sana hatta kukiondoa kibanzi katika jicho la ndugu yako. Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararueni. Ombeni na mtapewa; tafuteni na mtaona; bisheni na mtafunguliwa: kwa maaua killa aombae hupokea; nae atafutae huona, nae abishae alafunguliwa. Au mtu yupi katika ninyi, ambae, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au akiomba samaki, atampa nyoka? Kama ninyi, bassi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! si zaidi Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wamwombao? Bassi yo yote mtakayo kutendewa na watu, nanyi mwatendee vivyo hivyo: maana hiyo ndiyo torati na manabii. Ingieni kwa kupita mlango ulio mwembamba: maana ujia iendayo hatta upotevu ni pana, na mlango wake mpana, na wengi waingiao kwa mlango huo. Bali njia ni nyembamba iendayo hatta uzima, na mlango wake ni mwembamba: nao waionao ni wachache. Jihadharini na manabii wa uwongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa wa mwitu wakali. Mtawalambua kwa matunda yao. Je, watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo killa mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti uliopea huzaa matunda hafifu. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda hafifu, wala mti uliopea kuzaa matunda mazuri. Killa mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Bassi kwa matunda yao mtawatambua. Siye killa mtu aniambiae, Bwana, Bwana, atakaeingia katika ufalme wa mbinguni; hali yeye afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kufukuza pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwafahamu ninyi wakati wo wote: ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. Bassi killa asikiae haya maneno yangu, na kuyafanya, nitamfananisha na mtu mwenye akili aliyejenga nyumba vake juu ya mwamba: mvua ikanya, maji mengi yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa katika mwamba. Na killa asikiae haya maneno yangu, asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, alivejenga nyumba yake katika mchanga; mvua ikanya, maji mengi yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; anguko lake likawa kubwa. Ikawa, Yesu alipomaliza maneno haya, makutano wakashangaa kwa mafundisho yake: kwa maana alikuwa akiwafundisha kwa namna ya mwenye mamlaka, wala si kama waandishi wao. ALIPOSHUKA mlimani, makutano mengi walimfuata. Akaja mwenye ukoma akamsujudu, akinena, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa. Yesu akanyosha mkono wake, akamgusa, akinena, Nataka: takasika. Marra ukoma wake ukatakasika. Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; illa enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, utoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao. Hatta Yesu alipoingia Kapernaum, akida alimjia, akamsihi, akinena, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. Yesu akamwambia. Nitakuja, nimponye. Akida akamjibu, akasema, Si stahili yangu wewe uingie chini ya dari yangu: lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona. Maana na mimi ni mtu chini ya mamlaka, nina askari chini yangu: nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; au mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya. Yesu aliposikia haya, akastaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa kama hii, hatta katika Israeli. Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magbaribi, wataketi pamoja na Ibrabimu, na Isaak, na Yakob katika ufalme wa mbinguni; bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje; ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno. Yesu akamwambia akida, Nenda zako: na kadiri ulivyoamini upate. Mtumishi wake akapona saa ileile. Hatta Yesu alijiofika nyumbani kwa Petro, akamwona mama wa mkewe amelala hawezi homa. Akamgusa mkono wake, homa ikamwacha; nae akaondoka, akawatumikia. Ilipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo: akawafukuza pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi, illi litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe alitwaa magonjwa yetu, na kuchukua maradhi zetu. Yesu alipoona makutano mengi wakimzunguka, akaamuru kuvuka hatta ngʼambu. Mwandishi mmoja akamwendea, akamwambia, Mwalimu, nitakufuata ko kote uendako. Yesu akamwambia, Mbweha wana matundu, na ndege za anga vituo; bali Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake. Mwingine katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, nipe rukhusa kwanza, niende nikamzike baba yangu. Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao. Akapanda chomboni, wanafunzi wake wakamfuata. Kukawa msukosuko mkuu baharini, hatta chombo kikafunikizwa na mawimbi: nae alikuwa amelala. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakinena, Bwana, tuokoe tunaangamia. Akawaambia, Mbona mu waoga, enyi wa imani haba? Marra akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu. Wale watu wakastaajabu, wakinena. Huyo ni mtu wa namna gani hatta pepo na bahari zamtii? Alipofika ngʼambu, katika inchi ya Wagergesene, watu wawili wenye pepo walikutana nae, wanatoka makaburini, wakali mno, hatta mtu asiweze kupita njia ile. Wakapiga kelele, wakinena, Tuna nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu? Je, umekuja kutuadhibu kabla ya muhulla? Bassi, kulikuwako mbali kundi la nguruwe wengi wakilisha. Pepo wakamsihi, wakinena, Ukitufukuza, tuache twende, tukaingie katika kundi la nguruwe. Akawaambia. Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika kundi la nguruwe: na, kumbe! kundi lote la nguruwe likatelemka kwa kassi gengeni, wakaingia baharini, wakafa majini. Wachungaji wakakimbia, wakaenda zao mjini, wakayakhubiri yote, na mambo ya wenye pepo pia. Mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; walipomwona, wakamsihi aondoke mipakani mwao. AKAPANDA chomboni, akavuka, akafika mjini kwake. Wakamletea mgonjwa wa kupooza, amelala kitandani: na Yesu, akiona imani yao, akamwambia yule mgonjwa wa kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanaugu; umeondolewa dhambi zako. Baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. Nae Yesu, akijua mawazo yao, akasema, Jinsi gani mnawaza maovu mioyoni mwenu? Kwa maana vipi vyepesi, kusema, Umeondolewa dhambi zako; au kusema, Ondoka, ukaende? Lakini illi mjue ya kuwa Mwana wa Adamu yuna mamlaka katika dunia kuondoa dhambi, (amwambia yule mgonjwa wa kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende nyumbani kwako. Akaondoka, akaenda zuke nyumbani kwake. Makutano wakimwona, wakastaajabu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu mamlaka ya jinsi hii. Yesu alipokuwa anaondoka kutoka huko akaona mtu amekeli fordhani, aitwae Mattayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata. Ikawa alipoketi ale ndani ya nyumba, wutoza ushuru wengi na wenye dhambi wakaja wakaketi pamoja na Yesu ua wanafunzi wake. Mafarisayo walipoona, wakawaambia wanafunzi wake, Kwa nini mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Nae Yesu akisikia, akawaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi. Lakini shikeni njia, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka: kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu. Wakati ule wanafunzi wa Yohana wakamwendea, wakinena, Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga marra nyingi, bali wanafunzi wako hawafungi? Yesu akawaambia, Wana wa arusi wawezaje kuomboleza, maadam Bwana arusi yupo pamoja nao? Lakini siku zitakuja atakapoondolewa bwana arusi; udipo watakapofunga. Hakuna mtu atiae kipande cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, likazidi kutatuka. Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; ikiwa watia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika: bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote. Alipokuwa akiwaambia haya, yuaja jumbe mmoja, akamsujudia, akinena, Binti yangu udio kwanza afe: lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, uae atapona. Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake. Na mwanamke, aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka thenashara, alikuja kwa nyuma, akagusa upindo wa vazi lake: kwa maana alisema kimoyomoyo, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona. Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile. Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, akaona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo, akawaambia, Ondokeni: kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana. Hatta makutano walipoondoshwa, akaingia, akamshika mkono wake; yule kijana akasimama. Zikaenea khabari hizi katika inchi ile yote. Yesu alipokuwa anaondoka kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaaza sauti, wakinena. Uturehemu, Ee mwana wa Daud. Alipolika nyumbani, wale vipofu wakamwendea: Yesu akawaambia. Mnaamini kwamba naweza kufanya haya? Wakamwambia, Naam, Bwana. Marra akawagusa macho yao, akanena, Kwa kadiri ya imani yenu mpate. Macho yao yakafumbuka. Yesu akawaagiza kwa nguvu, akinena, Angalieni hatta mtu mmoja asijue. Lakini wakatoka, wakaeneza khabari zake katika inchi ile yote. Hatta wale walipokuwa wakitoka, wakamletea mtu bubu mwenye pepo. Na pepo alipofukuzwa, yule bubu akasema, makutano wakastaajabu, wakanena, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote. Lakini Mafarisayo wakanena, Kwa mkuu wa pepo afukuza pepo. Na Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masunagogi yao, akikhubiri injili ya ufalme, akiponya magonjwa yote na dhaifu zote katika watu. Na alipowaona makutano, akawahurumia, kwa maana walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchunga. Ndipo akawaambia wanafunzi wake, Mavuno ni makubwa, bali watenda kazi wachache. Bassi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake. AKAWAITA wanafunzi wake thenashara, akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, wawafukuze, na kuponya magonjwa yote na dhaifu zote. Na majina ya mitume thenashara ni haya: Wa kwanza Simon aliyekwitwa Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake; Filipo, na Bartolomayo, na Tomaso, na Mattayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Lebbayo, aliyekwitwa Thaddayo; Simon Kananayo, na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti. Hawa thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akinena, Katika njia ya Mataifa msiende, wala mjini mwa Wasamaria msiingie: afadhali shikeni njia kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Na katika kuenenda kwenu, khubirini, nikinena, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Ponyeni wagonjwa, takaseni wenye ukoma, fufueni wafu, fukuzeni pepo; mmepata burre, toeni burre. Msichukue dhahabu, wala fedha, wala shaba mishipini mwenu; wala mkoba wa safari, wula kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo: maana mtenda kazi astahili posho lake. Na mji wo wote au kijiji cho chote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu amini; kakaeni humo hatta mtakapotoka. Na mkiingia katika nyumba, isalimuni. Na nyumba ile ikistahili, amani yenu iifikilie: la, haistahili, amani yenu iwarudieni. Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kungʼuteni mavumbi ya miguuni mwenu. Amin, nawaambieni, Itakuwa rakhisi inchi ya Sodoma na Gomora istahimili adhabu yao siku ya hukumu, kuliko mji ule. Angalieni, mimi nawatumeni kama kondoo kati ya mbwa wa mwitu: bassi mwe na busara kama nyoka, na msio na dhara kama hua. Jihadharini na wana Adamu; kwa maana watawapelekeni mbele ya baraza, na katika masunagogi yao watawapiga; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, illi kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa. Lakini hapo wakatapowapelekeni, msifikirifikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. Kwa kuwa si ninyi msemao, bali Roho ya Baba yenu asemae ndani yenu. Na ndugu atamsaliti ndugu apate kufa, na baba atamsaliti mtolo; na watoto wataondoka kuwashitaki wazee wao, wawafishe. Na mtakuwa mkichukiwa na watu wole kwa ajili ya jina langu: lakini adumuye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka. Watakapowaudhi katika mji huu, kimbilieni mwingine: kwa maana ni kweli nawaambieni, Hamtaimaliza miji yote ya Israeli, hatta ajapo Mwana wa Adamu. Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumishi hampiti bwana wake. Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebul, je, si zaidi wale walio nyumbani mwake? Bassi, msiwaogope, kwa maana hakuna jambo lililostirika, ambalo halitafunuliwa baadae; wala lililofichwa, ambalo halitajulikana baadae. Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni kalika nuru; na msikialo kwa siri, likhubirini juu ya nyumba. Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho: afadhali mmwogopeni yule awezae kuangamiza mwili na roho pia katika jehannum. Videge viwili haviuzwi kwa pesa moja? Na hatta mmoja haanguki chini asijiojua Baba yemi: hatta na nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope bassi; hora ninyi kuliko videge vingi. Bassi killa mtu atakaenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. Bali mtu ye yote atakaenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. Msidhani ya kuwa nalikuja kueneza amani duniani; la! sikuja kueneza amani, bali upanga. Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na baba yake, na binti na mama yake, na mkwe na mkwe mtu: na adui wa mtu ndio wale wa nyumbani mwake. Apendae baba au mama kuliko mimi, hanifai; na apendae mwana au binti kuliko mimi hanifai. Nae asiyechukua msalaba wake na kufuata nyuma yangu, hanifai. Anaeipata roho yake ataiangamiza; nae anaeitoa roho yake kwa ajili yangu ataipata. Awapokeae ninyi, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeae nabii kwa kuwa yu nabii, atapata thawabu ya nabii; nae ampokeae mwenye haki kwa kuwa yu mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki. Na mtu aliye yote atakaemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa kikombe cha maji ya baridi tu, kwa kuwa yu mwanafunzi, amin, nawaambieni, haitampotea kamwe thawabu yake. IKAWA Yesu alijiokwisha kuwaagiza wanafunzi wake thenashara, akatoka huka kwenda kufundisha na kukhubiri katika miji yao. Nae Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wawili katika wanafunzi wake, kumwambia, Wewe ndiye ajae, au tumtazamie mwingine? Yesu akajibu akawaambia, Enendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona: vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema. Na yu kheri ye yote asiyechukiwa nami. Nao wakienda zao, Yesu akaanza kuwaambia makutano khabari za Yohana, Mlitoka kwenda jangwani kutazama nini? Unyasi ukilikiswa na upepo? Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi meroro? Watu wavaao mavazi meroro, wamo katika nyumba za wafalme. Lakini mlikwenda kuona nini? Nabii? Naam, nawaambieni, na aliye zaidi ya nabii. Kwa maana huyo ndiye aliyeandikiwa, Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako. Atakaeitengeneza njia yako mbele yako. Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji: illakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. Tangu siku za Yohana Mbatizaji hatta leo ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. Na ikiwa mantaka kukubali, yeye ndiye Elia atakaekuja. Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie. Nitafananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na watoto wakikaa sokoni, wanaowaita wenzao, wakinena, Twaliwapigia filimbi, wala hamkucheza; twaliomboleza, wala hamkulia. Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakanena. Yuna pepo. Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakanena, Mlafi huyu, na mnywa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imepewa haki na watoto wake. Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu. Ole wako, Korazin! Ole wako, Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Turo na Sidon, wangalitubu zamani kwa kuvaa gunia na majivu. Lakini, nawaambieni, itakuwa rakhisi Turo na Sidon istahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi. Nawe Kapernaum, uliyeinuliwa hatta mbinguni, utashushwa hatta kuzimu: kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwako, ingalifanyika katika Sodom, ungalikuwapo hatta leo. Lakini nawaambieni, itakuwa rakhisi inchi ya Sodom istahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe. Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo: Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele yako. Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu: wala hakuna mtu amjuae Mwana, illa Baba; wala hakuna mtu amjuae Baba illa Mwana, na ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia. Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye mizigo nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, jifunzeni kwa mfano wangu; kwa kuwa mimi ni mpole na moyo wangu umenyenyekea: nanyi mtapata raha rohoni mwenu; kwa maana nira yangu laini, na mzigo wangu mwepesi. WAKATI ule Yesu alipita katika makonde siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala. Na Mafarisayo walipoona, wakamwambia, Tazama! wanafunzi wako wanatenda lililo haramu kutenda siku ya sabato. Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daud, alipokuwa na njaa, yeye na wenzi wake; jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate iliyotolewa kwa Mungu, isiyo halali kuliwa nae wala na wenzi wake, illa na makuhani peke yao? Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate khatiya? Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu. Kama mngalijua maana ya maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, hamngaliwalaumu wasio na khatiya. Kwa maana Mwana wa Adamu udiye Bwana wa sabato. Akaondoka huko, akaiugia katika sunagogi lao. Na tazama mtu mwenye mkono umepooza, wakamwuliza, wakinena, Ni halali kuponya watu siku ya sabato? wapate kumshtaki. Akawaambia, Ni mtu yupi miongoni mwenu mwenye kondoo mmoja, yule kondoo akatumbukia shimoni siku ya sabato, asiyemshika akamwondosha? Je! mtu si hora sana kuliko kondoo? Bassi ni halali kutenda mema siku ya sabato. Akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako; akaunyosha, ukapona, nkawa mzima kama mkono wa pili. Lakini Mafarisayo wakatoka wakamfanyia shauri la kumwangamiza. Nae Yesu akijua haya akatoka huko: makutano mengi wakamfuata; akawaponya wote, akawaagiza wasimdhihirishe; illi litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Tazama, mtumishi wangu niiliyemteua; Mpendwa wangu, ambae moyo wangu umependezwa nae; Nitamtia roho yangu, Nae atuwatangazia Mataifa hukumu. Hatateta, wala hatapaaza sauti yake; Wala mtu hatasikia sauti yake njiani. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala kitani kitokacho moshi hatakizima, Hatta aletapo hukumu yake ikashinda. Na jina lake Mataifa watalitumainia. Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu na bubu; akamponya, hatta yule kipofu na bubu akasema na kuona. Makutano wote wakashangaa wakasema, Huyu siye mwana wa Daud? Lakini Mafarisayo waliposikia, wakasema, Huyu hafukuzi pepo, illa kwa uweza wa Beelzebul mkuu wa pepo. Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Killa ufalme ukifitinika na nafsi yake, hufanyika ukiwa; na killa mji au nyumba ikifitinika na nafsi yake, haitasimama. Na Shetani akimfukuza Shetani, amefitinika na nafsi yake; bassi ufalme wake utasimamaje? Na mimi nikifukuza pepo kwa uweza wa Beelzebul, je! wana wenu wawafukuza kwa uweza wa nani? Kwa sababu hii hawo ndio watakaokuwa waamuzi wenu. Lakini mimi nikifukuza pepo kwa uweza wa Bobo ya Mungu, bassi ufalme wa Mungu umekujieni. Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? ndipo atakapoiteka nyumba yake. Mtu asiye upande wangu yu kinyume changu; na mtu asivekusanya pamoja nami hutapanya. Kwa sababu hii nawaambieni, Killa dhambi na killa neno la kufuru watasamehewa wana Adamu, bali kumtukana Roho hawatasamehewa wana Adamu. Na killa mtu atakaenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakaenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ntakaokuwa. Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hujulikana. Uzao wa nyoka, mwawezaje kusema mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa mema: na mtu mbaya katika hazina yake mbaya hutoa mabaya, Bassi, nawaambieni, Killa neno lisilo maana, watakalolisema wana Adamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. Maana kwa maneno yako utapewa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa. Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakinena, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zina chataka ishara, wala hakitapewa ishara, ilia ishara ya nabii Yunus. Maana kama vile Yunus alivyokuwa siku tatu mchana na nsiku katika tumbo la nyamgumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa inchi. Watu wa Ninawi watasimama siku ile ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watakihukumu: maana wao walitubu kwa makhubiri ya Yunus; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yunus. Malkia wa kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nae atakihukumu: maana yeye alikuja kutoka pande za mwisho za ulimwengu asikie hekima ya Sulemani; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani. Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupita kati ya pahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. Khalafu hunena, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. Marra huenda, akachukua pamoja nae pepo wengine saba walio waovu kupita nafsi yake, nao huingia na kukaa humo; na mambo, ya mwisho ya mtu yule huwa mabaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kiovu. Alipokuwa katika kusema na makutano, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wakitaka kusema nae. Mtu akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe. Akajihu, akamwambia yule aliyempa khabari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni nani? Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema. Tazama, Mama yangu na ndugu zangu! Kwa maana ye yote atakaeyafanya mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu. SIKU ile Yesu akatoka nyumbani, akaketi kando ya bahari. Wakamkusanyikia watu wengi, hatta akapanda chomboni, akaketi; na mkutano wote wakasimama pwani. Akasema nao mengi kwa mifano, akinena, Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu. Hatta alipokuwa akipanda, nyingine zikaanguka njiani, ndege wakaja wakazila: nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa udongo mwingi: marra zikaota, kwa kuwa na udongo haba; na jua lilipozuka zikanyauka; na kwa kuwa hazina mizizi zikakauka. Nyingine zikaanguka penye miiba; miiba ikamea, ikazisonga: nyingine zikaanguka penye udongo mwema, zikazaa, hizi mia, hizi sittini, hizi thelathini. Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie. Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano? Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wale hawakujaliwa. Kwa maana ye yote aliye na mali atapewa, na hado atazidishiwa tele: lakini ye yote asiye nayo, hatta ile aliyo nayo ataondolewa. Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawatazami na wakisikia hawasikii, wala hawafahamu. Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likinena, Kusikia mtasikia, wala hamtafahamu; Mkitazama mtatazama, wala hamtaona: Maana moyo wa watu hawa umekuwa mzito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao Wakasikia kwa masikio yao, Wakafahama kwa mioyo yao, Wakaongoka, Nikawaponya. Lakini ya kheri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia. Kwa maana amin, nawaambieni, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasivaone; na kuyasikia mnayoyasikia, wasiyasikie. Bassi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi. Killa alisikiae neno la ufalme asifahamu, huja yule mwovu, akaliteka lililopandwa moyoni mwake. Huyu ndiye aliyepandwa njiani. Nae aliyepandwa penye miamba, huyu ndiye alisikiae lile neno, akalipokea marra kwa furaha; lakini hana mizizi udani yake, hukaa muda mchache; ikitukia shidda au udhia kwa sababu ya lile neno, marra huchukizwa. Nae aliyepandwa penye miiba, huyu ndiye alisikiae lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno, likawa halizai. Nae aliyepandwa penye udongo mwema, huyu ndive alisikiae lile neno, na kulifahamu; yeye ndiye azaae matunda, huyu mia, na huyu sittini, na huyu thelathini. Akawatolea mfano mwingine, akinena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake: lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya nganu, akaenda zake. Baadae majani ya nganu yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Watumishi wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? limepatapi bassi magugu? Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumishi wakamwambia, Bassi, wataka twende tukayakusanye? Akasema, La; labuda wakati wa kukusanya magugu, mtangʼoa na nganu pamoja nayo. Viacheni vyote vikue hatta wakati wa mavuno: na wakati wa mavuno nitawaambia wavimao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita, mkayachome; bali nganu ikusauyeni ghalani mwangu. Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya kharadali, aliyotwati mtu akaipanda katika shamba lake; nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, ni kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hatta ndege za anga huja na kutua katika matawi yake. Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke, akaisetiri katika pishi tatu za unga, hatta ukachacha wote pia. Haya yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; na pasipo mfano hakuwaambia neno: illi litimizwe neno lililonenwa mi nabii, akisema, Nitafunua kinywa changu kwa mifano, Nitatoa mambo yaliyostirika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Kisha Yesu akawaacha makutano, akaingia nyumbani: wanafunzi wake wakamwendea, wakinena, Tufafanulie mfano wa magugu ya konde. Akajibu, akasema, Azipandiie zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu; na lile konde ni ulimwengu; na zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu; na yule adui aliyeyapanda ni shetani; na mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika. Bassi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia hii. Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya katika ufalme wake machukizo yote, nao watendao maasi, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno. Ndipo wenye haki watangʼaa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie. Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyostirika katika shamba; mtu akaiona, akaificha; na kwa furaha yake akaenda akanza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile. Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mfanya biashara, afafutae lulu nzuri: nae alipoona lulu moja ya thamani kubwa, akaenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua. Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya za killa namna: hatta lilipojaa, wakalipandisha pwani; wakaketi, wakakusanya zilizo njema vyomboni, bali zilizo mbaya wakazitupa. Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia: malaika watatokea, watawatenga waovu na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno. Yesu aliwaambia, Mmeyafahamu haya yote? Wakamwambia, Naam, Bwana. Akawaambia, Kwa sababu hii, killa mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoae katika hazina yake vitu vipya na vya kale. Ikawa Yesu alipomaliza mifano hii, akatoka, akaenda zake. Na alipofika inchi yake, akawafundisha katika sunagogi yao, hatta wakashangaa, wakanena, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii? Huyu si mwana wa sermala? mama yake sio yeye aitwae Mariamu? Na ndugu zake Yakobo, na Yose, na Simon, na Yuda? na maumbu yake, wote hawako kwetu? Bassi huyu amepata wapi haya yote? Wakachukizwa nae. Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika inchi yake mwenyewe, na nyumbani mwake mwenyewe. Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao. WAKATI ule Herode tetrarka alisikia khabari za Yesu, akawaambia watumishi wake, Huyu ndiye Yohana Mbatizaji; amefufuka katika wafu; na kwa sababu hii nguvu hizo zinatenda kazi ndani yake. Maana Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodias, mke wa Filipo ndugu yake. Kwa sababu Yohana alimwambia, Ni haramu kwako kukaa uae. Na alipotaka kumwua, aliwaogopa watu, maana walimwona kuwa nabii. Hatta panapo siku kuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodias alicheza kati ya watu, akampendeza Herode. Hatta akakiri kwa kiapo atampa lo lote atakaloliomba. Nae, akishawishwa na mama yake, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. Mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya nyapo zake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja nae, akaamuru apewe; akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani. Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule kijana: akakichukua kwa mama yake. Wanafunzi wake wakaenda, wakauchukua mwili wake, wakauzika; wakaenda wakampasha Yesu khabari. Yesu aliposikia, akatoka huku katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, kwa faragha. Na makutano waliposikia, wakamfuata kwa miguu toka miji yao. Yesu akatoka, akaona makutano mengi, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao. Hatta ilipokuwa jioni, wanafunzi wake wakamwendea, wakanena, Mahali hapa nyika tupu, na saa imekwisha pita; waage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula. Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi kula. Wakamwambia, Hatuna kitu hapa illa mikate mitano na samaki mbili. Akasema, Nileteeni vitu vile hapa. Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akamega, akawapa wanafunzi ile mikate, wanafunzi wakawapa makutano. Wakala wote wakashiba: wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu thenashara, vimejaa. Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto. Marra Yesu akawalazimisha wamifunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ngʼambu, wakati yeye alipokuwa akiwaaga makutano. Alipokwisha kuwaaga makutano, akapanda mlimani kwa faragha, kwenda kusali. Na ilipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho. Hatta zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akitembea juu ya bahari. Wanafunzi walipomwona akitembea juu ya bahari, wakafadhaika, wakinena. Ni kivuli; wakapiga yowe kwa khofu. Marra Yesu akasema nao, akinena, Jipeni moyo; ni mimi; msiogope. Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akatembea juu ya maji, illi kumwendea Yesu. Lakini alipoona upepo wa nguvu, akaogopa: akaanza kuzama, akapiga yowe, akinena, Bwana, niokoe. Marra Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? Walipopanda chomboni, upepo ukakoma. Nao waliokuwa ndani ya chombo wakamwendea, wakamsujudia, wakinena, Hakika wewe u Mwana wa Mungu. Na walipokwisha kuvuka, wakafika inchi ya Genesareti. Na watu wa mahali pale walipomtambua, wakatuma watu kwenda inchi zile zote zilizo kandokando, wakamletea wote waliokuwa hawawezi; wakamsihi waguse hatta pindo la vazi lake; na wote waliogusa wakaponywa kabisa. NDIPO waandishi na Mafarisayo toka Yerusalemi wakamwendea Yesu wakinena, Mbona wanafunizi wako huyakhalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula. Akajibu, akawaambia, Mbona na ninyi huikhalifu amri ya Mungu kwa mapokeo yenu? Kwa kuwa Mungu aliamuru, akisema, Mheshimu baba yako na mama yako; na, Amtukanae baba yake au mama yake na afe. Bali ninyi hunena, Afakaemwambia baba yake au mama yake, Cho chote kikupasacho kufaidiwa nami ni sadaka, asimheshimu baba yake au mama yake, huwa bassi. Mkalitangua neno la Mungu kwa mapokeo yemi. Enyi wanafiki, ni vyema alivyotabiri Isaya katika khabari zenu, akinena, Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao, Na kwa midomo yao huniheshimu; Bali mioyo yao iko mbali yangu. Nao waniabudu ibada ya burre. Wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wana Adamu. Akawaita makutano akawaambia, Sikieni, mfahamu: Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho najis mwana Adamu; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho najis mwana Adamu. Ndipo wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa? Akajibu, akasema, Killa pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni, litangʼolewa. Waacheni hawo; ni vipofu, viongozi wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumhukia shimoni wote wawili. Petro akajibu, akamwambia, Tueleze mfano huo. Yesu akasema, Hatta na ninyi mngali hamna akili? Hamjafahamu bado ya kuwa killa kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni? Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo najis mwana Adamu. Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, mauaji, mazini, asharati, uizi, ushuhuda wa uwongo, na matukano; hayo ndiyo yamtiayo najis mwana Adamu; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mwana Adamu najis. Yesu akatoka huko, akaenda pande za Turo na Sidon. Na mwanamke Mkauanaya wa mipaka ile akatokea, akampaazia sauti, akinena, Unirehemu. Bwana, Mwana wa Daud; binti yangu amepagawa sana na pepo. Nae hakumjibu neno. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakinena. Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. Nae akajibu, akasema, Sikupelekwa illa kwa kondoo zilizopotea za nyumba ya Israeli. Nae akaja akamsujudia, akinena. Bwana, nisaidie. Akajibu akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Akasema, Ndio, Bwana, illakini hatta mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao. Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Ee mwanamke, imani yako kubwa; pata utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile. Yesu akapita huko, akafika kando ya bahari ya Galilaya; akapanda mlimani, akaketi huko. Wakamwendea makutano mengi walio na viwete, vipofu, bubu, vilema, na wengine wengi pamoja nao, wakawaweka miguuni pa Yesu; akawaponya; hatta makutano wakastaajabu, walipowaona bubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli. Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia makutano, kwa kuwa yapata siku tatu wamekaa pamoja nami, hawana kitu cha kula: na kuwaaga wakifunga sitaki, wasije wakazimia njiani. Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hatta kushibisha makutano mengi namna hii? Yesu akawaambia, Mikate mingapi mnayo? Wakasema, Saba, na visamaki vichache. Akawaagiza makutano waketi chini: akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru, akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano. Wakala wote wakashiba: wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, makanda saba, yamejaa. Nao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila wanawake na watoto. Akawaaga makutano, akapanda chomboni, akaenda pande za Magdala. WAKAMJIA Mafarisayo na Masadukayo, wakamjaribu, wakamwomba awaonyeshe ishara itokayo mbinguni. Akajibu, akawaambia, Kukichwa, mwanena, Kutakuwa na kianga: kwa maana uwingu ni mwekundu. Na assubuhi, Leo dhoruba; kwa maana uwingu ni mwekundu, na kumetanda. Enyi wanafiki, mnajua kuutamhua uso wa uwingu; hali ishara za zamani hizi hamziwezi. Kizazi kibaya na cha zina chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya nabii Yunus. Akawaacha, akaenda zake. Wanafunzi wake wakaenda hatta ngʼambu, wakasahau kuchukua mikate. Yesu akawaambia, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masudukayo. Wakabishana wao kwa wao, wakinena, Ni kwa sababu hatukuchukua mikate. Yesu akajua, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani haba, kwa sababu hamkuchukua mikate? Hamjafahamu hado, wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa wale elfu tano, na vikapu vingapi mlivyookota? Wala ile mikate saba kwa wale elfu nne, na makanda mangapi mliyookota? Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si kwa sababu ya mkate naliwaambieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo? Ndipo wakafahamu ya kuwa hakuwaambia kujihadhari na chachu ya mkate, bali elimu ya Mafarisayo na Masadukayo. Yesu akaenda pande za Kaisaria Filipi, akawauliza wanafunzi wake akinena, Watu huninena mimi, Mwana wa Adamu, kuwa nani? Wakasema, Wengine Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaambia, Na ninyi mwaninena mimi kuwa nani? Simon Petro akajibu, akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi. Yesu akajibu, akamwambia, U kheri Simon bar Yunus; kwa kuwa nyama na damu hazikukufunulia haya, bali Baba yangu aliye mbinguni. Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na jun ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; na milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litafungwa mbinguni: na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. Ndipo akawaagiza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu ya kwamba yeye ndiye Yesu aliye Kristo. Toka wakati huo Yesu akaanza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemi, na kuteswa mengi na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akinena, Hasha, Bwana, haya hayatakupata. Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u chukizo kwangu: maana huyawazi mambo ya Mungu, bali yaliyo ya wana Adamu. Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu atakae kuandama nyuma yangu, ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate. Maana mtu atakae kuisalimisha roho yake, ataiangamiza; na mtu atakaeitoa roho yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwa maana atafaidiwa mtu nini akiupata ulimwengu wote, na kupata khasara ya roho yake? au mtu atatoa nini badala ya roho yake? Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake. Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake. NA baada ya siku sita Yesu akawachukua Petro, na Yakobo, na Yohana ndugu yake, akawaleta juu ya mlima mrefu peke yao; akageuka sura yake mbele yao: uso wake ukangʼaa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru. Wakawatokea Musa na Eliya, wakizumgumza nae. Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka tutafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. Alipokuwa akisema, wingu jeupe likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, niliyependezwa nae; msikieni yeye. Na wale wanafunzi waliposikia, wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana. Yesu akaja, akawagusa, akasema, Ondokeni, msiogope. Wakainua macho yao, wasione mtu illa Yesu peke yake. Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaagiza, akinena, Msimwambie mtu khabari ya mambo hayo, hatta Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu. Wanafunzi wake wakamwuliza, wakinena, Mbona bassi waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? Yesu akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, nae atatengeneza yote; lakini nawaambieni, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu nae atateswa nao. Ndipo wakafahamu wale wanafunzi ya kuwa amesema nao khabari za Yohana Mbatizaji. Nao walipoufikia mkutano, mtu akamjia, akampigia magoti, akinena, Bwana, mrehemu mwana wangu, kwa kuwa hushikwa na kifafa, na kuteswa vibaya: maana marra nyingi huanguka motoni, na marra nyingi majini. Nikamleta kwa wanafunzi wako, nao hawakuweza kumponya. Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini na kipotofu, nitakuwa pamoja nanyi hatta lini? Nitachukuliana nanyi hatta lini? Mleteni huku kwangu. Yesu akamkaripia pepo, akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile. Kiisha wale wanafunzi wakaniwendea Yesu kwa feragha, wakasema, Mbona sisi hatukuweza kumfukuza? Yesu akawaambia, Kwa sababu ya kutokuamini kwenu. Kwa maana, amin, nawaambieni, Mkiwa na imani kama punje ya kharadali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa hatta kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. Lakini namna hii haitoki illa kwa kusali na kufunga. Walipokuwa wakikaa Galilaya, Yesu akawaambia, Mwana wa Adamu karibu atatiwa mikononi mwa watu, nao watamwua, na siku ya tatu atafufuka. Wakasikitika sana. Hatta walipofika Kapernaum, wale watozao nussu shekeli wakamwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi nussu shekeli? Akanena, Hutoa. Nae alipoingia nyumbani, Yesu akatangulia kumwuliza, akinena, Waonaje, Simon? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? kwa wana wao au kwa wageni? Petro akamwambia, Kwa wageni. Yesu akamwambia, Bassi, kama ni hivyo, wana ni huru. Lakini tusije tukawachukiza, enenda baharini ukatumbukize ndoana, ukatwae samaki yule azukae kwanza; na ukifunua mdomo wake utaona shekeli; ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako. SAA ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakinena, Ni nani bassi aliye mkuu kafika ufalme wa mbinguni? Yesu akaita kitoto, akamweka katikati yao, akasema, Amin, nawaambieni, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kabisa katika ufalme wa mbinguni. Bassi, ye yote anyenyekeae kama kitoto hiki, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. Na ye yote atakaepokea kitoto kimoja mfano wa hiki kwa jina langu, anipokea mimi: bali atakaekosesha mmoja wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake, na kutoswa katika kilindi cha bahari. Ole wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana buddi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletae jambo la kukosesha! Mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate, ukautupe mbali nawe; ni vyema zaidi kuingia katika uzima umepungukiwa mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele. Na jicho lako likikukosesha, lingʼoe, ukalitupe mbali nawe; ni vyema zaidi kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jebannum ya moto. Angalieni msidharau mmoja wa wadogo hawa; kwa maana nawaambieni ya kwamba malaika zao mbinguni siku zote wanamtazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni. Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea. Mwaonaje? mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je, hawaachi wale tissa na tissaini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea? Hatta akipata kumwona, amin nawaambieni, amfurahia huyu zaidi, kuliko wale tissa na tissaini wasiopotea. Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni mmoja wa wadogo hawa apotee. Na ndugu yako akikutenda dhambi, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu: akikusikia, umempata ndugu yako. La, hakusikia, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, illi kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu killa neno lithubutike. Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa: na asipolisikiliza kanisa pia, na awe sawasawa na mtu wa Mataifa na mtoza ushuru. Amin, nawaambieni, Yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. Tena nawaambieni, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa wawili au watatu walipo wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao. Kiisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu akinitenda dhambi nimsamehe marra ngapi? hatta marra saba? Yesu akamwumbia, Sikuambii hatta marra saba, bali hatta marra sabaini fi saba. Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumisbi wake. Alipoanza kuifanya, akaletewa mtu mmoja awiwae nae talanta elfu kumi. Na asipokuwa na kitu cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni. Bassi yule mtumishi akaanguka, akamsujudia akinena, Bwana, niwie kwa saburi, nami nitakulipa vyote pia. Bwana wa mtumishi yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. Mtumishi yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyewiwa nae dinari mia; akamkamata, akamshika koo, akinena, Nilipe uwiwacho. Bassi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akinena, Niwie kwa saburi, nami nitakulipa vyote pia. Nae hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hatta atakapoilipa ile deni. Bassi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, wakasikitika sana, wakaenda wakamfafanulia bwana wao yote yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumishi mwovu, nalikusamehe deni ile yote, uliponisihi: nawe, je, haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? Bwana wake akaghadhabika, akampeleka kwa watesaji, hatta atakapoilipa deni ile yote. Vivyo hivyo na Baba yangu wa mbinguni atawatenda ninyi, kama ninyi kwa mioyo yenu hamkusamehe killa mtu ndugu yake makosa yake. IKAWA Yesu alipomaliza maneno haya, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Yahudi, ngʼambu ya Yordani. Makutano mengi wakamfuata, akawaponya huko. Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je, ni halali mtu kumwacha mkewe kwa killa sababu? Akajihu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema. Kwa sababu hii, mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe; na hawo wawili watakuwa mwili mmoja? Hatta wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Bassi alivyoviunganisha, Mungu, mwana Adamu asivitenganishe. Wakamwambia, Jinsi gani bassi Musa aliamuru kumpa khati ya talaka, na kumwacha? Akawaambia, Musa kwa sabau ya ugumu wa mioyo yenu aliwapeni ruksa kuwaacha wake zenu: lakini langu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Killa mtu atakaemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya asharati, akaoa mwingine, azini; nae amwoae yule aliyeachwa azini. Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa liivi, haifai kuoa. Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, illa wale waliojaliwa. Maana wako matawashi waliozaliwa katika hali hii toka matumboni mwa mama zao; teua wako matawashi waliofanywa kuwa matawashi na watu: tena wako matawashi waliojifanya kuwa matawashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezae kulipokea neno hili, na alipokee. Ndipo akaletewa vitoto aweke mikono yake juu yao na kuwaombea; wanafunzi wake wakawakemea. Lakini Yesu akasema, Waacheni vitoto, wala msiwakataze kuja kwangu; kwa maana walio mfano wa hawo, ufalme wa mbinguni ni wao. Akaweka mikono yake juu yao, akatoka huko. Mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu mwema, nitende jambo gani jema, illi nipate uzima wa milele? Akamwambia, Ya nini kuniita mwema? Hakuna mwema illa mmoja, ndiye Mungu. Lakini ukitaka kuingia katika nzima, zishike amri. Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudu uwongo, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Yule kijima akamwambia, Haya yote nimeyashika tangu utoto wangu: nimepmigukiwa nini tena? Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze mali zako, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kiisha njoo unifuate. Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali mengi. Yesu akawaambia wanafunzi wake, Amin, nawaambieni, ya kwamba itakuwa shidda tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. Nawaambieni tena, Ni rakhisi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Wanafunzi wake waliposikia, wakashangaa sana, wakinena, Nani bassi awezae kuokoka? Yesu akawatazama, akawaambia, Kwa wana Adamu hili haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana. Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata: tutapata nini bassi? Yesu akamwambia, Amin, nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata, katika zamani za kuzaliwa upya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli. Na killa mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea marra mia, na kurithi uzima wa milele. Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho, wa kwanza. KWA maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba, aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu. Na alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, akawapeleka katika shamba lake la mizabibu. Akatoka muamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi; na hawo nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo liaki nitakupeni. Wakaenda. Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vilevile. Hatta mnamo saa edashara akatoka, akakuta wengine wakisimama wasiokuwa na kazi, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi? Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, Enendeni na ninyi katika shamba la mizabibu, na iliyo haki mtapata. Kulipokuchwa, yule bwana wa mizabibu akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ijara yao, ukianzia wa mwisho hatta wa kwanza. Walipokuja wale wa saa edashara, wakapokea killa mtu dinari. Na wale wa kwanza walipokuja, wakadhani watapokea zaidi; na wao pia wakapokea killa mtu dinari. Wakiisha kupokea, wakamnungʼunikia mwenye nyumba, wakinena, Hawa wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana. Nae akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari? Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe. Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu nipendavyo? Au jicho lako ni ovn kwa sababu ya kuwa mimi mwema? Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza wa mwisho: maana waitwao wengi, hali wateule wachache. Hatta Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalemi, aliwachukua wanafunzi thenashara kwa faragha njiani, akawaambia, Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemi; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa makuhani wakuu na waandishi; nao watamhukumu afe; na watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumsulibi; na siku ya tatu atafufuka. Ndipo mama ya wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akimsujudia, akimwomba neno. Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza hawa wanangu waketi mmoja mkono wako wa kunme; na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako. Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomha. Mwaweza kuuywea kikombe nitakachonywea mimi, na kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi? Wakamwambia, Twaweza. Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu, na mtabatizwa ubatizo nibatizwao mimi; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri niwapeni, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu. Na wale kumi waliposikia, wakawakasirikia wale ndugu wawili. Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wafalme wa Mataifa huwatawala, na wakuu wao huwatumikisha. Lakini kwemi ninyi haitakuwa hivi: bali ye yote atakae kuwa mkuu kwenu, na awe mkhudumu wenu; na ye yote atakae kuwa wa kwanza kwenu awe mtumishi wenu: kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kukhudumiwa, bali kukhudumu, na kutoa roho yake kuwa dia ya wengi. Hatta walipokuwa wakitoka Yeriko mkutano mkubwa wakamfuata. Na vipofu wawili wameketi kando ya njia, nao waliposikia ya kwamba Yesu anapita, wakapaaza sauti zao, wakinena, Uturehemu, Ee Bwana, mwana wa Daud! Makutano wakawakaripia, wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaaza sauti zao, wakinena, Uturehemu, Ee Bwana, mwana wa Daud! Yesu akasimama, akawaita, akasema, Mnataka niwafanyie nini? Wakamwambia, Bwana, macho yetu yafumbuliwe. Yesu akawahurumia, akawagusa macho yao; marra macho yao yakapata kuona, wakamfuata. HATTA walipokaribia Yerusalemi, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu akatuma wanafunzi wawili, akiwaambia, Enendeni zenu hatta kijiji kile kinachowakabili, na marra mtaona punda amefungwa, na mwana punda pamoja nae: mfungueni mkaniletee. Na kama mtu akiwaambieni neno, semeni, Bwana ana haja nao; na marra moja atawapeleka. Haya yote yamepata kuwa, illi litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Mwambieni binti Sayuni, Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, amepanda punda, Na mwana punda, mtoto wa punda. Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru, wakamleta yule punda na mwana punda, wakaweka nguo zao juu yao, wakamketisha. Watu wengi katika makutano wakatandaza nguo zao njiani; wengine wakikata matawi ya miti, wakiyatandaza njiani. Na makutano waliotangulia, na waliofuata, wakapaaza sauti zao, wakinena, Utuokoe sasa, Mwana wa Daud; amebarikiwa ajae kwa jina la Bwana; Utuokoe sasa wewe uliye juu. Hatta alipoingia Yerusalenn, mji wote ukataharuki, nkinena, Ni nani huyu? Makutano wakanena, Huyu ni Yesu, yule nabii wa Nazareti ya Galilaya. Yesu akaingia ndani ya hekalu la Mungu, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa; akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itakwitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi. Vipofu na viwete wakamwendea hekaluni, akawaponya. Lakini makuhani wakuu na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto wakipaaza sauti zao hekaluni, wakinena, Utuokoe sasa, mwana wa Daud! wakakasirika, wakamwambia, Wasikia hawa wanenavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa? Akawaacha, akatoka nje ya mji mpaka Bethania, akalala huko. Hatta assubuhi alipokuwa akirudi mjini, akashikwa na njaa. Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake illa majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hatta milele. Mtini ukauyauka marra moja. Wanafunzi wake walipoona, wakastaajabu, wakinena, Umenyaukaje mtini marra moja? Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambieni, Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hatta mkiuambia mlima huu, Ngʼoka, ukatupwe baharini, itatendeka. Na yo yote mtakayoyaomba katika kusali, mkiamini, mtapokea. Hatta alipokwisha kuingia hekaluni, makuhani wakuu na wazee wa watu wakamwendea alipokuwa akifundisha, wakinena, Kwa mamlaka gani unafanya haya? Na nani aliyekupa mamlaka haya? Yesu akajibu, akawaambia, Nami nitawaulizeni neno moja; mkinijibu, nami nitawaambieni, kwa mamlaka gani ninafanya haya. Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? Ulitoka mbinguni, au kwa wana Adamu? Wakasemezana wao kwa wao, wakinena, Tukisema, Ulitoka mbinguni; atatuambia, Mbona bassi hamkumwamini? Na tukisema, Kwa wana Adamu; twaogopa makutano; maana watu wote wanaona ya kuwa Yohana ni nabii. Wakamjibu Yesu, wakasema, Hatujui. Nae akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi kwa mamlaka gani ninafanya haya. Mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na watoto wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo enenda kufanya kazi katika shamba langu la mizabibu. Akajibu akasema, Sitaki; baadae akatubu, akaenda. Akamwendea yule wa pili, akasema vilevile. Nae akajibu akasema, Nakwenda, Bwana: asiende. Katika hawa wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya baba yake? Wakamwambia, Yule wa kwanza. Yesu akawaambia, Amin, nawaambieni, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, nanyi hamkumwamini; lakini watoza ushuru na makahaha walimwamini: nanyi mlipoona, hamkutuhu haada ya haya, na kumwamini. Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, nae alipanda mizabibu, akazungusha uzio, akachimba shimo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumishi wake kwa wale wakulima, wajiokee matunda yake. Wale wakulima wakawakamata watumishi wake, huyu wakampiga, na mwingine wakamwua, na mwingine wakampiga mawe. Akatuma tena watumishi wengine wengi kuliko wa kwanza, wakawatenda vilevile. Baadae akamtuma mwanawe kwao, akinena, Mwana wangu watamjali. Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. Wakamkamata, wakamtupa uje ya shamba la mizabibu, wakamwua. Bassi atakapokuja yule bwana wa mizabibu, atawatendea nini wale wakulima? Wakamwambia, Atawaangamiza wabaya wale; nae atawapangisha mizabibu wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake. Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hili lilikuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu? Kwa sababu hii nawaambieni, ya kwamba ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, na watapewa taifa lingine wenye kuzaa matunda yake. Nae aangukiae juu ya jiwe hili atavunjikavunjika: nae amhae litamwangukia, litampondaponda. Makuhani wakuu na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, wakatambua ya kuwa anawanena wao. Nao walipotafuta kumkamata, wakawaogopa makutano, kwa maana walimwona kuwa nabii. YESU akajibu, akawaambia tena kwa mifano, akinena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwana wake arusi. Akawatuma watumishi wake wawaite walioalikwa kuja arusini: nao hawakutaka kuja. Akatuma tena watumishi wengine, akinena, Waambieni wale walioalikwa, Tʼazameni nimeandaa karamu yangu: ngʼombe na vinono vimekwisha kuehinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini. Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake: nao waliosalia wakawakamata watumishi wake, wakawatenda jeuri, wakawana. Bassi yule mfalme alipopata khahari, akaghadhabika: akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao. Kisha akawaambia watumishi wake. Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili. Bassi enendeni hatta njia panda za njia kuu, na wote mwaonao waiteni arusini. Watumishi wale wakatoka wakaingia njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu na wema: arusi ikajaa wageni. Alipoingia yule mfalme kuwatazama wageni, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi. Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Akatekewa. Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni miguu na mikono, mchukueni mkamtupe katika giza la nje: ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno. Kwa maana wengi waitwao, wateule wachache. Ndipo Mafarisayo wakaenda zao, wakafauya shauri, jinsi ya kumtega kwa maneno. Wakawatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodiano, wakanena, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, ua njia va Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu, kwa maana hutazami sura za watu. Bassi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, au si halali? Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema, Mbona mnanijaribu, enyi wanafiki? Nionyesheni fedha ya kodi. Nao wakamletea dinari. Akawaambia, Ya nani sanamu hii, na anwani hii? Wakamwambia, Ya Kaisari. Akawaambia, Bassi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu. Waliposikia, wakataajabu, wakamwacha, wakaenda zao. Siku ile Masadukayo, watu wanenao kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza, wakinena, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, nae hana watoto, ndugu yake amwoe mkewe, illi ampatie ndugu yake mzao. Bassi, kwetu palikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia ndugu yake nike wake. Vivyo hivyo wa pili nae, na wa tatu, hatta wote saba. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa nae. Katika kiyama, hassi, atakuwa mke wa nani katika wale saba? Maana wote walikuwa nae. Yesu akajihu, akawaamhia, Mwajidanganya, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu. Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaozwi, bali huwa kama malaika wa Mungu mbinguni. Tena katika khabari ya kiyama ya wafu, hamjaiisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaak, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, hali wa wahayi. Makutano waliposikia, wakashangaa kwa elimu yake. Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, wakakusanyika pamoja. Mmoja wao, mwana sharia, akamwuliza, akimjaribu; akinena, Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Amri ya kwanza na iliyo kuu ndiyo hii. Na ya pili yafanana nayo, ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Amri hizi mbili yazitegemea torati yote nao manabii. Mafarisayo walipokusanyika, Yesu akawauliza, akinena, Mwaonaje katika khabari za Kristo? Yu mwana wa nani? Wakamwambia, Wa Daud. Akawaambia, Imekuwaje bassi Daud katika Roho kumwita Bwana, akinena, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume, Hatta niwawekapo adui zako chini ya miguu yako? Bassi, Daud akimwita Bwana, amekuwaje mwana wake? Hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu tangu siku ile kumwuliza neno tena. KIISHA Yesu akasema na makutano na wanafunzi wake, akinena, Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa: bassi, yo yote watakayowaambieni myashike; yashikeni na kuyatenda: lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende: maana hunena wala hawatendi. Kwa maana hufunga mizigo mizito isiyochukulika na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuisogeza kwa kidole chao. Tena matendo yao yote huyatenda illi kutazamwa na watu: hupanua fulakteria zao, huongeza matamvna ya mavazi yao; hupenda mahali pa mbele katika karamu, na viti vya mbele katika sunagogi, na kusalimiwa sokoni, na kuitwa na watu, Rabbi, Rabbi. Bali ninyi nisiitwe Rabbi; maana mwalimu wenu yu mmoja ndiye Kristo, na ninyi nyote ni ndugu. Wala msimwite mtu baba yenu duniani: maana Baba yeuu yu mmoja, aliye mbinguni. Wala msiitwe wakufunzi; maana mkufunzi wenu yu mmoja, ndiye Kristo. Nae aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. Na ye yote atakaejikuza, atadhiliwa; na ye yote atakaejidhili, atakuzwa. Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, nao wanaoingia hamwaachi waingie. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnazunguka katika bahari na inchi kavu illi kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehannum marra mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe. Ole wenu viongozi vipofu, ninyi mnenao, Mtu atakaeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakaeapa kwa dhababu ya hekalu, amejifunga. Wapumbavu ninyi na vipofu: maana ipi iliyo kubwa, ile dhahabu, au lile hekalu liitakasalo dhababu? Tena, Mtu atakaeapa kwa madhbahu, si kitu; bali mtu atakaeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga. Wapumbavu ninyi na vipofu; maana ipi kubwa, ile sadaka, au ile madhbahu iitakasayo sadaka? Bassi yeye aapae kwa madhbahu, yuapa kwayo na kwa vitu vyote vilivyo juu yake. Nae aapae kwa hekalu, yuapa kwalo, na kwa yeye akaae ndani yake. Nae aapae kwa mbingu, yuapa kwa kiti cha Mungu, na kwa yeye akaae juu yake. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnalipa zaka za mnaana na bizari na kumini, mkaacha mambo makuu ya sharia, hukumu, na rehema, na imani: haya imewapasa kuyafanya, na mengine yale msiyaache. Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa nmasafisha nje ya kikombe na chungu, na ndani yake vimejaa unyangʼanyi na kutoa kuwa na kiasi. Ewe Farisayo kipofu, takasa kwanza ndani ya kikombe na chungu, illi nje yake nayo ipate kuwa safi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa yamepambwa, bali kwa ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, hali kwa ndani mmejaa unafiki na maasi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki? kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki, na kunena, Kama sisi tungalikuwako zamani za haha zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii. Hivi mwajishuhudia nafsi zenu, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowana manabii. Kajazeni kipimo cha baba zenu. Enyi nyoka, mazao wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehannum? Kwa sababu hii, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi: na wengine wao mtawaua na mtawasulibi, na wengine wao mtawapiga katika sunagogi zenu, na mtawafukuza mji kwa mji; illi iwajieni damu yote ya haki iliyomwagika katika inchi, tangu damu ya Habil, yule mwenye haki, hatta damu ya Zakaria, mwana wa Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhbahu, Amin, nawaambieni, Mambo haya yote yatakijia kizazi hiki. Ee Yerusalemi, Yerusalemi, wenye kuwaua manabii, na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! marra ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkukubali! Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa tupu. Kwa maana nawaambieni, Hamtaniona kamwe tangu leo, hatta mtakaposema, Ameharikiwa ajae kwa jina la Bwana. YESU akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea illi kumwonyesha majengo ya hekalu. Yesu akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitahomolewa. Hatta alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakinena, Tuambie, haya yatakuwa lini? Na nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganyeni. Kwa maana wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ni Kristo; na watadanganya wengi. Na mtasikia khabari za vita na uvumi wa vita: angalieni, msitishwe: maana haya hayana buddi kuwa; lakini mwisho wenyewe hado. Maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwako na njaa, na maradhi, na matetemeko ya inchi pahali pahali. Haya yote ni mwanzo wa utungu. Wakati huo watawasaliti ninyi mpate kuteswa, na watawaua; na mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa vote kwa ajili ya jina langu. Ndipo wengi watajikwaa, na watasalitiana, na kuchukiana. Na manabii wengi wa uwongo wataondoka, watadanganya wengi. Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, pendo la watu wengi litapoa. Lakini astahimiliye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka. Na injili hii ya ufalme itakhubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; ndipo ule mwisho utakapokuja. Bassi mlionapo chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama mahali patakatifu (asomae afahamu), ndipo walio katika Yahudi wakimbilie milimani; nae aliye juu ya nyumba asishuke avichukue vitu vilivyomo nyumbani mwake; nae aliye mashamba asirudi nyuma azichukue nguo zake. Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku zile! Ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. Maana wakati ule itakuwapo shidda kubwa, jinsi isivyopata kuwa tangu mwanzo wa ulimweugu hatta leo, wala haitakuwa kamwe. Na kama siku zile zisingalikatizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitakatizwa siku zile. Wakati huo mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko huko, msisadiki. Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule. Angalieni, nimetangulia kuwaambieni. Bassi wakiwaamhieni, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hatta magharibi; hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Maana po potemzoga utakapokuwapo, ndipo tai watakapokusanyika. Marra baada ya shidda ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbingu zitatikisika: ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni: ndipo mataifa yote ya ulimwengu wataomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbingu kwa nguvu pamoja na utukufu mwingi. Nae atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya panda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande mmoja wa mwisho wa mbinguni mpaka upande wa pili. Kwa mtini jifunzeni mfano: tawi lake likiisha kuwa laini na kuchanua majani, mwafahamu ya kuwa wakati wa hari ni karibu; vivyo hivyo na ninyi, myaonapo haya yote, fahamuni ya kuwa yu karibu, tena milangoni. Amin, nawaambieni, Hakitapita kizazi hiki, hatta yatakapokuwa haya yote. Mbingu na inchi zitapita; bali maneno yangu hayatapita kamwe. Na khabari ya siku ile na saa ile hakuna ajuae, hatta malaika walio mbinguni, illa, Baba yangu peke yake. Lakini kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo na kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa maana kama vile siku ziie zilizokuwa kabla ya gharika watu walivyokuwa wakila, wakinywa, wakioa, wakioza, hatta siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hatta gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo na kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Wakati huo watu wawili watakuwa mashamba; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. Kesheni bassi: kwa maana hamwijui saa atakayokuja Bwana wenu. Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angalijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa sababu hii na ninyi mwe tayari; kwa sababu saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja. Nani bassi aliye mtumishi yule amini mwenye haki, ambae bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape chakula kwa saa yake? Yu kheri mtumishi yule, ambae bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivi. Amin, nawaambieni, atamweka juu ya mali zake zote. Bali mtumishi yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; nae akianza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi: bwana wa mtumishi yule atakuja siku asiyotazamia, na saa asiyotambua, atamkata vipande viwili, ataweka sehemu yake pamoja na wanafiki: ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno. NDIPO ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wenye busara, ua watauo wapumbavu. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao: bali wale wenye busara walitwaa na mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Hatta bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala. Hatta usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi anakuja; tokeni kwenda kumlaki. Marra wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakinena, Labuda hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia kwenda kwao wauzao, mkanunue wenyewe. Nao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja nae arusini: mlango ukafungwa. Khalafu wakaja na wale wanawali wengine, wakinena, Bwana, Bwana, utufungulie. Akajibu, akasema, Amin, nawaambieni, siwajui ninyi. Bassi kesheni, maana hamwijui siku wala saa ajapo Mwana wa Adamu. Maana ni mfano wa mtu atakae kusafiri kwenda inchi ya ugeni, aliwaita watumishi wake, akaweka kwao mali zake. Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; killa mtu kwa kadri ya uwezo wake; marra akasafiri. Bassi yule aliyepokea talanta tano akashika njia, akafanya kazi nazo, akachuma talanta nyingine tano. Vilevile na yule mwenye mbili, yeye nae akachuma nyingine mbili faida. Bali yule aliyepokea moja, alikwenda akafukua chini, akaiticha fedha ya bwana wake. Baada ya siku nyingi yuaja bwana wa watumishi wale, akafanya hesabu nao. Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akinena, Bwana, uliweka kwangu talanta tano: tazama, talanta nyingine tano zaidi nilizopatafaida. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema, na amini: ulikuwa amini kwa machache, nitakuweka juu ya mengi: ingia katika furaha ya bwana wako. Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili: tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na amini: ulikuwa amini kwa machache, nitakuweka juu ya mengi: ingia katika furaha ya bwana wako. Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya: nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako chini ya inchi: tazama, unayo iliyo yako. Bwana wake akajibu, akamwambia, Mtumishi mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; bassi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwao wawekao fedha ya watu; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. Bassi, mnyangʼanyeni talanta yake, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. Kwa maana killa aliye na mali atapewa, na kuongezewa: nae asiye nayo, hatta ile aliyo nayo atanyangʼanywa. Na mtumishi yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza ya nje; huko kutakuwa kilio na kusaga meno. Hatta atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja nae, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake: na mataifa yote watakusanyika mbele yake: nae atawabagua kama vile mchunga abaguavyo kondoo na mbuzi: atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu: kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. Ndipo wenye haki watakaponijibu, wakinena, Bwana, lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Lini tulipokuona u mgonjwa, an kifungoni, tukakujia? Na mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambieni. Kadiri mlivyomtendea mmojawapo katika hawo ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Kisha atawaambia na wale walio mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, kwenda katika moto wa milele, aliowekewa tayari Shetani na malaika zake: kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike: nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. Ndipo hawo pia watajibu, wakinena, Bwana, lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikukhudumu? Nae atawajibu, akinena, Amin, nawaambieni, Kadiri msivyomtendea mmojawapo katika hawo walio wadogo, na mimi hamkunitendea. Na hawo watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele: bali wenye haki katika uzima wa milele. IKAWA Yesu alipomaliza maneno haya yote, akawaambia wanafunzi wake, Mwajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa apate kusulibiwa. Ndipo makubani wakuu, na waandishi, na wazee wa watu wakakusanyika katika behewa ya kuhani mkuu aliyeitwa Kayafa; wakafanya shauri pamoja, illi wamkamate Yesu kwa hila na kumwua. Wakanena, Sio wakati wa siku kuu, isije ikatokea ghasia katika watu. Nae Yesu, alipokuwa Bethania katika nyumba ya Simon mwenye ukoma, mwanamke mwenye chombo cha alabastro cha marhamu ya thamani kubwa alimkaribia, akaimimina kichwani pake alipoketi akila. Wanafunzi wake walipoona, wakachukiwa, wakinena, Ya nini upotevu huu? Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa fedha nyingi wakapewa maskini. Yesu akijua akawaambia, Mbona mnamtaabisha mwanamke? Maana ni kazi njema aliyonitendea mimi. Kwa maana siku zote maskini mnao pamoja nanyi; lakini mimi hamnami siku zote. Maana kwa kunimwagia mwili wangu marhamu hii, ametenda hivi illi kuniweka tayari kwa maziko yangu. Amin, nawaambieni, Killa ikhuhiriwapo injili hii katika ulimwengu wote, na hilo alilolitenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake. Kisha mmoja wa wale thenashara, jina lake Yuda Iskariote, alikwenda zake kwa makuhani wakuu, akasema, Nini mtakayonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vijiande thelathini vya fedha. Tokea wakati huo akawa akitafuta nafasi ajiate kumsaliti. Hatta siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi wake wakamwendea Yesu, wakamwambia, Wapi unataka tukuandalie uile pasaka? Akasema, Enendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie, Mwalimu anena, Majira yaugu i karibu; kwako nitafanya pasaka pamoja na wanafunzi wangu. Wanafunzi wakatenda kama Yesu alivyowaagiza, wakaiandaa pasaka. Bassi ilipokuwa jioni akaketi chakulani pamoja na wale thenashara. Walipokuwa wakila, akasema, Amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti. Wakahuzunika sana, wakaanza kumwambia mmoja mmoja, Ni mimi, Bwana? Akajibu, akasema, Yeye aliyetia mkono wake pamoja nami katika sahani, ndiye atakaenisaliti. Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa: lakini ole wake mtu yule ambae Mwana wa Adamu anasalitiwa nae! Ingekuwa kheri kwake mtu yule kama asingalizaliwa. Yuda, yule mwenye kumsaliti, akajibu, akasema, Ni mimi, Rabbi? Akamwambia, Wewe umesema. Walipokuwa wakila, Yesu akatwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ni mwili wangu. Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akinena, Nyweeni nyote hiki; maana hii ni damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu leo nzao huu wa mzabibu, hatta siku ile nitakapounywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu. Walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni. Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu: kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchunga, na kondoo wa kundi watatawanyika. Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitatangulia mbele yenu kwenda Galilaya. Petro akajibu, akamwambia, Wajapochukizwa wote kwa ajili yako, mimi sitachukizwa kabisa. Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, usiku huu kabla ya kuwika jogoo, utanikana marra tatu. Petro akamwambia, Ijaponipasa kufa nawe, sitakukana. Na wanafuuzi wote wakasema vivi hivi. Kiisha Yesu akaenda pamoja nao hatta kiwanja kiitwacho Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa, hatta niende kule nikasali. Akamchukua Petro na wana wawili wa Zebedayo, akaanza kufadhaika, na kuhuzunika moyo. Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkakeshe pamoja nami. Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomba, akinena, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kinipitie; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe. Kisha akawaendea wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! hamkuweza kukesha pamoja nami hatta saa moja? Kesheni, kaombeni, msije mkaingia majaribuni: Roho ina nia njema, bali mwili ni dhaifu. Akaenda tena marra ya pili, akaomba, akinena, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kinipitie nisipokinywa, bassi, mapenzi yako yafanyike. Akaenda, akawakuta wamelala tena; maana macho yao yalikuwa mazito. Akawaacha tena, akaenda akaomba marra ya tatu, akisema maneno yaleyale. Khalafu akawaendea wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa hatta mwisho, kapumzikeni: saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dbambi. Ondokeni, twende zetu. Angalieni, anaenisaliti anakaribia. Hatta alipokuwa akisema, Yuda, mmoja wa wale thenashara akaja, na pamoja nae makutano mengi, wana panga na marungu, wametoka kwa makuhani wakuu na wazee wa watu. Na yeye anaemsaliti amewapa ishara, akinena, Nitakaembusu, ndiye; mkamateni. Marra akamwendea Yesu, akasema, Salam, Rabbi, akambusu sana. Yesu akamwambia, Rafiki, umejia nini? Wakaenda, wakanyosha mikono yao wakamkamata Yesu. Mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake: maana wote washikao upanga, wataangamia kwa upanga. Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu sasa hivi, akaniletea zaidi ya majeshi thenashara ya malaika? Yatatimizwaje bassi maandiko, kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kuwa? Saa ile Yesu akawaambia makutano, Je, mmetoka, mfano wa watu wafukuzao mnyangʼanyi mna panga na marungu, kunitwaa? Killa siku naliketi mbele zenu hekaluni, nikifundisha, wala hamkunikamata. Lakini jambo hili lote limekuwa, illi maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia. Nao waliomkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa kuhani mkuu, walipokuwapo waandishi na wazee wamekusanyika. Na Petro akamfuata kwa mbali hatta behewa ya kuhani mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho. Makuhani wakuu na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa nwongo juu ya Yesu, wapate kumwua; wasipate; na ijapokuwa walitokea mashahidi wa uwongo wengi, hawakupata. Baadae mashahidi wa uwongo wawili wakatokea wakasema, Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu ya Mungu, na kuijenga kwa siku tatu. Kuhani mkuu akasimama akamwambia, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudiani? Lakini Yesu akanyamaza. Kuhani mkuu akamjihu, akamwambia, Nakuapisha Mungu aliye hayi, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu. Yesu akamwambia. Wewe umesema: lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwoua Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu. Marra kuhani mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru: tuna haja gani ya mashahidi wengine? Sasa mmesikia kufuru yake: mwaonaje? Wakajibu, wakasema, Ana sharti ya kufa. Ndipo wakamtemea mate va uso, wakampiga konde; wengine wakampiga makofi, wakinena, Ee Kristo, ni nani aliyekupiga? Na Petro alikuwa ameketi nje behewani: kijakazi kimoja akamwendea, akanena, Wewe nawe ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya. Akakana mbele ya wote, akinena, Sijui unenalo. Alipotoka nje hatta ukumbini, mwanamke mwingine akamwona, akawaambia watu waliokuwa huko, Na huyu nae alikuwa pamoja na Yesu Mnazareti. Akakana tena kwa kiapo, Simjui mtu huyu. Punde kidogo, wale waliosimama karibu wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika na wewe u mmoja wao; maana hatta usemi wako wakutambulisha. Ndipo akaanza kulaani na kuapa, Simjui mtu huyu. Marra akawika jogoo. Petro akalikumbuka lile neno la Yesu aliloambiwa nae, Kabla ya kuwika jogoo, utanikana marra tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi. ILIPOKUWA assubuhi, makuhani wakuu wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumfisha; wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa liwali Pontio Pilato. Ndipo Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akinena, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na khatiya. Wakanena, Bassi, haya yatukhussu nini sisi? Tazama wewe hayo. Akavitupa vile vipande vya fedha katika patakatifu, akaondoka; akaenda, akajinyonga. Makuhani wakuu wakavitwaa vile vipande vya fedha, wakasema, Ni haramu kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa kuwa ni kima cha damu. Wakafanya shauri, wakavitumia kwa kununua konde la mfinyangi liwe mahali pa kuzikia wageni. Kwa hiyo konde lile linakwitwa konde la damu, hatta leo. Ndipo likatimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, Wakavitwaa vipande thelathini vya fedha, kima chake aliyetiwa kima, ambae watu miongoni mwa wana wa Israeli walimtia kima; wakavitumia kwa kununua konde la mfinyangi, kama Bwana alivyoniagiza. Yesu akasimama mbele ya liwali: liwali akamwuliza, akinena, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akamwambia, Wewe wanena. Aliposhitakiwa na makuhani wakuu na wazee, hakujibu hatta neno. Ndipo Pilato akamwambia, Husikii mambo mangapi wanayokushuhudia? Nae hakumjibu hatta kwa neno moja, hatta liwali akataajabu sana. Bassi wakati wa siku kuu liwali desturi yake huwafungulia makutano mfungwa mmoja waliyemtaka. Bassi walikuwa na mfungwa mashuhuri siku zile, jina lake Barabba. Bassi walipokutanika, Pilato akawaambia, Mnataka niwafungulie nani? Barabba, au Yesu aitwae Kristo? Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa husuda. Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki: kwa sababu nimeteswa mengi leo katika udoto kwa ajili yake. Nao makuhani wakuu na wazee wakawashawishi makutano illi wamtake Barabba, na kumwangamiza Yesu. Lakini liwali akajibu, akawaambia, Mnataka niwafungulie nani katika hawo wawili? Wakasema, Barabba. Pilato akawaambia, Bassi, nimtendeni Yesu aitwae Kristo? Wakanena wote, Asulibiwe. Liwali akasema, Kwani? ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakinena, Asulibiwe. Pilato alipoona ya kuwa hafai neno, bali ya kuwa inazidi kuwa ghasia, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya makutano, akasema, Mimi sina khatiya kwa khabari ya damu ya mtu huyu mwenye haki: tazameni hayo ninyi wenyewe. Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu. Ndipo akawafungulia Barabba: na alipokwisha kumpiga Yesu mijeledi, akamtoa apate kusulibiwa. Ndipo askari wa liwali wakamchukua Yesu ndani ya praitorio, wakamkusanyia kikosi kizima. Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu. Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na unyasi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamfanyizia dhihaka, wakinena, Salamu, Mfalme wa Wayahudi! Wakamtemea mate, wakautwaa ule unyasi, wakampiga kichwa. Walipokwisha kumfanyia dhihaka, wakalivua lile vazi, wakamvika nguo zake, wakamchukua kumsulibi. Hatta walipokuwa wakitoka humo, wakakutana na mtu Mkurene, jina lake Simon; huyu wakamtumikisha auchukue msalaba wake. Walipofika mahali paitwapo Golgotha, maana yake, Mahali pa kichwa, wakampa kunywa siki iliyochanganyika na safura; nae alipoonja hakutaka kunywa. Walipokwisha kumsulibi, wakagawa nguo zake, wakipiga kura: illi litimie neno lililonenwa na nabii. Waligawa nguo zangu kati yao, na juu ya vazi langu walipiga kura. Wakaketi, wakamwangalia huko. Wakaweka juu ya kichwa chake mshitaka wake, ulioandikwa, HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI. Ndipo wanyangʼanyi wawili wakasulibiwa pamoja nae, mmoja mkono wake wa kuume, na mmoja mkono wake wa kushoto. Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisatikisa vichwa vyao, wakinena, Ewe ulivunjae hekalu na kuijenga kwa siku tatu, jiponye nafsi yako; ukiwa Mwana wa Mungu, shuka msalahani. Kadhalika ua wale makuhani wakuu wakimdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakinena, Aliponya watu wengine, hawezi kujiponya nafsi yake. Akiwa mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani, naswi tutamwamini. Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kamii akimtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu. Vilevile wa ayangʼanyi nao waliosulibiwa pamoja nae walimshutumu. Tangu saa sita palikuwa giza juu ya inchi yote hatta saa tissa. Na kama saa tissa, Yesu akapaaza sauti yake kwa nguvu akinena, Eli, Eli, lama sabakhthani? maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Baadhi yao waliosimama huko, waliposikia, wakanena, Huyu anamwita Elia. Marra mmoja wao akaenda mbio, akatwaa sifongo, akaijaza siki, akaitia juu ya unyasi, akamnywesha. Wale wengine walinena, Acha; na tuone kwamba Elia anakuja kumponya. Nae Yesu akiisha kupaaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hatta chini: inchi ikatetema; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka; ikafufuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini, baada ya kufufuka kwake, wakaingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi. Bassi yule akida, nao walio pamoja nae wakimwangalia Yesu, walipoliona tetemeko la inchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakinena, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu. Na palikuwa na wanawake wengi huko wakitazama kwa mbali, hawo ndio waliomfuata Yesu toka Galilaya, na kumtumikia. Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yose, na mama yao wana wa Zebedayo. Ilipokuwa jioni akafika mtu tajiri wa Arimathaya, jina lake Yusuf, nae mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu; mtu huyu alimwendea Pilato, akauomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe mwili wake. Yusuf akautwaa mwili, akauzinga katika kitambaa cha kitani safi, akanweka katika kaburi lake jipya, alilolikata mwambani; akafingirisha jiwe kubwa hatta mlango wa kaburi, akaenda zake. Walikuwako hapo Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, wameketi kulielekea kaburi. Hatta siku ya pili, ndiyo iliyo baada ya Maandalio, makuhani wakuu na Mafarisayo wakamkusanyikia Pilato, wakinena, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa hayi bado, Baada ya siku tatu nitafufuka. Bassi amuru kaburi lilindwe sana hatta siku ya tatu; wasije wanafunzi wake usiku wakamwiba, wakawaambia watu, Amefufuka katika wafu: na kosa la mwisho litapita lile la kwanza. Pilato akawaambia, Mna askari: enendeni kalilindeni sana kadiri mjuavyo. Wakenda zao, wakalilinda sana kaburi, wakilitia lile jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi. SABATO ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, akaenda Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, kulitazama kaburi. Na kumbe! palikuwa na tetemeko kubwa la inchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka mbinguni, akakaribia akalifingirisha lile jiwe mbali ya mlango, akaketi juu yake. Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama thuluji. Na kwa kumwogopa walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu. Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnanitafuta Yesu aliyesulibiwa. Hayupo hapa; kwa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni, patazameni mahali alipolazwa Bwana. Shikeni njia upesi, kawaambieni wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu; Tazama, anatangulia mbele yenu kwenda Galilaya; huko mtamwona: haya, nimewaambieni. Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa khofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake khabari. Nao walipokuwa wakienda kuwapasha wanafunzi wake khabari, Yesu akakutana nao, akinena, Salam! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia. Yesu akawaambia, Msiogope: enendeni, mkawaambie ndugu zangu waemle Galilaya, ndiko watakakoniona. Nao walipokuwa wakienda njiani, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha makuhani wakuu khabari za mambo yote yaliyotendeka. Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi, wakinena, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala. Na jambo hili likisikilikana kwa liwali, tutasema nae, nanyi tutawaondoa shaka. Bassi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno lile likaenea katika Wayahudi hatta leo. Na wale wanafunzi edashara wakaenda Galilaya hatta mlima ule aliowaagiza Yesu. Nao walipomwona, wakamsujudia; lakini wengine waliona shaka. Yesu akaja kwao, akasema nao, akinena, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na juu ya dunia. Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: nti tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hatta mwisho wa dunia. Amin. Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu; kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, Angalia, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, Atakaefanyiza njia yako mbele yako. Sauti yake aliae jangwani, Itengenezeni njia ya Bwana, Nyosheni mapito yake. Akatokea Yohana, akibatiza jangwani, na kuukhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Wakamwendea inchi yote ya Yahudi, nao wa Yerusalemi, wakabatizwa nae katika mto Yardani, wakiziungama dhambi zao. Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kimioni mwake, akila nzige na asali ya mwitu. Akakhubiri akinena, Yuaja nyuma yangu aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba sistabili kuinama na kuzifungua kanda za viatu vyake. Mimi naliwabatizeni kwa maji; bali yeye atawabalizeni kwa Roho Mtakatifu. Tena, siku zile, alikuja Yesu kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yardani. Marra akapanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kwa mfano wa hua, akishuka juu yake; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwana wangu mpendwa, ndiwe unipendezae. Marra Roho akamwongoza hatta jangwani. Akawako huko jangwani siku arubaini, akijaribiwa na Shetani; nae alikuwa pamoja na nyama wakali, na malaika walikuwa wakimkhudumia. Hatta baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiikhubiri injili ya ufalme wa Mungu, akineua, Wakati umetimia, na ufalme wa Muugu umekaribia; tubuni, kaiaminim injili. Nae akipita kando ya bahari ya Galilaya, akamwona Simon na Andrea ndugu yake, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. Yesu akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Marra wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. Akaendelea mbele kidogo, akamwona Yakobo wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake, nao pia walikuwa chomboni, wakizitengeneza nyavu zao. Marra akawaita: wakamwacha baba yao Zebedayo ndani ya chombo pamoja na watu wa mshahara, wakaenda, wakamfuata. Wakashika njia hatta Kapernaum; na siku ya sabato akaingia sunagogi, akafundisha. Wakashangaa kwa mafundisho yake; kwa sababu alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka wala si kama waandishi. Palikuwapo katika sunagogi yao mtu mwenye pepo mchafu; akapaaza sauti, akinena, Tʼuna nini nawe, Yesu Mnazareti? umekuja kutuangamiza? Nakutambua wewe, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkaripia, akinena, Fumba kinywa, umtoke. Yule pepo mchafu akamrarua, akalia kwa sauti kuu, akamtoka. Wakashangaa wote hatta wakaulizana, wakinena, Nini hii? Elimu hii mpya ni elimn gani? Maana kwa mamlaka awaamuru pepo wachafu nao wakamtii! Khahari zake zikaenea marra inchi zote kando ya Galilaya. Marra walipotoka katika sunagogi, wakalika nyumbani kwa Simon na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohana. Mama wa mkewe Simon alikuwa kitandani, hawezi homa; marra wakamwambia khahari zake: akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akawakhudumia. Hatta ilipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, wakamletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo. Na mji wote nlikuwa umekusanyika mlangoni. Akaponya wengi waliokuwa na maradhi nyingine nyingine, akafukuza pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua. Hatta alfajiri na mapema sana, akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipo watu akasali huko. Simon ua wenziwe wakamfuata; wakamwona, wakamwambia, Watu wote wanakutafuta. Akawaambia, Twende pengine hatta vijiji vilivyo karibu, nipate kukhubiri na huko; maana kwa hiyo nalitokea. Akawa akikhubiri katika masuuagogi yao, katika inchi yote ya Galilaya, na kufukuza pepo. Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa. Yesu akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika. Marra hiyo ukoma wake ukamwondoka, akatakasika. Akamkataza kwa nguvu, marra akamwondosha, akamwambia, Fahamu, usimpe khabari mtu ye yote, bali enenda zako ukajiouyeshe kwa kuhani ukatoe alivyoamuru Musa kwa kutakasika kwako, illi kuwa ushuhuda kwao. Nae akatoka, akaanza kukhubiri mengi, na kulitangaza lile neno, hatta Yesu asiweze tena kuingia mjini kwa wazi; bali alikuwa nje mabali pasipo watu; wakamwendea kutoka killa pahali. AKAINGIA Kapernaum tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani. Marra wakakusanyika watu wengi isibaki nafasi hatta mlangoni: akasema nao neno lake. Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wane. Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu va makutano, wakaitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakakitelemsha kitanda alichokilalia yule mwenye kupooza. Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, dhambi zako zimeondolewa. Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezae kuondoa dhambi isipokuwa mmoja, ndive Mungu? Marra Yesu akafahamu rohoni mwake kama wanafikiri hivi nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? Vipi vyepesi, kumwambia mwenye kupooza, Dhambi zako zimeondolewa, au kusema, Ondoka, njitwike kitanda chako, ukaenende? Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu ana mamlaka duniani ya kuondoa dbambi (amwambia yule inwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako ukaende nyumbani kwako. Akaondoka marra, akajitwika kitanda chake, akatoka mbele yao wote; hatta wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakinena, Namna hii hatujapata kuyaona kamwe. Akatoka tena, akaenda kando ya bahari, makutano yote wakamwendea, akawafundisha. Hatta alipokuwa akipita akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata. Hatta alipokuwa akila nyumbani mwake, watoza ushuru wengi na wenye dhambi waliketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake: kwa maana walikuwa wengi wakamfuata. Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Kwa nini anakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Yesu aliposikia akawaambia, Wenye afya hawabitaji tabibu bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dbambi wapate kutubu. Wanafunzi wake Yohana nao wa Mafarisayo walikuwa wakifunga: wakaja, wakamwambia, Kwa nini wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wra Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi? Yesu akawaambia, Wana wa arusi wawezaje kufunga maadam Bwana arusi yupo pamoja nao? Maadam Bwana arusi yupo pamoja nao hawawezi kufunga. Lakini siku zitakuja atakapoondolewa Bwana arusi, ndipo watakapofunga siku zile. Hakuna mtu ashonae kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu: ikiwa ashona, kile kipya kilicholiwa huliharibu lile vazi kuukuu, na pale palipolatuka huzidi. Wala hapana mtu atiae divai mpya katika viriba vikuukuu: ikiwa atia, ile divai nipya itavipasua viriba vile, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika. Bali hutia divai mpya katika viriba vipya. Hatta alipokuwa akipita katika makonde siku ya sabato, wanafunzi wake wakaanza kuendelea wakivunja masuke. Mafarisayo wakamwambia, Tazama, mbona wanatenda lisilo halali siku ya sabato? Akawaambia, Hamkusoma kabisa alivyofanya Daud, alipokuwa ana haja, akaona njaa, yeye na wenziwe? Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, zamani za kuhani mkuu Abiatbar, akaila mikate iliyotolewa kwa Mungu, isiyo halali kuliwa illa na makuhani, akawapa na wenziwe? Akawaambia, Sabato ilikuwa kwa ajili ya mwana Adamu, si mwana Adamu kwa ajili ya sabato. Bassi yeye aliye Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato. AKAINGIA tena katika sunagogi: na palikuwako huko mtu mwenye mkono umepooza: wakamvizia kuona kwamba atampotiya siku ya sabato: wapate kumshitaki. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati. Akawaambia, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? kuokoa roho au kuua? Wakanyamaza. Akawakazia macho pande zote kwa ghadhabu, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu. Nyosha mkono wako. Akaunyosha: mkono wake ukapona ukawa mzima kama wa pili: marra wakaloka wale Mafarisayo, wakamfanyia shauri pamoja na Maherodiano jinsi ya kumwangamiza. Yesu akajitenga, yeye na wanafunzi wake, akaenda baharini. Watu wengi sana wakamfuata toka Galilaya, na toka Yahudi, na toka Yerusalemi, na toka Idumaya, na ngʼambu ya Yardani, na pande za Turo na Sidon, mkutano mkuu, waliposikia khabari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda; wakamwendea. Akawaambia wanafunzi wake ya kama chombo kidogo kikae karibu nae, kwa sababu ya makutano, wasije wakamsonga. Maana aliponya wengi, hatta wote waliokuwa na misiba wakamrukia wapate kumgusa. Na pepo wachafu, killa walipomwona, wahanguka mbele yake, wakalia wakinena, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu. Akawagombeza sana, wasimdhihirishe. Akapanda mlimani, akawaita aliowataka mwenyewe; wakamwendea. Akaweka thenashara, wapate kuwa pamoja nae, na kusudi awatume kukhubiri, na wawe na mamlaka ya kufukuza pepo. Na Simon akampa jina, Petro; na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake Yakobo, akawapa jina, Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo, na Andrea, na Filipo, na Bartolomayo, na Mattayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thaddayo na Simon Mkanani, na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti. Kiisha wakaingia nyumbani; makutano wakakusanyika tena, wao wenyewe wasiweze kula hatta mkate. Jamaa zake walipopata khabari wakatoka kwenda kumkamata: maana walinena, Amerukwa na akili. Waandishi walioshuka kutoka Yahudi wakanena, Ana Beelzebul, na kwa uwezo wa mkuu wa pepo awafukuza pepo. Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumfukuza Shetani? Na ufalme nkilitinika juu ya nafsi yake ufalme ule hauwezi kusimama; na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba ile haiwezi kusimama. Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake akafitinika, hawezi kusimama, bali ana kikomo. Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake. Amin, nawaambieni, Dbambi zote watasamehewa wana Adamu, na kufuru zao watakazokufuru zote; bali mtu atakaemkufuru Roho Mtakatifu hana masamaha hatta milele; bali atakuwa ana dhambi ya milele; kwa vile walivyonena, Ana pepo mchafu. Wakaja mama yake na ndugu zake; wakasimama nje, wakamtuma mtu kumwita. Na makutano walikuwa wameketi, wakimzunguka; wakamwambia, Mama yako, na ndugu zako wako nje, wanakutafuta. Akawajibu, akinena, Mama yangu na ndugu zangu ni nani? Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote, akanena, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu. Kwa maana mtu ye yote atakaeyafanya mapenzi ya Mungu, huyu ndive ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu. AKAANZA kufundisha tena kando ya bahari. Wakamkusanyikia mkutano mkuliwa, hatta yeye akapanda chomboni, akakaa baharini; mkutano wote ulikuwako katika inchi kavu kando ya bahari. Akawafundisha mengi kwa mifano, akawaambia katika mafundisho yake, Sikilizeni: Mpanzi alitoka kwenda kupanda; ikawa alipokuwa akipanda, baadhi ya mbegu zikaangukia njiani, wakaja ndege wakazila. Nyingine zikaanguka penye mwamba, pasipokuwa na udongo mwingi; marra zikamea kwa kuwa na udongo haba; hatta jua lilipoznka zikaungua, na kwa kuwa hazina mizizi zikakauka. Nyingine zikaanguka penye miiba: ile miiba ikakua, ikazisonga, zisizae matunda. Nyingine zikaanguka panapo udongo ulio mzuri, zikazaa matunda, zikimea na kukua, na kuzaa, moja thelathini, moja sittini, na moja mia. Akanena, Aliye na masikio ya kusikilia, na asikie. Alipokuwa peke yake, watu waliomzunguka, na wale thenashara wakamwuliza khabari za ule mfano. Akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu; hali wale walio nje yote huwawia kwa mifano, illi wakitazama watazame, wasione; na wakisikia wasikie, wasifahamu; wasije wakageuka, wakasamehewa dbambi zao. Askawaambia, Hamjui mfano huu? Bassi mifano yote mtaitambuaje? Mpanzi yule hulipanda neno. Hawa ndio walio njiani, lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, marra huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao. Kadhalika na hawa ndio wapandwao penye mwamba, ambao kwamba wakiisha kulisikia lile neno, marra hulipokea kwa furaha; waki hawana mizizi ndani yao, hali hudumu muda mehache; kiisha ikitokea shidda au udhia kwa sababu ya lile neno, marra huchukizwa. Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba, ni watu walisikiao lile neno, na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai. Na hawa ndio waliopandwa panapo udongo mzuri; ni watu walisikiao lile neno na kulipokea, na kuzaa matunda, moja thelathini, moja sittini, na moja mia. Akawaambia, Mwaonaje? Taa huletwa illi kutiwa ehini ya kikapu, au ehini ya kitanda? si kutiwa juu ya kibao cha kuwekea taa? Kwa maana hakuna neno lililostirika, illa kusudi lije likadhihirika; wala halikuwa siri, illa kusudi lije likatokea dhahiri. Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie. Akawaambia, Tafakarini msikialo, kipimo mpimacho mtapimiwa kile kile, na bado mtazidishiwa. Kwa maana mtu aliye na kitu atapewa, nae asiye na kitu, hatta kile alicho nacho ataondolewa. Akanena, Ufalme wa Mungu, mithili yake ni mtu aliyemwaga mbegu juu ya inchi: akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikimea na kukua, asivyojua yeye. Maana inchi huzaa yenyewe, kwanza jani, tena suke, kiisha nganu mpevu katika suke. Hatta matunda yakiiva, marra aupeleka mundu kwa kuwa mavuno yamewadia. Akanena, Tuulinganishe na nini ufalme wa Mungu? au tuutie katika mfano gani? Ni kama punje ya kharadali ambayo, ipandwapo katika inchi, ni ndogo kuliko mbegu zote zilizo katika inchi, na ikiisha kupandwa, hukua, ikawa kubwa kuliko miti yote ya mboga, ikifanya matawi makuhwa; hatta ndege za anga waweza kukaa chini ya uvuli wake. Kwa mifano mingi ya namna hii alikuwa akisema nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza kusikia; wala pasipo mfano hakusema nao: akawaeleza wanafunzi wake mambo yote kwa faragha. Siku ile ilipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke hatta ngʼambu. Wakawaacha makutano, wakamchukua vile vile katika chomho kile kile. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja nae. Ikatokea dharuba kuu ya npepo, mawimbi yakapiga chombo hatta kikaanza kujaa maji. Yeye mwenyewe alikuwa katika shetri, amelala juu ya mto: wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunapotea? Akaamka: akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, tulia. Upepo nkakoma, kukuwa shwari kuu. Akawaambia, Mbona mu waoga? Hamna imani bado? Wakaingizwa na khofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, bassi, hatta upepo na bahari zamtii? WAKAFIKA ngʼambu ya bahari hatta inchi ya Wageraseni. Na alipokwisha kushuka chomboni, marra akakutwa na mtu ambae ametoka makaburini, nae ana pepo mchafu, makao yake yalikuwa pale makaburini: wala hakuna mtu aliyeweza kumfunga, hatta kwa minyororo: kwa sababu alikuwa amefungwa marra nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunjavunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. Na siku zote, usiku na mchana, alikuwa makaburini na milimani, akilia na kujikata kwa mawe. Alipomwona Yesu kwa mbali, akampiga mbio, akamsujudia; akalia kwa sauti kuu akanena, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi, uniapie kwa Mungu kwamba hutaniadhibu. Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. Akamwambia, Jina lako nani? Akajibu, akamwambia, Jina langu Legioni: kwa kuwa tu wengi. Akamsihi sana asiwapeleke nje ya incbi ile. Na pale milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, walisha. Pepo wote wakamsihi, wakinena, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao. Akawapa rukhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale ngumwe: kundi lote likatelemka kwa kassi gengeni, wakaingia baharini; walikuwa wapata elfeen; wakafa baharini. Wachungaji wa wale nguruwe wakakimbia wakaeneza khahari mjini na mashamba. Wakatoka waone khabari iliyotukia. Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, nae ndiye aliyekuwa na ile legione; wakaogopa. Nao walioona wakaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na khabari za nguruwe. Wakaanza kumsihi atoke katika mipaka yao. Alipokuwa akipanda chomboni, yule aliyekuwa na pepo akamsihi awe pamoja nae: Yesu hakumrukhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawakhubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu. Akaenda zake, akaanza kukhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakataajabu. Hatta Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ngʼambu katika kile chombo, wakamkusanyikia makutano mengi: nae alikuwa kando ya bahari. Kumbe! akaja mtu mmoja katika wakuu wa sunagogi, jina lake Yairo: hatta alipomwona, akaanguka miguuni pake, akimsihi sana, akinena. Binti yangu mdogo yu katika kufa: nakuomba nje, nweke mkono wako juu yake, apate kupona, nae ataishi. Akaenda pamoja nae: makutano mengi wakamfuata, wakimsongasonga. Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka thenashara, na kuteswa mengi kwa mikono ya tabibu wengi, akagharimu vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hatta kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya, bassi aliposikia khabari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; maana alinena, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona. Marra chemchemi ya damu yake ikakauka, akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule. Marra Yesu akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya makutano, akanena, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu? Wanafunzi wake wakamwambia, Wawaona makutano wanavyokusongasonga, nawe wanena, Ni nani aliyenigusa? Akatazama pande zote illi amwone yule aliyelitenda neno hili. Na yule mwanamke akaingiwa na khofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote. Akamwambia, Binti imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, ukawe mzima, usiwe na msiba wako tena. Hatta alipokuwa akisema wakaja watu kutoka kwa mkuu wa sunagogi, wakinena, Binti yako amekwisha kufa: ya nini kuzidi kumsumbua mwalimu? Yesu, marra alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sunagogi, Usiogope, amini tu. Wala hakumrukhusu mtu afuatane nae, illa Petro, na Yakobo, na Yohana ndugu yake Yakobo. Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sunagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo mengi. Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Mtoto hakufa, bali amelala tu. Wakamcheka sana. Nae alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa baba yake yule mtoto na mama yake, na wale walio pamoja nae, akaingia ndani alimokuwamo yule mtoto. Akamshika mkono yule kijana, akamwambla, Talitha, kumi: tafsiri yake, Kijana, nakuambia, Ondoka. Marra akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata miaka thenashara. Wakashangaa mshangao mwingi. Akawaagiza sana, mtu asijue khabari ile; akaamuru apewe chakula. AKATOKA huko, akafika hatta inchi ya kwao: wanafunzi wake wakamfuata. Ilipokuwa sabato, akaanza kufundisha katika sunagogi: wengi wakisikia, wakashangaa, akinena, Huyu amepata wapi haya? Na, Hekima gani hii aliyopewa huyu, na nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? Huyu si yule sermala, mwana wa Mariamu, na ndugu wii Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simon? na ndugu zake wanawake hawapo hapa petu? Wakachukizwa nae. Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, illa katika inchi yake, na kwa jamaa zake, na katika nyumba yake. Wala hakuweza kufanya mwujiza wo wote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya. Akastaajahu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazungukazunguka katika vile vijiji, akifundisha. Akawaita wale thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili; akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu: akawaagiza wasichukue kitu cha njiani isipokuwa gongo tu, wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni: lakini wajifungie viatu; akasema, Msivae kanzu mbili. Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hatta mtakapotoka mahali pale. Na watu wote wasiokaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakungʼuteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu kuwa ushuhuda kwao. Wakatoka, wakakhubiri kwamba watu watubu. Wakafukuza pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagoujwa, wakawaponya. Mfalme Herode akasikia khabari; kwa maana jina lake limepata kutangaa, akanena, Yohana Mbatizaji amefufuka, na kwa hiyo nguvu hizi zinatenda kazi ndani yake. Wengine walinena, Yu Eliya. Wengine walinena, Huyu ni nabii au kama mmoja wa manabii. Lakini Herode aliposikia, alinena, Huyu ndiye Yohana, niliyemkata kichwa; amefufuka. Kwa maana Herode mwenyewe alikuwa ametuma wata, akamkamata Yohana, akamfunga gerezani, kwa ajili va Herodias, nikewe Filipo ndugu yake: kwa kuwa amemwoa; bassi Yohana alimwambia Herode, Si halali kwako kuwa na mke wa ndugu yako. Bassi yule Herodias akawa akimvizia, akataka kumwua, asipate. Maana Herode alimwogopa Yohana: hatta akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamhami, na alipokwisha kumsikiliza alifanya mambo mengi: nae alikuwa akimsikiliza kwa furaha. Hatta ilipotokea siku ya kufaa, na Herode (siku kuu ya kuzaliwa kwake) alipowafanyia karamu masheki na majemadari na watu wakubwa wa Galilaya, ndipo binti yake yule Herodias akaingia, akacheza, akampendeza Herode nao walioketi pamoja nae karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lo lote utakalo, nitakupa. Akamwambia, Lo lote utakaloniomba, nitakupa hatta nussu ya ufalme wangu. Akatoka, akamwambia mama yake, Niombe nini? Akasema, Kichwa cha Yohana Mbatizaji. Marra akaingia kwa haraka mbele ya mfalme akaomba akinena, Nataka unipe sasa hivi katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. Mfalme akafanya huzuni sana, lakini kwa ajili ya nyapo zake, na kwa ajili yao walioketi karamuni, hakutaka kumkataa. Marra mfalme akatuma askari, akiamuru kuleta kichwa chake. Akaenenda, akamkata kichwa mle gerezani, akaleta kichwa chake katika kombe, akampa yule kijana, yule kijana akampa mama yake. Wauafunzi wake waliposikia khabari, wakaenda, wakachukua mayiti yake, wakamzika. Na mitume wakakusanyika mbele ya Yesu; wakampa khabari za mambo yote waliyoyafanya na mambo yote waliyoyafundisha. Akawaambia, Njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipo watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hatta haikuwapo nafasi ya kula. Wakaenda zao chomboni, mahali pasipo watu, kwa faragha. Watu wakawaona wakienda zao, wengi wakamtambua, wakaenda huko mbio, toka miji yote, wakatanguha kufika, wakakusanyika mbele yake. Yesu aliposhuka chomboni, akaona makutano mengi, akawahurumia, kwa sababu walikuwa kana kondoo wasio mchunga; akaanza kuwafundisha mengi. Hatta zikapita saa nyingi za mchana, ikawa karibu na magharibi, wanafunzi wake wakamwendea, wakasema, Mahali hapa nyika tupu, na sasa kunakuchwa; uwaage watu hawa, illi waende zao mashambani na vijijini huko na huko, wakajinunulie chakula. Akajibu, akawaambia, Wapeni ninyi chakula: Wakamwambia, Je! twende zetu tukanunue mikate ya dinari miateen tukawape kula? Akawaambia, Mikale mingapi mnayo? Enendeni mkatazame. Walipokwisha kujua wakanena, Mitano, na samaki mbili. Akawaagiza wawaketishe wote, vikao vikao, penye majani mabiehi. Wakaketi kwa safu, nyingine mia, nyingine khamsimi. Akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama mbinguni, akavibariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake awaandikie: na zile samaki mbili akawagawia wote. Wakala wote wakashiba. Wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu thenashara: navyo vipande vya samaki. Na wanaume walioila ile mikate wapata elfu tano. Marra akawashurutisha wanafunzi wake wapande chomboni, watangulie kwenda ngʼambu hatta Betsaida wakati yeye alipokuwa akiwaaga makutano. Hatta alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kusali. Ilipokuwa jioni chombo kilikuwa kati ya bahari, na yeye peke yake katika inchi kavu. Akawaona wakitaahika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa wa mbisho; hatta yapata zamu ya nne ya usiku akawaendea akitemhea juu ya bahari; akataka kuwdpita. Nao walipomwoua anatembea juu ya bahari walidhani ya kuwa ni kivuli, wakapiga yowe, kwa sababu wote walimwona, wakafadhaika. Marra akasema nao, akawaambia, Jipeni moyo: ni mimi msiogope. Akapanda mle cbomboni walimo; npepo ukakoma; wakashangaa sana, kupita kiasi, wakastaajabu; kwa maana hawakufahamu khabari za ile mikate, walakini mioyo yao ilikuwa migumu. Hatta walipokwisha kuvuka wakafika inchi ya Genesareti, wakatia nanga. Na wakiisha kutoka chomboni, marra watu walimtambua, wakaenda mbio, wakizunguka inchi ile yote, wakaanza kuwachukua walio hawawezi vitandani, kwenda killa mahali waliposikia kwamba yupo. Na killa alikokwenda, akiingia vijijini, au mijini, au mashambani, wakawaweka wagonjwa sokoni, wakamsihi waguse walao upindo wa vazi lake: nao wote waliomgusa wakapona. KIISHA Mafarisayo na baadhi ya waandishi waliotoka Yerusalemi wakakusanyika mbele yake, wakaona baadhi ya wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najis, yaani, yasiyonawiwa, wakawalaumu. Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono kwanza, hawali, wakishika hadithi za wazee wao: tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyushika kama vile kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba na meza. Bassi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuzifuata hadithi za wazee, bali hula chakula kwa mikono najis? Akawaambia, Isaya aliwakhubiri vema ninyi wanaliki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa hunibeshimu kwa midomo, Bali mioyo yao iko mbali nami; Lakini waniabudu ibada ya burre, Wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wana Adamu. Kwa maana mmeiacha amri ya Mungu, na kuzishika hadithi za wana Adamu, kuosha midumu na vikombe: na mengine mengi ya namna hii mwayafanya. Akawaambia, Mwaikataa vema amri ya Mungu mpate kushika hadithi zenu. Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanae baba yake au mama yake na afe. Bali ninyi hunena, Mtu akimwambia baba yake au mama yake, Ni Korban (yaani kimewekwa wakfu) kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho: wala hamrukhusu baada ya hayo kumtendea neno baba yake wala mama yake; mkilitangua neno la Mungu kwa hadithi yenu mliyohadithia; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo. Akawaita makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote, fahamuni. Hapana kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia najis, bali vimtokayo, ndivyo vimtiavyo najis yule mtu. Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie. Hatta alipoingia nyumbani, amewaacha makutano, wanafunzi wake wakamwuliza khabari za ule mfano. Akawaambia, Hivi na ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kuwa killa kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia najis; kwa sababu hakimwingii moyoni, illa tumboni tu; kiisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote. Akanena, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho najis. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, zina, asharati, wizi, uuaji, tamaa mbaya, hila, jeuri, kijicho, matukano, kiburi, upumbafu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu najis. Akaondoka huko, akaenda zake hatta mipaka ya Turo na Sidon. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kustirika. Kwa sababu mwanamke, ambae binti yake yuna pepo mchafu, alisikia khabari zake, akaja akamwangukia miguu. (Na vule mwanamke ni Myunani, kabila yake Msurofenissa). Akamwomba amfukuze pepo katika binti yake. Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza: maana si vema kukitwaa chakula cha watoto, na kuwatupia mbwa. Nae akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hatta mbwa chini ya meza hula makombo ya watoto. Akamwambia, Kwa sababu ya neno hilo, nenda zako; pepo amemtoka binti yako. Akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta yule kijana amelazwa kitandani, na yule pepo amekwisha kumtoka. Akatoka tena katika mipaka ya Turo akapita katikati ya Sidon, akaenda hatta bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli. Wakamletea kiziwi, nae ana kigugumizi, wakamsihi aweke mikono yake juu yake. Akamtenga na makutano kwa faragha, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa nlimi, akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Effatha, maana yake, Funguka! Marra masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri. Akawaagiza wasimwambie mtu; lakini kwa kadiri alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza khabari, wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena, Ametenda yote vizuri; viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme. TENA siku zile, kwa kuwa mengi mno makutano, nao hawana kitu cha kula, Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Nawahurumia makutano kwa sababu yapata siku tatu wamekaa nami, wala hawana kitu cha kula: hatta nikiwaaga waende zao nyumbani kwao wanafunga, watazimia njiani: na baadhi yao wametoka mbali. Wanafunzi wake wakamjibu, Atawezaje mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani? Akawauliza, Mikate mingapi mnayo? Wakasenia, Saba. Akawaagiza makutano waketi chini: akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandalie: wakawaandalia makutano, Walikuwa na visamaki vichache; akavibariki, akasema, na hivi waviandae. Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba. Na watu waliokula wapata elfu nne. Akawaaga. Marra akapanda chomboni pamoja na wanafunzi wake, akaenda pande za Dalmanutha. Wakatokea Mafarisayo wakaanza kuhujiana nae; wakitafuta kwake ishara itokayo mbinguni; wakimjaribu. Akaugua rohoni mwake, akanena, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki. Akawaacha, akapanda tena chomboni, akaenda zake hatta ngʼambu. Wakasahan kuchukua mikate, wala chomboni hawana illa mkate mmoja tu. Akawaagiza, akisema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode. Wakabishana wao kwa wao, kwa kuwa hawana mikate. Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana kwa sababu hamna mikate? Hamfahamu bado, wala hamjaelewa? Mioyo yenu i migumu hatta sasa? Mna macho, hamwoni; mna masikio, hamsikii? wala hamkumbuki? Nilipoimega ile mikate mitano na kuwapa wale elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vimejaa vipande? Wakamwambia, Thenashara. Na ile saba kuwapa wale elfu nne, mlichukua makanda mangapi yamejaa vipande? Wakamwambia, Saba. Akawaambia, Imekuwaje hamjafahamu? Wakalika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse. Akamshika mkono vule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akaweka mikono yake juu yake, akamwuliza, Waona kitu? Akatazama juu, akanena, Naona watu kama miti, inakwenda. Ndipo akaweka mkono wake juu yake marra ya pili machoni mwake, akamwagiza atazame juu; akapata kuwa mzima, akaona wote waziwazi, wajapokuwa mbali. Akampeleka nyumbani kwake, akinena, Usiingie mjini, wala usiseme na mtu mjini. Akatoka Yesu na wanafunzi wake wakaenda vijiji vya Kaisaria ya Filipo: hatta njiani akawauliza wanafunzi wake, akiwaambia, Watu huninena mimi ni nani? Wakamjibu, Yohana Mbatizaji; wengine Eliya; wengine mmojawapo wa manabii. Yeye akawauliza, Na ninyi mnasema ya kuwa mimi ni nani? Petro akamjibu akamwambia, Wewe ndiwe Kristo. Akawaagiza wasimwambie mtu khabari zake. Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na makuhani, wakuu na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka. Petro akamchukua akaanza kumkemea. Akageuka akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akinena, Enenda zako nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, hali ya wana Adamu. Akawaita makutano na wanafunzi wake, akawaambia, Atakae kuniandama na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa maana atakae kuisalimisha roho yake, ataiangamiza, na mtu atakaeitoa roho yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya injili, huyu ataisalimisha. Maana itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote akapata khasara ya roho yake? Ama mtu atoe nini badala ya roho yake? Maana killa mtu atakaenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha zina na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya yeye atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu. AKAWAAMBIA, Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa ambao hawataonja mauti hatta watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu. Hatta baada ya siku sita Yesu akawachukua Petro, na Yakobo, na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu kwa faragha peke yao: akageuka sura yake mbele yao: mavazi yake yakawa yakimetameta, meupe kwa mfano wa thuluji, jinsi asivyoweza fundi duniani kuyafanya meupe. Wakatokewa na Eliya pamoja na Musa, nao walikuwa wakisemezana na Yesu. Petro akajibu, akamwambia Yesu, Rabbi, ni vizuri sisi kuwapo hapa: na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, na kimoja eha Eliya. Maana yake hakujua la kunena, kwa kuwa waliingiwa na khofu nyingi. Likawako wingu, likawatia uvuli: sauti ikatoka katika lile wingu, Huyu ui Mwana wangu, mpendwa wangu, msikieni yeye. Na marra hiyo walipotazama huku na huku, hawakumwona mtu, illa Yesu peke yake pamoja nao. Walipokuwa wakishuka mlimani akawaagiza wasimweleze mtu waliyoyaona, illa Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka katika wafu. Wakalishika neno lile, wakiulizana wao kwa wao, Huku kufufuka katika wafu maana yake nini? Wakamhoji, wakinena, Waandishi wanena ya kuwa imempasa Eliya kuja kwanza. Akajihu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kutengeneza yote; lakini, pamoja na haya ameandikwaje Mwana wa Adamu ya kwamba atateswa mengi na kudharanliwa? Lakini nawaambieni, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtenda yote waliyoyataka kama alivyoandikiwa. Hatta alipowafikia wanafunzi wake, akaona makutano mengi wakiwazunguka na waandishi wakijadiliana nao; marra makutano yote wakimwona wakashangaa wakamwendea mbio, wakamsalimu. Akawauliza wale waandishi, Nini mnajadiliana nao? Mtu mmoja katika makutano akamjibu, Nalimieta mwana wangu kwako, ana pepo bubu: na killa ampagaapo, humrarua: nikasema na wanafunzi wako wapate kumfukuza, wasiweze. Akamjibu, akanena, Ee kizazi kisichoamini, niwe kwenu hatta lini? nichukuliane nanyi hatta lini? Mleteni kwangu. Wakanileta kwake: hatta alipomwona marra yule pepo akamrarua: akaanguka chini, akagaagaa, akitoka povu. Akamwuliza baba yake, Tangu wakati gani amepatwa na haya? Akasema, Tangu utoto. Na marra nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno, utuhurumie, utusaidie. Yesu akamwambia, Ukiweza kuamini: yote yawezekana kwake aaminiye. Marra baba yake yule kijana akapaaza sauti, machozi yakimtoka, akanena, Naamini, Bwana, nisaidie kutokuamini kwangu. Nae Yesu akiona ya kuwa makutano yanakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu ua kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke, wala usimwingie tena. Akalia, akamrarua sana, akamtoka: akawa kama amekufa: hatta wengi wakasema, Amekufa. Lakini Yesu akamshika mkouo akamwinua; nae akasimama. Hatta alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumfukuza? Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kusali na kufunga. Wakatoka huko, wakapita kati kati ya Galilaya: nae hakutaka mtu ajue. Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akiwaambia ya kwamba Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; hatta akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka. Nao hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza. Wakafika Kapernaum: hatta alipokuwa nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani? Wakanyamaza. Kwa maana walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa. Akaketi chini akawaita wathenashara akawaambia, Mtu atakae kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mkhudumu wa wote. Akatwaa kitoto, akamweka kati kati yao, akamkumbatia, akawaambia, Mtu akimpokea kitoto kimoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi: na mtu akinipokea mimi, hanipokei mimi, bali yeye aliyenituma. Yohana akamjibu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akifukuza pepo kwa jina lako, nae hatufuati sisi: tukamkataza, kwa sababu hatufuati sisi. Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakaefanya mwujiza kwa jina langu akaweza wakati huo huo kuninena mabaya; kwa sababu asiye kiuyume chetu, ni upande wetu. Kwa kuwa ye yote atakaewanywesha ninyi kikombe cha maji kwa jina langu, kwa kuwa ninyi watu wa Kristo, amin nawaambieni hatakosa thawabu yake. Na ye yote atakaemkosesha mmoja katika wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini. Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni kheri kuiingia katika uzima u kilema, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehannum, kwenye moto usiozimika; ambao funza wao hafi, wala moto hauzimiki. Na mguu wako ukikukosesha, ukate: ni kheri kuingia katika uzima, umepungukiwa mguu, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jebannum, katika moto usiozimika; ambao funza wao hafi, wala moto hauzimiki. Na jicho lako likikukosesha, litupe: ni kheri kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehannum ya moto: ambapo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. Kwa sababu killa mtu atatiwa chumvi kwa moto, na killa dhabihu itatiwa chumvi kwa chumvi. Chumvi ni njema; lakini chumvi ikitokwa na ladhdha yake, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi. AKAONDOKA huko akafika mipaka ya Yahudi kwa niia ya ngʼambu ya Yardani; watu wengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea. Mafa risayo wakamwendea, wakamwuliza, Ni balali mtu kumwaeha mkewe? wakimjaribu. Nae akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini? Wakasema, Musa alitoa rukhusa kuandika khati ya talaka na kumwacha. Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yemi aliwaandikia amri hii. Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, Mungu aliwafanya mtu mume na mtu mke. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe: na hawo wawili watakuwa mwili mmoja; hatta wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Bassi alivyoviunganisha Mungu, mwana Adamu asivitenganishe. Hatta nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza khabari ya neno hilohilo. Akawaambia, Killa mtu atakaemwacha mkewe na kuoa mwingine azini na kumkosa: na mke, akimwacha mume wake na kuolewa na mtu mwingine, azini. Wakamletea watoto wachanga illi awaguse: wanafunzi wake wakawakemea wao waliowaleta. Lakini Yesu alipoona akachukiwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wachanga waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawo ufalme wa mbinguni ni wao. Amin, nawaambieni, Yeye yote asiyeukubali nfalme wa Mungu kama mtoto mchanga hatauingia kabisa. Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki. Hatta alipokuwa akitoka kwenda njiani mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanyeni nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia, Mbona waniita mwema? hakuna mwema illa mmoja, ndiye Mungu. Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudu uwongo, Usidanganye, Waheshimu haha yako na mama yako. Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu ujana wangu. Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa neno moja Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni: ukiisha, njoo ukajitwike msalaba wako unifuate. Walakini yeye akakunja uso kwa neno lile, akaenda zake kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi. Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Kwa shidda gani wenye mali wataingia katika ufalme wa Mungu! Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, kwa shidda gani wenye kuitegemea mali wataingia katika ufalme wa Mungu! Ni rakhisi ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Nao wakashangaa mno, wakiambiana, Nani, bassi, awezae kuokoka? Yesu akawakazia macho, akanena, Kwa wana Adamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maana yote yawezekana kwa Mungu. Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. Yesu akajibu, akasema, Amin, nawaambieni, Hapana mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume au ndugu wake, au baba, au mama, au mke, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, au kwa ajili ya Injili, illa atapewa marra mia sasa wakati huu, nyumba na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na mateso: na katika ulimwengu ujao uzima wa milele. Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho: na wa mwisho wa kwanza. Wakawa njiani, wakipanda kwenda Yerusalemi; na Yesu alikuwa akiwatangulia: wakashangaa, na wakifuata wakaogopa. Akawachukua tena wale thenashara akaanza kuwaambia khabari za mambo yatakayompata, akinena, Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemi: na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa makuhani wakuu na waandishi, na watamhukumu afe, watamtia mikononi mwa mataifa, nao watamdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumtemea mate, na kumwua: na siku ya tatu atafufuka. Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakamwendea, wakimwambia, Mwalimu, twataka utufanyie lo lote tutakalokuomba. Akawaambia, Mwalaka niwafanyie nini? Wakamwambia, Utujalie sisi tuketi, mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto katika utukufu wako. Yesu akawaambia, Hamjui mnaioliomba. Mnaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, na kubatizwa nbatizo nibatizwao mimi? Wakamwambia, Twaweza. Yesu akawaambia, Kikombe ninyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo nibatizwao mimi mtabatizwa: bali khabari ya kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto sina amri kuwapeni, illa wao watapewa waliowekewa tayari. Hatta wale kumi waliposikia wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana. Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa majumbe wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivi kwemi; bali mtu atakae kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mkhudumu wenu, na mtu atakae kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote. Kwa maana Mwana wa Adamu nae hakuja kukhudumiwa bali kukhudumu, na kutoa roho yake iwe dia ya wengi. Wakafika Yeriko: hatta alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia, akiomba sadaka. Aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, akaanza kupaaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daud, Yesu, unirehemu. Yesu akasimama akaagiza aitwe. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; ondoka, anakuita. Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu. Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyieni? Yule kipofu akamwambia, Rabbi, nipate kuona tena. Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Marra akapata kuona tena; akafuata Yesu njiani. HATTA walipokaribia Yerusalemi karibu na Bethfage na Bethania, kukabili mlima wa Mizeituni, akawatuma wawili katilia wanafunzi wake, akawaambia, Enendeni zenu hatta kile kijiji kinachowakahili. Katika kuingia ndani yake marra mtaona mwana punda amefungwa, asiyepandwa na mtu hado; mfungueni, kamleteni. Na mtu akiwaambieni, Mbona mnafanya hivi? semeni, Bwana ana haja nae; na marra atampeleka hapa. Wakaenda zao, wakamwona mwana punda amefungwa penye mlango, nje katika njia kuu, wakamfungua. Baadhi ya watu waliosimama huko wakawaamhia, Mnafanyani mkimfungua mwana punda? Wakawaambia kama Yesu alivyowaagiza. Wakamletea Yesu yule mwana punda, wakatandika mavazi yao juu yake; akaketi juu yake. Watu wengi wakatandaza mavazi yao njiani, wengine wakakata matawi ya miti na kuyatandaza njiani. Watu waliotangulia na wale waliofuata wakapaaza sauti zao, wakinena, Utuokoe sasa; amebarikiwa ajae kwa jina la Bwana; umebarikiwa ufalme ujao kwa jina la Bwana, ufalme wa baba yetu Daud. Utuokoe sasa, wewe uliye juu. Yesu akaingia Yerusalemi hatta ndani ya hekalu: na alipokwisha kutazama yote pande zote, kwa kuwa ni wakati wa jioni, akatoka akaenda Bethania pamoja na wathenashara. Hatta assubuhi yake walipotoka Bethania akaona njaa. Akaona toka mbali mtini wenye majani, akaenda illi labuda aone kitu juu yake: na alipofika hakuona kitu illa majani: maana haukuwa wakati wa tini. Yesu akajibu, akauambia, Tangu leo hatta milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia. Wakafika Yerusalemi, Yesu akaingia ndani ya hekalu, akaanza kuwafukuza watu waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadilio fedha, na viti vyao wauzao njiwa; wala hakuacha mtu achukue chombo kati ya hekalu. Akafundisha, akiwaambia, Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali nanyi mmeifanya kuwa pango ya wanyangʼanyi. Waandishi na makuhani wakini wakapata khabari wakatafuta jinsi ya kumwangamiza: maami walimwogopa, kwa sababu makutano yote walishangaa kwa elimu yake. Na ilipokuwa jioni alitoka mjini. Na assubuhi walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini umekauka tangu shina lake. Petro akakumbuka khabari yake, akamwabia, Rabbi, tazama, mtini ulioulaani umekauka. Yesu akajibu, akamwambia, Mwe na imani kwa Mungu, Amin, nawaambieni, Ye yote atakaenambia mlima huu, Ngʼoka ukatupwe baharini, asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yamekuwa, yatamtukia hayohayo aliyosema. Kwa sababu biyo nawaambieni, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea nayo yatakuwa yenu. Nanyi, killa msimamapo na kusali, sameheni, kama mkiwa na neno juu ya mtu: illi Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. La, kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu. Wakafika Yerusalemi tena: hatta alipokuwa akitembea hekaluni, makuhani wakuu na waandishi na wuizee wakamwambia, Kwa mamlaka gani utendayo haya? Na ni nani aliyekupa mamlaka hii uyatende haya? Yesu akajibu akawaambia, Mimi nami nitawauliza neno moja, nanyi nijibuni, kiisha nitawaambieni kwa mamlaka gani nitendayo haya. Ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au kwa wana Adamu? Nijibuni. Wakasemezana wao kwa wao, wakinena, Kama tukisema, Toka mbinguni, atasema, Mbona, bassi, hamkuniwamini? Bali tukisema, Ulitoka kwa wana Adamu—waliogopa watu: maana watu wote walimwona Yohana kuwa nabii kweli kweli. Wakamjibu Yesu, wakanena, Hatujui. Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi kwa mamlaka gani nitendayo haya. AKAANZA kusema nao kwa mifano. Mtu alipanda mizabibu, akazungusha nzio, akachimbia shimo lake shinikizo, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. Hatta kwa wakati wake akatuma mtumwa kwa wale wakulima, illi apokee kwa wakulima baadhi ya matunda ya mizabibu. Wakamtwaa, wakampiga, wakamtoa nje, hana kitu. Akatuma tena kwao mtumwa mwingine. Na huyo wakampiga mawe, wakamtia jeraha ya kichwa, wakamtoa ametiwa aibu. Akamtuma mwingine, huyo wakamwua; na wengine wengi, wakiwapiga hawa, na wakiwana hawa. Bassi alikuwa na mwana mmoja bado, mpendwa wake; huyu nae akamtuma kwao wa mwisho, akinena, Watamjali mwana wangu. Wale wakulima wakasemezana, Huyu ni mrithi; haya, na tumwue, na urithi utakuwa wetu. Wakamkamata, wakamwua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu. Bassi atafanyani yule Bwana wa mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa watu wengine. Hatta andiko hili hamjalisoma? Jiwe walilokataa waashi Hili limekuwa jiwe kuu la pembeni. Neno hili limetoka kwa Bwana Nalo ni ajabu machoni petu. Wakatafuta kumkamata, wakaogopa makutano; maana walitambua ya kwamba ule mfano amewanena wao. Wakamwacha wakaenda zao. Wakatuma kwake baadhi ya Mafarisayo na Maherodiano, illi wamnase kwa maneno. Hatta walipofika wakamwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu: lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! ni halali kumpa Kaisari kodi au sivyo? Tumpe, tusimpe? Nae, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? nileteeni dinari niione. Wakaleta. Akawaambia, Ya nani sanamu hii na anwani hii? Wakamwambia, Ya Kaisari. Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu. Wakamtaajahia sana. Na Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hapana kiyama, wakamwendea, wakamwuliza wakinena, Mwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mke wake wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mke wake akampatie ndugu yake mzao. Bassi palikuwa na ndugu saba; wa kwanza akatwaa mke, akafa, asiache mzao. Wa pili nae akamtwaa akafa, wala yeye hakuacha mzao. Hatta na wa tatu kadhalika; wukamtwaa wote saba wasiache mzao. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa nae. Bassi, katika kiyama watakapofufuka atakuwa mke wa nani katika hawa? Maana wote saba walikuwa nae. Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hamjidanganyi kwa sababu hii, kwa kuwa bamyajui maandiko wala uweza wa Mungu? Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaozwi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni. Na katika khabari ya wafu ya kwamba wafufuka, hamjasoma katika Kitabu cha Musa, mwenye Kijiti, jinsi Mungu alivyomwambia, akinena, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaak, na Mungu wa Yakobo? Yeye si Mungu wa wafu, bali wa wahayi. Kwa hiyo mwajidanganya sana. Mmojawapo wa waandishi akafika, amewasikia wakisemezana nae, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ipi iliyo ya kwanza? Yesu akamjibu, Katika amri zote ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Amri ya kwanza ndiyo hii. Na ya pili yafanana na bayo, ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hapana nyingine iliyo kuu kuliko hizi. Yule mwandishi akamwambia, Hakika, mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hapana mwingine illa yeye: na kumpenda kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa roho yote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko kafara zote na dhabihu zote. Yesu, alipoona kwamba amejibu kwa busara, akamwambia, Wewe huwi mbali na ufalme wa Mungu. Wala hakuthubutu mtu kumsaili neno tena tokea hapo. Hatta Yesu alipokuwa akifundisha katika hekalu, akajibu, akanena, Kwa maana gani waandishi hunena ya kwamba Kristo yu Mwana wa Daud? Kwa sababu Daud mwenyewe alisema, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume Hatta niwafanyapo adui zako kuwa chini ya miguu yako. Daud mwenyewe amwita Bwana: bassi amekuwaje mwana wake? Na ule mkutano mkubwa walikuwa wakimsikiliza kwa furaha. Akawaambia katika mafundisho yake, Jibadharini na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, na kukaa mbele katika sunagogi, na mahali pa mbele katika karamu: wanakula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu: hawa watapokea hukumu iliyo kubwa. Yesu akaketi kuielekea sanduku ya hazina, akatazama jinsi makutano watiavyo fedha katika sanduku. Matajiri wengi wakatia vingi. Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia sarafu mbili za shaba, kiasi cha nussu pesa. Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambieni, Huyu mjane maskini ametia vingi kuliko wote wanaotia katika sanduku ya hazina: maana hawa wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi: bali huyu katika mahitaji yake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndio maisha yake yote pia. HATTA alipokuwa akitoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, Mwalimu, namna gani ya mawe! namna gani ya majengo! Yesu akajibu, akawaambia, Waona majengo haya makuhwa makubwa? Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomelewa. Hatta alipokuwa ameketi katika mlima wa mizeituni, kuelekea hekalu, Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea wakamwuliza kwa faragha, Tuambie, haya yatakuwa lini? Na nini dalili ya wakati hayo yote yatakapokuwa karibu kutimia? Yesu akajibu, akaanza kuwaambia, Jihadharini, mtu asiwadanganye; kwa maana wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ndiye: na watadanganya wengi. Tena mtakaposikia vita na khabari za vita, msitishwe: maana hayana buddi kutukia, lakini mwisho wenyewe bado. Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme utapigana na ufalme: kutakuwa na matetemeko ya inchi mahali mahali; kutakuwa na njaa, na fitina: Hayo ndio mwanzo wa utungu. Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapelekeni maharazani: na katika masunagogi mtapigwa: na mtachukuliwa mbele za maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao. Tena sharti Injili ikhubiriwe kwanza katika mataifa yote. Na watakapowachukueni, na kuwateni katika mikono ya watu, msianze kuwaza mtakayosema, wala msishughulike: lakini lo lote mtakalopewa saa ile, lisemeni: kwa maana si ninyi mseniao, hali Roho Mtakatifu. Na ndugu atamsaliti ndugu yake illi anawe, na baba mtoto wake, na watoto wataondoka jun ya wazazi wao, na kuwafisha. Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kustahimili hatta mwisho, ndiye atakaeokoka. Lakini mlionapo chukizo la uharibifu (lile lililoneuwa ua nabii Danieli) likisimama pasipolipasa (asomae na afahamu) ndipo walio katika Yahudi wakimbilie milimani; nae aliye juu ya dari asishuke nyumbani, wala asiingie kuchukua kitu katika nyumba yake, Nae aliye shambani asirudi nyuma kulichukua vazi lake. Ole wao wenye mimba, nao wanyonyeshao siku zile! Ombeni kukimbilia kwerm kusiwe wakati wa baridi. Kwa maana siku zile zitakuwa na shidda jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hatta sasa, wala hazitakuwa kamwe. Na kama Bwana asingalizikatiza siku zile, asingeokoka mtu aliye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku zile. Na wakati huo mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko huko, msisadiki: kwa maana wataondoka Makristo wa nwongo, na manabii wa uwongo, watatoa ishara na ajabu, wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wale wateule. Bali ninyi mwe macho: nimekwisha kuwaonyeni yote mbele. Lakini siku hizo baada ya shidda ile jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na nguvu nyingi na utukufu. Ndipo atakapowatuma malaika zake na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa inchi hatta upande wa mwisho wa mbingu. Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liauzapo kuwa laini, na kuchanua majani yake, mwajua ya kuwa karibu wakati wa bari: kadhalika na ninyi, myaonapo haya yanatukia, fahamuni ya kuwa ni karibu milangoni. Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita kabisa, hatta haya yote yapatapo kuwa. Mbingu na inchi zitapita: maneno yangu hayatapita kamwe. Lakini khabari ya siku ile na saa ile hakuna aijuae, hatta malaika walio mbinguni, wala Mwana, illa Baba. Angalieni, kesheni, ombeni, kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwa. Ni kana kwamba mtu mwenye kusafiri, ameacha nyumba yake, amewapa amri watumwa wake, na killa mtu kazi yake, amemwamuru bawabu akeshe. Kesheni bassi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au usiku wa manane, au awikapo jogoo, an assubuhi: asije akawasili ghafula akawakuta mmelala. Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia Wote, Kesheni. BAADA ya siku mbili ilikuwa siku kuu ya Pasaka, na mikate isiyochachwa: makuhani wakuu na waandishi wakatafuta njia ya kumkamata kwa hila na kumwua. Kwa maana walisema, Sio wakati wa siku kuu, isije ikawa fitina katika watu. Nae akiwapo Bethania, nyumbani mwa Simon mwenye ukoma, ameketi chakulani, akaja mwanamke mwenye kibweta cha alabastro cha marhamu ya hali udi, safi, ya thamani nyingi; akakivunja kibweta cha alabastro akaimimina kichwani pake. Palikuwa na watu waliochukiwa katika nafsi zao wakisema, Ya nini kupoteza marhamu namna hii? maana marhamu hii ingalikuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi wakapewa maskini. Wakamnungʼunikia sana yule mwanamke. Yesu akasema, Mwacheni; mbona mnamwudhi? amenitendea kazi njema: maana siku zote mnao maskini pamoja nanyi, na killa mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamnami sikuzote. Ametenda alivyoweza; amenipaka mwili marhamu kwa ajili ya maziko yangu. Amin, nawaamhieni, Killa ikhubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake. Yuda Iskariote, mmoja wa wathenashara, akaenda zake kwa makuhani wakuu, apate kumsaliti kwao. Nao waliposikia wakafurahi, wakaahidi kumpa fedha. Akatafuta njia ya kumsaliti wakati wa kufaa. Hatta siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja Pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Wapi unataka tuende tukaandalie uile pasaka? Akapeleka wawili katika wanafunzi wake, akawaambia, nendeni zenu mjini; atakutana nanyi mwanamume akichukua mtungi wa maji; mfuateni: na po pote atakapoingia, mwambieni mwenye nyumba, Mwalimu asema, I wapi sebule ya wageni, niile pasaka, pamoja na wanafunzi wangu? Nae mwenyewe atawaonyesha orofa kuhwa, imetandikwa tayari: huko tuandalieni. Wanafunzi wakatoka, wakaenda mjini, wakaona kama alivyowaambia, wakaiandaa pasaka. Ilipokuwa jioni yuaja pamoja na wathenashara. Nao wakiisha kuketi chakulani, wakila, Yesu akasema, Amin, nawaambieni, mmoja wenu, nae anakula pamoja nami, atanisaliti. Wakaanza kuhuzunika, wakamwambia, mmoja mmoja, Ni mimi? na mwingine, Ni mimi? Akawaamhia, Ni mmoja wa wathenashara, yeye achovyae pamoja nami katikakombe. Kwa maana Mwana wa Adamu aenda zake kama alivyoandikiwa: lakini ole wake mtu yule ambae Mwana wa Adamu amesalitiwa nae: ingekuwa kheri kwake kama asingezahwa mtu yule. Nao wakila, akatwaa mkate, akahariki, akamega, akawapa, akasema, Twaeni; huu ni mwili wangu. Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote. Akawaambia, Hii ni damu yangu, ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya watu wengi. Amin, nawaambieni, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hatta siku ile nitakaponnywa mpya katika ufalme wa Mungu. Wakiisha kuimba wakatoka kwenda mlima wa mizeituni. Na Yesu akawaambia, Mtachukizwa nyote kwa ajili yangu nsiku huu: kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchunga, na kondoo watatawanyika. Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya. Petro akamwambia, Wajapochukizwa wote, lakini sio mimi. Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, Wewe leo, usiku huu, kabla ya kuwika jogoo marra mbili, utanikana marra tatu. Nae akazidi sana kusema, Ijaponipasa kufa nawe, sitakukana kabisa. Na wote wakasema vivi hivi. Tena wakaja mahali jina lake Gethsemane; akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa muda nisalipo. Akamchukua Petro na Yakobo na Yohana pamoja nae, akaanza kufadhaika sana na kuhangaika. Akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa mkakeshe. Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomha, ya kuwa, ikiwezekana, saa hii impitie. Akasema, Abba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikomhe hiki: walakini, si nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe. Akaenda akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Simon, umelala? Hukuweza kukesha saa moja? Kesheni, kasalini, msipate kuingia majaribuni: roho ina nia njema, hali mwili dhaifu. Akaenda zake fena, akaomha, akasema neno lili hili. Hatta akaenda akawakuta wamelala tena, maana macho yao yanickuwa mazito, wala hawakujua la kumjibu. Akaja marra ya tatu, akawaambia, Laleni sasa, hatta mwisho, kapumzikeni: yatosha, saa imekuja; Mwana wa Adamu anatiwa mikononi mwao wenye dhambi. Ondokeni, twende; tazama, yeye anaenisaliti amekaribia. Na alipokuwa katika kusema marra Yuda akafika, mmoja wa wathenashara, na pamoja nae mkutano, wana panga na marungu, wametoka kwa makuhani wakuu, na waandishi, na wazee. Na yeye anaemsaliti amewapa ishara, akisema, Nitakaembusu, ndiye; mkamateni, mehukueni salama. Alipokuja, marra akamwendea, akasema, Rabbi, Rabbi; akambusu sana. Wakanyosha mikono yao wakamkamata. Na mmoja wao waliohudhuria akavuta upanga, akampiga mtumwa wa kuhani mkuu, akamkata sikio. Yesu akajibu, akawaambia, Kama juu ya mnyangʼanyi mmetoka na panga na marungu, kuja kunitwaa? Killa siku nalikuwa mbele yenu bekaluni nikifundisha, wala hamkunikamata: lakini maandiko yapate kutimia. Wote wakamwacha, wakakimbia. Na kijana mmoja alimfuata, amejitanda nguo ya katani; wakamkamata; nae akaiacha ile nguo ya katani, akawakimbia, yu uchi. Wakamchukua Yesu kwa mkubani mkuu; wakamkusanyikia wote, makhani wakuu na wazee na waandishi. Petro akamfuata mbali, hatta ndani katika behewa ya kuhani mkuu; akaketi pamoja na watumishi, anakota moto. Makuhani wakuu na baraza wote wakatafuta ushuhuda juu ya Yesu wapate kumwua: wasione. Kwa maana wengi walimshuhudia uwongo, na ushuhuda wao haukupatana. Hatta watu wakasimama wakamshubudia kwa uwonoo, wakisema, Sisi twalimsikia akiseina, Mimi nitaivunja hekalu hii iliyofanyika kwa mikono, na kwa siku tatu nitajenga ingine isiyofanyika kwa mikono; hatta hivi ushuhuda wao haukuwa sawa. Kuhani mkuu akasimama kati kati, akamwuliza Yesu, akisema, Hujibu neno? Hawa wakushuhudiani? Lakini akanyamaza, wala hakujibu neno. Knbani mkuu akamwuliza tena, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wake aliye Mtukufu? Yesu akasema, Mimi ndio yeye, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija na mawingu ya mbingu. Kuhani mkuu akararua nguo zake, akisema, Tuna baja gani ya mashahidi wengine? Mmesikia kufuru yake; mwaonaje? Wote wakamhukumu kuwa amepasiwa kufa. Wengine wakaanza kumtemea mate, na kumfunika uso, na kumpiga konde, na kumwambia, Fanya unabii. Watumishi wakampiga makofi. Na Petro alikuwa chini sebuleni, akaja mmoja wa vijakazi wa kuhani mkuu: akamwona Petro akikota moto; akamtazama, akasema, Wewe nawe ulikuwa pamoja na yule Mnazareti, Yesu. Akakana, akasema, Sijui wala si sikii usemavyo. Akatoka nje hatta ukumbini; jogoo akawika. Na yule kijakazi akamwona tena, akaanza kuwaambia waliohudhuria, Huyu ni mmoja wao. Akakana tena. Punde kidogo wale waliohudhuria wakamwambia Petro, Hakika u mmoja wao, kwa sababu u Mgalilaya wewe, na usemi wako kama usemi wao. Akaanza kulaani na kuapiza, Simjui mtu huyu mnenae. Jogoo akawika marra ya pili. Petro akalikumbuka neno lile aliloambiwa na Yesu, Kabla ya kuwika jogoo marra mbili, utanikana marra tatu. Na alipolifikiri, akalia. MARRA ilipokuwa assubuhi makuhani wakuu wakafanya shauri pamoja na wazee na waandishi na haraza zima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta kwa Pilato. Pilato akamwuliza, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajihu, akamwambia, wewe unasema. Makuhani wakamshitaki mengi. Pilato akamwuliza tena akinena, Hujibu neno? Tazama mambo mangapi wanayokushitaki! Wala Yesu hakujibu neno tena, hatta Pilato akataajabu. Bassi katika siku kuu huwafungulia mfungwa mmoja, wamtakae. Palikuwa na mtu aitwae Barabba, amefungwa pamoja na watu waliofanya fitina na kufanya uuaji katika fitina. Makutano wakapaaza sauti zao, wakaanza kuomba vile kama alivvozoea kuwatendea. Pilato akawajibu, akisema, Mnataka niwafungulie mfalme wa Wayahudi? Kwa maana alifahamu ya kuwa makuhani wakuu wamemtoa kwa husuda. Makuhani wakuu wakawataharakisha makutano, illi apende kuwafungulia Barabba. Pilato akajibu tena akawaambia, Bassi wataka nimtendeni huyu mnenae kuwa Mfalme wa Wayahudi? Wakapiga kelele tena, Msulibishe. Pilato akawaambia, Kwani, ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, Msulihishe. Pilato akapenda kuwafanyia radhi makutano, akawafungulia Barabba: akamtoa Yesu, baada ya kumpiga mijeledi, asulibiwe. Askari wakamchukua ndani ya sebule, ndiyo Praitorio, wakakusanya pamoja kikosi kizima. Wakamvika vazi jekundu, wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani; wakaanza kumsalimu, Salamu Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga kichwa kwa unyasi, wakamtemea mate, wakapiga magoti, wakamsujudu. Hatta wakiisha kumdhihaki, wakamvua lile vazi jekundu, wakamvika nguo zake mwenyewe; wakamchukua nje wamsulibishe. Wakamtumikisha mtu aliyekuwa akipita, Simon Mkurene, akitoka mashamba, baba wa Iskander na Rufo, auchukue msalaba wake. Wakamleta mahali palipokwitwa Golgotha, tafsiri yake, mahali pa kichwa. Wakampa mvinyo iliyotiwa manemane anywe, nae hakupokea. Wakamsulibi, wakagawanya nguo zake wakizipigia kura killa mtu atwae nini. Ikawa saa tatu wakamsulibi. Anwani ya mshitaka wake iliandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDU. Na pamoja nae walisulibi wanyangʼanyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto. Bassi andiko likatimizwa linenalo, Alihesabiwa pamoja na maasi. Nao waliopita wakamtukana, wakitikisatikisa vichwa vyao, wakisema, Ah! wewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiponye nafsi yako, shuka msalabani. Kadhalika na makuhani wakuu wakamdhihaki wao kwa wao, pamoja na waandishi, wakisema, Aliwaponya wengine; hawezi kujiponya nafsi yake. Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. Nao waliosulibiwa pamoja nae wakamlaumu, Ilipokuwa saa sita, pakawa na giza juu ya inchi yote, hatta saa tissa. Na saa tissa Yesu akapiga kelele kwa sauti kuu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? tafsiri yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Na baadhi yao waliohudhuria, wakisikia, wakasema, Anamwita Eliya. Mtu akapiga mbio, akajaza sifongo siki, akaitia jim ya unyasi, akamnywesha, akisema, Acheni; na tuone kwamba Eliya anakuja kumshusha. Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. Pazia la patakatifu likapasuka vipande viwili toka juu hatta chini. Bassi yule akida, aliyesimama akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa, Mwana wa Mungu. Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; katika hawa alikuwa Mariamu Magdalene, na Mariamu mama wa Yakobo mdogo na wa Yose, na Salome: hawa ndio waliomfuata alipokuwa Galilaya, na kumkhudumia; na wengine wengi waliopanda pamoja nae hatta Yerusalemi. Hatta ikiisba kuwa jioni, kwa sababu ni Maandalio, ndiyo siku iliyo kabla ya sabato, akaenda Yusuf, mtii wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza la mashauri, nae mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu. Pilato akastaajabu, kwa sababu amekwisha kufa. Akamwita yule akida, akamwuliza kwamba amekufa kitambo. Hatta alipokwisha kupata hakika, akamtunukia Yusuf maiti. Akanunua saanda, akamshusha, akamfungia ile saanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani: akafingirisha jiwe mbele ya mlango wa kaburi. Mariamu Magdalene na Mariamu wa Yose wakapatazama alipowekwa. HATTA sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu wa Yakobo na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka. Hatta assubuhi mapema, siku ya kwanza ya sabato, wakaenda kaburini, jua lilipochomoza; wakasemezana wao kwa wao, Nani atakaetufingirishia lile jiwe kutoka mlangoni mwa kaburi? Hatta walipotazama, wakaona ya kuwa lile jiwe limekwisha kufingirishwa; nalo lilikuwa kubwa nmo. Na wakiingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe: wakastaajabu. Nae akawaambia, Msistaajabu; muamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa: amefufuka: bayupo hapa: patazameni pahali walipomweka. Lakini enendeni zenu, mkawaambie wanafunzi wake, na Petro, ya kwamba awatangulia kwenda Galilaya: huko mtamwona, kama alivyowaambia. Wakatoka humo, wakakimbia kutoka kaburini: kwa maana waliingia tetemeko na ushangao: wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa. Alipofufuka Yesu assubuhi siku ya kwanza ya sabato alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambae kwamba alimtoa pepo saba. Huyu akashika njia akawapa khabari wale waliokuwa pamoja nae tangu zamani, wangali wakiomboleza na kulia. Na hawa waliposikia kama yu hayi akaonwa nae, hawakusadiki. Baada ya haya akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shamba. Na hawa wakaenda zao wakawapa khabari wale wengine: wala hawakuwasadiki hawa. Baadae akaonekana na wale edashara walipokuwa wakila, akawalaumu kwa kutoamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki waliomwona alipofufuka. Akawaambia, Enendem nlimwenguni mwote, mkaikhubiri injili kwa killa kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; Kwa jina langu watafukuza pepo; watasema kwa ndimi mpya; watashika nyoka; hatta wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. Nao wakatoka, wakakhubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithubutishia neno kwa ishara zilizofuatana nalo. Amin. KWA kuwa wiitu wengi wametia mkono kutunga khabari za mambo yale yaliyotimizwa kati yetu, kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi, ua watumishi wa lile neno tokea mwanzo, nimeona vema na mimi, nikiisha kujipatia khabari zilizo sahihi za mambo yote tokea awali, kukuandikia kwa taratibu. Theofilo il-aziz: upate kujua usahihi wa maneno yale uliyofundishwa. Zamani za Herode, mfalme wa Yahudi, palikuwa na kuliani mmoja, jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya: na mkewe alikuwa mmojawapo wa binti Haruni, jina lake Elizabeti. Nao wote wawili wenye haki mbele ya Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na hukumu zake zote bila lawama. Nao walikuwa hawana mtoto; maana Elizabeti alikuwa tassa, nao wote wawili wazec sana. Bassi ikawa alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele ya Mungu, kama ilivyokuwa desturi ya ukubani, kura ikamwangukia kuingia katika hekalu la Bwana, na kufukiza uvumba. Na mkutano wote wa watu walikuwa wakisali nje, saa ya kufukiza. Akatokewa na Malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhbahu ya kufukizia. Zakaria akafadhaika alipomwona, khofu ikamwingia. Yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mke wako Elizabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. Nawe utakuwa na furaha na shangwe; na watu wengi watafurahia kuzaliwa kwake. Kwa maani atakuwa mkuu mbele ya Mungu, hatakunywa divai wala kileo: nae atajazwa Roho Mtakatifu hatta tangu tumbo la mama yake. Na wengi katika wana wa Israeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. Nae atatangulia mbele ya uso wake, mwenye roho ya Eliya, na nguvu zake, kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na kuwageuza maasi waelekee akili zao wenye haki; illi kumfanyia tayari Bwana watu waliotengenezwa. Zakaria akamwambia malaika, Nitajuaje hayo? Maana mimi mzee na mke wangu kongwe wa siku nyingi. Malaika akamjibu, akamwambia, Mimi ni Gabrieli nisimamae mbele ya Mungu: nami nalitumwa niseme nawe, na kukupasha khabari hizi njema. Nawe utakuwa bubu, usiweze kusema hatta siku ile yatakapotokea hayo: kwa sababu hukusadiki maneno yangu: nayo yatatimizwa wakati wake. Na wale watu walikuwa wakimugojea Zakaria, wakastaajabu kwa kukawia kwake mle hekaluni: hatta alipotoka hakuweza kusema nao, wakatambua ya kuwa ameona maono mle hekaluni; nae alikuwa akiwapungia mkouo, akadumu kuwa bubu. Ikawa siku za khuduma yake zilipotimia, akaenda zake nyumbani kwake. Hatta baada ya siku zile mkewe Elizabeti akachukua mimba akajificha miezi mitano, akisema, Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana, siku zile alizoniangalia, kuniondolea aibu yangu mbele ya watu. Mwezi wa sita malaika Gabrieli alipelekwa na Mungu kwenda mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamke bikira aliyekuwa ameposwa na mume, jina lake Yusuf, wa nyumba ya Daud; na jina la yule mwanamke Mariamu. Akaja kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. Nae akafadhaika kwa khabari ya neno hili, akawaza moyoni mwake, Hii ni salamu gani? Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu; kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba, utazaa mwana, utamwita jina lake Yesu. Huyu atakuwa mkuu, atakwitwa Mwana wake Aliye juu; na Bwana Mungu atampa kiti cha Daud baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hatta milele; wala ufalme wake hautakuwa na mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili; kwa maana simjui mume? Malaika akajibu, akamwambia, Roho Mtakatifu atakujia, na nguvu zake Aliye juu zitakutilia kivuli: kwa biyo kitakachozaliwa kitakwitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. Na tazama, nae Elizabeti jamaa yako, ana mimba ya mtoto mume katika uzee wake: na mwezi hun wa sita kwake yeye aliyekwitwa tassa: kwa maana hapana neno lisilowezekana kwa Mungu. Mariamu akasema, Tazama, mimi mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kwa neno lako. Malaika akaondoka kwake. Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda milimani kwa haraka hatta mji mmoja wa Yuda. Akaingia nyumbani kwa Zakaria, akamwamkia Elizabeti. Ikawa Elizabeti alipoisikia salamu ya Mariamu, mtoto mchanga akaruka ndani ya tumbo lake; Elizabeti akajazwa Roho Mtakatifu, akapaaza sauti yake kwa nguvu, akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, na uzao wa tumbo lako umebarikiwa. Na latoka wapi neno hili lililonipata, mama wa Bwana wangu anijilie mimi? Kwa maana sauti ya salamu yako ilipoingia masikioni mwangu, mtoto mchanga aliruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu. Na yu kheri aliyesadiki, kwa maana maneno hayo aliyoambiwa na Bwana yatatimizwa. Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, Roho yangu yamfurahia Mungu, Mwokozi wangu. Kwa kuwa ameutazama unyonge wa mjakazi wake: Kwa maana hakika, tokea leo vizazi vyote wataniita kheri. Kwa kuwa aliye hodari amenitendea makuu; Na Jina lake ni takatifu. Na rehema zake vizazi hatta vizazi Kwao wanaomcha. Ametenda nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mioyo yao. Amewashusha wakuu katika viti, Amewakweza wanyonge. Wenye njaa amewashibisha mema; Wenye mali amewaondoa mikono mitupu Kwa kukumbuka rehema Amemsaidia Israeli mtumishi wake, (Kwa jinsi alivyowaambia baba zetu) Ibrahimu na nzao wake, hatta milele. Mariamu akakaa nae kadri ya miezi mitatu, akarudi nyumbani kwake. Hatta Elisabeti akatimiziwa wakati wake wa kuzaa, akazaa mwana mume. Wakasikia jirani zake na jamaa zake ya kwamba Bwana amemwongezea rehema zake; wakafurahiwa pamoja nae. Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto; wakataka kumpa jina la babae, Zakaria. Akajibu mamae, akasema, Sivyo, lakini atakwitwa Yohana. Wakamwambia, Hapana mtu katika jamaa zako aitwae jina hilo. Wakamwashiria babae, kumwuliza atakaje aitwe. Akataka kibau, akaandika, akanena, Yohana ni jina lake. Wakataajabu wote. Marra akafunguliwa kinywa na ulimi wake, akanena, akimbariki Mungu. Khofu ikawaingia wote waliokaa karibu nao; yakaenea maneno haya pia milimani mwote Uyahudi. Na wote waliosikia wakayaweka mioyoni mwao, wakinena, Mtoto gani bassi atakuwa huyu? Kwa maana mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nae? Zakaria babae akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akinena, Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli; Kwa kuwa amewajia watu wake na kuwakomboa. Ametuondokeshea wokofu wa nguvu Katika nyumba ya Daud mtumishi wake. (Kama alivyosema kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu mwanzo), Tuokolewe na adui zetu, na katika mikono yao wote wauaotuchukia; Illi kuwatendea rehema baba zetu, Na kukumbuka agano lake takatifu; Uapo aliomwapia Ibrahimu baba yetu, Ya kwamba atatupa sisi, tukiokoka mikononi mwa adui zetu, tumwabudu pasipo khofu, Katika utakatifu na kwa haki mbele zake siku zetu zote. Na wewe nawe, Mtoto, utakwitwa nabii wake Aliye juu: Kwa maana utatangulia mbele ya uso wake Bwana ufanyize njia zake; Uwajulishe watu wake wokofu Zikiondolewa dhambi zao, Kwa rehema zake Mungu wetu, Kwazo mwangaza wa juu umetujia, Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuelekeza miguu yetu mnamo njia ya amani. Yule mtoto akakua akaongezeka nguvu rohoni; akawako majangwani hatta siku ya kutokea kwake kwa Israeli. HATTA siku zile kulitoka amri kwa Kaisari Augusto ya kama iandikwe orodha ya majina ya walimwengu wote: orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa wakati Kurenio alipotawala Sham. Watu wote wakashika njia kwenda kuandikwa, killa mtu mjini kwake. Na Yusuf nae akaondoka Galilaya kutoka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Yahudi hatta mji wa Daud, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye wa nyumba na jamaa ya Daud, illi aandikwe pamoja na Mariamu mkewe ambae ameposwa nae; nae ana mimba. Ikawa katika kukaa kwao huko, siku zake za kuzaa zikatimia. Akamzaa mtoto wake wa kifungua mimba, akamfunga nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakuona nafasi katika nyumba ya wageni. Katika inchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni usiku na kulinda kundi lao kwa zamu. Malaika wa Bwana akawatokea, utukufu wa Bwana ukawangʼaria: wakaingiwa na khohi nyingi. Malaika akawaambia, Msifanye khofu; kwa maana nawaletea ninyi khabari njema za furaha kuu, itakayokuwa kwa watu wote: maana leo katika mji wa Daud amezaiiwa Mwokozi kwa ajili yenu, ndiye Kristo Bwana. Na hii ni ishara kwenu: Mtamkuta mtoto amefungwa nguo za kitoto; amelazwa horini. Ghafula hiyo walikuwapo pamoja na yule malaika wengi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, wakisema, Utukufu una Mungu palipo juu, Na katika inchi amani, kwa watu aliowaridhia. Ikawa malaika walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji wakaambiana, Haya na twende zetu mpaka Bethlehemu, tukaone neno hili lililofanyika, Bwana alilotujulisha. Wakaenda kwa haraka, wakamkuta Mariamu na Yusuf, na mtoto amelazwa horini. Walipoona wakaeneza khabari za neno waliloambiwa, la huyu mtoto. Wote waliosikia wakataajabu kwa yale waliyoambiwa na wachungaji. Bali Mariamu aliyahifadhi maneno haya yote akiyatafakari moyoni. Wachungaji wakarudi, wakimtukuza Mungu na kumhimidi kwa mambo yote waliyosikia, na waliyoona, kwa namna waliyoambiwa. Na zilipotimia siku nane za kumtahiri, alikwitwa jina lake Yesu, lile lililotajwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba. Nazo siku za kutakasika kwao zilipotimia, kwa sharia ya Musa, wakamleta Yerusalemi, wampe Bwana; (kama ilivyoandikwa katika sharia ya Bwana, Killa mume afunguae tumbo la mama yake aitwe mtakatifu kwa Bwana;) wakatoe sadaka kama ilivyonenwa katika sharia ya Bwana, Hua wawili, au makinda ya njiwa mawili. Bassi kulikuwako mtu katika Yerusalemi, jina lake Sumeon; na yule mtu mwenye haki, mtawa, akitazamia faraja ya Israeli: na Roho Mtakatifu alikuwa pamoja nae. Nae alikuwa amebashiriwa na Roho Mtakatifu ya kwamba haoni mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. Bassi akaja hekaluni kwa roho: na wazee wake walipomleta mtoto Yesu, wamfanyie kwa desturi ya sharia, mwenyewe akampokea mikononi mwake, akimhimidi Mungu, akasema, Sasa wamrukhusu, Bwana, mtumishi wako kwa amani, Kama ulivyosema: Kwa kuwa macho yangu yamenona wokofu wako, Uuliouweka tayari machoni pa watu wote; Nuru ya kuwaangaza mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli. Yusuf na mama yake wakawa wakistaajahu kwa yale yaliyonenwa juu yake; Sumeon akawabariki, akamwambia Mariamu, mama yake, Hakika huyu amewekwa, waanguke, wasimame wengi katika Israeli; awe ishara inenwayo; hatta na wewe upanga utakupenya roho yako; illi yafumike mawazo ya mioyo mingi. Kulikuwa na Auna, nabii mke, binti Fanueli, wa kabila ya Asher; nae kongwe wa siku nyingi, amekuwa na mume miaka saba baada ya ujana wake; nae mjane wa miaka themanini na mine; asiyeondoka hekaluni, kwa kufunga na kusali akiabudu usiku na mchana. Akitokea yeye nae saa ileile, alimshukuru Mungu, akawapasha khabari zake watu wote waliokuwa wakitazamia ukombozi katika Yerusalemi. Nao walipokwisha kuyatimiza yote yaliyomo katika sharia ya Bwana, wakarudi Galilaya hatta mji wao Nazareti, Mtoto yule akakua, akaongezeka nguvu, akajazwa hekima; neema ya Mungu ikawa pamoja nae. Bassi wazee wake, killa mwaka walikuwa wakienda Yerusalemi siku kuu ya Pasaka. Hatta alipopata miaka kumi na miwili, wakapanda kwenda Yerusalemi, kama ilivyokuwa desturi ya siku kuu: na wakiisha kuzitimiza siku, walipokuwa wanarudi kwao, yule mtoto Yesu akabaki nyuma Yerusalemi, wala mama yake na Yusuf hawakujua; wakadhani yumo katika msafara yao, wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao, wasimwone, wakarejea Yerusalemi, wakimtafuta. Ikawa baada ya siku tatu, wakamwona hekaluni, ameketi kati ya waalimu, akiwasikiliza, na kuwauliza. Wote waliomsikia wakataajahu kwa akili zake na majibu yake. Nao walipomwona wakashangaa sana; mama yake akamwambia, Mwanangu, kwani ukatutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni. Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwa katika nyumba ya baba yangu? Wala hawakuelewa na neno lile alilowaanibia. Akashuka pamoja nao, akafika Nazareti, akawa anawatii: mama yake akayahifadhi maneno haya yote moyoni mwake. Yesu akazidi kuendelea katika hekima, na kimo, na neema kwa Mungu na kwa watu. HATTA katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Tiberio Kaisari, Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Yahudi, na Herode tetrarka wa Galilaya, na Filipo ndugu yake tetrarka wa Iturea, na wa inchi ya Trakoniti, na Lusania tetrarka wa Abilene, wakati wa ukuhani ukuu wa Anna na Kayafa, neno la Mungu likamfikia Yohana, mwana wa Zakaria, jangwani. Akalika inchi yote iliyo kando ya Yardani, akikhuhiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi, kaina ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya, Sauti yake apigae mbiu jangwani, Itengenezeni njia ya Bwana, Nyosheni mapito yake. Killa bonde litajazwa, Na killa jabali na mlima utashushwra, Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na njia zilizoparuza zitakuwa njia sawa; Na wote wenye mwili watanona wokofu wa Mungu. Bassi akawaambia makutano waliotokea illi kubatizwa nae, Enyi uzao wa nyoka, ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu itakayokuja? Zaeni, bassi, matunda yapatanayo na toba wala msianze kusema ndani ya nafsi zenu, Tunae baba ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni, ya kwamba Mungu katika mawe haya aweza kumwinulia Ibrahimu watoto. Na sasa hivi shoka limekwisha kutiwa katika shina la miti, bassi killa mti usiozaa matunda mema hukatwa ukatupwa motoni. Nao makutano wakamwuliza wakinena, Tufanyeni, bassi? Akajibu akawaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe yeye asiye nayo, na mwenye vyakula, na afanye vivyo hivyo. Watoza ushuru nao wakaja illi kubatizwa, wakamwambia, Mwalimu, tufanyeni? Akawaambia, Msifoze kitu zaidi ya vile mlivyoamriwa. Askari nao wakamwuliza wakisema, Nasi tufanyeni? Akawaambia, Msimtende jeuri mtu aliye yote, wala msitoze kitu bila haki; tena mwe radhi na mshsahara wenu. Bassi wale watu walipokuwa katika hali ya kutazamia, wakitafakari wote khabari za Yohana, kwamba yeye huenda akawa Kristo, Yohana akajibu, akawaambia wote, Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yuaja aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba mimi sistahili kumfungulia ukanda wa viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto: pepeto lake li mkononi mwake, nae ataitakasa sana sakafu yake; afakusanya nganu yake ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika. Bassi kwa maonyo mengi na ya namna nyingine mengi akawakhubiri watu. Lakini Herode tetrarka, akikaripiwa nae kwa ajili ya Herodias, mke wa Filipo, ndugu yake, na kwa ajili ya maovu yote aliyoyafanya Herode, akaongeza na hili jun ya yote, alimfunga Yohana gerezani. Na watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu nae akiisha kubatizwa, na akisali, mbingu zilifunuka. Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili kama hua, sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe mwana wangu, mpendwa wangu, ndiwe unipendezae. Nae Yesu mwenyewe alipokuwa akianza kufundisha, umri wake amekuwa miaka thelathini, akidhaniwa kuwa mwana wa Yusuf, wa Eli, wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yanna, wa Yusuf, wa Matathia, wa Amos, wa Nahum, wa Esli, wa Nagai, wa Maathi, wa Matathia, wa Semei, wa Yosef, wa Yuda, wa Yohana, wa Resa, wa Zorobabel, wa Salathiel, wa Neri, wa Melki, wa Addi, wa Kosan, wa Elmadam, wa Eri, wa Yesua, wa Eliezer, wa Yorim, wa Mathati, wa Lawi, wa Sumeon, wa Yuda, wa Yusuf, wa Yona, wa Eliakim, wa Melea, wa Mainan, wa Mattatha, wa Nathan, wa Daud, wa Yese, wa Obed, wa Boaz, wa Salmon, wa Nahason, wa Aminadab, wa Aram, wa Esrom, wa Fares, wa Yuda, wa Yakob, wa Isaak, wa Ibrahimu, wa Tara, wa Nahor, wa Saruhu, wa Ragau, wa Faleg, wa Eber, wa Sala, wa Kainan, va Arfaksad, wa Sem, wa Nuhu, wa Lamek, wa Methusala, wa Enok, wa Yared, wa Maleleel, wa Kainan, wa Enos, wa Seth, wa Adamu, wa Mungu. NA Yesu, akijaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani: akaongozwa na Roho kwenda jangwani, akijaribiwa na Shetani muda wa siku arubaini. Na siku zile hakula kitu; hatta zilipotimia, akaona njaa. Shetani akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate. Yesu akamjibu, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, hali kwa killa neno la Mungu. Shetani akampandisha juu ya mlima mrefu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Shetani akamwambia, Nitakupa mamlaka haya yote, na fakhari yake: kwa kuwa nimekabidhiwa, nami nampa ye yote nimtakae: bassi, wewe ukisujudu mbele yangu, yote yatakuwa yako. Yesu akamwambia, Nenda zako nyuma yangu, Shetani: maana imeandikwa, Utamsujudia Bwana Mungu wako, nae peke yake utamwabudu. Akamwongoza hatta Yerusalemi, akamweka juu ya ukumbi wa hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini, toka huku: maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde, na, Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako kalika jiwe. Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. Hatta alipomaliza killa jaribu Shetani akaondoka kwake kwa muda. Yesu akarudi kwa nguvu za Roho hatta Galilaya, khabari zake zikaenea katika inchi yote iliyo kando kando. Nae alikuwa akifundisha katika masunagogi yao, akitukuzwa na watu wote. Akaenda Nazareti, mahali alipokuwa amelelewa: akaingia katika sunagogi siku ya sabato, kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama illi asome. Akapewa chuo cha nabii Isaya: bassi alipokwisha kukifunua chuo hicho, akapaona pahali palipoandikwa, Roho ya Bwana ni juu yangu, Kwa sababu amenitia mafuia kuwakhubiri maskini khabari njema. Amenituma kuwaponya waliopondeka moyo, Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa, na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha wa huru waliosetwa, Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Akakifunga chuo, akampa mkhudumu, akaketi: watu wote waliokuwa katika sunagogi wakamkazia macho. Akaanza kuwaambia, Leo andiko hili limetimia masikioni mwenu. Wakamshuhudia wote, wakayastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake: wakanena, Huyu siye Mwana wa Yusuf? Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia methali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako: mambo yote tuliyosikia yametendeka Kapernaum, yatende na hapa pia katika inchi yako mwenyewe. Akawaambia, Amin, nawaambieni, Hapana nabii apatae kukubaliwa katika inchi yake mwenyewe. Lakini kwa kweli nawaambieni, Palikuwa wajane wengi katika Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita; njaa kuu ikaingia inchi yote: wala hakutumwa Eliya kwa mmojawapo wao, illa kwa mjane mmoja wa Sarepta, mji wa Sidon. Tena palikuwa wengi wenye ukoma katika Israeli zamani za nabii Elisha: wala hapana aliyetakasika illa Naaman, mtu wa Sham. Wakajazwa hasira wote katika sunagogi walipoyasikia haya. Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakamchukua hatta ukingo wa kilima kile kilichojengwa mji wao, wapate kumporomosha: lakini yeye akapita katikati yao akaenda zake. Akashukia Kapernaum, mji wa Galilaya, akawa akifundisha siku ya sabato: wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa sababu neno lake lilikuwa na uweza. Na palikuwapo katika sunagogi yao mtu mwenye roho ya pepo mchafu: akapaaza sauti kwa nguvu, akinena, Ah, tuna nini nawe Yesu Mnazareti? umekuja kutuangamiza? Nakutambua wewe, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akinena, Fumba kinywa, mtoke. Yule pepo akamwangusha katikati, akamtoka, asimdhuru. Ushangao ukawashika wote, wakaambiana wao kwa wao, wakinena, Neno gani hili, maana kwa mamlaka na uweza awaamuru pepo wachafu, nao watoka? Khabari zake zikaenea katika inchi zilizo kando kando killa pahala. Akatoka katika sunagogi, akaingia nyumba ya Simon. Bassi mkwewe Simon alikuwa ameshikwa na homa kali, wakamwomba kwa ajili yake. Akasimama karibu nae akaikemea ile homa, ikamwacha; marra akaondoka akawakhudumu. Hatta jua lilipokuwa likichwa watu wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbali mbali wakawaleta kwake: nae akaweka mikono yake juu ya killa mmoja, akawaponya. Pepo wakawatoka wengi wakipaaza sauti zao wakisema, Wewe u Kristo, Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walijua ya kuwa yeye ndiye Kristo. Hatta ulipokuwa mchana akatoka akaenda mahali pasipokuwa na watu: makutano wakamtafutatafuta, wakamfikilia, wakataka kumzuia asiondoke kwao. Akawaambia, Imenipasa kukhubiri khabari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia: maana kwa hiyo nalitumwa. Akawa akikhubiri katika sunagogi za Galilaya. IKAWA makutano walipomsonga, wakisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa akisimama kando ya ziwa la Genesareti: akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa: na wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao. Akaingia chombo kimoja, kilichokuwa cha Simon, akamtaka asogeze kidogo kutoka pwani. Akakaa, akawafundisha makutano katika chombo. Alipokwisha kusema, akamwambia Simon, Sogea hatta kilindini, mkashushe nyavu zenu kwa uvuvi. Simon akajibu, akasema, Bwana, tulisumbuka usiku kucha, tusipate kitu: illakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. Bassi, walipofanya hivi, wakakusanya wingi wa samaki: nyavu zao zikaanza kukatika. Wakawaashiri wenzi wao katika chombo cha pili, waje kuwasaidia. Wakaenda wakavijaza vyombo vyote viwili, hatta kuvizamisha. Simon Petro alipoona haya, akaanguka magotini pa Yesu, akasema, Toka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana. Kwa maana ushangao umemshika yeye, na wote waliokuwako pamoja nae, kwa uvuvi wa samaki walioupata. Kadhalika Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, waliokuwa washiriki wa Simon, Yesu akamwambia Simon, Usiogope; tangu sasa utakuwa ukivua watu. Na walipoleta vyombo pwani, wakaacha vyote wakamfuata. Ikawa alipokuwa katika mji mmoja wa miji ile, tazama, palikuwa na mtu amejawa ukoma; nae alipomwona Yesu, akaanguka kifudifudi, akamwomba, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa. Nae akauyosha mkono wake, akamgusa, akinena, Nataka; takasika. Marra ukoma wake ukamwounoka. Akamwagiza asimwambie mtu: illa enenda, ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe kwa kutakasika kwako alivyoamuru Musa, illi kuwa ushuhuda kwao. Lakini khabari zake zikazidi kuenea, wakakutana makutano mengi kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Lakini yeye alikuwa akijitenga jangwani na kusali. Hatta siku moja ya siku zile alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waandishi wameketi, waliokuwa wametoka katika killa kijiji cha Galilaya, na cha Yahudi, na Yerusalemi; uweza wa Bwana ulikuwa pamoja nae apate kuwaponya. Na kumbe! watu wanachukua mtu kitandani mwenye kupooza: wakitaka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake. Hatta walipokosa pa kumpeleka ndani kwa sababu ya lile kundi la watu, wakapanda juu ya dari wakampisha katika matofali, wakamshusha na kitanda chake hatta katikati mbele ya Yesu. Alipoona imani yao, akamwambia, Ee mtu, dhambi zako zimeondolewa. Wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kutafakari wakanena, Nani huyu anaesema kufuru? Nani awezae kuondoa dhambi, isipokuwa mmoja ndiye Mungu? Yesu akafahamu fikara zao akajibu, akawaambia, Mnafikiri nini mioyoni mwenu? Vipi vyepesi, kusema, Dhambi zako zimeondolewa, au kusema, Ondoka, ukaende. Lakini mpate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu ana mamlaka duniani ya kuondoa dhambi (alimwambia yule mwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako ukaende nyumbani kwako. Marra akasimama mbele yao, akajitwika kile alichokilalia, akaenda zake nyumbani kwake, akimhimidi Mungu. Ushangao ukawashika wote wakamtukuza Mungu: wakajaa khofu, wakinena, Tumeona maajabu leo. Baada ya haya akatoka, akaona mtoza ushuru, jina lake Lawi, amekaa forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaacha vyote akaondoka akamfuata. Nae Lawi akamfanyia karamu kubwa nyumbani mwake: na palikuwa na kundi kubwa la watoza ushuru, na watu wengine waliokuwa wameketi pamoja nao chakulani. Mafarisayo na waandishi wao wakawanungʼunikia wanafunzi wake, wakisema, Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Yesu akajibu, akawaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi: sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu. Nao wakamwambia, Kwa nini wanafunzi wa Yohana wanafunga marra nyingi na kusali, na wanafunzi wa Mafarisayo wanafanya vilevile, bali wanafunzi wako hula na hunywa? Yesu akawaambia, Je! mwaweza kuwafungislia wana wa arusi, maadam Bwana arusi yupo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa Bwana arusi, ndipo watakapofunga siku zile. Akawaambia mithali, Hakima apasuae kiraka cha nguo mpya na kukitia katika vazi kuukuu: ikiwa atia aipasua ile mpya, na kile kiraka cha nguo mpya hakilingani na lile vazi kuukuu. Wala hakuna mtu atiae divai mpya katika viriba vikuukuu: ikiwa atia, ile divai mpya itavipasua vile viriba, divai yenyewe ikamwagika, viriba vikapotea. Lakini divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya. Wala hakuna mtu anywae divai ya kale, marra akatamani divai mpya, maana asema, Ile ya kale ni njema zaidi. IKAWA siku ya Sabato alikuwa akipita katika makonde, wanafunzi wake wakavunja masuke, wakayala, wakiyapukusapukusa mikononi mwao. Bassi baadhi ya Mafarisayo wakawaambia, Mbona mnatenda lisilo halali siku ya Sabato? Yesu akajibu, akawaambia, Hatta neno hili hamkulisoma, alilolitenda Daud, alipokuwa na njaa, yeye nao waliokuwa pamoja nae, jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaitwaa mikate iliyotolewa kwa Mungu, akaila, akawapa na hawo waliokuwa pamoja nae, isiyo halali kuliwa illa na makuhani peke yao? Akawaambia ya kwamba, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato pia. Ikawa Sabato nyingine akaingia katika sunagogi, akafundislia: na palikuwako huko mtu mwenye mkono umepooza, mkono wa kuume. Mafarisavo na waandishi wakamvizia kuona kwamba ataponya siku ya Sabato, wapate kumshitaki. Lakini yeye akatambua mawazo yao, akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Ondoka, kasimama katikati. Yesu akawaambia, Nitawaulizeni neno moja. Ni halali siku ya Sabato kutenda mema au kutenda mabaya? kuokoa roho au kuua? Akawakazia macho wote pande zote, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Akatenda hivyo. Mkono wake ukapona, ukawa mzima kama wa pili. Nao wakatekewa moyo: wakisemezana wao kwa wao, wamtendeje Yesu. Ikawa katika siku zile akaomloka akaenda mlimani kuomba, akashinda usiku kucha, akimwomba Mungu. Ulipokuwa mchana akawaita wanafunzi wake: akachagua watu thenashara miongoni mwao, ambao aliwaita mitume. Simon ambae alimpa jina la pili Petro, na Andrea, ndugu yake; Yakobo na Yohana, Filipo na Bartholomayo. Mattayo na Tomaso, Yakobo wa Alfayo, na Simon aliyeitwa Zelote, Yuda wa Yakobo; na Yuda Iskariote, ndiye aliyekuwa khaini. Akatelemka pamoja nao, akasimama panapo uwanda, pamoja na kundi la wanafunzi wake, na kundi la watu waliotoka Yahudi wote, na Yerusalemi, na pwani ya Turo na Sidon, waliokuja wamsikilize na kuponywa maradhi zao; nao waliosumbuliwa na pepo wachafu; wakaponywa. Makutano yote wakatafuta kumgusa: kwa maana nguvu zilikuwa zikimtoka, zikawaponya wote. Nae akainua macho yake akawatazama wanafunzi wake, akasema, M kheri ninyi mlio maskini: kwa sababu ufalme wa Mungu ni wemi. M kheri ninyi mnaoona njaa sasa: kwa subabu mtashiba. M kheri ninyi mliao sasa: kwa sababu mtacheka. M kheri ninyi, wana Adamu watakapowachukieni na watakapowaharamisha, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kuma kitu kiovu, kwa ajili yake Mwana wa Adamu. Furahini siku ile, mkaruke: kwa kuwa bakika thawabu yenu nyiugi mbinguni, maana baba zao waliwatenda manabii mambo kama hayo. Bali ole wemi ninyi mlio na mali: kwa sababu mmekwisha kuwa na faraja yenu. Ole wenu ninyi mlioshiba: kwa sababu mtaona njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka sasa: kwa sababu mtaomboleza na kulia. Ole wenu ninyi, wana Adamu wote watakapowanena vema: maana baba zao waliwatenda manabii ya uwongo mambo kamsi hayo. Bali nawaambia ninyi mnaosikiliza, Wapendeni adui zenu, watendeni mema wao wawachukiao ninyi, wabarikini wao wawalaanio ninyi, waombeeni wao watendao ninyi jeuri. Akupigae shavu moja, umgeuzie la pili, nae akunyangʼanyae joho yako usimzuilie na kanzu. Killa akuombae mpe; nae akunyangʼanyae mali zako, usitake akurudishie. Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, nanyi watendeeni vivyo hivyo. Bassi mkiwajienda wao wawapendao ninyi mna neema gani? Maana hatta wenye dhambi huwapenda wao wawapendao. Na mkiwatenda mema wao wawatendao ninyi mema, mna neema gani? Maana hatta wenye dhambi hufanya vivyo hivyo. Na mkikopesha watu mkitumaini kupata kitu kwao tena, mna neema gani? Maana hatta wenye dhambi hukopesha wenye dhambi, illi wapokee sawasawa. Bali wapendeni adui zenu, katendeni kwa ihsani, kopeshani, bali kutumaini kupata kitu tena: na thawabu yenu itakuwa nyingi, na mtakuwa wana wa Aliye juu sana; kwa sabahu Yeye yu mwema kwa watu wasio na shukrani, na waovu. Bassi mwe na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma. Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa: msipatilize, nanyi hamtapatilizwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa. Toeni, nanyi mtapewa: kipimo chema kilichoshindiliwa, kilichosukwasukwa, kinachofurika ndicho watu watakachowapa ninyi kifuani mwenu. Kwa maana kipimo kile kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa na ninyi. Akawaambia mfano, Aweza kipofu kumwongoza kipofu? Hawatatumbukia wote wawili shimoni? Mwanafunzi hampiti mwalimu wake; illa killa aliyekhitimu atakuwa sawa na mwalimu wake. Bassi, mbona watazama kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako, na boriti iliyomo jichoni mwako huioni? Au wawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu, niache niondoe kibanzi kilichomo jichoni mwako, na wewe mwenyewe huioni boriti iliyomo jichoni mwako? Mnafiki, toa kwanza boriti iliyomo jichoni mwako, ndipo utakapoona vema kutoa kibanzi jichoni mwa ndugu yako. Maana hapana mti mwema uzaao matunda mabovu; wala mti mbovu uzaao matunda mema. Kwa maana killa mti hujulikana kwa matunda yake. Kwa kuwa katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa lililo jema: na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa lililo ovu: kwa sababu kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. Ya nini kuniita Bwana, Bwana, nanyi hamyatendi niyanenayo? Killa mtu ajae kwangu na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda nitawaonyesha mfano wake mtu huyu. Mfano wake ni mtu ajengae nyumba, akafukua, akachimba chini sana, akaweka msingi wake juu ya mwamba. Bassi palipokuwa na gharika, mto ukairukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa, kwa kuwa msingi wake umewekwa juu ya mwamba. Nae asikiae bila kutenda afanana na mtu aliyejenga nyumba juu ya udongo pasipo msingi: bassi mto ukairukia kwa nguvu, ikaanguka marra, na kuanguka kwake ile nyumba kulikuwa kukubwa. ALIPOKWISHA kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu akaingia Kapernaum. Na mtumishi wa akida mmoja alikuwa hawezi, karibu kufa, nae ni mtu aliyependwa nae sana. Aliposikia khabari za Yesu akatuma baadhi ya wazee wa Wayahudi kwake, akimwomba aje, amwokoe mtumishi wake. Nao walipolika kwa Yesu, wakamsihi kwa jubudi wakisema, ya kama, Astahili umtendee neno hili, maana apenda taifu letu, nae alitujengea sunagogi letu. Bassi Yesu akaenda pamoja nao. Hatta alipokuwa si mbali ya nyumba yake, yule akida akatuma rafiki kwake akimwambia, Bwana, usijisumbue, maana si stahili yangu wewe uingie chini ya dari yangu: kwa biyo nalijiona sistahili kuja kwako: lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona. Sababu mimi nami ni mtu aliyewekwa chini ya mamlaka, nina askari chini yangu: nikimwambia huyu, Nenda, huenda: na huyu, Njoo, huja; na mtumishi wangu, Fanya hivi, hufanya. Yesu aliposikia haya akamstaajabia akawageukia makutano waliokuwa wakimfuata, akisema, Nawaambieni, Hatta katika Israeli sikuona imani nyingi namna hii. Bassi wale waliotumwa waliporudi nyumbani kwake, wakamkuta yule mtumishi, aliyekuwa hawezi, yu mzima. Ikawa khalafu yake, akaenda mji uitwao Nain, wanafunzi wake na watu wengi wakafuatana nae. Bassi, alipokaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, mwana pekee wa mama yake, nae mjane; na watu wa mji wengi pamoja nae. Na Bwana alipomwona, akamhurumia, akamwambia, Usilie. Akaenda karibu, akaligusa jeneza; wale wachukuzi wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Ondoka. Yule maiti akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake. Khofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu: na Mungu amewajilia watu wake. Zikatoka hizo khabari zake katika Yahudi yote, na katika inchi yote iliyozunguka. Bassi wanafunzi wake Yohana wakamwarifu haya yofe. Yohana akaita wawili katika wanafunzi wake akawapeleka kwa Yesu, akisema, Wewe ndiye yule ajae, au tumtazamie mwingine? Bassi watu hawo walipofika kwake wakasema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiye ajae au tumtazamie mwingine? Saa ileile akawaponya watu wengi maradhi zao, na misiba yao, na pepo wabaya: na vipofu wengi akawakarimia kuona. Akajibu, akawaambia, Enendeni, mkamweleze Yohana mliyoyaona na kuyasikia: vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanakhubiriwa khahari njema: na yu kheri ye yote asiyechukizwa nami. Na wale wajumbe wa Yohana, walipokwisha kwenda zao, akaanza kuwaambia makutano khabari za Yohana, Mlitoka kwenda jangwani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi meroro? Fahamuni, watu wenye nguo za umalidadi na kuishi maisha ya anasa wamo katika majumba ya wafalme. Bali mlitoka kwenda kuona nini? Nabii? Naam, nawaambieni, na aliye zaidi ya nabii. Huyu ndiye aliyeandikiwa, Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako atakaeitengeneza njia yako mbele yako. Maana nawaambieni, Katika wazao wa wanawake hapana nabii aliye mkuu kuliko Yobana Mbatizaji: lakini aliye mdogo katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko yeye. Watu wote na watoza ushuru waliposikia wakampa Mungu haki, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana. Bali Mafarisayo na wana sharia walijikatalia shauri la Mungu kwa kuwa hawakubatizwa nae. Bwana akasema, Nitawafananisha na nini watu wa kizazi hiki? Nao wamefanana na nini? Wamefanana na watoto, waketio sokoni, wakiitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi nanyi hamkucheza, tuliomboleza, nanyi hamkulia. Kwa maana Yohana Mbatizaji amekuja, hali mkate, wala hanywi divai, mkasema, Yuna pepo. Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa, mkasema, Mlafi huyu, na mnywaji wa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi. Na hekima imepata haki yake kwa watoto wake wote. Mtu mmoja katika Mafarisayo akamtaka ale chakula pamoja nae. Akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani. Kumbe! Mwanamke mmoja katika mji ule ahyekuwa mwenye dhambi, alipopata khabari ya kuwa ameketi katika nyumba ya yule Farisayo, akaleta chupa cha alabastro yenye marhamu, akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumchuruzia miguu kwa machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake akibusu sana miguu yake, na kuipaka yale marhamu. Yule Farisayo aliyemwalika, alipoona haya akasema kimoyomoyo, akinena, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angalimjua huyu ni nani! na ni mwanamke gani anaemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi. Yesu akajibu akamwambia, Simon, nina neno la kukuambia. Akanena, Mwalimu, sema. Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili: mmoja aliwiwa nae dinari khamsi mia, na wa pili khamsini. Nao wakiwa hawana kitu cha kulipa, akawasamehe wote wawili. Bassi, sema, Katika hawo ni nani atakaempenda zaidi? Simon akajibu akasema, Nadhani ni yule aliyesamehewa nae mengi. Akamwambia, Umehukumu haki. Akamgenkia yule mwanamke, akamwambia Simon, Wamwona mwanamke huyu? Naliingia nyumbani mwako, hukunipa maji ya kunawia miguu, bali huyu amenichuruzia miguu kwa machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake. Hukunibusu: bali huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu. Hukunipaka kichwa changu mafuta: bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu. Kwa ajili hiyo, nakuambia, Amesamehewa dhambi zake zilizo nyingi kwa kuwa amependa sana. Nae asamehewae kidogo hupenda kidogo. Akamwambia, Umesamehewa dhambi zako. Na wale walioketi pamoja nae wakaanza kusema ndani ya mioyo yao, Nani huyu hatta akasamehe dhambi? Akamwambia yule mwanamke, Imani yako imekuokoa; enenda zako kwa amani. IKAWA muda si muda alikuwa akizungukazunguka katika miji na vijiji, akikhutubu na kukhubiri khabari njema za ufalme wa Mungu. Na wale thenashara walikuwa pamoja nae, na wanawake kadha wa kadha waliokuwa wameponywa pepo wabaya na magonjwa, Mariamu aliyeitwa Magdalene, aliyetokwa na pepo saba, na Joanna mkewe Kuza waklli wake Herode, na Susanna, na wengine wengi, waliokuwa wakimkhudumia kwa mali zao. Makutano mengi yalipokutanika, na watu wa killa mji wakimjia, akasema kwa mfano: Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akipanda, nyingine zikaanguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege za anga wakazila. Nyingine zikaanguka penye mwamba, zikamea, zikakauka kwa kukosa maji. Nyingine zikaanguka kati ya miiba, nayo miiba ikamea pamoja nazo, ikazisonga. Nyingine zikaanguka penye udongo mwema, zikamea, zikazaa mia mia. Alipokuwa akinena haya, akapaaza sauti yake, akisema, Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie. Wanafunzi wake wakamwuliza, wakinena, Mfano huu ni nini? Akasema, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa Mungu, bali wengineo kwa mifano, illi wakiona, wasione, na wakisikia, wasitambue. Na mfano ndio huu: Mbegu ni neno la Mungu. Na wale wa njiani, ndio wasikiao, ndipo huja Shetani na kulitoa lile neno mioyoni mwao, illi wasije wakaamini, wakaokoka. Na wale juu ya mwamba ndio wale ambao, walisikiapo neno, hulipokea kwa furaha; na hawa hawana mizizi, huamini kwa kitambo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga. Nazo zilizoangukia miibani, hawa ndio waliosikia, nao wakienda zao husongwa na shughuli, na mali, na anasa za maisha, wasizae kwa utimilifu. Nazo penye udongo mwema, hawa ndio ambao kwamba kwa moyo mzuri na mwema hulisikia neno, wakalishika, wakazaa kwa saburi. Hakuna mtu awashae taa na kuifunika kwa chombo au kuiweka mvunguni, bali huiweka juu ya kibao cha kuwekea faa, illi waingiao wauone mwanga. Kwa maana hakuna neno lililostirika ambalo halitakuwa dhabiri, wala neno lililofichwa ambalo halitajulikana, na kutokea wazi. Jihadharini, bassi, jinsi msikiavyo. Maana yeye aliye na kitu, atapewa: nae asiye na kitu ataondolewa hatta kitu kile ambacho anaonekana kuwa anacho. Mama yake na ndugu zake wakamwendea wala hawakuweza kumkaribia kwa sababu ya mkutano. Akapewa khabari na watu, waliosema, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kukuona. Lakini yeye akajibu akawaambia, Mama yangu na ndugu zangu ndio hawa walisikialo neno la Mungu na kulitenda. Ikawa siku mojawapo ya siku zile akapanda chomboni, yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke hatta ngʼambu ya ziwa: wakatweka matanga. Na walipokuwa wakienda kwa matanga akalala usingizi. Ikashuka dharuba ya upepo juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika khatari. Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Mwalimu, Mwalimu, tunaangamia. Akaondoka, akaukemea upepo, na msukosuko wa maji, vikakoma, kukawa shwari. Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakastaajabu, wakasemezana, Huyu ni nani, bassi, kwa kuwa hatta upepo na bahari aviamuru vikamtii? Wakashuka pwani katika inchi ya Wagadareni, inayokabili Galilaya. Hatta aliposhuka pwani, alikutwa na udu mmoja wa mji ule, aliyekuwa ua pepo siku nyingi, nae kwa muda mrefu alikuwa havai nguo, wala hakai nyumbani illa makaburini. Alipomwona Yesu, akapiga kelele, akamwangukia, akasema kwa sauti kuu. Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuomba usiniadhibu. Kwa sababu amemwamuru yule pepo mchafu kumtoka mtu yule. Maana marra nyingi amempagaa, nae akafungwa, akilindwa, na kufungwa minyororo na pingu, akavikata vile vifungo, akafukuzwa na yule pepo hatta jangwani. Yesu akamwuliza, akisema, Jina lako nani? Akasema, Legioni, kwa sababu pepo wengi wamemwingia. Akamsihi asiwaamuru waende zao hatta abusso. Na kulikuwako kundi la nguruwe wengi, wakilisha mlimani. Wakamsihi awape rukhusa kuwaingia wao. Akawapa rakhusa: wale pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, lile kundi likatelemka kwa kassi gengeni, wakafa baharini. Wachungaji walipoona, wakakimbia, wakaenda zao wakaeneza khabari mjini na mashambani. Wakatoka waone khabari iliyotokea. Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mtu aliyetokwa na wale pepo ameketi migunni pa Yesu, amevaa nguo, ana akili zake: wakaogopa. Nao walioona wakawaeleza jinsi yule mwenye pepo alivyoponywa. Na watu wote wa inchi ya Wagadarene iliyo kando kando wakamwomba aondoke kwao, kwa sababu walishikwa na khofu nyingi; bassi akakiingia chombo akarudi. Na yule mtu aliyetokwa na pepo akamsihi awe pamoja nae: lakini Yesu akamwaga, akisema, Rudi nyumbani kwako, ukayakhubiri mambo makuu aliyokutendea Mungu. Akaenda zake, akikhubiri katika mji mzima mambo makuu ambayo Yesu amemtendea. Yesu alipokuwa akirudi makutano wakamkaribisha, kwa maana watu wote walikuwa wakimngojea. Na tazama, mtu mmoja jina lake Yairo akamjia: nae alikuwa mkuu wa sunagogi: akaanguka miguuni pa Yesu, akamsihi aingie nyumbani mwake: kwa sababu ana binti, mwana wa pekee, umri wake amepata miaka thenashara, nae yu katika kufa. Na katika kwenda kwake makutano wakamsonga. Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu tangu miaka thenashara, aliyegharimu vitu vyote alivyo navyo akawapa tabibu asipate kuponywa na mtu aliye yote, akamwendea kwa nyuma, akamgusa upindo wa nguo yake, marra kukakoma kule kutoka damu kwake. Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Bassi watu wote walipokana, Petro nao walio pamoja nae wakamwambia, Bwana, Makutano wanakuzunguka na kukusonga, nawe unasema, Ni nani aliyenigusa? Yesu akasema, Mtu alinigusa, kwa kuwa naliona nguvu zimenitoka. Yule mwanamke alipoona ya kuwa hakustirika, akaja akitetemeka, akamwangukia, akamweleza mbele ya watu wote sababu hatta akamgusa, na jinsi alivyoponywa marra moja. Akamwambia. Jipe moyo mkuu, binti, imani yako imekuponya; enenda zako kwa amani. Alipokuwa akinena haya, mtu akaja, ametoka kwa yule mkuu wa sunagogi, akamwambia, Binti yako amekwisha kufa, usimsumbue mwalimu. Yesu aliposikia, akamjibu, akasema, Usiogope, amini tu, nae ataokolewa. Alipofika nyumbani, hakumwacha mtu aingie pamoja nae, illa Petro, na Yakobo na Yohana, na baba yake yule kijana na mama yake. Na watu wote walikuwa wakilia, wakimwombolezea. Akasema, Msilie; kwa maana hakufa, bali amelala usingizi. Wakamcheka sana, wakijua ya kuwa amekwisha kufa. Nae akawatoa nje wote, akamshika mkono wake, akapaaza sauti yake, akisema, Kijana, ondoka. Roho yake ikarudi, akasimama marra moja. Akaagiza apewe chakula. Wazazi wake wakastaajabu sana, akawaamuru wasimwambie mtu lililotukia. AKAWAITA wale thenashara akawapa uweza na mamlaka juu ya pepo wote, na kuponya maradhi. Akawatuma kuukhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. Akawaambia, Msichukue kitu cha njiani, fimbo wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala msiwe na kanzu mbili. Na nyumba yo yote mtakayoingia, kaeni humo, katokeni humo. Na wo wote wasiowakarihisheni, mtokapo katika mji ule, yakungʼuteni mavumbi ya miguuni mwenu illi kuwa ushuhuda juu yao. Wakaenda zao, wakazunguka katika vijiji, wakiikhubiri injili, na kuponya watu killa pahali. Hatta Herode tetrarka akasikia yote yaliyotendwa nae, akaona mashaka, kwa kuwa wengine walisema kwamba Yohana amefufuka katika wafu: na wengine kwamba Eliya ametokea: na wengine kwamba nabii mmoja katika wale wa kale amefufuka. Herode akasema, Yohana nimemkata kichwa: bassi, nani huyu ambae ninasikia khabari zake za namna hii? Akatafuta kumwona. Wale mitume waliporudi wakamweleza mambo yote waliyoyatenda; akawachukua, akaenda zake kwa faragha mahali pasipo watu, karibu na mji uitwao Bethsaida. Namakutano walipojua wakamfuata: akawakaribisha, akanena nao khabari za ufalme wa Mungu, akawaponya waliokuwa na haja ya kuponywa. Hatta jua lilipoanza kuchwa wale thenashara wakamwendea wakamwambia, Uwaage makutano illi waende zao hatta vijiji vilivyo kandokando na mashamba wakapate mahali pa kulala na vyakula: maana hapa tulipo nyika tupu. Akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakasema, Hatuna kitu zaidi ya mikate mitano na samaki mbili, tusipokwenda sisi wenyewe tukawannnulie vyakula watu hawa wote. Kwa maana walikuwako wanaume wapata elfu tano. Akawaambia wanafunzi wake, Waketisheni watu kwa safu, killa safu watu khamsini. Wakafanya hivi, wakawaketisha wote. Akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama juu mbinguni, akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi, kuviweka mbele ya makutano. Wakala, wakashiba wote: na vile vipande vilivyowabakia vikaokotwa, vikapu thenashara. Ikawra alipokuwa akisali peke yake wanafunzi wake walikuwa pamoja nae: akawanliza, akisema, Makutano huninena mimi kuwa nani? Wakajibu, wakasema, Yohana Mbatizaji: na wengine, Eliya: na wengine kwamba nabii mmoja katika wale wa kale amefufuka. Akawaambia, Na ninyi mwaninena mimi kuwa nani? Petro akajibu, akasema, Kristo wa Mungu. Akawaagiza na kuwaamuru wasimwambie mtu neno hili, akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Akawaamhia wote, Atakae kuniandama, na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake killa siku, anifuate. Kwa maana mtu akitaka kuisalimisha roho yake ataiangamiza, nae atakae kuitoa roho yake kwa ajili yangu, huyu ataisalimisha. Maana itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote na kujipoteza, au kupata khasara ya roho yake? Kwa sababu killa mtu atakaenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya huyo atakapokuja katika utukufu wake, na wa Baba yake, na wa malaika watakatifu. Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataionja mauti kabisa hatta watakapouona ufalme wa Mungu. Hatta baada ya maneno haya, panapo siku nane, akamchukua Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani kusali. Ikawa alipokuwa akisali, sura ya uso wake ikageuka, na mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta. Na tazama, watu wawili walikuwa wakisemezana nae, nao ni Musa na Eliya, walioonekana katika utukufu, wakanena khahari ya kufariki kwake atakakotimiza Yerusalemi. Petro, nao waliokuwa pamoja nae, walikuwa wamelemewa sana na usingizi: lakini walipokwisha kuamka wakauona utukufu wake, na wale watu wawili, waliosimama pamoja nae. Ikawa hawo walipokuwa wakijitenga nae, Petro akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa: na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, kimoja cha Eliya: nae hajui asemalo. Hatta alipokuwa akisema haya likawako wingu, likawatia uvuli; wakaogopa walipoingia katika lile wingu. Sauti ikatoka katika lile wingu ikasema, Huyu ni Mwana wangu, mpendwa wangu, msikieni yeye. Na sauti hii ilipokuja Yesu akaonekana peke yake. Nao wakanyamaza wasimwambie mtu siku zile neno lo lote la hayo waliyoyaona. Ikawa siku ya pili yake, waliposhuka mlimani, mkutano mkuu wakakutana nae. Na tazama, mtu mmoja katika ule mkutano akapaaza sauti yake, akisema, Mwalimu, nakuomha, mwangalie mwanangu, kwa kuwa yeye ni mwanangu pekee; na tazama, pepo humshika, nae marra hulia; tena humrarua, akatoka povu, wala hamtoki illa kwa shidda, akimchubuachubua. Nikawaomba wanafunzi wako wamfukuze, wasiweze. Yesu akajibu akasema, Enyi kizazi kisichoamini na upofu, nikae nanyi hatta hui? Mlete mwana wako hapa. Alipokuwa katika kumwendea, yule pepo akambwaga akamraruararua. Yesu akamkaripia yule pepo mchafu, akamponya yule mtoto, akamrudishia baba yake. Watu wote wakashangaa kwa adhama yake Mungu. Hatta wote walipokuwa wakistaajabia mambo yote aliyoyafanya akawaambia wanafunzi wake, Yawekeni maneno haya masikioni mwenu: kwa maana Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu. Lakini hawakulifuhamu neno lile, likawa limefichwa kwao wasipate kulitambua. Wakaogopa kumwuliza maana ya neno lile. Yakawaingia mabishano, ni nani atakaekuwa mkubwa miongoni mwao. Nae Yesu alipoona mawazo ya mioyo yao, akatwaa kitoto akamweka karibu yake, akawaambia, Killa mtu atakaempokea kitoto hiki kwa jina langu, anipokea mimi, na killa mtu atakaenipokea mimi, ampokea yeye aliyenituma. Maana yeye aliye mdogo miongoni mwenu ninyi nyote, huyu atakuwa mkubwa. Yohana akajibu, akasema, Mwalimu, tulimwona mtu anafukuza pepo kwa jina lako, tukamkataza kwa kuwa hatufuati sisi. Yesu akamwambia, Msimkataze, kwa maana yeye asiye kinyume chetu ni upande wetu. Ikawa siku za kupandishwa kwake juu zilipokuwa karibu kutimia, yeye mwenyewe akauelekeza nso wake kwenda Yerusalemi. Akatuma wajumbe mbele ya uso wake, wakashika njia, wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, illi kumfanyia tayari. Nao hawakumkaribisha, kwa sababu nso wake ameuelekeza kwenda Yerusalemi. Wanafunzi wake Yokobo na Yohana walipoona haya, wakasema, Bwana, wataka tuambie moto ushuke kutoka mbinguni uwaangamize, kama na Eliya alivyofanya? Akageuka, akawakaripia, akasema, Hamjui ni moyo wa namna gani mlio nao. Maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za wana Adamu, bali kuziokoa. Wakaenda zao hatta mji mwingine. Na walipokuwa wakienda njiani, mtu mmoja akamwambia, Nitakufuata ko kote uendako, Bwana. Yesu akamwambia, Mbweha wana matundu, na ndege za anga vioto vyao, bali Mwana wa? Adamu hana pa kujilaza kichwa chake. Akamwambia mwingine, Nifuate. Akasema, Bwana, nipe rukhusa niende kwanza, nikamzike baba yangu. Akamwambia, Waache wafu wazike wafu wao, bali wewe enenda zako ukautangaze ufalme wa Mungu. Na mwingine nae akasema, Nitakufuata, Bwana, lakini kwanza nipe rukhusa nikawaage watu wa nyumbani mwangu. Yesu akamwambia, Hakuna mtu aliyetia mkono wake alime, khalafu akatazama nyuma, afaae kwa ufalme wa Mungu. BASSI baada ya mambo haya Bwana akachagua wengine sabaini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda killa mji na pahali atakakokwenda mwenyewe. Akawaambia, Mavuno ni mengi, illakini watenda kazi wachache; mwombeni, bassi, Bwana wa mavuno, apate kupeleka watenda kazi mavunoni mwake. Enendeni: angalieni, nakutumeni ninyi kama wana kondoo kati ya mbwa wa mwitu. Msichukue kifuko, wala mkoba, wala viatu: wala msimsalimu mtu njiani. Na nyumba yo yote mwingiayo, kwanza neneni, Amani iwe nyumbani humu. Na kama yumo mwana wa amani, amani yenu itakaa kwake. La! si hivyo, itawarudia ninyi. Kaeni katika nyumba hiyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; kwa maana mtenda kazi astahili kupewa ijara yake. Msihame nyumba kwa nyumba. Na mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisheni, vileni vitu vile viwekwavyo mbele yenu. Waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni ya kama, Ufalme wa Mungu umewakaribieni. Na mji wo wote mtakaouingia nao hawawakaribishi utokeni, mkipita katika njia zake semeni, Hatta mavumbi haya ya mji wenu, yaliyogandamana nasi, twayakungʼuta juu yenu: illakini jueni haya, ya kuwa ufalme wa Mungu umewakaribieni. Nawaambieni, itakuwa rakhisi Sodoma istahimili adhabu yake siku ile kuliko mji ule. Ole wako, Korazin! Ole wako Bethsaida! kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu, ingalifanyika katika Turo na Sodom, wangalitubu zamani, wakiketi katika nguo za kigunia na majivu. Lakini itakuwa rakhisi Turo na Sidoni istahimili adhabu zao siku ile ya hukumu, kuliko ninyi. Nawe Kapernaum, wewe uliyeinuliwa hatta mhinguni, ntashushwa hatta kuzimu. Awasikiae ninyi, anisikia mimi, nae awakataae ninyi, anikataa mimi; nae anikataae mimi amkataa yeye aliyenituma. Wale sabaini wakarudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hatta pepo wanatutii kwa jina lako. Akawaambia, Nalimwona Shetani kama umeme akianguka toka mbinguni. Tazameni, nawapeni mamlaka va kuwakanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hapana kitu kitakachowadhuru ninyi kamwe. Lakini msifurahi kwa sababu hii ya kuwa pepo wanawatiini: hali furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni. Saa ileile Yesu akashangilia katika Roho, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na busara mambo haya, ukawafunulia watoto wachanga: Naam, Baba, kwa maana ndivyo vilivyokuwa vinapendeza mbele yako. Akawagenkia wanafunzi wake akasema, Nimekahidhiwa vyote na Baba yangu: wala hapana mtu ajuae khabari za Mwana illa Baba: wala khabari za Baha illa Mwana, na mtu ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia. Akawageukia wanafunzi wake kwa faragha, akawaambia, Ya kheri macho yatazamayo mnayoyatazama ninyi. Maana nawaambia; Manabii wengi na wafalme walitaka kuyaona mnayoyatazama ninyi wasiyaone, na kuyasikia mnayoyasikia wasiyasikie. Mwana sharia mmoja akasimama akimjaribu, akasema, Mwalimu, nifanyeni niurithi uzima wa milele? Akamwambia, Katika torati imeandikwa nini? Wasomaje? Nae akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako. Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi, ndipo utaishi. Nae akitaka kujifanya ana haki akamwambia Yesu, Na jirani yangu ni nani? Yesu akajibu akasema, Kulikuwa na mtu akishuka kutoka Yerusalemi kwenda Yeriko; akaangukia katika mikono ya wanyangʼanyi, wakamvua nguo zake, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakamwacha nussu ya kufa. Na kwa nasibu kukashuka kuhani mmoja njia ileile, akamwona, akapita upande. Na Mlawi kadhalika alipofika pahali pale, akamwona akapita upande. Lakini Msamaria mmoja akisafiri, akamjia, nae alipomwona akamhurumia; bassi akamjongelea, akamfunga jeraha zake, akitia mafuta na mvinyo: akampandisha juu ya nyama wake, akamleta katika nyumba ya wageni, akamwuguza. Hatta assubuhi yake akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba, akasema, Mwuguze: na cho chote utakachogharimia zaidi, nirudipo, nitakulipa. Waonaje bassi? Katika hawa watatu yupi aliyekuwa jirani yake mwenye kuangukia katika mikono ya wanyangʼanyi? Akasema, Ni yule aliyemfanyia huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye kama hayo. Nao walipokuwa wakienenda, akaingia katika kijiji kimoja; na mwanamke mmoja, jina lake Martha, akamkaribisha nyumbani mwake. Nae alikuwa na ndugu mwanamke aitwae Mariamu, nae alikuwa ameketi miguuni pa Yesu, akasikia maneno yake. Bali Martha alihangaika kwa khuduma nyingi: akamwendea, akasema, Bwana, haikukhussu wewe ya kuwa ndugu yangu ameniacha kukhudumu peke yangu? Bassi mwambie anisaidie. Bwana akamjibu akamwambia, Martha, Martha, unajisumbua na kujifadhaisha kwa ajili ya mambo mengi: lakini kuna haja ya kitu kimoja tu, na Mariamu ameichagua sehemu iliyo njema, ambayo hataondolewa. IKAWA alipokuwa mahali fullani, anasali, alipokoma, mmoja katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali kama Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake. Akawaambia, Msalipo, semeni: Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako takatifu litukuzwe. Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe, kama mbinguni, kadhalika duniani. Utupe leo riziki zetu. Utusamehe dhambi zetu, kwa maana sisi nasi tunamsamehe killa mtu anaewiwa nasi. Usituingize majaribuni, hali utuokoe na yule mwovu. Akawaambia, Nani kwenu aliye na rafiki akamwendea usiku wa manane akamwambia, Ee rafiki, uniazime mikate mitatu: maana rafiki yangu amekuja kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kumwandikia. Na yule mle ndani akamjibu, akimwambia, Usiniudhi: mlango umekwisha kufungwa, na watoto wangu wamelala pamoja nami kitandani; siwezi kuondoka nikupe. Nawaambieni, Ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, illakini kwa kuwa yule hana haya ataondoka na kumpa yote ahitajiyo. Nami nawaambia ninyi, Ombeni na mtapewa: tafuteni na mtapata: bisheni na mtafunguliwa. Kwa sababu killa aombae hupewa: nae atafutae hupata: nae abishae hufunguliwa. Kwa maana ni nani kwenu aliye baba, mwanawe akamwomba mkate, je! atampa jiwe? au akimwomba samaki, badala ya samaki atampa nyoka? au akimwomba yayi, atampa nge? Bassi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, Baba aliye mbinguni, je! hatazidi na kuwapa wote wamwombao Roho Mtakatifu? Na Yesu alikuwa akifukuza pepo bubu. Ikawa yule pepo alipotoka, bubu akasema, makutano wakastaajabu. Wengine wao wakasema, Kwa Beelzebul, mkubwa wa pepo atoa pepo. Wengine kwa kumjaribu wakataka ishara ya mbinguni. Nae, akiyajua mawazo yao, akawaambia, Killa ufalme uliogawanyika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa, na nyumba iliyogawanyika nyumba kwa nyumba huanguka. Nae Shetani vivyo hivyo akigawanyika katika nafsi yake, ufalme wake utasimamaje? kwa maana ninyi mnasema ninafukukuza pepo kwa Beelzebul. Lakini mimi nikifukuza pepo kwa Beelzebul, wana wenu huwafukuza kwa nani? bassi kwa hiyo hawo ndio watakaokuwa waamuzi wenu. Lakini nikifukuza pepo kwa kidole cha Mungu, bassi ufalme wa Mungu umewajieni. Aliye na nguvu, mwenye silaha zake, alindapo na wake, mali zake zimo katika amani: lakini mwenye nguvu za kumpita yeye atakapokuja na kumshinda, amnyangʼanya silaha zake zote alizotegemea, na mateka yake ayagawanya. Mtu asiye pamoja nami ni adui yangu: nae asiyekusanya pamoja nami hutapanya. Pepo mchafu amtokapo mtu, hupita kati ya mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika: asipopata hunena, Nitarudi uyumbani kwangu nilikotoka. Akija, huiona imefagiwa, imepambwa. Marra huenda, huchukua pepo saba wengine walio waovu kupita nafsi yake: nao huingia na kukaa humo: na mambo ya mwisho ya mtu yule huwa mabaya kuliko ya kwanza. Ikawa alipokuwa akinena haya, mwauamke mmoja katika makutano akapaaza sauti yake akamwambia, Li kheri tumbo lililokuehukua, na maziwa uliyonyonya. Lakini yeye akasema, Bali afadhali wa kheri wenye kulisikia neno la Mungu na kulishika. Makutano walipokuwa wakimkusanyikia akaanza kunena, Kizazi hiki ni kizazi kibaya: chatafuta ishara: wala hakitapewa ishara illa ishara ya nabii Yunus. Maana kama vile Yunus alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa kwa kizazi hiki. Malkia wa kusini atafufuliwa siku ile ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nae atawahukumu; kwa sababu yeye alikuja kutoka ncha za dunia illi kuisikia hekima ya Sulemani; na hapa pana khabari kubwa kuliko Sulemani. Watu wa Ninawi watasimama siku ile ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao wataihukumu: maana wao walitubu kwa ajili ya makhubiri ya Yunus, na hapa pana khabari kubwa kuliko Yunus. Hapana mtu awashae taa na kuiweka mahali pa siri au chini va pishi, bali huiweka juu ya kibao cha kuwekea taa: illi waingiao wanone mwanga. Taa ya mwili ni jicho, bassi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote nna nuru, lakini jicho lako likiwa ovu, mwili wako nao una giza. Angalia bassi, ile nuru iliyo ndani yako isije ikawa giza. Bassi, kama mwili wako wote nna nuru, tena kama hanna sehemu iliyo na giza, mwili wako utakuwa na nuru kabisa kama vile taa ikumulikiavyo kwa mwangaza wake. Hatta alipokuwa akisema, Farisayo mmoja akamwita ale chakula cha assubuhi kwake: akaingia, akaketi. Yule Farisayo alipoona akastaajabu kwa sababu hakunawa kabla ya chakula. Bwana akamwambia, Sasa ninyi Mafarisayo mwasafisha kikombe na sabani kwa nje, lakini ndani yenu mmejaa unyangʼanyi ua uovu. Enyi wapumbavu, yeye aliyekifauya cha nje, siye aliyekifanya cha ndani naebo? Lakini toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vitu vyote ni safi kwemi. Bali ole wenu Mafarisayo, kwa sababu mnalipa zaka za mnaana na mchicha, na killa mboga, mkaacha adili na upendo wa Mungu: iliwapaseni kuyafanya haya ya kwanza bila kuacha haya ya pili. Ole wenu, Mafarisayo, kwa sababu mwapenda kukaa mbele katika sunagogi na kusalimiwa masokoni. Ole wenu, maana mfano wenu ni makaburi yasiyoonekana, na watu wapitao juu yao hawana khabari. Mtu mmoja katika wana sharia akajibu, akamwambia, Mwalimu, ukisema haya watushutumu sisi nasi. Akasema, Na ninyi wana sharia, ole wenu, kwa sababu mwawachukuza watu mizigo isiyochukulika, na ninyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo kwa kimojawapo cha vidole vyenu. Ole wenu kwa sababu mnajenga makaburi ya manabii, na baba zenu waliwaua. Hivyo ndivyo mnavyoshuhudia matendo ya baba zenu na kupendezwa nayo: maana wao waliwaua, na ninyi mnajenga makaburi yao. Na kwa hiyo hekima ya Mungu ilisema, Nitatuma kwao manabii na mitume, na wataua baadhi yao, na kuwaudhi, illi kwa kizazi hiki itakwe damu ya manabii wote ilivomwagika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu; tangu damu ya Habil hatta damu ya Zakaria aliyeuawa kati ya madhhahu na patakatifu. Naam, nawaambieni, itatakwa kwa kizazi hiki. Ole wenu, enyi wana sharia, kwa sababu mliuchukua ufunguo wa maarifa; ninyi wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mliwazuia. Alipokuwa akiwaambia haya, waandishi na Mafarisayo wakaanza kumsonga vibaya, na kumchokoza kwa masiala mengi, wakimwotea, wakitaka kudaka neno kinywani mwake wapate kumshitaki. HUKO nyuma mkutano wa watu, watu elfu nyingi walipokusanyika hatta wakakanyagana, akaanza kuwaambia wanafunzi wake khassa, Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki. Lakini hakuna neno lililofunikwa ambalo halitafunuliwa khalafu, wala lililostirika ambalo halitajulika khalafu. Bassi yo yote mliyoyasema gizani, yatasikiwa katika nuru: nalo mlilolisema katika sikio la mtu katika vyumba vya ndani litakhubiriwa juu darini. Lakini nawaambia ninyi rafiki zangu, Msiwaogope wao wauuao mwili na baada ya haya hawana neno la kutenda la zaidi. Illa nitawaonya mtakaemwogopa: Mwogopeni yule aliye na uweza baada ya kuua mtu kumtupa katika Jehannum: naam, nawaambieni, Mwogopeni yule. Haviuzwi videge vitano kwa pesa mbili? na hatta kimojawapo hakisahauliwi mbele ya Mungu: walakini hatta nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope bassi: ninyi bora kuliko videge vingi. Nami nawaambieni, Killa atakaenikiri mbele za watu, Mwana wa Adamu nae atamkiri mbele za malaika wa Mungu. Nae aliyenikana mbele ya watu, atakanwa mbele za malaika wa Mungu. Na killa mmoja atakaesema neno juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, bali yeye aliyemtukana Roho Mtakatifu hatasamehewa. Na watakapowapeleka mbele za sunagogi na maliwali na wenye mamlaka, msifadhaike kwa kuwaza jinsi mtakavyojibu au mtakavyosema: kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa hiyo hiyo yawapasavyo kuyanena. Mtu mmoja katika makutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu. Akamwambia, Ee mwana Adamu, nani aliyemweka kuwa kadhi au mgawanyi juu yenu? Akawaambia, Angalieni, jilindeni na kutamani, maana uzima wa mtu hautoki katika mali zake, kwa sababu ana wingi wa mali. Akawaambia mfano, akisema, Palikuwa na mtu tajiri, shamba lake likastawi. Akaanza kuwaza moyoni, akisema, Nifanyeje, maana sina pa kuweka akiba mavuno yangu? Akasema, Nitafanya hivi: nitavunja ghala zangu, nitajenga kubwa zaidi: na humo nitaweka akiba nafaka zangu zote, na mali zangu. Kiisha nitaiambia roho yangu, Ee roho yangu, nna mali nyingi ulizojiwekea akiba kwa miaka mingi: pumzika, hassi, ule, unywe, ufurahi. Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo, wanakutaka roho yako. Nayo uliyojiwekea tayari yatakuwa ya nani? Ndivyo alivyo yeye ajiwekeae nafsi yake akiba wala hawi tajiri machoni pa Mungu. Akawaambia wanafunzi wake, Kwa sababu hii nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mleni: wala miili yenu mvaeni. Kwa maana maisha ni zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi. Watafakarini kunguru, hawapandi wala hawavuni: hawana pa kuweka akiba wala ghala, na Mungu huwalisha. Ninyi si hora sana kuliko ndege? Yupi wenu awezae kwa kusumbuka kujiongeza kimo chake mkono mmoja? Bassi ikiwa hamwezi hatta neno lililo dogo, ya nini kujisumbulia mambo mengine? Yatafakarini maua jinsi yameavyo: hayatendi kazi wala hayasokoti, nami nawaambieni ya kwamba hatta Sulemani, katika fakhari yake yote hakuvikwa kama mojawapo la hayo. Bassi ikiwa Mungu huvika hivi haya majani ya kondeni yaliyopo leo, yakatupwa kalibuni kesho, si ninyi zaidi sana, enyi wa imani haba? Bassi ninyi msitafute mtakavyokula wala mtakavyokunywa, wala msiwe na roho yenye tashwishi. Maana mataifa wa dunia huyatafuta hayo yote, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mnahitaji hayo. Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na haya yote mtazidishiwa. Msiogope, enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapeni ufalme. Viuzeni mlivyo navyo, katoeni sadaka, jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, asikokaribia mwizi, wala nondo kuharibu. Kwa maana hazina yenu ilipo ndipo na itakapokuwa na mioyo yenu. Mwe, bassi, mmefungwa viuno, na taa zikiwaka; na ninyi kama watu wanaomngojea bwana wao, atakapoondoka arusini, illi akija na kubisha, wamfungulie marra moja. Wa kheri watumishi wale ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesba. Amin, nawaambieni, atajifunga, atawaketisha, atakuja kuwakhudumia. Na akija kesha la pili au akija kesha la tatu, na kuwakuta hivi, wa kheri watumishi wale. Lakini jueni haya ya kuwa mwenye nyumba angaliijua saa atakayokuja mwizi, angalikesha asiache nyumba yake kuvunjwa. Na ninyi, bassi, mwe tayari, kwa sababu saa msiyodhani, Mwana wa Adamu yuaja. Petro akasema, Bwana, unatuambia sisi mfano huu au watu wote pia? Bwana akasema, Nani, bassi, aliye wakili mwaminifu niwenye busara, ambae Bwana wake atamweka juu ya ntumishi wake wote, awape watu posho lao kwa saa yake? Yu kheri mtumishi yule ambae bwana wake ajapo atamkuta amefanya hivyo. Amin, nawaambieni, atamweka juu ya mali zake zote. Bali mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja; akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume na wanawake, na kula na kulewa; bassi, bwana wa mtumwa yule atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande vipande, atampa sehemu yake pamoja na wasioamini. Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya Bwana wake, asijiweke tayari, wala kutenda mapenzi yake, atapigwa mapigo mengi; na yule asiyejua, nae amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa mapigo machache. Killa aliyepewa vingi kwake huyu vitatakwa vingi: nae waliyemkabidhi vingi, kwake yeye watataka vingi zaidi. Nimekuja kutupa moto duniani, na ukiwa umekwisha kuwashwa nataka nini zaidi? Nina ubatizo wa kubatizwa nao, na nina dhiiki namna gani hatta utakapotimizwa! Je! wadhani kwamba nimekuja niipe dunia amani? Nawaambieni, Sivyo, bali mafarakano. Kwa maana tangu sasa katika nyumba moja watakuwa watu watano wamefarakana, watatu na wawili, na wawili na watatu. Baba wa mtu atafarakana na mwanawe, na mwana na baba yake, mama ya mtu na binti yake, na binti na mama yake, mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu. Akawaambia na makutano pia, Killa muonapo wingu likizuka magharibi, mwasema marra, Mvua inakuja. Na killa ivumapo kaskazi mwasema, Itakuwa joto; ikawa. Enyi wanafiki, mwajua kuufasiri uso wa inchi na mbingu; imekuwaje, bassi, hamjui kuyafasiri majira haya? Na mbona ninyi katika nafsi zenu hamwamui yaliyo haki? Bassi, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa liwali, njiani ujitahidi kupatanishwa nae: asije akakukokota mbele ya kadhi, yule kadhi akakutia katika mikono ya askari, yule askari akakutupa gerezani. Nakuambia, Hutoki humo kabisa hatta uishe kulipa roho pesa ya mwisho. WAKATI huohuo walikuwapo watu wakimwarifu khabari za Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao. Akajibu, akawaambia, Je! Mwadhani ya kuwa Wagalilaya hawo walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote hatta wakapata mateso kama hayo? Nawaambieni sivyo: lakini msipotuhu nyote mtaangamia vivyo hivyo. Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara katika Siloam, ukawaangamiza, mwadhani ya kuwa walikuwa wakosaji kuliko watu wote wakaao Yerusalemi? Nawaanibieni, Sivyo: lakini msipotubu, nyote mtaangamia vivyo hivyo. Akanena mfano huu: Mtu mmoja alikuwa na mtini, umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake wala hakupata. Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda katika mtini huu, nisipate. Ukate, kwa nini uiharibu inchi pia? Akamjibu, akamwambia, Bwana, uache mwaka huu nao, hatta nikaupalilie, na kuusamadi: nao ukizaa matunda, vyema, la! haukuzaa, ndipo utaukata. Akawa akifundisha katika sunagogi mojawapo siku ya sabato. Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu miaka kumi na minane: nae amepindana, asiweze kujiinua kabisa. Bassi Yesu alipomwona, akamwita, akamwambia, Ee mwanamke, umefunguliwa udhaifu wako. Akaweka mikono yake juu yake, akanyoka marra hiyo, akaanza kumtukuza Mungu. Mkuu wa ile sunagogi akajibu, akiona hasira kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akawaambia makutano, Kuna siku sita itupasapo kufauya kazi: katika hizo, bassi, njoni mponywe wala si katika siku ya sabato. Bassi Bwana akamjibu, akasema, Ewe mnafiki, killa mmoja wenu je! hamfungui ngʼombe wake au punda wake mazizini siku ya sabato, akaenda nae kumnywesha? Na huyu, aliye binti Ibrahimu, amhae Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato? Na aliposema haya, watu wote walioshindana nae wakatahayarika, mkutano wote wakafurahi kwa ajili ya mambo matukufu yaliyotendwa nae. Bassi, akasema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Na niufananishe na nini? Umefanana na punje ya kharadali, aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake, ikakua, ikawa mti mkubwa, ndege za anga wakatua katika matawi yake. Akasema marra ya pili, Niufananishe na nini ufalme wa Mungu? Umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke akaisetiri katika pishi tatu za unga, hatta ukachacha wote pia. Akawa akizungukazunguka katika miji ni vijiji, akifundisha, na kufanya safari kwenda Yerusalemi. Mtu mmoja akamwambia, Bwana, wao wanaookolewa ni wachaehe? Akawaambia, Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba; kwa maana nawaambieni ya kwamba watu wengi watatafuta kuingia nao bawataweza. Tokea wakati ule atakapoondoka mwenye nyumba na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkinena, Bwana, Bwana! utufungulie; nae akajibu, akawaambieni, Siwajui mtokako; ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula, na kunywa mbele yako; nawe ulifundisha kalika njia zetu; nae atasema, Nawaambieni, Siwajui mtokako: ondokeni mbali nami, ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. Hapo kutakuwako kulia na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaak na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, na ninyi wenyewe nikitupwa nje. Na watakuja watu toka maawio ya jua na machweo yake na toka kaskazini na kusini, nao wataketi katika ufalme wa Mungu. Kafahamuni, wako wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wako wa kwanza watakaokuwa wa mwisho. Siku ile ile baadhi ya Mafarisayo wakamwendea, wakamwambia, Ondoka hapa, ukaende zako: kwa maana Herode anataka kukuua. Akawaambia, Enendeni zenu, nikamwambie yule mbweha, Tazama, nafukuza pepo, nafanya kazi ya kuwaponya watu leo na kesho, nami siku ya tatu nakamilika. Illakini imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa, kwa maana haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemi. Ee Yerusalemi, Yerusalemi, uwauae manabii na kuwapiga mawe wao waliotumwa kwako! marra ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hanikutaka! Angalieni, nyumba yenu imeachwa ukiwa. Amin, nawaambieni, Hamtaniona kabisa hatta wakati ule mtakaposema, Amebarikiwa yeye ajae kwa jina la Bwana. IKAWA, Yesu alipoingia katika nyumba ya mtu mmoja, mtu mkuu katika Mafarisayo, siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia. Bassi mbele yake palikuwa mtu hawezi safura. Yesu akajibu akawaambia wana sharia na Mafarisayo, akisema, Je? ni halali kuponya siku ya sabato, ama sivyo? Wakanyamaza. Akamtwaa, akamponya, akamrukhusu. Akajibu akawaambia, Nani wenu mwenye punda au ngʼombe ametumbukia kisimani, asiyemwondoa marra moja siku ya sabato? Nao hawakuweza kumjibu kwa haya. Akawaambia mfano wale waliokwitwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya kwanza; akiwaambia, Ukiitwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha kwanza, isiwe labda mwenye sifa kupita zako amekwitwa nae, akaja mwenye kuwaiteni wewe nae, akakuambia, Mpishe huyu; ndipo utaanza kwa aibu kutwaa pahali pa chini. Walakini ukiitwa, enenda ukaketi pahali pa chini: illi akija yeye aliyekuita akuamhie, Rafiki yangu, jongea huku mbele; ndipo utakapokuwa na heshima machoni pao wote waketio pamoja nawe. Kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa. Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha assubuhi au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako walio na mali, wasije na wao wakakualika wewe, ukapata malipo. Bali ufanyapo karamu, wakaribishe maskini, vilema, viwete, vipofu: nawe utakuwa kheri: kwa sababu hawana kitu cha kukulipa; maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki. Bassi mtu mmoja katika hawo walioketi pamoja nae, alipoyasikia haya, akamwambia, Yu kheri atakaekula mkate katika ufalme wa Mungu. Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa, akaalika watu wengi, akamtuma mtumishi wake saa ya karamu kwenda kuwaambia walioalikwa, Njoni, maana vitu vyote vimekwisha kuwa tayari. Wakaanza kutoa udhuru, wote pia kwa nia moja. Wa kwanza akamwambia, Nimenunua shamba, sina buddi kwenda na kulitazama; nakuomba, unisamehe. Mwingine akasema, Nimenunua ngʼombe, jozi tano: naenda niwajaribu; nakuomba unisamehe. Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hii siwezi kuja. Yule mtumishi akaenda, akamwarifu Bwana wake mambo haya. Ndipo yule mwenye nyumba akaghadhabika, akamwambia mtumishi wake, Toka upesi ukaende njia kuu na vichochoro vya mji, ukalete hapa maskini, na vilema, na viwete, na vipofu. Yule mtumishi akasema, Yamekwisha kutendeka hayo uliyoniagiza na ingaliko nafasi. Yule Bwana akamwambia mtumishi wake, Kaenda barabarani na mipakani, ukawashurutishe waingie illi nyumba yangu ipate kujaa. Maana nawaambieni ya kwamba katika watu wale walioalikwa hapana hatta mmoja atakaeionja karamu yangu. Bassi makutano mengi wakafuatana nae; akageuka akawaambia, Mtu akija kwangu, nae hamehukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake wanaume na wanawake, na uzima wake pia, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Na mfu ye yote asiyechukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuihesabu gharama kama ana vitu vya kuumaliza? Asije akawa hawezi kuumaliza baada ya kuweka msingi, watu wote wakaanza kumdhihaki, wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza. Au mfalme gani, kama anakwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana nae anaemjia pamoja na watu elfu ishirini? Kama sivyo, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, yule mtu akiwa angali mbali. Bassi, kadhalika killa mmoja wenu asiyeviacha vitu vyote alivyo navyo hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Chumvi ni njema, illakini ile chumvi ikiwa imeharibika, itatiwa nini ikolee? Haiifai inchi wala jaa; watu huitupa nje. Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie. BASSI watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia kumsikiliza. Mafarisayo na wandishi wakanungʼunika, wakasema, Huyu hukaribisha wenye dhambi, hula pamoja nao. Akawaambia mfano huu, akisema, Mtu gani wenu aliye na kondoo mia, akipotewa na mmoja, asiyewaacha wale tissa na tissaini jangwani, na kumwendea yule aliyepotea, hatta atakapomwona? Bassi amwonapo humweka mabegani mwake, akifurahiwa. Nae akija kwake huwaila rafiki zake na jirani zake, huwaambia, Furahini pamoja nami, kwa maana nimemwona kondoo wangu aliyepotea. Nawaambieni, Kadhalika itakuwako furaha mbinguni kwa mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa wenye haki tissa na tissaini, wasiohitaji toba. Ama mwanamke gani aliye na rupia kumi, akipotewa na rupia mmoja, asiyewasha taa, na kuifagia nyumba, akitatuta kwa bidii, hatta atakapoiona? Bassi, aionapo, huwaita shoga zake na jirani zake, hunena, Furahini pamoja nami, kwa maana nimeiona ile mpia niliyoipoteza. Kadhalika nawaambia ninyi, iko furaha mbele ya malaika zake Mungu kwa mwenye dhambi mmoja atubuye. Akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili. Yule aliye mdogo akamwambia baba yake, Baba, nipe sehemu ya mali iniangukiayo. Akawagawanyia vitu vyake. Hatta baada ya siku si nyingi yule mdogo akakusanya vitu vyake vyote, akasafiri kwenda inchi ya mbali: akatapanya huko mali zake kwa maisha ya uasharati. Alipokwisha kutumia vyote njaa kuu ikaingia inchi ile, yeye nae akaanza kuhitaji. Akaenda akashikamana na mmojawapo wa wenyeji wa inchi ile, nae akampeleka shambani kwake, kulisha nguruwe. Akawa akitamani kujishihisha tumbo lake kwa maganda yale waliyokula nguruwe: wala hapana mtu aliyemna kitu. Hatta alipojirudia nafsi yake, akasema, Watumishi wa mshahara wangapi wa baba yangu wanakula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu, nitamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu, na mbele yako: sistahili kuitwa mwana wako baada ya hayo: unifanye kuwa kama mmojawapo wa watumishi wako. Akaondoka, akaenda kwa baba yake. Alipokuwa angali mbali, baba yake akamwona, akamhurumia, akapiga mbio, akamwangukia shingoni, akambusu sana. Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili baada ya hayo kuitwa mwana wako. Lakini baba yake akawaambia watumishi wake, Ileteni joho iliyo bora, mkamvike: mpeni pete kwa kidole chake na viatu kwa miguu yake. Kamleteni yule ndama aliyenona, mkamchinje: tukale na kufurahi. Kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, nae amefufuka: alikuwa amepotea, nae ameonekana. Wakaanza kufanya furaha. Bassi, yule mwanawe mkubwa alikuwa shamba, na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, akasikia sauti ya kuimba na kucheza. Akamwita mmojawapo wa watumishi wake akamwuliza khabari, Mambo bayo, maana yake nini? Akamwambia, Ndugu yako amekuja: na baba yako amemchinja yule ndama aliyenona kwa sababu amempata yu mzima. Akakasirika wala hakutaka kuingia: bassi, baba yake akatoka akamsihi. Akamjibu baba yake akamwambia, Tazama, mimi nimekutumikia hii miaka mingapi: wala sikukhalifu amri yako wakati wo wote wala hukunipa mimi mwana mbuzi wakati wo wote illi nifurahi pamoja na rafiki zangu. Bali alipokuja mwana wako huyo, aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona. Nae akamwambia, Mwanangu, wewe siku zote u pamoja nami, na vitu vyote nilivyo navyo ni vyako. Tena kufanya furaha na kuona furaha kulikuwa wajib, kwa maana huyu ndugu yako alikuwa amekufa, nae amefufuka: alikuwa amepotea, nae ameonekana. TENA Yesu akawaambia wanafunzi wake, Kulikuwa na mtu tajiri, aliyekuwa na wakili; huyu akashitakiwa kwake kuwa anatapanya mali zake. Akamwita, akamwambia, Nini hii nisikiayo juu yako? Toa khabari ya uwakili wako, maana huwezi tena kuwa wakili. Yule wakili akasema moyoni, Nifanyeje, kwa maana bwana wangu ananiondolea nwakili? Kulima siwezi; kuomba natahayari. Nimekwisha kujua nitakalotenda, illi, nitolewapo katika nwakili, wanikaribishe nyumbani mwao. Bassi akawaita wadeni wa bwana wake killa mmoja, akamwambia wa kwanza, Wawiwani na bwana wangu? Akasema, Tanaki mia za mafuta. Akamwambia, Twaa khati yako; haya, kaa kitako, andika khamsini. Akiisha, akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Mikanda mia ya nganu. Akamwambia, Twaa khati yako, andika themanini. Yule bwana akamsifu wakili asiye haki, kwa kuwa alitenda kwa busara: kwa maana wana wa zamani hizi wana busara kuliko wana wa nuru, katika kizazi chao wenyewe. Na mimi nawaambia ninyi, Jifanyieni rafiki kwa mamona ya udhalimu, illi itakapopunguka wawakaribishe ninyi katika makao ya milele. Aliye mwaminifu katika kile kilicho kidogo huwa mwaminifu na katika kile kilicho kikubwa: nae aliye mdhalimu katika kile kilicho kidogo, huwa mdhalimu na katika kile kilicho kikubwa. Bassi, ikiwa hamkuwa waaminifu katika mamona ya udhalimu, nani atakaewaaminisheni mali ya kweli? Na ikiwa hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, nani atakaewapeni mali iliyo yenu wenyewe? Hakuna mtumishi awezae kuwatumikia bwana wawili: maana au atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na Mamona. Mafarisayo nao wakayasikia haya yote, nao walikuwa wakipenda fedha; wakamdhihaki. Akawaambia, Ninyi ndio watu wanaodai kuwa wenye haki mbele ya wana Adamu, lakini Mungu anajua mioyo yenu; kwa maana lililotukuka kwa wana Adamu, ni chukizo mbele ya Mungu. Torati na manabii zilikuwako mpaka Yohana. Tangu wakati ule, khabari njema ya ufalme wa Mungu inakhubiriwa, na killa mtu anauingia kwa nguvu. Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na inchi vitoweke kuliko nukta moja ya torati itanguke. Killa amwachae mkewe na kumwoa mwingine, amezini; nae amwoae yeye aliyeachwa na mumewe azini. Palikuwa na mtu tajiri, aliyevaa porfuro na bafuta, akafanya furaha kilia siku na anasa. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, hutupwa mlangoni pake, ana vidonda, akitamani kushibishwa na makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri: hatta mbwa nao huja, humramba vidonda vyake. Ikawa maskini akafa, akachukuliwa na malaika kifuani kwa Ibrahimu. Akafa na yule tajiri, akazikwa. Bassi katika akhera akainua macho yake, akiwa katika adhabu, akamwona Ibrahimu yuko mbali, na Lazaro kifuani pake. Akalia, akasema, Baba Ibrahimu, unirehemu, umtume Lazaro, achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa maana naumia katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kuwa ulipokea mema yako katika maisha yako, na Lazaro kadhalika mabaya; lakini sasa yeye yupo hapa anafarajiwa, nawe unanmizwa. Na zaidi ya haya yote, kati yetu sisi na ninyi lipo shimo kuhwa limewekwa, hatta watu watakao kutoka huku wasiweze kuja kwenu, wala wale wa huko wasivuke kuja kwetu. Akasema, Bassi, nakuomba, Baha, umtume nyumnani kwa haha yangu; maana nina ndugu watano; awashuhudie, wasije nao mahali hapa pa adhabu. Ibrahimu akasema, Wana Musa na manabii; wawasikilize wao. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini akienda kwao mmoja kutoka wafu watatubu. Akamwambia, Wasiposikia Musa na manabii, ajapoondoka mtu katika wafu, hawatashawishwa. AKAWAAMBIA wanafunzi wake, Mambo ya kukosesha hayana buddi kutokea, lakini ole wake mtu yule ayaletae! Ingemfaa huyu zaidi jiwe la kusagia litiwe shingoni pake akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa hawa wadogo. Jihadharini: ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu, msamehe, na akikosa marra saba katika siku moja, akakurudia marra saba, akisema, Natubu, msamehe. Mitume wakamwambia, Bwana, utuongezee imani yetu. Bwana akasema, Mkiwa na imani kama punje ya kharadali, mngeuambia mzambarau huu, Ngʼoka ukapandwe baharini, nao ungewatiini. Lakini nani kwenu mwenye mtumishi anaelima, an anaeehunga kondoo? je! amwambia marra atakapoingia, akitoka mashamba, Njoo upesi, keti, ule chakula? La! kinyume cha hayo, atamwambia, Pakua chakula, nile; jifunge, unikhudumie hatta nikiisha kula na kunywa; na baada ya haya utakula na kunywa mwenyewe. Je! amshukuru yule mtumishi kwa sahahu alifanya alivyoamriwa? Sidhani. Kadhalika na ninyi, mkiisha kufanya vyote mlivyoamriwa, semeni, Sisi watumishi wasiofaa; tumetenda yaliyotupasa kutenda. Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemi, alikuwa akipita kati ya Samaria na Galilaya. Alipokuwa akiingia kijiji kimoja, wakakutana nae watu kumi wenye ukoma, waliosimama mbali; nao wakapaaza sauti zao wakisema, Yesu, Bwana, uturehemu. Alipowaona, akawaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa katika kwenda kwao wakatakasika. Mmoja wao akiona ya kuwa amepona, akarudi akimtukuza Mungu kwa sauti kuu; akaanguka kufudifudi miguuni pake, akimshukuru; nae ni Msamaria. Yesu akajiliu, akasema, Si wote kumi waliotakasika? Wale tissa wa wapi? Hiawakupatikana waliorudi kumpa Mungu sifa zake, illa mgeni huyu. Akamwambia, Simama; enenda zako; imani yako imekuokoa. Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu waja lini? akawajibu, akasema, Ufalme wa Mungu hauji kwa kupelelezwa. Wala hawatasema, Tazama, huko au huko! maana fahamuni! ufalme wa Mungu umo ndani yenu. Akawaambia wanafunzi wake, Siku zitakuja mtakapotamani kuona siku mojawapo ya siku za Mwana wa Adamu wala hamtaiona. Na watawaambieni, Tazama huko, au tazama huko! Msiondoke hapo mlipo wala msiwafuate. Kwa maana kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hatta upande huu chini ya mbingu, ndivyo na Mwana wa Adamu atakavyokuwa katika siku yake. Lakini kwanza hana buddi kupata mateso mengi, na kukataliwa na kizazi biki. Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa na katika siku za Mwana wa Adamu. Walikuwa wakila, wakinywa, wakioa, wakiozwa, hatta siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, gbarika ikafika, ikawaangamiza wote. Vivyo hivyo kama ilivyokuwa siku za Lut: walikuwa wakila, wakinywa, wakimmua, wakiuza, wakipanda, wakijenga; hatta siku ile amhayo Lut alitoka Sodom, kukanya moto na kiberiti kutoka mbinguni, vikawaangamiza wote. Kadhalika itakuwa katika siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu. Katika siku ile, aliye juu darini, na vyombo vyake ndani ya nyumba, asishuke illi kuvitwaa: nae aliomo shambani vivyo hivyo asirejee nyuma. Mkumbukeni mkewe Lut. Mtu ye yote atakaeisalimisha roho yake ataiangamiza, na mtu ye yote atakaeitoa ataihifadhi. Nawaambieni, Usiku ule watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja, mmoja atatwaliwa, na mmoja ataachwa. Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja, mmoja atatwaliwa, na mmoja ataachwa. Watu wawili watakuwa mashambani; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. Wakajibu wakamwambia, Wapi, Bwana? Akawaambia, Mzoga uliko ndiko watakakokutana tai. AKAWAAMBIA na mfano ya kama imewapasa kumwomba Mungu siku zote wala wasikate tamaa, akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani; hamchi Mungu wala hajali mtu. Na katika mji huo palikuwa na mjane aiiyemwendeaendea, akisema, Nipatie haki yangu, ukaniokoe na adui yangu. Nae hakukubali muda wa siku kadha wa kadha; khalafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa mimi simchi Mungu wala sijali mtu; illakini kwa kuwa mjane huyu ameniudhi, nitampatia haki yake, asije akanidhoofisha kwa kunijia daima. Bwana akasema, Sikieni asemavyo yule kadhi asiye haki. Bassi Mungu je! hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, nae ni mvumilivu kwao? Nawaambieni atawapatia haki upesi. Walakini Mwana wa Adamu atakapokuja, je! ataiona imani duniani? Yesu akawaambia mfano huu watu waliojidhani nafsi zao kuwa wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Watu wawili walipanda hekaluni kusali; mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama, akasali hivi kwa nafsi yake, Mungu, nakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine, wanyangʼanyi, wazinzi, waia kama na huyu mtoza ushuru. Nafunga marra mbili kwa juma; nalipa zaka za mapato yangu yote. Na yule mtoza ushuru akasimama mbali, asitake hatta kuinua macho yake mbinguni; hali akajipigapiga kifua, akisema, Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia ninyi, huyu alishuka nyumbani kwake amepata kibali kuliko yule: kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa. Bassi wakamletea hatta watoto wachanga illi awaguse; lakini wanafunzi wake walipoona wakawakaripia. Bali Yesu akawaita waje kwake, akisema, Waacheni watoto waje kwangu, kwa maana watu kama hawo ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni, Yeye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto, hatauingia kamwe. Na mtu mkuhwa mmoja akamwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanyeni nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia, Mbona waniita mwema? Hakuna mwema illa mmoja ndiye Mungu. Wazijua amri, Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudu uwongo, Waheshimu baba yako na mama yako. Akasema, Haya yote nimeyashika tangu ujana wangu. Yesu aliposikia haya, akamwambia, Neno moja hujalipata bado; viuze vitu vyote ulivyo navyo, ukawagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kiisha, njoo unifuate. Lakini aliposikia maneno haya akafanya huzuni nyingi: maana alikuwa mtu tajiri sana. Bassi Yesu alipoona ya kuwa amefanya huzuni nyingi, akasema, Kwa shidda gani wenye mali watauingia ufalme wa Mungu. Kwa maana ni rakhisi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Nao waliposikia, wakasema, Nani, bassi, awezae kuokoka? Akasema, Yasiyowezekana kwa wana Adamu, yawezekana kwa Mungu. Petro akasema, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. Akawaambia, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au wazazi, au ndugu, au mke, au watoto kwa ajili ya ufalme wa Mungu, illa atapokea zaidi marra nyingi sasa wakati huu, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele. Bassi, Yesu akawachukua wale thenashara akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemi, na yatatimizwa mambo yote aliyoandikiwa Mwana wa Adamu na manabii. Kwa maana atatiwa katika mikono ya Mataifa, atafanyiwa dhihaka na kutendwa jeuri, na kutemewa mate; na wakiisha kumpiga mijeledi, watamwua; na siku ya tatu atafufuka. Nao hawakufahamu haya hatta kidogo, neno hili likawa limefichwa kwao, wala hawakuyajua yaliyonenwa. Ikawa alipokaribia Yeriko, pafikuwa na kipofu, amekaa kando ya njia akiomba. Aliposikia makutano yanapita, akauliza khabari, Kuna nini? Wakamweleza, Yesu wa Nazareti anapita. Akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daud, unirehemu. Bassi, waliotangulia wakamkemea, anyamaze; lakini yeye akazidi sana kupiga makelele, Mwana wa Daud, unirehemu. Yesu akasimama, akaamuru aletwe kwake; na alipomkaribia akamwuliza, Wataka nikufanyie nini? Akasema, Bwami, nipate kuona. Yesu akamwambia, Upewe kuona imani yako imekuponya. Marra akapata kuona, akamfuata, akimtukuza Mungu; na watu wote walipoona wakampa Mungu sifa. AKAINGIA Yeriko akawa akipita katikati yake. Na tazama, mtu mmoja, jina lake alikwitwa Zakkayo, mkubwa wa watoza ushuru, nae tajiri: akatafuta kumwona Yesu, ni mtu gani, asiweze lakini kwa sababu ya makutano, maana kimo chake alikuwa mfupi. Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa sababu alitaka kupita njia ile. Na Yesu, alipofika mahali pale, akatazama juu, akamwona, akamwambia, Zakkayo, shuka upesi; maana leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. Akashuka upesi, akamkaribisha kwa furaha. Hatta watu walipoona wakanungʼunika wote, wakisema, ya kama, Ameingia akae kwa mtu mwenye dhambi. Zakkayo akasimama, akamwambia Bwana, Bwana, nussu ya mali zangu ninawapa maskini; na kama nimetoza mtu kitu kwa kumsingizia uwongo ninamrudishia marra nne. Yesu akamwambia, Leo wokofu umefika nyumbani humu, kwa kuwa huyu nae ni mwana wa Ibrahimu. Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja illi kutafuta kilichopotea na kukiokoa. Nao wakisikia haya akaongeza akawaambia mfano, kwa sababu alikuwa akikaribia Yerusalemi, nao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana marra moja. Bassi akasema, Mtu mmoja, mungwana, alisafiri kwenda inchi ya mbali illi kujipatia ufalme na kurejea. Akawaita watu kumi katika watumishi wake, akawapa mane za fedha kumi, akawaambia, Fanyeni biashara hatta nitakaporudi. Wenyeji wake wakanichukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatutaki mtu huyu atutawale. Ikawa aliporejea, baada ya kuupokea ufalme, akatoa amri waitwe wale watumishi aliowapa ile fedha, apate kujua jinsi walivyofanya biashara. Wa kwanza akaja akasema, Bwana, mane yako imepata mane kumi. Akasema, Vema, mtumishi mwema, kwa sababu umekuwa mwaminifu kwa kitu kilicho kidogo, bassi, uwe na mamlaka juu ya miji kumi. Akaja wa pili, akisema, Mane yako, Bwana, imepata mane tano. Akamwambia yule nae, Na wewe uwe juu ya miji mitano. Akaja mwingine akasema, Bwana, tazama, mane yako hii niliyokuwa nayo, imewekwa akiba katika leso: maana nalikuogopa, kwa sababu wewe mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda. Akamwambia, Kwa kinywa chako nitakuhukumu, ee mtumishi mwovu wewe. Ulijua ya kuwa mimi mtu mgumu, naondoa nisichoweka, navuna nisichopanda; mbona, bassi, hukuweka fedha yangu kwao watoao riba, nami nikija ningaliipata pamoja na faida? Akawaambia waliohudhuria, Mnyangʼanyeni mane yake moja mkampe yule mwenye mane kumi. (Wakamwambia, Bwana, ana mane kumi). Maana nawaambieni, Killa aliye na kitu, atapewa, bali yeye asiye na kitu hatta kile alicho nacho atanyangʼanywa. Walakini wale adui zangu wasiotaka niwatawale, waleteni huku mkawachinje mhele zangu. Alipokwisha kusema haya, akaendelea mbele, akipanda kwenda Yerusalemi. Hatta alipokaribia Bethfage na Bethania karibu ya mlima wa mizeituni, akatuma wawili katika wanafunzi wake, akisema, Enendeni zenu hatta kile kijiji kinachowakabili ninyi, na mkiingia ndani, mtaona mwana punda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni. Na mtu akiwaambieni, Mbona mnamfungua? semeni hivi, Bwana ana haja nae. Bassi, wale waliotumwa wakaenda, wakaona vile vile kama alivyowaambia. Na walipokuwa wakimfungua mwana punda, wenyewe wakawauliza, Mnamfunguliani huyu mwana punda? Wakasema, Bwana ana haja nae. Wakampeleka kwa Yesu, wakatandika nguo zao juu ya yule mwana punda wakampandisha Yesu. Nae alipokuwa akienda, wakatandaza nguo zao njiani. Hatta alipokuwa amekwisha kukaribia matelemko va mlima wa mizeituni, kundi lote la wanafunzi wake wakaanza kufurahi na kumhimidi Mungu kwa sauti kuu, kwa ajili ya miujiza yote waliyoiona, wakinena Amebarikiwa mfalme ajae kwa jina la Bwana, amani mbinguni, na utukufu palipo juu. Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, wakemee wanafunzi wako. Akajibu, akasema, Nawaambieni kwamba, wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele. Nae alipokaribia akauona mji, akaulilia, akasema, Laiti ungalijua siku hii yaliyo ya amani! lakini sasa yamefichwa machoni mwenu; Kwa maana siku zitakujilia, adui zako watakapokujengea boma; watakuzunguka, watakudhiikisha pande zote; watakuangusha chini, na watoto wako ndani yako; wasikuachie jiwe juu ya jiwe; kwa kuwa hukujua majira ya kujiliwa kwako. Akaingia hekaluni, akaanza kuwatoa wakuzao na wanunuao ndani yake; akiwaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi. Akawa akifundisha killa siku hekaluni, makuhani wakuu na waandishi na wakubwa wa watu wakatafuta kumwangamiza, nao bawakuona la kutenda; maana watu wote waliambatana nae, wakimsikiliza. IKAWA siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni na kuikhubiri Injili, makuhani wakuu na waandishi, na pamoja nao wazee, wakamtokea ghafula, wakasema nae, wakinena, Kwa mamlaka gani unatenda haya? Na ni nani aliyekupa mamlaka hii? Akajibu, akawaambia, Nami nitawauliza ninyi neno moja, kaniambieni. Ubatizo wa Yohana, ulitoka mbinguni au kwa wana Adamu? Wakasemezana wao kwa wao, wakinena, Kama tukisema, Toka mbinguni, atasema, Mbona hamkumwamini bassi? Bali tukisema, Kwa wana Adamu, watu wote watatupiga mawe: kwa sababu wamesadiki ya kuwa Yohana ni nabii. Wakajibu kwamba, Hatujui atokako. Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani ninatenda haya. Akaanza kuwaambia watu mfano huu: Mtu alipanda mizabibu, akapangisha wakulima, akaenda inchi nyingine kwa muda wa siku nyingi. Na wakati wa mavuno akatuma mtumishi kwa wale wakulima illi wampe baadhi ya matunda ya mizabibu, wakulima wakampiga, wakamtoa hana kitu. Akaongeza akampeleka mtumishi mwingine, wakampiga huyu wakamfedhehesha, wakamtoa hana kitu. Akaongeza akampeleka wa tatu, wakamtia jeraha, wakamfukuza. Yule Bwana wa mizabibu akasema, Nifanyeje? Nitampeleka mwana wangu, mpendwa wangu, labuda wakimwona yeye watamheshimu. Lakini wale wakulima, walipomwona, wakafanya shauri wao kwa wao, wakinena, Huyu ndiye mrithi; na tumwue bassi, urithi upate kuwa wetu. Wakamtupa nje ya shamba la mizabibu wakamwua. Bassi yule bwana wa shamba la mizabibu atawatendani? Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine. Waliposikia wakasema, Mungu na apishe mbali. Akawakazia macho, akasema, Maana yake nini, bassi, neno hili lililoandikwa, Jiwe walilolikataa waashi Hili limekuwa jiwe kuu la pembeni? Killa mtu aangukae juu ya jiwe hilo atavunjikavunjika, nae ambae litamwangukia litamsagasaga. Makuhani wakuu na waandishi wakatafuta kumkamata saa hiyo hiyo, wakawaogopa watu: maana walitambua ya kuwa ule mfano amewanena wao. Wakamvizia wakatuma wapelelezi, nao wakajifanya kuwa wenye haki, illi wamnase kwa neno lake, kusudi wamtie katika enzi na mamlaka ya liwali. Wakamwuliza, wakinena, Mwalimu, twajua ya kuwa wanena yaliyo kweli na kuyafundisha, wala hujali cheo cha mtu, bali katika kweli waifundisha njia ya Mungu: Je! ni halali kumpa Kaisari kodi au sivyo? Lakini akatambua ujanja wao, akawaambia, Nionyesheni dinari: ina sura ya nani? ina anwaui ya nani? Wakasema, ya Kaisari. Akawaambia, Bassi, mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu. Wala hawakuweza kumshika kwa neno lake mbele ya watu: wakastaajabia jawabu lake, wakanyamaza. Kiisha baadhi ya Masadukayo wakamwendea, watu wanenao ya kwamba hakuna kiyama: wakamwuliza, wakinena, Mwalimu, Musa alituandikia ya kama ndugu ya mtu akifa, nae ana mke, na mtu huyo akifa hana mtoto, ni lazima ndugu yake amtwae yule mke, akampatie ndugu yake mzao. Bassi, palikuwa na ndugu saba: wa kwanza akatwaa mke akafa, hana mtoto, wa pili akamtwaa yule mke, akafa nae, hana mtoto. Hatta wa tatu akamtwaa, na kadhalika hawa saba hawakuacha watoto, wakafa. Mwisho wa hawo wote yule mwanamke akafa nae. Bassi katika kiyama, atakuwa mke wa nani katika hawo? maana wale saba walikuwa nae. Yesu akajibu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa, na kuozwa, bali wao watakaohesabiwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na ufufuo wa wafu, hawaoi wala hawaozwi, kwa kuwa hawawezi kufa tena, maana huwa sawasawa na malaika; tena ni wana wa Mungu kwa kuwa wana wa ule ufufuo. Walakini ya kuwa wafu wafufuka, Musa nae alionyesha katika sura ya Kijiti, hapo amtajapo Bwana kuwa ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaak, na Mungu wa Yakobo. Bassi, yeye siye Muugu wa wafu, bali Mungu wa wahayi, maana wote ni wahayi kwake. Baadhi ya waandishi wakajibu wakasema, Mwalimu, umesema vema. Wala hakuthubutu mtu kumwuliza neno baada ya haya. Akawaambia, Kwa maana gani hunena ya kwamba Kristo yu mwana wa Daud? Na Daud mwenyewe asema katika chuo cha Zaburi, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume, Hatta niwafanyapo adui zako kuwa chini ya miguu yako. Daud, bassi, amwita Bwana, na amekuwaje Mwana wake? Hatta watu wote walipokuwa wakimsikiliza, akawaambia wanafunzi wake, Jihadharini na waandishi wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, na kuketi mbele katika sunagogi, na mahali palipo mbele katika karamu. Wanakula nyumba za wajane: na kwa unafiki husali sala ndefu. Hawo watapokea hukumu iliyo kubwa zaidi. AKAINUA macho yake akawaona watu wakitia sadaka zao katika sanduku ya hazina, watu matajiri. Akamwona na mjane mmoja maskini, akitia robo pesa mbili. Akasema, Amin, nawaambieni, Huyu mjane maskini ametia vingi kuliko wote: kwa maana hawa wote wametia katika sadaka za Mungu baadhi ya mali iliyowazidi, bali huyu katika mahitaji yake ametia vitu vyote alivyokuwa navyo. Hatta watu kadha wa kadha walipokuwa wakinena khabari za hekalu, ya kama lilipambwa kwa mawe mazuri, na sadaka za watu, akasema, Haya mnayoyatazama, siku zitakuja, halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa. Wakuimwuliza, wakisema, Mwalimu, haya yatakuwa lini, bassi? Na nini dalili ya kuwa haya yote ni karibu ya kutimia? Akasema, Jibadharini, msidanganyike; kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ndiye, na, Majira yamekaribia. Bassi, msiwafuate hawo. Nanyi mtakaposikia khabari za vita na fitina msitishwe: maana haya hayana buddi kutukia kwanza, lakini mwisho wenyewe hauji marra moja. Kiisha akawaambia, Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme: kutakuwa na matetemeko makubwa ya inchi mahali mahali, na njaa, na tauni. Kutakuwa na mambo ya kutisha, na ishara kuu kutoka mbinguni. Lakini kabla ya haya yote watawakamateni na kuwaudhini, watawapelekeni mbele ya sunagogi na gerezani, mkichukuliwa mbele ya wafalme na maliwali kwa ajili ya jina langu. Lakini haya yatapata kuwa ushuhuda wenu. Azimuni bassi mioyoni mwenu, msitafakari mbele mtakavyojibu. Kwa maana mimi nitawapeni kinywa na hekima, ambayo watesi wenu hawataweza kuikana wala kushindana nayo. Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha wengine wenu. Mtachukizwa na watu wote kwa ajili ya jina langu. Na unywele wa vichwa vyenu hautapotea kamwe. Kwa subira yenu mtazipata robo zenu. Lakini, mtakapoona Yerusalemi unazungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kuwa uharibifu wake umekaribia. Ndipo walio katika Yahudi wakimbilie milimani, na walio katikati yake watoke waende zao, na walio shambani wasiuingie. Kwa sababu hizi ni siku ya mapatilizo, yote yaliyoandikwa yapate kutimizwa. Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku zile! kwa maana itakuwa shidda kuu juu ya inchi, na ghadhabu juu ya watu hawa. Nao wataanguka kwa ukali wa upanga, watachukuliwa mateka mpaka mataifa yote: nao Yerusalemi utakanyagwa na mataifa, hatta majira ya mataifa yatakapotimia. Na kutakuwa ishara katika jua na mwezi na nyota: na katika inchi dhiiki ya mataifa, wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake; watu wakizimia kwa khofu, na kwa kutazamia yanayoujia ulimwengu; kwa maana nguvu za mbingu zitatikisika. Ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu kwa nguvu na utukufu mwingi. Bassi hayo yaanzapo kuwa, tazameni juu, mkainue vichwa vyenu kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia. Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti yote; iishapo kuchupua, mwaona na kutambua nafsini mwenu ya kwamba mavuno yameisha kuwa karibu. Nanyi vivyo hivyo mwonapo hayo yanakuwa, tambueni ya kuwa ufalme wa Mungu u karibu. Amin, nawaanibieni, Kizazi hiki hakitapita kamwe hatta haya yote yatimizwe. Mbingu na inchi zitapita; bali maneno yangu hayatapita kamwe. Bassi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi na ulevi, na masumbufu ya maisha haya, siku ile ikawajieni kwa ghafula, kama mtego, maana hivyo ndivyo itakavyowajia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia yote. Kwa hiyo kesheni killa wakati, mkiomba mpate kuhesabiwa kuwa mmestahili kuponea haya yote yatakayokuwa, na kusimama mahali penu mbele ya Mwana wa Adamu. Bassi killa siku alikuwa akifundisha hekaluni wakati wa mchana; na wakati wa usiku akitoka, na kulala katika mlima uitwao mlima wa mizeituni. Watu wote wakaamka mapema wakamwendea alfajiri mle hekaluni illi kumsikiliza. IKAKARIBIA siku kuu ya mikate isiyochachwa, iitwayo Pasaka. Makuhani wakuu na waandishi wakatafuta njia ya kumwua, kwa maana walikuwa wakiwaogopa watu. Shetani akamwingia Yuda, aitwae Iskariote, nae alikuwa katika hesabu ya wale thenashara. Akaenda zake akasema na makuhani wakuu na majemadari jinsi ya kumtia katika mikono yao. Wakafurahi, wakapatana kumpa fedha. Akaahidi, akatafuta nafasi kumsaliti kwao pasipo kuwapo makutano. Ikawadia siku ya mikate isiyochachwa, ilipopasa kuchinja pasaka. Akapeleka Petro na Yohana, akisema, Enendeni, mkatuandikie pasaka, illi tuile. Wakamwambia, Wapi utakapo tuiandalie? Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini, atakutana nanyi mtu mume achukuae mtungi wa maji: mfuateni mpaka nyumba atakayoingia. Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu akuambia, Ki wapi chumba cha wageni, nipate kula Pasaka humo pamoja na wanafunzi wangu? Na mtu yule atawaonyesha orofa kubwa iliyopambwa; huko andalieni. Wakaenda wakaona kama alivyowaambia, wakaiandalia Pasaka. Bassi saa ilipowadia, akaketi, na mitume pamoja nae. Akawaambia, Nimetamani sana kula pasaka hii pamoja nanyi, kabla va kuteswa: kwa maana nawaambieni, Sitaila kabisa hatta itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu. Akakipokea kikombe, akashukuru, akasema: Twaeni hiki mkagawanye ninyi kwa ninyi; Maana nawaambieni, Sitakunywa tangu sasa mazao ya mzabibu hatta ufalme wa Mungu utakapokuja. Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Nacho kikombe vivyo hivyo baada ya kula, akinena, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu. Illa angalieni, mkono wake anisalitiye u pamoja nami mezani. Kwa maana Mwana wa Adamu aenda zake kama ilivyoamriwa; lakini ole wake mtu yule ambae anasalitiwa nae! Nao wakaanza kuulizana wao kwa wao, ni nani katika wao atakaetenda neno hili. Kulikuwa na mashindano kwao, ni nani anaehesabiwa kuwa mkubwa. Akawaambia, Wafalme wa Mataifa huwatawala, na wenye mamlaka juu yao huitwa wafadhili. Lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa wenu awe kama aliye mdogo; nafe atanguliae kama akhudumuye. Maana nani mkubwa, aketiye chakulani, ama akhudumuye? Siye aketiye chakulani? Lakini mimi kati mwenu kama akhudumuye. Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu. Nami nawawekea ninyi ufalme, kama alivyoniwekea Baba yangu; mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu, na kuketi katika viti vya enzi, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli. Bwana akasema, Simon, Simon, tazama, Shetani amewataka ninyi awapepete kama nganu: lakini nimekuombea, illi imani yako isipunguke; nawe uongokapo, wathubutishe ndugu zako. Akamwambia, Bwana, pamoja nawe mimi ni tayari kwenda gerezani na kufa. Akasema, Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo, kabla hujanikana marra tatu kwamba hunijui. Akawaambia, Nilipowatuma bila mifuko na mkoba na viatu, mlipunguka kitu? Wakasema, Hapana. Akawaambia, Bali sasa mwenye kifuko akitwae, na mkoba vivyo hivyo; nae asiye na upanga, auze joho yake, akanunue mmoja. Kwa maana nawaambieni, Hili lililoandikwa halina buddi kutimizwa kwangu, Alihesabiwa pamoja na maasi; kwa maana linipasalo lina mwisho. Wakasema, Bwana, tazama, panga mbili hizi. Akawaambia, Zatosha. Akatoka, akaenda zake hatta mlima wa mizeituni, kama ilivyo kawaida yake: wanafunzi wake wakamfuata. Alipofika pahali pale, akawaambia, Ombeni, msiingie majaribuni. Akiisha akajitenga nao kadiri ya mtupo wa jiwe, akapiga magoti, akaomba, akisema, Baba, ukipenda, uniondolee kikombe hiki: lakini si kama nitakavyo mimi, illa utakavyo wewe vifanyike. Akamtokea malaika toka mbinguni akimtia nguvu. Nae kwa kuwa alikuwa na huzuni sana, akazidi kuomba kwa bidii. Hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka hatta inchi. Alipoondoka katika kuomba, akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala kwa huzuni, akawaambia, Mbona mnielala? Ondokeni, mkaombe, msipate kuingia majaribuni. Nae alipokuwa akisema, tazama, makutano, nae aitwae Yuda, mmoja wa wathenashara, akitangulia mbele yao, akamkaribia Yesu kumbusu. Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu? Nao waliokuwa pamoja nae walipoona yatakayokuwa, wakasema, Bwana, na tupige kwa upanga? Mmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio la kuume. Yesu akajibu, akasema, Acheni kadiri hii. Akamgusa sikio, akamponya. Yesu akawaambia waliomjia, makuhani wakuu, na majemadari wa hekalu, na wazee, Kama juu ya mnyanyangʼanyi mmetoka kwa panga na marungu? Killa siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono; lakini saa yenu hii, na mamlaka ya giza. Wakamkamata, wakamchukua, wakamleta nyumbani kwa kuhani mkuu; na Petro akafuata mbali. Hatta walipowasha moto kati yasebule wakaketi pamoja, akaketi Petro kati yao. Bassi, mjakazi mmoja akamwona ameketi mwangani, akamkazia macho akisema, Huyu nae alikuwa pamoja nae. Akakana, akisema, Mwanamke, simjui. Na punde baadae mwingine akamwona, akasema, Na wewe u mmoja wao. Petro akasema, Ewe mtu, sio mimi. Hatta khalafu, kaciiri ya saa moja, mtu mwingine akahakikisha, akisema, Hakika na huyu alikuwa pamoja nae: kwa maana ni Mgalilaya. Petro akasema, Ewe mtu, sijui unenalo. Papo hapo alipokuwa akisema yeye, jogoo akawika. Bwana akageuka, akamtazamisha Petro: Petro akalikumbuka neno la Bwana, jinsi alivyomwambia, Kabla hajawika jogoo leo, utanikana marra tatu. Akatoka nje, akalia kwa uchungu. Na wale watu waliomshika Yesu, wakamdhihaki, wakampiga. Wakamfunika macho, wakamwuliza, wakisema, Fanya unabii, ni nani aliyekupiga? Wakamnena na mengine mengi kwa kufuru. Hatta ulipokuwa mchana wakakusanyika jamii ya wazee wa watu, na makuhani wakuu, na waandishi, wakamleta kwa haraza yao, wakisema, Kama wewe u Kristo, tuambie. Akawaambia, Nijapowaambieni, hamtaamini kabisa: nami nikiwaulizeni, hamtanijibu wala kuniachilia. Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi mkono wa kuume wa ukuu wa Mungu. Wakasema wote, Bassi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mnasema kama mimi ndiye. Wakasema, Bassi, mbona tunahitaji ushuhuda? Kwa maana sisi wenyewe tumesikia kwa kinywa chake. WAKAONDOKA jamii yote, wakamleta kwa Pilato. Wakaanza kumshitaki, wakisema, Tumemwona mtu huyu amipotosha taifa letu, anawakataza watu wasimpe Kaisari kodi, akisema ya kwamba yeye mwenyewe yu Kristo, mfalme. Pilato akamwuliza, akisema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu, akamwambia, Unasema wewe. Pilato akawaambia makuhani wakuu na makutano, Mimi sioni khatiya yo yote katika mtu huyu. Nao wakamshurutisha, wakisema, Awataharakisha watu, akifundisha katika Yahudi yote, akianzia Galilaya hatta hapa. Pilato aliposikia neno hili Galilaya, akauliza, Mtu huyu ni Mgalilaya? Alipojua ni chini ya mamlaka ya Herode, akampeleka kwa Herode; nae alikuwa katika Yerusalemi siku zile. Na Herode alipomwona Yesu, akafurahiwa sana: kwa kuwa tangu zamani alikuwa akitaka kumwona, kwa sababu amesikia mambo yake; akataraja kuona ishara inafanyika nae. Akamwuliza kwa maneno mengi, yeye asimjibu lo lote. Wakasimama makuliani wakuu na waandishi, wakimshitaki kwa nguvu. Bassi Herode akamtweza pamoja na askari zake akamdhihaki, akamvika mavazi mazurimazuri, akamrudisha kwa Pilato. Ndipo Herode na Pilato wakapatana, siku ileile; kwa maana kwanza walikuwa na uadui wao kwa wao. Pilato akawaita pamoja makuhani wakuu, na wakubwa, na watu, akawaambia, Mmeniletea mtu huyu, kana kwamba anapotosha watu; nami hassi nilipomhukumu mbele yenu, sikuona khatiya katika mtu huyu katika yale mliyomshitaki; wala Herode nae; kwa maana naliwapelekeni kwake, wala hapana neno la kustahili kufa lililotendwa nae. Bassi nikiisha kumrudi, nitamfungua. Maana ilimlazimu kuwafungulia mmoja wakati wa siku kuu. Wakapiga kelele wote pamoja, wakisema, Mchukue huyu, tufungulie Barabba. Nae ni mtu aliyetiwa gerezani kwa sababu ya fitina iliyofanyika mjini, na kwa uuaji. Bassi marra ya pili Pilato akasema nao, akitaka kumfungua Yesu. Nao wakalia, wakisema, Msulibishe, msulibishe. Nae akawaambia marra ya tatu, Kwani? ubaya gani alioutenda huyu? sikuona hatta neno kwake la kustahili kufa; bassi nikiisha kumrudi nitamfungua. Lakini wakakaza kusema kwa santi kuu, wakitaka asulibiwe; zikashinda sauti zao na za makuhani wakuu. Pilato akakata maneno yafanyike waliyoyataka. Akamfungua yeye aliyetiwa gerezani kwa fitina na uuaji, waliyemtaka: akatoa Yesu kwa mapenzi yao. Walipokuwa wakimchukua, wakamshika Mkurene Simon, aliyekuwa akitoka shamba, wakamtwika yeye msalaba, auchukue nyuma yake Yesu. Wakamfuata makutano mengi ya watu, na ya wanawake, waliojipigapiga, wakaomboleza. Yesu akawageukia, akasema, Binti za Yerusalemi, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu. Kwa maana siku zinakuja watakaposema, Wa kheri walio tassa, na matumbo yasiyozaa, na maziwa yasiyonyonyesha. Ndipo watakapoanza kuiambia milima, Tuangukieni, na vilima, Tusetirini. Kwa kuwa wakifanya haya wakati wa mti ulio mbichi, wakati wa ule ulio mkavu yatakuwaje? Wakachukuliwa wawili tena, wakhalifu, wauawe pamoja nae. Hatta walipofika pahali paitwapo Kichwa, ndiko walikomsulibisha, na wale wakhalifu, mmoja mkono wa kuume, na mmoja mkono wa kushoto. Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui watendalo. Wakagawanya nguo zake, wakipiga kura. Watu wakasimama, wakitazama. Nao wakuu wakamfanyizia mzaha, wakisema, Aliokoa wengine; na ajiokoe nafsi yake, kama huyu ndiye Kristo wa Mungu, mtenle wake. Askari wakamdhihaki, wakimjia, wakimpa siki, na kusema, Kama wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi, njiokoe nafsi yako. Palikuwa na anwani juu yake kwa harufi za kiyunani na kirumi na kiebrania, HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI. Mmoja wa wale wakhalifu waliotundikwa akamtukana, akisema, Si wewe uliye Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi. Wa pili akajibu, akamkemea akasema, Humwogopi wewe hatta Mungu, ukiwa katika hukumu ile ile? Na sisi kweli ina haki; kwa maana sisi tunalipwa ijara ya haki ya matendo yetu: bali huyu hakutenda neno lisilofaa. Akamwambia Yesu, Bwana, unikumbuke ujapo katika ufalme wako. Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo utakuwa pamoja nami Peponi. Ikapata kama saa a sita, pakawa giza juu ya inchi yote hatta saa a tissa, jua likipunguka: pazia ya hekalu ikapasuka katikati. Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu: na alipokwisha kusema haya akatoa roho. Akida alipoona lililokuwa, akamtukuza Mungu, akisema, Kwa kweli mtu huyu alikuwa mwenye haki. Na makutano wote waliokusanyika kutazama haya, walipotazama yaliyofanyika, wakarudi, wakijipiga vifua. Marafiki zake wote wakasimama kwa mbali, nao wanawake waliofuatana nae toka Galilaya, wakiangalia haya, Akatoka mtu, jina lake Yusuf, nae ni mtu wa baraza yao, mtu mwema, mwenye haki (mtu huyu hakuwa akikubali shauri lao wala tendo lao), mwenyeji wa Arimathaya, mji wa Wayahudi, nae mwenyewe akiutazamia ufalme wa Mungu. Bassi mtu huyu akamwendea Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu. Akaushusha, akauzinga nguo za katani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani; hajawekwa mtu aliye yote ndani yake kamwe. Ilikuwa siku ya Maandalio, sabato ikawadia. Wanawake wakafuatana nao, wale waliokuja pamoja nae kutoka Galilaya, wakalitazama kaburi na jinsi ulivyowekwa mwili wake. Wakarudi wakafanya tayari manukato na marhamu. Na siku ya sabato wakastarehe kama ilivyoamriwa. HATTA siku ya kwanza ya juma, ikianza kupambazuka, wakaenda kaburini wakiyaleta yale manukato waliyoyaweka tayari, na wengine pamoja nao. Wakalikuta lile jiwe limefingirishwa mbali ya kaburi. Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu. Ikawa wangali wakishangaa kwa haya, kumbe! watu wawili wakisimama karibu yao, wamevaa nguo za kumetameta. Nao wakiingiwa na khofu na kuinama kifudifudi hatta inchi, wakawaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hayi katika wafu? Hayupo hapa, bali amefufuka. Kumbukeni jinsi alivyosema nanyi alipokuwa hajatoka Galilaya, akinena, ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kutiwa katika mikono ya watu wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tafu. Wakakumbuka maneno yake, wakarejea kutoka kaburi, wakawaarifu wale edashara na wale wengine wote pia mambo hayo yote. Na hao waliowaambia mitume mambo haya ni Mariamu Magdalene, na Yoanna, na Mariamu mama yake Yakobo na wengine waliokuwa pamoja nao. Maneno yao yakaonekana kuwa ni upuzi kwao, wala hawakuwasadiki. Lakini Petro akaondoka, akaenda mbio kaburini, akainama, akachungulia ndani, akaviona vile vitambaa vimewekwa peke yake, akarudi kwake, akistaajabu kwa yale yaliyotokea. Siku ileile wawili wao walikuwa wakienda hatta kijiji, jina lake Emmao, kilichokuwa mbali ya Yerusalemi yapata stadio sittini. Nao wakawa wakizumgumza haya yote yaliyotukia. Ikawa katika kuzumgumza kwao na kuulizana, Yesu mwenyewe akakaribia, akafuatana nao. Macho yao yakafumbwa, wasipate kumtambua. Akawaambia, Maneno gani haya mnayobishana katika kutembea kwenu? na tena nyuso zenu zimekunjamana. Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemi, usiyajue yaliyokuwa ndani yake siku hizi? Akawaambia, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu Mnazareti, aliyekuwa mtu nabii mwenye nguvu kwa tendo na kwa neno mbele za Mungu na watu wote; na jinsi makuhani wakuu na wakubwa wetu walivyomtoa kwa hukumu ya kufa, wakamsulibisha; nasi twalitaraja ya kuwa yeye ndiye atakaekomboa Israeli. Hatta pamoja na haya yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipokuwa haya. Kuna tena wanawake wengine wa kwetu waliotustusha, wakiamkia mapema kwenda kaburini: wasioukuta mwili wake, wakaja, wakasema ya kwamba wametokewa na malaika, waliowaambia yu hayi. Na wengine waliokuwa pamoja nasi wakaenda kaburini, wakaona vivyo hivyo kama wanawake walivyosema; illa yeye hawakumwona. Nae akawaambia, Enyi wapumbavu, na wenye mioyo mizito katika kuyaamini yote waliyoyasema manabii! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya, ndipo aingie enzini mwake? Akaanza toka Musa na manabii, akawafasiria katika maandiko yote mambo yaliyomkhusu yeye. Wakakikaribia kijiji walikokuwa wakienda; nae akajifanya kama anataka kwenda mbele. Wakamshurutisha, wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa maana kumekuchwa, na mchana unakwisha sasa. Akaingia kukaa nao. Ikawa, akiketi pamoja nao, akautwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawagawia. Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua, akatoweka asionekane nao. Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwa ikiwaka ndani yetu, alipokuwa akisema nasi njiani, akitufunulia maandiko? Wakaondoka saa ileile, wakarudi Yerusalemi, wakawakuta wale edashara wamekusanyika, nao waliokuwa pamoja nao, wakisema, Hakika Bwana amefufuka, amemtokea Simon. Nao wakawahadithia yale ya njiani, na jinsi alivyotambulikana nao kwa kumega mkate. Walipokuwa wakisema hivyo, Yesu mwenyewe akasimama kati yao, akiwaambia, Amani kwenu. Wakafadhaika, wakaingiwa na khofu, wakidhani ya kuwa wanaona pepo. Akawaambia, Mbona mmefadhaika? na kwa nini mashaka yanatokea mioyoni mwenu. Tazameni mikono yangu, na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nipapaseni, mkatazame; kwa maana pepo hana mwili na mifupa, kama mnionavyo mimi kuwa nayo. Na baada ya kusema haya akawaonyesha mikono yake na miguu yake. Bassi, wakiwa bado kuamini kwa furaha, wakitaajabu, akawaambia, Mna kitu cha kula hapa? Wakampa kipande cha samaki kilichookwa na asali kidogo. Akakitwaa, akala mbele yao. Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi. Ndipo akaamsha akili zao, wapate kuyatambua maandiko matakatifu. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, na ndivyo ilivyompasa Kristo kuteswa, na kufufuka siku ya tatu; na mataifa yote wakhubiriwe kwa jina lake toba na ondoleo la dhambi, kuanzia Yerusalemi. Nanyi mashahidi wa mambo haya. Angalieni, bassi, naituma ahadi ya Baba yangu kwenu: lakini kaeni katika mji huu Yerusalemi, hatta mtakapovikwa nguvu zitokazo juu. Akawaongoza nje mpaka Bethania: akainua mikono yake, akawabariki. Ikawa katika kuwabariki, akajitenga nao, akachukuliwa juu mbinguni. Nao wakamsujudia, wakarudi Yerusalemi na furaha kuu: wakawa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu na kumhimidi. Amin. MWANZO alikuwako Neno, nae Neno alikuwako kwa Mungu, nae Neno alikuwa Mungu. Huyu mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vyalifanyika kwa huyu. Wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao uzima ulikuwa nuru ya watu, nayo nuru yangʼaa gizani, wala giza halikuiweza. Palitokea mtu ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. Huyu alikuja kwa ushuhuda, illi aishuhudie nuru, wote wapate kuamini kwa yeye. Huyu hakuwa ile nuru, illakini aishuhudie ile nuru. Kulikuwako nuru halisi, imtiayo nuru killa mtu ajae katika ulimwengu. Alikuwako ulimwenguni, ulimwengu umepata kuwa kwa veye, wala ulimwengu haukumtambua. Alikuja kwake, nao walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa mamlaka ya kufanyika watoto wa Mungu, ndio waliaminio jina lake: waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli. Yohana akamshuhudia, akapaaza sauti yake, akinena, Huyu ndiye niliyemnena khabari zake, kwamba, Ajae nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. Na katika ujazi wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa, neema na kweli zilikuwa kwa mkono wa Yesu Kristo. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote, Mwana wa pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyefasiri khabari yake. Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma makuhani na Walawi toka Yerusalemi wamwulize, Wewe u nani? Nae aliungama wala hakukana; aliungama, Mimi siye Kristo. Wakamwuliza, Nini bassi? U Eliya wewe? Akanena, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La. Bassi wakamwambia, U nani? tuwape majibu waliotupeleka. Wajinenaje? Akasema, Mimi ni sauti ya mtu apaazae sauti jangwani, Inyosheni njia ya Bwana! kama alivyonena nabii Isaya. Nao waliotumwa walitoka kwa Mafarisayo. Wakamwuliza, wakimwambia, Mbona bassi wabatiza, kama wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule? Yohana akawajibu akanena, Mimi nabatiza kwa maji: kati mwenu amesimama msiyemjua ninyi. Ndiye ajae nyuma yangu, aliyekuwa mbele yangu, wala mimi sistahili niilegeze gidam ya kiatu chake. Haya yalifanyika Bethania ngʼambu ya Yardani, alikokuwako Yohana akibatiza. Siku ya pili yake Yohana amwona Yesu anakuja kwake, akanena, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuae dhambi ya ulimwengu! Huyu ndiye niliyemnena khabari zake, Yuaja mtu nyuma yangu, aliyekuwa mbele yangu, kwa maana alikuwa kabla yangu. Nami sikumjua: lakini kusudi adhibirishwe kwa Israeli ndio maana nalikuja nikibatiza kwa maji. Yohana akashuhudu, akasema, Nimemwona Roho akishuka, kama hua, kutoka mbinguni; akakaa juu yake. Nami sikumjua, lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyu aliniambia, Yeye ambae utakaemwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyu ndiye abatizae kwa Roho Mtakatifu. Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu. Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama na wawili katika wanafunzi wake. Akamtazama Yesu, akitembea, akasema, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu! Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. Yesu akageuka, akawaona wakifuata: akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabbi (tafsiri yake, Mwalimu), unakaa wapi? Akawaambia, Njoni muone. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Ilikuwa karibu na saa kumi. Andrea, ndugu ya Simon Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata. Huyu akamwona kwanza Simon, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi, (tafsiri yake Kristo). Akampeleka kwa Yesu. Yesu akamtazama, akasema, Wewe Simon, mwana wa Yona, utakwitwa Kefa (tafsiri yake, Petro). Siku ya pili yake Yesu akataka kuondoka kwenda Galilaya, akamwona Filipo, akamwambia, Nifuate. Nae Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mtu wa mji wa Andrea na Petro. Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na na manabii, Yesu, mwana wa Yusuf, mtu wa Nazareti Nathanaeli akamwambia, Chaweza kitu chema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone. Yesu akamwona Nathanaeli akija kwake, akamtaja khabari zake, Tazama, huyu ni Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake. Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunijua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwa chini ya mtini, nalikuona. Nathanaeli akajibu, akamwambia, Rabbi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe mfalme wa Israeli. Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nalikuambla, Nalikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya. Akamwambia, Amin, amin, nakuambieni, Tangu sasa mtaziona mbingu zimefunguka, na malaika wa Mungu wakipanda, wakishuka juu ya Mwana wa Adamu. NA siku ya tatu palikuwa arusi katika Kana ya Galilaya, na mama yake Yesu alikuwako. Yesu nae akaitwa pamoja na wanafunzi wake arusini. Hatta divai ilipowatindikia, mama yake Yesu akamwambia, Hawana divai. Yesu akamwambia, Bibi, ina nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. Mama yake akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambieni fanyeni. Palikuwako mabalasi sita ya mawe, yamewekwa huko kwa desturi ya kutawaza kwao Wayahudi, killa moja lapata kadiri ya nzio mbili au tatu. Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Wakayajaliza hatta juu. Akawaambia, Sasa tekeni, mpelekeeni mkuu wa meza. Wakapeleka. Mkuu wa meza alipoyaonja maji yaliyofanyika kuwa divai, asijue ilikotoka, (lakini watumishi walijua walioyateka maji), mkuu wa meza akamwita bwana arusi, akamwambia, Killa mtu kwanza huandaa divai iliyo njema, hatta watu wakiisha kunywa sana, ndipo huleta iliyo dhaifu: wewe umeweka divai iliyo njema hatta sasa. Mwanzo huu wa ishara Yesu alifanya Kana ya Galilaya, akauonyesha utukufu wake, wanafunzi wake wakamwamini. Baada ya haya akashuka hatta Kapernaum, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake: wakakaa huko siku chache. Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu: Yesu akapanda hatta Yerusalemi. Akaona hekaluni watu waliokuwa wakiuza ngʼombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi; Akafanya mjeledi kwa kambaa akawatoa wote katika hekalu, na kondoo, na ngʼombe, akamwaga fedha yao wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoem haya: msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara. Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako umenila. Bassi Wayahudi wakajibu wakamwambia, Ishara gani utuonyeshayo, iwapo unafanya haya? Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hii, nami kwa siku tatu nitaisimamisha. Bassi Wayahudi wakasema, Hekalu hii ilijengwa katika muda wa miaka arubaini na sita, nawe utaisimamisha kwa siku tatu? Lakini yeye alinena khabari za hekalu ya mwili wake. Bassi alipofufuliwa katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa amenena neno hili, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu. Hatta alipokuwapo Yerusalemi wakati wa Pasaka katika siku kuu, watu wengi wakaliamini jina lake, wakiona ishara zake alizozifanya. Lakini Yesu hakujiaminisha kwao, kwa kuwa yeye aliwajua wote; na kwa sababu hakuwa na haja ya watu kushuhudia khabari za niwana Adamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwana Adamu. PALIKUWA na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi; huyu alikuja kwa Yesu usiku, akamwambia, Rabbi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezae kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, illa Mungu awe pamoja nae. Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa marra ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo amwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mama yake marra ya pili akazaliwa? Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Usitaajahu kwa kuwa nilikuambia, Hamna buddi kuzaliwa marra ya pili. Upepo huenda utakako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na killa mtu aliyezaliwa kwa Roho. Nikodemo akajibu, akamwambia, Yawezaje kuwa haya? Yesu akajibu akamwambia, Je! Wewe u mwalimu katika Israeli, na haya huyafahamu? Amin, amin, nakuambia, Tulijualo twalisema, na tuliloliona twalishuhudu; na ushuhuda wetu hamwukubali. Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, nanyi hamwa, mini, mtaaminije, niwaambiapo mambo ya mbinguni? Na hapana mtu aliyepanda mbinguni, illa yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, Mwana wa Adamu alioko mbinguni. Na kama Musa alivyomwinua nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana buddi kuinuliwa: illi asipotee mtu aliye yole amwaminiye, bali awe na uzima wa milele. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hatta akampeleka Mwana wake wa pekee, illi mtu aliye yote amwaminiye asipotee, bali apate uzima wa milele. Maana Mungu hakumpeleka Mwana wake ulimwenguni auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe nae. Amwaminiye hahukumiwi; asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa, kwa maana hakuliamini jina la Mwana wa pekee wa Mungu. Na hii ndiyo hukumu, ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, watu wakapenda giza zaidi ya nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana killa atendae manyonge huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasikemewe; hali aitendae kweli huja kwenye nuru, matendo yake yaonekane ya kuwa yametendwa katika Mungu. Baada ya haya Yesu na wanafunzi wake walikwenda hatta inchi ya Kiyahudi; akashinda huko pamoja nao, akibatiza. Yohana nae alikuwa akibatiza huko Ainon, karibu na Salim, kwa sababu palikuwa na maji tele; watu wakamwendea wakabatizwa. Maana Yohana alikuwa hajatiwa gerezani. Bassi palitokea mashindano ya wanafunzi wa Yohana na Wayahudi katika khabari ya utakaso. Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabbi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ngʼambu ya Yardani, uliyemshuhudia wewe, huyu nae anabatiza, na watu wote wanamwendea. Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni. Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. Aliye nae bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi anaesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi: bassi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana buddi kuzidi, bali mimi kupungua. Ajae kutoka juu huyu yu juu ya yote: aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, na anena mambo ya dunia: yeye ajae kutoka mbinguni yu juu ya yote. Aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoshuhudia, wala hapana anaeukubali ushuhuda wake. Aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri yake kwamba Mungu ni kweli. Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima. Baba ampenda Mwana, amempa vyote mikononi mwake. Amwaminiye Mwana ana uzima wa milele; na asiyemtii Mwana hataona uzima, hali ghadhabu ya Mungu inamkalia. BASSI Bwana alipojua ya kuwa Mafarisayo wamesikia kwamba Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kubatiza, (lakini Yesu mwenyewe hakuhatiza, hali wanafunzi wake), akaacha Yahudi akaenda zake Galilaya marra ya pili. Na alikuwa hana buddi kupita katikati ya Samaria. Bassi akafika mji wa Samaria, uitwao Sukar, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusuf mwanawe. Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Bassi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Ilikuwa yapata saa sita. Akaja mwanamke wa Kisamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe. Maana wanafunzi wake wamekwenda mjini wanunue chakula. Bassi yule mwanamke wa Kisamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke wa Kisamaria? kwa maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria. Yesu akajibu akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, nae ni nani akuambiae, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, nae angalikupa maji yaliyo hayi. Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea na kisima kinakwenda chini sana; bassi, umeyapata wapi haya maji yaliyo hayi? Je! wewe u mkubwa kuliko baba yetu Yakobo aliyetupa kisima hiki, nae mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na nyama zake? Yesu akajibu, akamwambia, Killa anywae maji haya ataona kiu tena: walakini ye yote atakaekunywa maji yale nitakayompa mimi, hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika hatta uzima wa milele. Yule mwanamke akamwambia, Bwana, nipe maji hayo, nisione kiu wala nisije huku kuteka. Yesu akamwambia, Enenda, kamwite mume wako uje nae hapa. Yule mwanamke akajibu akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume, kwa maana umekuwa na waume watano, na yeye uliye nae sasa siye mume wako; hapo umesema kweli. Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii. Baba zetu waliabudu katika mlima huu, na ninyi husema kwamba Yerusalemi ni mahali patupasapo kuabudia. Yesu akamwambia, Ee mwanamke, uniamini, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala katika Yerusalemi. Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho: kwa kuwa wokofu watoka kwa Wayahudi. Lakini saa inakuja, na sasa ipo, ambayo wenye ibada khalisi watamwabudu Baba katika roho na kweli: kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni roho, nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi (aitwae Kristo). Atakapokuja yeye, atatufunulia yote. Yesu akamwambia, Mimi nisemae nawe, ndiye. Marra hiyo wakaja wanafunzi wake wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke; lakini hapana aliyesema, Unatafuta nini? au, Kwa nini unasema nae? Bassi yule mwanamke akauacha mtungi wake, akaenda zake mjini, akawaambia watu, Njoni, nitazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! haimkini huyu kuwa ndiye Kristo? Bassi wakatoka mjini wakamwendea. Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabbi, ule. Akawaambia, Mimi nina chakula msichokijua ninyi. Bassi wanafunzi wake wakasemezana, Je! mtu amemletea chakula? Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka nikaimalize kazi yake. Hamsemi ninyi, Imebaki miezi mine bado, ndipo yaja mavuno? Nami nawaambieni, Inueni macho yenu, mkayatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe tayari kwa mavuno. Avunae hupokea mshahara na kukusanya matunda kwa uzima wa milele, illi yeye apandae na yeye avunae wafurahi pamoja. Maana neno lile, Mmoja hupanda, mwingine akavuna, huwa kweli. Mimi naliwatuma myavune msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao. Na katika mji ule Wasamaria wengi wakaamini kwa sababu ya maneno ya yule mwananike, aliposhuhudu, kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda. Bassi wale Wasamaria walipomwendea walimsihi akae kwao; akakaa huko siku mbili. Watu wengi zaidi wakamwamini kwa sababu ya neno lake. Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako; maana tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika yake huyu ni Mwokozi wa ulimwengu. Baada ya siku hizo mbili akaondoka huko, akaenda Galilaya. Kwa maana Yesu mwenyewe alishuhudu ya kwamba nabii hana heshima katika inchi yake mwenyewe. Bassi alipofika Galilaya Wagalilaya wakampokea, kwa kuwa wameona mambo yote aliyoyatenda Yerusalemi wakati wa siku kuu; maana hao nao waliendea siku kuu. Bassi akafika tena Kana ya Galilaya, hapo alipofanya maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja, ana mwana hawezi Kapernaum. Huyu aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Yahudi hatta Galilaya, akamwendea, akamsihi ashuke akamponye mwana wake; kwa maana alikuwa kufani. Bassi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa. Yule diwani akamwambia, Bwana, shuka kabla hajafa mtoto wangu. Yesu akamwambia, Shika njia yako: mwana wako yu hayi. Mtu yule akaliamini lile neno aliloambiwa na Yesu, akashika njia. Hatta alipokuwa akishuka, watumishi wake wakamlaki, wakampasha khabari, wakisema ya kama, Mtoto wako yu hayi. Bassi akawauliza khabari ya saa alipoanza kuwa hajambo. Bassi wakamwamhia, Jana, saa saba, homa ilimwacha. Bassi baba yake akafahamu ya kuwa ni saa ileile aliyoambiwa na Yesu, Mwana wako yu hayi. Akaamini yeye na nyumba yake yote. Na hii ni isharaya pili aliyoifanya Yesu, alipotoka Yahudi kwenda Galilaya. BAADA ya haya palikuwa na siku kuu ya Wayahudi; Yesu akapanda kwenda Yerusalemi. Na huko Yerusalemi penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiehrania Bethesda, nayo ina matao matano. Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, na waliopooza, wakingoja maji yachemke. Kwa maana kuna wakati malaika hushuka akaiingia ile birika, akayatibua maji: bassi yeye aliyeingia kwanza baada ya maji kutibuliwa, akaponea ugonjwa wote uliokuwa umempata. Na huko palikuwa na mtu, amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane. Yesu alipomwona huyu amelala, akijua ya kuwa amekuwa hali hii siku nyingi, akamwambia, Wataka kuwa nizima? Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; bali wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. Yesu akamwambia, Simama, jitwike kitanda chako, ukaende. Marra yule mtu akawa mzima, akajitwika kitanda chake, akaenda. Bassi ilikuwa sabato siku ile. Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, si halali kwako kujitwika kitanda chako. Akawajibu, Yeye aliyenifanya kuwa mzima, ndiye aliyeniambia, Jitwike kitanda chako, ukaende. Bassi wakamwuliza, Yule mtu aliyekuambia, Jitwike kitanda chako ukaende, ni nani? Lakini yule aliyeponywa, hakujua ni nani; maana Yesu amejitenga, kwa sababu palikuwa na watu wengi mahali pale. Baada ya haya Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima: usitencle dhambi tena, jambo lililo baya zaidi lisije likakupata. Yule mtu akaenda zake, akawapasha Wayahudi khabari ya kwamba Yesu ndiye aliyemfanya kuwa mzima. Kwa sababu hiyo Wayahudi wakaanza kumwudhi Yesu, wakitaka kumwua, kwa kuwa alitenda haya siku ya sabato. Yesu akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hatta sasa, nami ninatenda kazi. Bassi kwa sababu hii Wayahudi wakazidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na haya alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Bassi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Mwana hawezi kutenda neno kwa nafsi yake, illa lile amwonalo Baba analitenda; kwa maana yote atendayo yeye, hayo na Mwana ayatenda vilevile. Maana Baba ampenda Mwana, amwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; na kazi kubwa zaidi kuliko hizi atamwonyesha illi ninyi mpate kustaajabu. Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha awatakao. Maana Baba hamhukumu mtu aliye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; illi wote wamheshimu Mwana kama wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyempeleka. Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima. Amin, amin, nawaambieni, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hayi. Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake; akampa mamlaka ya kufanya hukumu kwa sababu yu Mwana wa Adamu. Msistaajabie haya: kwa maana saa inakuja, ambayo watu wote waliomo makaburini watakapoisikia sauti yake, nao watatoka: wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliofanya manyonge kwa ufufuo wa hukumu. Mimi siwezi kufanya neno kwa nafsi yangu: kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo, na hukumu yangu ina haki: kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mwenyewe, bali mapenzi yake Baba aliyenipeleka. Mimi nikijishuhudia nafsi yangu, ushuhuda wangu si kweli. Yuko mwingine anaenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli. Ninyi mlituma watu kwa Yohana, akaishuhudia kweli. Lakini mimi sipokei ushuhuda kwa wana Adamu; walakini ninasema haya illi ninyi mpate kuokoka. Yeye alikuwa taa iwakayo na kuangaza, na ninyi mlipenda kuishangilia nuru yake kitambo. Lakini ushuhuda nilio nao ni mkubwa kuliko ule wa Yohana: kwa kuwa zile kazi nilizopewa na Baba nizimalize, kazi hizo zenyeye ninazozitenda zinanishuhudia kwamba Baba amenituma. Nae Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona. Na neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hamwamini yeye alivetumwa nae. Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yanayonishuhudia: wala hamtaki kuja kwangu, mpate kuwa na uzima. Sipokei utukufu kwa wana Adamu. Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu. Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei: mwingine akija kwa jina lake mwenyewe mtampokea huyo. Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokezanya utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti? Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba: yuko anaewashitaki, yaani Musa, mnaemtumaini ninyi. Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; maana yeye aliandika khahari zangu. Illakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaaminije maneno yangu? BAADA ya haya Yesu alikwenda zake ngʼambu ya bahari ya Galilaya, bahari ya Tiberia. Makutano mengi wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa. Yesu akapanda mlimani, akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. Na Pasaka, siku kuu ya Wayahudi, ilikuwa karibu. Bassi Yesu alipoinua macho yake akaona makutano mengi yanakuja kwake, akamwambia Filipo, Tununue wapi mikate, hawa wapate kula? Alinena haya illi amjaribu: kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda. Filipo akamjibu, Mikate ya dinari miateen haiwatoshi, killa mmoja apate kidogo tu. Mmoja wa wanafunzi wake, Andrea, ndugu wa Simon Petro, akamwambia, Yupo mtoto hapa, ana mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini haya nini kwa watu wengi kama hivi? Yesu akasema, Waketisheni watu. Palikuwako majani tele mahali pale. Bassi watu waume wakaketi, jumla yao wapata elfu tano. Bassi Yesu akaitwaa mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka. Waliposhiba, akawaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki, kitu kisipotee. Bassi wakavikusanya, wakajaza vikapu thenashara kwa vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyowabakia waliokula. Bassi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya Yesu, wakasema, Huyu hakika ni nabii yule ajae ulimwenguni. Bassi Yesu, akitambua ya kuwa walitaka kuja kumchukua illi wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani, yeye peke yake. Hatta ilipokuwa jioni, wanafunzi wake wakatelemka baharini: wakapanda chomboni wakaanza kuivuka bahari kwenda Kapernaum. Na giza imekwisha kuwa, nae Yesu hajawafikia. Bahari ikaanza kuchafuka, upepo mwingi ukivuma. Bassi wakavuta makasia kadiri ya stadio ishirini na tano au thelathini, wakamwona Yesu anakwenda juu ya bahari, anakikaribia chombo: wakaogopa. Nae akawaambia. Ni mimi, msiogope. Bassi wakataka kumpokea chomboni; na marra hiyo chombo kikaifikilia inchi waliyokuwa wakienda. Siku ya pili yake makutano waliosimama ngʼambu ya bahari wakaona ya kuwa hakuna mashua nyingine huko illa ile moja waliyoingia wanafunzi wake; tena ya kuwa Yesu hakuingia katika mashua ile pamoja na wanafunzi wake, bali wanafunzi wake walikwenda peke yao, (lakini mashua nyingine zilikuja kutoka Tiberia karibu na pahali pale walipokula mikate, wakati Bwana aiiposhukuru); bassi makutano walipoona ya kuwa Yesu hakuwako huko wala wanafunzi wake, wenyewe wakaingla vyomboni, wakaenda Kapernaum wakimtafuta Yesu. Hatta walipomwona ngʼambu ya bahari, wakamwambia, Rabbi, umekuja lini hapa? Yesu akawajibu, akasema, Amin, amin, nawaambieni, Mnanitafuta, si kwa sababu mliona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate, mkashiba. Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hatta uzima wa milele, Mwana wa Adamu atakachowapeni: maana huyu ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu. Bassi wakamwambia, Tufanyeje tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ni kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa nae. Wakamwambia, Unafanya ishara gani bassi illi tuone tukaamini? Unatenda kazi gani? Baba zetu waliila manna jangwani, kama ilivyoandikwa, Aliwapa mkate kutoka mbinguni wale. Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa mkate ule kutoka mbinguni, bali Baba yangu anawapa mkate ule utokao mbinguni ulio wa kweli. Kwa maana mkate wa Mungu ni ule ushukao kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima. Bassi, wakamwambia, Bwana, siku zote utupe mkate huo. Yesu akawaambia, Mimi ni mkate wa uzima; yeye ajae kwangu hataona njaa kabisa, nae aniaminiye hataona kiu kamwe. Lakini naliwaambieni ya kwamba mmeniona bila kuniamini. Yote anipayo Bwana itakuja kwangu; nae ajae kwangu sitamtupa nje kamwe. Kwa kuwa sikushuka kutoka mbinguni illi niyafanye mapenzi yangu, hali mapenzi yake aliyenipeleka. Na mapenzi yake Baba aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika vyote alivyonipa nisipoteze kitu hatta kimoja, hali nikifufue siku ya mwisho. Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya ya kwamba killa amtazamae Mwana na kumwamini awe ua uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho. Bassi Wayahudi wakamnungʼunikia, kwa sababu alisema, Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni. Wakanena, Huyu siye Yesu, mwana wa Yusuf, ambae twamjua baba yake na mama yake? Bassi, anenaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni? Bassi Yesu akajibu, akawaambia, Msinungʼunike ninyi kwa ninyi. Hakuna mtu awezae kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka: nami nitamfufua siku ya mwisho. Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Bassi killa aliyesikia na kujifunza kwa Baba, huja kwangu. Si kwamba mtu amemwona Baba, illa yeye atokae kwa Mungu huyu ndiye aliyemwona Baba. Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi ana uzima wa milele. Mimi ni mkate wa uzima. Baba zetu waliila manna jangwani wakafa. Huu ni mkate ushukao kutoka mbinguni, illi mtu aule wala asife. Mimi ni mkate wa uzima ulioshuka kutoka mbinguni; mtu akila mkate huu, ataishi milele: na mkate nitakaotoa mimi ni nyama yangu nitakayotoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. Bassi Wayahudi wakashindana wao kwa wao, wakinena; Awezaje mtu huyu kutupa sisi nyama yake tuile? Bassi Yesu akawaambia, Amin, amin, nsiwaambieni. Msipoila nyama yake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani jemi. Ailae nyama yangu na kuinywa damu yangu ana uzima wa milele; mimi nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maima nyama yangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli, Ailae nyama yangu na kuinywa damu yangu, hukaa ndani yangu, na mimi ndani yake. Kama vile Baba aishiye alivyonituma mimi, nami naishi kwa ajili ya Baba, kadhalika yeye nae anilae ataishi kwa ajili yangu. Huu ni mkale ulioshuka kutoka mbinguni; si kama baba zenu walivyoila manna wakafa; aulae mkate huu ataishi milele. Maneno haya aliyasema sunagogini, alipokuwa akifundisha huko Kapenaum. Bassi watu wengi katika wanafunzi wake waliposikia haya, wakasema, Neno hili ni gumu, nani awezae kulisikia? Yesu akajua nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanaliumigʼunikia neno hili, akawaambia, Neno hili linawachukiza? Itakuwaje, bassi, mmwonapo Mwana wa Adamu akijianda huko alikokuwa kwanza? Roho ndiyo itiayo uzima; mwili haufai kitu; maneno ninayowaambieni ni roho, tena ni uzima. Lakini kuna wengine miongoni mwemi wasioamini. Maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini na ni nani atakaenisaliti. Akanena, Kwa sababu hii nimewaambia ya kwamba hapana mtu awezae kuja kwangu, isipokuwa amejaliwa na Baba yangu. Kwa ajili ya haya wengi katika wanafunzi wake wakarejea nyuma, wala hawakuandamana nae tena. Bassi Yesu akawaambia wathenashara, Ninyi nanyi mnataka kuondoka? Bassi Simon Petro akamjibu, Bwana! twende kwa nani? Wewe una maneno ya uzima wa milele. Nasi tumeamini, tena tumejua ya kuwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi. Yesu akawajibu, Je! sikuwachagua ninyi thenashara, na mmoja wenu ni Shetani? Alimnena Yuda, mwana wa Simon Iskariote: maana huyu ndiye atakaemsaliti: nae ni mmoja wa wathenashara. NA baada ya haya Yesu akawa akitembea katika Galilaya: maana hakutaka kutembea katika Yahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua. Na siku kuu ya Wayahudi, siku kuu ya vibanda, ilikuwa karibu. Bassi ndugu lake wakamwambia, Ondoka bapa uende Yahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. Kwa maana hakuna mtu afanyae neno kwa siri, na yeye mwenyewe anataka kujulikana. Ukifanya haya, jidhihirishe kwa ulimwengu. Maana hatta ndugu zake hawakumwamini. Bassi Yesu akawaambia, Haujafika wakati wangu; wakati wenu sikuzote u tayari. Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi: bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. Pandeni ninyi kwenda kushika siku kuu hii; mimi sipandi bado kwenda kushika siku kuu hii: kwa kuwa wakati wangu haujatimia bado. Alipokwisha kuwaambia haya, akakaa katika Galilaya. Hatta ndugu zake walipokwisha kupanda, ndipo yeye nae akapanda kwenda kuishika siku kuu, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri. Bassi Wayahudi wakamtafuta katika siku kuu wakanena, Yuko wapi huyo? Kukawa manungʼuniko mengi katika makutano kwa khabari zake; wengine wakisema, Yu mtu mwema; na wengine wakisema, Sivyo, bali anawadanganya makutano. Illakini hapana mtu aliyemtaja kwa wazi kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi. Hatta ilipokuwa katikati ya siku kuu Yesu akapanda, akaingia hekalui akafundisha. Wayahudi wakastaajabu, wakinena, Amepataje huyo kujua elimu, nae hajasoma? Bassi Yesu akawajibu akasema, Elimu yangu siyo yangu, illa yake yeye aliyenipeleka. Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua khabari ya elimu hii kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. Yeye anenae kwa nafsi yake tu, hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anaetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyu ni wa kweli wala ndani yake hamna udhalimu. Aliyewapeni torati si Musa? wala hapana mmoja wenu aitendae torati. Mbona mnatafuta kuniua? Makutano wakajibu, wakasema, Una pepo; ni nani anaetafuta kukuua? Yesu akajibu, akawaambia, Nalitenda kazi moja, nanyi nyote mnastaajabu. Kwa sababu hii Musa aliwapa tohara, si kwamba yatoka kwa Musa bali kwa babu zenu: nanyi siku ya sabato humtahiri mtu. Bassi ikiwa mtu apashwa tohara siku ya sabato, torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato? Msihukumu hukumu ya macho, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki. Bassi baadhi ya watu wa Yerusalemi wakanena, Huyu si yeye wanaemtafuta illi kumwua? Na kumbe! ananena waziwazi wala hawamwambii neno? Yumkini wakuhwa wanajua kwa hakika ya kuwa huyu ni Kristo! Lakini huyu twamjua atokako, bali Masihi atakapokuja, hakuna ajuae atokako. Bassi Yesu akapaaza sauti yake hekaluni, akifundisha, akisema, Mimi mnanijua, na nitokako mnakujua; wala sikuja kwa naisi yangu, illa yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. Lakini mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, nae ndiye aliyenituma. Bassi wakatafuta kumkamata: lakini hapana aliyenyosha mkono wake illi kumshika kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado. Watu wengi katika makutano wakamwamini: wakasema, Atakapokuja Kristo, je! atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu? Mafarisayo wakawasikia makutano wakinungʼunika hivi kwa khabari zake: bassi Mafarisayo na makuhani wakuu wakatuma watumishi illi wamkamate. Bassi Yesu akanena, Bado muda kitambo nipo pamoja nanyi, kiisha nakwenda zangu kwake yeye aliyenipeleka. Mtanitafuta, wala hamtaniona; nami nilipo, ninyi hamwezi kuja. Bassi Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, Huyu atakwenda wapi hatta sisi tusimwone? Atakwenda kwa Utawauyiko wa Wayunani na kuwafundisha Wayunani? Neno gani hilo alilolisema, Mtanitafuta wala hamtaniona; na nilipo mimi, ninyi hamwezi kuja? Hatta siku ya mwisho, siku ile kubwa ya siku kuu, Yesu akasimama, akapaaza sauti yake, akinena, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyonena, mito ya maji ya uzima itamtoka tumhoni. Neno hili alilisema katika khabari ya Roho, ambae wale wamwaminio watampokea khalafu: kwa maana Roho Mtakatifu alikuwa bado kuwapo, kwa sababu Yesu alikuwa bado kutukuzwa. Bassi watu wengi katika makutano waliposikia neno lile, walinena, Huyu hakika yake ndiye nabii yule. Wengine walinena, Je! Kristo atoka Galilaya? Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daud, na kutoka Bethlehemu, kijiji kile alichokaa Daud? Bassi yakaingia matangukano kwa ajili yake. Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hapana mtu aliyenyosha mkono wake illi kumshika. Bassi wale watumishi wakawaendea makuhani wakuu na Mafarisayo, nao wakawaambia, Mbona hamkumleta? Wale watumishi wakajibu, Hajanena kamwe mwana Adamu aliye yote kama huyu anavyonena. Bassi Mafarisayo wakawajibu, Je! ninyi nanyi mmedanganyika? Ni nani katika wakubwa amwammiye, au katika Mafarisayo? Lakini makutano hayo wasioifahamu torati wamelaaniwa. Akawaambia Nikodemo (ni yule aliyemwendea usiku, maana ni mmojawapo wao), Je! sharia yetu humhukumti mtu kabla ya kumsikia kwanza na kujua atendavyo? Wakajibu, wakamwambia, Wewe nawe umetoka Galilaya? Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii. Wakaenda killa mtu nyumbani kwake: lakini Yesu akaenda mlima wa mizeituni. Hatta assubuhi ilipokucha akaingia tena hekaluni, watu wote wakamwendea: nae akaketi akawa akiwafundisha. Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati, wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. Bassi katika torati Musa alituamuru kuwapiga mawe watu kama hao; bassi wewe wasema nini? Wakasema neno hili wakimjaribu wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika inchi. Nao wakazidi kumhoji, akajiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika inchi. Nao, waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianza tangu wazee hatta wa mwisho; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke akisimama katikati. Yesu akajiinua asimwone mtu illa yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Hapana aliyekuhukumu? Akamwambia, Hapana Bwana. Yesu akamwambia, Nami sikuhukumu. Enenda, wala usitende dhambi tena. Bassi Yesu akanena nao tena, akisema. Mimi ni nuru ya ulimwengu; anifuatae hatakwenda katika giza kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. Bassi Mafarisayo wakamwambia, Wewe unajishuhudia nafsi yako; ushuhuda wako si kweli. Yesu akajibu akawaambia, Ningawa mimi ninajishuhudia nafsi yangu, ushuhuda wangu ni kweli, kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka, wala niendako. Ninyi mwahukumu kwa jinsi ya kiwiliwili; mimi simhukumu mtu. Na nijapohukumu, hukumu yangu ni kweli, kwa kuwa mimi si peke yangu bali mimi na Baba aliyenipeleka. Na tena katika sharia yenu imeandikwa, Ushuhuda wa watu wawili ni kweli. Mimi ndimi ninaejishuhudia nafsi yangu, nae Baba aliyenipeleka ananishuhudia. Bassi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngaliuijua mimi, mngalimjua na Baba yangu. Maneno haya aliyasema Yesu akifundisha kakika hekalu, katika chumba cha hazina; wala hapana mtu aliyemkamata, kwa kuwa saa yake ilikuwa haijaja bado. Bassi Yesu akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta, na mtakufa katika dhambi yenu: niendako mimi, ninyi hamwezi kuja. Bassi Wayahudi wakanena, Je! atajiua, kwa kuwa anena, Niendako mimi hamwezi kuja? Akawaambia, Ninyi wa chini, mimi wa juu; ninyi wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu. Bassi naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa kuwa msipoamini ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu. Bassi wakamwambia, U nani wewe? Yesu akawaambia, Neno lilo hilo nisemalo nanyi tangu mwanzo. Nina maneno mengi ya kusema na kuhukumu katika khabari zenu; lakini yeye aliyenipeleka ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu. Hawakufahamu ya kuwa awatajia Baba. Bassi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye, na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu tu, illa kama Baba yangu alivyonifundisha, ndivyo nisemavyo. Nae aliyenipeleka yu pamoja nami; Baba hakuniacha peke yangu: kwa sababu mimi nafanya siku zote yampendezayo. Alipokuwa akisema haya, wengi walimwamini. Bassi Yesu akawaamhia Wayahudi wale waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mu wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru. Wakamjihu, Tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wanenaje, Mtawekwa huru? Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambieni, Killa atendae dhambi, ni mtumwa wa dhambi. Na mtumwa hakai ndani ya nyumba siku zote; mwana hukaa siku zote. Bassi Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli. Najua ya kuwa m mzao wa Ibrahimu; lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halina nafasi ndani yenu. Niliyoyaona kwa Baba yangu udiyo niyanenayo: nanyi vivyo hivyo mliyoyaona kwa baba yenu, ndiyo myatendayo. Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ni Ibrahimu. Yesu akawaambia, Kama mugekuwa watoto wa Ibrahimu, mngetenda kazi zake Ibrahimu. Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu niliyewaambia kweli ile niliyoisikia kwa Baba yangu. Ibrahimu hakufanya hivi. Ninyi nmazitenda kazi za baba yenu. Wakamwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zina; tuna baba mmoja, yaani Mungu. Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, na nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma. Mbona hamyafahamu maneno yangu haya niyasemayo? Ni kwa sababu hamwezi kulisikia neno langu. Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo. Nami, kwa sababu naisema kweli, hamniamini. Nani wenu anishuhudiae kuwa nina dhambi? Nikisema kweli, mbona ninyi hamniamini? Aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; kwa hiyo ninyi hamsikii, kwa sababu ninyi si wa Mungu. Wayahudi wakajibu wakamwambia, Hatuneni vema sisi kwamba wewe u Msamaria, na una pepo? Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini namheshimu Baba yangu, nanyi hamniheshimu. Nami siutafuti ntukufu wangu; yuko atafutae na kuhukumu. Amin, amin, nawaambieni, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti kabisa hatta milele. Bassi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumefahamu ya kuwa una pepo; Ibrahimu amekufa na manabii, na wewe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti kabisa hatta milele. Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, nae amekufa? Na manabii wamekufa; wajifanya kuwa nani? Yesu akajibu, Nikijitukuza nafsi yangu, utukufu wangu si kitu; anitukuzae ni Baba yangu; mmnenae ninyi kuwa ni Mungu wenu. Nanyi hamkumjua; lakini mimi namjua, na nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua na neno lake nalishika. Ibrahimu baba yemi alishangilia apate kuiona siku yangu; akaona, akafurahi. Bassi Wayahudi wakamwambia. Hujapata bado miaka khamsini, na Ibrahimu umemwona? Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Kabla Ibrahimu hajakuwapo, Mimi nipo. Bassi wakatwaa mawe wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni. HATTA alipokuwa akipita akamwona nitu, kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamwuliza, wakinena, Rabbi, ni nani aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hatta akazaliwa kipofu? Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe kwake. Yanipasa kuzifanya kazi zake aliyenipeleka maadam ni mchana: usiku waja, asipoweza mtu kufanya kazi. Maadam nipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu. Alipokwisha kusema haya, akatema mate chini, akafanya tope kwa yale mate, akampaka kipofu macho kwa lile tope, akamwambia, Enenda, kanawe katika birika ya Siloam (tafsiri yake, Aliyetumwa). Bassi akaenda, akanawa, akarudi, anaona. Bassi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni kipofu, wakanena, Je! huyu siye yule aliyekuwa akiomba, ameketi? Wengine wakimena, Amefanana nae. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye. Bassi wakamwambia, Macho yako yalifumhuliwaje? Yeye akajibu, akanena, Mtu aitwae Yesu alifanya tope, akanipaka macho yangu, akaniambia, Enenda hatta birika ya Siloam, ukanawe; bassi nikaenda nikanawa, nikapata kuona. Wakamwambia, Yuko wapi mtu huyo? Akanena, Sijui. Wakampeleka yule aliyekuwa kipofu zamani kwa Mafarisayo. Na ilikuwa sabato hapo Yesu alipofanya tope na kumfumbua macho. Bassi Mafarisayo nao wakamwuliza tena jinsi alivyopata kuona. Akawaambia, Alitia tope juu ya macho yangu nikanawa, na sasa naona. Bassi baadhi ya Mafarisayo wakanena, Mtu huyu hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakanena, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo? Kukawa matangukano kati yao. Bassi wakamwambia yule kipofu marra ya pili, Wewe unasema nini katika khabari zake kwa kuwa alikufumbua macho? Akasema, Yu nabii. Bassi Wayahudi hawakusadiki khabari zake ya kuwa alikuwa kipofu akapata kuona, hatta wakawaita wazazi wake yule aliyepata kuona; wakawauliza, wakinena, Huyu ndiye mwana wenu msemae kwamba alizaliwa kipofu? Amepataje, bassi, kuona sasa? Wazazi wake wakawajibu, wakasema, Tunajua ya kuwa huyu ni mwana wetu, na ya kuwa alizaliwa kipofu; lakiui jinsi aonavyo sasa, hatujui, na ni nani aliyemfumbua macho, hatujui; yeye ni mtu mzima; mwulizeni yeye mwenyewe, atajisemea. Wazazi wake waliyasema haya kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi wamekwisha kuwafikana kwamba mtu akimwungama kuwa Kristo, ataharamishwa sunagogi. Ndio sababu wazazi wake walisema, Yeye ni mtu mzima, mwulizeni. Bassi marra ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyu ni mwenye dhambi. Bassi yule mtu akajibu akasema, Kwamba yeye m mwenye dhambi, sijui. Najua neno moja, mimi nalikuwa kipofu, na sasa naona. Wakamwambia tena, Alikutenda nini? Alikufumbuaje macho? Akawajibu, Nimekwisha kuwaambieni, wala hamkusikia: Mbona mnataka kusikia marra ya pili? Ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake? Bassi wakamshutumu, wakasema, Wewe u mwanafunzi wake mtu yule; sisi tu wanafunzi wa Musa. Sisi twajua ya kuwa Mungu alisema na Musa, bali huyo hatujui atokako. Yule mtu akajibu akawaambia, Neno hili ni la ajabu, kwamba ninyi hamjui atokako, nae alinifumbua macho. Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi: bali mtu akiwa mcha Mungu, na kufanya mapenzi yake, huyo amsikia. Tangu awali haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya kipofu aliyezaliwa hali hii. Kama huyu asingalitoka kwa Mungu, asingeweza kutenda neno. Wakajibu, wakamwambia, Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufuudisha sisi? Wakamtoa nje. Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; akamwona, akasema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu? Nae akajibu, akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? Yesu akamwambia, Umemwona, na yeye anaesema nawe ndiye. Akasema, Naamini, Bwana; akamsujudia. Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, illi wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu. Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja nae wakasikia haya, wakamwambia, Je! sisi nasi tu vipofu? Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema Twaona; bassi dhambi yenu inakaa. AMIN, amin, nawaambieni, asiyeingia kwa mlango katika zizi la kondoo, lakini apanda penginepo, huyu ni mwizi na mnyangʼanyi. Aingiae kwa mlango ni mchunga wa kondoo. Bawabu humfungulia huyu, na kondoo humsikia sauti yake, nae huwaita kondoo zake kwa majina yao, huwapeleka nje. Awatoapo nje kondoo zilizo zake, huwatangulia; na kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. Mgeni hawatamfuata kabisa, hali watamkimbia, kwa maana hawaijui sauti ya wageni. Methali hii Yesu aliwaambia; lakini wao hawakuelewa na mambo hayo aliyowaambia. Bassi Yesu aliwaamhia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi niliye mlango wa kondoo; wote walionitangulia ni wezi na wanyangʼanyi: lakini kondoo hawakuwasikia. Mimi ndimi niliye mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka, ataingia, atatoka, na atapata malisho. Mwizi haji illa aibe, achinje, aharibu; mimi nalikuja wawe na uzima, na wawe nao tele. Mimi ndimi niliye mchunga aliye mwema: mchunga aliye mwema huweka maisha yake kwa ajili ya kondoo. Mtu wa mshahara, na asiye mchunga, ambae kondoo si mali yake, humwona mbwa wa mwitu anakuja, huziacha kondoo, hukimbia; na mbwa wa mwitu huziteka, huzitawanya. Mtu wa mshahara hukimhia kwa kuwa ni mtu wa mshahara, wala hatii moyoni mambo ya kondoo. Mimi ndimi niliye mchunga aliye mwema; na walio wangu nawajua, na walio wangu wananijua, kama vile Baba anijuavyo, na mimi nimjuavyo Baba: na uzima wangu nauweka kwa ajili ya kondoo. Na kondoo wengine ninao, wasio wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta, na sauti yangu wataisikia; na kutakuwapo kundi moja na mchunga mmoja. Ndio maana Baba anipenda, kwa sababu nauweka uzima wangu illi niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleae, bali mimi nauweka mwenyewe. Nina uweza wa kuuweka, tena nina uweza wa kuutwaa tena. Agizo hili nalilipokea kwa Baba yangu. Yakaingia tena matangukano katika Wayahudi, kwa ajili ya maneno haya. Wengi wao wakasema, Ana pepo, tena ana wazimu; mbona mnamsikiliza? Wengine wakasema, Maneno haya siyo ya mtu mwenye pepo. Je! pepo aweza kuwafumbua macho vipofu? Bassi ilikuwa siku kuu ya kutabaruku huko Yerusalemi; ni wakati wa baridi. Na Yesu alikuwa akitembea ndani ya hekalu, katika ukumbi wa Sulemani. Bassi Wayahudi wakamzunguka, wakamwambia, Hatta lini utatuangaisha roho zetu? Kama wewe u Kristo, tuambie wazi wazi. Yesu akawajibu, Naliwaambieni, nanyi hamwamini; kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu, ndizo zinazonishuhudia. Lakini ninyi hamwamini kwa sababu hammo katika kondoo zangu, kama nilivyowaambieni. Kondoo zangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata; nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakaewapokonya katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa ni mkuu kuliko wote; wala hakuna awezae kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Mimi na Baba yangu tu nmoja. Bassi Wayahudi wakaokota mawe tena, illi wampige. Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha zitokazo kwa Baba yangu: katika kazi hizo ni ipi mnayonipigia mawe? Wayahudi wakamjibu wakinena, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi mawe, bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe, uliye mwana Adamu, wajifanya nafsi yako u Mungu. Yesu akawajibu, Haikuandikwa katika torati yenu, ya kama, Mimi nilisema, Ninyi m miungu? Ikiwa aliwaita wale miungu waliojiliwa na neno la Mungu (na maandiko hayawezi kutanguka), je! yeye ambae Baba alimtakasa akamtuma ulimwenguni, ninyi mwamwambia, Unakufuru, kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu? Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini; lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi, mpate kujua na kuamini ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba. Wakatafuta marra ya pili kumkamata: akatoka mikononi mwao. Akaenda zake tena ngʼambu ya Yardani, hatta pahali ptile alipokuwa Yohana akihatiza hapo kwanza; akakaa huko. Watu wengi wakamwendea, wakanena, Yohana hakufanya ishara yo yote, lakini yote aliyosema Yohana katika khabari zake huyu yalikuwa kweli. Wengi wakamwamini huko. BASSI mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mtu wa mji wa Mariamu na Martha dada yake. Ni Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu yake kwa nywele zake, ambae ndugu yake Lazaro alikuwa hawezi. Bassi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake, wakisema, Bwana, yeye umpendae hawezi. Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali kwa ajili ya utukufu wake Mungu, illi Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo. Nae Yesu alimpenda Martha na dada yake ua Lazaro. Bassi aliposikia kwamba hawezi alikaa bado siku mbili mahali pale alipokuwapo. Kiisha baada ya haya akawaambia wanafunzi wake, Twende Yahudi tena. Wale wanafunzi wakamwambia, Rabbi, juzi juzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga mawe, nawe unakweuda huko tena? Yesu akajibu, Saa za mchana je si thenashara? Mtu akienda mchana hajikwai, kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu. Bali akienda usiku, hujikwaa, kwa sababu nuru haimo ndani yake. Aliyasema haya: kiisha baada ya liaya akawaambia, Lazaro rafiki yetu amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha. Bassi wale wanafunzi wake wakamwambia, Bwana, kama amelala atapona. Lakini Yesu amenena khabari za mauti yake: nao walidhani ya kuwa ananena khabari za kulala usiugizi. Bassi hapo Yesu akawaambia kwa wazi, Lazaro amekufa. Nami nafurahi kwa ajili yenn kwamba sikuwa huko, mpate kuamini: lakini na twende kwake. Bassi Tomaso, aitwae Didumo, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twende na sisi, tufe pamoja nae. Bassi alipofika Yesu, akamkuta amekwisha kuwa kaburini yapata siku nne. Na Bethania ilikuwa karibu ya Yerusalemi, kadiri ya stadio khamstashara; na watu wengi katika Wayahudi wamekuja kwa Martha na Mariamu, illi kuwafariji kwa ajili ya ndugu yao. Bassi Martha, aliposikia kwamba Yesu anakuja, akaenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani. Bassi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu asingalikufa. Lakini hatta sasa najua ya kuwa vyovyote utakavyomwomba Mungu, Mungu atakupa. Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. Yesu akamwambia, Mimi ni ufufuo na uzima; aniaminiye mimi, ijapo afe, atakuwa ataishi, na killa mwenye uzima na kuniamini mimi hatakufa kabisa hatta milele. Je! waamini haya? Akamwambia, Naam, Bwana; mimi nimeamini ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajae ulimwenguni. Na alipokwisha kusema haya, akaenda zake, akamwita dada yake, Mariamu, kwa siri, akisema, Mwalimu yupo, anakuita. Nae aliposikia, akaondoka upesi, akamwendea. Na Yesu alikuwa hajafika ndani ya kijiji, lakini alikuwa pale pale alipomlaki Martha. Bassi wale Wayahudi waliokuwa pamoja nae nyumbani, wakimfariji, walipomwona Mariamu, jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, wakamfuata, wakidhani ya kuwa anakwenda kaburini illi alie huko. Bassi Mariamu, alipofika pale alipokuwapo Yesu, akamwona, akaanguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungaliwapo hapa, ndugu yangu asingalikufa. Bassi, Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana nae wanalia, akaugua rohoni, akajifadhaisha nafsi yake, akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo, utazame. Yesu akatoka machozi. Bassi Wayahudi wakanena, Angalieni jinsi alivyompenda. Bali wengine walisema, Je! huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife? Bassi Yesu akiugua tena nafsini mwake akatika kaburini. Nalo lilikuwa pango, na jiwe limewekwa juu yake. Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule mtu aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa: maana amekuwa mayiti siku nne. Yesu akamwambia, Sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? Bassi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya makutano hawa wanaozunguka nalisema haya, wapate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma. Akiisha kusema haya, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, toka, njoo huku. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa saanda miguuni na mikononi, na uso wake umefungwa kitambaa. Yesu akawaambia, Mfungueni, kamwacheni aende zake. Bassi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu na kuyaona aliyoyafanya Yesu, wakamwamini. Lakini baadhi yao wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu. Bassi makuhani wakuu na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakanena, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi. Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini: na Warumi watakuja, wataondoa mahali petu na taifa letu. Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote, wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu hawa, wala lisiangamie taifa zima. Na hili hakusema kwa nafsi yake, hali kwa kuwa alikuwa kuhani mkuu mwaka ule alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa lile; wala si kwa ajili ya taifa lile tu, lakini pamoja na haya awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika wawe wamoja. Bassi tangu siku ile walifanya shauri wapate kumwua. Bassi Yesu hakutemhea tena kwa wazi kati ya Wayahudi, hali alitoka huko akaenda mahali karibu ya jangwa, hatta mji nitwao Efraim; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake. Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; wengi wakapanda toka inchi yote pia kwenda Yerusalemi kabla ya Pasaka, illi wajitakase. Bassi wakamtafuta Yesu, wakasemezana wao kwa wao, wakisimama katika hekalu, Mwaonaje? Haji kabisa siku kuu hii? Na Makuhani na Mafarisayo wametoa amri ya kwamba, mtu akimjua alipo, alete khabari, wapate kumkamata. BASSI Yesu siku sita kabla ya Pasaka akafika Bethania, hapo alipokuwapo Lazaro, yule aliyekufa akaihfuliwa nae. Bassi wakamfanyizia karamu huko; Martha akakhudumu. Na Lazaro alikuwa mmoja wa wale walioketi chakulani pamoja nae. Bassi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akaifuta miguu yake kwa nywele zake; nyumha ikajaa harufu ya yale marhamu. Bassi Yuda Iskariote, mwana wa Simon, mmoja wa wanafunzi wake, aliye tayari kumsaliti, akanena, Mbona marhamu haya hayakuuzwa kwa dinari mia tatu, na kupewa maskini? Aliyasema haya, si kwa kuwahurumia maskini; hali kwa kuwa ni mwizi, nae ndiye aliyeshika mfuko, akavichikua vilivyotiwa humo. Bassi Yesu alisema, Mwache, ameyaweka haya kwa siku ya maziko yangu. Maana maskini mnao siku zote pamoja nauyi; bali mimi hamnami siku zote. Bassi kundi kubwa la Wayuhudi walijua ya kuwa yeye yuko huko; wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, bali wamwone na Lazaro, ambae alimfufua katika wafu. Makuhani wakuu wakafanya shauri wamwue Lazaro nae; maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walikwenda zao, wakamwamini Yesu. Siku ya pili watu wengi walioijia siku kuu, waliposikia kwamba Yesu anakuja Yerusalemi, wakatwaa matawi ya mitende wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana; Amebarikiwa ajiie kwa jina la Bwana, mfalme wa Israeli. Yesu akapata mwana punda, akampanda, kama ilivyoandikwa, Usiogope, binti Sayuni: angalia, Mfalme wako anakuja, ameketi juu ya mwana wa punda. Mambo haya wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walikumbuka ya kwamba ameandikiwa haya na ya kwamba walimtendea haya. Bassi wakamshuhudia makutano waliokuwa pamoja nae alipomwita Lazaro kutoka kaburini akamfufua. Kwa sababu hiyo makutano wakaenda kumlaki, kwa sababu wamesikia ya kwamba amefanya ishara hii. Bassi Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, Mwaona kwamba hamfai neno: tazameni, ulimwengu umekwenda nyuma yake. Na palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliopanda kwenda kuabudu wakati wa siku kuu. Bassi hao walimwendea Filipo wa Bethsaida wa Galilaya, wakimwuliza, wakisema, Bwana, tunataka kumwona Yesu. Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kiisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu. Yesu akajibu, akinena, Saa imefika, atukuzwe Mwana wa Adamu. Amin, amin, nawaambieni, Punje ya nganu isipoanguka katika inchi ikafa, hukaa katika hali ya peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi. Aipendae roho yake ataiangamiza; nae aichukiae roho yake katika ulimwengu huu ataihifadhi hatta uzima wa milele. Mtu akinitumikia, anifuate: nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo; tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu. Sasa roho yangu imefadhaika; niseme nini? Baba, uniokoe na saa hii. Lakini kwa ajili ya hayo naliifikia saa hii. Baba, ulitukuze jina lako. Bassi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena. Bassi makutano waliosimama karibu wakasikia, wakanena kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema nae. Yesu akajibu, akasema, Sauti hii haikuwa kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu. Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo, sasa mkuu wa ulimwengu him atatupwa nje. Nami nikiinuliwa juu ya inchi nitavuta wote kwangu. Alinena haya, illi kuonyesha ni mauti gani atakayokufa. Bassi makutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hatta milele: nawe wanenaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani? Bassi Yesu akawaambia, Nuru ingali pamoja nanyi muda kitambo. Enendeni maadam mnayo ile nuru, giza lisije likawaweza; nae aendae gizani hajui aendako. Maadam mnayo nuru, iaminini nuru, mpate kuwa wana wa nuru. Hayo aliyasema Yesu, akaenda zake akajificha nao. Lakini ijapokuwa amefanya ishara kubwa namna hii mbele yao, hawakumwamini; illi litimizwe lile neno la nabii Isaya alilolisema, Bwana, nani aliyeziamini khabari zetu? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Kwa sababu hii hawakuweza kuamini, kwa sababu Isaya alisema tena, Amewapofusba macho, amefanya migumu mioyo yao, Wasije wakaona kwa macho yao, wakafahamu kwa mioyo yao, Wakagenka, nikawaponya. Maneno hayo aliyasema Isaya alipouona utukufu wake, akataja khabari zake. Walakini hatta katika wakubwa wengi walimwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumwungama, wasije wakalolewa katika masunagogi. Kwa maana waliupenda utukufu wa wana Adamu kuliko utukufu wa Mungu. Yesu akapaaza sauti yake akasema, Aniaminiye mimi, haniamini mimi, bali yeye aliyenipeleka. Nae anitazamae mimi, amtazama yeye aliyenipeleka. Mimi nimekuja niwe nuru ulimwenguni, illi kilia aniaminiye mimi asikae gizani. Na mtu akisikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja niuhukumu ulimwengu, bali niuokoe ulimwengu. Anikataae mimi, asiyekubali maneno yangu, anae amhukumuye: neno lile nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. Kwa maana mimi sikusema kwa nafsi yangu tu; bali yeye aliyenipeleka, yaani Baba, ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele: bassi haya ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo. HATTA kabla ya siku kuu ya Pasaka, Yesu akijua ya kuwa saa yake imefika atakayotoka katika ulimwengu huu kwenda kwa Baba, akiwa aliwapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapeuda ukomo wa upendo. Hatta wakati wa chakula cha jioni, Shetani alipokwisha kumtia Yuda, mwana wa Simon Iskariote, moyo wa kumsaliti, bassi Yesu akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu, na anakwenda kwa Mungu, akaondoka chakulani, akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifungia. Kiisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu yao, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifungia. Bassi akafika kwa Simon Petro. Huyu akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyayo mimi, wewe huyafahamu sasa; lakini utayajua baadae. Petro akamwambia. Hutanitawadha miguu milele. Yesu akamwambia, Nisipokutawadha, huna fungu pamoja nami. Simon Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hatta mikono yangu na kichwa changu pia. Yesu akamwambia, Aliyekwisha kuoga hana haja illa ya kunawa miguu, hali yu safi mwili wote; na ninyi m safi, lakini si nyote. Maana alimjua atakaemsaliti, ndio maana alisema, Hamwi safi nyote. Bassi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Mmeelewa niliyowatendea. Ninyi mwaniita Mwalimu, na Bwana; na mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. Bassi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa ninyi nanyi kutawadhana miguu. Kwa kuwa nimewapeni mfano illi hayo niliyowatendea ninyi, na ninyi mtende yayo hayo. Amin, amin, nawaambieni, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake: wala mtume si mkuu kuliko yeye aiiyempeleka. Mkiyajua hayo, m kheri mkiyatenda. Sisemi khabari za ninyi nyote: nawajua niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aulae mkate pamoja nami ameinua kisigino chake juu yangu. Tangu sasa nawaambieni kabla hayajatukia, illi yatakapotukia, mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye. Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeae ye yote nimpelekae, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenipeleka. Alipokwisha kusema haya, Yesu akafadhaika rohoni, akashuhudu, akinena, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti. Wanafunzi wakatazamana, wakiona mashaka, ni nani anaemtaja, Palikuwako mmoja wa wanafunzi wake, amemwegamia Yesu kifua chake, ambae Yesu alimpenda. Bassi Simon Petro akampungia mkono huyo, amwulize, Ni nani anaemtaja? Bassi yeye akimwegamia Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani? Bassi Yesu akajibu, Ni mtu yule nitakaemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akampa Yuda, mwana wa Simon Iskariote. Na baada ya lile tonge, Shetani akamwingia. Bassi Yesu akamwambia, Uyatendayo, yatende upesi. Wala hapana mtu katika wale walioketi chakulani aliyeijua sababu hatta akamwambia hivi. Maana wengine, kwa kuwa Yuda aliuchukua mfuko, walidhani ya kuwa Yesu alimwambia, Nunua tunavyovihitaji kwa siku kuu; au kwamba awape maskini kitu. Bassi huyu, akiisha kupokea lile tonge, akatoka marra hiyo; na ulikuwa usiku hapo alipotoka. Bassi huyo alipokwisha kutoka, Yesu akanena, Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, na Mungu ametukuzwa ndani yake: Mungu akiwa ametukuzwa ndani yake, Mungu nae atamtukuza ndani ya nafsi yake; na marra atamtukuza. Enyi watoto wachanga, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta: na kama nilivyowaambia Wayahudi, ya kama, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja: sasa nawaambia na ninyi. Amri mpya nawapeni, mpendane; kama vile nilivyowapenda ninyi, na ninyi mpendane vivyo hivyo. Hivi watu wote watajua ya kuwa m wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. Simon Petro akamwambia, Bwana, unakwenda wapi? Yesu akamjibu, Niendako, huwezi kunifuata sasa; lakini utanifuata baadae. Petro akamwambia, Bwana, kwa nini nisiweze kukufuata sasa? Nitauweka uzima wangu kwa ajili yako. Yesu akamjibu, Je! uzima wako utauweka kwa ajili yangu? Amin, amin, nakuambia, Jogoo hatawika hatta utakapokuwa umenikana marra tatu. MSIFADHAIKE mioyo yenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambieni; nashika njia kwenda kuwaandalia mahali. Bassi nikishika njia kwenda kuwaandalia mahali, nitakuja tena, niwakaribisheni kwangu; illi nilipo mimi, nanyi mwepo. Na mimi niendako, mwaijua njia. Tomaso akamwambia, Bwana, hatujui uendako; twaijuaje njia? Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. Filipo akamwambia, Bwana, tuonyeshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia, Nimekuwa pamoja nanyi siku hizi zote wala hukunijua, Filipo? Aliyeniona mimi, amemwona Baba; wasemaje wewe, Tuonyeshe Baba? Huamini ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba ndani yangu? Maneno niwaambiayo mimi, sisemi kwa shauri langu tu; lakini Baba akaae ndani yangu huzifanya kazi zake. Niaminini ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba ndani yangu; la! hamwamini hivyo, niaminini kwa sababu ya kazi zenyewe. Amin, amin, nawaambieni, Aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi na yeye atazifanya; atafanya na kubwa kuliko hizi, kwa kuwa nashika njia kwenda kwa Baba. Na mkiomba lo lote kwa jina langu, hili nitalifanya, Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiomba neno kwa jina langu, hili nitalifanya. Mkinipenda mtazishika amri zangu. Na mimi nitamwomba Baba, nae atawapa Mfariji mwingine, akaae nanyi hatta milele, Roho ya kweli; ambae ulimwengu hauwezi kumkubali, kwa kuwa haumwoni wala haumjui: bali ninyi mnamjua; maana anakaa kwenu, nae atakuwa ndani yenu. Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. Bado kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona; kwa sababu mimi ni hayi, ninyi nanyi mtakuwa hayi. Katika siku ile mtajua ninyi, ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, na ninyi ndani yangu, na mimi ndani yenu. Aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendae; nae anipendae atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda, na kujidhihirisha kwake. Yuda akamwambia (siye Iskariote), Bwana, imekuwaje, ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? Yesu akajibu akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. Asiyenipenda, hayashiki maneno yangu; na neno mnalolisikia silo langu, bali lake Baba aliyenipeleka. Haya nimewaambia, nikikaa kwenu. Lakini Mfariji, Roho Mtakatifu, ambae Baba atampeleka kwa jina langu, yeye atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. Amani nawaachieni; amani yangu nawatolea; si kama ulimwengu utoavyo, mimi nawatolea. Msifadhaike moyo wenu, wala msiwe na woga. Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Nakwenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi, kwa sababu nashika njia kwenda kwa Baba: kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi. Na sasa nimewaambieni kabla haijawa, kusudi iwapo, mwamini. Sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana mkuu wa ulimwengu anakuja, wala hana kitu kwangu: lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na, kama Baba alivyoniamuru, ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, tufoke huku. MIMI ndimi niliye mzabibu wa kweli, na Baba yangu ni mkulima. Kilia tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na killa lizaalo hulisafisha illi lizidi kuzaa. Ninyi mmekwisba kuwa safi kwa sababu ya neno nililowaambia. Kaeni ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu, kadhalika na ninyi, msipokaa ndani yangu. Mimi mzabibu; ninyi matawi; akaae ndani yangu, na mimi ndani yake, huyu huzaa Sana; maana pasipo mimi hamwezi kufanya neno. Mtu asipokaa ndani yangu, atupwa nje kama tawi, akauka; huyakusanya, huyatupa motoni, yakateketea. Mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, mtaomba killa mtakalo, na mtafanyiziwa. Kwa hiyo atukuzwa Baba yangu, mzae sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. Kama Baba alivyonipenda mimi, nami nimewapenda ninyi; kaeni katika pendo langu. Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu, na kukaa katika pendo lake. Haya nimewaambieni, illi furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe. Amri yangu ndio hii, mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. Hakima aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuweka uzima wake kwa ajili ya rafiki zake. Ninyi m rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyosikia kwa Baba nimewaarifuni. Si ninyi mlionichagua mimi, bali mimi niliyewachagua ninyi, nikawaamuru, mwende zenu mkazae, mazao yenu yakakae: illi lo lote mmwombalo Baba kwa Jina langu, awapeni. Haya nawaamuru, mpate kupendana. Ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeyapenda yaliyo yake: lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua ninyi katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambieni, Mtumwa si mkubwa kuliko Bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi nanyi: ikiwa walilishika neno langu, watalishika na lenu. Lakini haya yote watawatenda kwa sababu ya jina langu, kwa kuwa hawamjui aliyenipeleka. Kama singalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; sasa hawana udhuru kwa dhamhi yao. Anichukiae mimi, humchukia na Baba yangu. Kama singalitenda kazi kwao asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia. Lakini litimie neno lililoandikwa katika sharia yao, Walinichukia burre. Lakini ajapo Mfariji, nitakaewapelekea toka kwa Baba, Roho ya kweli atokae kwa Baba, yeye atanishuhudia. Na ninyi pia mnashunudu, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwa pamoja nami. MANENO haya nimewaambieni msije mkachukizwa. Watawaharamisha masunagogi: naam, saa inakuja, atakapodhani killa mtu awauae kuwa amtolea Mungu ibada. Na hayo watawatendeni kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. Lakini nimewaambieni haya, illi kusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambieni. Haya sikuwaambieni tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwa pamoja nanyi. Lakini sasa nakwenda zangu kwake aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizae, Unakwenda zako wapi? Illa kwa sababa nimewaambieni haya, huzimi imejaa mioyoni mwenu. Lakini mimi nawaambieni iliyo kweli; Yawafaa ninyi mimi niondoke: kwa maana nisipoondoka, Mfariji hatakuja kwenu; bali nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Na akiisha kuja yeye, atauhakikisha ulimwengu kwa khabari ya dhambi, na haki, na hukumu; Kiva khabari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; kwa khabari ya haki, kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; kwa khabari ya hukumu, kwa sababu mkuu wa ulimwengu huu amehukumiwa. Hatta ninayo mengi bado ya kuwaambieni, lakini hamwezi kuyastahimili sasa. Lakini ajapo yeye, Roho ya kweli, atawaongozeni katika yote iliyo kweli: kwa maana hatasema kwa shauri lake yeye, lakini yote atakayosikia, atayasema, na mambo yajayo atawapasha khabari yake. Yeye atanitukuza mimi: kwa kuwa atatwaa katika iliyo yangu, atawapasheni khabari. Yote aliyo nayo Baba m yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika iliyo yangu, atawapasheni khabari. Bado kitambo, nanyi hamnioni tena; na bado tena kitambo, na mtaniona. Kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba. Bassi baadhi ya wanafunzi wake walisemezana, Neno gani hili analosema, Bado kitambo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo na mtaniona? na, Kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba? Bassi walisema. Neno gani hili analosema, hili Bado kitambo? Hatujui asemalo. Yesu alifahamu ya kwamba walitaka kumwuliza akawaambia, Hili ndilo mnalotafuta ninyi kwa ninyi, ya kuwa nalisema, Bado kitambo nanyi hamnioni, na bado kitambo na mtaniona? Amin, amin, nawaambieni, Ninyi mtalia, na kuomboleza, bali, ulimwengu utafurahi: ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha, Mwanamke azaapo, yuna huzuni kwa kuwa saa yake imekuja; hatta, akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena shidda, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni. Bassi na ninyi sasa hivi mna huzuni; lakini nitawaona tena, na moyo wenu utafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleae. Na siku ile hamtaniuliza neno. Amin, amin, nawaambieni, Mkimwomba Baba neno kwa jina langu atawapeni. Mpaka leo hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, na mtapata, furaha yenu iwe timilifu. Haya nimesema nanyi kwa methali: saa inakuja, sitasema nanyi tena kwa methali, lakini nitawapa kwa wazi khabari ya Baba. Katika siku ile mtaomba kwa jina langu; wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea Baba; kwa maana Baba mwenyewe awapenda ninyi, kwa kuwa ninyi mmenipenda mimi, mkaamini ya kwamba mimi nalitoka kwa Baba. Nalitoka kwa Baba, nimekuja ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu, nashika njia kwenda kwa Baba. Wanafunzi wake wakasema, Tazama, sasa wasema waziwazi, wala huneni methali yo yote. Sasa tumejua ya kuwa unajua yote, wala huhitaji mtu akuulize; kwa hiyo twaamini ya kwamba ulitoka kwa Mungu. Yesu akawajihu, Sasa hivi mnaamini? Saa inakuja, naam, imekwisha kuja, mtatawanyika killa mmoja kwa mambo yake, mtaniacha mimi peke yangu; wala mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami. Haya nimewaambieni, mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mtapata shidda: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. MANENO hayo aliyasema Yesu: akainua macho yake kuelekea mbinguni, akanena, Baba, saa ile imekuja. Mtukuze Mwana wako, illi Mwana wako nae akutukuze wewe; kama vile ulivyompa mamlaka juu ya killa mwenye mwili, illi yote uliyompa awape uzima wa milele. Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani. Kazi ile uliyonipa niifanye nimeimaliza. Na sasa unitukuze wewe, Baba, pamoja nawe, kwa utukufu nle niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya kuwako ulimwengu. Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; wahkuwa wako, ukanipa mimi: na neno lako wamelishika. Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako: kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; wakavapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakaamini ya kwamba ndiwe uliyenituma. Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu, bali wao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako. Na yote yaliyo yangu ni yako, na yaliyo yako ni yangu: nami nimetukuzwa ndani yao. Na mimi simo tena ulimwenguni, na hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, uwalinde kwa jina lako wale ulionipa; wawe moja, kama sisi. Nilipokuwa pamoja nao ulimwenguni, mimi naliwalinda kwa jina lako: wale ulionipa naliwatunza, wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, illa yule mwana wa upotevu maandiko yapate kutimizwa. Na sasa naja kwako; na haya nayasema ulimwenguni, illi wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao. Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu uliwachukia, kwa kuwa wao si watu wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Siombi uwatoe katika ulimwengu, hali uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisiyvo wa ulimwengu. Uwatakase kwa kweli; neno lako ndio kweli. Kama ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma wao ulimwenguni. Na kwa ajili yao najitakasa, illi na hawa watakaswe katika kweli. Wala si hao tu ninaowaombea, bali na wao walakaoniammi kwa sababu ya neno lao. Wote wawe umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, na mimi ndani yako, illi na hawa wawe umoja ndani yetu: ulimwengu upate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma. Nami, utukufu ule ulionipa nimewajia wao, wawe umoja, kama sisi tulivyo umoja: mimi ndani yao, na wewe ndani yangu, wapate kukamilika na kuwa umoja; illi ulimwengu ujue ya kuwa udiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua, lakini mimi nalikujua; na hawa walijua ya kuwa ndiwe uliyenituma. Naliwajulisiia jina lako, tena nitawajulisha, illi pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, na mimi niwe ndani yao. ALIPOKWISHA kusema haya, Yesu akatoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ngʼambu ya kijiti Kedron, palipo bustani; akaingia, yeye na wanafunzi wake. Yuda nae, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikwenda huko marra nyingi pamoja na wanafunzi wake. Bassi Yuda akiisha kupokea kikosi cha askari, na watumishi waliotoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaenda huko na makandili na taa za mkono na silaha. Bassi Yesu, akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Mnamtafuta nani? Wakamjibu, Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Mimi ndiye. Yuda nae aliyemsaiiti alikuwa akisimama pamoja nao. Bassi alipowaambia. Mimi ndiye, walirudi nyuma, wakaanguka chini. Bassi akawauliza marra ya pili, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti. Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni kwaniba mimi ndiye; bassi mkinitafuta mimi, waacheni hawa waende zao; illi litimizwe lile neno alilolisema, Hawa ulionipa sikupoteza hatta mmoja wao. Bassi Simon Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumishi wa kuhani mkuu akamkata sikio lake la kuume. Na yule mtumishi jina lake alikwitwa Malko. Bassi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga wako alani mwake. Kikombe alichonipa Baba, nisikinywee? Bassi kile kikosi na yule jemadari na wale watumishi wa Wayahudi wakamkamata Yesu, wakanifunga, wakamchukua kwa Anna kwanza: maana alikuwa mkwewe Kayafa, yule aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule. Na Kayafa ndiye aliyewapa Wayahudi shauri kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu. Simon Petro akamfuata Yesu, na mwanafunzi mwingine: na yule mwanafunzi alikuwa anajulika na kuhani mkuu: akaingia pamoja na Yesu behewani mwa kuhani mkuu; lakini Petro akasimama nje mlangoni. Bassi yule mwanafunzi mwingine aliyejulika na kuhani mkuu akatoka akasema na mwanamke aliye mngoje mlango, akamleta Petro ndani. Bassi yule kijakazi aliye mngoje mlango akamwambia Petro, Wewe nawe, je! huwi mmojawapo wa wanafunzi wake mtu huyu? Yeye akasema, Si mimi. Na wale watumishi na askari walikuwa wamesimama, wamefanya moto wa makaa; maana ilikuwa baridi, wakawa wakikota moto. Petro nae, alikuwa pamoja nao, anakota moto. Bassi kuhani mkuu akamwuliza Yesu khabari za wanafunzi wake, na khabari za mafundisho yake. Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu kwa wazi; mimi siku zote nalifundisha katika masunagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi siku zote; wala kwa siri sikusema neno. Ya nini kumuliza? waulize wale waliosikia, ni nini niliyosema nao: wao wanajua niliyowaambia. Aliposema maneno haya, mmoja wa wale watumishi aliyesimama karibu akampiga Yesu koli, akinena, Wamjibu hivi kuhani mkuu? Yesu akamjibu, Kama nimesema mabaya, yashuhudie yale mabaya; bali kama nimesema mema, wanipigia nini? Bassi Anna akampeleka amefungwa kwa Kayafa kuhani mkuu. Na Simon alikuwa akisimama, anakola moto. Bassi wakamwambia, Wewe nawe je! huwi mmojawapo wa wanafunzi wake? Yeye akanena, Sio mimi. Mmoja wa wale watumishi wa kuhani mkuu, ni jamaa yule aliyekatwa sikio na Petro, akasema, Mimi sikukuona bustanini pamoja nae? Bassi Petro akakana tena, jogoo akawika marra. Bassi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa hatta Praitorio; ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya Praitorio, wasije wakatiwa najis, bali waile Pasaka. Bassi Pilato akawatokea nje akasema, Mashitaka gani mnayoleta juu ya mtu huyu? Wakajibu, wakamwambia, Kama huyu asingekuwa mtu mwovu, tusingemleta kwako. Bassi Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi, mkamhukumu kwa sharia yenu. Wayahudi wakamwambia, Sisi hatuna rukhusa kuua mtu; illi neno lake Yesu litimizwe, alilolisema, akionyesha ni mauti gani atakayokufa. Bassi Pilato akaingia Praitorio tena, akamwita Yesu, akamwambia, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akajibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, ama watu wengine walikuambia khabari zangu? Pilato akajibu, Je! mimi Myahudi? Taifa lako na makuhani wakuu ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini? Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu, kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu: watumishi wangu wangalinipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi: lakini sasa ufalme wangu sio wa hapa. Bassi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme bassi? Yesu akajibu, Wewe wanena ya kwamba mimi ni mfalme. Mimi nalizaliwa kwa ajili ya haya na kwa ajili ya haya nalikuja ulimwenguni, illi niishuhudie kweli. Killa aliye wa kweli hunisikia sauti yangu. Pilato akamwambia, Kweli ni kitu gani? Akiisha kusema neno hili akawatokea Wayahudi marra ya pili, akawaambia, Mimi sioni khatiya yo yote kwake. Lakini kwenu kuna desturi, ya mimi kuwafungulia mtu mmoja wakati wa Pasaka: bassi, wapenda niwafungulie mfalme wa Wayahudi? Bassi wakapiga kelele marra ya pili, wote pia, wakinena, Si huyu, bali Barabba. Nae Barabba alikuwa mnyangʼanyi. BASSI ndipo Pilato akamtwaa Yesu, akampiga mijeledi. Askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi jekundu; wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi! wakimpiga makofi. Pilato akatokea tena nje akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa sioni khatiya yo yote kwake. Bassi Yesu akatoka nje, amevaa ile taji ya miiba, na lile vazi jekundu. Pilato akawaambia, Tazama, Mtu huyu! Bassi wale makuhani wakuu na watumishi walipomwona, wakapiga kelele, wakisema, Msulibishe, msulibishe. Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi, kamsulibisheni: kwa maana mimi sioni khatiya kwake. Wayahudi wakamjibu, Sisi tuna sharia, na kwa sharia hiyo amepasiwa kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu. Bassi Pilato aliposikia neno hilo, akazidi kuogopa; akaingia tena Praitorio, akamwamhia Yesu, Umetoka wapi wewe? Lakini Yesu hakumpa jibu lo lote. Bassi Pilato akamwambia, Husemi na mimi? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukusulibisha na nina mamlaka ya kukufungua? Yesu akamjibu, Usingekuwa na mamlaka yo yote, kama usingepewa toka juu: kwa sababu hii yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi. Tangu hapo Pilato akatafuta kumfungua; lakini Wayahudi wakapiga makelele wakisema, Ukimfungua huyu, wewe si mpenda Kaisari; killa ajifanyae kuwa mfalme amfitini Kaisari. Bassi Pilato, aliposikia maneno haya, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti, mahali paitwapo Sakafu ya mawe, na kwa Kiebrania Gabbatha. Ilikuwa Maandalio ya Pasaka: ilikuwa panapo saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, mfalme wenu! Bassi wale wakapiga kelele, Mwondoshe, mwondoshe, msulibishe. Pilato akawaambia, Nimsulibishe mfalme wenu? Makuhani wakuu wakajibu, Hatuna mfalme illa Kaisari. Bassi ndipo akamtia mikononi mwao asulibishwe. Bassi wakampokea Yesu: akatoka, akijichukulia msalaba wake, hatta mahali paitwapo pa kichwa, na kwa Kiebrania Golgotha; wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja nae, huko na huko, na Yesu katikati. Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI. Bassi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali paie aliposulihiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani. Bassi makuhani wakuu wa Wayahudi wakamwambia Pilato, Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; hali ya kwamba yule alisema, Mimi mfalme wa Wayahudi. Pilato akajihu, Niliyoandika nimeyaandika. Bassi askari, walipomsulibisha Yesu, wakatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu mane, kwa killa askari fungu lake; nayo kanzu: na kanzu ile haikushonwa, imefumwa pia tangu juu. Bassi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani; andiko litimie linenalo, Waligawanya nguo zangu, na vazi langu walilipigia kura. Bassi ndivyo walivyofanya askari. Na penye msalaba wake Yesu wamesimama mama yake, na ndugu ya mama yake, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene. Bassi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, akamwambia mama yake, Bibi, tazama, mwana wako. Baadae akamwambia mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua kwake. Baada ya haya Yesu, akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizwa, andiko litimizwe, akasema, Nina kiu. Kikawako chombo kimejaa siki; bassi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya husopo, wakampelekea kinywani. Bassi Yesu alipoipokea siki, akasema, Imekwisha: akainama kichwa, akatoa roho. Bassi Wayahudi, kwa maana ni Maandalio, miili isikae juu va msalaba siku ya sabato (maana siku ya sabato ile ilikuwa siku kuhwa), wakamwomba Pilato, miguu yao ivunjwe, wakaondolewe. Bassi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili aliyesulibiwa pamoja nae. Walipomjia Yesu, wakiona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; lakini askari mmoja kwa mkuki alimchoma ubavu, ikatoka marra damu na maji. Nae aliyeona ameshuhudu, na ushuhuda wake ni kweli; na yeye anajua ya kuwa asema kweli, ninyi mpate kuamini. Kwa maana haya yalitukia andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na tena, andiko la pili lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma. Hatta baada ya haya, Yusuf, aliye wa Arimathaya, nae vu mwanafunzi wa Yesu, lakini kwa siri (maana aliwaogopa Wayahudi), akamwomba Pilato rukhusa auondoe mwili wake Yesu: Pilato akampa rukhusa. Bassi akaenda akauondoa mwili wake. Akaenda Nikodemo nae, yule aliyemwendea usiku hapo kwanza, akaleta machanganyiko ya manemane na uudi, yapata ratli mia. Bassi wakautwaa mwili wa Yesu, wakaufunga saanda ya bafta, pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika. Na mahali pale aliposulibiwa palikuwa na bustani; na ndani ya bustani kaburi jipya, bado hajatiwa mtu aliye yote ndani yake. Humo bassi, kwa sababu ya Maandalio ya Wayahudi, wakamweka Yesu; maana lile kaburi lilikuwa karibu. HATTA siku ya kwanza ya sabato Mariamu Magdalene akaenda kaburini alfajiri, kungali giza bado, akaliona jiwe limeondolewa kaburini. Bassi akaenda mbio hatta kwa Simon Petro, na kwa mwanafunzi yule mwingine aliyependwa na Yesu, akawaambia, Wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka. Bassi Petro akatoka, na mwanafunzi yule mwingine, wakashika njia kwenda kaburini. Wakaenda mbio wawili pamoja: yule mwanafunzi mwingine akaenda mbio upesi kuliko Petro, akawa wa kwanza wa kufika kaburini; akainama, akaviona vitambaa vimewekwa; illakini hakuingia. Bassi akaja na Simon Petro, akimfuata, akaingia kaburini; akavitazama vitambaa vimewekwa, na ile leso iliyokuwa kichwani pake, haikuwekwa pamoja na vitambaa, bali imekunjwa, na kuwekwa mahali pa peke yake. Bassi ndipo akaingia nae mwanafunzi yule mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika kaburini, akaona, akaamini. Kwa maana hawajalifahamu andiko bado, kwamba imempasa kufufuka. Bassi wanafunzi wale wakaenda zao nyumbani kwao. Lakini Mariamu alikuwa amesimama karibu na kaburi, nje yake, analia; bassi, akilia hivi, akainama, akachungulia ndani ya kaburi; akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani, na mmoja miguuni, hapo ulipowekwa mwili wa Yesu. Nao wakamwambia, Bibi, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala sijui walikomweka. Alipokwisha kusema haya, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu. Yesu akamwambia, Bibi, unalilia nini? Unamtafuta nani? Yeye, akidhani ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, kama umemchukua wewe, niambie ulipomweka, nami nitamwondoa. Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Rabboni (tafsiri yake Mwalimu). Yesu akamwambia, Usiniguse; kwa maana sijapaa kwa Baba yangu. Lakini enenda kwa ndugu zangu, ukawaambie, Ninapaa kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu. Mariamu Magdalene akaenda akawapasha wanafunzi khabari ya kwamba amemwona Bwana, na ya kwamba amemwambia haya. Ikawa jioni katika siku ile ya kwanza ya sabato, na milango imefungwa walipokuwapo wanafunzi kwa khofu ya Wayahudi, akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani kwenu. Akiisha kusema haya, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Bassi wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana. Bassi Yesu akawaambia marra ya pili, Amani kwenu; kama Baba alivyonipeleka, nami nawatuma ninyi. Akiisha kusema haya, akawapulizia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia, wamefungiwa. Tomaso, mmoja wa wathenashara aitwae Didumo, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu. Bassi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Nisipoona mikononi mwake alama za misumari, na kutia kidole changu katika alama za misumari, na kutia mkono wangu uhavuni mwake, sitaamini kabisa. Baada ya siku nane wanafunzi wake walikuwamo ndani marra ya pili, na Tomaso pamoja nao. Yesu akaja, milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani kwenu. Akiisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako, ukatazame mikono yangu; kalete mkono wako, uutie katika ubavu wangu; wala nsiwe asiyeamini, bali aaminiye. Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu, na Mungu wangu. Yesu amwambia, Kwa kuwa umeniona, umeamini; wa kheri wasioona wakaamini. Bassi ziko ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki; lakini hizi zimeandikwa mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. BAADA ya haya Yesu alijionyesha tena kwa wanafunzi wake, penye bahari ya Tiberia; nae alijionyesha hivi. Simon Petro, na Tomaso aitwae Didumo, na Nathanael wa Kana wa Galilaya, na wana wa Zebedayo, na watu wengine wawili katika wanafunzi wake, walikuwa mahali pamoja. Simon Petro akawaambia, Ninakwenda kuvua samaki. Wakamwambia, Na sisi tutakwenda pamoja nawe. Wakatoka, wakapanda chomboni; na usiku ule hawakupata kitu. Hatta assubuhi kulipokucha, Yesu akasimama ufukoni, walakini wanafunzi hawakujua ya kuwa ni Yesu. Bassi Yesu akawaambia, Wanangu, mna kitoweo? Wakamjibu, Hapana. Akawaambia, Litupeni jarife upande wa kuume wa chombo, nanyi mtapata. Bassi wakatupa, wala hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa samaki. Bassi mwanafunzi yule ambae Yesu alimpenda akamwambia Petro, Ndiye Bwana. Bassi Simon Petro, aliposikia ya kwamba ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana alikuwa uchi), akajitupa baharini. Wanafunzi wengine wakaja katika mashua (maana hawakuwa mbali ya inchi kavu, illa yapata dhiraa miateen) wakilikokota jarife lenye samaki. Bassi waliposhuka pwani, wakaona moto wa makaa huko, na kitoweo kimetiwa juu yake, na mkate. Yesu akawaambia, Leteni hapa baadhi ya samaki mlizozivua sasa hivi. Bassi Simon Petro akapanda chomboni, akalivuta jarife pwani, limejaa samaki kubwa, mia na khamsini na tatu: na ijapokuwa zilikuwa nyingi namna hii, jarife halikupasuka. Yesu akawaambia, Njoni mle. Wala hapana mtu katika wale wanafunzi aliyethubutu kumwuliza, Wewe nani? wakijua ya kuwa ni Bwana. Yesu akaenda akautwaa mkate, akawapa, na kitoweo vivyo hivyo. Hii ndiyo marra ya tatu Yesu alionekana na wanafunzi wake baada ya kufufuka katika wafu. Bassi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simon Petro, Simon wa Yohana, wanipenda kuliko bawa? Akamwambia, Naam, Bwana; wewe wajua ya kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana kondoo wangu. Akamwambia marra ya pili, Simon wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Naam, Bwana; wewe wajua ya kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu. Akamwambia marra ya tatu, Simon wa Yohana, Wanipenda mimi? Petro akahuzunika kwa kuwa alimwambia marra ya tatu, Wanipenda mimi? Akamwambia, Bwana, wewe unajua yote; unajua ya kuwa nakupenda. Yesu amwambia, Lisha kondoo zangu. Amin, amin, nakuambia, Ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga, ukienda ulikotaka; utakapokuwa mzee, utanyosha mikono yako, na mwingine atakufunga, atakuchukua usikotaka. Akasema hili kwa kuonyesha ni mauti gani atakayomtukuza Mungu. Na akiisha kusema haya, akamwambia, Nifuate. Na Petro akigeuka, akamwona mwanafunzi yule aliyependwa na Yesu akifuata; yeye ndiye aliyeegamia kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni na kusema, Bwana yu nani akusalitiye? Petro akimwona huyu, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je? Yesu akamwambia, Nikitaka huyu akae hatta nijapo imekukhusu nini? wewe unifuate mimi. Bassi neno hili lilienea katika ndugu kwamba mwanafunzi yule hafi: walakini Yesu hakumwambia, Hafi; bali, Nikitaka akae hatta nijapo imekukhusu nini? Huyu ndiye mwanafunzi ayashuhudiae haya, na aliyeandika haya; na twajua ya kuwa ushuhuda wake ni wa kweli. Kuna na mengine mengi aliyoyafanya Yesu, nayo yakiandikwa moja moja, nadhani hatta ulimwengu wote usingetosha kwa vitabu vitakavyoandikwa. Amin. KITABU kile cha kwanza nalikifanya, Theofilo, katika khabari ya mambo yote aliyoanza kufanya Yesu na kufundisha, hatta siku ile alipowaagiza kwa Roho Mtakatifu mitume aliowachagua, akachukuliwa juu: na baada ya kuteswa kwake, akawadhihirisbia ya kwamba yu hayi, kwa dalili nyingi, akiwatokea muda wa siku arubaini, na kuyanena mambo yaliyonkhusu ufalme wa Mungu. Hatta, akikutana nao, akawaagiza wasitoke katika Yerusalemi, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia khabari zake kwangu; ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi si nyingi. Bassi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Bwana, wakati huu ndipo unapomrudishia Israeli ufalme wake? Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemi, na katika Yahudi yote, na Samaria, na hatta mwisho wa inchi. Akiisha kusema haya, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakasema, Watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni. Kiisha wakarudi kwenda Yerusalemi kutoka mlima ulioitwa wa mizeituni, ulio karibu na Yerusalemi, wapata mwendo wa sabato. Hatta walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartolomayo na Mattayo, Yakobo wa Alfayo, na Simon Zelote, na Yuda wa Yakobo. Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kuomba, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama wake Yesu, na ndugu zake. Siku zile akasimama Petro kati ya wanafunzi, akasema (jumla ya majina ilipata mia na ishirini), Ndugu imepasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daud, katika khabari za Yuda, aliyekuwa kiongozi wao waliomkamata Yesu: kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi, akapata sehemu ya khuduma hii. (Bassi huyu alinunua konde kwa ijara ya ndhalimu; akaanguka kifudifudi akapasuka, matumbo yake yote yakatoka. Ikajulikana na watu wote wakaao Yerusalemi; hatta konde lile likaitwa kwa lugha yao Akeldama, maana yake, konde la damu.) Kwa maana imeandikwa katika kitabu cha Zaburi, Kikao chake kiwe ukiwa, wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo; tena, Usimamizi wake autwae mwingine. Bassi katika watu waliofuatana nasi wakati wote ambapo Bwana Yesu alikuwa akiingia kwetu na kutoka kwetu, akianza tangu ubatizo wa Yohana, hatta siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, lazima mmoja wao afanywe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi. Wakaweka wawili, Yusuf, aitwae Barsaba, aliyepewa jina la pili Yusto, na Mattiya. Wakasali, wakasema, Wewe, Bwana, ujuae mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili, atwae sehemu yake ya khuduma hii na utume huu, alioukosa Yuda aende zake mahali pake. Wakawapigia kura: kura ikamtoa Mattiya; akachaguliwa kuwa pamoja na mitume edashara. HATTA ilipotimia siku ya Pentekote walikuwako wote pamoja mahali pamoja. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kassi, ukaijaza nyumba yote walipokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia killa mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha mbalimbali, kama Roho alivyowajalia kutamka. Na walikuwako Yerusalemi Wayahudi wakikaa, watu watawa, watu wa killa taifa chini ya uwingu. Bassi sauti hii ilipokuja makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa killa mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake. Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Si hawa wote wasemao Wagalilaya? Imekuwaje bassi sisi kusikia killa mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? Waparthi na Wamedi na Waelamiti, nao wakaao Mesopotamia, Yahudi ua Kappadokia, Ponto na Asia, Frugia na Pamfulia, Misri na pande za Libua karibu na Kurene, na Warumi wageni, Wayahudi na Waongofu, Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa maneno yetu matendo makuu ya Mungu. Wakashangaa wote wakaingiwa na mashaka, wakaambiana, Maana yake nini mambo haya? Wengine walidhihaki, wakisema, Wamelewa kwa mvinyo mpya. Lakini Petro akasimama pamoja na wale edashara, akapaaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemi, jambo hili lijulike kwenu, mkasikilize maneno yangu. Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana; lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoel: Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, Nitawamwagia watu wote Roho yangu, Na wana wenu na binti zenu watatabiri, Na vijana wenu wataona maono: Na wazee wenu wataota ndoto: Na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wauawake Roho yangu, Nao watatabiri, Nitatoa ajabu katika mbingu juu, Na ishara katika inchi chini, Damu na moto, na mvuke wa moshi: Jua litageuka kuwa giza, Na mwezi kuwa damu, Kabla ya kuja ile siku ya Bwana Iliyo kuu, dhahiri. Na itakuwa killa atakaeliitia jiua la Bwana ataokolewa. Enyi waume wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua; mtu huyu alitwaliwa nanyi kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake taugu zamani, nanyi mkamsulibisha kwa mikono mibaya, mkamwua: Mungu akamfufua, akilegeza utungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao. Maana Daud amtaja khabari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko mkono wangu wa kuume, nisitikisike. Kwa hiyo moyo wangu ukapendezwa, ulimi wangu ukafurahi; Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini. Kwa maana hutaniacha roho yangu katika kuzimu: Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu. Umenifundisha njia ya uzima; Utanijaza furaha kwa uso wako. Ndugu, mniwie radhi, niseme pasipo khofu mbele yenu khabari za baba yetu mkuu Daud, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hatta leo. Bassi kwa kuwa nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake kwa jinsi ya kiwiliwili atamwinua Kristo, akae katika kiti chake cha enzi; yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja khabari za kufufuka kwake Kristo, ya kama roho yake haikuachwa katika kuzimu, wala mwili wake hankuona uharibifu, Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake. Bassi akiisha kupandishwa hatta mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia. Maana Daud hakupanda mbinguni: bali yeye mwenyewe amesema, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume. Hatta nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako. Bassi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo. Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe killa mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na watoto wenu, na watu wote walio mbali, na wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu. Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. Nao waliolipokea neno lake kwa furaha wakabatizwa: na siku ile wakazidishiwa watu wapata elfu tatu. Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. Killa mtu akaingiwa na khofu: ajabu nyingi na ishara zikafanyika kwa ujumbe wa mitume. Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama killa mtu alivyokuwa na haja. Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kupokea chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza wutu wote. Bwana akalizidisha kanisa killa siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa. BASSI Petro na Yohana walikuwa wakipanda pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tissa. Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mama yake alichukuliwa na watu, wakamweka killa siku katika mlango wa hekalu nitwao Mzuri, illi aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu. Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka. Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi. Akawaangalia, akitaraja kupewa kitu nao. Petro akanena, Fedha sina, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Mnazareti, simama uende. Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, marra nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikapata nguvu. Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda: akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka, akimsifu Mungu. Watu wote wakamwona akieuda, akimsifu Mungu. Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa ameketi na kuomba sadaka penye mlango mzuri wa hekalu: wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata. Bassi yule kiwete aliyeponywa alipokuwa akiwashika Petro na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika tao lile lililokwitwa tao la Sulemani; wakishangaa sana. Hatta Petro alipoona haya akawajibu watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utawa wetu sisi? Mungu wa Ibrahimu na Isaak na Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambae ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe. Ninyi mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe muuaji: mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambae Mungu amemfufua: na sisi tu mashahidi wake. Na kwa imani ya jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnaemwona na kumjua: na imani ile iliyo kwa njia yake yeye imempatia huyu mbele yemi ninyi nyote uzima huu mkamilifu. Bassi sasa ndugu, najua ya kuwa mliyatenda haya kwa kutokujua kwenu, kama na wakuu wenu walivyotenda. Lakini mambo yale aliyokhubiri Mungu tangu zamani kwa vinywa vya manabii wake wote, ya kama Kristo atateswa, ameyatimiza hivyo. Tubuni bassi, mrejee, illi dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuhurudishwa kwa kuwako kwake Bwana: apate kumtuma Kristo aliyekhubiriwa kwenu tangu zamani; ambae ilimpasa kupokewa mbinguni hatta zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa vinywa vya manabii wake tokea mwanzo wa ulimwengu. Kwa maana Musa aliwaambia baba zetu ya kama, Bwana Mungu atawainulieni nabii, atakaetoka katika ndugu zenu, kama mimi, msikieni yeye katika mambo yote atakayonena. Na itakuwa ya kwamba kilia mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake. Naam, na manabii wote tangu Samwil na wale waliokuja nyuma yake, wote walionena, walikhubiri khabari za siku hizi. Ninyi m watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa. Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, illi kuwabarikini kwa kumwepusha killa mmoja wenu na maovu wake. HATTA walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea, wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuukhubiri ufufuo wa wafu unaopatikana kwa Yesu. Wakawakamata, wakawaweka garezani hatta assubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni. Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini: na hesabu ya watu ilikuwa kama elfu tano. Hatta assubuhi wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemi, na Kayafa pia, na Yohana, na Iskander, na wo wote waliokuwa jamaa zake kuhani mkuu. Wakawaweka katikati, wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani mmefanya haya ninyi? Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli, kama tukiulizwa leo khabari ya yule mtu dhaifu jinsi alivyoponywa, jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Mnazareti, ambae ninyi mlimsulibisha, Mungu akamfufua, kwa jina hilo mtu huyu anasimama mzima mbele yenu. Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. Wala hakuna wokofu katika mwingine aliye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wana Adamu litupasalo kuokolewa nalo. Bassi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kujua ya kuwa ni watu wasio elimu, wasio maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu. Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu. Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri, wakisemii, Tuwafanyieni watu hawa? maana ishara mashuhuri imefanywa nao, iliyo dhabiri kwa watu wote wakaao Yerusalemi, wala hatuwezi kuikana. Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, tuwaogofishe wasiseme tena na mtu aliye yote kwa jina hili. Wakawaita, wakawaagiza wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu. Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia. Nao walipokwisha kuwaogofya tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu: kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka: maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arubaini. Hatta walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha khabari ya mambo yote waliyoambiwa na makuhani wakuu na wazee. Nao waliposikia, wakampaazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na inchi na bahari na vitu vyote vilivyomo: nawe ulinena kwa kinywa cha Daud mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na watu wametafakari ubatili? Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja, Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake. Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika juu ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta, illi wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee. Bassi sasa, Bwana, yaangalie maogofya yao; ukawajalie watumishi wako kunena neno lako kwa uthabiti, ukinyosha mkono wako kuponya: ishara na maajabu zifanyike kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu. Hatta walipokwisha kumwomba Mungu, pahali paie walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa uthabiti. Na jamii ya watu walioamini walikuwa moyo mmoja na roho moja: wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa uguvu nyingi. Neema nyingi ikawa juu yao wote. Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na uwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa wakaiweka miguuni jia mitume; killa mtu akagawiwa kwa kadiri alivyohitaji. Na Yusuf, aliyeitwa na mitume Barnaba (tafsiri yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kupro, alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume. LAKINI mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza uwanja, akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe nae akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. Petro akamwambia, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo kumwambia uwongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya uwanja? Ulipokuwa kwako, haukuwa mali yako? Na ulipokuwa umekwisha kuuzwa haukuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hatta ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uwongo mwana Adamu, bali Mungu. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Khofu nyiugi ikawapata watu wote walioyasikia haya. Vijana wakaondoka, wakamtia katika saanda, wakamchukua nje, wakamzika. Hatta muda wa saa tatu baadae mkewe akaingia, nae hana khabari ya hayo yaliyotokea. Petro akamjibu, Niambie, Mliuuza uwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndio, kwa thamani hiyo. Petro akamwambia, Hikuwaje hatta mkapatana kumjaribu Roho ya Bwana? angalia, miguu yao waliomzika mume wako ipo mlangoni, nao watakuchukua wewe nawe. Marra akaanguka miguuni pake akafa: wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe. Khofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya. Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu: nao wote walikuwa kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani: na katika wote wengine hapana hatta mmoja aliyethubutu kuambatana nao: illa watu waliwaadhimisha: waamini wakazidi kuja kwa Bwana, wengi, wanaume ha wanawake: hatta katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, huwaweka juu ya mifarashi na vitanda, illi, Petro akija, kivuli chake tu kimtie kivuli mmojawapo wao. Nayo makutano ya miji ilioyo kando kando ya Yerusalemi yakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu: nao wote wakaponywa. Akaondoka kuhani mkuu na wote waliokuwa pamoja nae (hao ndio walio wa madhehehu ya Masadukayo) wamejaa wivu, wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza; lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema, Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya uzima huu. Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja kuhani mkuu nao walio pamoja nae, wakawaita watu wa haraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani illi wawalete. Hatta watumishi walipofika hawakuwaona gerezani, wakarudi wakatoa khabari, wakisema, Gereza tumeikuta imefungwa salama salamini, nao walinzi wamesimama mbele ya mlango: lakini tuliponfungua hatukukuta mtu ndani. Kuhani mkuu na jemadari wa hekalu na makuhani wakuu waliposikia haya, wakaingiwa na mashaka kwa ajili yao, yatakuwaje mambo hayo. Mtu mmoja akaja akawapasha khabari ya kama, Watu wale mliowaweka gerezani wako ndani ya hekalu, wamesimama wakiwafundisha watu. Yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawatupia mawe. Wakawaleta, wakaweka katika baraza. Kuhani mkuu akawauliza, akisema, Je! hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili: nanyi mmeijaza Yerusalemi mafundisho yenu, na mnataka kuleta damu ya mtu yule juu yetu. Petro na mitume wakajibu, wakaaena, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wana Adamu. Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambae ninyi mlimwua mkamtundika katika mti. Mtu kuyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toha na masamaha ya dhambi. Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambae Mungu amewapa wote wamtiio. Waliposikia wakachomwa mioyo yao; wakafanya shauri kuwaua. Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamaliel, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza, akaamuru mitume wawekwe nje kitambo, akawaambia, Enyi waume wa Israeli, jihadharini jinsi mtakavyowatenda watu hawa. Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akidai ya kuwa yeye ni mtu, mkuu watu wapata aroba mia wakashikamana nae, na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu. Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa kodi, akawavuta watu kadha wa kadha nyuma yake, nae akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika. Bassi sasa nawaambieni, Jiepusheni na watu hawa, waacheni: kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa ya kibinadamu, itavunjwa, illakini ikiwa ya Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu. Wakakubali maneno yake; wakawaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kiisha wakawaacha waende zao. Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya jina lake. Na killa siku ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kukhubiri khabari njema za Yesu kwamba ni Kristo. HATTA siku ziie wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manungʼuniko ya Wahelenisti juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika khuduma ya killa siku. Wale thenashara wakawaita jamii va wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kukhudumu mezani. Bassi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, illi tuwaweke juu ya jambo hili: na sisi tutadumu katika kumwomba Mungu na kulikhudumia Neno lake. Neno hili likapendeza machoni jia mkutano wote: wakamehagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu na Filipo, na Prokoro, na Nikanor, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia. Wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao. Nenu la Mungu likaenea: hesahu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemi: jamii kubwa la makuhani wakaitii Imani. Na Stefano, akijaa imani na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu. Lakini baadhi ya watu wa sunagogi lililokwitwa sunagogi la Malibertino, na la Wakurene na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka wakajadiliana na Stefano: lakini hawakuweza kushindana na hekima yake wala na Roho aliyosema nayo. Hatta wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu. Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi: wakaniwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza. Wakasimamisha mashahidi wa uwongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati: maana tumemsikia akisema kwamba Yesu huyo Mnazareti atapaharibu pahali hapa, na kuzihadili desturi tulizopewa na Musa. Watu wote walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao, wakamwona uso wake kuwa kama uso wa malaika. KUHANI mkuu akasema, Je! Mambo hayo ndivyo yalivyo? Nae akasema, Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Ibrahimu, alipokuwa katika Mesopotamia, kabla hajakaa Kharran, akamwambia, Toka katika inchi yako na katika jamaa zako, ukaende hatta inchi nitakayokuonyesha. Ndipo alitoka katika inchi ya Wakaldayo, akakaa Kharran, akatoka huko baada ya kufa baba yake, Mungu akamhamisha hatta inchi hii mnayokaa ninyi sasa. Wala hakumpa urithi humu hatta kiasi cha kuweka mguu: akaahidi kwamba atampa, iwe milki yake, na ya, uzao wake baadae, alipokuwa hana mtoto. Mungu akanena hivi, ya kama wazao wake watakuwa wageni katika inchi ya watu wengine, nao watawafanya kuwa watumwa wao, na kuwatenda mabaya kwa muda wa miaka aroba mia. Na lile taifa watakaowafanya watumwa nitawahukumu mimi, alisema Mungu; na baada ya hayo watatoka, nao wataniabudu mahali hapa. Akampa agano la Tohara; bassi Ibrahimu akazaa Isaak, akamtahiri siku ya nane. Isaak akamzaa Yakobo, Yakobo akawazaa wale thenashara, wazee wetu. Wale wazee wetu wakamwonea wivu Yusuf, wakamwuza aende Misri. Mungu akawa pamoja nae, akamtoa katika misiba yake yote, akampa kibali na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri: nae akamfanya msimamizi wa Misri na nyumba yake yote. Bassi kukawa njaa juu ya inchi yote ya Misri na Kanaan, na dhiki nyingi, wala baba zetu hawakupata chakula cha kuwatosha. Hatta Yakobo aliposikla ya kwamba huko Misri kuna nafaka, akawatuma baba zetu marra ya kwanza. Hatta safari ya pili Yusuf akajitambulisha kwa ndugu zake, jamaa ya Yusuf ikawa dhahiri kwa Farao. Yusuf akatuma watu akamwita Yakobo baba yake na jamaa zake wote pia, watu sabaini na watano. Yakobo akashuka hatta Misri, akafariki yeye na baba zetu; wakachukuliwa hatta Sukem wakazikwa katika kaburi lile, ambalo Ibrahimu alilinunua kwa kimo cha fedha kwa wana wa Emmor, huko Sukem. Bassi wakati wa ile ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu ulipokuwa unakaribia, wale watu wakazidi na kuongezeka sana huko Misri, mpaka mfalme mwingine akaondoka, asiyemfahamu Yusuf. Huyo akawafanyia hila baba zetu, na kuwatenda mabaya baba zetu, akiwaamuru watupe watoto wao wachanga, illi wasiishi. Wakati huo akazaliwa Musa, nae alikuwa mzuri sana, akalelewa muda wa miezi mitatu katika nyumba ya baba yake. Hatta alipotupwa, binti Farao akamtwaa, akamlea awe kama mwana wake. Musa akafundishwa hekima yote ya Misri, akawa hodari wa maneno na matendo. Umri wake ulipopata kama miaka arubaini akaazimu moyoni kwenda kuwatazama ndugu zake wana wa Israeli. Akamwona mmoja akidhulumiwa, akamhami, akamlipia kisasi yule aliyekuwa akionewa, akampiga Mmisri. Alidhani kwamba ndugu zake watafahamu ya kuwa Mungu anawapa wokofu kwa mkono wake, lakini hawakufahamu. Siku ya pili yake akawatokea walipokuwa wakishindana, akataka kuwapatanisha, akisema, Enyi bwana zangu, ninyi m ndugu: Mbona mnadhulumiana? Lakini yeye aliyemdhulumu mwenziwe akamsukumia mbali, akisema, Ni nani aliyekuweka kuwa mkuu wetu, na mwamuzi wetu? Je! wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri jana? Musa akakimbia kwa neno hilo, akakaa hali ya mgeni katika inchi ya Madiani, akazaa wana wawili huko. Hatta miaka arubaini ilipotimia, malaika wa Bwana akamtokea katika jangwa la mlima Sinai katika mwali wa moto, kijitini. Musa alipouona, akastaajabia maono yale, na alipokaribia illi atazame, sauti ya Bwana ikamjia, Mimi ni Mungu wa baba zako, Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaak, na Mungu wa Yakobo. Musa akatetemeka, asithubutu kutazama. Bwana akamwambia, Vua viatu vyako, kwa maana mahali hapa unaposimama ni inchi takatifu. Yakini nimeona mateso ya watu wangu waliomo Misri, nimesikia kuugua kwao, nimeshuka niwatoe. Bassi sasa, nitakutuma hatta Misri. Musa huyo waliyemkataa, wakisema, Ni nani aliyekuweka kuwa mkuu na mwamuzi? ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa mkuu na mkombozi, kwa mkono wa yule malaika aliyemtokea katika kile kijiti. Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika inchi ya Misri, na katika bahari ya Sham, na katika jangwa muda wa miaka arubaini. Musa huyo ndiye aliyewaambia wana wa Israeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii katika ndugu zenu, kama mimi: mtamsikia huyo. Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema nae katika mlima Sinai, tena pamoja na baba zetu: ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi. Mtu huyo baba zetu hawakutaka kumtii, bali wakamsukumia mbali, na kwa mioyo yao wakarudi Misri, wakamwambia Haruni, Tufanyie miungu, watakaotutangulia: maana huyo Musa, aliyetutoa katika inchi ya Misri, hatujui lililompata. Wakafanya ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa sanamu ile, wakafurahia kazi ya mikono yao. Bassi Mungu akaghairi, akawaacha, wakaliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii, Je! mlinitolea dhabihu na sadaka Miaka arubaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli? Nanyi mlichukua khema ya Molok, Na nyota za mungu wenu Refan, Sanamu mlizozifanya illi kuziabudu: Nami nitawabamisha mwende mbali hatta Babel. Ile khema ya shahada ilikuwa pamoja na baba zetu jangwani, kama alivyoagiza yeye aliyesema na Musa, ya kwamba aifanye sawa sawa na mfano ule aliouona; ambayo baba zetu waliipokea; wakaiingiza pamoja na Yoshua katika milki ya mataifa wale, ambao Mungu aliwafukuza mbele ya baba zetu, mpaka siku za Daud: aliyepata kibali mbele ya Mungu, nae aliomba ampatie Mungu wa Yakobo maskani. Lakini Sulemani alimjengea nyumba. Illakini yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizofanyika kwa mikono, kama vile asemavyo nabii: Mbingu ni kiti changu cha enzi, Na inchi ni mahali pa kutia miguu yangu: Ni nyumba gani mtakayonijengea? asema Bwana: Au ni mahali gani nitakapostarebe? Sio mkono wangu uliofanya haya yote? Enyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya na ninyi vivyo hivyo. Ni yupi katika manabii ambae baba zenu hawakumwudhi? nao waliwaua wale waliotabiri khabari za kuja kwake yule mwenye haki; ambae ninyi sasa mmemsaliti mkamwua; ninyi mlioipokea torati kwa khuduma ya malaika wala hamkuishika. Bassi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo, wakamsagia meno. Nae akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama mkono wa kuume wa Mungu. Akasema, Tazama! naona mbingu zimefunuliwa, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa Mungu. Wakapiga kelele kwa sauti kuu, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja, wakamtoa nje ya mji, wakampiga mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyekwitwa Saul. Wakampiga mawe Stefano, nae akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu. Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. NA Saul alikuwa akiona vema auawe. Siku ile kukatukia adha nyingi juu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemi: wote wakatawanyika katika inchi ya Yahudi na Samaria, illa mitume. Watu watawa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo mengi. Saul akaliharibu kanisa, akiingia killa nyumba, na kuwabarura wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani. Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilikhubiri neno. Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawakhubiri Kristo. Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yote yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuiona miujiza aliyokuwa akiifanya. Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu: na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa. Ikawa furaha kubwa kafika mji ule. Na mtu mmoja, jina lake Simon, alikuwa amefanya uchawi katika mji ule tokeapo, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa. Wote wakamsikiliza kwa muda mwingi, tangu mdogo hatta mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni nweza wa Mungu, ule mkuu. Wakamwangalia, kwa maana muda mwingi amewashangaza kwa uchawi wake. Lakini walimpomwamini Filipo, akizikhubiri khabari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. Na yeye Simon mwenyewe aliamini akabatizwa, akakaa na Filipo: akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka. Na mitume walioko Yerusalemi, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana. Wakashuka, wakawaombea wrampokee Roho Mtakatifu: kwa maana bado hajawashukia hatta mmoja wao, illa wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. Wakaweka mikono yao juu yao, nao wakapokea Roho Mtakatifu. Hatta Simon alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekwa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha, akisema, Nipe na mimi uwezo huu, illi killa mtu nitakaemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu. Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhani ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele ya Mungu. Bassi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana illi, kama yumkini, usamebewe fikara lui ya moyo wako. Kwa maana nakuona una nchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu. Simon akajibu, akasema, Niombeeni ninyi kwa Mungu, yasinifikilie mambo haya uliyosema. Nao walipokwisha kushuhudia na kulikhubiri neno la Bwana wakarudi Yerusalemi wakaikhubiri Injili katika vijiji vingi vya Wasamaria. Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka uende upande wa kusini hatta njia ile itelemkayo kutoka Yemsalemi kwenda Gaza; nayo ni jangwa. Akaondoka, akaenda; marra akamwona mtu wa Ethiopia, tawashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkiya wa Ethiopia, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; nae amekwenda Yerusalemi kuabudu, akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari bili, ukashikamane nalo. Bassi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya: akanena, Je, yamekuelea haya unayosoma? Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiougoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja nae. Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili: Alichukuliwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana kondoo asivyolia mbele yake amkatae manyoya, Vivyo hivyo yeve nae hafunui kinywa chake. Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakaeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika inchi. Yule tawashi akamjibu Filipo, Nakuomba, nabii huyu asema maneno haya kwa khabari ya nani; ni khabari zake mwenyewe an khabari za mtu mwingine? Filipo akafunua kinywa chake na akilianzia andiko hili, akamkhubiri khabari njema za Yesu. Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji: yule tawashi akasema, Yanizuia nini nisibatizwe? Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, ni halali. Akajibu, akanena, Namwamini Mwana wa Mungu kuwa ndiye Yesu Kristo. Akaamuru lile gari lisimame: wakatelemka wote wawili majini. Filipo na yule tawashi: akambatiza. Kiisha, walipotoka majini, Roho ya Bwana ikamnyakua Filipo, yule tawashi asimwone tena; maana alikwenda zake akifurahi: Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akakhubiri Injili katika miji yote, hatta akafika Kaisaria. LAKINI Saul, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea kuhani mkuu, akataka ampe khati za kwenda Dameski zilizoandikwa kwa masunagogi, illi akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemi. Hatta alipokuwa akisafiri akawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Saul, Saul, mbona wanifukuza? Akasema, U nani Bwana? Akasema, Mimi ndimi Yesu unaeniudhi wewe. Lakini simama, uingie mjini, utaambiwa yatakayokupasa kutenda. Na watu waliosafiri pamoja nae wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu. Saul akaondoka katika inchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu: wakamshika mkono wakamleta hatta Dameski. Akawa siku tatu haoni, wala hali, wala hanywi. Bassi palikuwapo mwanafunzi Dameski, jina lake Anania. Bwana akamwambia katika njozi, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana. Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Sawa, ukatafute ndani ya nyumba ya Yuda mtu jina lake Saul, wa Tarso: maana yuko anasali: nae amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, akiweka mikono juu yake, apate kuona tena. Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia khabari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemi: hatta hapa ana mamlaka kwa makuhani wakuu awafunge wote wakuitiao Jina lako. Lakini Bwana akamwambia, Shika njia; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. Maana nitamwonyesba mambo mengi makuu yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu. Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Saul, Bwana amenipeleka, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. Marra yakaanguka machoni pake kama magamba, akapata kuona akasimama, akabatizwa; akala chakula, akapata nguvu. Akawa huko siku kadhawakadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski. Marra akamkhubiri Yesu katika masunagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu. Na wote waliosikia wakashangaa, wakasema, Siye huyu aliyewateka walioliita Jina hili Yerusalemi? Na hapa amekuja kusudi hili, awafunge na kuwapeleka kwa makuhani wakuu? Saul akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithubutisha ya kuwa huyu udiye Kristo. Hatta siku nyingi zilipopita, Wayahudi wakafanya shauri illi wamwue: lakini hila yao ikajulikana na Saul. Wakamvizia malangoni mchana na usiku wapate kumwua. Wanafunzi wakamtwaa usiku wakamshusha ukutani, wakimtelemsha katika kapu. Na Saul alipofika Yerusalemi, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi. Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema nae, na jinsi alivyokhubiri pasipo khofu katika Dameski kwa jina lake Yesu. Nae akawa pamoja nao katika Yerusalemi akiingia na kutoka. Akaneua kwa jina lake Yesu pasipo khofu, akinena na kushindana na Wahelenisti. Nao wakajaribu kumwua. Lakini ndugu walipopata khabari wakamchukua hatta Kaisaria wakampeleka Tarso. Bassi makanisa wakapata raha katika Yahudi yote na Galilaya na Samaria, wakajengewa, wakiendelea katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu. Hatta Petro alipokuwa akizungukazunguka pande zote akawatelemkia watakatifu waliokaa Ludda. Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea mtu huyo amelala kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza. Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya: ondoka, ukatandike kitanda chako. Marra akaondoka. Na watu wote waliokaa Ludda na Saron wakamwona, wakamgeukia Bwana. Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yoppa, jina lake Tabitha, (tafsiri yake ni paa:) mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. Ikawa siku zile akaugua, akafa: hatta walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani. Na kwa kuwa Ludda ulikuwa karibu na Yoppa, nao wamesikia ya kwamha Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi asikawie kuja kwao. Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika wakampeleka juu orofani: wajane wote wakasimama karibu nae, wakilia na kuniwonyesha zile kanzu na nguo alizozifanya Paa wakati ule alipokuwa pamoja nao. Petro akawatoa wote, akapiga magoti, akaomba, akaielekea mayiti, akanena, Tabitha, ondoka. Nae akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi. Akampa mkono, akamwinua; hatta akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, yu hayi. Ikajulikana katika Yoppa, katika mji mzima, watu wengi wakamwamini Bwana. Hatta Petro akakaa siku kadha wa kadha huko Yoppa, nyumbani mwa mtu mmoja, jina lake Simon, mtengenezaji wa ngozi. PALIKUWA na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitaliano, mtu nitawa, mcha Mungu, yeye na nyumba yake yote, nae alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu siku zote. Akaona katika njozi wazi wazi, panapo saa tissa ya mchana, malaika wa Mungu akimjia na kumwambia, Kornelio! Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Maombi yako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu. Bassi, peleka watu Yoppa, ukamwite Simon, aitwae Petro: Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simon, mtengenezaji wa ngozi; nyumba yake iko pwani; atakuambia yakupasayo kutenda. Na yule malaika aliyesema nae akiisha kuondoka, Kornelio akaita watumishi wawili wa nyumba yake, na askari mmoja, mtu mtawa, katika wale waliomkhudumia daima: na alipokwisha kuwaeleza mambo yote akawatuma kwenda Yoppa. Hatta siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, panapo saa sita ya mchana: akaingiwa na njaa nyingi, akataka kula: lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia, akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikimshukia kama nguo kubwa, kinatelemshwa kwa pembe zake nne hatta inchi. Ndani yake aina zote za nyama zenye miguu mine, na nyama za mwituni, nazo zitambaazo, na ndege za anga. Sauti ikamjia, Ondoka, Petro, ukachinje ule. Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijala kamwe kitu kilicho kichafu au najis. Sauti ikamjia marra ya pili, Kilichotakaswa na Mungu, usikiite najis. Jambo hili likatendeka marra tatu: kiisha kile chombo kikapokewa tena mbinguni. Hatta Petro alipokuwa akiona mashaka ndani ya nafsi yake, maana yake nini maono hayo aliyoyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, wakiislia kuiulizia nyumba ya Simon, wakasimama mbele ya mlango, wakaita, wakauliza kwamba Simon aitwae Petro anakaa humo. Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutaka. Ondoka ushuke ufuatane nao, usione mashaka, kwa maana ni mimi niliyewaleta. Petro akawashukia wale watu waliotumwa kwake na Kornelio, akanena, Mimi ndiye mnaemtaka. Mmekuja kwa sababu gani? Wakasema, Kornelio akida, mtu mwenye haki, mcha Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, apate kusikiliza maneno yako. Akasema, Ingieni; akawakaribisha. Hatta siku ya pili, Petro akatoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu waliokaa Yoppa wakafuatana nae. Hatta siku ya pili yake wakaingia Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwangojea, amekusanya jamaa zake na rafiki zake. Petro alipokuwa akiingia, Kornelio akatoka amlaki akamwangukia miguu, akamsujudia. Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni mwana Adamu. Na katika kusema nae akaingia, akaona watu wengi wamekusanyika. Akawaambia, Mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi aongee na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, hikini Mungu amenionya, nisimwite mtu awae yote mchafu wala najis. Kwa sababu hiyo naiikuja nilipoitwa nisikatae; hassi nauliza, ni neno gani mliloniitia? Kornelio akanena, Leo ni siku ya nne tangu nilijiokuwa nikifunga hatta saa hii: na saa tissa nalikuwa nikisali nyumbani mwangu: kumbe! mtu amesimama mbele yangu, mwenye nguo zingʼaazo, akasema, Kornelio, maombi yako yamesikiwa, na sadaka zako zinakumbukwa mbele za Mungu. Bassi, tuma watu kwenda Yoppa, ukamwite Simon aitwae Petro, aje hapa; anakaa katika nyumha ya Simon, mtengenezaji wa ngozi, karibu ya pwani: nae akija atasema nawe. Marra nikatuma watu kwako, nawe umefanya vyema kuja. Bassi sasa sisi sote tupo hapa mbele za Mungu, tupate kuyasikiliza maneno yote uliyoamriwa na Mungu. Petro akafumhua kiuywa chake, akasema, Hakika nimekwisha kutambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; bali katika killa taifa mtu amchae na kutenda haki hukuhaliwa nae. Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli, akikhubiri amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote), jambo lile mmelijua, lililoenea katika Yahudi yote likianzia Galilaya, haada ya ubatizo alioukhubiri Yohana; khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae. Nasi tu mashahidi ya mambo yote aliyoyatenda katika inchi ya Wayahudi na katika Yerusalemi; ambae walimwua wakamtundika mtini. Huyu Mungu alimfufua siku ya talu, akamjalia kudhilurika, si kwa watu wote, bali kwa mashahidi waliokuwa wamekwisha kuchaguliwa na Mungu, ndio sisi, tuliokula na kunywa pamoja nae baada ya kufufuka kwake. Akatuagiza tuwakhubiri watu na kushuhudu ya kuwa huyu udiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa hayi na wafu. Huyu manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake killa amwaminiye atapewa ondoleo la dhambi. Petro alipokuwa akisema maueno haya Roho Mtakatifu akawashukia wote waliosikia maneno yake. Na wale waliotahiriwa walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu mataifa nao wameshukiwa kipaji cha Roho Mtakatifu. Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, wakimwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu, Aweza mtu kuwakataza hawa maji, wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi? Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha. BASSI mitume na ndugu waliokuwa katika Yahudi wakapata khabari ya kwamba watu wa mataifa nao wamelipokea neno la Bwana. Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemi, wale walio wa Tohara wakashindana nae, wakisema, Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao. Petro akaanza kuwaeleza kwa taratibu, akasema, Nalikuwa katika mji wa Yoppa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kama nguo kubwa kikishuka, kinashushwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia. Nikaitazama sana, nikifikiri, nikaona nyama za inchi zenye miguu mine, Ua nyama za mwituni, nazo zitambaazo, na ndege za anga. Nikasikia sauti ikiniambia, Ondoka, Petro, ukachinje ule. Nikasema, Hasha, Bwana, kwa maana kitu kilicho kichafu au kilicho najis hakijaingia kinywani mwangu. Sauti ikanijibu marra ya pili kutoka mbinguni, Alivyovitakasa Mungu, usivinene wewe najis. Jambo hili likatendeka marra tatu, kiisha vitu vyote vikavutwa juu tena mbinguni. Kumbe! marra hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba niliyokuwamo, waliotumwa kwangu kutoka Kaisaria. Roho akaniambia nifuatane nao, nisione mashaka. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule: akatueleza jinsi alivyomwona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kumwambia, Tuma watu kwenda Yoppa ukamwite Simon, aitwae Petro atakaekuambia maneno ambayo utaokolewa nayo, wewe na nyumba yako yote. Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo. Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu. Bassi ikiwa Mwenyiezi Mungu amewapa wao karama ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu? Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Bassi, Mungu amewajalia mataifa nao toba liletalo uzima. Bassi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile shidda iliyotukia kwa khabari ya Stefano, wakasafiri hatta Foiniki na Kupro na Antiokia, wasilikhubiri lile neno illa kwa Wayahudi peke yao. Baadhi ya hao walikuwa watu wa Kupro na Kurene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wahelenisti, wakakhubiri khabari njema za Bwana Yesu. Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao: watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana. Khabari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwa katika Yerusalemi: wakaintuma Barnaba, aende hatta Antiokia. Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo. Maana alikuwa mtu mwema, amejaa Roho Mtakatifu na imani: watu wengi wakajitia upande wa Bwana. Barnabi tikatoka akaenda Tarso kumtafuta Saul: hatta alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hajio Antiokia. Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yemsalemi hatta Antiokia. Akasimama mmojawapo wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa nweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima; nayo ikatukia katika siku za Klaudio Kaisari. Na wale wanafunzi, killa mtu kwa kadiri alivyofanikiwa wakaazimu kupeleka msaada kwa ndugu zao waliokaa Yahudi. Wakafanya hivyo, wakawapelekea wazee kwa mikono ya Barnaha na Saul. PANAPO majira yaleytile Herode mfalme tw akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa Kanisa. Akamwua Yakobo ndugu wa Yohana kwa upauga. Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamtwaa na Petro. Siku hizo ndizo siku za mikate isiyochachwa. Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa askari wanewane, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa mbele ya watu. Bassi Petro akalindwa gerezani, sala zikawa zinafanyika kwa juhudi sana na Kanisa mbele za Mungu kwa ajili yake. Hatta wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku uleule. Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili: walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza. Marra malaika wa Bwana akasimama karibu nae, nuru ikamulika chumbani mle, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo ikamwanguka. Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu: akafanya hivyo. Akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate. Akatoka, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni khabari ya kweli iliyofanyika na malaika; bali alidhani anaona njozi. Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hatta mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia. Wakatoka, wakapita katika njia moja; marra malaika akamwacha. Hatta Petro alipofahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na kutazamia kwa taifa la Wayahudi. Na alipokuwa akifikiri haya akafika nyumbani kwa Mariamu, mama yake Yohana, ambae jina lake la pili ni Marko; na wafu wengi wamekutana wakiomba. Na Petro alipobisha kilango cha lango, kijakazi, jina lake Rhoda, akaja kusikiliza. Alipoitambua sauti ya Petro, hakulifungua lango kwa furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani akawaambia kwamba Petro anasimama mbele ya lango. Wakamwambia, Una wazimu. Lakini yeye akakaza sana, akasema ya kwamba ndivyo bivyo. Wakanena, Ni malaika wake. Petro akafuliza kugonga; hatta walipokwislia kumfungulia wakamwona, wakastaajabu. Nae akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Enendeni, mkampashe Yakobo na ndugu zetu khabari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine. Hatta kulipopambazuka askari wakaingiwa na fadhaa nyingi, amekuwaje Petro. Na Herode alipomtafuta, asimwone, akawauliza walinzi, akaamuru wanawe. Nae akatelemka kutoka Yahudi kwenda Kaisaria, akakaa huko. Nae Herode aliwakasirikia sana watu wa Tʼuro na Sidon: wakamwendea kwa nia moja, na wakiislia kufanya urafiki na Blasto, mwenye kukitunza chumba cha mfalme cha kulalia, wakataka amani; kwa maana inchi yao ilipata riziki kwa inchi ya mfalme. Bassi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifaume, akaketi katika kiti cha enzi, akatoa khotuba. Watu wakapiga kelele, wakinena, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwana Adamu. Marra malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu: akaliwa na funza, akatoa roho. Neno la Bwana likazidi na kuenea. Na Barnaba na Saul, walipokwisha kuitimiza khuduma yao, wakarejea kutoka Yerusalemi wakamchukua pamoja nao Yohana aitwae Marko. NA huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, Barnaba na Sumeon aitwae Niger, na Lukio Mkurene, na Manaen aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa Herode mfalme, na Saul. Bassi hawa walipokuwa wakimkhudumia Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Niwekeeni Barnaba na Saul kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo, wakiisha kuomba na kufunga, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao. Bassi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Selukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hatta Kupro. Na walipokuwa katika Salamini wakalikhubiri neno la Bwana katika masunagogi ya Wayahudi, nao walikuwa nae Yohana kuwakhudumia. Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote cha Kupro, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa nwongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu: mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paolo, mtu mwenye akili. Yeye akawaita Barnaba na Saul waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. Lakini Eluma, yule mchawi (maana ndio tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha Imani. Lakini Saul ambae ndiye Paolo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akanena, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa shetani, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? Bassi, angalia, mkono wa Bwana ni juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda kitambo. Marra kiwi kikamwangukia na giza, akazungukazunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini akiyastaajabia mafundisho ya Bwana. Kiisha Paolo na wenziwe wakangʼoa nanga wakasafiri kutoka Pafo, wakafika Perga katika Pamfulia. Yohana akawaacha akarejea Yerusalemi. Lakini wao wakatoka Perga, wakapita kati ya inchi, wakafika Antiokia mji wa Pisidia, wakaingia katika sunagogi siku ya sabato, wakaketi. Kiisha baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa sunagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni. Paolo akasimama, akawtipungia mkono, akanena, Enyi wanme wa Israeli, na ninyi mnaomcha Mungu, sikilizeni. Mungu wa watu hawa Israeli aliwachagua baba zetu, akawatukuza watu, walipokuwa wakikaa kama wageni katika inchi ya Misri, na kwa mkono ulioinuliwa akawatoa, akawaongoza. Na panapo muda wa miaka arubaini akawaruzuku katika jangwa. Na alipokwisha kuwaharibu mataifa saba katika inchi ya Kanaan akawajia inchi yao iwe urithi. Baada ya muda wa miaka aruba mia na khamsini, akawapa waamuzi hatta zamani za nabii Samwil. Khatimae wakaomba kupewa mfalme; Mungu akawapa Saul mwana wa Kish, mtu wa kabila ya Benjamin, kwa muda wa miaka arubaini. Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwmua Daud awe mfalme wao, akamshuhudia, akisema, Nimemwona Daud, mwana wa Yese, mtu nimpendae, atakaefanya mapenzi yangu vote. Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani Yesu, kama alivyoahidi, Yohana alipokuwa amekwisha kuwakhubiri watu wote wa Israeli khabari za ubatizo wa toba, kabla ya kuja kwake. Nae Yohana alipokuwa akimaliza mwendo wake alinena, Mwanidhani mimi kuwa nani? Mimi siye. Lakini, angalieni, anakuja mmoja nyuma yangu ambae mimi sistahili kumlegezea viatu vya miguu yake. Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, nao miongoni mwenu mnaomcha Mungu, kwenu ninyi neno la wokofu huu limepelekwa. Kwa maana wakaao Yerusalemi, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua huyu, wala sauti za manabii wanaosomwa killa sabato, wamezitimiza kwa kumhukumu. Na wasipopata sababu ya kumfisha wakamwomba Pilato auawe. Hatta walipomaliza yote aliyoandikiwa, wakamshusha katika mti, wakamweka kaburini. Lakini Mungu akamfufua: akaonwa siku nyingi nao waliopanda nae kutoka Galilaya hatta Yerusalemi, na hao ndio walio sasa mashahidi wake mbele va watu. Na sisi tunawakhubirieni ahadi ile waliyopewa baba zetu, ya kwamba Mungu ametutimizia sisi watoto wao ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu: kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili, Wewe ndiwe Mwana wangu, mimi leo nimekuzaa. Tena ya kuwa alimfufua, asipate kurudia uharibifu, amenena hivi, Nitakupa wewe mambo matakatifu ya Daud yaliyo amini. Kwa hiyo na penginepo anena, Hutamwachia Mtakatifu wako kuona uharibifu. Kwa maana Daud, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu. Bali huyu aliyefufuliwa na Mungu hakuona uharibifu. Bassi, ibainike kwenu, ndugu, ya kuwa kwa huyu mnakhubiriwa ondoleo la dhambi; na kwa huyu killa amwaminiye huhesabiwa kuwa hana khatiya katika mambo yale asiyoweza kuhesabiwa kuwa hana khatiya kwa torati ya Musa. Angalieni, bassi, isije khabari ile iliyonenwa katika manabii, Tazameni, enyi mnaodharau, kjitaajabuni, katowekeni; kwa kuwa natenda kazi mimi siku zenu, kazi msiyoisadiki kabisa, ijapo mtu akiwasimulia sana. Na walipokuwa wakitoka katika sunagogi la Wayahudi, watu wa mataifa wakawasihi kuwaambia maneno haya sabato ya pili. Sunagogi lilipofumukana, Wayahudi wengi na waongofu watawa wakashikamana na Paolo na Barnaba; nao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu. Hatta sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu. Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayabisha maneno yaliyonenwa na Paolo, wakibisha na kutukana. Paolo na Barnaba wakanena kwa uthabiti wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza: illakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, wala hamjioni nafsi zenu kuwa mmestahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia mataifa. Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya mataifa, Upate kuwa wokofu hatta mwisho wa dunia: Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. Neno la Bwana likaenea katika inchi ile yote. Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watawa na watu wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paolo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao. Nao wakawakungʼutia mavumbi ya miguu yao, wakaenda Ikonio. Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu. IKAWA huko Ikonio wakaingia pamoja katika sunagogi ia Wayahudi, wakanena; hatta jamaa kubwa ya Wayahudi na ya Wayunani wakaamini. Walakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu. Bassi wakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa uthabiti katika Bwana, aliyelishuhudia neno la neema yake, akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao. Lakini jamii ya watu wa mjini wakagawanyikana: bawa walikuwa upande wa Wayahudi, na hawa upande wa Mitume. Hatta palipotokea shambulio la watu wa mataifa na Wayahudi pamoja na wakubwa wao juu yao, kuwatenda jeuri na kuwapiga mawe, bassi, wakapata khabari wakakimbilia miji ya Lukaonia. Lustra na Derbe, na inchi zilizo kando kando: wakakaa huko, wakiikhubiri Injili. Na huko Lustra palikuwa na mtu mmoja, dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mama yake, ambae hajaenda kabisa. Mtu huyo alimsikia Paolo akinena; nae akamkazia macho akaona ya kuwa ana imani ya kuponywa, akanena kwa sauti kuu, Simama kwa miguu yako sawa sawa. Akasimama upesi akaenda. Na makutano walipoona aliyoyafanya Paolo wakapaaza sauti zao, wakisema kwa Kilukaonia, Mungu wametushukia kwa mifano ya wana Adamu. Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paolo, Herme, kwa sababu ndiye aliyetakadamu katika kimena. Kuhani wa Zeu ambae hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ngʼombe na taji za maua hatta malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na makutano. Walakini mitume Barnaba na Paolo, walipopata khabari, wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika makutano, wakipiga kelele, wakisema, Akina hwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wana Adamu hali moja na ninyi; twawakhubiri khabari njema mgenke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hayi, aliyeumba mbingu na inchi na bahari na vitu vyotc vilivyomo: ambae zamani zilizopita aliwaacha mataifa yote waende katika njia zao wenyewe. Illakini hakujiacha hana shahidi kwa kuwa alitenda mema akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwajaza mioyo yenu chakula na furaha. Na kwa maneno haya wakawazuia makutano kwa shidda, wasiwatolee dhabihu. Wayahudi wakalika toka Antiokia na Ikonio, wakawashawishi makutano hatta wakampiga mawe Paolo wakamhurura nje ya mji, wakidhani ya kuwa amekwisha kufa. Lakini wanafunzi walipokuwa wakimzunguka pande zote, akasimama, akaingia ndani ya mji; na siku ya pili yake akatoka, akaenda zake pamoja na Barnaba hatta Derbe. Hatta walipokwisha kuikhubiri Injili katika niji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea hatta Lustra na Ikonio na Antiokia, wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi. Na walipokwisha kuchagua wazee katika killa mji, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka kafika mikono ya Bwana waliyemwamini. Wakapita kati ya Pisidia wakamgia Pamfulia. Na baada ya kukhubiri katika Perga wakatelemka hatta Attalia. Na kutoka huko wakasafiri baharini kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza. Hatta walipolika wakalikutanisha Kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwaruba amewafungulia mataifa mlango wa imani. Wakashinda huko wakati usio mchache, pamoja na wanafunzi. WAKASHUKA wafu waliotoka Yahudi wakawafundisha ndugu ya kama, Msipotahiriwa na kuifuata desturi ya Musa hamwezi kuokoka. Bassi baada ya Paolo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhujiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paolo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemi kwa mitume na wazee kwa khabari ya swali hilo. Bassi, wakisafirishwa na Kanisa, wakapita kati ya inchi ya Foiniki na Samaria, wakitangaza khabari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana. Walipofika Yerusalemi wakakaribishwa na Kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao. Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika Torati ya Musa. Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo. Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwetu mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini. Na Mungu, ajuae mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vilevile kama alivyotupa sisi; wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani. Bassi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka nira juu ya shingo za wanafunzi, ambayo baba zetu na sisi hatukuweza kuichukua. Bali twaamini kwamba kwa neema ya Bwana Yesu tutaokoka kama wao. Bassi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paolo wakiwapasha khabari za ishara na maajabu ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika mataifa. Na bao walipokwisha kunyamaza Yakobo akajibu, akinena, Ndugu zangu, nisikilizeni, Simeon ametueleza jinsi Mungu alivyowaangalia mataifa illi achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake. Na maneno ya manabii yapatana na bayo, kama ilivyoandikwa: Baada ya mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena nyumba ya Daud iliyoanguka. Nitajenga tena maanguko yake, Na nitaisimamisha; Illi wana Adamu waliosalia wamtafute Bwana, Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao: Asema Bwana afanyae mambo haya yote. Kazi zake zote zimejulika na Mungu tangu mwanzo wa ulimwengu. Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi: Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa: balituwaandikie wajiepushe na unajisi wa sanamu na asharati na nyama zilizosongwa na damu. Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wakhubirio mambo yake; katika killa mji husomwa killa siku katika masunagogi. Bassi ikawapendeza mitume na wazee na Kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paolo na Barnaba: nao ni hawa, Yuda aliyekwitwa Barsaba, na Sila, watu wakuu katika ndugu. Wakaandika hivi kwa mikono yao, Mitume na wazee na ndugu, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shami na Kilikia, walio wa mataifa, salamu. Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbueni kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, wakisema, ya kuwa hamna buddi kutahiriwa na kuishika Torati, ambao sisi hatukuwapa agizo lo lote; bassi tumeona vema tukiwa tumepatana kwa moyo mmoja, kuwachagua watu na kuwapeleka kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paolo, watu waliokhatirisha maisha zao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Bassi tumewatuma Yuda na Sila, watakaowaambieni maneno yayo hayo kwa vinywa vyao. Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo illa hayo yaliyo faradhi, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongwa, na asharati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Salamu. Hatta hao wakiisha kupewa rukhusa wakatelemkia Antiokia; na baada ya kuwakusanya jamii yote wakawapa ule waraka. Wakausoma, wakafurahi kwa ajili ya faraja ile. Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathubutisha. Nao wakiisha kukaa huko muda kitambo, wakarukhusiwa na ndugu waende kwa amani kwao waliowatuma. Lakini Sila akaona vema kukaa huko. Na Paolo na Barnaba wakakaa huko Antiokia, wakifundisiia na kulikhubiri neno la Bwana, pamoja na watu wengine wengi. Baada ya siku kadha wa kadha Paolo akamwambia Barnaba, Haya! turejee sasa tukawaangalie ndugu katika killa mji tulipolikhubiri neno la Bwana, wa hali gani. Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyekwitwa Marko pamoja nao. Bali Paolo hakuona vema kumchukua huyo aliyewaacha huko Pamfulia, asiende nao kutenda ile kazi. Bassi palitokea maneno makali beina yao hatta wakatengana: Barnaba akamchukua Marko akatweka kwenda Kupro. Paolo akamchagua Sila akaondoka, akiombewa na wale ndugu, apewe neema ya Mungu. Akapita katika Shami na Kilikia akawatia moyo makanisa. AKAFIKA Derbe na Lustra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke mmoja Myahudi aliyeamini: lakini baba yake alikuwa Myunani. Mtu huyo alishuhudiwa na ndugu waliokaa Lustra na Derbe. Paolo akamtaka huyu afuatane nae, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile: kwa maana wote walijua ya kuwa baba yake ni Myunani. Bassi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, wakawapa zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemi, illi wazishike. Makanisa yakatiwa nguvu kwa imani, hesabu yao ikaongezeka killa siku. Wakapita katika inchi ya Frugia na Galatia, wakakatazwa na Roho Mtakatifu, wasilikhubiri Neno katika Asia. Walipofika kukabili Musia, wakajaribu kwenda Bithunia, lakini Roho ya Yesu hakuwapa rukhusa, wakapita Musia wakatelemkia Troa. Paolo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi akimwambia, Vuka uje Makedonia utusaidie. Bassi alipokwisha kuona yale maono, marra tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Bwana ametuita tuwakhubiri Injili. Tukangʼoa nanga kutoka Troa, tukafika Samothraki kwa tanga moja. Siku ya pili tukafika Neapoli na kutoka hapo tukafika Filippi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika wilaya ile, nayo ni Kolonia ya Kirumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha. Hatta siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, tukidhani ya kuwa hapo pana mahali pii kuomba; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. Mwanamke mnioja, jina lake Ludia, mwenye kuuza rangi ya zambarao, mwenyeji wa Thuatira, mcha Mungu, akatusikiliza. Moyo wake huyu ukafunguliwa na Bwana, ayaangalie mineno yaliyonenwa na Paolo. Hatta alipokwisha kumbatiza, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae; akatushurutisha. Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kuombea, kijakazi kimoja aliyekuwa na pepo ya Puthoni akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kutabiri. Akamfuata Paolo na sisi, akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kutukhubiri njia ya wokofu. Akawa akifanya hayo siku nyingi. Lakini Paolo akakasirika akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile. Bassi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paolo na Sila, wakawakokota hatta sokoni mbele ya wakuu wa mji; wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanataharakisha mji wetu, nao ni Wayahudi. Tena wanatangaza khabari ya desturi zisizo halali kwetu tuzipokee wala kuzifuata, kwa kuwa sisi tu Warumi. Makutano wote wakaondoka wakawaendea, Makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora. Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana. Nae akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. Lakini panapo usiku wa manane Paolo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakisikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la inchi, hatta misingi ya gereza ikatikisika, na marra hiyo milango ikafunguka, vifungo vya watu wote vikalegezwa. Yule mlinzi wa gereza akaamka, akaona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, akafuta upanga wake, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia. Paolo akapaaza sauti yake kwa uguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa. Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa khofu, akawaangukia miguu Paolo na Sila; kiisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka pamoja na uyumba yako. Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake. Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, akahatizwa, yeye ua watu wote wa nyumbani mwake wakati huohuo. Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu. Kulipopambazuka makadhi wakawatuma wakubwa wa askari wakisema, Waacheni watu wale waende zao. Yule mlinzi wa gereza akamwarifu Paolo maneno haya ya kama, Makadhi wametuma watu kuwafungulieni! bassi, sasa tokeni nje, enendeni zenu kwa amani. Paolo akawaambia, Wametupiga mbele ya watu wote bila kutuhukumu, na sisi tu Warumi, teua wametutupa gerezani; na sasa wanataka kututoa kwa siri? la, sivyo, na waje wenyewe wakatutoe. Wakubwa wa askari wakawapasha makadhi khabari za maneno haya: nao wakaogopa, waliposikia ya kwamba ni Warumi. Wakaja wakawasihi: na walipokwisha kuwatoa nje, wakawaomba watoke katika mji ule. Nao wakatoka gerezani wakaingia nyumbani mwa Ludia; na walipokwisha kuwaona ndugu wakawafariji, wakaenda zao. WAKIISHA kupita kati ya Amfipoli na Apollonia wakafika Thessalonika, na hapo palikuwa na sunagogi la Wayahudi. Na Paolo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahujiana nao kwa maneno yii maandiko sabato tatu, akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kama, Yesu huyu ninaewapasha ninyi khabari zake ndiye Kristo. Wengine wakaamini, wakasuhubiana na Paolo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye eheo si wachache. Na Wayahudi wasioamini wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yason wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji; na wasipowakuta, wakamkokota Yason na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika na huku, Yason akawakaribisha; na hawa wote wanatenda mambo yaliyo kinyume cha amri za Kaisari, wakisema ya kwamba yupo mfalme mwingine, aitwae Yesu. Wakautabarakisha nle mkutano na wakubwa wa mji walipoyasikia hayo. Nao walipokwisha kumtoza dhamana Yason na wenziwe wakawaacha waende zao. Marra ndugu wakawapeleka Paolo na Sila usiku hatta Beroya. Walipofika huko wakaingia katika sunagogi la Wayahudi. Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thessaloniki, kwa kuwa walilipokea Neno kwa uelekefu wa moyo, wakayachunguza maandiko, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. Wafu wengi wakaamini miongoni mwao, nao wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache. Lakini Wayahudi wa Thessaloniki walipopata khabari ya kwamba Neno la Mungu linakhubiriwa na Paolo katika Beroya, wakaenda huko wakawachafua makutano. Marra hiyo wale ndugu wakampeleka Paolo aende zake kana kwamba anakwenda njia ya pwani; bali Sila na Timotheo wakashinda huko. Nao walimsindikiza Paolo wakampeleka hatta Athene; na wakiisha kupokea maagizo kuwapelekea Sila na Timotheo, ya kama wasikawie kumfuata, wakaenda zao. Paolo alipokuwa akiwangojea katika Athene akaona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake. Bassi katika sunagogi akahujiana na Wayahudi nao waliomcha Mungu, na killa siku sokoni na wale waliokutana nae. Na baadhi ya Waepikurio na Wastoiko, matilosofo, wakakutana nae. Wengine wakasema, Mtu huyu mwenye maneno mengi anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza khabari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akikhubiri khabari za Yesu na ufufuo. Wakamshika, wakamchukua hatta Areopago, wakisema, Je, twaweza kujua maana ya elimu hii mpya inenwayo nawe? Kwa maana unaleta mambo mageni masikioni mwetu, tutapenda kujua, bassi, maana ya mambo haya. Kwa maana Waathene na wageni waliokaa huko walikuwa hawana faragha kwa neno lo lote illa kutoa khabari na kusikiliza khabari za jambo jipya. Paolo akasimaina katikati ya Areopago, tikasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini. Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona maabudu yenu, naliona madhliahu iliyoandikwa maneno haya, Kwa Mungu yule asiyejulikana. Bassi mimi nawakhubirini khabari zake yeye ambae ninyi mnamwabudu hila kumjua. Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na inchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono: wala hatumikiwi kwa mikono ya wana Adamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anaewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote. Nae alifanya killa taifa ya wana Adamu kuwa wa damu moja, wakae juu ya uso wa inchi yote, akiisha kuwaandikia nyakati alizowaamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; illi wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasapapasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na killa mmoja wenu. Kwa maana ndani yake tunaishi, tunakwenda, tuna uhayi wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi, alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake. Bassi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wana Adamu. Bassi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hauoni; bali sasa anawakhuhiri watu wote wa killa mahali watubu. Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa ujumbe wa mtu yule aliyemchagua; nae amewapa watu wote bayana ya mambo haya kwa kumfufua katika wafu. Bassi waliposikia khabari za ufufuo wa wafu wengine wakadhihaki: wengine wakasema, Tutakusikiliza tena khabari hiyo. Bassi Paolo akaondoka akawaacha. Baadhi ya wanaume wakashikamana nae, wakaamini; katika hao alikuwamo Dionuso, Mwareopago, na mwanamke mmoja jina lake Damari, na watu wengine pamoja na hao. BAADA ya mambo haya Paolo akatoka Athene akalika Korintho. Akamwona Myahudi mmoja, jina lake Akula, mzalia wa Ponto; nae amekuja kutoka inchi ya italia siku za karibu, pamoja na Priskilla mkewe, kwa sababu Klaudio amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi. Akafika kwao; na kwa kuwa kazi yake na kazi yao ni moja, akakaa kwao, akafanya kazi yake, kwa maana walikuwa mafundi wa kufanyiza khema. Akatoa hoja zake katika sunagogi killa sabato akawavuta Wayahudi na Wayunani waamini. Hatta Sila na Timotheo walipotelemka kutoka Makedonia, Paolo akashurutishwa rohoni mwake, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo. Walipopingamana nae na kutukana, akakungʼuta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu: mimi ni safi: langu sasa nitakwenda kwa watu wa mataifa. Akaondoka huko akaingia katika nyumba ya mtu mmoja jina lake Yusto, mcha Mungu, ambae nyumba yake ilikuwa mpaka mmoja na sunagogi. Na Krispo, mkuu wa sunagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi wakasikia, wakaamini, wakabatizwa. Bwana akamwambia Paolo kwa njozi nsiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze, kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakaekushambulia illi kukudhuru; kwa matina mimi nina watu wengi katika mji huu. Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akawafundisha neno la Mungu. Hatta Gallio alipokuwa Prokonsuli wa Akaya, Wayahudi wakamwendea Paolo kwa nia moja, wakamleta mbele ya kiti cha hukumu, wakisema, Mtu huyu huwavuta watu illi wamwabudu Mungu kinyume cha sharia yetu. Na Paolo alipotaka kufunua kinywa chake, Gallio akawaambia Wayahudi, Kama lingetendeka tendo la dhuluma au la hila mbaya, enyi Wayahudi, ingekuwa haki kuchukuliana nanyi; bali ikiwa ni hoja juu ya maneno na majina na sharia yenu, liangalieni ninyi wenyewe, maana mimi sitaki kuwa mwamuzi wa mambo hayo. Akawafukuza mbele ya kiti cha hukumu. Na Wayunani wote wakamshika Sosthene, mkuu wa sunagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu. Na Gallio hakuyaona mambo hayo kuwa kitu. Paolo akazidi kukaa huko siku nyingi, kiisha akaagana na ndugu akatweka kwenda Shami; na Priskilla na Akula wakaenda pamoja nae, alipokwisha kunyoa kichwa chake katika Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri. Wakalika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sunagogi, akahujiana na Wayahudi. Walipotaka akae wakati mwingi zaidi, hakukubali: bali aliagana nao, akisema. Sina buddi kufanya siku kuu hii inayokuja Yerusalemi: lakini nitarejea kwenu, Mungu akinijalia. Akatweka, akatoka Efeso, na alipokwisha kushuka Kaisaria, akapanda juu, akawasalimu Kanisa, akatelemkia Antiokia. Hatta akiisha kukaa huko siku kadha wa kadha akaondoka, akapita kati ya inchi ya Galatia na Frugia, mji kwa mji, akiwatia moyo wanafunzi. Bassi Myahudi mmoja, jina lake Apollo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akalika Efeso; nae alikuwa hodari wa maandiko. Mtu huyu alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikiwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi khabari za Bwana; nae alijua ubatizo wa Yohana tu. Akaanza kunena bila khofu katika sunagogi: hatta Akula na Priskilla walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi. Na alipotaka kuvuka bahari aende hatta Akaya, ndugu wakamhimiza, wakamwandikia barua kwa wanafunzi wale wamkaribishe; nae alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu. Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akiwaonyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo. IKAWA, Apollo alipokuwa Korintho, Paolo, akiisba kupita kati ya inchi za juu, akafika Efeso: akakutana na wanafunzi kadha wa kadba huko: akawauliza, Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hatta kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, Bassi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. Paolo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakaekuja nyuma yake, yaani Kristo Yesu. Waliposikia baya wakabatizwa katika jina la Bwana Yesu. Na Paolo, alipokwisba kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri. Na jumla yao walipata wanaume thenashara. Akaingia ndani ya sunagogi, akanena kwa ujasiri, akihujiana na watu kwa muda wa miezi mitatu, na kuwavuta waamini mambo ya ufalme wa Mungu. Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; bassi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi nao, akahujiana na watu killa siku katika darasa ya mtu mmoja, jina lake Tyranno. Mambo haya yakaendelea kwa muda wa miaka miwili, hatta wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani. Mungu akafanya kwa mikono ya Paolo miujiza ya kupita kawaida; hatta wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizogusa mwili wake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka. Baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga, nao ni waganga wa pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Twawaapizeni kwa Yesu, yule anaekhubiriwa na Paolo. Nao waliofanya haya walikuwa wana saba wa Skewa, Myahudi, kuhani mkuu. Yule pepo akawajibu, Yesu namjua na Paolo namfahamu, bali ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo akawarukia, akawaweza, akawashinda, hatta wakatoka mbio katika nyumba ile uchi na wamejeruhi. Khabari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, khofu ikawaingia wote, jina la Bwana Yesu likaadhimishwa. Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao. Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote: wakafanya hesabu ya thamani yake wakaona ya kwamba yapata fedha khamsini elfu. Hivyo neno la Mungu likazidi na kushinda kwa nguvu. Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paolo akaazimu rohoni mwake kupita kati ya Makedonia na Akaia aende Yerusalemi, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi. Akatuma watu wawili miongoni mwa wale waliomkhudumia kwenda Makedonia, nao ni Timotheo na Erasto, yeye mwenyewe akakaa katika Asia kitambo. Hatta wakati huo kukatukia ghasia si haba katika khabari ya Njia ile. Kwa maana mtu mmoja, jina lake Demetrio, mfua fedha, kazi yake kufanya vihekalu vya fedha vya Artemi, alikuwa akiwapatia mafundi faida nyingi. Akawakusanya hao, pamoja na wengine wenye kazi ile ile, akasema, Enyi wanaume, mnajua ya kuwa utajiri wetu hutoka katika kazi hii. Tena mnaona na kusikia ya kwamba si katika Efeso tu, bali katika Asia yote pia, Paolo huyo amewaaminisha watu wengi na kuwageuza nia zao, akisema ya kwamba miungu inayofanywa kwa mikono siyo Mungu. Si kwamba kazi hii yetu ina khatari ya kudharauliwa, bassi; bali na hekalu ya mungu mke aliye mkuu kuhesabiwa si kitu, na kuondolewa utukufu wake, ambae Asia yote pia na walimwengu wote humwtihudu. Waliposikia haya wakajaa hasira, wakapiga kelele, wakisema, Artemi wa Waefeso m mkuu. Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia theatro kwa moyo mmoja, wakiisha kuwakamata Gaio na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paolo. Na Paolo alipotaka kuingia kati ya watu, wanafunzi hawakumwacha aingie. Walakini baadhi ya Waasiarko walio rafiki zake wakatuma watu kwake, wakimsihi asijihudhurishe nafsi yake ndani ya theatro. Bassi wengine walikuwa wakilia hivi na wengine hivi: kwa maana ule mkutano umekwisha kuchafukachafuka, na walio wengi hawakuijua sababu ya kukusanyika kwao pamoja. Wakatoa Iskander katika mkutano, Wayahudi wakimweka mbele ya watu. Iskander akawapungia mkono, akitaka kuwapa wale watu majibu. Lakini walipotambua ya kuwa yeye ni Myahudi, wakapiga kelele wote pia kwa sauti moja kwa muda wa saa mbili au karibu, wakilia, Artemi wa Waefeso ni mkuu. Na karani wa mji alipokwisha kuwatuliza watu, akasema, Enyi wanaume wa Efeso, ni mtu gani asiyejua ya kuwa mji wa Efeso ni mtunzaji wa hekalu ya Artemi, mungu mke aliye mkuu, na wa kitu kile kilichoanguka kutoka mbinguni? Bassi kwa kuwa mambo haya hayawezi kukanushwa, imewapaseni kutulia, msifanye neno la haraka haraka. Kwa maana mmewaleta watu hawa, wasiokwiba vitu vya hekalu wala kumtukana mungu mke wetu. Bassi ikiwa Demetrio na mafundi walio pamoja nae wana neno juu ya mtu, baraza ziko, na maliwali wako: na washitakiane. Bali mkitafuta neno lo lote katika mambo mengine, yatatengenezwa katika kusanyiko lililo halali. Kwa maana tuna khatari ya kushtakiwa fitina kwa ajili ya mambo haya ya leo, ikiwa hakuna sababu ambayo kwa ajili yake tutaweza kujiudhuru kwa mkutano huu. Alipokwisba kusema haya akauvunja mkutano. KISHINDO kile kilipokoma, Paolo akawaita wanafunzi akaagana nao, akaondoka aende zake hatta Makedonia. Na, akiisha kupita pande zile na kuwafariji kwa maneno mengi, akafika Uyunani. Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, Wayahudi wakamfanyyia vitimbi, alipotaka kwenda Sham kwa njia ya bahari: bassi akaazimu kurejea kwa ujia ya Makedonia. Watu hawa wakafuataua nae mpaka Asia, Sopater Mberoya, na Aristarko na Sekundo, watu wa Thessalonika, na Gayo mtu wa Derbe, na Tukiko na Trofumo watu wa Asia. Watu hao wamekwisha kutangulia wakatungojea Troa. Sisi tukatweka baada ya siku ya mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filippi, tukawafikia Troa, safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba. Hatta siku ya kwanza ya juma, wanafunzi walipokusanyika illi kumega mkate, Paolo akawakhutubu, akaazimu kusafiri siku ya pili yake, akafuliza maneno yake mpaka nsiku wa manane. Palikiuwa na taa nyingi katika orofa ile walipokuwa wamekusanyika. Kijana mmoja, jina lake Eutuko, ameketi dirishani, akalemewa na usingizi, akaanguka toka orofa ya tatu: akainuliwa amekwisha kufa. Paolo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana uzima wake ungalimo ndani yake. Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi kuongea nao hatta alfajiri, ndipo akaenda zake. Wakamleta yule kijana, yu mzima, wakafarajika faraja kubwa sana. Sisi tukatangulia kwenda merikebuni, tukasafiri hatta Asso, tukikusudia kumpokea Paolo huko: kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe akiazimu kwenda kwa miguu. Alipotufikia huko Asso, tukampokea, tukafika Mitulene. Tukatweka kutoka huko, na siku ya pili tukafika mahali panapokabili Kio: siku ya pili yake tukawasili Samos, tukakaa Trogullio, siku ya pili tukafika Mileto. Kwa sababu Paolo amekusudia kupita Efeso merikebuni, asije akakawia katika Asia: kwa maana alikuwa akifanya haraka, akitaka kuwahi Yerusalemi siku ya Pentekote, kama ikiwezekana. Toka Mileto Faolo akatuma watu kwenda hatta Efeso, akawaita wazee wa Kanisa. Walipofika kwake, akawaambia, Ninyi mnajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu wakati wote, nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na machozi, na majaribu yaliyonipata kwa hila za Wayahudi; ya kuwa sikuficha neno lo lote liwezaio kuwafaeni, bali naliwaonyesha na kuwafundisha kwa wazi na nyumba kwa nyumba, nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani toba iliyo kwa Mungu, na imani iliyo kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Bassi, sasa angalieni, nashika njia kwenda Yerusalemi nimefungwa rohoni, nisijue mambo yatakayonikuta huko; illa ya kuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na mateso yaningoja. Lakini siyahesabu maisha yaugu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na khuduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu. Na sasa mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowakhubirini ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena. Kwa hiyo nawashuhudia wote siku hii ya leo, ya kuwa mimi sina khatiya kwa damu ya mtu aliye yote. Kwa maana sikujiepusha na kuwakhubirini khabari ya shauri lote la Mungu. Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe. Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa za mwitu wakali watakuja kwenu, wasiliachie kundi: tena katika baadhi yenu wataondoka watu, wakisema mapotofu, wawavute wanafunzi kwenda nyuma yao. Kwa biyo kesheni, mkikumbuka kama miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya killa mtu kwa machozi. Bassi, sasa ndugu, nawawekeni katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, kwake yeye awezae kuwajengeni na kuwapeni urithi pamoja nao wote waliotakasika. Sikutamani fedha, wala dhahabu, wala mavazi ya mtu. Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono hii imetumika kwa mahitaji yangu na yao walio pamoja nami. Nimewapeni mfano katika mambo yote ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapaseni kuwasaidia wasio na nguvu, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni kheri kutoa kuliko kupokea. Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote. Wakalia sana wote, wakamwangukia Paolo shingoni, wakambusu, wakihuzunika zaidi kwa sababu ya neno lile alilosema, ya kwamba hawatamtazama uso tena. Wakamsindikiza hatta merikebuni. IKAWA tulipokwisha kujitenga nao ua kutweka, tukafika Koos kwa tanga moja, na siku ya pili yake tukafika Rodo na kutoka huko tukafika Patara, tukapata merikebu itakayovuka hatta Foiniki tukapanda tukatweka. Na tulipoona Kupro tukaiacha upande wa kushoto: tukasafiri hatta Shami tukashuka Turo. Kwa maana huko ndiko marikebu yetu itakakoshusha shehena yake. Tukiisha kuwaona wanafunzi tukakaa huko siku saba, nao wakamwambia Paolo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu asipande kwenda Yerusalemi. Hatta tulipotimiza siku zile tukaondoka tukaenda zetu, na watu wote pamoja na wake zao na watoto wao wakatusindikiza hatta nje ya mji, wakapiga magoti pwani wakaomba: na baada ya kuagana tukapanda merikebuni, nao wakarudi kwao. Hatta tulipomaliza safari yetu kutoka Troa tukafika Ptolemai, tukawasalimu ndugu tukakaa kwao siku moja. Assubuhi yake sisi tulifuatana na Paolo tukatoka, tukafika Kaisaria, tukaingia nyumbani mwa Filipo, Mwinjilisti, aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake. Mtu huyu alikuwa na binti wane, mabikira, waliotabiri. Bassi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Yahudi. Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paolo akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemi watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa mataifa. Bassi tuliposikia haya, sisi na watu wa mahali pale, tukamsihi asipande kwenda Yerusalemi. Paolo akajibu, Mnafanyaje, kulia na kunivnnja moyo? kwa maana mimi, licha ya kufungwa tu, ni tayari hatta kuuawa katika Yerusalemi kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu. Alipokataa shauri letu, tukanyamaza, tukisema. Mapenzi ya Bwana na yatendeke. Baada ya siku zile tukachukua vyombo vyetu tukapanda kwenda Yerusalemi. Baadhi ya wanafunzi wa Kaisaria wakafuatana na sisi, wakachukua na Mnason, mtu wa Kupro, mwanafunzi wa zamani ambae ndiye tutakaekaa kwake. Tulipolika Yerusalemi ndugu wakatukaribisha kwa furaha. Hatta siku ya pili yake Paolo akaingia kwa Yakobo pamoja naswi, na wazee wote walikuwako. Na baada ya kuwasalimu, akawaeleza mambo yote moja moja Mungu aliyotenda katika mataifa kwa khuduma yake. Nao waliposikia wakamhimidi Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona kwamba Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati. Nao wameambiwa khabari zako, ya kwamba unawafundisha Wayahudi wote wakaao katika mataifa kumwacha Musa, ukiwaambia wasiwatahiri watoto wao, wala wasizifuate desturi. Bassi, ni nini? Bila shaka mkutano hauna buddi kukutanika, kwa maana watasikia kwamba umekuja. Bassi fanya neno hili tunalokuambia: Wako kwetu watu wane waliofungwa na nadhiri. Chukua watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia illi wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa khabari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika sharia. Kwa khabari za watu wa mataifa walioamini, tumekwisha kutoa hukumu yetu, wsio wasishike neno linginelo illa kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongwa, na uasharati. Ndipo Paolo akawatwaa wanaume wale, na siku va pili yake akajitakasa nafsi yake pamoja nao, akaingia ndani ya hekalu, akitangaza khabari ya kutimiza siku za utakaso, hatta sadaka itolewe kwa ajili ya kilia mmoja wao. Bassi zile siku saba zilipokuwa karibu kutimizwa, Wayahudi waliotoka Asia wakamwona ndani ya hekalu, wakawataharakisha watu wote, wakamkamata, wakapiga kelele, Enyi wanaume wa Israeli, saidieni. Huyu ndiye mtu yule afundishae watu katika killa mahali kinyume cha taifa letu na torati na pahali hapa. Tena, zaidi ya haya, amewaingiza Wayunani katika hekalu, akapatia najis pahali hapa palakatifu. Kwa maana wamemwona Trofimo Mwefeso, pamoja nae mjini, wakadhani ya kuwa Paolo amemwingiza katika hekalu. Mji wote ukataharuki, watu wakakutanika mbio mbio, wakamkamata Paolo, wakamwokota, wakamtoa hekaluni; marra milango ikafungwa. Na walipokuwa wakitafuta njia ya kumwua, khabari zikamfikilia jemadari wa kikosi ya kwamba mji Yerusalemi umechafuka, mji mzima. Marra hiyo akatwaa askari na maakida, akawashukia mbio. Nao walipomwona jemadari na askari wakaacha kumpiga Paolo. Kiisha jemadari akakaribia, akamshika, akaamuru afungwe kwa minyororo miwili: akauliza, Nani huyu? tena, amefanya nini? Wengine katika makutano wakapiga kelele wakisema hivi, na wengine hivi. Bassi alipokuwa hawezi kupata hakika ya khabari kwa sababu ya zile kelele, akatoa amri aletwe ndani ya ngome. Bassi alipolika darajani ilikuwa yeye kuchukuliwa na askari kwa sababu ya jeuri ya makutano. Maana kundi kubwa la watu wakamfuata, wakipiga kelele, Mwondoe huyu. Na Paolo alipokuwa anaingizwa ndani ya ngome, akamwambia jemadari, Nina rukhusa nikuambie neno? Nae akasema, Je! unajua Kiyunani? Wewe si vnle Mmisri ambae kabla ya siku hizi aliwafitinisha wale watu elfu nne, walioitwa Wauaji, akawaongoza jangwani? Paolo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usio mnyonge. Nakuomba, nipe rukhusa niseme na wenyeji hawa. Bassi, alipompa rukhusa, Paolo akasimama madarajani, akawapunjia mkono wale wenyeji; na ilipokuwa kimya kabisa, akanena nao kwa lugha ya Kiebrania, akisema, ENYI wanaume, ndugu zangu ua baba zangu, nisikilizeni, nikijitetea nafsi yangu mbele yemi sasa. Waliposikia kwamba anasema nao kwa lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza: akanena, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, nikalelewa katika niji huu miguumi pa Gamaliel, nikafundishwa sharia ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa ijtihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi: nikawaudhi watu wa Njia hii kiasi cha kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na wanawake. Kama kuhani mkuu nae anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipewa barua nao kwa ndugu zao, nikaenda Dameski, illi niwalete wale waliokuwa huko hatta Yerusalemi, wamefungwa waadhibiwe. Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhdhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote. Nikaanguka chini, nikasikia sauti ikiniambia, Saul, Saul, Mbona unaniudhi? Nikajibu Wewe nani Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambae wewe unaniudhi. Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, wakaingia khofu, illakini hawakuisikia ile sauti. Nikasema, Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uende hatta Dameski, na huko utaambiwa khabari za mambo vote yaliyoamriwa uyafanye. Na nilipokuwa sioni kwa sababu ya fakhari ya nuru ile, nikaongozwa na mikono yao waliokuwa pamoja nami, nikafika Dameski. Bassi mtu mmoja, Anania, mcha Mungu kwa kuifuata sharia, aliyeshuhudiwa na Wayahudi wote waliokaa huko, akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu, Saul, uone. Nikamwinulia macho yangu saa ile ile. Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua upate kujua mapenzi yake, na kumwona Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake. Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia. Bassi sasa, unakawiliani? Simama ubatizwe ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina la Bwana. Ikawa nilipokwisha kurudi Yerusalemi, nilipokuwa nikisali ndani ya hekalu, nikawa katika hali ya rohoni, nikamwona akiniambia, Hima, toka katika Yerusalemi upesi, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako katika khabari zangu. Nami nikasema, Bwana, wanajua hao ya kuwa mimi nalikuwa nikwafunga wale wanaokuamini na kuwapiga katika masunagogi yao. Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali auawe, nikizitunza nguo zao waliomwua. Nae akaniambia, Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma mbali kwa watu wa mataifa. Wakamsikiliza mpaka neno lile, wakapaaza sauti zao, wakisema, Mwondoe huyu katika inchi, kwa maana haifai aishi. Walipokuwa wakipiga kelele na kutupa mavazi yao na kurusharusha mavumbi juu, yule jemadari akaamuru aletwe ndani ya ngome, akisema aulizwe khabari zake kwa kupigwa, illi ajue sababu hatta wakampigia kelele namna hii. Hatta walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paolo akamwambia akida aliyesimama karibu, Je! ni halali kumpiga mtu Mrumi nae hajahukumiwa bado? Yule akida aliposikia, akaenda akamwarifu yule jemadari, akisema, Unataka kufanya nini? kwa maana mtu huyu ni Mrumi. Jemadari akaja, akamwambia, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndio. Jemadari akajibu, Mimi nalipata wenyeji huu kwa ras-il-mali nyingi. Paolo akasema, Na mimi nalizaliwa katika hali hiyo. Bassi wale waliokuwa tayari kumwuliza wakaondoka wakamwacha. Na yule jemadari nae akaogopa, alipojua ya kuwa ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga. Siku ya pili yake akitaka kujua hakika, ni kwa sababu gani ameshitakiwa na Wayahudi, akamfungua, akawaamuru makuhani wakuu na baraza yote waje. Akamleta Paolo chini, akamweka mbele yao. PAOLO akawakazia macho watu wa baraza, akasema, Ndugu zangu, mimi kwa nia safi kabisa nimeishi mbele za Mungu hatta leo hivi. Kuhani akawaamuru wale waliosimama karibu kumpiga kinywa chake. Ndipo Paolo akamwambia, Mungu atakupiga wewe, ukuta uliopakwa chokaa. Wewe umeketi kunihukumu sawasawa na sharia, nawe unaamuru nipigwe kinyume cha sharia? Wale waliosimama karibu wakasema, Je! unamtukana kuhani mkuu wa Mungu? Paolo akasema, Sikujua, ndugu zangu, ya kuwa yeye ni kuhani mkuu; maana imeandikwa, Usimnenee mabaya mkuu wa watu wako. Paolo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Mafarisayo, na sehemu ya pili Masadukayo, akapaaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo, mwana wa Farisayo: mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu. Alipokwisha kunena hayo palikuwa na fitina beina ya Mafarisayo na Masadukayo, mkutano ukagawanyika. Kwa maana Masadukayo husema ya kwamba hakuna kiyama wala malaika na roho: bali Mafarisayo hukiri yote mawili. Pakawa makelele mengi. Waandishi wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakamtetea, wakisema, Hatuoni uovu wo wote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesema nae tusishindane na Mungu. Ugomvi mkubwa ulipotokea, yule jemadari akachelea Paolo asije akararuliwa nao, akaamuru askari washuke na kumpokonya mikononi mwao, na kumleta ndani ya ngome. Usiku ule Bwana akasimama karibu nae, akasema, Uwe na moyo mkuu, Paolo; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia khabari zangu Yerusalemi, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi. Kulipopambazuka, baadhi ya Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo wakisema. Hatuli wala hatunywi hatta tutakapokwisha kumwua Paolo. Na hao walioapiana hivyo walipata watu arubaini. Nao wakaenda kwa makuhani wakuu na wazee, wakasema, Tumejifunga kwa kiapo, tusionje kitu hatta tutakapomwua Paolo. Bassi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua khabari zake vizuri zaidi; na sisi tu tayari kumwua kabla hajakaribia. Mjomba wake Paolo akasikia khabari za kuotea kwao, akaenda akaingia ndani ya ngome akampasha Paolo khabari. Paolo akamwita akida mmoja, akasema, Mchukue huyu kwa jemadari; maana ana neno la kumwarifu. Bassi akamchukua, akampeleka kwa jemadari, akamwambia, Paolo, yule mfungwa, aliniita akataka nikuletee kijana huyu kwa kuwa ana neno la kukuambia. Yule jemadari akamshika mkono akaenda nae kando, akamwuliza kwa faragha, Una neno gani utakalo kuniarifu? Akasema, Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paolo chini kesho, ukamweke mbele ya baraza, kana kwamba wanataka kupata khabari zake kwa usahihi zaidi. Bassi wewe usikubali; kwa maana watu zaidi ya arubaini wanamwotea, wamejifunga kwa kiapo wasile wala wasinywe hatta watakapomwua; nao sasa wako tayari, wakiitazamia ahadi kwako. Bassi yule jemadari akamwacha kijana aende zake, akimwagiza, Usimwambie mtu awae yote ya kwamba umeniarifu haya. Akaita maakida wawili, akasema, Wekeni tayari askari miateen kwenda Kaisaria, na askari wapanda farasi sabaini, na wenye mikuki miateen, panapo saa tatu ya usiku. Akawaambia kuweka nyama tayari wampandishe Paolo, na kumchukua salama kwa Feliki liwali. Akaandika barua, kwa nanma hii: Klaudio Lusia kwa liwali il aziz Feliki salamu! Mtu huyu alikamatwa na Wayahudi, akawa karibu kuuawa nao, nikaenda pamoja na kikosi cha askari nikamwokoa, nilipopata khabari ya kuwa yeye ni Mrumi. Na nikitaka kuijua sababu hatta wakamshitaki, nikamleta chini nikamweka mbele ya baraza: nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sharia yao, wala hakushitakiwa neno lo lote la kustahili kuuawa wala kufungwa. Hatta nilipopewa khabari kwamba patakuwa na vitimbi juu ya mtu huyu, marra nikampeleka kwako, nikawaagiza na wale walioshitaki, wanene khabari zake mbele yako. Salamu. Bassi, wale askari wakamchukua Paolo kamu walivyoamriwa, wakampeleka hatta Antipatri usiku: hatta assubuhi wakawaacha wale wapanda farasi waende pamoja nae, nao wakarudi zao ngomeni. Na wale walipofika Kaisaria, wakampa liwali ile barua, wakamweka Paolo mbele yake. Nae alipokwislia kuisoma, akawauliza, Mtu huyu ni wa wilaya gani? Alipoarifiwa ya kuwa ni mtu wa Kilikia, akasema, Nitakusikia maneno yako watakapokuja wale waliokushitaki; akaamuru alindwe katika praitorio ya Herode. BAADA ya siku tano, Anania, kuhani mkuu, akatelemka na baadhi ya wazee pamoja nae, na msemi mmoja, Tertullo nao wakamweleza liwali khabari za Paolo. Na alipoitwa Tertullo akaanza kumshitaki, akisema, Kwa kuwa tunapata amani nyingi chini yako, ee Feliki il aziz, na kwa maangalizo yako mambo mabaya yanatengenezwa kwa ajili ya taifa hili, bassi tunayapokea killa wakati na killa mahali, kwa shukrani yote. Lakini nisikuudhi zaidi, nakusihi utusikilize maneno machache kwa fadhili zako. Kwa maana tamemwona mtu huyu mkorofi, muanzishaji wa fitina katika Mayahudi waliomo duniani, tena ni kichwa cha uzushi wa Wanazorayo. Na tena alijaribu kuitia hekalu najis: tukamkamata: tukataka kumhukumu kwa sharia yetu. Lakini Lusia jemadari akafika, akampokonya mikononi mwetu kwa nguvu, akawaamuru wale waliomshitaki waje kwako. Wewe mwenyewe utaweza kumwuliza na kupata khabari ya mambo yale tunayomshitaki sisi. Wayahudi nao wakamshitaki, wakisema ya kuwa ndivyo yalivyo. Na liwali alipompungia mkono illi anene, Paolo akajibu, Kwa kuwa ninajua kama wewe umekuwa mwamuzi wa taifa hili kwa muda wa miaka mingi, najitetea nafsi yangu kwa moyo wa furaha. Maana waweza kujua ya kuwa hazijapita siku zaidi ya thenashara tangu nilipopanda kwenda Yerusalemi illi kuabudu. Watu hawa hawakuniona ndani ya hekalu, nikihujiana na mtu, wala nikifanya fujo katika mkutano, wala katika masunagogi wala ndani ya mji. Wala hawawezi kuyathubutisha mambo haya wanayonishitaki sasa. Illa neno hili naliungama kwako ya kwamba kwa Njia ile ambayo waiita uzushi, ndivyo ninavyomwabudu Mungu wa baba zetu, nikiyaamini yote yanayopatana na torati na yaliyoandikwa katika vyuo vya manabii. Nina tumaini kwa Mungu, na hatta hao nao wanalitazamia, ya kwamba kutakuwa ufufuo wa wafu wenye haki na wasio haki pia. Nami ninajizoeza katika neno hili kuwa na dhamiri isiyo na khatiya mbele ya Mungu na mbele ya watu. Baada ya miaka mingi nalifika niwaletee watu wa taifa langu sadaka na matoleo. Baadhi ya Wayahudi waliotoka Asia wakaniona ndani ya hekalu nikishughulika na mambo haya, nimetakaswa, wala sikuwa pamoja na mkutano wala ghasia. Imewapasa hao kuwapo hapa mbele yako na kunishitaki kama wana neno lo lote juu yangu. Au watu hawa wenyewe na waseme, ni kosa gani waliloliona kwangu niliposimama mbele ya baraza, isipokuwa kwa ajili ya sauti hii moja, nilipolia nikisimama katikati yao, Kwa ajili ya ufufuo wa wafu ninahukumiwa mbele yenu hivi leo. Bassi Feliki, alijiokwisha kusikia haya, aliwaakhirisha, kwa sababu alijua khabari za Njia ile kwa usahihi zaidi, akasema, Lusia jemadari, atakapotelemka nitakata maneno yenu. Akamwamuru yule akida amlinde Paolo; illa awe na nafasi, wala asimkataze mmojawapo wa rafiki zake kumkhudumu au kuja kumtazama. Baada ya siku kadha wa kadha, Feliki akafika pamoja na Drusilla mkewe aliyekuwa Myahudi, akamwita Paolo akamsikiliza khabari za imani ya Kristo. Na Paolo alipokuwa akitoa hoja zake katika khabari ya haki na kiasi na hukumu itakayokuja, Feliki akafanya khofu akajihu, Sasa enenda zako, nami nikipata wasaa nitakuita tena. Tena alitaraja kwamba atapewa fedha na Paolo illi amfungue: kwa hiyo alimwita marra nyingi akaongea nae. Na miaka miwili ilipotimia. Feliki akampokea Porkio Festo atawale badala yake. Na Feliki, akitaka kuwafanyia Wayahudi fadhili, akamwacha Paolo amefungwa. HATTA Festo alipokwisha kuingia katika wilaya yake, baada ya siku tatu akapanda kwenda Yerusalemi kutoka Kaisaria. Kuhani mkuu na Wayahudi wakampasha khabari za Paolo, wakamsihi, na kumwomba awafadhili, na kutoa amri aletwe Yerusalemi, wapate kumwotea na kumwua njiani. Festo akajibu ya kama Paolo atalindwa Kaisaria; nae mwenyewe yu tayari kwenda huko karibu. Akasema, Wale walio na mamlaka na watelemke pamoja nami wakamshitaki, ikiwa liko neno baya katika mtu huyu. Alipokwisha kukawia kwao siku kumi na zaidi, akatelemkia Kaisaria: hatta siku ya pili akaketi katika kiti cha hukumu akaamuru Paolo aletwe. Walipokuja Wayahudi walioshuka kutoka Yerusalemi wakasimama karibu yake wakaleta mashitaka mengi na mazito juu yake, wasiyoweza kuyathuhutisha. Paolo akajitetea hivi, ya kama, Mimi sikukosa neno juu ya sharia ya Wayahudi, wiila juu ya hekalu wala juu ya Kaisari. Lakini Festo akitaka kujipendekeza kwa Wayahudi akamjibu Paolo, akisema, Wataka kwenda Yerusalemi, ukahukumiwe huko mbele yangu? Paolo akasema, Mimi ninasimama hapa mbele ya kiti cha hukumu cha Kaisari, panipasapo kuhukumiwa: sikuwakosa Wayahudi neno, kama wewe ujuavyo sana. Ikiwa nimekosa au nimetenda neno la kustahili kufa, sikatai kufa; hali, kama si kweli neno hili wanalonishitaki, hapana awezae kunitia mikononi mwao. Nataka rufaani kwa Kaisari. Bassi Festo alipokwisha kusema na watu wa baraza, akajibu, Umetaka rufaani kwa Kaisari! bassi, utakwenda kwa Kaisari. Siku kadha wa kadha zilipokwisha kupita, Agrippa mfalme na Bereniki wakafika Kaisaria, wakimwamkia Festo. Na walipokuwa wakikaa huko siku nyingi, Festo akamweleza mfalme khabari za Paolo, akisema, Yupo hapa mtu aliyeachwa na Feliki kifungoni; nami nilipokuwa Yerusalemi makuhani wakuu na wazee wa Wayahudi wakaniarifu khabari zake, wakitaka ahukumiwe. Nikawajibu kwamba sio desturi ya Warumi kumtoa mtu aliye yote auawe, kabla mtu yule aliyeshitakiwa hajaonana na washitaki wake uso kwa uso, na kupewa nafasi ya kujitetea katika mashitaka yake. Bassi walipokutanika hapa sikukawia; bali siku ya pili nikaketi katika kiti cha hukumu nikaamuru mtu huyo aletwe. Na wale waliomshitaki waliposimama karibu nae, hawakumshitaki neno baya, kama nilivyodhani, hali walikuwa na maswali juu yake katika dini yao wenyewe, na katika khabari ya mtu mmoja Yesu, aliyekuwa amekwisha kufa, ambae Paolo alishika kusema kwamba yu hayi. Nami nikaona mashaka jinsi ya kutafuta hakika ya khabari hii, nikamwuliza kama anataka kwenda Yerusalemi ahukumiwe huko katika mambo haya. Lakini Paolo alipodai kuwekwa ahukumiwe na Augusto, nikaamuru alindwe hatta nitakapompeleka kwa Kaisari. Agrippa akamwambia Festo, Mimi nami nalikuwa nikitaka kumsikia mtu huyu. Akasema, Utamsikia kesho. Hatta assubuhi Agrippa akaja pamoja na Bereniki kwa fakhari nyingi, wakapaingia mahali pa kusikia maneno, pamoja na maakida na watu wakuu wa mji: Festo akatoa amri Paolo aletwe. Festo akasema, Mfalme Agrippa, na ninyi nyote mliopo hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu, ambae jamii yote ya Wayahudi huku Yerusalemi na hapa pia wamenitaka niwasaidie, wakipiga kelele kwamba haimpasi kuzidi kuishi. Nami nilipoona kama hakutenda neno la kustahili kuuawa, na yeye mwenyewe alipotaka kuhukumiwa na Augusto, nalikusudia kumpeleka kwake. Nami sina neno la hakika la kumwandikia Bwana. Kwa hiyo nimemleta hapa mbele yenu, illi akiisha kuulizwa khabari zake, nipate neno la kuandika. Kwa maana naona ni neno lisilo maana kumpeleka mfungwa, bila kuonyesha mashitaka yale aliyoshitakiwa. AGRIPPA akamwambia Paolo, Una rukhusa kusema mimeno yako. Ndipo Paolo akanyosha mkono wake, akajitetea. Najiona nafsi yangu kuwa na kheri, ee mfalme Agrippa, kwa kuwa nitajitetea mbele yako leo, katika mambo yale niliyoshitakiwa na Wayahudi. Khassa kwa sababu wewe unajua sana desturi na maswali yote waliyo nayo Wayahudi: kwa sababu hiyo nakuomba unisikilize kwa uvumilivu. Kwa maana Wayahudi wote wanajua maisha yangu tangu ujana, yaliyokuwa tangu mwanzo katika taifa langu Yerusalemi, wakinijua sana tangu mwanzo, kama wakipenda kushuhudia, ya kwamba nalikuwa Farisayo kwa kuifuata madhehebu ya dini yetu iliyo sahihi kabisa. Na sasa ninasimama hapa nihukumiwe kwa ajili ya tumaini la ahadi waliyopewa baba zetu na Mungu, ambayo kabila zetu thenashara wanataraja kuifikia, wakimkhudumu Mungu kwa bidii mchana na usiku. Nami ninashitakiwa na Wayahudi kwa ajili ya tumaini hilo, ee Mfalme. Kwa nini limedhaniwa nanyi kuwa neno lisilosadikika, kwamba Mungu awafufua wafu? Kweli, mimi mwenyewe naliona ndani ya nafsi yangu kwamba yanipasa kutenda mambo mengi yaliyopingamana na jina lake Yesu Mnazareti; nikayafanya Yerusalemi: niliwafunga wengi miongoni mwa watakatifu ndani ya magereza, nikiisha kupewa amri na makuhani wakuu; na walipouawa nalitoa idhini yangu. Na marra nyingi katika masunagogi mengi naliwaadhibu, nikawashurutisha kukufuru; nikawaonea hasira kama nina wazimu, nikawaudhi hatta katika miji ya ugenini. Bassi katika kazi hiyo nalikuwa nikienda Dameski, nimepewa mamlaka na maagizo na makuhani wakuu. Ee Mfalme, wakati wa adhdhuhuri njiani naliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua, ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote. Tukaanguka chini sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya Kiebrania, Saul! Saul! ya nini kunindhi? ni vigumu kwako kunpiga mateke mchokoo. Nami nikasema, Wewe u nani, Bwana? Bwana akaniambia, Mimi ni Yesu, ambae wewe unaniudhi. Lakini inuka, usimame, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke nwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo kwayo nitajidhihirisha kwako; nikikuokoa na watu wako, na watu wa mataifa, ambao nakutuma kwao; uwafumhue macho yao, waiache giza na kuielekea nuru, na waziache nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu, na wapate masamaha ya dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu. Kwa hiyo, ee Mfalme Agrippa, sikuiasi ile njozi ya mbinguni, hali kwanza niliwakhubiri wale wa Dameski na Yerusalemi, na katika inchi yote ya Yahudi, na watu wa mataifa, watubu wakamwelekee Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao. Kwa sababu ya hayo Wayahudi wakanikamata ndani ya hekalu wakajaribu kuniua. Bassi nikiisha kuupata msaada utokao kwa Mungu nimesimama hatta leo hivi nikiwashuhudia wadogo kwa wakubwa, wala sisemi neno illa yale ambayo manabii na Musa waliyasema, kwamba yatakuwa; ya kwamba Kristo hana buddi kuteswa na ya kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika wafu atatangaza khabari za nuru kwa watu wake na kwa watu wa mataifa. Alipokuwa akijitetea hivi, Festo akasema kwa sauti kuu, Paolo, una wazimu, kusoma kwako kwingi kumekugenza akili zako. Lakini Paolo akasema, Sina wazimu, ee Festo il-aziz, bali nanena maneno ya kweli na ya akili kamili. Kwa maana mfalme anajua khabari za mambo haya, na naweza kusema nae bila khofu, kwa sababu najua sana ya kuwa hapana neno moja katika hayo asilolijua; kwa maana jambo hilo halikutendeka pembeni. Mfalme Agrippa, wawaamini manabii? Najua ya kuwa wawaamini. Agrippa akamwambia Paolo, Kwa maneno machache wataka kunifanya kuwa Mkristo. Paolo akamjibu, Namwomba Mungu kwamba ikiwa kwa machache au ikiwa kwa mengi si wewe tu illa na hao wote wanaonisikia leo wawe kama mimi pasipo vifungo hivi. Na alipokwisha kusema haya mfalme na liwali na Bereniki na wale walioketi pamoja nao wakasimama, wakaenda mbali kidogo wakasemezana, wakisema, ya kama, Mtu huyo hatendi neno linalostahili kifo wala kufungwa. Agrippa akamwambia Festo, Mtu huyo angeweza kufunguliwa kama asingalitaka rufaani kwa Kaisari. BASSI ilipoamriwa tusafiri hatta Italia, wakamtia Paolo na wafungwa wengine katika mikono ya akida mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto. Tukapanda katika merikebu ya Adramuttio iliyokuwa tayari kusafiri hatta miji ya pwani za Asia, tukatweka; Aristarko, Mmakedoni wa Thessalonika, akiwa pamoja nasi. Siku ya pili tukawasili Sidon; Yulio akamfadhili sana Paolo akampa rukhusa kwenda kwa rafiki zake, kutunzwa nao. Kutoka huko tukatweka, tukasafiri chini ya Kupro illi kuukinga upepo, kwa maana pepo zilikuwa za mbisho, tukaipita bahari ya upande wa Kilikia na Pamfulia, tukafikia Mura, mji wa Lukia. Na huko yule akida akakuta merikebu ya Iskanderia, tayari kusafiri hatta Italia, akatupandisha. Tukasafiri pole pole kwa muda wa siku nyingi, tukafika hatta Knido kwa shidda; na kwa sababu upepo ulikuwa ukituzuia tukapita chini ya Krete illi kuukinga upepo, tukaikabili Salmone. Tukaipita kwa shidda, pwani kwa pwani, tukafika mahali paitwapo Bandari Nzuri. Karibu na hapo pana mji uitwao Lasaya. Na wakati mwingi ulipokwisha kupita, na safari ikiwa ina khatari sasa kwa sababu siku za kufunga zilikuwa zimekwisha kupita, Paolo akawaonya, akawaambia, Wanaume, naoua kwamba safari hii itakuwa ina madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, illa na ya maisha zetu pia. Lakini yule akida akawasikiliza nakhodha na mwenye merikebu zaidi ya yale aliyoyasema Paolo. Na kwa sababu bandari haikukaa vema, watu wakae ndani yake wakati wa haridi, walio wengi wakatoa shauri tutweke tukatoke huko illi wapate kufika Foiniki, kama ikiwezekana, na kukaa huko wakati wa baridi: nayo ni bandari ya Krete, inaelekea kaskazini-mashariki na kusini-mashariki. Na upepo wa kusi ulipoanza kuvuma kidogo, wakidhani ya kuwa wamepata walioazimu kupata, wakangʼoa nanga, wakasafiri karibu na Krete pwani kwa pwani. Baada ya muda mchache upepo wa nguvu wa namna ya tufani, uitwao Eurakulo, ukaipiga merikebu. Ikachukuliwa, maana haikuweza kushindana na upepo, tukaiacha tukiichukuliwa. Na tukipita upesi karibu na kisiwa kiitwacho Klaudia tukadiriki kuikweza mashua; kwa shidda lakini. Walipokwisha kuikweza wakatumia misaada, wakaikaza merikehu kwa kupitisha kamba chini yake; na wakiogopa wasije wakakwama kwenye Surtis, wakatua matanga wakachukuliwa vivi hivi. Na kwa kuwa tukawa tukipigwa sana na ile tufani, siku ya pili yake wakaanza kuitupa shehena baharini. Siku ya tatu tukatupa vyombo vya merikebu kwa mikono yetu wenyewe. Na jua na nyota hazikuonekana kwa muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, bassi tukakata tamaa ya kuokoka. Na tulipokuwa tumekaa wakati mwingi bila kula chakula, Paolo akasimama katikati yao, akasema, Wanaume, ingalikuwa kheri kama mngalinisikiliza na kutokungʼoa nanga huko Krete, na kupata madhara haya na hasara hii. Sasa nawapeni shauri, mwe na moyo mkuu, kwa maana hapana hatta nafsi mmoja miongoni mwenu atakaepotea, illa merikebu, bassi. Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambae mimi ni mtu wake, na udiye nimtumikiae, alisimama karibu nami akaniambia, Usiogope, Paolo, huna buddi kusimama mbele ya Kaisari: tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Bassi, wanaume, changaʼmkani; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa. Lakini hatuna buddi kupwelewa katika kisiwa kimoja. Hatta usiku wa kumi na nne ulipowadia, tukichukuliwa huko na huko katika bahari ya Adria, usiku wa manane baharia wakadhani ya kuwa wanaikaribia inchi kavu. Wakatupa bildi wakakuta pima ishirini, wakaendelea kidogo wakatupa bildi tena, wakakuta pima kumi na tano. Wakachelea wasije wakapwelewa mahali penye miamba, wakatupa nanga nne, wakaomba kuche. Na baharia walipotaka kukimbia na kuiacha merikebu, wakiishusha mashua baharini kana kwamba wanataka kutupa nanga za omo, Paolo akawaambia akida na askari, Hawa wasipokaa ndani ya marikebu hamtaweza kuokoka. Bassi askari wakazikata kamba za mashua, wakaiacha ianguke. Na kulipokuwa kukipambazuka Paolo akawasihi wote wale chakula, akisema, Leo ni siku ya kumi na nne kungoja na kufunga, hamkula kitu cho chote. Bassi nawasihi mle chakula, maana itakuwa kwa wokofu wenu; kwa maana hapana unywele wa vichwa vyenu utakaopotea. Alipokwisha kusema haya akatwaa mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote akaumega akaanza kula. Wakachangaʼmka wote, wakala vyakula wenyewe. Na sisi tuliokuwa ndani ya merikebu tulipata watu miateen na sabaini na sita. Walipokwisha kushiba wakaipunguza shehena va merikebu, wakaitupa nganu baharini. Kulipokucha hawakuitambua ile inchi, illa waliona hori yenye ufuko, wakashauriana kuiegesha merikebu huko, kama ikiwezekana. Wakazitupilia mbali zile nanga, wakaziacha baharini, wakazilegeza kamba za sukani, wakalitweka tanga dogo illi liushike upepo, wakauendea ule ufuko. Lakini wakafikia mahali palipokutana bahari mbili, wakaiegesha merikebu, omo ikakwama ikakaa isitikiswe, bali shetri ilikuwa imefumuliwa kwa nguvu za mawimbi. Shauri la askari lilikuwa wafungwa wauawe, mtu asiogelee na kukimbia. Bali akida, akitaka kumponya Paolo, akawazuia, wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe baharini, wafike inchi kavu; nao waliosalia, hawa juu ya mbao na hawa juu ya vitu vingine vya merikebu. Na hivyo watu wote wakapata kuifikia inchi kavu salama. TULIPOKWISHA kuokoka, ndipo tukajua ya kuwa kisiwa kile chaitwa Melita. Washenzi wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida. Kwa maana walikoka moto, wakatukaribisha sote, kwa sababu ya mvua iliyokunywa na kwa sababu ya baridi. Paolo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na kuuweka juu ya moto, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto, akamzingisha katika mkono wake. Washenzi walipomwona yule nyoka akimwangikia mkono, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni muuaji; na ijapokuwa ameokoka katika bahari, haki haimwachi kuishi. Lakini yeye akamtikisia motoni asipate madhara. Wakamwangalia sana wakidhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini, amekwisha kufa kwa ghafula; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lo lote, wakabadili fikara zao, wakasema kwamba yeye ni Mungu. Karibu na mahali pale palikuwa na mashamba ya mkubwa wa kisiwa, jina lake Publio; mtu huyu akatukaribisha kwa moyo wa urafiki, akatufanya wageni wake kwa muda wa siku tatu. Ikawa baba yake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu. Paolo akaingia kwake, akaomba, akaweka mikono yake juu yake, akamponya Yalipokwisha kutendeka hayo wengine waliokuwa na magonjwa katika kisiwa wakaja wakaponywa; nao wakatuheshimu kwa heshima nyingi. Na tulipoondoka wakatupakilia vitu vile tulivyokuwa na haja navyo. Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Dioskuri. Tukafika Surakusa, tukakaa siku tatu. Kutoka huko tukazunguka tukafikia Regio: baada ya siku moja upepo wa kusi ukavuma, na siku ya pili tukawasili Puteoli. Huko tukakuta ndugu, tukasihiwa nao tukae siku saba; na hivi tukafika Rumi. Na kutoka huko ndugu, waliposikia khabari zetu, wakaja kutulaki mpaka Appiiforo na Trestaberne. Paolo alipowaona akamshukuru Mungu, akachangaʼmka. Tulipoingia Rumi akida akawatia wafungwa katika mikono ya jemadari wa walinzi wa Praitorio: bali Paolo alipewa rukhusa kukaa kwake mwenyewe pamoja na askari aliyemlinda. Ikawa baada ya siku tatu akawaita wakuu wa Wayahudi wakutane; hatta walipokuja akawaambia, Wanaume ndugu, ningawa sikufanya neno kinyume cha watu wetu wala neno lililopingamana na desturi za baba zetu, nalitiwa katika mikono ya Warumi, nimefungwa, tokea Yerusalemi. Na hao walipokwisha kuniuliza walitaka kunifungua, kwa maana hapakuwa na sababu yo yote ya kuuawa kwangu. Lakini Wayahudi walipotoa hoja juu ya shauri hili nalishurutishwa kutaka rufaani kwa Kaisari. Si kwamba nalikuwa na neno la kuwashitaki watu wa taifa langu. Bassi kwa ajili ya hayo, nimewaiteni mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli. Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye khabari zako kutoka Yahudi, wala hapana ndugu hatta mmoja aliyefika hapa na kutupasha khabari, au kunena neno baya juu yako. Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika khabari za madhehebu hiyo tumekwisha kujua kwamba inanenwa vibaya kilia mahali. Wakiislia kuwekana kwa siku, wakaja kwake nyumbani kwake, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sharia ya Musa na ya manabii, tangu assubuhi hatta jioni. Wengine waliamini yaliyonenwa, wengine hawakuyaamini. Na walipokuwa hawapatani wao kwawao, wakaenda zao, Paolo alipokwisha kusema neno hili moja ya kama, Roho Mtakatifu alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya, Enenda kwa watu hawa, ukawaamhie, Kusikia, mtasikia wala hamtafahamu; Na kuona mtaona, wala hamtapata kujua neno: Kwa maana mioyo ya watu hawa imepumbaa, Na masikio yao ni wazito wa kusikia, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo yao, Na kuhadili nia zao Nikawaponya. Bassi ijulikane kwenu ya kwamba wokofu huu wa Mungu umepelekwa kwa mataifa, nao watasikia. Alipokwisha kusema haya, Wayahudi wakaenda zao, wakiulizana mengi wao kwa wao. Paolo akakaa muda wa miaka miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea, akikhubiri khabari za ufalme wa Mungu, na kuwafundisha watu mambo ya Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu. PAOLO, mtumwa wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kuwekwa aikhubiri Injili ya Mungu, ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa vinywa vya manabii wake katika maandiko matakatifu, khabari za Mwana wake, aliyekuwa katika ukoo wa Daud kwa jinsi ya mwili, na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo; Yesu Kristo Bwana wetu, ambae katika yeye tulipokea neema na utume illi mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake; katika hawa na ninyi mmekuwa, mmeitwa na Yesu Kristo: kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu: Neema iwe kwenu na imani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwaua Yesu Kristo. Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inakhubiriwa katika dunia yote. Kwa maana Mungu, nimwabuduye kwa roho yangu katika Injili ya Mwana wake ni shahidi wangu jinsi niwatajavyo pasipo kukoma, siku zote katika sala zangu nikiomba nije kwenu sasa katika siku hizi hizi, Mungu akipenda kuifanikisha safari yangu: kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapeni karama ya rohoni, illi mfanywe imara; yaani, tufarijiane mimi na ninyi, killa mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu. Sipendi msiwe na khahari, ndugu zangu, ya kuwa marra nyingi nalikusudia kuja kwemi, nikazuiliwa hatta sasa, illi nipate kuwa na matunda kwenu ninyi pia kama nilivyo navyo katika mataifi mengine. Nawiwa na Wayunani na washenzi, nawiwa na wenye hekima na wajinga. Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi ni tayari kuikhubiri Injili hatta na kwenu ninyi muaokaa Rumi; kwa maana siionci haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokofu, kwa killa aaminiye, kwa Myahudi kwanza, hatta kwa Myunani pia. Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hatta imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani. Kwa maana ghadhahu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wana Adamu waipingao kweli kwa uovu wao. Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana ni dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo yake yasiyoonekima tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, yanafahamika kwa viumbe vyake, yaani uweza wake wa milele na Uungu wake; wtisiwe na udhuru: kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza: wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika, wakaubadili utukufu wa Mungu asiye ua uharibifu kwa mfano wa sura ya bin-Adamu aliye ua uharibifu, na ya nyama wenye mbawa, na ya nyama wenye miguu mine, na ya nyama watambaao. Kwa ajili ya bayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hatta wakavunjiana heshima miili yao: kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kwa uwongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anaehimidiwa milele. Amin. Kwa hiyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hatta wanawake wakahadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili: wanaume vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume kwa wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wuyafanye yasiyowapasa; wakijawa na udhalimu wa killa namna ya zina, na novu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na khadaa; watu wti nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakahari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema, ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao haya wamestahili mauti, wanafanya haya, wala si hivyotu, bali wakubaliana nao wayatendao. KWA hiyo, ee mtu uhukumuye uwae yote, huna udhuru; kwa maana katika hayo uhukumuyo mwingine wajihukumu nafsi yako; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale. Na twajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo. Ee bin-Adamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je! wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu? Au waudharau wingi wa wema wake na uvumilivu wake na kusubiri kwake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvutia toba? bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu, atakaemlipa killa mtu kwa kadiri ya matendo yake; wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele; na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, hasira na ghadhabu; mateso na shidda juu ya killa roho ya mwana Adamu atendae uovu, kwanza Myahudi na Myunani pia: bali utukufu na heshima na amani kwa killa mtu atendae mema, Myahudi kwanza na Myunani pia; kwa maana hapana upendeleo kwa Mungu. Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sharia watapotea pasipo sharia, na wote waliokosa, wakiwa na sharia, watahukumiwa kwa sharia. Kwa sababu sio waisikiao torati walio wenye haki mbele ya Mungu, bali ni wale waitendao torati watakaohesabiwa kuwa wenye haki. Kwa maana watu wa mataifu wasio na sharia wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, bao wasio na sharia wamekuwa sharia kwa nafsi zao wenyewe: hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na wakishitakiana killa mtu mwenzake kwa fikara zao na kuteteana; katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wana Adamu, sawa sawa na injili yangu, kwa Yesu Kristo. Lakini wewe, ukiwa unakwitwa Myahudi na kuitegemea torati, na kujisifu katika Mungu, na kuyajua mapenzi yake na kuyatambua manibo yaliyo bora, umeelimishwa katika torati, na kujua hakika ya kuwa wewe mwenyewe u kiongozi wa vipofu, mwanga wao walio gizani, mkufunzi wra wajiuga, mwalimu wa watoto wachanga, mwenye namna ya maarifa na ya kweli katika torati, hassi wewe umfundishae mwiugine, je! hujifimdishi nafsi yako? Wewe nkhubiriye kwamha mtu asiibe, waiba mwenyewe? Wewe usemae kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe uchukiae sanamu, wateka mahekidu? Wewe ujisifuye katika torati, kwa kuiasi torati wamvunjia Mungu heshima? Kwa maana jina la Mungu lanenwa unajisi katika mataifa kwa ajili yenu, kama ilivyoandikwa. Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sharia, lakini ukiwa mvunjaji wa sharia kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa. Bassi ikiwti yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, je! kutokutahiriwa kwake hakutahesahiwa kuwa kutahiriwa? Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikae torati, hatakuhukumu wewe, uliye na maandiko na kutahiriwa, ukaikhalifu torati? Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili; hali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; na sifa yake haitoki kwa wana Adamu hali kwa Mungu. BASSI Myahudi ana ziada gani? na kutahiriwa kwafaa nini? Kwafaa sana kwa killa njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu. Ni nini, bassi, ikiwa hawakuamini wengine? Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na killa mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Illi upewe haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu. Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithubutisha hakiya Mungu, tuseme nini? Mungu ni dhalimu aletae ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibin-Adamu.) Hasha! kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu? Kwa maana, ikiwa kweli ya Mungu imezidi kwa sababu ya uwongo wangu hatta akapata utukufu, mbona mimi nami ningali nikihukumiwa kama ni mwenye dhambi? Kwa maana tusiseme (kama tulivyosingiziwa nakama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba sisi twanena), Na tufanye mabaya, illa yaje mema? kuhukumiwa kwao kuna haki. Ni nini bassi? Tu bora kuliko wengine? Hatta kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba wote pia wa chini ya dhambi; kama ilivyoandikwa, ya kama, Hakuna mwenye haki hatta mmoja. Hakuna afahamuye, Hakuna amtafutae Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema hatta mmoja: Koo lao kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila, Sumu ya pili ni chini ya midomo yao. Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. Miguu yao ina mbio kumwaga damu. Uharibifu na mashaka njiani mwao. Na njia ya amani hawakuijua. Kumwogopa Muungu hakuwi machoni pao. Twajua ya kuwa mambo yote yasemwayo na torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, illi killa kinywa kifumbwe, ulimwengu wote ukapasiwe na hukumu ya Mungu: kwa maana hapana mwenye mwili atakaehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu, kwa matendo ya sheria: kwa maanii kujua dhambi kabisa huja kwa njia ya sharia. Sasa, lakini, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sharia, inashuhudiwa na torati na manabii, ni haki ya Mungu, ipatwayo kwa kuwa na imani kwa Yesu Kristo, huja kwa watu wote, huwakalia watu wote waaminio. Maana hapana tofauti; kwa sababu wote wamefanya dhambi, wanaona kwamba wamepungukiwii utukufu wa Mungu: wanapewa haki burre kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Yesu Kristo: ambae Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa damu yake, kwa njia ya imani, illi aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia dhambi zilizotangulia, katika uvumilivu wa Mungu: illi aonyeshe haki yake wakati huu, awe mwenye baki na mwenye kumpa haki yeye aaminiye kwa Yesu. Ku wapi, bassi, kujisifu? Knmefungiwa mlango. Kwa sharia ya namna gani? Kwa sharia ya matendo? La! bali kwa sharia ya imani. Bassi, twahasibu ya kuwa mwana Adamu hupewa baki kwa imani pasipo matendo ya sharia. Au Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa mataifa pia? Naam, wa mataifa pia; kama tukijali kwamba Mungu ni mmoja, atakaewapa wale waliotahiriwa haki itokayo katika imani, nao wasiotahiriwa liaki kwa njia ya imani hiyo hiyo. Bassi, je! twaibatilisha sharia kwa imani hiyo? Hasha! kinyume cha hayo twaithubutisha sharia. BASSI, tusemeje? Ibrahimu baba yetu kwa jinsi ya mwili amepata nini? Kwa maana ikiwa Ibrahimu alipewa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia, lakini si mbele za Mungu. Maana maandiko yasemaje? Ibrabimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki. Lakini kwa mtu afanyae kazi ujira wake hauhesabiwi kuwa neema bali kuwa deni. Lakini kwa mtu asiofanya kazi, bali anamwammi yeye ampae haki asiye mtawa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki. Kama vile Daud aunenavyo ukheri wake mtu yule ambae Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo; Wa kheri waliosamehewa maasi yao, Na waliosetiriwa dhambi zao. Yu kheri mtu yule ambae Bwana hamhesabii dhambi. Bassi ukheri huu ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa twanena ya kwamba Ibrahimu kwa ajili ya imani yake aliliesabiwa wema. Alihesabiwaje bassi? Alipokwisha kutahiriwa, au kabla hajatahiriwa? Si baada ya kutahiriwa, bali kabla ya kutahiriwa. Nae aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya wema wa imani aliyokuwa nayo kabla asijatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, illi na wao pia wahesahiwe wema; na baba ya kutahiriwa, si kwa hao waliotahiriwa tu, bali kwa hao waliotahiriwa na kuzifuasa uyayo za imani yake baba yetu Ibrahimu aliyokuwa nayo kabla asijatahiriwa. Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sharia bali kwa wema aliopata kwa imani. Maana ikiwa wale wa sharia ndio warithi, imani imekuwa burre, na ahadi imebatilika. Kwa sababu sharia ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipo sharia, hapana kosa. Kwa hiyo ilitoka kwa imani, iwe kwa njia ya neema, illi ile ahadi iwe imara kwa wazao wote, si kwa wale wa torati tu, illa na kwa wale wa imani ya Ibrahimu aliye baba yetu sisi sote, (kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi) mbele zake aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, avitajae vitu visivyokuwa kana kwamba vimekuwa. Ambae aliamini kwa kutazamia yasiyoweza kutazamiwa, kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa nzao wako. Asiyekuwa dhaifu wa imani, wala hakutia moyoni hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa (akiwa amekwisha kupata miaka mia), wala hali ya kufa ya tumbo lake Sara. Wala hakuionea shaka ahadi ya Mungu kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani yake, akimtukuza Mungu, akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi. Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa haki. Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake, bali na kwa ajili yetu sisi tutakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu katika wafu, Bwana wetu, aliyetolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa illi tupate kupewa haki. BASSI tukiisha kuhesabiwa wema utokao katika imani, tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo; kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo tunasimama ndani yake; na twafurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. Wala si hivyo tu, illa twafurahi katika mateso pia, tukijua ya kuwa dhiiki, kazi yake ni kuleta uvumilivu, na kazi ya uvumilivu uthabiti wa moyo, na kazi ya uthabiti wa moyo tumaini, na tumaini halitahayarishi, kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepcwa sisi. Kwa maana hapo tulipokuwa sisi hatuna nguvu, wakali ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya maasi. Kwa maana ni shidda mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki, illakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Bali Mungu aonyesha pendo lake kwetu, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Bassi zaidi sana tukiisha kupewa haki katika damu yake tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Kwa maana tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Wala si hivyo tu, illa na twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo ambae kwa yeye tuliupokea upatanisho. Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote; kwa maana wote wamefanya dhambi; maana kabla ya sharia dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi sharia isipokuwapo; lakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hatta wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu aliye mfano wake yeye atakaekuja. Lakini kipawa kile hakikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kuanguka kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema ya mtu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi. Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyekosa si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu, bali kipawa cha neema kilikuja kwa ajili ya makosa mengi, kikaleta kuachiliwa. Kwa maana ikiwa kwa kuteleza mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. Bassi tena, kama vile kwa anguko moja watu wote walihukumiwa, vivyo hivyo kwa tendo moja la haki watu wote walipewa haki yenye uzima. Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wote waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, vivyo hivyo kwa kutii kwake mtu mmoja watu wote wameingizwa katika hali ya wenye haki. Sharia iliingia illi anguko lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi; illi, kama vile dhambi ilivyotawaia katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hatta uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu. TUSEME nini bass? Tudumu katika dhambi illi neema iwe nyingi zaidi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Yesu Kristo, twalibatizwa katika mauti yake? Bassi tulizikwa pamoja nae kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tutembee katika upya wa uzima. Kwa maana kama tulivyounganika nae katika mfano wa mauti yake, kadhalika kwa mfano wa kufufuka kwake; tukijua haya, ya kuwa mtu wetu wa kale alisulibishwa pamoja nae, illi mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; kwa maana yeye aliyekufa ameachiliwa akawa mbali ya dhambi. Lakini tukiwa twalikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja nae, tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka hafi tena, mauti haimtawali tena. Kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi marra moja; lakini kule kuishi kwake, amwishia Mungu. Vivyo hivyo na ninyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi, na wahayi kwa Mungu katika Kristo Yesu. Bassi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti hatta mkazitii tamaa zake; wala msitoe viungo vyenu kuwa silaha ya dhulumu kwa dhambi; bali jitoeni nafsi zenu sadaka kwa Mungu kama walio hayi baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sharia, hali chini ya neema. Ni nini bassi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sharia bali chini ya neema? Hasha! Hamjui ya kuwa kwake yeye ambae mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake na kumtumikia, m watumwa wake yule mmtiiye, ikiwa utumishi wa dhambi uletao mauti, au utumishi wa utii uletao haki. Lakini Mungu ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; na mlipokwisha kuandikwa huru mkawa mbali ya dhambi, mlifanywa watumwa wa haki. Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa maana kama mlivyotoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na maasi mpate kuasi, vivyo sasa toeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa. Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali ya haki. Faida gani bassi mliyopata siku zile kwa mambo haya mnayotahayarikia sasa? kwa maana mwisho wa mambo haya ni mauti. Lakini sasa mkiisha kuandikwa huru, na kuwa mbali ya dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, faida yenu mnayo, ndio kutakaswa, na mwisho wake uzima wa milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; hali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. HAMJUI, ndugu (maana nasema nao waijuao sharia), ya kuwa torati humtawala mtu maadam yu hayi. Kwa maana mwauamke aliye na mume amefungwa na sharia kwa yule mume maadam yu hayi: bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sharia ya mume. Bassi wakati awapo hayi mume wake, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Bali mume wake akifa, amekuwa huru, hafungwi na sharia hiyo, hatta yeye si mzinzi, ajapokuwa na mume mwingine. Kadhalika, ndugu zangu, na ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka, kusudi tumzalie Mungu matunda. Kwa maana tulipokuwa katika mwili, tamaa za dhambi zilizokuwako kwa sababu ya torati zilitenda (kazi) katika viungo vyetu hatta tukaizalia mauti mazao. Bali sasa tumetolewa katika torati isitukhusu kitu, tumeilia hali ile iliyotupinga, tupate kutumika sisi katika hali mpya chini ya roho, si katika hali ya zamani, ya dini ya sharia iliyoandikwa. Tusemeje, bassi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalijua dhambi illa kwa sharia: kwa maana singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani. Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanza ndani yangu killa namna ya tamaa. Kwa maana dhambi hila sharia ni kifu. Na mimi nalikuwa hayi hapo kwanza hila sharia; illa ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, na mimi nikafa. Nikaona ile amri iletayo uzima, ya kuwa kwangu mimi ilileta mauti. Kwa maana dhambi, ikipata nafasi kwa iie amri, ilinidanganya, ikaniua kwayo. Bassi torati ni takatifu na ile amri takatifu ua ya haki na wema. Bassi je! Ile iliyo njema ilikuwa manti kwangu mimi? Hasha! hali dhambi, illi ionekane kuwa dhambi, ilinifanyizia mauti kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno. Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni, bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi. Maana sijui nifanyalo; kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; na lile nilichukialo nalitenda. Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, nakiri ya kuwa sheria ile ni njema. Bassi sasa si mimi nilitendalo, bali ile dhambi ikaayo ndani yangu. Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu, halikai neno jema: kwa kuwa kutaka ni katika uwezo wangu, bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi, bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Bassi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nilitendae, bali ile dhambi ikaayo ndani yangu. Bassi nimeona sharia hii ya kuwa nipendapo kutenda lililo jema, liapo lililo baya ni karibu nami. Kwa maana naifurahia sharia ya Mungu kwa mtu wa ndani, lakini katika viungo vyangu naona sharia nyingine inapiga vita na ile sharia ya akili zangu, na kunifanya mateka va ile sharia ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. Ole wangu mimi bin Adamu! nani atakaeniokoa na mwili huu wenye kunifisha. Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Bassi, kama ni hivi, kwa akili zangu naitumikia sharia ya Mungu, bali kwa mwili sharia ya dhambi. SASA, bassi, hapana hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu, wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya roho. Kwa sababu sharia ya Roho ya uzima ule ulio katika Yesu Kristo imeniacha huru, nikawa mbali ya sharia ya dhambi na mauti. Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili: illi wema uagizwao na torati utimizwe ndani yetu, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Kwa maana wale wafuatao mambo ya mwili huyafikiri mambo ya mwili, bali wale wafuatao mambo ya roho hufikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti, bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sharia ya Mungu wala haiwezi. Wafuatao mambo ya mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ikiwa Roho ya Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamfuati mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Lakini mtu aliye yote asipokuwa na Roho ya Kristo, huyo si mtu wake. Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu u katika hali ya kufa kwa sababu ya dhambi, bali roho yenu i katika hali ya uzima, kwa sababu ya haki. Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu. Bassi, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili, kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa: bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho ya Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea roho ya utumwa uletao khofu, hali mlipokea roho ya kufanywa waua, kwa hiyo twalia, Abba, Baba. Roho yenyewe hushuhudu pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; kama tu watoto, bassi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja nae illi tutukuzwe pamoja nae. Kwa maana nayahasibu mateso ya wakati wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu. Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi siku ile watakayofunuliwa wanawa Mungu. Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili, si kwa khiari yake, illa kwa sababu yake aliyevitiisha, katika tumaini: kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu viingie uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, na vina utungu pamoja mpaka sasa. Wala si hivyo tu, illa na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho tunaugua katika nafsi zetu, tukitazamia kufanywa wana, ukombozi wa mwili wetu. Kwa maana tuliokolewa kwa kutumaini; lakini kitu kilichotumainiwa kikionekana hakuna kutumaini tena. Kwa maana kile akionacho mtu, ya nini kukitumaini? Bali tukikitumaini kitu tusichokiona, twakingojea kwa uvumilivu. Na kadhalika Roho nae hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuomhea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzae mioyo aijua nia ya Roho, ya kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. Na twajua ya kuwa mambo yote hushiriki kazi moja, ndio kuwapatia mema wale wampendao Mungu, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, illi awe mzaliwa wa kwanza katika ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hawa akawatukuza. Bassi, na tuseme nini baada ya hayo? Mungu akiwa upande wetu, nani aliye juu yetu? Yeye asiyemwachilia Mwana wake yeye, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukarimia na vitu vyote pamoja nae? Ni nani atakaewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye awahesabiae haki. Ni nani atakaewahukumu? Kristo ndiye aliyekufa, naam, na zaidi ya haya, amefufuka, nae yuko mkono wa kuume wa Mungu, tena ndiye anaetuombea. Ni nani atakaetutenga na upendo wa Kristo, Je! ni shidda, au dhiiki, au adha, au njaa, au uchi, au khatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kama, Kwa ajili yako tunauawa mchana kuchwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo haya yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana tumekwisha kujua hakika ya kuwa hatta mauti haiwezi kututenga, wala nzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala wenye uwezo, wala yaliyopo, wala yatakayokuwa, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe cho chote kinginecho hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Yesu Kristo Bwana wetu. NASEMA kweli katika Yesu Kristo, sisemi uwongo, dhamiri yangu ikinishuhudia katika Roho Mtakatifu, ya kwamba nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu. Kwa maana naliomba mimi mwenyewe niharamishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili; ambao ni Waisraeli, wenye kufanywa wana, wenye utukufu na maagano, wenye kupewa torati na ibada ya Mungu na ahadi zake; ambao mababu ni wao, na katika bao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili, aliye juu ya mambo yote, Mungu, anaehimidiwa milele. Amin. Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka; maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli. Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaak wazao wako watakwitwa; yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanabesabiwa kuwa wazao. Kwa maana neno la ahadi ni hili, Panapo wakati huu nitakuja, na Sara atakuwa na mwana. Wala si hivyo tu, lakini Rebeka nae, akiisha kuchukua mimba kwa mmoja, nae ni Isaak baba yetu— kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, illi lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitae aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo. Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia. Tuseme nini bassi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha! Maana alimwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiae. Bassi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakae, wala wa yule apigae mbio, bali wa yule arehemuye, yaani Mungu. Kwa maana maandiko yasema na Farao, ya kama, Nilikusimamisha, illi niouyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika inchi yote. Bassi, kama ni hivyo, atakae (kumrehemu) humrehemu, na atakae kumfanya mgumu humfanya mgumu. Bassi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana nani aliyeshindana na kusudi lake? La! si hivyo, ee bin-Adamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Ya nini nkanifanza hivi? An mfinyangi je! bana nguvu juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kufanya chombo kimoja, kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima? Bassi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kujulisha uweza wake kwa uvumilivu mwingi alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu; tena ajulishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema alivyovitengeneza tangu zamani, vipate utukufu, ndio sisi tulioitwa nae, si watu wa Wayahudi tu, illa watu wa mataifa pia, utasemaje? Ni vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita wale kuwa watu wangu wasiokuwa watu wangu, Na yeye mpenzi wangu asiyekuwa mpenzi wangu. Na itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo watakwitwa wana wa Mungu aliye hayi. Isaya nae atoa santi yake juu ya Israeli, Hesabu ya wana wa Israeli, ijapokuwa kama mchanga wa bahari, ni mabaki yao tu watakaookolewa. Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya inchi, akilimaliza na kulikata. Na kama isaya alivyotangulia kunena, Kama Bwana wa Sabaoth asingalituachia uzao, Tungalikuwa kama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora. Tuseme nini, bassi? Ya kwamba watu wa mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; yaani ile haki iliyo ya imani; bali Israeli wakiifuata sharia ya haki hawakuifikilia ile sharia. Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuitafuta kwa njia ya imani bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwaazalo, kama ilivyoandikwa, Tazama, Naweka katika Sayuni jiwe likwaazalo, na mwamba uangushao: Na killa amwaminiye hataaibishwa. NDUGU, nia njema ya moyo wangu, na dua yangu niombayo Mungu kwa ajili ya Waisraeli ndio bii, waokolewe. Kwa maana nawashuhudia kwamba wana wivu kwa ajili ya Mungu, lakini hauna msingi wa maarifa. Kwa maana, wakiwa hawajui haki ya Mungu, na wakitaka kuithubutisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. Kwa maana Kristo ni mwisho wa sharia, illi killa aaminiye apate haki. Kwa maana Musa aieleza haki itokayo kwa sharia, akiandika ya kuwa, Mtu afanyae haya ataishi kwa haya. Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakaepanda mbinguni? (yaani ni kumleta Kristo chini,) au, Ni nani atakaeshuka kuzimuni? (yaani, ni kuleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.) Lakini yasemaje? Lile neno ni karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani ni lile neno la imani tulikhubirilo; kwa sababu, ukimkiri Kristo Yesu kwa kinywa chako, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua, utaokoka; kwa maana kwa moyo watu huamini hatta kupata haki, na kwa kinywa hukiri hatta kupata wokofu. Kwa maana andiko lanena, Killa amwaminiye hatatahayarika. Kwa maana hapana tofanti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri wa kufaa watu wote wamwitiao; kwa kuwa killa atakaemwita Bwana kwa Jina lake ataokoka. Bassi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mkhubiri? Tena wakhubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri namna gani miguu yao wakhubirio khabari ya mema. Lakini si wote walioitii khahari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, nani aliyeamini khabari zetu? Bassi imani, chanzo chake ni kusikla; na kusikia kunakuja kwa neno la Mungu. Lakini nasema, Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imetoka ikaenea katika inchi yote, Na maneno yao hatta miisho ya ulimwengu. Lakini nasema, Israeli hakufahamu? Hapo kwanza Musa anena, Nitawatieni moyo wa bidii kwa watu wasio taifa, Kwa taifa lisilo na fahamu nitawaghadhabisha. Na Isaya ana ujasiri mwingi, anasema, Nalipatikana nao wasionitafuta, Nalidhihirika kwao wasioniulizia. Lakini kwa israeli asema, Mchana kutwa naliwanyoshea mikono watu wasiotii na ubishi. BASSI, nauliza. Mungu aliwasukumia mbali watu wake? Hasha! maana mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya Benjamin. Mungu hakuwasukumia mbali watu wake aliowajua tokea asili. Au hamjui yale yaliyonenwa na maandiko juu ya Eliya? jinsi anavyowashitaki Waisraeli mbele ya Mungu, Bwana, wamewaua nabii zakowamezibomoa madhbabu zako, nami mmesalia peke yangu, nao wanatafuta roho yangu. Lakini ile jawabu yamwanibiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baal. Bassi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako maliaki waliochaguliwa kwa neema ya Mungu. Lakini ikiwa ni kwa neema yake, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema; na ikiwa ni kwa matendo, haiwi neema tena, au hapo matendo yasingekuwa matendo. Imekuwaje bassi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata, lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa ugumu. Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hatta wasione, na masikio hatta wasisikie mpalla leo. Na Daud asema, Meza yao iwe tanzi na mtego, Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao; Macho yao yatiwe giza wasione, Ukawainamisbe mgongo wao siku zote. Bassi nasema, Je! wamejikwaa hatta wameanguka kabisa? Hasha! Lakini kwa kosa lao wokofu umewafikilia mataifa, illi wao watiwe wivu: bassi ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa mataifa, je! si zaidi sana utimilifu wao? Lakini nasema na ninyi, watu wa mataifa. Kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa mataifa, naifukuza khuduma iliyo yangu. Huenda nikapata kuwatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi vao. Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhayi baada ya kufa? Tʼena malimbuko yakiwa matakatifu, vivyo hivyo na, donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo vivyo hivyo. Lakini iwapo matawi mengine yamekatiwa, na wewe mzeituni mwitu ulitiwa kati yao ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake, usijisifu juu ya matawi; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuae shina bali shina likuchukualo wewe. Bassi utasema, Matawi yalikatiwa illi nitiwe mimi. Marra haba. Yalikatiwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune bali uogope; kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe. Fahamu, bassi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka ukali, bali kwako wema, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali. Na hao pia, wasipokaa katika kulokuamini kwao, watatiwa, kwa maana Mungu aweza kuwatia temi. Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, ukatiwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema; si zaidi sana wale walio wa asili watatiwa katika mzeituni wao wenyewe. Kwa maana sitaki ndugu msiijue siri hii, ms jione kuwa wenye akili, ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka ntimilifu wa mataifa uwasili; na hivi Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Yeye aokoae atakuja kutoka Sayuni Atamtenga Yakobo na maasi yake, Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao. Bassi kwa khabari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu, bali kwa khabari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya haha zetu. Kwa sababu karama za Mungu na wito wake hazina majuto. Kwa maana kama ninyi zamani mlimwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kutokuamini kwao, vivyo hivyo na hao wameasi sasa, illi kwa kurehemiwa kwenu wao nao wapate rehema. Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi illi awarehemu wote. Ee ajabu ya utajiri na hekima na maarifa ya Mungu; hazina hatta kiasi! hukumu zake hazichunguziki, na njia zake hazitafutikani! Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, nae atalipwa? Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amin. BASSI, nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, mtoe miili yenu iwe dhabihu hayi, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ibada yenu yenye maana. Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufunya upya nia zenu, mpate kujua kwa hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia killa mtu alioko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyoamgawi killa mtu kadiri ya imani. Kwa maana kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, navyo viungo vyote havitendi kazi moja; vivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na sisi sote tu viungo killa mmoja kwa wenzake. Bassi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa khuduma, tuwemo katika khuduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukarimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia, kwa bidii; mwenye kurehemu, kwa furaha. Pendo niwe nalo pasipo unafiki; mkichukia lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu, mwe na shauku ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; kwa tumaini, mkifurahi; katika shidda, mkivumilia; katika kusali, mkidumu; kwa mahitaji ya watakatifu, mkiwashirikisha; katika kukaribisha wageni, mkijitahidi. Wabarikini wanaowafukuzeni; barikini, wala msilaani. Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. Mwe na nia moja ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili. Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Andaeni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yumkini, kwa upande wenu, mwe na amani na watu wote. Msijilipize kisasi, wapenzi, bali ipisheni ghadhabu; maana imeandikwa, Kisasi juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Bassi adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivi, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema. KILLA nafsi itumikie mamlaka makuu; kwa maana hapana mamlaka yasiyotoka kwa Mungu: na mamlaka yaliyopo yameamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka ashindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. Kwa maana watawalao hawatii watu khofu kwa ajili ya matendo mema, bali kwa ajili ya matendo mabaya. Bassi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, utapata sifa kwake; kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga burre: ni mtumishi wa Mungu, amlipizae kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. Kwa hiyo lazima kutumika, si kwa sababu ya ghadhabu tu, illa na kwa sababu ya dhamiri. Kwa sababu hiyo tena mwatoa kodi; kwa kuwa wao ni watumishi wa Mungu, wakidumu katika kazi hiyohiyo. Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru: astahiliye khofu, khofu; astahiliye heshima, heshima. Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendae mtu mwenzake ameitimiza sharia. Maana ile, Usizini, Usiue, Usiibe, Usishududu uwongo, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani wako kama nafsi yako. Peudo halimfanyizii jirani neno baya; bassi pendo ndio utimilifu wa sharia. Na hayo, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia: kwa maana sasa wokofu u karibu yetu kuliko tulipoamini. Usiku unakwisha, mchana umekaribia; bassi tuyavue matendo ya giza, tuzivae silaha za nuru. Kama ilivyokhusika na mchana tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufasiki na uasharati, si kwa ugomvi na wivu. Bali mvaeni Bwana Yesu, wala msitafakari mahitaji ya mwili, nisije mkawasha tamaa zake. LAKINI yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, illakini msimhukumu mawazo yake. Mtu mmoja ana imani, anakula vyote, lakini yeye aliye dhaifu hula mboga. Yeye alae asimdharau yeye asiyekula, nae asiyekula asimhukumu yeye alae; kwa maana Mungu amemkubali. Wewe u nani unaemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa Bwana wake mwenyewe husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, maana Bwana aweza kumsimamisha. Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwingine aona siku zote kuwa sawa sawa. Killa mtu athuhutike katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishae siku, kwa Bwana aiadhimisha; na yeye asiyeadhimisha siku, haiadhimishi kwa Bwana; nae alae, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; nae asiokula, hali kwa Bwana, nae amshukuru Mungu. Kwa sababu hapana mtu miongoni mwenu aishiye kwa nafsi yake, wala hapana afae kwa nafsi yake. Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Bassi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana. Maana Kristo alikufa akafufuka akawa hayi tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hayi pia. Lakini wewe je! mbona wamhukumu ndugu yako? na wewe je! mbona wamdbarau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo. Kwa maana imeandikwa, Kwa uhayi wangu, anena Bwana, magoti yote yatapigwa mbele zangu, Na ndimi zote zitamkiri Mungu. Bassi kama ni hivyo, killa mtu miongoni mwetu atatoa khabari za nafsi yake mbele za Mungu. Bassi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali mtoe hukumu hii, ndugu asitiwe kitu cha kumkwaza au cha kumwangusha. Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najis asili yake, lakini kwake huyu akionae kitu kuwa najis, kwake huyo kitu kile ni najis. Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambae Kristo alikufa kwa ajili yake. Bassi, usitajwe vibaya kwa huo wema wenu. Maana ufalme wa Muugu si kula na kunywa, bali baki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. Kwa kuwa yeye amtumikiae Kristo katika mambo haya humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wana Adamu. Bassi kama ni hivyo, tufuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana. Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Vyote ni safi; bali ni vibaya mtu kula akajikwaza. Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno ambalo ndugu yako hukwazwa au kuangushwa au kuwa dhaifu. Je! unayo imani? Uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Yu kheri mtu yule asiyejihukumu katika neno lile alikubalilo. Lakini aliye na mashaka, kama akila, amehukumiwa, kwa maana hakula kwa imani. Na killa tendo lisilotoka katika imani ni dhambi. BASSI imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza nafsi zetu. Killa mtu miongoni mwetu ampendeze jirani yake apate wema akajengwe. Kwa maana Kristo nae hakujipendeza nafsi yake; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu yalinipata mimi. Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa kutufundisha sisi, illi kwa uvumilivu na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini. Na Mungu mwenye uvumilivu na faraja awajalieni kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa namna ya Yesu Kristo; illi kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa liwima wetu Yesu Kristo. Kwa hiyo mkaribishane, kama nae Kristo alivyotukaribisha, illi Mungu atukuzwe. Bassi nasema, Yesu Kristo amefanyika mkhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithubutishe ahadi walizopewa haha zetu; nao Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa sababu hii nitakusifu katika Mataifa, Na jina lako nitaliimba. Na tena anena, Furahini, Mataifa, pamoja na watu wake. Na tena, Msifuni Bwana, Mataifa wote; Mpeni sifa watu wote. Na tena Isaya anena, Litakuwa shina la Yesse, Nae aondokeae kuwatawala Mataifa; ndiye Mataifa watakaemtumaini. Bassi Mungu wa tumaini awajazeni furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mataktifu. Na mimi mwenyewe, ndugu zangu, nimehakikishwa kwa khahari zenu kama ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana. Lakini nimewaandikieni, ndugu zangu, kwa ujasiri zaidi katika sehemu za waraka huu kana kwamba nawakumbusheni, kwa neema ile niliyopewa na Mungu, illi niwe kuhani wa Yesu Kristo katika watu wa mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu. Bassi, nina sababu ya kujisifu katika Kristo Yesu mbele za Mungu. Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yanga, mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo, kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu; hatta ikawa tangu Yerusalemi, na kando kando yake, hatta Illuriko nimekwisha kuikhubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu, kadhalika nikijitahidi kuikhubiri Injili, nisikhubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine, bali kama ilivyoandikwa, Wale wasiokhubiriwa khahari zake wafaona, Na wale wasiosikia watafahamu. Ndio sababu nalizuiwa marra nyingi nisije kwenu. Lakini sasa, kwa kuwa sina wasaa tena pande hizi, tena tangu miaka mengi nikiwa na shauku kuja kwenu; wakati wo wote nitakaosafiri kwenda Hispania nitakuja kwenu, kwa maana nataraja kuwaona ninyi katika kusafiri kwangu, na kupelekwa mbele nanyi, moyo wangu ushibe kwenu ijapokuwa ni kidogo. Na sasa ninakwenda Yerusalemi, nikiwakhudumu watakatifu; maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo kwa ajili ya watakatifu katika Yerusalemi walio maskini. Naam, imewapendeza, tena wanawiwa nao. Kwa maana ikiwa mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwakhudumu kwa mambo yao ya mwili. Bassi nikiisha kumaliza hazi hii, na kuwatilia muhuri tunda hili, nitapita kwenu na kutoka kwenu nitakwenda Hispania. Nami najua ya kuwa nikija kwenu nitakuja kwa utimilifu wa haraka ya Injili ya Kristo. Nakusihini, ndugu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami kwa maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu, niokolewe nao waasio katika Yahudi, na tena khuduma yangu niliyo nayo huko Yerusalemi ipate kibali kwa watakatifu, nipate kufika kwenu kwa furaha, kama Mungu akipenda, nikapate kupumzika pamoja nanyi. Mungu wa amani awe pamoja nanyi nyote. Amin. NAWAPENI sifa njema za Foibe ndugu yetu, aliye mwenye khuduma katika kanisa lilioko Kenkrea, illi mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu, mkamsaidie katika neno lo lote atakalohitaji kwenu, kwa sababu yeye nae amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia na mimi pia. Nisalimieni Priska na Akula, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu, waliokuwa tayari hatta kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, illa na makanisa ya mataifa yote pia; nisalimieni kanisa lililomo katika nyumba yao. Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo. Nisalimieni Mariamu, aliyejitaabisha sana kwa ajili yetu. Nisalimieni Androniko na Junia; jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, walio maarufu katika mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu. Nisalimieni Amplia, mpenzi wangu katika Bwana. Nisalimieni Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Staku, mpenzi wangu. Nisalimieni Apelle, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Nisalimieni watu wa nyumba ya Aristobulo. Nisalimieni Herodioni, jamaa yangu. Nisalimieni watu wa nyumba ya Nakisso, walio katika Kristo. Nisalimieni Trufina na Trufosa, wenye ijtihadi katika Kristo. Nisalimieni Rufo, mteule katika Kristo, na mama yake, aliye mama yangu pia. Nisalimieni Asunkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma, na ndugu walio pamoja nao. Nisalimieni Filologo na Julia, Nereu na ndugu yake, na Olumpa, na watakatifu wote walio pamoja nao. Salimianeni kwa busu takatifu. Makanisa yote ya Kristo yawasalimu. Nawasihini, ndugu, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao. Kwa sababu bao ndio wasiomtumikia Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wasio wabaya. Maana utii wenu umewafikilia watu wote; bassi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka mwe wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya. Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu kwa upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi. Timotheo, mtenda kazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, na Yason, na Sosipatro, jamaa zangu. Mimi Tertio, niliyeandika waraka huu, nawasalimu katika Bwana. Gayo, mwenyeji wangu na wa Kanisa lote pia awasalimu. Erasto, wakili wa mji awasalimu, na Kwarto, ndugu yetu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi nyote. Amin. Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele, ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulika na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, illi waitii imani; yeye ndiye Mungu mwenye hekima peke yake; na atukuzwe kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amin. PAOLO, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, lililotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo killa mahali, Bwana wao na wetu: Neema na iwe kwenu, na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo. Namshukuru Mungu wangu siku zote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu; kwa kuwa katika killa jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote; kama ushuhuda wa Kristo ulivyothubutika kwenu; hatta hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; na yeye atawathubutisheni hatta mwisho, msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. Mungu ni mwaminifu, ambae mliitwa nae muingie katika ushirika wa Mwana wake, Yesu Kristo Bwana wetu. Nawasihi ninyi, ndugu, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mnene nyote mamoja, pasiwe kwenu faraka, bali mwe mmekhitimu katika nia moja na shauri moja. Kwa maana nimearifiwa khabari zenu, ndugu, na wale walio wa nyumba ya Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu. Bassi, nasema neno hili, ya kwamba killa mtu wa kwenu husema, Mimi wa Paolo, na mimi wa Apollo, na mimi wa Kefa, na mimi wa Kristo. Je! Kristo amegawanyika? Paolo alisulibiwa kwa ajili yenu? An mlibatizwa kwa jina la Paolo? Namshukuru Mungu, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, illa Krispo na Gayo; mtu asije akasema kwamba nimebatiza kwa jina langu mwenyewe. Tena nalibatiza watu wa nyumba ya Stefano; zaidi ya hao, sijui kama nalimbatiza mtu mwingine. Maana Kristo hakunituma illi nibatize, bali niikhubiri Injili; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo nsije nkabatilika. Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. Maana imeandikwa Nitaharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa. Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mleta hoja wa dunia bii? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia liii kuwa upumbavu? Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upumbavu wa lile neno linalokhubiriwa. Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima; bali sisi tunamkhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upumbavu, bali kwao waitwao, Wayahudi na Wayunani pia, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu. Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wana Adamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wana Adamu. Maana angalieni wito wenu, ndugu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo waliokwitwa; bali Mungu aliyachagua mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena alivichagua vitu dhaifu vya dunia illi wenye nguvu waaibishwe; nae alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, na vitu ambavyo haviko, illi avibatilishe vilivyoko; mwenye mwili aliye yote asije akajisifu mbele ya Mungu. Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyekuwa kwenu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakatifu na ukombozi; kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye ajisifuye ajisifu katika Bwana. NAMI nilipokuja kwenu ndugu, sikuja niwakhubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima. Maana naliazimu nisijue neno kwenu illa Yesu Kristo, nae amesulibiwa. Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na khofu na matetemeko mengi. Na neno langu na kukhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima ya kibinadamu yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho zenye nguvu, imani yenu isiwe katika hekima ya wana Adamu, bali katika nguvu za Mungu. Illakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; nayo si hekima ya dunia hii, wala yao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilishwa; bali twanena hekima ya Mungu katika fumbo, ile iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu asili, kwa utukufu wetu; ambayo wenye kutawala dunia hii hawakuijua hatta mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu; lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, Wala hayakuingia katika moyo wa kibinadamu, Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho yake. Maana Roho huchunguza yote, hatta mafumbo ya Mungu. Maana ni nani ayajuae mambo ya bin Adamu illa roho ya bin Adamu iliyo ndani yake? Na vivyo hivyo mambo ya Mungu hakuna ayajuae illa Roho ya Mungu. Na sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho itokayo kwa Mungu, tupate kuyajua tuliyokarimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya binadamu, bali tuliyofimdishwa na Roho, tukiyalinganisha mamho ya rohoni na mambo va rohoni. Bassi mwana Adamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Mungu; maana kwake huyu ni mapumbavu, wala hawezi kuyajua, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huvatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. Maana ni nani aliyejua nia ya Bwana, amwelemishe? Lakini sisi tuna nia ya Kristo. NA mimi, ndugu, sikuweza kunena nanyi kama na watu wenye tabia za rohoni, bali kama na watu wenye tabia za mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo. Nimewanywesha maziwa, sikuwalisha chakula; kwa maana mlikuwa hamjakiweza; naam, hatta sasa hamkiwezi, kwa maana hatta sasa m watu wa tabia za mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina na faraka, je! si watu wa tabia za mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu. Maana hapo mtu mmoja anenapo, Mimi ni wa Paolo; na mwingine, Mimi ni wa Apolio, je! hamwi watu wa tabia za mwilini? Bassi Apollo ni nani? na Paolo ni nani? Ni wakhudumu ambao kwao mliamini; na killa mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apollo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Kama ni hivyo, apandae si kitu, wala atiae maji, bali Mungu akuzae. Bassi yeye apandae, na yeye atiae maji ni kitu kimoja, na killa mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe. Maana ninyi mwafanya kazi pamoja na Mungu: ninyi m shamba la Mungu, m jengo la Mungu. Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, nimeuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini killa mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake. Maana msingi wa namna nyingine hapana mtu awezae kuweka, illa ule uliokwisha kuwekwa, yaani Yesu Kristo. Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huu dhahabu au fedha au vitu vya thamani au miti au majani an manyasi, kazi ya killa mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto utajaribu kazi ya killa mtu, ni wa namna gani. Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. Kazi ya mtu ikiteketea, atapata khasara; lakini yeye mwenyewe ataokolewa; lakini kule kuokolewa kama kwa moto. Hamjui ya kuwa ninyi hekalu ya Mungu, na ya kuwa Roho Mtakatifu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiiharibu hekalu ya Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu ya Mungu ni takatifu, ambayo ni ninyi. Mtu asijidanganye nafsi yake: kama mtu akijiona kuwa mweuye hekima kati yeuu katika dunia hii, na awe mpumbavu, apate kuwa mwenye hekima. Maana hekima ya dunia hii ni upumbavu mbele ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasae wenye hekima katika hila yao. Na tena, Bwana anajua mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni ya ubatili. Bassi, asijisifu mtu katika wana Adamu. Kwa maana vyote ni vyenu; ikiwa ni Paolo, au Apollo, au Kefa, au dunia, au uzima, au mauti, au vile vilivyo sasa, au vile vitakavyokuwa, vyote ni vyenu, na ninyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu. MTU na atubesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Tena inayohitajiwa katika mawakili, ndio mtu aonekane amini. Kwangu, lakini, si kitu kabisa nibukumiwe na ninyi, ama na hukumu ya kibinadamu, wala sijihukumu hatta nafsi yangu. Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabikiwi haki kwa ajili hiyo; illa aninukumuye ni Bwana. Bassi msihukumu neno kabla ya wakati wake, mpaka ajapo Bwana; nae atayamulika yaliyosetirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo killa mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu. Mambo haya, ndugu, nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na wa Apollo kwa ajili yemi, illi kwa khabari zetu mpate kujifunza katika fikara zenu kutokuruka mpaka wa yale yaliyoandikwa; mtu mmoja asijivune juu ya mwenziwe, kwa ajili ya mtu mwingine. Maana ni nani anaekupambanua na mwingine? na una, nini usiyoipokea? Na iwapo uliipokea, wajisifiani kana kwamba hukuipokea? Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Na ingekuwa kheri kama mngalimiliki, illi sisi nasi tumiliki pamoja nanyi. Maana nadhani ya ku wa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho kama watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia na malaika na wana Adamu. Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi wenye akili katika Kristo; sisi dhaifu, lakini ninyi hodari; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima. Hatta saa hii ya sasa, tuna njaa na kiu, tu uchi, twapigwa makofi, hatuna makao; tena twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twavumilia; tukisingiziwa twasihi: tumefanywa kama takataka za dunia, na kifusi cha vitu vyote hatta sasa. Siyaandiki haya illi kuwatahayarisha, hali kuwaonya kama watoto niwapendao. Maana ijapokuwa mna waalimu elfu katika Kristo, illakini hamna baba wengi. Maana mimi ndiye aliyewazaa katika Kristo Yesu kwa Injili. Bassi, nawasihini, mwe wafuasi wangu. Kwa hiyo nalimtuma Timotheo kwenu, aliye mwana wangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakaewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama nifundishavyo killa pahali katika killa kanisa. Wengine wamejivuna kana kwamba siji kwenu. Lakini nitakuja kwemi upesi, Bwana akipenda, nami nitajua, si neno lao waliojivuna, bali nguvu zao. Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, hali katika nguvu. Mnataka nini? Nije kwenu na fimbo, au katika upendo na roho ya upole? YAKINI khabari imeenea ya kama kwenu kuna zina, na zina hiyo ya namna isiyonenwa hatta katika mataifa, kwamba mtu awe na mke wa baba yake. Nanyi minejivuna wala hamkusikitika illi aondolewe kati yenu yeye aliyetenda jambo hilo. Kwa maana mimi kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo. Katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na nweza wa Bwana wetu Yesu Kristo, kumtolea Shetani mtu huyo, mwili uadhibiwe, illi roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu. Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulitia chachu donge zima? Bassi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, illi mwe donge jipya, kama vule mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka yetu amekwisha kutolewa sadaka kwa ajili yetu, yaani Kristo; bassi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochacha, ndio weupe wa moyo na kweli. Naliwaandikieni katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. Sisemi msichangamane kabisa kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani an wanyangʼanyi, an wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. Lakini sasa nimewaandikieni kwamba msichangamane na mtu aitwae ndugu, akiwa mzinzi au mwenye kutamani an mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnangʼanyi; mtu wa namna hii msikubali hatta kula nae. Maana yanikhusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu walio ndani? Bali hao walio nje Mungu atawahukumu. Mwondoeni mtu yule mbaya, asikae kwenu. JE! mtu wa kwenu akiwa na neno juu ya mwenzake athubutu kuhukumiwa mbele ya wasio haki wala si mbele ya watakatifu? Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! hamstahili kuhukumu hukumu zilizo ndogo? Hamjui ya kuwa tutawahukumu malaika, bassi si zaidi sana mambo ya maisha haya? Bassi, mkiwa ita mahali yanapohukumiwa mambo ya maisha haya, wekeni hao waliohesabiwa kuwa si kitu katika kanisa. Nasema haya nipate kuwatahayarisheni. Je! ndivyo hivyo, kwamba kwenu hakuna hatta mtu mmoja mwenye hekima, awezae kukata maneno ya ndugu zake? Bali mwashitakiana, ndugu na ndugu, tena mbele yao wasioamini. Bassi imekuwa upungufu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyangʼanywa mali zenu? Bali ninyi mwadhulumu watu na kunyangʼanya mali zao; naam, za ndugu zenu. Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike. Waasharati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wa kike, wala wafira, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyangʼanyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hizi; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa kuwa na haki katika jina la Bwana Yesu na katika Roho ya Mungu wetu. Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote. Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu ataharibu vyote viwili, tumbo na vyakula. Na mwili si kwa zina, hali ni kwa Bwana, nae Bwana ni kwa mwili. Na Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua na sisi kwa uweza wake. Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Bassi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaha? Hasha! Hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja nae? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja nae. Ikimbieni zina. Killa dhambi aifanyayo mwana Adamu ni nje ya mwili wake; bali yeye afanyae zina hufanya dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu ya Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyopewa na Mungu? Na ninyi si mali yenu wenyewe; Maana mlinunuliwa kwa thamani. Kwa kuwa ni hivyo, mtukuzeni Mungu kwa mwili wenu, na kwa roho yenu, ambayo ni mali ya Mungu. BASSI kwa mambo yale mliyoniandikia, ni kheri mwanamume asiguse mwanamke. Lakini kwa sababu ya mambo ya zina killa mtu na awe na mke wake mwenyewe, na killa mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mume wake; na vivyo hivyo mume hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mke wake. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, illi mpate faragha kwa kufunga na kuomba, mkajiane tena, Shetani asije akawajarihu kwa kutokuwa na kiasi kwenu. Lakini nasema haya, nikitoa idhini yangu; sitoi amri. Maana nipendalo ni watu wote wawe kama mimi nilivyo; illakini killa mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi. Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni kheri wakae kama mimi nilivyo. Lakini kama hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka moto. Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza, wala si mimi, illa Bwana, mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana nae, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe. Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana; ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke buyo anakubali kukaa nae, asimwache. Na mwanamke, ambae ana mume asiyeamini, mume huyo na anakubali kukaa nae, asimwache. Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa kwa mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa kwa mumewe; kama isingekuwa bivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu. Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani. Kwa maana wajuaje, ee mwanamke, kama ntamwokoa mume wako? au wajuaje ee mwanamume, kama utamwokoa mke wako? Lakini Mungu alivyomgawia killa mtu—kama Mungu alivyomwita killa mtu, na aenende vivyo hivyo. Na ndivyo ninavyoagiza katika Makanisa yote. Mtu fullani ameitwa nae amekwisha kutahiriwa? asijifanye kana kwamba hakutabiriwa. Mtu fullani amekwitwa nae hajatahiriwa bado? bassi asitahiriwe. Kutabiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu; bali kuzihifadhi amri za Mungu. Killa mtu na akae katika hali ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa. Je! ulikwitwa u mtumwa? usione ni vibaya; lakini kama ukiweza kuwa na uburu, afadhali kuutumia. Kwa maana yeye aliyekwitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye nae aliyekwitwa hali ya uhuru, ni mtuniwa wa Kristo. Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wana Adamu. Killa mtu, ndugu zangu, na akae katika hali hiyo hiyo aliyoitwa. Kwa khabari za mabikira sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kuwa mwaminifu kwa rehema za Bwana. Bassi, naona hili kuwa jema, kwa ajili ya shidda hii tuliyo nayo, kwamba ni vyema mtu akae kama alivyo. Umefungwa kwa mke? usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? usitafute mke. Lakini, kama ukioa, huna khatiya, na bikira akiolewa, hana khatiya; lakini watu hao watakuwa na mateso katika mwili; lakini nataka kuwazuilia haya. Lakini, nasema hivi, ndugu, muda ubakio si mwingi; bassi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana; na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi: na wale wanunuao, kama hawana kitu. Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita. Lakini nataka inwe hamna masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana; bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe. Tena iko tofauti hii kati ya mke na hikira. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu katika mwili na katika roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia, jinsi atakavyompendeza mumewe. Nasema haya niwafaidie; si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, na mpate kumkhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine. Lakini mtu awae yote akiona ya kuwa hamtendei bikira wake vipendezavyo, na ikiwa amepita uzuri wa ujana wake, na kama pana haja, bassi, afanye apendavyo, hafanyi dhambi; na waoane. Lakini yeye aliyesimama kwa uthabiti wa moyo wake, hana sharti, lakini aweza kuitawala nia yake, tena amekusudia moyoni mwake kumlinda bikira wake, atenda vyema. Bassi, amwozae bikira wake afanya vyema; na yeye asiyemwoza afanya vyema zaidi. Mwanamke hufungwa maadam mumewe yu hayi, lakini iki va mumewe amefariki, yu huru; aweza kuolewa na mtu ye yote amtakae; katika Bwana tu. Lakini yu kheri zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi; nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho ya Bwana. NA kwa khabari ya vitu, vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna elimu. Elimu huleta majivuno, bali upendo hujenga. Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua. Lakini mtu akimpenda Mungu, huyo amejuliwa nae. Bassi, kwa khabari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hapana Mungu mwingine illa mmoja tu. Kwa maana ijapokuwa wako waitwao waungu, ikiwa mbinguni au duniani, kama vile wako waungu wengi na bwana wengi; illakini kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu, aliye Baba, ambae vitu vyote vimetokana nae, na sisi twarejea kwake; na yuko Bwana mmoja Yesu Kristo, ambae kwa sabiki yake vitu vyote vimekuwa, na sisi kwa sabiki yake. Bali elimu hii haimo ndani ya watu wote; illa wengine kwa kuizoelea ile sanamu hatta sasa hula kama ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu; na dhamiri yao, kwa kuwa dhaifu, hunajisika. Lakini chakula hakituleti mbele ya Mungu; maana, tukila, hatuongezewi kitu, na tusipokula hatupunguziwi kitu. Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaze wale walio dhaifu. Kwa maana, mtu akikuona wewe uliye na elimu, umeketi chakulani ndani ya hekalu ya sanamu, je! dhamiri yake mtu huyu, kwa kuwa yu dhaifu, haitathubutika hatta ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu? Na yule aliye dhaifu aangamizwa kwa elimu yako, nae ni ndugu ambae Kristo alikufa kwa ajili yake. Na hivyo, mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuwajeruhi dhamiri zao zilizo dhaifu, mnamtenda dhambi Kristo. Kwa hiyo, chakula kikimkosesha ndugu yangu, sitakula nyama hatta milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu. JE! mimi si mtume? mimi si huru? sikumwona Yesu Kristo Bwana wetu? ninyi si kazi yangu katika Bwana? Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, illakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana muhuri ya utume wangu ni ninyi katika Bwana. Jawabu yangu kwa wale wanaoniuliza ni hii. Je! hatuna uwezo wa kula na kunywa? Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa? Au je! ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo kutokufanya kazi? Nani aendae vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Nani apandae mizabibu asiokula baadhi ya matunda yake? Au nani achungae kundi, asiyekula haadhi ya maziwa ya kundi? Je! ninanena haya kama mwana Adamu? Au sharia nayo haisemi yayo hayo? Kwa maana katika sharia ya Musa imeandikwa, Usimfunge kinywa ngʼombe apurae nafaka. Je! Mungu aangalia mambo ya ngʼombe? Au anena hayo kwa ajili yetu bassi? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu kama alimae nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini; nae apurae nafaka kwa matumaini ni haki yake kupata sehemu ya matumaini yake. Ikiwa sisi twaliwapandieni vitu vya rohoni, je! ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini? Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huu; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Injili ya Kristo. Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula sehemu ya vitu vya hekalu, na wale waikhudumiao madhbahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhbahu? Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waikhubirio Injili wamzukiwe kwa Injili. Lakini sikutumia mambo haya hatta moja. Wala sikuvaandika haya illi iwe hivyo kwangu; maana ni kheri nife kuliko mtu aliye vote abatilishe huku kujisihi kwangu. Maana, ijapokuwa naikhubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimepewa sharti; tena ole wangu nisipoikhubiri. Maana nikiitenda kazi hii kwa khiari yangu nina thawabu; kama si kwa khiari yangu, illakini nimeaminiwa uwakili. Bassi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nikhubiripo, nitatoa Injili ya Kristo bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu haki yangu niliyo nayo katika Injili. Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, illi nipate watu wengi zaidi. Nalikuwa Myahudi kwa Wayahudi, illi niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sharia, nalikuwa kama chini ya sharia, illi niwapate walio chini ya sharia. Kwa wale wasio na sharia nalikuwa kama sina sharia. Si kana kwamba sina sharia mbele za Mungu, hali mwenye sharia mbele za Kristo, illi niwapate wasio na sharia. Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, illi niwapate wanyonge. Nalikuwa mtu wa hali zote kwa watu wote, illi nipate kuwaokoa watu kwa njia zote. Nami nafanya haya yote kwa ajili ya Injili nipate kuishiriki pamoja na wengine. Hamjui, ya kuwa washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeao tunzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, illi mpate. Na killa ashindanae hujiweza katika yote: bassi hao kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi isiyoharibika. Hatta mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitae; napigana vivyo hivyo, si kama apigae hewa: bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwakhubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa. NDUGU, sitaki mkose kufahamu ya kuwa baba zetu wote walikuwa chini ya wingu, wote wakapita kati ya bahari; wote wakabatizwa kwa Musa katika wingu na katika bahari; wote wakala chakula kile kile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho: kwa maana walikunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ni Kristo. Lakini walio wengi, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. Haya yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu ya kutamani mabaya, kama wale walivyotamani. Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, wakasimama wacheze. Wala tusifanye uasharati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka muda wa siku moja watu ishirini na tatu elfu. Wala tusimjaribii Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. Wala msinungʼunike, kama wengine wao walivyommgʼunika, wakaharibiwa na mharabu. Haya yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa illi kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. Bassi anaejidhani amesimama aangalie asianguke. Jaribu halikuwapata ninyi, illa ya kadiri ya kibinadamu; na Mungu yu amini; hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, illi mweze kustahimili. Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. Nasema kama nti watu wenye akili; ufikirini ninyi ninenalo. Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule timmegao, si ushirika wa mwili wti Kristo? Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. Waangalieni Israeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! hawana shirika na madhbahu? Bassi niseme nini? ya kwamba sanamu ni kitu? au ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo mataifi, wavitolea mashetani, wala si Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. Au twamtia Bwana wivu? au tuna nguvu zaidi ya yeye? Vitu vyote ni halali kwangu; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali kwangu; hali si vitu vyote vijengavyo. Mtu asitafute kujifaidia nafsi yake, bali kumfaidia mwenzake. Killa kitu kiuzwacho sokoni kulani, bila kuulizauliza, kwa ajili ya dhamiri; maana dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo. Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kulani killa kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuulizauliza, kwa ajili ya dhamiri. Lakini mtu akiwaambieni, Kitu hiki kimetolewa sadaka kwa sanamu, msile, kwa ajili yake yeye aliyekuonyesha, na kwa ajili ya dhamiri; maana dunia ni mali ya Bwana na vitu vyote viijazavyo. Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine? Na nikitumia sehemu yangu kwa shukrani, kwa nini nitukanwe, kwa ajili ya kitu nikishukuriacho? Bassi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunaui wala Kanisa la Mungu: vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, bali faida yao walio wengi, wapafe kuokolewa. MWE wafuasi wangu kama mimi nilivyo mfuasi wa Kristo. Tena nawasifu, ndugu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale niliyowatolea vile vile kama nilivyowatolea. Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha killa mwanamume ni Kristo na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu. Killa mwanamume, asalipo, au atoapo unabii, nae ana kitu kichwani, yuaibisha kichwa chake. Bali killa mwanamke asalipo, au atoapo unabii, bila kufunika kichwa chake, yuaibisha kichwa chake; kwa maana yu sawa sawa nae aliyekata nywele zake. Maana mwanamke asipofunikwa na anyoe. Au ikiwa ni unyonge mwanamke akate nywele zake au kunyoa, na afunikwe. Kwa maana haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanake ni utukufu wa mwanamume. Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume. Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume. Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani pake, kwa ajili ya malaika. Illakini mwanamume hawi pasipo mwanamke, wala mwanamke pasipo mwanamume, katika Bwana. Maana kama vile mwanamke alitoka katika mwanamume, vivyo hivyo mwanamume nae huzaliwa na mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu. Hukumuni ninyi wenyewe katika nafsi zenu. Je! inapendeza mwanamke amwombe Mungu asipofunikwa kichwa chake? Je! sharia ya asili yenyewe haiwafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake; lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni ntukufu kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu illi ziwe badala ya mavazi. Lakini mtu aliye yote, akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu. Katika kuagiza hayo, siwasifu, ya kwamba mnakusanyika, si kwa faida bali kwa khasara; kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; na nussu kidogo nasadiki: kwa maana lazima kuwapo uzushi kwenu, illi waliokubaliwa wawe dhahiri kwenu. Bassi mkutanikapo pamoja haiwezekani kula chakula cha Bwana; kwa maana killa mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hatta huyu ana njaa, na huyu amelewa. Je! hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau Kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha wasio na kitu? Niwaambieni? niwasifu kwa haya? Siwasifu. Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowakhubirini, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, na akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangii. Vivi hivi nacho kikombe baada ya kula, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu: fanyeni liivi killa mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana killa mwulapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hatta ajapo. Bassi killa aulae mkate huu, au kunywea kikombe hiki, asivyostahili, atakuwa amejipatia khatiya kwa ajili ya mwili na damu ya Bwana. Lakini mtu ajihoji nafsi yake, ndivyo aule mkate, na kukinywea kikombe. Maana alae na kunywa asivyostahili, hula na hunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua mwili wa Bwana. Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala. Lakini tukijihukumu vema nafsi zetu, tusingehukumiwa. Tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, tusipate kupasishwa adhabu pamoja na dunia. Bassi, ndugu zangu, mkutanikapo mpate kula, mngojane; mtu akiwa na njaa, ale nyumbani; msipate kukutanika kwa hukumu. Nayo yaliyosalia nijapo nitayatengeneza. KWA khabari za karama za roho, ndugu, sitaki mkose kufahamu. Mwajua ya kuwa mlipokuwa Mataifa mlichukuliwa kwa sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa. Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hapana mtu asemae katika Roho ya Mungu, anenae, Yesu ni anathema; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu. Pana tofauti za karama; bali Roho yule yule. Pana tofauti za khuduma, na Bwana vule yule; pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu yule yule azitendae kazi zote katika wote. Lakini killa mmoja hupewa ufunuo wa Roho illi kufaidia. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, ipendavyo Roho yule yule; mwingine imani katika Roho yule yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine kutenda kazi za miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yule yule, akimgawia killa mmoja peke yake kama apendavyo yeye. Maana kama vile mwili ni mmoja, nao nna viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule mmoja, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa tukaingia katika mwili mmoja, ikiwa tu Wayahudi, au ikiwa tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja. Kwa maana mwili hauwi kiungo kimoja, bali vingi. Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! si wa mwili kwa sababu hiyo? Na sikio likisema, Mimi si jicho, mimi si wa mwili; je! si wa mwili kwa sababu hiyo? Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? kama wote ni sikio ku wapi kuona? Bali Mungu amevitia viungo killa kimoja katika mwili kama alivyotaka. Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? Lakini sasa viungo ni vingi, na mwili ni mmoja. Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina baja na ninyi. Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi. Na vile vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana. Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; hali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima kile kiungo kilichopungukiwa; illi kusiwe fitina katika mwili, hali viungo vitunzane. Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia navyo, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja. Na ninyi m mwili wa Kristo, na viungo vya mwili huo, mmoja hiki na mmoja hiki. Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kiisha miujiza, kiisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na kutawala, na aina za lugha. Je! wote ni mitume? wote ni manabii? wote ni waalimu? wote wanatenda miujiza? wote wana karama za kuponya wagonjwa? wote wanena lugha? wote wafasiri? Takeni sana karama zilizo njema zaidi. Na tena nawaonyesha njia iliyo bora sana. NIJAPOSEMA kwa lugha za wana Adamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upato uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama simi upendo, si kitu mimi. Tena mkiwagawia maskini mali yangu yote, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. Upendo husubiri, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; hustahimili yote, huamini yote, hutumaini yote, huvumilia yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; lakini ijapo iliyo kamili, iliyo kwa, sehemu itabatilika. Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto. Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule uso kwa uso: wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana jinsi ninavyojuliwa na mimi sana. Bassi, sasa inabaki imani, tumaini, upendo, hizi tatu; na iliyo kuu katika hizi ni upendo. UFUATIENI upendo, katakeni sana karama za rohoni, lakini zaidi mpate kukhutubu. Maana yeye anenae kwa lugha, haneni na watu, bali na Mungu; maana hapana asikiae; lakini anena mambo ya siri katika roho yake. Bali yeye akhutubuye, anena na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo. Anenae kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali akhutubuye hulijenga Kanisa. Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kukhutubu; maana yeye akhutubuye ni mkuu kuliko yeye anenae kwa lugha, isipokuwa afasiri, illi kusudi Kanisa lipate kujengwa. Bassi, ndugu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini, isipokuwa nanena nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya elimu, au kwa njia ya khotuba, au kwa njia ya fundisho? Hatta vitu visivyo na uhayi vitoapo sauti, ikiwa filimbi, ikiwa kinubi, visipotoa sauti zilizo na tofauti, itatambulikanaje ni wimbo gani unaopigwa kwa filimbi au kwa kinubi? Kwa maana baragumu ikitoa sauti isiyojulikana, nani atakaejifanya tayari kwa vita? Vivyo hivyo na ninyi, msipotoa kwa ile lugha neno lililo dhahiri, neno lile linenwalo litajulikanaje? Maana nitakuwa mkinena katika hewa tu. Yumkini ziko sauti za namna nyingi duniani, wala hapana moja isiyo na maana. Bassi nisipojua maana ya ile sauti nitakuwa mshenzi kwake yeye anenae; nae atakuwa mshenzi kwangu. Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni mzidi sana kuwa nazo illi kulijenga Kanisa. Kwa hiyo yeye anenae kwa lugha na aombe apewe kufasiri. Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazizai matunda. Imekuwaje, bassi? Nitaomba kwa roho, na nitaomba kwa akili; nitaimba kwa roho, na nitaimba kwa akili. Kwa maana wewe ukibariki kwa roho, yeye aketiye katika daraja ya mjinga ataitikaje, Amin, baada ya kushukuru kwako, nae hayajui usemayo? Maana ni kweli, wewe washukuru vema, bali yule mwingine hajengwi. Namshukuru Mungu wangu, nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote; lakini napenda kunena maneno matano katika kanisa kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno elfu kumi kwa lugha. Ndugu, msiwe watoto katika akili zenu; illakini katika uovu mwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mwe watu wazima. Imeandikwa katika torati ya kama, Nitanena na watu hawa kwa watu wa lugha nyingine, na kwa midomo ya wageni, na hatta hivi hawatanisikia, asema Bwana. Bassi, lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini. Lakini kukhutuhu si kwa ajili yao wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio. Bassi ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wananena kwa lugha, kiisha wakaingia watu wajinga au wasioamini, je! hawatasema ya kwamba mna wazimu? Lakini wote wakikhutubu, akaingia mtu asiyeamini, au mjinga, alaumiwa na wote, ahukumiwa na wote; na hivyo siri za moyo wake huwa wazi; na hivyo, akianguka kifudifudi, atamwabudu Mungu, akikiri ya kuwa Mungu yu kati yenu hila shaka. Imekuwaje bassi, ndugu? Mkutanapo pamoja, killa mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana lugha, ana ufunuo, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga. Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja afasiri. Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; anene na nafsi yake au na Mungu. Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapamhanue. Lakini mwingine aliyeketi, akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze. Kwa maana nyote mwaweza kukhutubu mmoja mmoja, illi wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe. Na roho za manabii huwatii manabii. Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu. Wanawake wanyamaze katika kanisa, maana hawana rukhusa kunena; bali watii, kama vile inenavyo sharia nayo. Na wakitaka kujifunza neno, na waulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu, wanawake kunena katika kanisa. Je! neno la Mungu limetoka kwenu tu? au limewafikia ninyi peke yenu? Mtu akijiona kuwa nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue haya ninayowaandikieni, ya kwamba ni maagizo ya Bwana. Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga. Kwa ajili ya hayo, ndugu, takeni sana kukhutubu, wala msikataze kunena kwa lugha. Mambo yote yatendeke kwa uzuri na kwa utaratihu. NAWAARIFU, ndugu, injili niliyowakhubirieni; ndiyo mliyoipokea, katika hiyo mnasimama, na kwa hiyo mnaokolewa, ikiwa mnayashika sana maneno niliyowakhuhirieni; isipokuwa mliamini burre. Kwa maana naliwapasha khabari ya mambo niliyoyapokea, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alionekana na Kefa; tena na wathenashara; baadae alionekana na ndugu zaidi ya khamsi mia pamoja; katika hao walio wengi wanaishi hatta sasa, wengine wamelala; baadae alionekana na Yakobo; tena na mitume wote; na mwisho wa watu wote, alionekana na mimi, kama nae aliyezaliwa si kwa wakati wake. Maana mimi mdogo katika mitume, nisiyestahili kutajwa mtume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu. Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si burre, bali nalizidi sana kushika kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali neema ya Mungu pamoja nami. Bassi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tukhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini. Bassi, ikiwa Kristo amekhubiriwa kwenu ya kwamba amefufuka, mbona wengine wenu wasema kwamba hakuna kiyama ya wafu? Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo nae hakufufuliwa: tena kama Kristo hakufufuliwa, bassi, kukhubiri kwetu ni burre na imani yenu ni burre. Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uwongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambae hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo nae hakufufuliwa. Na kama Kristo hakufufuliwa, imani yenu ni burre; mngali katika dhambi zenu. Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. Kama katika maisha haya tu tumemtumainia Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote. Lakini sasa Kristo amefufuka, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. Lakini killa mmoja mahali pake; limbuko Kristo; baadae walio wake Kristo, atakapokuja. Ndipo palipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. Maana sharti amiliki yeye, hatta awaweke maadui wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakaebatilishwa ni mauti. Kwa kuwa alitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini akisema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hamo. Bassi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe nae atatiishwa chini yake aliyemtiishia vitu vyote, illi Mungu awe yote katika yote. Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje, bassi, kama wafu hawafufuki? Kwa nini wakabatizwa kwa ajili yao? Na sisi, kwa nini tumo khatarini killa saa? Naam, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa killa siku. Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na nyama wakali kule Efeso, nina faida gani wasipofufuka wafu? Tule, tukanywe, maana kesho tutakufa. Msidanganyike: mazumgumzo mabaya huharibu tabia njema. Erevukeui kama ipasavyo, wala insiteude dhambi; kwa maana wengine hawamfahamu Mungu. Ninasema haya niwafedheheshe. Labda mtu atasema, Wafufukaje wafu? Na kwa mwili gani waja? Mpumbavu! uipandayo wewe haihuiki, isipokufa; nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, illa punje tupu, ikiwa ya nganu au nyingineyo; lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na killa mbegu mwili wake. Nyama yote si nyama moja; bali nyingine ya wana Adamu, nyingine ya ngʼombe, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki. Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fakhari yake ya mbingu ni mbali, na fakhari yake ya duniani mbali. Fakhari ya jua mbali, na fakhari ya mwezi mbali, na fakhari ya nyota mbali; maana iko tofauti ya fakhari kati ya nyota na nyota. Kadhalika na kiyama ya wafu. Hupandwa katika nharibifu; hufufuka pasipo nharibifu; hupandwa katika aibu; hufufuka katika fakhari; hupandwa katika udhaifu; hufufuka katika nguvu; hupandwa mwili wa asili; hufufuka mwili wa roho. Ikiwa upo mwili wa asili, na wa roho upo. Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza Adamu alikuwa nafsi hayi; Adamu wa mwisho roho yenye kuhuisha. Lakini hautangulii wa roho, bali wa asili; baadae huja wa roho. Mtu wa kwanza atoka katika inchi, wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. Alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. Na kama tulivyoichukua sura yake wa udongo, kadhalika tulaichukua sura yake wa mbinguni. Nisemayo ni haya, ndugu, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharihika. Angalieni, nawaambieni siri; hatutalala wote, lakini wote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa panda la mwisho; maana panda litalia, na wafu watafufuka, wasiwe na uharibifu, na sisi tutahadilika. Maana sharti huu wenye uharibifu uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Bassi, uharibifu huu utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda. U wapi, mauti, uchungu wako? Ku wapi, kaburi, kushinda kwako? Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni sharia. Lakini tumshukuru Mungu atupae kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana. KWA khabari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisaya Galatia, na ninyi fanyeni vivyo hivyo. Siku ya kwanza ya juma killa mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; changizo zisifanyike hapo nitakapokuja: nami nitakapofika nitawatuma wale mtakaowachagua kwa nyaraka, wachukue ihsani yenu hatta Yerusalemi. Na kama ikifaa niende na mimi, watasafiri pamoja nami. Lakini nitakuja kwenu, nikipita kati ya Makedonia; maana napita kati ya Makedonia. Labda nitakaa kwenu; naam, labda nitashinda kwenu wakati wa baridi, mpate kunisafirisha wakati uwao wote nitakapokwenda. Maana sitaki kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu nataraja kukaa kwenu mda wa kitambo, Bwana akinijalia. Lakini nitakaa katika Efeso mpaka Pentekote; kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wengi wako wanipingao. Lakini, Timotheo akija, angalieni akae kwenu pasipo khofu; maana anaifanya kazi ya Bwana kama mimi nami: bassi mtu aliye yote asimdharau, lakini msafirisheni kwa amani, illi aje kwangu; maana ninamtazamia pamoja na ndugu zetu. Lakini kwa khabari za Apollo, ndugu yetu, nalimsihi sana aende kwenu pamoja nao ndugu, nae hakupenda kabisa kwenda sasa; lakini atakwenda sitakupopata nafasi. Kesheni, simameni imara katika Imani, mwe waume, mwe hodari. Mambo yenu yote yatendeke katika upendo. Tena nawasihi, ndugu, (mnaijua nyumba ya Stefano kwamba ni malimbuko ya Akaia, nao wamejitia katika kazi ya kuwakhudumu watakatifu), bassi watiini watu kama hawa, na killa mtu afanyae kazi pamoja nao, na kujitaabisha. Nami nafurahi, kwa sababu ya kuwako kwao Stefano na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikarimia kwa wingi nilivopungukiwa kwenu. Maana wamenihurudisha roho yangu, na roho zenu pia; bassi wajueni sana watu kama hao. Makanisa ya Asia wawasalimu. Akula na Priskilla wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililo ndani ya nyumba yao. Ndugu wote wawasalimu. Kasalimianeni kwa busu takatifu. Hii ni salamu yangu mimi Paolo kwa nikono wangu mwenyewe. Mtu aliye yote asiyempenda Bwana Yesu Kristo, na awe anathema. Maranatha. Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja nanyi. Pendo langu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu. Amin. PAOLO, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timothieo ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, pamoja na watakatifu wote walio katika inchi yote ya Akaia: Neema iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo. Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; atufarijiye katika shidda zetu zote illi tupate kuwafariji wale walio katika shidda za namna zote, kwa faraja tunazofarijiwa na Mungu. Kwa kuwa vile vile kama mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo. Lakini ikiwa sisi tu katika shidda, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokofu wenu, ufanyao kazi yake kwa kuvumilia mateso yale yale tuteswayo na sisi: au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokofu wenu. Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa vile vile kama mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo m washiriki wa zile faraja. Maana hatupendi, ndugu, msijue khabari ya shidda ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hatta tukakata tamaa ya kuishi. Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu, illi tusijitumainie nafsi zetu, hali Mungu, awafufuae wafu, aliyetuokoa sisi na mauti kuu namna ile, tena ataokoa; ambae tumemtumainia kwamba atazidi kutuokoa; ninyi nanyi mkisaidiana kwa ajili yetu katika kuomba, illi, kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa kazi ya watu wengi, watu wengi watoe mashukuru kwa ajili yetu. Hwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa unyofu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu, si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu, tulienenda katika dunia, na khassa kwenu ninyi. Maana hatuwaandikii ninyi neno, illa yale msomayo, au kuyakiri; nami nataraja ya kuwa mtayakiri hatta mwisho; vile vile kama mlivyotukiri kwa sehemu, ya kwamba sisi tu sababu ya kujisifu kwenu, kama ninyi mlivyo kwetu sisi, katika siku ile ya Bwana Yesu. Na nikiwa na timiaini hilo nalitaka kwenda kwenu hapo kwanza, illi mpate karama ya pili; na kupita kwenu na kuendelea hatta Umakedoni; na tena toka Makedonia kurudi kwenu na kusafirishwa nanyi kwenda Yahudi. Bassi, nilipokusudia haya nalitumia kigeugeu; au niyakusudiayo, nayakusudia kwa jinsi ya mwili illi iwe hivi kwangu, kusema ndiyo, ndiyo, na siyo, siyo? Lakini kama Mungu alivyo mwaminifu, neno letu kwenu halikuwa ndiyo na siyo. Maana Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, aliyekhubiriwa na sisi kati yenu, na mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa ndiyo na siyo; bali katika yeye ndiyo imepata kuwako. Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo; na katika yeye ni Amin, Mungu apate kutukuzwa kwa kazi yetu. Bassi Yeye atufanyae imara pamoja na ninyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu, nae ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu. Lakini mimi namwitia Mungu awe shahidi juu ya roho yangu, ya kwamba, kwa kuwahurumia sijaenda Korintho. Si kwamba tunatawala imani yenu; hali tu wasaidizi wa furaha yenu; maana mnasimama kwa imani. LAKINI nafsini mwangu nalikusudia hivi, nisije kwenu tena kwa huzuni. Maana mimi nikiwatia huzuni, hassi ni nani anifurahishae illa yeye ahuzunishwae nami? Nami naliwaandikia neno lili hili, illi, nijapo nisitiwe huzuni na wale ambao ilinipasa kuwafurahia; nikiwatumainia ninyi nyote kwamba furaha yangu ni yenu nyote pia. Maana katika shidda nyingi na dhiiki ya moyo niliwaandikieni nikitoka machozi mengi; si kwamba mhuzunishwe, bali mpate kujua upendo wangu nilio nao kwenu jinsi ulivyo mwingi. Lakini iwapo mtu amehuzunisha, hakunihuzunisha mimi, bali kwa sehemu ninyi nyote, nisije nikawalemea. Yamtosha mtu wa jinsi hii adhabu ile aliyopewa na walio wengi; hatta, kiuyume cha hiyo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyu asije akatoswa katika huzuni ipitayo kiasi. Kwa hiyo nawasihi kumthubutishia upendo wenu. Maana naliandika kwa sababu hii pia, illi nipate bayana kwenu kwamba m wenye kutii katika mambo yote. Maana kama mkimsamehe mtu lo lote, na mimi; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele ya Kristo, Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana sisi si wajinga, tunajua fikara zake. Bassi nilipofika Troa kwa ajili ya Injili ya Kristo nikafunguliwa mlango katika Bwana, sikupata raha nafsini mwangu, kwa sababu sikumwona Tito ndugu yangu, bali niliagana nao, nikaondoka kwenda Makedonia. Mungu ashukuriwe, anaetushangiliza daima katika Kristo, na kuyadhihirisha manukato ya hawa wamjuao killa pahali kwa kazi yetu. Kwa maana sisi tu manukato va Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea; katika hao wa kwanza manukato ya mauti yao waendao hatta mauti; katika hao wengine manukato ya uzima wao waendao hatta uzima. Na nani atoshae kwa mambo haya? Kwa maana sisi si kama wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama watu wasemao kwa weupe wa moyo, kaina watu watumwao na Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo. JE! tunaanza tena kujisifu nafsi zetu? au tunahitaji, kama wengine, barua zenye sifa zetu kwenu, au zitokazo kwenu? Barua yetu ni ninyi iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote; mnadhihirishwa kuwa m barua ya Kristo iliyo kazi ya khuduma yetu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho ya Mungu aliye hayi; si katika vibao vya mawe, bali katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama. Na tumaini hiio tunalo mbele za Mungu kwa Kristo; si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu, aliyetutosheleza kuwa wakhudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha. Bassi, ikiwa khuduma ya mauti katika maandiko, iliyochorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hatta wana wa Israeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao utukufu uliokuwa ukibatilika; je! khuduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu? Kwa maana ikiwa khuduma ya hukumu ina utukufu, khuduma ya haki ina utukufu unaozidi sana. Maana hatta ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu kwa sababu hii, kwa ajili ya utukufu uzidio sana. Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu ukomao, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu udumuo. Bassi, kwa kuwa tuna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi; nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, illi wana wa Israeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika; pamoja na hayo fikara zao zilitiwa ugumu; kwa maana hatta leo utaji huo huo, wakati lisomwapo Agano la Kale, wakaa, haukuondolewa; ambao buoudolewa katika Kristo; bali hatta leo, Musa asomwapo, utaji huikalia mioyo yao. Lakini wakati wo wote itakapomgeukia Bwana ule utaji huondolewa. Bassi Bwana ndiye Roho huyo; walakini alipo Roho ya Bwana, hapo ndipo panapo uhuru. Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiuangalia utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa na kufananishwa na mfano huo huo, toka utukufu hatta utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana aliye Roho. KWA sababu hiyo, kwa kuwa tuna khuduma hii, kwa jinsi tulivyorehemiwa, hatulegei; lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyosetirika, wala hatuenendi kwa ujanja, wala kulichanganya neno la Mungu na uwongo; hali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mhele za Mungu. Ijapokuwa injili yetu imesetirika, imesetirika kwao wanaopotea; ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. Kwa maana hatujikhubiri nafsi zetu, hali Kristo Yesu Bwana; na sisi wenyewe kuwa watumishi wenu kwa ajili ya Kristo. Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itangʼaa toka gizani, ndive aliyengʼaa mioyoni mwetu, atupe nuru va elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo. Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, illi adhama ya uwezo iwe ya Mungu, wala si yetu sisi. Pande zote twasongwa, bali hatudhiikiki; twaona mashaka, hali hatukati tamaa; twaudhiwa, hali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi; siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake Yesu, illi uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu. Maana sisi tulio hayi siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, illi uzima wa Yesu udhihirishwe katika miili yetu ipatwayo na manti. Bassi hapo mauti hufanya kazi yake ndani yetu, hali nzima ndani yenu. Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani, kama ilivyoandikwa. Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena; tukijua kama yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua na sisi pamoja na Yesu, na kutuhudhurisha pamoja nanyi. Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, illi, neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao wengi mashukuru yazidishwe, Mungu akatukuzwe. Kwa hiyo hatuzimii; bali ijapokuwa mtu wetu wa nje unaharibiwa, illakini mtu wetu wa ndani unafanywa npya siku baada ya siku. Maana mateso mepesi yetu, yaliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele ulio mwingi sana zaidi; tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele. KWA maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia ikiharibiwa, tuna jengo litokalo kwa Mungu, nyumha isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele katika mbingu. Maana na sisi katika hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa vazi jingine, yaani kao letu litokalo mbinguni; ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi. Kwa maana sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, hali kuvikwa vazi jingine, illi kitu kile kipatwacho na mauti kimezwe na uzima. Bassi yeye aliyetufanya kwa ajili ya neno lili hili ni Mungu, aliyetupa arabuni ya Roho. Bassi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali ya Bwana. Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona. Lakini tuna moyo mkuu; na tunaona vema zaidi kutoka katika mwili na kukaa pamoja na Bwana. Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye. Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu ya Kristo, illi killa mtu apokee kadiri alivyotenda kwa mwili, vikiwa vyema au vikiwa vibaya. Bassi tukiijua khofu ya Bwana, twawavuta wana Adamu; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tunadhihirishwa katika dhamiri zenu pia. Maana hatujisifu nafsi zetu mbele yenu marra ya pili, bali tukiwapeni sababu ya kujisifu kwa ajili yetu, illi mpate kuwa nayo mbele yao wanaojisifu kwa mambo ya nje tu, wala si kwa mambo ya moyoni. Maana ikiwa tumerukwa na akili zetu, ni kwa ajili ya Mungu; au ikiwa tunazo akili zetu timamu, ni kwa ajili yenu. Maana upendo wa Kristo watulazimisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba ikiwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote, bassi walikufa wote; tena alikufa kwa ajili ya wote, illi walio hayi wasiwe hayi kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao. Hatta imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awae yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemjua Kristo kwa jinsi ya mwili, sasa lakini hatumjui hivi tena. Hatta imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo ni kiumbe kipya, vya kale vimepita; kumbe! vyote vimekuwa vipya. Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, nae alitupa khuduma ya upatauisho; yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; nae ametia ndani yetu neno la upatanisho. Bassi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anakusihini kwa vinywa vyetu: twawaombeni kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. Maana alimfanya yeye asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili vefu, illi sisi tuwe haki ya Mungu katika Yeye. NASI tukitenda kazi pamoja nae tunakusihini msiipokee neema ya Mungu burre, (maana anena, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokofu nilikusaidia; tazama, sasa ndio wakati uliokubalika sana; tazama, sasa ndio siku ya wokofu). Tusiwe kwao la namna yo yote katika jambo lo lote, khuduma yetu isilaumiwe; bali katika killa neno tukijipatia sifa njema, kama wakhudumu wa Mungu, katika saburi nyingi, kalika mateso, katika shidda, katika taabu, kafika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika kazi, katika kukesha, katika kufunga; katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki, katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za wema za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto, kwa utukufu na aibu, kwa kunenwa vibaya na kunenwa vyema; kama wadanganyao, bali watu wa kweli; kama wasiojulika, bali wajulikao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hayi; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa; kama wenye huzuni, bali siku zote wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali wenye vitu vyote. Vinywa vyetu vimewafunukia ninyi, enyi Wakorintho; mioyo yetu imekunjuliwa. Hamsongwi ndani yetu, bali mwasongwa katika mioyo yenu. Bassi, illi mlipe kadiri ile ile mliyopewa (nasema nanyi kama na watoto), mkunjuliwe mioyo na ninyi. Msifungiwe kongwa pamoja na wasioamini, wasio na tabia kama zenu; kwa maana pana shirika gani kati ya haki na uasi? tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Belial? Au aammiye ana sehemu gani pamoja na asiyeamini? Tena pana mapatano gani ya hekalu ya Mungu na sanama? Kwa maana ninyi hekalu la Mungu aliye hayi; kama Mungu alivyosema, ya kama, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo Tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana, Wala msiguse kitu kilicho kichafu. Nami nitawakaribisheni, Nitakuwa Baba kwenu, Na ninyi mtakuwa kwangu wana na binti, anena Bwana Mwenyiezi. BASSI, kwa kuwa tuna ahadi hizo, wapenzi, tujitakase nafsi zelu uchafu wote wa mwili na roho, tukitimiza utakatifu katika kumeha Mungu. Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu, hatukumharibu mtu, hatukumkalamkia mtu. Sisemi neno hili illi niwahukumu ninyi; kwa maana nimetangulia kusema ya kwamba ninyi m katika mioyo yetu mpaka kufa pamoja, na kuishi pamoja. Nina ujasiri mwingi kwemi; kujisifu kwangu kwa ajili yenu ni kwingi. Nimejawa na faraja, katika mateso yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi. Kwa maana hatta tulipokuwa tumelikia Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tuliteswa kote kote; nje palikuwa na vita, ndani khofu. Illakini Mungu, mwenje kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuwapo kwake Tito. Wala si kwa kuwapo kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu, akituarifu khabari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu, hatta nikazidi kufurahi. Maana ijapokuwa naliwahuzunisha kwa waraka ule sijuti, ijapokuwa nalijuta; maana naona ya kwamba waraka ule nliwahuzunisha, ijapokuwa ni kwa kitambo. Sasa nafurahi, si kwa sababu ya kuhuzunishwa ninyi, bali kwa sababu mlihuzunishwa hatta mkatuhu. Maana mlihuzunishwa mmele za Mungu, msipate khasara kwa tendo letu katika neno lo lote. Maana huzuni iliyo mbele za Mungu hufanyiza toba iletayo wokofu isiyo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanyiza mauti. Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko mbele za Mungu kwalitenda bidii ya namna gani ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na khofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi. Kwa killa njia mmejionyesha kuwa safi katika jambo hilo. Bassi, ijapokuwa naliwaandikia, sikuandika kwa ajili yake yeye aliyedhulumu, wala si kwa ajili yake aliyedhulumiwa, bali ijtihadi yenu kwa ajili yetu ipate kudhihirishwa kwenu mbele za Mungu. Kwa hiyo tulifarijiwa; na katika kufarijiwa kwetu tulifurahi sana kupita kiasi kwa sababu ya furaha ya Tito; maana roho yake imeburudishwa na ninyi nyote. Kwa maana, ikiwa nimejisifu kwake kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; hali, kama tulivyowaambieni mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli. Na mapenzi yake kwenu yamekuwa mengi kupita kiasi, akumbukapo kutii kwenu ninyi nyote, jinsi mlivyomkaribisha kwa khofu na kutetemeka. Nafurahi, kwa sababu katika killa neno nina moyo mkuu kwa ajili yenu. TENA twawaarifu ninyi, ndugu, kliahari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia; maana walipokuwa wakijaribiwa kwa shidda nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa unyofu wao. Maana nawashuhudia, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa khiari yao wenyewe walitoa vitu vyao; wakituomba pamoja na kutusihi tuipokee neema hii, na kushirikiana nao huku kuwakhudumia watakatifu. Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini, bali kwanza walijitoa nafsi zao, wakampa Bwana; kiisha wakatupa sisi pia, kwa mapenzi ya Mungu, hatta tukamwonya Tito kuwatimilizieni neema hii kama vile alivyoianza. Lakini kama mlivyo na wingi wa vitu vyote, imani, na matamko, na elimu, na bidii yote, na mapenzi yenu kwetu sisi; bassi vivyo hivyo mwe na wingi wa neema hii pia. Sineni illi kuwaamuru, bali kwa bidii ya watu wengine nijaribu unyofu wa upendo wenu. Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yetu, alipokuwa tajiri, illi ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake. Nami katika neno hili natoa shauri langu; maana neno hili lawafaa ninyi mliotangulia, wapata mwaka, licha ya kutenda hivi, hatta kutaka pia. Lakini sasa mkatimize kule kutenda nako, illi kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, vivyo hivyo mwe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo. Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo. Maana sisemi haya, illi wengine waachiliwe ninyi mkalemewe, bali mambo yawe sawa sawa: wakati huu wa sasa wingi wenu uwafae upungufu wao, illi na wingi wao uwafae ninyi upungufu wenu; illi mambo yawe sawa sawa. Kama ilivyoandikwa, Aliyekusanya vingi, hakuzidi, nae aliyekusanya vichache hakupungukiwa. Lakini Mungu ashukuriwe atiae bidii ile ile kwa ajili yenu katika moyo wa Tito. Maana alipokea yale maonyo; nae, akizidi kuwa na bidii, alisafiri kwenda kwenu kwa khiari yake mwenyewe. Na pamoja nae tukamtuma ndugu yule ambae sifa zake katika Injili zimeenea makanisani mwote. Wala si hivyo tu, bali alichaguliwa na makanisa asafiri pamoja nias katika jambo la neema hii inayokhudumiwa nasi, illi Bwana atukuzwe, ikadhihirike ya kuwa mioyo yenu ilikuwa tayari. Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu katika khabari ya karama hii inayokhudumiwa nasi; tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele ya Bwana tu, bali na mbele ya wana Adamu. Nasi pamoja nae tumemtuma ndugu yetu tuliyemwona katika mambo mengi kuwa ana bidii, na sasa ana bidii zaidi sana kwa sababu ya tumaini alilo nalo kwenu. Bassi mtu akitaka khabari za Tito, yeye ni mshirika wangu, na mtenda kazi pamoja nami; tena akitaka khabari za ndugu zetu, wao ni mitume ya makanisa, na utukufu wa Kristo. Bassi waonyesheni mbele ya makanisa bayana ya upendo wenu, na ya kujisifu kwetu kwa ajili yenu. KWA khabari za kuwakhudumia watakatifu sina haja ya kuwaandikia. Maana najua utajiri wenu, niliojisifia kwa Wamakedoni, kwamba Akaya ilikuwa tayari tangu mwaka mzima; na bidii yenu imewatia moyo watu wengi. Lakini naliwatuma ndugu, illi kujisifu kwangu kwa ajili yenu kusibatilike katika jambo hili; mpate kuwa tayari, kama nilivyosema: kusudi, wakija Wamakedoni pamoja nami, na kuwakuta hamjawa tayari, tusije tukatahayarika sisi, tusiseme ninyi, katika hali hii va kutumaini. Bassi naliona ya kuwa ni lazima niwaonye ndugu hawa watangulie kufika kwenu, na kutengeneza mapema karama yenu mliyoahidi tangu zamani, illi iwe tayari, na hivi iwe kama kipawa, wala si kama kitu kitolewacho kwa choyo. Lakini nasema neno liili, Apandae haha atavuna haha; apandae kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Killa mtu na atende alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoae kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza killa neema kwa wingi, illl ninyi, mkiwa na riziki za killa namna siku zote, mpate kuzidi sana katika killa tendo jema; kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele. Na yeye amruzukuye mbegu mwenye kupanda, atoae mkate uwe chakula, atawapeni mbegu za kupanda na kuzizidisha, atayaongeza mazao ya haki yenu; mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. Maana utumishi wa khuduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu; kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huu, mnamtukuza Mungu kwa ajili ya ntii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote. Nao wenyewe, wakiwaombea ninyi, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sanu ndani yenu. Mungu ashukuriwe kwa sababa ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu ipasavyo. NAMI Paolo, nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo, mimi niliye mnyenyekevu niwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo mwenye ujasiri kwenu; naam, naomba kwamba nikiwapo, nisiwe na ujasiri kwa uthabiti ambao nahesabu kuwa nao juu ya wale wanaodhani ya kuwasisi tunaenenda kwa jinsi ya mwili. Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; maana silaha za vita yetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu kuangusha ngome; tukiangusha mawazo na kiila kitu kilichoinuka, kijiinuacho jun ya elimu ya Mungu; na tukifanya mateka fikara zote zipate kumtii Kristo: tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia. Je! mnayaangalia yaliyo mbele ya macho yenu? Mtu akijitumainia nafsi yake ya kuwa yeye ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo na sisi tu watu wa Kristo. Maana, nijapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yetu (tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga ninyi wala si kuwaangusha), sitatahayarika; nisije nikaonekana kana kwamba nataka kuwaogofya kwa nyaraka zangu. Maana wasema, Nyaraka zake nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini yu dhaifu, na maneno yake hayawi kitu. Mtu kama huyu na afikiri hivi, ya kwamba jinsi tulivyo kwa maneno katika nyaraka tusipokuwapo, ndivyo tulivyo kwa matendo tukiwapo. Maana hatuthubutu kujihesabu pamoja nao wenye kujisifu nafsi zao, wala kujilinganisha nao: bali wao wakijipima nafsi zao na nafsi zao na wakijilinganisha nafsi zao na nafsi zao, hawana akili. Lakini sisi hatutajisifu zaidi ya kadiri yetu; bali kwa kadiri ya cheo tulichopimiwa na Mungu, yaani kadiri ya kufika hatta kwenu. Maana hatujitanui nafsi zetu kupita kadiri yetu, kana kwamba hatuwafikii ninyi; maana tulifika hatta kwenu katika injili ya Kristo; wala hatujisifu zaidi ya kadiri yetu, katika kazi za watu wengine; bali tukiwa na tumaini ya kwamba, imani yenu ikuapo, tutakuzwa kwenu kwa kadiri yetu; na kupata ziada hatta kuikhuhiri Injili katika inchi zilizo mpaka mmoja na inchi zenu; tusijisifu katika cheo cha mtu mwingine kwa mambo yaliyokwisha kutengenezwa. Lakini yeye ajisifuye, na ajisifu kukatika Bwana. Maana mtu mwenye kubaliwa si yeye ajisifuye, hali yeve asifiwae na Bwana. INGEKUWA kheri kama mngenisamehe kidogo upumbavu wangu; naam, kanisameheni. Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; maana naliwaposea mume mmoja, nimletee Kristo bikira safi. Lakini naogopa; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikara zenu, mkauacha unyofu wenu kwa Kristo. Maana yeye ajae akikhubiri Yesu mwingine ambae sisi hatukumkhubiri, au mkipokea Roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumilia nae. Maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa kitu walicho nacho mitume walio wakuu. Lakini nijapokuwa mimi ni mtu asiojua kunena, illakini hii si hali yangu katika ilmu; lakini katika killa neno tumedhihirishwa kwenu. Je! nalifanya dhambi kwa kujinyenyekea illi ninyi mtukuzwe, kwa sababu naliwakhubiri Injili ya Kristo bila ujira? Naliwanyangʼanya makanisa mengine mali yao, nikitwaa posho langu niwakhudumie ninyi. Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana ndugu walipokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; na katika mambo yote nalijilinda nafsi yangu nisiwalemee hatta kidogo; tena nitajilinda. Kama vile kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu, hapana mtu atakaenifumba kinywa katika kujisifu huku, katika mipaka ya Akaya. Kwa nini? kwa sababu siwapendi ninyi? Mungu anajua. Lakini nifanyalo nitalifunya, illi niwapinge watafutao nafasi wasipate nafasi; illi katika neno hilo wajisifulo waonekane kuwa kama sisi. Maana hawo ni mitume wa uwongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume ya Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Bassi si neno kubwa wakhudumu wake nao wakijigeuza wawe mfano wa wakhudumu wa haki. Mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao. Nasema tena mtu asidhani ya kuwa mimi ni mpumbavu; lakini mjaponidhania hivi, mnikubali kama mpumbavu; mimi nami nipate kujisifu kidogo. Nisemalo silisemi agizo la Bwana, bali kama kwa upumbavu, katika ujasiri huu wa kujisifu. Iwapo wengi wanajisifu kwa jinsi ya mwili mimi nami nitajisifu. Ninyi, kwa kuwa mna akili, mnavumilia na wajinga kwa furaha. Maana mwavumilia na mtu akiwatieni utumwani, akiwameza, akiwateka, akijikuza, akiwapiga usoni. Nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Illakini, akiwa mtu anao ujasiri kwa lo lote, (nanena kipuuzi), na mimi niuao ujasiri. Wao Waebrania? Na mimi. Wao Waisraeli? Na mimi. Wao uzao wa Ibrahimu? Na mimi. Wao wakhudumu wa Kristo? (nanena kiwazimu), mimi zaidi; kwa kazi kuzidi sana; kwa mapigo kupita kiasi; kwa vifungo kuzidi sana; kwa mauti marra nyingi. Kwa Wayahudi marra tano nalipata mapigo arubaini kasoro moja. Marra tatu nalipigwa bakora; marra moja nalipigwa mawe; marra tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini; kwa kusafiri marra nyingi; khatari za mito; khatari za wanyangʼanyi; khatari kwa jamaa; khatari kwa mataifa; khatari za mijini; khatari za jangwani; khatari za baharini; khatari kwa ndugu za uwongo; kwa kazi na kusumbuka; kwa kukesha marra nyingi; kwa njaa na kiu; kwa kufunga marra nyingi; kwa baridi na kuwa uchi. Baghairi ya mambo ya nje, yako yanijiayo killa siku, ndio maangalizi ya makanisa yote. Nani aliye dhaifu, nisiwe dhaifu na mimi? Nani aliyechukizwa na mimi nisiwake? Ikinibidi kujisifu, nitajisifia mambo ya udhaifu wangu. Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliye mtukufu hatta milele, ajua va kuwa sisemi nwongo. Katika Dameski liwali wa Areta mfalme alikuwa akiulinda mji wa Wadameski, akitaka kunikamata; nikashushwa ndani ya kapu, katika dirisha la ukutani, nikaokoka na mikono yake. SINA buddi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia njozi na mafunuo ya Bwana. Namjua mtu mmoja katika Kristo, impita sasa miaka arobatashara, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui, Mungu ajua). Mtu huyu alichukuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui: Mungu ajua): ya kuwa alichukuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwana Adamu ayanene. Kwa khabari za mtu huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa katika khabari ya udhaifu wangu. Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini nitajizuia, mtu asinihesabie zaidi ya haya ayaonayo kwangu au kuyasikiakwa kinywa changu. Na kwa sababu ya wingi wa mafunuo hayo, kwa sababu hiyo, nisipate kujivuna kupita kiasi, nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani illi anipige, nisije mkajivuna kupita kiasi. Kwa ajili ya kitu hiki nalimsihi Bwaua marra tatu kinitoke. Akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Bassi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, illi uweza wa Kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na maumivu, na dhiiki, na adha, na shidda, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo ua nguvu. Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu, nijapokuwa si kitu. Maana ishara za mtume zilitendwa kati yenu katika uvumilivu wote, kwa ishara na maajabu na nguvu. Maana ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, illa kwa kuwa mimi sikuwalemea. Mnisamehe udhalimu huo. Tazama hii ni marra ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawidemea. Maana sitafuti vitu vyenu, bali ninyi: maana haiwapasi watoto kuwawekea akiba wazazi, bali wazazi watoto. Na kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu: ingawa nizidipo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa? Lakini na iwe hivyo, mimi sikuwalemea; bali kwa kuwa mwerevu naliwapata kwa hila. Je! mtu aliye yote niliyemtuma kwenu, kwa mtu huyo naliwatoza kitu? Nalimwonya Tito, nikamtuma yule ndugu pamoja nae. Je! Tito aliwatoza kitu? Hatukuenenda kwa Roho yeye yule na katika nyayo zile zile? Mwadhani ya kuwa tunajindhuru kwenu tena? Mbele za Mungu twanena katika Kristo. Na haya yote, wapenzi, kwa ajili ya kuwajenga. Maana naogopa, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekane kwenu si kama vile mtakavyo: nisije nikakuta labuda fitina, na wivu, na hasira, na ugomvi, na masingizio, na manongʼonezo, na majivuno, na ghasia; nami nitakapokuja tena, Mungu wangu akanidhili kwenu, nikawasikitikia wengi waliokosa zamani, wala hawakutubia nchafu, na uzinzi, na uasharati walioufanya. HII ndio marra ya tatu ya mimi kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu killa neno litathubutishwa. Nimetangulia kuwaambia: na kama vile nilipokuwapo marra ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo natangulia kuwaambia wao waliofanya dhambi zamani, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia: kwa kuwa mnatafuta dalili ya Kristo, asemae ndani yangu, ambae si dhaifu kwenu, bali ana uweza ndani yenu. Maana, ijapokuwa alisulibiwa katika udhaifu, illakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; bali tutaishi pamoja nae kwa uweza wa Mungu ulio ndani yenu. Jijaribuni nafsi zenu kwamba m katika imani; jithubutisheni nafsi zenu. Au bamjijui nafsi zenu, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu isipokuwa mmekataliwa? Lakini natumaini kama mtajua ya kuwa sisi hatukukataliwa. Na namwomba Mungu, msifanye lo lote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, bali ninyi mfanye lililo jema, tujapokuwa sisi kama waliokataliwa. Maana hatuwezi kutenda neno kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli. Maana twafurahi, sisi tulipo dhaifu, na ninyi hodari. Tena twaomba hili nalo, mtimilike. Kwa biyo, naandika liayo nisipokuwapo, illi, nikiwapo, nisitumie ukali kwa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana illi kujenga wala si kubomoa. Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi. Salimianeni kwa busu takatifu. Walio watakatifu wote wawasalimu. Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. Amin. PAOLO, mtume (si mtume wa wana Adamu, wala hakutumwa na mwana Adamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua), na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia, Neema iwe kweuu, na amani itokayo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana Yesu Kristo, aliyejitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu illi atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu: ambae ana utukufu milele na milele, Amin. Nastaajabu kwa kuwa mmemwacha hivi upesi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, mkageukia injili ya namna nyingine; wala si nyingine. Lakini wapo watu wawataabishao na watakao kuigeuza injili ya Kristo. Lakini sisi au malaika wa mbinguni tukiwakhubiri ninyi injili illa hiyo tuliyowakhubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awae yote akiwakhubiri injili illa hiyo tuliyowakhubiri, na alaaniwe. Maana sasa je! nawashawishi wana Adamu au Mungu? au nataka kuwapendeza wana Adamu? Kama ningekuwa hatta sasa nawapendeza wana Adamu, singekuwa mtumwa wa Kristo. Kwa maana injili biyo niliyowakhubiri nawajulisha, ndugu, ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu. Maana sikuipokea kwa mwana Adamu wala sikufundishwa na mtu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo. Maana mmesikia khabari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi nikaliharibu, nami nalitangulia katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kushika mapokeo ya baba zangu. Lakini Mungu aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, alipoona vema kumdhihirisha Mwana wake ndani yangu, illi niwakhubiri mataifa khabari zake, marra sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu, wala sikupanda kwenda Yerusalemi kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nalikwenda zangu Arabuni nikarudi teua Dameski. Kiisha, baada ya miaka mitatu, nalipanda kwenda Yerusalemi illi nionaue na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano. Lakini sikumwona mtume mwingine illa Yakobo ndugu yake Bwana. Na bayo ninayowaandikieni, angalieni, mbele za Mungu, sisemi uwongo. Khalafu nalikwenda pande za Sham na Kilikia. Lakini sikujulika uso wangu na makanisa ya Yahudi yaliyo katika Kristo; ilia wamesikia tu ya kwamba yeye aliyetuudhi kwanza sasa anaikhubiri imani ile aliyoiharibu zamani. Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu. KIISHA, baada va miaka kumi na minane, nalipanda kwenda Yerusalemi pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito pamoja nami. Nami nalikwenda kwa kufunuliwa, nikawaeleza injili ile niikhubirivyo katika mataifa, lakini kwa faraglia kwa hao walio wenye sifa, isiwe labda napiga mbio burre au nalipiga mbio burre. Lakini Tito aliyekuwa pamoja nami, aliyekuwa Myunani, hakulazimishwa kutahiriwa: bali kwa ajili ya ndugu za uwongo walioingizwa kwa siri. Hao waliingia kwa siri wapate kuupeleleza uhuru wetu tulio nao katika Yesu Kristo illi watutie utumwani: ambao hatta saa moja hatukujitia chini yao, illi kweli ya Injili ikae pamoja nanyi. Lakini wale wenye sifa kwamba wana cheo, walivyo vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwana Adamu—nasema, wale wenye sifa hawakuniongezea kitu, bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili va wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa (maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha kwenda kwa mataifa); tena walipokwisha kuijua neema niliyopewa, Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika, illi sisi tuende kwa mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara; illa neno moja walitutakia, tuwakumbuke maskini; na neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya. Lakini Petro alipokuja Antiokia, nalishindana nae uso kwa uso, kwa sababu amepasiwa hukumu; kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikula pamoja na watu wa mataifa, illakini walipokuja akarudi nyuma akajitenga, akiwaogopa waliotahiriwa. Na Wayahudi wakajigeuza pamoja nae, hatta Barnaba nae akachukuliwa na unafiki wao. Lakini, nilipoona ya kuwa njia yao haikwenda sawa sawa na kweli ya Injili, nalimwambia Kefa mbele ya watu wote, Ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za mataifa, wala si za Wayahudi, kwa nini unawashurutisha mataifa kufuata desturi za Wayahudi? Sisi tulio Wayahudi kwa asili, wala si wenye dhambi wa mataifa, tukijua ya kuwa mwana Adamu hafanyiziwi wema kwa matendo ya sharia, hali kwa imani ya Yesu Kristo, sisi tulimwamini Yesu Kristo illi tufauyiziwe wema kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sharia; maana kwa matendo ya sharia hapana mwenye mwili atakaefanyiziwa wema. Lakini kama sisi wenyewe tulipokuwa tukitafuta kufanyiziwa wema katika Kristo, tulionekana kuwa wenye dhambi, je! Kristo amekuwa mtumishi wa dhambi? Hasha. Maana nikiyajenga tena yale niliyoyabomoa, naonyesha ya kuwa mimi mwenyewe ui mkosaji. Maana mimi kwa sharia naliifia sharia illi nimwishie Mungu. Nimesulibiwa pamoja na Kristo, illakini ni hayi; wala si mimi tena, bali Kristo yu hayi ndani yangu; na uhayi nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. Siibatili neema ya Munga. Maana, ikiwa haki hupatikana kwa sharia, bassi, Kristo alikufa burre. ENYI Wagalatia msio akili, ni nani aliyewaloga, msiisadiki kweli, ninyi ambao Kristo aliwekwa mbele ya macho yemi ya kuwa amesulibiwa? Nataka kujifunza neno bili moja kwenu. Mlipokea Roho kwa matendo ya sharia, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Je! m wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa kwa mwili? Mmepatikana na mateso makubwa namna hii burre? ikiwa ni burre. Bassi, yeye awaruzukiae Roho na kufanya miujiza kati yenu, afanya hayo kwa matendo ya sharia, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa kuwa ana haki. Jueni bassi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio walio wana wa Ibrahimu. Na andiko, likiona tangu zamani kwamba Mungu atawafanyizia mataifa wema kwa imani, lilimkhubiri Ibrahimu Injili zamani, ya kama, Kwa wewe mataifa yote yatabarikiwa. Bassi walio wra imani wabarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwaminifu. Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sharia, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu asiodumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sharia, ayafanye. Ni dhahiri ya kwamba hapana mtu ahesabiwae kuwa ana haki nibele za Mungu katika sharia; kwa sababu Mwenye haki ataisbi kwa imani. Na sharia haikuja kwa imani, bali, Mtu atendae hayo ataishi katika hayo. Kristo alitukomboa na laana ya sharia, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu: maaua imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu atuudikwae juu ya mti: illi baraka ya Ibrahimu iwafikilie mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupewa ahadi ya Roho kwa njia ya imani. Ndugu, nanena kwa jiusi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwana Adamu, illakini likiisha kuthuimtika, hapana mtu alibatilishae, wala kuliongeza neno. Ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa uzao, kana kwamba ni watu wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani Kristo. Nisemayo ni haya; agano lililofanywa imara kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka aruba mia na thelathini baadae hailitangui, hatta kuibatilisha abadi. Kwa maana urithi nkiwa kwa sharia, hauwi tena kwa abadi; lakini Mungu alimkarimia Ibrahimu kwa abadi. Torali ni nini bassi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hatta mzao atakapokuja aliyepewa ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe. Aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni mmoja. Bassi, torati haipatani na ahadi za Mungu? Hasha. Kwa kuwa, kama ingalitolewa sharia iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sharia. Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi waaminio wapewe ahadi kwa imani ya Yesu Kristo. Lakini kabla ya kuja imani tulikuwa tumewekwa chini ya sharia, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa. Na hivyo sharia imekuwa mwalimu wa kutuleta kwa Kristo, illi tufanyiziwe wema kwa imani. Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini va mwalimu. Maana ninyi nyote ni wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo. Maana ninyi nyote mliobatizwa na kuingizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu. Na kama ninyi ni wa Kristo, bassi, nimekuwa mzao wa Ibrahimu, na wrarithi kwa ahadi. LAKINI nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, ajapokuwa bwana wa yote; bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hatta muhulla uliokwisha kuamriwa na baba. Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia. Hatta ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwana wake, amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sharia, illi awakomboe waliokuwa chini ya sharia, tupate kupokea hali ya wana. Na kwa kuwa ninyi ni wana, Mungu alimtuma Roho ya Mwana wake mioyoni mwenu, aliaye, Abba, Baba. Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali mwana; na kama u mwana, bassi, u mrithi wa Mungu kwa Kristo. Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkujua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu. Bali sasa, mkiisha kumjua Mungu, ya nini kurejea tena kwa mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge na yenye upungufu ambayo mnataka kuyatumikia tena. Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka. Nawachelea, isiwe labda nimejitaabisha burre kwenu. Nakusihini, ndugu, mwe kama mimi, maana mimi kama ninyi. Hamkunidhulumu neno. Lakini mwajua ya kuwa naliwakhubiri Injili marra ya kwanza kwa sababu ya ndhaifu wa mwili; na jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Yesu Kristo. Ku wapi, bassi, kule kujiita kheri? Maana nawashuhudia, kwamba, kama ingaliwezekana, mngaliugʼoa macho yenu, mkanipa mimi. Bassi, je! nimekuwa adui wenu kwa sababu nawa ambieni yaliyo kweli? Wao wawaonea uinyi shauku lakini si kwa vema bali wanataka kuwafungia mlango illi ninyi mwaonee wao shauku. Na ni vyema kuonewa shauku katika neno jema siku zote, wala si wakati nikiwapo mimi tu. Vitoto vyangu, ambao nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu. Naam, ningependa kuwa pamoja nanyi sasa, na kuigeuza santi yangu; maana nawaonea maashaka. Niambieni, ninyi ninaotaka kuwa chini ya sharia, hamwisikii torati? Kwa maana, imeandikwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili, mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio maagano mawili, moja toka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ndio Hajir. Maana Hajir ni mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemi wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto wake. Bali Yerusalemi wa juu ni mwungwana, ndio mama yetu sisi. Kwa maana imeandikwa, Fanya furaha, tassa usiyezaa; Paaza sauti, ukalie, wewe usiye na utungu; Kwa sababu watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko wake aliye na mume. Sisi, ndugu, kama Isaak, tu watoto wa ahadi. Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alimwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, vivyo hivyo na sasa. Lakini lanenani Andiko? Mtupe nje mjakazi na mwana wake, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. Kwa hiyo, ndugu, sisi si watoto wa mjakazi, hali wake aliye mwungwana. KRISTO alitufanya huru kwa uhuru; bassi, simameni, msinaswe tena kwa kifungo cha utumwa. Fahamuni, mimi Paolo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno. Tena namshuhudia killa mtu atahiriwae, kwamba ni wajibu wake kuitimiza sharia yote. Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kufanyiziwa wema kwa sharia; mmeanguka toka hali ya neema. Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la wema kwa njia ya imani. Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo. Mlikuwa mkipiga mbio vizuri: ni nani aliyewazuia msiitii kweli? Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye aliyewaita. Chachu kidogo huchachua donge nzima. Nina matumaini kwenu katika Bwana, kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anaewafadhaisha atachukua hukumu yake awae yote. Na mimi, ndugu, ikiwa ninakhubiri khabari ya kutahiriwa, mbona ningali nikiudhiwa? Hapo kwazo la msaiaba limebatilika. Ningependa hawo wanaowatieni mashaka wangejikata nafsi zao. Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali khudumianeni kwa upendo. Maana sharia yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako. Lakini mkiumana na kulana angalieni msije mkaangamizana. Nasema, Enendeni kwa Roho, nanyi hamtatimiza tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho hushindana na mwili; kwa maana liizi zimepingana, hatta hamwezi kufanya nmayotaka. Lakini nikiongozwa na Roho, hunpo chini ya sharia. Na matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasharati, uchafu, ufasiki, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, nzushi, husuda, ulevi, ulafi, na yanayofanana na haya; juu ya haya nawaambieni mapema, kama nilivyokwisha kuwaambieni, watu watendao mambo ya jinsi hii hawatanrithi ufalme wa Mungu. Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo ya jinsi hii hapana sharia. Nao walio watu wa Kristo Yesu wameusulibisha niwili pamoja na mawazo mabaya na tamaa mbaya. Tukiisbi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Tusijisifu burre, tukichokozana na kuhusudiana. NDUGU, mtu ajapogbafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrudini mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako nsijaribiwe wewe mwenyewe. Mchukuliane mizigo mkaitimize hivyo sharia ya Kristo. Maana mtu akijiona kuwa kitu, nae si kitu, ajidanganya nafsi yake. Lakini killa mtu aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakuwa na sababu ya kujisifu kwa nafsi yake tu, wala si kwa kujilinganislia na mwenzake. Maana killa mtu atachukua mzigo wake mwenyewe. Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote. Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandae kwa mwili wake, katika mwili atavuna uharibifu; bali yeye apandae kwa Roho, katika Roho atavima uzima wa milele. Na tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia. Tuwapo na nafasi na tuwatendee watu wote mema; khassa watu walio wa nyumba ya imani. Tazameni kwa harufi gani kubwa nimewaandikieni kwa mkono wangu mimi mwenyewe. Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mwili, ndio wanaokushurutisheni kutahiriwa: wasiudhiwe tu kwa ajili ya msalaba wa Kristo. Kwa maana hatta wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sharia; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kujisifia miili yenu. Lakini mimi, hasha nisijisifie kitu illa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu. Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya. Na wote watakaoiendea kanuni hii, amani kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu. Tangu sasa mtu asinitie taabu; kwa maana ninachiukua mwilini mwangu chapa zake Yesu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amin. PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa mapenzi ya Mungu, kwa watakatifu walio katika Efeso na wanaomwamini Kristo Yesu; Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwaua Yesu Kristo. Atukuzwe Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani ya Kristo; kama alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, tuwe watakatifu, wasio khatiya mbele zake, katika pendo. Kwa kuwa ametuchagua tangu zamani illi tufanywe waua wake yeye kwa njia ya Yesu Kristo, kwa mapenzi ya nia yake, illi usifiwe utukufu wa neema yake, aliyotukarimu katika mpendwa wake: Katika yeye tuna ukombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi, kwa wingi wa neema yake; aliyotuzidishia katika hekima yote na ujuzi; akiisha kutujulisha siri ya nia yake, kwa kadiri ya mapenzi yake, aliyoyakusudia katika yeye huyu, ya kwamba wakati mkamilifu utakapowadia atajumlisha vitu vyote viwe umoja katika Kristo, vitu vilivyo mbinguni, navyo vilivyo duniani, katika yeye huyu: ambae ndani yake sisi tumepata urithi, tukichaguliwa tangu awali kwa kusudi lake yeye afanyae yote kwa shauri la nia yake; illi sisi tuwe sifa ya utukufu wake, tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu; katika huyo na ninyi, mkiisha kulisikia neno la kweli, khabari njema ya wokofu wenu, katika huyo tena mkiisha kumwamini, mlitiwa muhuri na Roho yule Mtakatifu wa ahadi yake, aliye arabuni ya urithi wetu, hatta ukombozi wa milki yake Mungu, kwa sifa ya utukufu wake. Kwa sababu hiyo na mimi, tangu nilipopata khabari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote, siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu; Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awapeni roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye: macho ya akili zenu yakitiwa nuru, mjue tumaini la wito wake jinsi lilivyo, na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo, na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio, jinsi ulivyo, kwa kadiri ya kazi ya nguvu zake hodari, aliyotenda katika Kristo alipomfufua, akamweka mkono wake wa kuume katika mbingu, juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na killa jina litajwalo, si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao nao; akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajiii ya kanisa, lililo mwili wake, ukamilifu wake akamilishae vitu vyote katika vyote. NA ninyi, mlipokmva wafu kwa sababu ya makosa yenu na dhambi zemi, mlizoziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendae kazi sasa katika wana wa kuasi; ambazo sisi nasi sote tuliziendea, hapo zamani, katika tamaa za mwili wetu, tukiyatimiza mapenzi ya mwili wetu na ya nia zetu, tukawa kwa tabia yetu watoto wa ghadhabu kama na hao wengine. Lakini Mungu kwa kuwa mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda, hatta wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu, alituhuisha pamoja na Kristo (mmeokolewa kwa neema); akatufufua pamoja nae, akatuketisha pamoja nae katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu: illi katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu katika Kristo Yesu. Maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu: wala si kwa matendo, asije mtu awae yote akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo Mungu aliyatengeneza tokea awali illi tuenende nayo. Kwa ajili ya hayo kumbukeni kwamba zamani, ninyi mlio watu wa mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa jina lenu wasiotahiriwra na wale wanaoitwa jina lao waliotahiriwa, yaani tohara ya mwili kwa mikono: kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni, wasio wa maagano ya ahadi; mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani. Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza, mmekuwa karibu kwa damu ya Kristo. Maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja, akakibomoa kiyambaza cha kati kilichotutenga, akiisha kuuondoa kwa mwili wake ule uadui, ndio sharia ya amri zilizo katika maagizo; illi afanye wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake, akifanya amani; na kuwapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa msalaba, akiisha kuuua ule uadui kwa huo msalaba; akaja, akakhubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na kwao waliokuwa karibu. Maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Mungu Baba katika Roho mmoja. Bassi tangu sasa ninyi si wapitaji wala wageni, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumba ya Mungu, mmejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii, na Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni; katika yeye jengo lote likiungamanishwa vema linakua hatta liwe hekalu takatifu katika Bwana; katika yeye na ninyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho. KWA sababu biyo mimi Paolo, mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa,— ikiwa mmesikia khabari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu; ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri ile, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache, kwa hayo, myasomapo, mtaweza kutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo; ambayo hawakujulishwa wana Adamu katika vizazi vingine, jinsi walivyofunuliwa zamani hizi mitume wake watakatifu na manabii katika Roho; ya kwamba mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi ahadi yake iliyo katika Kristo kwa njia ya injili; ambayo nilifanywa mkhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema yake Mungu niliyopewa kwa kadiri ya kutenda kazi kwa uweza wake. Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; na kuwaangaza watu wote, wajue khabari ya kuishiriki siri ile, ambayo tangu zamani zote ilisetirika katika Mungu, aliyeviumba vyote kwa Yesu Kristo: illi sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka ya mbinguni; kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu. Katika yeye tuna ajasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya imani yake. Bassi naomba, msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, yaliyo utukufu kwenu. Kwa hiyo nampigia magoti Baba, ambae kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unakwitwa, awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho yake, katika mtu wa ndani; Kristo akae mioyoni mwemi kwa imani; illi ninyi, mkiwa na mizizi na misingi katika upendo, mpale kufahamu pamoja na watakatifu wofe, mapana na marefu na kwenda juu na kwenda chini; na kimjua upendo wake Kristo, ambao hauwezi kufahamiwa vema kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu. Bassi, kwake yeye awezae kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuombayo au tuwazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu, kwake yeye utukufu katika Kanisa, na katika Kristo Yesu hatta vizazi vyote vya milele na milele. Amin. BASSI nawasihini, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa, kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendano; mkijitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. Mwili mmoja, na Roho moja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu; Bwana mmoja, imani moja, ubatizo umoja, Mungu mmoja, nae Baba wa wote, aliye juu yote, na kwa yote, na katika yote. Lakini killa mmoja wetu alipewa neema, kwa kadiri ya kipawa cha Kristo. Kwa biyo asema, Alipopanda juu, aliteka mateka, Akawapa watu vipawa. (Bassi, neno lile, Alipanda, maana yake nini kania sio kusema kwamba alishuka hatta pande za chini za inchi? Aliyeshuka ndiye aliyepanda juu sana kupita mbingu zote, vitu vyote vijae nae.) Na yeye aliwatoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji, na waalimu, kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, kazi ya khuduma itendeke, mwili wa Kristo ujengwe; hatta wote tutakapoufikia umoja wa imani, na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, tuwe watu wakamilifu, hatta cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; illi tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukulivva kwa killa upepo wa elimu, kwa bila ya watu, kwa ujanja, tukifuata njia za udanganyifu; lakini tukiishika kweli katika upendo, tukue mpaka tumfikie ycye katika yote, aliye kichwa, Kristo; katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa, kwa msaada wa killa kiungo, kwa kadiri ya kazi ya killa sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo. Bassi nasema neno bili, tena nashuhudu katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waendavyo, katika ubatili wa nia zao, akili zao zimetiwa giza, wamekaa mbali na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo niwao, kwa sababu mioyo yao imekufa ganzi: watu waliopooza kabisa, wamejitia katika mambo ya ufasiki, wapate kufanyiza killa namna ya uchafu kwa kutamani. Bali ninyi hamkujifunza hivi khabari za Kristo; mkiwa mwalimsikia mkafundishwa katika yeye, kama ilivyo kweli katika Yesu; mvue kwa khabari ya desturi za kwanza mtu wa zamani, anaeharibiwa kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya kwa roho ya nia zenu, mkavae mtu mpya, aliyeumbwa kwa namna ya Mungu katika baki na utakatifu wa kweli. Bassi uvueni uwongo, mkaseme kweli killa mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, killa mmoja kiungo cha wenzake. Mwe na ghadhabu, wala msifanye dhambi; jua lisichiwe na uchugu wenu bado kukutokeni; wala msimpe nafasi Shetani. Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo njema kwa mikono yake mwenyewe, apafe kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji. Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, liwape neema wanaosikia. Wala msimhuzunishe Roho yule Mtakatifu wa Mungu; kwa yeye mlitiwa muhuri mpaka siku ya ukombozi. Uchungu wote na hasira na ghadhabu na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na killa ubaya; tena mwe wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkiachiliana, kama na Mungu katika Kristo alivyowaachilia ninyi. BASSI mwe wafuasi wa Mungu, kama watoto wanaopendwa; mkaenende katika upendo, kama na Kristo alivyowapenda ninyi, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu nzuri. Lakini uasharati na uchafu wote au kutamani kusinenwe kwenu kabisa, kama iwastahilivyo watakatifu; wala aibu wala maneno ya upuuzi wala ubishi; haya hayapendezi; bali afadhali kushukuru. Maana neno hili mnalijua kwa kulifaliamu, kwamba hapana asharati, wala mchafu, wala mtu wa tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu. Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo maana; maana kwa sababu ya haya ghadhabu ya Mungu huwajia wana wa uasi. Bassi msishirikiane nao. Kwa maana zamani mlikuwa giza, bali sasa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru; (kwa kuwa tunda la nura ni katika wema wote na haki na kweli); mkihakiki nini impendezayo Bwana. Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee; kwa kuwa yanayotendeka nao kwa siri, ni aibu hatta kuyanena. Lakini yote yakemewapo, hudhihirishwa na nuru; maana killa kitu kinachodhihirisha ni nuru. Kwa biyo anena, Amka, wewe usinziae, kafufuka, na Kristo atakuangaza. Angalieni sana, bassi, jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio hekima, bali kama wenye hekima; mkiukomboa wakati, kwa maana zamani bizi zina novu. Kwa sababu hii msiwe wajinga, bali watu wanaofahamu nini mapenzi ya Bwana. Tena msilevye kwa mvinyo, kwa kuwa haina kiasi, bali mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na fenzi na nyimbo za roho, mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; mkimshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; mkitumikiana katika khofu ya Kristo. Ninyi wake, watumikieni waume zenu kama kumtumikia Bwana wetu. Maana mume ni kichwa cha mke, kama nae Kristo ni kichwa cha kanisa; nae ni mwokozi wa mwili. Kwa hivyo kama Kanisa limtumikiavyo Kristo, vivyo hivyo nao wake wawatumikie waume zao katika killa jambo. Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake, kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji, na kwa Neno; apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na ila ama kunyanzi ama lo lole kama haya; bali liwe takatifu na lisilo na mawaa. Vivyo hivyo imewapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendae mkewe hujipenda nafsi yake; maana hakuna mtu anaechukia mwili wtike, bali huulisha na kuutunza, kama Bwana anavyolitendea Kanisa; kwa kuwa tu viungo vya mwili wake, na nyama yake, na mifupa yake. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha haha yake na mama yake, ataamhatana na mkewe; nao wawili watakuwa mwili mmoja. Hii ni siri kubwa; lakini nanena khabari ya Kristo na Kanisa. Illakini killa mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; na mke asikose kumstahi mumewe. WATOTO, watiini wazazi wenn katika Bwana, maana hii ndio haki. Waheshimu baba yako na mama yako (amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi), upate ukheri, nkakae sana katika dunia. Na ninyi, akina baba, msiwachokoze watoto wemi; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana. Watumwa, watiini walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili kana kwamba ni kumtii Kristo, kwa khofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, wala si kwa utumwa wa macho kama wajipendekezao kwa wana Adamu; bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo; kwa nia njema mkimtumikia Bwana wala si mwana Adamu: mkijua ya kuwa killa neno jema atendalo mtu, atapewa lilo hilo na Bwana, akiwa ni mtumwa, au akiwa ni huru. Na ninyi, akina bwana, watendeni yayo bayo, mkiacha kuwaogofya, mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, na kwake hapana upendeleo. Ndugu zangu, mwe hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila zake Shetani. Kwa maana shindano letu si juu ya damu na nyama, bali juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza ya ulimwengu huu, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kutimiza yote kusimama. Simameni, bassi, mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa haki vifuani, na kufungiwa miguu bali ya kuwa fayari tupatayo kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chepeo ya wokofu, na upanga wa Roho, ndio neno la Mungu; kwa sala zote na kuomha mkisali killa wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo, mkifanya juhudi sana, na kuwaombea watakatifu wote, na mimi pia, nipewe usemi, kwa kufumhua kinywa changu kwa ujasiri, niikhubiri siri ya Injili, kwayo ni mjumbe kifungoni; nipate ujasiri katika kunena jinsi nipaswavyo kusema. Illakini ninyi nanyi mpate kuyajua mamho yangu ni hali gani, Tukiko, ndugu mpendwa, mkhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisha mambo yote; ambae nilimpeleka kwenu kwa kusudi hili hili mpate kuyajua mambo yetu, nae akawafariji mioyo yenu. Amani kwa ndugu, na pendo pamoja na imani, zitokazo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana Yesu Kristo. Neema iwe pamoja na wote wampendao Bwana wetu Yesu pasipo hila. Amin. PAOLO na Timotheo, watumwa wa Yesu Kristo, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walio katika Filipi, pamoja na maaskofu na wakhudumu; Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo. Namshukuru Mungu wangu killa niwakumbukapo, siku zote killa niwaombeapo ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha, kwa sababu ya ushirika wenu katika kuieneza Injili, tangu siku ya kwanza hatta leo hivi; niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hatta siku ya Yesu Kristo; kama ilivyo wajib wangu kufikiri haya juu yenu nyote; kwa sababu ninyi mmo moyoni mwangu; kwa kuwa katika kufungwa kwangu na katika kazi ya kuitetea Injili na kuithubutisha, ninyi nyote mmeshirikiana nami neema hii. Maana Mungu ni shahidi wangu, jinsi ninavyowaonea shauku katika moyo wake Kristo Yesu. Na hii ndiyo sala yangu, pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote; mpate kuyakubali yaliyo mema; illi mwe na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo, mmejazwa matuuda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu. Lakini, ndugu zangu, nataka mjue ya kuwa mambo yote yaliyonipata yamekuja yakaieneza Injili; hatta vifungo vyaugu vimekuwa dhahiri katika Kristo, katika praitorio, na kwa wengine wote. Na walio wengi wa ndugu walio katika Bwana, wakipata kuthubutika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kulinena neno la Bwana pasipo khofu. Wengine wanakhubiri khabari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina: na wengine kwa nia njema. Hawa wanamkhubiri Kristo kwa fitina wala si kwa moyo mweupe, wakidhani kuongeza taabu za kufungwa kwangu; na hawa wengine kwa pendo, wakijua ya kuwa nimewekwa illi niitetee Injili. Yadhuru nini? bali kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anakhubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi. Maana najua ya kuwa haya yatanigeukia kuwa wokofu wangu, kwa sababu ya kuomba kwenu, na kuruzukiwa Roho ya Yesu Kristo, kama nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kabisa, bali kwa nthabiti wote, kama siku zote, na sasa tena Kristo atatukuzwa katika mwili wangu, ikiwa kwa maisha yangu, au kwa mauti yangu. Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. Illa ikiwa kuishi katika mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; bassi nitakalolichagua sitambui. Ninasongwa kati kati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo; maana ni vizuri zaidi; bali kudumu katika mwili kwuhitajiwa zaidi kwa ajili yenu. Nami nikitumaini haya, najua ya kuwa nitakaa na kudumu pamoja nanyi, illi muendelee mkapate kufurahi katika imani; kujisifu kwenu kupate kuzidi katika Kristo Yesu kwa ajili yangu kwa sababu ya kuwapo kwangu pamoja nanyi nyote tena. Lakini mwenendo wenu uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, illi, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili; wala hamwogopi adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni ishara wazi ya kupotea, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokofu, nao wa Mungu. Maana mmepewii kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, illa na kuteswa kwa ajili yake, mkiwa na mashindano yale yale mliyoyaona kwangu, mkasikia kvvamba ninayo hatta sasa. BASSI ikiwako faraja iliyo yote katika Kristo, yakiwako ma, tulizo yo yote ya mapenzi, ikiwako huruma yo yote na rehema, ijalizeni furaha yangu, illi mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. Msitende neno lo lote kwa kushindana na kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, killa mtu na amhesabu mwenziwe kuwa hora kuliko nafsi yake; killa mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, hali killa mtu mamho ya wengine. Maana mwe na nia lili ndani yenu iliyokuwamo na ndani ya Yesu Kristo; yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, nae hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa kitu cha kushikamana nacho, hali alijifanya hana utukufu, akitwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wana Adamu; tena, alipoonekana ana umho kama mwana Adamu, alijidhili, akawa mtii hatta mauti, nayo mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu akamtukuza mno, akamkarimia Jina lile lipitalo killa jina; illi kwa jina la Yesu killa goti likunjwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya inchi; killa ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. Bassi, wapendwa, kama vile mlivyotii siku zote, si wakati mimi nilipokuwapo, bali sasa zaidi mimi nisipokuwapo, utimizeni wokofu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka; kwa maana ni Mungu atendae ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa ajili ya kusudi lake jema. Yatendeni mambo yote pasipo manungʼuniko na mashindano, mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala ndanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, na kilichopotoka; kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, mkishika neno la uzima; nipate sababu ya kujisifu katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio burre wala sikujitaabisha burre. Naam, hatta nikimiminwa juu ya dhabihu na khuduma ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote. Nanyi vivyo hivyo furahini, tena furahini pamoja nami. Walakini natmnaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwemi karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu. Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakaeangalia hali yenu kweli kweli. Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Yesu Kristo. Maana mwajua ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake. Bassi, natumaini kumtuma huyu marra nitakapojua yatakayonipata. Maana naamini katika Bwana ya kuwa nitakuja na mimi mwenyewe karibu. Lakini naliona imenilazimu kumtuma Epafrodito, ndugu yangu, mtendaji wa kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mkhudumu wa muhitaji yangu. Kwa kuwa alikuwa na shanku kwenu ninyi nyote, akahuzunika sana, kwa sababu mlisikia ya kwamba alikuwa hawezi. Kwa maanu alikuwa hawezi kweli kweli, karibu na kufa; lakini Mungu alimhurumia; wala si yeye peke yake, illa na mimi pia: nisiwe na huzuni juu ya huzuni. Nikafanya hidii uyiugi zaidi kumtuma tena, nami nikapunguziwe huzuni yangu. Mpokeeni, bassi, katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa. Maana kwa ajili ya kazi ya Kristo alikaribia kufa, asiutunze uhayi wake; illi kusudi ayatimize yaliyopungua katika khuduma yenu kwangu. KHATIMAE, ndugu zangu, furahini katika Bwana. Kuwaandikieni yale yale hakuniudhi mimi, bali kutawafaa niuyi. Jihadharini na mbwa, jihadharini nao watendao mabaya, jihadharini nao wajikatao. Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Muugu kwa Roho, na kujisifu katika Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu ye yote akijiona anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi. Nalitabiriwa siku ya nane, ni lutu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benjamin, Mwebrania wa Waebrania, kwa khabari ya kuifuata sharia, Farisayo, kwa khabari ya wivu, mwenye kuliudhi Kanisa, kwa jinsi ya haki ipatikanayo kwa sharia sikuwa na khatiya. Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyaona kuwa khasara kwa ajili ya Kristo. Naam, naliona mambo yote kuwa khasara kwa ajili ya uzuri usio kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambae kwa ajili yake nimepata khasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kania mavi illi nimpate Kristo; tena nionekane katika yeye, nisiwe na baki ile ipatikanayo kwa sharia, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; illi nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu. Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! bali nafuatafuata illi nilishike lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; illa natenda kitu kimoja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele, nakaza mwendo, niifikilie thawabu ya wito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. Bassi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hatta mkiwaza mengine katika lo lote, Mungu atawafunulieni hilo nalo. Illakini, hapo tulipofika na tuenende kwa kanuni ile ile. Mwe wafuasi wangu, ndugu, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliokupeni. Maana wengi huenenda, nimewaambieni marra nyingi khabari zao, na hatta sasa nawaambieni kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo; mwisho wao uharibifu, mungu wao tumbo, utukufu wao u katika aibu yao, waniao mambo ya duniani. Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbiuguni; kutoka huko tena tunamtazamia mwokozi Bwana Yesu Kristo; atakaeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule awezao kuvitiisha hatta na vitu vyote chini yake. BASSI, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu. Namsihi Euodia, namsibi na Suntoke, wawe na nia moja katika Bwana. Naam, nakutaka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi nae, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima. Furahini katika Bwana siku zote; marra ya pili nasema, Furahini. Upole wenu ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika killa neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru haja zenu zijulike kwa Mungu. Na amani va Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. Khatimae, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya heshima, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye kuvuma vizuri, ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini haya. Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia, na kuyaona kwangu, yatendeni haya; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi. Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha fikara zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu; lakini hamkupata nafasi. Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yote, nimefundishwa kushiha na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiae nguvu. Lakini mlifanya vema sana, mkishiriki nami mateso yangu. Na ninyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa injili, nilipotoka Makedonia, hapana kanisa lingine lililoshirikana nami katika khabari hii ya kutoa na kupokea, illa ninyi peke yenu. Kwa kuwa hatta katika Tʼhessaloniki mliniletea msaada kwa mahitaji yangu wala si marra moja tu. Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu. Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi; tena nimejaa tele, nimepokea kwa mkono ya Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu. Na Mungu atawajazeni killa mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. Sasa Mungu, Baba yetu, atukuzwe milele na milele. Amin. Mnisalimie killa mtakatifu katika Kristo Yesu. Ndugu walio pamoja nami wawasalimu. Watakatifu wote wawasalimu, khassa wao walio wa nyumba ya Kaisari. Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu. Amin. PAOLO, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu, kwa ndugu watakatifu na waaminifu, walio ndani ya Kolossai, Neema iwe kwenu na imani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo. Twamshukuru Mungu, baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, siku zote tukiwaombeeni; tuliposikia khabari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote; kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, khabari zake mlisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili; iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, ikizaa matunda na kukua, kama na inavyokua kwenu, tangu siku mliposikia nikaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli; kama mlivyofundishwa na Epafra mjoli wetu mpenzi, aliye mkhudumu amini wa Kristo kwa ajili yenu; nae alitueleza upendo wenu katika Roho. Kwa sababu hiyo na sisi, tangu siku tuliposikia, hatuachi kuwaombeeni, na kuomba dua, mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; kwa killa kazi njema mkizaa matunda, mkizidi katika maarifa ya Mungu; mkiwezeshwa kwa nwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya killa namna na uvumilivu pamoja na furaha; mkimshukuru Baba, aliyetustahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru; aliyetuokoa na uguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; amliae katika yeye tuna nkombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi, nae ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya inchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni viti vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake, nae alikuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. Nae ni kichwa cha mwili, yaani cha kanisa; nae ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, illi awe mtangulizi katika yote. Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae, na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote nae, akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya inchi, au vilivyo mbinguni. Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, ua adui katika nia zenu, kwa matendo yemi mabaya, amewapatanisha sasa, katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, illi awalete ninyi mbele zake, watakatifu, hamna mawaa wala lawama, mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake. Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena natimiliza yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo katika mwili wangu, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake, ambalo nimekuwa mkhudumu wake, kwa uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu; siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake: ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu; ambae sisi tunakhubiri khabari zake, tukimwonya killa mtu, na tukimfundisha killa mtu katika hekima yote, tupate kumleta killa mtu mtimilifu katika Kristo Yesu; nami najitaabisha kwa hiyo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendae kazi ndani yangu kwa nguvu. MAANA nataka muijue juhudi niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili, jinsi ilivyo kuu; illi wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo, ambae ndani yake zimo hazina zote za hekima na maarifa, zimesetirika. Nasema neno hili, mtu asije akawadanganyeni kwa maneno yaliyotungwa illi kuwakosesha. Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, illakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo. Bassi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye, mmetia mizizi, na kujengwa katika yeye: mmefanywa imara kwa imani, kaina mlivyofundishwa, mkizidi kutoa shukrani. Angalieni intu asiwateke kwa filosofia yake na madanganya matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wana Adamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo. Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa namna ya kimwili. Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi vote na mamlaka. Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mkono, kwa kuuvua mwili wa dhambi, wa nyama, kwa tohara ya Kristo; mkizikwa pamoja nae katikti ubatizo, katika huo mlifufuliwa pamoja nae, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu. Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hayi pamoja nae, akiisba kuwasameheni makosa yote; akiisba kuifuta ile khati iliyoandikwa na kutushitaki kwa hukumu zake; iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwe kati kati yetu sisi na yeye, akaikaza msalabani; akiisha kuziteka enzi na mamlaka, na kuzimithilisha kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo. Bassi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au viuvwaji au kwa sababu ya siku kuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo. Mtu asiwanyangʼanye thawabu yenu, akijinyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kwa kuwaabudu malaika, akijishughulisha na asiyoyaona, akijivuna burre, kwa akili ya mwili wake, wala hakishiki kiehwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua mkuo utokao kwa Mungu. Bassi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkaacha mafundisho ya awali ya ulimwengu, ya nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani, Msishike, msionje, msiguse; (Mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa), mkifuata maagizo na mafundislio ya wana Adamu? Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kujinyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali: illakini hayafai kitu wala kuwa dawa ya tamaa za mwili. BASSI mkiwa mmefufuka panioja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko mkono wa kuume wa Mungu, ameketi. Nieni yaliyo juu, siyo yaliyo katika inchi. Kwa maana mlikufa, na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapoonekana, aliye uzima wetu, ndipo na ninyi mtaonekana pamoja nae katika utukufu. Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu: kwa ajili ya hayo ghadhabu ya Mungu huwafikia wana wa kuasi. Katika hayo na ninyi mlitembea zamani, mlipoishi katika haya. Lakini sasa yawekeni mbali haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu. Msiambiane uwongo, kwa kuwa mmemvua mtu wa kale, pamoja na matendo yake, mkamvaa mtu mpya anaefanywa upya apate maarifa kwa mfano wake yeye aliyemumba. Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mshenzi wala Mskuthi, mtumwa wala mungwana, bali Kristo ni yote, na katika wote. Bassi, kwa kuwa mu wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, vaeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kuachiliana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mtu; jinsi Kristo alivyowaachilieni, vivyo hivyo na ninyi. Juu ya haya yote vaeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. Na amani ya Mungu iamue mioyoni mwenu, ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; na mwe watu wa shukrani. Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; kwa neema mkimwimbia Bwana mioyoni mwenu. Na killa mfanjalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye. Ninyi wake, watiini waume zenu, kania ipendezavyo katika Bwana. Ninyi waume, wapendeni wake zenu, msiwe na uchungu nao. Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jamlio hili lapendeza katika Bwana. Ninyi haha, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa. Ninyi watumwa, watiini wao ambao kwa niwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wana Adamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimeha Mungu. Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wana Adamu, mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana njira wa urithi; kwa kuwa mnamtumikia Bwana Kristo. Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo. NINYI bwana, wapeni watumwa wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni. Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani, mkituombea na sisi pia, Mungu atufungulie mlango kwa Neno lake tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa, illi niidhihirishe, kama inipasavyo kunena. Enendeni kwa hekima mbele vao walio nje, mkiukomboa wakati. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea chumvi, mpate kujua jinsi iwapasa vyo kumjibu killa mtu. Tukiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mjoli wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote; ambae nimemtuma kwenu kwa sababu hiyo hiyo, ajue mambo yenu, akawafariji mioyo yenu; pamoja ua Onesimo, ndugu mwaminifu, mpendwa, aliye mtu wa kwenu; watawaarifuni mambo yote ya huku. Aristarko, aliyefumgwa pamoja nami, awasalimu, na Marko, mjomba wake Barnaba, amhae mmepokea maagizo kwa khabari yake; akifika kwenu mkaribisheni. Na Yesu aitwae Yusto; hao ni watu wa tohara. Tena hao peke yao ni watendaji wa kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao walikuwa faraja kwangu. Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu. Maana namshuhudia kwamba ana juhudi nyingi kwa ajili yenu, na kwa ajili yao walio katika Laodikia, na kwa ajili yao walio katika Hieropoli. Luka, yule tabibu mpendwa, awasalimu, na Dema. Wasalimuni ndugu walio katika Laodikia, na Numfa, na kanisa lililo katika nyumba yake. Waraka hun ukiisha kusomwa kwenu, fanyeni kwamba usomwe katika kanisa la Walaodikia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi. Mwambieni Arkippo, Iangalie sana khuduma ile uliyopewa katika Bwana, illi uitimize. Salamu yangu mimi Paolo, kwa mkono wangu mwenyewe. Yakumbukeni mafungo yangu. Neema na iwe pamoja nanyi. Amin. PAOLO, na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathessaloniki, katika Mungu Baba, na Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo. Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu; wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya amani, na taabu yenu ya upendo, na uvumilivu wenu wa tumaini lililo katika Bwana Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu; tukijua, ndugu mnaopendwa na Mungu, uteule wenu, kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthubutifu mwingi; kama mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu. Mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea Neno katika mateso mengi pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu, hatta mkawa mfano kwa watu wote waaminio katika Makedonia, na katika Akaya. Maana kutoka kwenu Neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu: bali na katika killa mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea, hatta hatuna haja sisi kunena lo lote. Maana wao wenyewe wanatangaza khabari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu, mkaziacha sanamu illi kumtumikia Mungu aliye hayi, wa kweli, na kumugojea Mwana wake kutoka mbinguni, ambae alimfufua katika wafu, Yesu, anaetuokoa na ghadhabu itakayokuja. MAANA ninyi wenyewe, udugu, mwakujua kuingia kwetu kwenu, ya kwamba hakukuwa burre, bali tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filippi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana. Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu wala ya uchafu, wala ya hila, bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuaminiwe Injili ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wana Adamu bali Mungu anaetupima mioyo yetu. Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya kuficha tamaa; Muugu ni shahidi. Hatukutaka kusifiwa na watia Adamu, wala na ninyi, wala na wengine, tulipokuwa tuliweza kuwalemea kama mitume wa Kristo; bali tulikuwa wapole kati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe. Vivyo hivyo sisi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapeni, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu. Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu, tukawakhubirini bivi Injili ya Mungu. Ninyi mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa; vile vile kama mjuavyo jinsi tulivyomwonya killa mmoja wemi kama baba amwonavyo mtoto wake, tukiwatieni moyo na kushuhudia, illi mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Mungu mwenende, awaitae muingie katika ufalme wake na utukufu wake. Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa mlipopokea lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la kibinadamu; bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini. Maana uinyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Yahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu, waliyopata na hao kwa Wayahudi; waliomwua Bwana Yesu na manabii wao wenyewe na kutuudhi sisi, wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wo wote; wakituzuia tusiseme na mataifa wapate kuokolewa; illi watimize dhambi zao siku zote; lakini hasira imewafikia hatta mwisho. Lakini sisi, ndugu, tukifarakana nanyi kwa kitambo, kwa nso si kwa moyo, tulitamani zaidi kuwaona nyuso zenu, kwa shauku nyingi. Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paolo, marra ya kwanza, na marra ya pili. Shelani akatuzuia. Maana tumnini letu, au furaha yetu, an taji ya kujisifu ni nini? Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu Kristo wakati wa kuja kwake? Maana ninyi utukufu wetu, na furaha yetu. BASSI kwa biyo, tulipokuwa hatukuweza kuvumilia zaidi, tuliona vema kuachwa Athene peke yetu; tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu, mfanya kazi pamoja naswi katika Injili ya Kristo, kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa ajili ya imani yenu, mtu asifadhaishwe na mateso haya: maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa haya. Kwa maana tulipokuwa kwenu tulitangulia kuwaambieni kwamba tutapata kuteswa, kama ilivyotukia, nanyi mwajua. Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalimtuma mtu illi niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, wala taabu yetu isiwe haina faida. Lakini Timotheo alipotujia siku hizi kutoka kwenu, akatuletea khabari njema za imani yenu na upendo wenu, na ya kwamba mnatukumbuka vema siku zote: mkitamani kutuona sisi vile vile kama sisi ninyi; kwa sababu hiyo tulifarijiwa, ndugu, kwa khabari zenu, katika shidda na mateso yetu yote, kwa imani yenu. Kwa kuwa sasa twaishi, ikiwa ninyi mnasimama imara katika Bwana. Maana shukrani gani tuwezayo kumlipa Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha ile yote tunayoifurahia, kwa sababu yenu mbele za Mungu wetu; usiku na mchana tukiomba kwa juhudi tupate kuwaona nyuso zenu na kuyatengeneza mapungufu ya imani yenu. Bassi Mungu mwenyewe, Baba yetu, na Bwana wetu Yesu Kristo atuongoze njia yetu tufike kwenu; Bwana na awaongozeni na kuwazidisheni katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile na sisi kwenu; apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote. ILIYOBAKI, ndugu, tunakusihini na kukuonyeni kuenenda katika Bwana Yesu, kama mlivyopokea kwetu, jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama na muavyoenenda, mpate kuzidizidi sana. Maana mnajua maagizo gani tuliyowapeni kwa Bwana Yesu. Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na nasharati; killa mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima, si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu; mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizae kisasi cha haya yote, kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudu sana. Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso. Bassi yeye anaekataa, hakatai mwana Adamu bali Mungu, anaewapeni Roho yake Mtakatifu. Kwa khabari ya upendano, hamna haja niwaandikie: maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana. Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia wote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana; tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe kama tulivyowaagiza; illi mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na baja ya cho chote. Lakini, ndugu, hatutaki msijue khabari zao waliolala, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu Mungu atawaleta pamoja nae. Maana twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hayi, tutakaosalia hatta wakati wa kuja kwake Bwana, hatutawatangulia wao waliokwisha kulala. Kwasababu Bwana mwenyewe atasbuka kutoka mbinguni na sauti kuu na sauti ya malaika mkuu, na panda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo, watafufuliwa kwanza; baada va haya sisi tulio hayi, tuliosalia, tutachukuliwa pamoja nao katika mawingu, illi tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Bassi, farijianeni kwa maneno haya. LAKINI kwa khabari ya nyakati na majira, ndugu, hamna haja niwaandikie. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwizi ajavyo usiku. Maana wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo niwenye mimba; nao hawataokolewa. Bali ninyi, ndugu, hamwi katika giza, siku ile iwapale kama mwizi. Maana ninyi nyote wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi hatuwi wa usiku, wala wa giza. Bassi tusilale kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi. Maana walalao hulala usiku, na walewao hulewa usiku. Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, tukijivika kifuani imani na upendo, na chepeo yetu iwe tumaini la wokofu. Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira vake bali tupate wokofu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyekufa kwa ajili vetu, illi tuishi pamoja nae, ikiwa twakesha au ikiwa twalala. Bassi, farijianeni mkajengeane, killa mtu mwenzake, vile vile kama mnavyofanya. Lakini, ndugu, tunataka mwajue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu na kuwasimamieni katika Bwana, na kuwaonyeni; mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Mwe na amani ninyi kwa ninyi. Twawasihi, ndugu, waonyeni wale wasiokaa kwa taratihu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote. Angalieni mtu awae yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote. Furahini siku zote; ombeni hila kukonia; shukuruni kwa killa jambo; maana haya ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. Msimzimishe Roho; msitweze unabii; jaribuni vyote; lishikeni lililo jema; jitengeni na ubaya wa killa namna. Mungu wa amani mwenyewe awatakase kahisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. Yeye ni mwaminifu awaitae, nae atafanya. Ndugu, tuombeeni. Wasalimuni ndugu kwa husu takatifu. Nawaapisha kwa Bwana, wasomewe ndugu wote waraka huu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi. Amin. PAOLO, Silwano, na Timotheo kwa kanisa la Wathessaloniki lililo katika Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo: Neema iwe kwenu na imani zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo. Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi. Hatta sisi wenyewe twajisifu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya uvumilivu wenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na mateso mnayoyavumilia; ndio ishara ya hukumu ya haki ya Mungu illi mstabilishwe kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa; kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi, na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake, katika mwako wa moto, akiwalipa kisasi wao wasiomjua Mungu, nao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo; watakaoadhibiwa kwa uharibifu wa milele, kutengwa na uso wa Bwana na na utukufu wa nguvu zake, atakapokuja illi kutukuzwa katika watakatifu wake, na kuajabiwa katika wote waaminio (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu), katika siku ile. Kwa hiyo twawaombea ninyi siku zote, illi Mungu wetu awahesabu kuwa nimeustahili wito wenu, akatimize killa haja ya wema na killa kazi ya imani kwa nguvu: jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe kwenu, na ninyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo. BASSI tunakusihini, ndugu, katika khabari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele yake, msifadhaishwe upesi na kuaeha nia yenu, wala msistushwe, kwa roho wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, ya kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo. Mtu aliye yote asiwadanganye kwa njia yo yote, maana haiji isipokuja kwanza ile faraka, akafumiliwa yule mtu wa dhambi, mwana wa uharibifu, yule mpingamizi, ajiinuae nafsi yake juu ya killa kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hatta yeye mwenyewe huketi katika hekalu la Mungu, kama Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba ndive Mungu. Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwa pamoja nanyi naliwaambieni hayo? Na sasa lizuialo mwalijua, apate kufunuliwa huyu wakati wake. Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiae sasa, hatta atakapoondolewa. Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambae Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa mafunuo ya kuwako kwake; ambae kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kazi kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za nwongo, na katika madanganya yote ya udhalimu kwao wanaopotea: kwa sababu hawakukubali kuipenda kweli, wapate kuokolewa. Kwa biyo Mungu atawaletea nguvu ya upotevu, wauamini uwongo, illi wahukumiwe wote wasioamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu. Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokofu, katika kutakaswa kwa Roho na kuiamini kweli, aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, illi kuupata ntukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. Bassi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ikiwa kwa maneno, au kwa waraka wetu. Na Bwana wetu Yesu Kristo, na Mungu Baba yetu aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema, awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika killa neno na tendo jema. ILIYOBAKI, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, likatunzwe vilevile kama ilivyo kwenu; tukaokolewe na watu wasio haki, wahaya; maana si wote walio na imani. Lakini Bwana ni mwaminifu, atakaewafanyeni imara na kuwaokoeni na yule mwovu. Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tuliyowaagizeni, tena kwamba mtayafanya. Bwana awaongozeni mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na uvumilivu wa Kristo. Twawaagizeni, ndugu, katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na killa ndugu aendae bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu. Mwajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata, kwa sababu hatukwenda bila utaratibu kwenu; wala hatukula chakula kwa mtu ye yote burre, bali kwa taabu na masumbufu, mchana na usiku, tulitenda kazi, illi tusimlemee mtu kwenu; si kwamba hatuna uwezo, bali tufanye nafsi zetu kuwa mfano kwenu, mtufuate. Kwa maana hatta wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, bassi, asile chakula. Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawʼana shughuli yao wenyewe, bali wanajishughulisha na mambo ya wengine. Bassi twawaagiza, hao na kuwaonya katika Bwana wetu Yesu Kristo, watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe. Lakini, ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema. Na ikiwa mtu aliye yote halishiki neno letu la waraka huu, jihadharini na mtu huyo, wala msizumgumze nae, apate kutahayarika; illakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu. Sasa, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani siku zote kwti njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote. Salamu zangu mimi Paolo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika killa waraka, ndivyo niandikavyo. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi nyote. Amin. PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Bwana Yesu Kristo, tumaini letu; kwa Timotheo, mwana wangu khassa katika imani, Neema, na rehema, na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. Kama vile nilivyotaka ukae katika Efeso nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, illi, nwaagize wengine wasifundishe elimu ya namna nyingine, wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si ujenzi wa Mungu ulio katika imani; bassi sasa nakuagiza vivyo hivyo. Bali kusudi la mausia hayo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki: wengine wakikosa bayo wamepotea, wakigeukia maneno ya ubatili; wapenda kuwa waalimu wa sharia, wasiyafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa utbabiti. Lakini twajua ya kuwa sharia ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia ya kisharia; nawe ufahamu neno hili, ya kuwa sharia haimkhusu mtu wa haki, bali maasi, mi wasio taratihu, na makafiri, na wenye dhambi, na wasio watakatifu, na wasiomcha Mungu, na wauao baba zao, na wauao mama zao, mi wauaji, na wazinzi, na wafiraji, na waibao watu, na wawongo, mi waapao uwongo, na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima; kama vile ilivyonenwa katika injili ya utukufu wa Mungu ahimidiwae, niliyoaminiwa mimi. Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu aliyenitia nguvu, kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akiniweka katika khuduma yake; mimi niliyekuwa kwanza mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri: lakini nalirehemiwa kwa kuwa nalitenda hivyo kwa njinga, na kwa kutokuwa na imani; na neema ya Bwana wetu ilizidi sana pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu. Ni neno la kuaminiwa, listahililo kukubaliwa na watu wote, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni, awaokoe wenye dhambi; na mimi wa kwanza wao. Lakini kwa sababu hii nalirehemiwa, illi katika mimi, wa kwanza, Yesu Kristo adhihirishe uvumilivu wote, niwe mfano kwa wale watakaomwamini baadae, wapate uzima wa milele. Kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu wa hekima peke yake, kwake yeye heshima na utukufu milele na milele. Amin. Agizo hilo nakupa iwe akiba, mwanangu Timotheo, kwa ajili ya maneno ya unabii yalivotangulia juu yako, illi katika hayo ufanye vile vita vizuri; nwe mwenye imani na dhamiri njema; wengine wamezisukumia mbali hizo, wakavunja chombo cha imani. Katika hao wamo Humenayo na Iskander, ambao nimempa Shetani wafundishwe wasimtukane Mungu. BASSI, kabla ya mambo yote, dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme, na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya ntulivu na amani, katika utawa wote, na ustahifu. Maana hili ni zuri, lenye kibali mbele za Mwokozi wetu Mungu atakae watu wote waokolewe wakapate kujua sana yaliyo kweli. Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wana Adamu ni mmoja, mwana Adamu, Kristo Yesu, aliyejitoa nafsi yake kuwa ukombozi kwa ajili ya wote utakaoshuhudiwa kwa majira yake; kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mkhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo, sisemi uwongo), mwalimu wa mataifa katika imani na kweli. Bassi nataka wanaume waombe killa mahali, wakimua mikono mitakatifu, pasipo hasira na majadiliano. Na vivyo hivyo wanawake wajipambe kwa mavazi ya kujisetiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi, si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kama iwapasavyo wanawake wanaokiri utawa, kwa matendo mema. Mwanamke na ajifunze kalika utulivu, akitii kwa killa namna. Simpi mwanamke rukhusa kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali kuwa katika utulivu. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadae. Na Adamu hakudanganywa, bali mwanamke akidanganywa aliingia hali ya kukosa. Lakini ataokolewa, kwa ule uzazi, kama wakidumu katika imani na npendo na utakatifu pamoja na moyo wa kiasi. AMINI neno hili, Mtu akitaka uaskofu, atamani kazi nzuri. Bassi imempasa askofu kuwa mtu asiyelaumiwa, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, mfundishaji; si mtu wa kuzoelea mvinyo, si mpigaji, si mtu apendae fedha; bali awe mpole, asiwe mtu wa kujadiliana, asitamani fedha; mwenye kusimamia vema nyumba yake, ajuae kuwatiisha watoto wake pamoja na kustahiwa; (mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje kanisa la Mungu?) si mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna, akaanguka katika hukumu ya Shetani. Imempasa tena kushuhudiwa mazuri na watu walio nje; asitumbukie katika lawama na mtego wa Shetani. Vivi hivi mashemasi, wawe watu wa utaratibu, si wenye nia mbili, si watu wa kutumia mvinyo nyingi, wawe watu wasiotamani fedha ya aibu; wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi. Na hawa pia wajaribiwe kwanza; baadae watumie daraja ya ushemasi, wakiisha kuonekana hawana khatiya. Vivi hivi wanawake wawe watu wa utaratibu, si wasingiziaji, watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote. Mashemasi wawe na mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. Kwa maana watendao kazi ya ushemasi vema hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu. Nakuandikia haya, nikitaraja kuja kwako karibu. Lakini nikikawia, upate kujua sana jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu iliyo kanisa la Mungu aliye hayi, nguzo na msingi wa kweli. Na bila shaka siri ya utawa ni kuu. Mungu alidhibirishwa katika mwili, alihesabiwa kuwa na wema katika roho, alionekana na malaika, alikhubiriwa katika mataifa, aliaminiwa katika ulimwengu, alichukuliwa juu katika utukufu. ROHO yanena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho watu watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani, kwa unafiki wa watu wasemao uwongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru kujiepusha na vyakula ambavyo Mungu aliviumba vopokewe kwa shukrani na walio na imani na wenye kuijua sana kweli. Kwa maana killa kiumhe cha Mungu ni kizuri, waki hakuma cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani: kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kuomba. Ukiwakumhusha ndugu hayo, utakuwa mkhudumu mwema wa Yesu Kristo, na mzoevu wa maneno ya imani, na ya mafundisho yale mazuri uliyoyafuata. Bali hadithi za kizee, zisizo za dini, uzikatae. Jitahidi kupata utawa. Maana, kujitahidi kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, hali utawa hufaa kwa mambo yote; maana nna ahadi ya uzima wa sasa na wa ule utakaokuwa. Neno hili ni amini, lastahili kukubaliwa na wote. Kwa maana twajitaabisha na kujitahidi katika jambo hili, kwa sababu twamtumaini Mungu aliye hayi aliye mwokozi wa watu wote, khassa wa hao waaminio. Uwaagize watu hayo na kuwafundisha hayo. Mtu asiudharau ujana wako, bali uwe mfano kwao waaminio, katika usemi, na katika mwenendo, na katika upendo, na katika imani, na katika utakatifu. Hatta nijapo, fanya bidii katika kusoma na kuonya ua kufundisha. Usiache kuitumia ile karama iliyo udani yako uliyopewa wewe kwa unabii, na kwa kuwekewa mikono ya wazee. Uyatafakari hayo, ukae katika hayo. Kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote. Jitunze nafsi yako, na yale mafundisho. Ukadumu katika hayo; maana kwa kufanya hivi utajiokoa nafsi yako nao wakusikiao. USIMKEMEE mzee, bali mwonye kama baba, na wadogo wako kama ndugu: wanawake wazee kama mama, wanawake vijana kama ndugu, kwa utakatifu wote. Waheshimu wajane walio wajane kweli kweli. Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kutenda yaliyo wajib wao katika nyumba yao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Maana jambo hili ni zuri, tena lipendezalo mbele za Mungu. Bali yeye aliye mjane kweli kweli, na kuachwa peke yake, amemwekea Mungu tumaini lake, nae hudumu katika maombi na sala mchana na usiku. Na yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hayi. Uwaagize haya, illi wawe bawana lawama. Lakini mtu asiyewatunza walio wake na khassa watu wa nyumba yake ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini. Mjane aandikwe, ikiwa umri wake amepata miaka sittini, isipungue, nae amekuwa mke wa mume mmoja, na kushuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata killa tendo jema. Bali wajane walio vijana nkatae kuwaandika, maana wakiona tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa, nao wana hukumu, kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza. Na pamoja na hayo wajifunza kuwa wavivu, wakizungukazunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi, hujishughulisha na mambo ya wengine wakinena maneno yasiyowapasa. Bassi napenda wajane wasio wazee waolewe, wazae watoto, watawale mambo ya nyumbani, wasimpe adui nafasi ya kulaumu; maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani. Mwanamume au mwanamke aamimye, akiwa na wajane, awasaidie, kanisa lisilemewe; illi liwasaidie wale walio wajane kweli kweli. Wazee watawalao vema wapewe heshima mardufu, khassa wao wajitaabishao kwa kukhutubu na kufundisha. Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ngʼombe apurapo nganu: na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake. Usikubali mashitaka juu ya mzee, illa kwa vinywa vyao mashahidi wawili au watatu. Wale watendao dhambi, uwakemee mbele ya watu wote, illi na wengine waogope. Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Bwana Kristo Yesu, na mbele ya malaika wateule, yatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo. Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usishiriki dhambi za watu wengine. Jilinde nafsi yako uwe safi; tokea sasa usinywe maji tu, bali tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo marra nyingi. Dhambi za watu wengine ni dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhamhi zao zawafuata. Vivyo hivyo matendo mazuri ni dhahiri; na yale yasiyo dhahiri hayawezi kusetiriwa. WO wote waiio chini ya mafungo, hali ya utumwa, wawahesabu bwana zao kuwa wamestahili heshima yote, jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu. Na wale walio na mabwana waaminio, wasiwadharau kwa kuwa ni ndugu; hali afadhali wawatumikie, kwa sababu hao waishirikio faida ya kazi zao wamekuwa wenye imani na kupendwa. Uwafundishe mambo haya, na kuonya. Mtu akifundisba mafundisho mengine, nae hayakubali maneno yenye afya va Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundislio yapatanayo na ntawa, amejivuna, nae hakufahamu neno lo lote, bali hali yake hali va ugonjwa, kwa khabari ya maswali na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya, na majadiliano ya watu walioharibiwa akili zao, walioikosa kweli, wakidhani ya kuwa utawa ni njia ya kupata faida; ujitenge na watu kama hao, Lakini utawa pamoja na kuridhia ni faida nyingi. Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena ni dhahiri va kuwa hatuwezi kutoka na kitu bali tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo. Watakao kuwa na mali waanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa zisizo maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wana Adamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina moja la mabaya yote ni kupenda fedha, ambayo wengine wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani na kujichoma kwa maumivu mengi. Bali wewe, mtu wa Mungu, yakimbie hayo, ukafuate haki, utawa, imani, upendo, uvumilivu, upole. Fanya vita vile vizuri vya imani, shika uzima wa milele ulioitiwa, ukayaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi. Nakuagiza mbele za Mungu avipae vitu vyote uzima, na mbele za Kristo Yesu aliyeungama maungamo yale mazuri mbele ya Pontio Pilato, ilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hatta kudhihiri kwake Bwana wetu Yesu Kristo, ambako katika nyakati zake mwenyewe ataonyesha yeye mwenye uweza wote, Mfalme wa Wafalme, Bwana wa Mabwana, ambae yeye peke yake hapatikani na mauti, akaae katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hapana mwana Adamu aliyemwona, wala awezae kumwona, ndiye mwenye heshima na uweza milele. Amin. Uwaagize walio matajiri katika ulimwengu huu wasijivune, wala wasitumainie utajiri usio yakini, bali Mungu aliye hayi atupae vitu vyote kwa wingi, tuvitumie kwa furaha; watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo, wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao illi wapate uzima wa milele. Timotheo, ilinde amana, ukijiepisha na maneno yasiyo ya dini, yasiyo maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa nwongo; wengine wakiikiri hiyo wameikosa Imani. Neema na iwe pamoja nawe. PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kama alivyopenda Mungu, kwa ahadi ya uzima ulio katika Yesu Kristo: kwa Timotheo mwanangu mpendwa; Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. Namshukuru Mungu, nimwabuduye tangu zamani za wazee wangu kwa dhamiri safi, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu, mchana na usiku, ninatamani sana kukuona, nikikumbuka machozi yako, illi nijae furaha; nikikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, iliyokaa kwanza katika bibi yako Loi, na katika mama yako Euniki; aa ninasadiki ya kwamba na wewe nawe unayo. Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu. Maana Mungu hakutupa roho ya khofu, bali ya nguvu na ya upendo ua ya moyo wa kiasi. Bassi usiutahayarikie ushuhuda wa Bwana wetu, wala mimi mtumwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja na Injili kwa kadiri ya nguvu ya Mungu; aliyetuokoa akatuita kwa wito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake, tuliyopewa sisi katika Kristo Yesu, kabla ya nyakati za zamani; na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Yesu Kristo, aliyebatili mauti na kuufunua uzima ua kutoa kuharibika, kwa ile Injili, aliyonifauya mkhubiri na mtume na mwalimu wa mataifa. Kwa sababu hiyo nimepata mateso haya, wala sitahayariki: maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki kwamba aweza kukilinda kile nilichakiweka amana kwake hatta siku ile. Shika sura ya maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo uiio katika Kristo Yesu. Ilinde ile amana nzuri kwa Rolio Mtakatifu akaae ndani yetu. Wajua hili, ya kuwa wote walio katika Asia wameniacha, katika hao ni Figello na Hermogene. Bwana awape rehema walio wa uyumba ya Onesiforo; maana marra nyingi aliniburudisha, wala hakuutahayarikia mnyororo wangu; bali, alipokuwa katika Rumi, alinitafuta kwa bidii, akanipata. Bwana na ampe kuona rehema kwa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonikhudumia katika Efeso, wewe wajua sana. BASSI wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu. Na yale uliyoyasikia kwangu kwa mashahidi wengi, uwakabidbi hayo watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine. Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Yesu Kristo. Hakuna mfanya vita ajitiae katika shughuli za dunia; illi ampendeze yeye aliyemwandika awe askari. Hatta mtu akishindana hapewi taji asiposhindana kwa halali. Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kuyashiriki matunda. Yafahamu sana hayo nisemayo, maana Bwana atakupa akili katika mambo yote. Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daud, kama inenavyo injili yangu. Katika huyu nimeteswa kiasi cha kufungwa, kama mtenda mabaya; illakini neno la Mungu halifungwi. Kwa ajili ya hilo nastahimili yote, kwa ajili ya wateule, wao nao waupate wokofu ulio katika Kristo Yesu pamoja ua utukufu wa milele. Neno hili ni neno la kuaminiwa. Maana kama tukifa pamoja nae, tutaishi pamoja nae pia; kama tukistahimili, tutamiliki pamoja nae pia; kama tukimkana yeye, yeye nae atatukana sisi: ikiwa hatuamini, yeye hudumu kuwa mwaminifu, hawezi kujikana nafsi yake. Uwakumbushe bayo, ukiwaonya katika Bwana, wasiwe na mashindano ya maneno, yasiyo na faida, bali huwaharibu wasikiao. Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiyetahayarishwa, ukitumia kwa halali neno la Mungu. Jiepushe na maneno yasiyo na maana, yasiyo ya dini; maana wataendelea zaidi katika maovu; na neno lao litakuwa likitafuna kama donda ndugu. Katika hao ni Humenayo na Fileto, walioikosa kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, nao waipindua imani ya watu wengine. Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake; tena, killa alilajae jina la Bwana na aache uovu. Bassi katika nyumba havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina heshima. Bassi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hawa atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa killa kazi iliyo njema. Lakini zikimbie tamaa za ujana; nkafuate haki, na imani, na uaminifu, na upendo, na amani, pamoja na hao wamwitiao Bwana kwa moyo safi. Walakini yakatae maswali ya upumbavu, yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi: Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi, bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezae kufundisha, mvumilivu, akiwaonya kwai npole washindanao nae, illi, kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na ujuzi wa kweli, wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Shetani, wamepatikana wahayi nae, hatta kuyafanya apendayo Mungu. LAKINI ujue neno hili, ya kuwa siku za mwisho zitakuwa nyakati za khatari. Maana watu walakuwa wenye kujipenda nafsi zao, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kufuru, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, makhaini, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko Mungu; wenye mfano wa utawa, lakini wakikana nguvu zake; ujiepushe na hao. Kwa maana katika hawa wamo wale wajiingizao kalika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi, wakijifunza siku zote, wasiweze kabisa kufikia ujuzi wa kweli. Vile vile kama Yanne na Yambre walivyopingana na Mnsa, vivyo hivyo na hawa wapingana na kweli, ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani. Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote kama na wa hao ulivyokuwa. Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na upole, na upendo, na uvumilivu, tena adha zangu na mateso yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Lustra; killa namna ya adha niliyoistahimili: nae Bwana akaniokoa katika yote. Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya ntawa katika Kristo Yesu wataudhiwa. Lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na wakidanganyika. Bali wewe ukae katika yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni nani ambae ulijifunza kwake, na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, yawezayo kukuhekimisha hatta upate wokofu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. Killa andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibu katika haki; illi mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa illi atende killa tendo jema. NAKUSHUHUDIA mbele za Mungu, na Bwana Yesu Kristo, atakaewahukumu walio hayi na waliokufa, kwa kudhihiri kwake, na kwa ufalme wake; likhubiri neno, fanya bidii, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, kaonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Maana ntakuja wakati watakapoikataa elimu yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti, nao watajiepusha na kusikia yaliyo kweli watageukia hadithi za uwongo. Bali wewe erevuka katika yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mwinjilisti, timiliza khuduma yako. Maana mimi sasa namiminwa, na siku ya kufunguliwa kwangu imekaribia. Nimevifanya vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake. Jitahidi kuja kwangu upesi; maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu wa sasa, akasafiri kwenda Thessaloniki; Kreske Galatia, Tito Daimatia. Luka peke yake yupo hapa pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe; maana anifaa kwa kazi ya khuduma. Lakini Tukiko nalimpeleka Efeso. Joho lile nililomwachia Karpo Troa, ujapo, lete, navyo vitabu, zaidi vile vya ngozi. Iskander mfua shaba alinionya mabaya mengi; Bwana atamlipa kwa jinsi ya matendo yake. Nawe ujibadhari na huyo, kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu. Katika jawabu yangu ya kwauza hakuna mtu aliyesimama pamoja nami, bali wote waliniacha; wasihesabiwe khatiya kwa jambo bili. Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, illi kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, mataifa wrote wakasikie; nikaokolewa katika kanwa la simba. Na Bwana ataniokoa na killa neno baya na kunihifadhi hatta uje ufalme wake wa milele. Nisalimie Priska, na Akula, na nyumba ya Onesiforo. Erasto alikaa Korintho. Trofimo nalimwacha Mileto, hawezi. Jitahidi kuja kabla ya wakati wa baridi. Eubulo akusalimu, na Pudente, na Lino, na Klaudia, na ndugu wote pia. Bwana Yesu Kristo awe pamoja na roho yako. Neema na iwe nanyi. Amin. PAOLO, mtumwa wa Mungu, mtume wa Yesu Kristo, illi ienee imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli iletayo utawa, katika tumaini la nzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema nwongo aliuahidi kabla ya nyakati za zamani; akalifunua neno lake kwa nyakati zake katika ule ujumbe nilioaminiwa mimi kwa amri ya Mwokozi wetu, Mungu: kwa Tito, mwanangu katika imani tuishirikiyo: Neema na rehema na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo, Mwokozi wetu. Kwa sababu hii nalikuaeba katika Krete, illi nyatengeneze yaliyosalia, na kuweka wazee katika killa mji kama nilivyokuamuru; ikiwa mtu hakushitakiwa neno, nae ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni asharati na wasiotii. Maana imempasa askofu awe mtu asioshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mzoelea mvinyo, asiwe mpigaji, asiwe mpenda mapato ya aibu, bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kujimudu nafsi yake; alishikae neno la imani kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupingana nae. Maana wako wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo maana, wadanganyaji, khassa wale waliotahiriwa, ambao yapasa wazibwe vinywa vyao. Hawo wanapindua uyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu. Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema. Wakrete ni wawongo siku zote, nyama mwitu wahaya, walafi, wasiofanya kazi. Ushuhuda huu ni kweli. Kwa sababu hiyo uwakemee kwa ukali wapate uzima katika Imani, wasisikilize hadithi za Kiyahudi, na maagizo ya wana Adamn wajiepushao na kweli. Vitu vyote ni sali kwao walio safi: lakini hapana kilicho safi kwa walio najis, wasioamini, bali akili zao na nia zao pia zimekuwa najis. Wanakiri kwamha wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana, ni wenye machukizo, maasi, na kwa killa tendo jema hawafai. BALI wewe nena mambo yapasayo mafundisho ya uzima, ya kama wazee wawe wenye kujimudu nafsi zao, wenye adahu, wenye kiasi, wazima katika imani na katika upendo na katika uvumilivu. Na wazee wa kike vivyo hivyo wawe na mwenendo wa utakatifu, wasiwe wasiugiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; illi wawatie akili wanawake vijana wawapende wanme zao, ka kuwapenda watoto wao, na kuwa wenye niasi, na kuwa safi, kukaa nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao weuyewe, illi neno la Muugu lisitukanwe. Na vijana vivyo hivyo nwaonye kuwa na kiasi; katika mambo yote ukijionyesha kuwa namna ya matendo mema, katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahifu, na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa, illi yule mwenye kupingana nawe ataliayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu. Watumwa wawatii Bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wenye kujibu, wasiwe waibaji, bali wakionyesha uaminifu mwema wote, illi wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu katika mambo yote. Maana neema ya Mungu iwaokoayo wana Adamu wote imeonekana; yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ua kuishi kwa kiasi, na haki, na utawa, katika ulimwengu wa sasa, tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu, Mwokozi wetu Yesu Kristo; aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema. Nena maneno hayo, ukaonye ukakaripie kwa mamlaka yote; mtu aliye yote asikudharau. WAKUMBUSHE kujinyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa killa kazi njema, wasimtukane mtu, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote. Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, maasi, tumedanganywa, tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukienenda katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. Lakini wenia wa Mwokozi wetu Mungu na upendo wake kwa wana Adamu ulipoonekana, alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda, bali kwa rehema yake, kwa josho la kuzaliwa kwa pili, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu, ambae alitumwagia kwa wingi kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu, tukifanyiziwa wema kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu. Neno hili ni amini, na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, illi wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Haya ni mazuri, tena yana faida kwa wana Adamu. Maswali ya upuzi, na vitabu vya nasaba, na magomvi, na mashindano ya sharia, ujiepushe nayo. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana. Mtu mzushi, baada ya kumwonya marra ya kwanza na marra ya pili, mkatae; ukijua ya kuwa mtu kama huyu amegeukia mbali, tena afanya dhambi, amejihukumu nafsi yake. Nitakapomtuma Artema kwako an Tukiko, jitahidi kuja kwangu hatta Nikopoli; maana huku nimekusudia kukaa wakati wa baridi. Zena, mjua sharia, na Apollo uwusafirishe kwa bidii; wasipungukiwe cho chote. Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema kwa matumizi yaliyo lazima, illi wasiwe hawana matunda. Watu wote walio pamoja nami wakusalimu. Tusalimie wale watupendao katika Imani. Neema na iwe nanyi nyote. Amin. PAOLO, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yelu, kwa Filemon mpendwa wetu, mtenda kazi pamoja nasi, na kwa Appia, ndugu yetu mpendwa, na kwa Arkippo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako; Neema lwe nanyi na amani zitokazo kwa Mungu, baba yetu, tta kwa Bwana Yesu Kristo. Namshukuru Mungu wangu, siku zote nikikukumbuka katika maombi yangu, nikisikia khabari ya upendo wako na ya imani uliyo nayo kwa Bwana Yesu na kwa watakatifu wote; illi ushirika wa imani yako ufanye kazi yake katika ujuzi wa killa kitu chema kilicho kwenu katika Kristo Yesu. Maana tuna furaha na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu lmeburudishwa nawe, ndugu. Kwa hiyo, nijapokuwa nina ujasiri katika Kristo kukuagiza likupasalo; illakini, kwa ajili ya upendo, nakusihi, kwa kuwa ni kama nilivyo, Paolo mzee, na sasa mfungwa wa. Yesu Krlsto pia. Nakusihi kwa ajili ya mtoto wangu niliyemzaa katika mafungo yangu, Onesimo, ambae zamani allkuwa hakufai, hali sasa akufaa saua, wewe na mimi pia; niliyemtuma kwako, nawe umkubali, maana ni moyo wangu; ambae mimi nalimtaka akae nami, apate kunikhudumia hadala yako katika mafungo ya Injili; lakini slkutaka kuteuda neno isipokuwa kwa shauri lako, illi wema wako usiwe kama kwa shuruti, hali kwa khiari yako. Maana, labda ndio sababu alitengwa nawe muda kitambo illi uwe nae tena milele; tokea sasa, si kama mtumwa, baii lieha ya mtumwa, ndugu mpendwa, kwangu mimi sana, na kwako wewe zaidi sana, katika mwili na katika Bwana. Bassi kama ukiniona mimi kuwa mshirika nawe, mpokee huyu kama mimi. Na kama amekudhulumu, au awiwa nawe kitu, ukiandike juu yangu. Mimi Paoio nimeandika kwa mkouo waugu mweuyewe, nitalipa. Sikuambii kwamba wawiwa nami hatta nafsi yako. Naam, ndugu yangu, nipate faida kwako katika Bwana; uniburudishe moyo waugu katika Kristo. Nikiamini kutii kwako nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo. Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa: maana nataraja ya kwamba kwa maombi yenu mtajaliwa kunipata. Epafra, aliyefuugwa pamoja nami katika Kristo Yesu, akusalimu; na Marko, na Aristarko, na Dema, na Luka, watendao kazi pamoja nami. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. KWA sehemu nyingi na kwa namna nyingi Mungu zamani alisema na babu zetu katika manabii, mwisho wa siku bizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi yote, kwa yeye aliufanya ulimwengu. Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu; amefanyika bora sana kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko wao. Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Mwana wangu ndiwe, mimi leo nimekuzaa? na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, na yeye kwangu mwana? Hatta amletapo tena mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, anena, Na malaika wote wa Mungu wamsujudu. Na katika khabari za malaika anena, Afanyae malaika zake kuwa pepo, na watumislii wake ndimi za moto. Lakini katika khabari ya Mwana anena, Kiti chako, Mungu, ni cha milele; na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya kunyoka. Umependa haki, umechukia maasi: kwa sababu hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, mafuta ya shangwe kupita wenzako. Na, wewe, Bwana, mwanzo umeitia misingi ya inchi, na mbingu ni kazi za mikono yako; hizi zitaharibika, na wewe hukaa; hizi zitachakaa kama nguo, na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika; lakini wewe u yeye yule, na miaka yako haitakoma. Je! yuko malaika aliyeambiwa nae maneno haya wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume hatta nitakapoweka adui zako chiui ya nyayo zako? Hawo wote si roho zitumikazo, wakitumwa kuwakhudumu wale watakaourithi wokofu? KWA hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi yaliyasikiwa tusije tukayakosa. Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na killa kosa na uasi ulipata ujira wa haki, sisi je! tutapataje kujiponya, tusipotunza wokofu mkiju namna hii? ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kiisha nkathubutika kwetu na wale waliosikia; Mungu nae akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe. Maana hakuuweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao tunaounena, illa mtu mmoja ameshuhudu hivi maliali fullani, Mwana Adamu ni nini hatta umkumbuke, ama mwana wa binadamu hatta umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko malaika, umemvika taji ya utukufu na heshima, umemweka jua ya kazi za mikono yako; nmetia vitu vyote chini ya uyayo zake. Kwa maana katika kutia vitu vyote chini yake hakusaza kitu kisichotiwa. Illakini sasa hado hatujaona vitu vyote kutiwa chini yake, illa twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, illi kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya killa mtu. Kwa kuwa ilimpasa veye, ambae kwa ajili yake na kwa kazi yake vitu vyote vimekuwa, akileta wana wengi hatta utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokofu wao kwa mateso. Maana yeye atakasae nao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake; akinena, Nitalikhubiri jina lako kwa ndugu zangu; kati kati ya kanisa nitakuimba, na tena, Nitamtumaini: na tena, Tazama, mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu. Bassi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye nae vivyo hivyo alishiriki yayo bayo, illi kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Shetani, akawaokoe wale ambao kwamba maisha zao zote kwa khofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, illa atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. Kwa hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, illi afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. Na kwa kuwa aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa. KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu, aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemfanya, kama Musa nae alivyokuwa katika nyumba yake yote. Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kamti vile yeye aitengenezae nyumba alivyo na heshima zaidi ya nyumba hiyo. Maana killa nyumba imetengenezwa na mtu; illa yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu. Na Musa alikuwa mwaminifu katika nyumba yake yote kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa; bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba yake; ambae nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na kujisifu kwetu, kwa kutumaini mpaka mwisho. Kwa hiyo, kama anenavyo Robo Mtakatifu, Leo, kama mtasikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu, kama wakati wa kunikasirisha, siku ya kujaribiwa katika jangwa, hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, wakaona matendo yangu miaka arubaini. Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki nikasema, Ni watu waliopotoka mioyo hawa; hawakujua njia zangu; kama nilivyoapa katika hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu. Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hayi. Lakini muonyane killa siku, maadam iitwapo leo; mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu mpaka mwisho; hapo inenwapo, Leo, kama mtasikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu kama wakati wa kunikasirisha. Maana ni nani waliomkasirisha, waliposikia? Si wale wote waliotoka katika Misri wakiongozwa na Musa? Na ni nani aliochukizwa nao miaka arubaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa? Na ni nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, illa wale wasioamini? Bassi twaona ya kuwa bawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao. BASSI, ikiwa ikaliko abadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa. Maana ni kweli, sisi nasi tumekhubiriwa khabari njema kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa bao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia. Maana sisi tulioamini tunaingia katika raba ile; kama vile alivyonena, Nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia katika raha yangu: ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Kwa maana amenena siku ya saba niabali fullani hivi, Mungu alistarche siku ya saba, akaziacha kazi zake zote; na hapa napo, Hawataingia katika raha yangu. Bassi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia, na wale waliokhubiriwa khabari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao, aweka tena siku fullani, akisema katika Daud baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo kama mtasikia sauti yake, msiifanye migumu mioyo yenu. Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadae. Bassi, imesalia hali ya raha kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarche mwenyewe baada ya kazi yake, kama vile Mungu alivyostarche baada ya kazi zake. Bassi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, mtu ye yote asije akaanguka kwti mfano huo huo wa kuasi. Maana Neno la Mungu li hayi, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko ukali wa upanga ukatao kuwili, tena lachoma kiasi cha kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisicho wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu, na kufunuliwa machoni pake aliye na mambo yetu. Bassi, iwapo tunae kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, tujashike sana maungamo yetu. Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuyachukua mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijuribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote, bila dhambi. Bassi na tukikaribie kiti cha neema kwa nthubuitifu, illi tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. MAANA killa Kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wami Adamu amewekwa kwa ajili ya wana Adamu katika mambo yamkhusuyo Mungu, illi atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi; awezae kuwachukulia wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe yu katika liali ya udhaifu; na kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi. Na hapana mtu ajitwaliae heshima hii, illa yeye aitwae na Mungu kama vile Harimi. Vivyo hivyo Kristo nae hakujitukuza nafsi yake kufanywa Kuhani mkuu, lakini yeye aliyenena nae: Mwana wangu ni wewe, Mimi leo nimekuzaa: kama asemavyo mahali pengine, Wewe u Kuhani milele Kwa mfano wa daraja la Melkizedeki. Yeye siku hizo za niwili wake alimtolea yeye awezae kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa sababu ya kicho chake; na, ingawa yu Mwana, alijifunza kutii kwa mateso haya yaliyompata; nae alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokofu wa milele kwa watu wote wanaomtii; ametajwa na Mungu kuwa Kuhani mkuu kwa mfano wa daraja la Melkizedeki. Ambae tuna maneno mengi ya kunena katika khabari zake; na ni shidda kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia. Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita) mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. Kwa maana killa mtu atumiae maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. Lakini chakula kigumu in cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya. KWA sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo illi tuuflkilie utimilifu; tusiweke misingi tena, yaani kuzitubia kazi zisizo na uhayi, na kuwa na imani kwa Mungu, na mafundisbo ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele. Na tutafanya hayo kama Mungu akitujalia. Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hatta wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu marra ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri. Maana inchi iinywayo mvua iijiayo marra kwa marra, na kuzaa maboga yejiye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hupokea baraka kwa Mungu; bali ikitoa miiba ua magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; mwisho wake ni kuteketea. Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, katika khabari zenu tumesadiki mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokofu: maana Mungu si dhalimu hatta asahau kazi zenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewakhudumia watakatifu, na hatta hivi sasa mngali mkiwakhudumia. Nasi twataka killa mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hatta mwisho; illi msiwe wavivu, hali wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imaui na uvumilivu. Kwa maana Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi, kwa kuwa alikuwa hana mkuhwa kuliko nafsi yake wa kumwapia, aliapa kwa nafsi yake, akisema, iiakika yangu nitakubariki, na hakika yangu nitakuongeza. Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi. Maana wana Adamu humwapia yeye aliye mkuu: na ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kiyathubutishe. Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonyesha wairithio ile ahadi jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati; illi kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu bawezi kusema nwongo, tupate faraja lililo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu; tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo mle mlimo ndani ya pazia, alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa Kuhani mkuu kwa jinsi ya Melkizedeki hatta milele. KWA maana Meikizedeki huyo, mfalme wa Salemi, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu baada ya kuwapiga wafalme, alimbariki; aliyegawiwa na Ibrahimu sehemu ya kumi ya vitu vyote; (kwanza kwa tafsiri, mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemi, maana yake, mfalme wa amani; hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhayi wake, bali amefanauishwa na Mwaua wa Mungu,) adumu kuhani milele. Bassi, angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambae Ibrahimu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya maleka yaliyo mema. Na katika wana wa Lawi, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani ndugu zao, kwa agizo la sharia, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu. Bali yeye, ambae uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu, akambariki yeye aliye na ile ahadi. Na haikanushiki kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa. Na hapo wana Adamu wapaswao na kufa hutwaa sehemu ya kumi; bali huku yeye ashubudiwae kwamba yu hayi. Na yaweza kusemwa ya kuwa, kwa njia ya Ibrahimu, hatta Lawi apokeae sehemu ya kumi alitoa sehemu ya kumi; kwa maana alikuwa katika viuno vya bada yake Ibrahimu, hapo Melkizedeki alipokutana nae. Bassi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi: (maana watu wale waliipata sharia kwa huo) kulikuwa na haja gani tena kuhani mwingine aondoke, wa daraja la Melkizedeki, wala si kwa daraja la Haruni? Maana ukuhani ule ukihadilika, hapana buddi sharia nayo ibadilike. Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa mshirika wa kahila nyingine, wala hapana mtu wa kahila hii aliyeikhudumia madhbahu. Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lolote la kuikhusu katika mambo ya ukuhani. Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine kwa mfano wa Melkizedeki; asiyekuwa kuhani kwa sharia ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na kikomo: maana ashuhudu, kwamba, Wewe u kuliani hatta milele kwa daraja la Melkizedeki. Maana, kima kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia, kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake (kwa maana sharia ile haikukamilisha neno); na pamoja na haya kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwayo twamkaribia Mungu. Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo, (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; hali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe kuhani hatta milele kwa daraja la Melkizedeki;) bassi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo hora zaidi. Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na manti wasikae; hali yeye, kwa kuwa akaa milele, ana ukuhani usioondoka. Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee. Maana ilipendeza sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii, aliye mtakatifu, asiokuwa na uovu, asiokuua na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu; asiye na baja killa siku, kwa mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kiisha kwa ajili ya dhambi za watu; maana yeye alifanya hivi marra moja, alipojitoa nafsi yake. Maana torati yawaweka wana Adamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hatta milele. BASSI, katika hayo tuuayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunae kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni, mkhudumu wa patakatifu, na wa khema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwana Adamu. Maana killa kuhani mkuu awekwa illi atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu nae awe na kitu akitoe. Kama angekuwa juu ya inchi, asingekuwa kuliani; maana wapo watoapo sadaka kama iagizavyo sharia; watumikao kwa mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile khema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima. Lakini sasa amepata khuduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mtengenezaji wa agano lililo bora, lililoamriwa kwa ahadi zilizo bora na kuzitegemea. Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili. Maana, awalaumupo, asema, Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya; halitakuwa kama agano lile nililofanyana na baba zao, katika siku ile nilipowashika mikono yao uiwatoe katika inchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, mimi nami sikuwaangalia, asema Bwana. Maana hili ndilo agano nitakalofanyana na nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Bwana; nitatia sharia zangu katika nia zao, na katika mioyo yao nitaziandika; nami mtakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu waugu. Nao hawatafundishana killa mtu na jirani yake, na killa mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; kwa maana wote watunijua, tangu mdogo wao hatta mkubwa wao. Kwa sababu nitawasamehe dhumlumu zao, na dhambi zao sitazikumbuka tena. Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikukuu na kuchakaa ni karibu na kutoweka. BASSI hatta agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidumia. Maana khema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na taa, na meza, na mikate iliyotolewa kwa Mungu; palipoitwa, Patakatifu. Na nyuma ya pazia la pili, ile khema iitwayo Patakatifu pa patakatifu, yenye cheteso cha dhahabu, na sanduku ya agano iliyofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye manna, na fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vibao vya agano; na juu yake makerubi ya utakatifu, yakilitia kivuli kao la rehema; bassi hatuma nafasi ya kueleza khabari za vitu hivi moja moja. Bassi, vitu hivi vikiislia kutengenezwa hivyo, makuhani huingia khema ya kwanza siku zote, wakiyatimiza mambo va ibada. Lakini katika khema ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, marra moja killa mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na dhambi za ujinga za watu. Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo khema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama. Hii ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhahihu zinatolewa, zisizoweza kumkamilisha mtu aabunduye dhamiri yake, kwa kuwa ni sharia za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hatta wakati wa matengenezo mapya. Lakini Kristo akiisha kuwapo, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwa, kwa khema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia marra moja katika patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ngʼombe waliyonyunyizwa wenye uchafu hutakasa hatta kuutakatisha mwili; bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi? Na kwa sababu hii yu mjumbe wa agauo jipya, illi, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya katika agano la kwanza, walioitiwa waipokee ahadi ya urithi wa milele. Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya. Kwa maana agano lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, maadam yu hayi yeye aliyelifanya. Kwa hiyo hatta lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu. Maana killa amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa watu wote, kama ilivyoamuru sharia, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi pamoja na maji na sufu nyekundu na husopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote, akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu. Na ile khema na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivi hivi. Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. Bassi sharti manukulu ya mambo yaliyo mbinguni yasafishwe kwa haya, lakini mambo ya mbinguni yenyewe kwa dhabibu zilizo bora kuliko haya. Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyiku kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu palipo patakatifu khalisi; hali aliingia mbinguni khassa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu; wala si kusudi ajitoe marra nyiugi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo patakatifu killa mwaka kwa damu isiyo yake; kana ni hivyo, ingalimpasa kuteswa marra nyingi tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu; lakini sasa, marra moja tu, katika mwisho wa dunia, ameonekana, atangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake. Na jinsi watu wanavyowekewa kufa marra moja, na baada ya kufa hukumu: kadhalika Kristo, akiisha kutolewa sadaka marra moja aziondoe dhambi za watu wengi, marra ya pili, pasipo dhambi, ataonekana nao wamtazamiao kwa wokofu. BASSI kwa kuwa torati ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo, kwa dhahihu zile zile wanazozitoa killa mwaka daima, hawawezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao. Kama wangeweza, wangeacha kuzitoa; kwa maana waabuduo, walipokwisha kusatishwa kwa marra moja, wasingejiona tena kuwa na dhamhi? Lakini katika hizo liko kumbukumbu la dhambi killa mwaka. Maana haiyumkini damu ya mafahali na mbuzi iondoe dhambi. Kwa biyo ajapo ulimwenguni, anena, Dhambi na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari: Kafara na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo: Ndipo nilisema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) niyafanye mapenzi yako, Mungu. Hapo juu anenapo, Dhabihu na matoleo na kafara na sadaka za dhamhi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo ilivyoamuru torati), ndipo alinena, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, illi kusudi alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo marra moja. Na killa kuhani husimama killa siku akifanya ibada, akitoa dhabihu zilezile marra nyingi; nazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. Lakini huyu, alipokwisha kutoa dhabihu nioja kwa dhambi, idumuyo hatta milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; akingojea hatta adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. Maana kwa toleo moja amewakamilisha hatta milele wanaotakaswa. Na Roho Mtakatifu yatushuhudia; kwa maana, baada ya kunena, Hili ni agano nitakalowapa baada ya siku zile, anna Bwana, Nitatia sharia zangu mioyoni mwao, na katika akili zao nitaziandika; ndipo anenapo. Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Bassi ondoleo la baya lilipo, hapana toleo tena kwa dhambi. Bassi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia aliyotuanzia mpya, hayi, ipenyayo katika pazia, yaani mwili wake; na Kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu; tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa mwili kwa maji safi. Tulishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni amini; tukaangaliane kiasi cha kusukumana katika upendo na kazi nzuri; tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tukionyana; na tukizidi, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuitazamia hukumu kwenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. Mtu aliyeidharau sharia ya Musa, alikufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa nayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho ya neema? Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake. Ni jambo la kutisba kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hayi. Lakini zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu; pindi mlipotwezwa kwa mashutumu na mateso, na pindi mliposhirikiana na wale waliotendewa hayo. Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika mafungo, mkakubali kwa furaba kunyangʼauywa mali zenu, mkijua nafsini mwenu kwamba mna mali mbinguni iliyo njema zaidi, idumnyo. Bassi msiutupe njasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Maana mnahitaji uvumilivu, illi mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu muipate abadi. Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajae atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye haki ataishi kwa imani; nae akisitasita, roho yangu haina furaha nae. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali miongoni mwao walio na imani ya kutuokoa roho zetu. BASSI imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa. Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hatta vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. Kwa imani Habil alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kain; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo ijapokuwa amekufa, angali akinena. Kwa imani Enok alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha: maana kabla ya kuhamishwa kwake alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu. Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu ampendezae Mungu lazima aamini kwamba yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani. Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, akatoka aende hatta mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. Kwa imani alikaa katika ile inchi ya ahadi, kama katika inchi isiyo yake, akikaa katika khema pamoja na Isaak na Yakobo, warithi pamoja nae wa ahadi ile ile. Maana waliutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuujenga na kuufanyiza ni Mungu. Kwa imani hatta Sara mwenyewe alipokea nwezo wa kuwa na mimba, alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimwona yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu. Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, nae kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufukoni, usioweza kuhesabiwa. Hawa wote wakafa katika imani, wasizipokee zile ahadi, bali wakiziona tokea mbali na kuzisalimu, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya inchi. Maana wasemao maneno kama hayo waonyesha kwa wazi kwamba wanatafuta inchi yao wenyewe. Na kama wangaliikumbuka inchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea. Lakini sasa waitamani inchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji. Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaak, awe dhabihu; na yeye aliyezipokea ahadi alikuwa akimtoa mwana wake, mzaliwa wake wa pekee; naam, yeye aliyeamhiwa, Katika Isaak uzao walio utaitwa, akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano. Kwa imani Isaak akawahariki Yakobo na Esau, hatta katika khabari ya mambo yatakayokuwa baadae. Kwa imani Yakobo, alipokuwa katika kufa, akambariki killa mmoja wa wana wa Yusuf, akaabudu akiegemea kitanda chake. Kwa imani Yusuf, alipokuwa amekaribia mwisho wake, alitaja khabari za kutoka kwao wana wa Israeli, akawaagizia mifupa yake. Kwa imani Musa, alipozatiwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; wala hawakuiogopa amri ya mfalme. Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao; akaona ui afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha kwa dhambi kitamho; akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mwingi kuliko hazina za Misri. Kwa imani akatoka Misri, asiogope hasira ya mfalme; maana alistahimili kama amwonae yeye asiyeonekana. Kwa imani akaifanya Pasaka, na kunyunyiza ile damu, illi mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao. Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Sham, kama katika inchi kavu; Wamisri wakaijaribia wakatoswa. Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zikiisha kuzungukwa siku saba. Kwa imani Rahab, yule kahaba, hakuangamia pamoja nao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wapelelezi kwa amani. Na niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta khabari za Gideon na Barak na Samson na Yeftha na Daud na Samwil na manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, waliziba makanwa ya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na ukali wa upanga. Walitiwa nguvu baada va kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni. Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa: na wengine walibanwa, wasiukubali ukombozi, wapate ufufuo ulio bora: wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani: walipigwa mawe, walikatwa kwa msumeno, walishawishwa, waliuawa kwa upanga: walizungukazunguka, wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; waiikuwa wahitaji, wakindhiwa, wakitendwa mabaya: (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao): walikuwa wakizungukazunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya inchi. Na watu hawa wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi: kwa kuwa Mungu ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, illi wasikamilishwe pasipo sisi. BASSI na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, tuweke kando killa mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa uvumilivu katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. Maana mtafakarini sana yeye aliyeyavumilia mapingamizi makuu namna hii ya wenye dhambi juu ya nafsi zao, msije mkadhoofika mkizimia mioyoni mwenu. Hamjafanya vita kiasi cha kumwaga damu, mkishindana na dhambi: tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama na wana. Mwanangu, usikudharau kurudi kwake Bwana, Wala, usizimie ukikemewa nae; Maana yeye ambae Bwana humpenda, humrudi, Nae humpiga killa mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwavumilia; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiorudiwa na baba yake. Bassi kama mkiwa hamna kurudiwa walikoshiriki wote, mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. Na pamoja na haya tulikuwa na baba za mwili wetu walioturudi, tukawastahi; bassi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi. Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu illi tuushiriki utakatifu wake. Killa adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini huwatolea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani. Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, mkaifanyia miguu yenu njia za kunyoka, illi kitu kilicho kilema kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe. Fanyeni bidii kutafuta amani kwa watu wote, na utakatifu, ambao hapana mtu atakaemwona Mungu asipokuwa nao; mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua watu wengi, wakatiwe najis kwa hilo. Asiwepo asharati au asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja. Maana mwajua ya kuwa hatta alipotaka baadae kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi. Maana hamkufikilia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingi jeusi, na giza, na tufani, na mlio wa baragumu na sauti ya maneno; ambayo wale waliosikia walisihi wasiambiwe neno lo lote lingine; maana hawakuweza kustahimili neno lile lililoamriwa, Hatta nyama akiugusa mlima atapigwa mawe au atachomwa kwa mkuki. Na baya yaliyoonekana yalikuwa ya kutisha, hatta Musa akasema, Nashikwa na khofu na kutetemeka. Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye tiayi, Yerusalemi wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mwenye kuleta agano jipya, na damu ya kunyunyizwa inenayo mema kuliko ile ya Habil. Angalieni msimkatae yeye anenae. Maana ikiwa wale hawakuokoka waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya inchi, sembuse sisi tukijiepusha nae atuonyae kutoka mbinguni: Ambae sauti yake iliitemetesha inchi wakati ule: lakini sasa ameahidi akinena, Marra moja tena naitetemesha inchi wala si inchi tu, bali na mbingu pia. Neno lile, Marra moja tena, ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, illi vitu visivyoweza kutetemeshwa vikae. Bassi tukipokea ufalme usioweza kutetemeshwa, tuwe na neema, illi kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho: maana Mungu wetu ni moto ulao. UPENDANO na udumu. Msisahau kuwafadhilia wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua. Wakumbukeni waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; nao wanaodhulumiwa, kwa kuwa nanyi m katika mwili. Ndoa iheshimiwe na watu wote, na malalo yawe safi: kwa maana waasharati na wazinzi Mungu atawahukumu. Msiwe na tabia ya kupenda fedha: mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Hatta twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiae, sitaogopa: mwana Adamu atanitenda nini? Wakumbukeni wale waliokuwa na mamlaka juu yenu, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa maisha zao, iigeni imani yao. Yesu Kristo, jana na leo yeye yule na hatta milele. Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida. Tuna madhbahu ambayo wale waikhudumiao khema bawana rukhusa kula vitu vyake. Maana nyama wale ambao damu yao ludetwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kituo. Kwa ajili hii Yesu nae, illi awatakase watu wake kwa damu yake miwenyewe, alitesyia nje ya mlango. Bassi na twende kwake nje ya kituo, tukichukua laumu lake. Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. Bassi na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo ya watu waliungamao jina lake. Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana na watu; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu. Watiini walio na mamlaka juu yenu, na kujinyenyekea kwao; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, illi wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi. Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote. Nami nawasihini zaidi sana kufanya hayo illi nirudishwe kwenu upesi. Bassi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka wafu Mchungaji wa kondoo aliye mkuu, kwa damu ya agano la milele, Bwana wetu Yesu, awafanye kuwa wrakamilifu katika killa tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, nae akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amin. Nawasihini, ndugu, livumilieni neno hili lenye maonyo; maana nimewaandikia kwa maneno machache. Jueni ya kuwa ndugu yetu Timotheo amekwisha kufunguliwa; pamoja nae nitawaoneni, kama akija upesi. Wasalimuni wote walio na mamlaka juu yenu, na watakatifu wote; walio wa Italia wanakusalimuni. Neema na iwe nanyi nyote. Amin. YAKOBO, mtumwa wa Mungu, na Bwana Yesu Kristo, kwa kabila thenashara zilizotawanyika, salamu, Hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, ndugu zangu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa imani yenu huleta saburi. Na saburi iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa neno. Lakini mtu wa kwemi akipungukiwa hekima, aombe dua kwa Mungu, awapae wote kwa ukarimu, wala hakemei; nae atapewa. Illa aombe kwa imani, pasipo shaka lo lote; maana mwenye mashaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa kwa upepo, na kupeperushwa huko na huko. Maana mtu yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana; mtu wa nia mbili asitasita katika njia zake zote. Lakini ndugu asiye na cheo afurahi kwa kuwa ametukuzwa; na tajiri kwa kuwa ameshushwa: kwa maana kama ua la majani atatoweka. Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; na lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo nae tajiri atanyauka katika njia zake. Yu kheri astahimiliye majaribu; kwa sababu akipata kibali ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. Mtu, ajarihiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu: maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini killa mmoja hujaribiwa akivutwa na kudanganywa na tamaa yake mwenyewe. Khalafu ile tamaa ikiisha kuchuikua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. Msidanganyike, ndugu zangu wapenzi. Killa kutoa kwenia, na killa kitolewacho kilicho kamili, chatoka juu, chashuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka. Alipopenda alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limhuko la viumbe vyake. Bassi killa mtu awe mwepesi wa kusikia, mzito wa kusema, mzito wa ghadhabu; kwa maana ghadhabu ya mwana Adamu haiitendi haki ya Mungu. Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, kapokeeni kwa upole neno lililopandwa, liwezalo kuokoa roho zenu. Mwe watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, mkijidanganya nafsi zenu. Kwa sababu mtu akiwa msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyu ni kama mtu anaejiangalia uso wake wa asili katika kioo. Maana hujiangalia, kiisha huendazake, marra akasahau jinsi alivyo. Lakini aliyeitazama sharia kamilifu ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyu atakuwa wa kheri katika kutenda kwake. Mtu akidhani ya kuwa ana dini, nae hazuii ulimi wake kwa khatamu, akijidanganya moyo wake, dini yake mtu yule haifai. Dini iliyo safi na isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika shidda yao, na kujilinda pasipo mawaa katika dunia. NDUGU zangu, msiwe na imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana mwenye utukufu, kwa kupendelea watu. Maana akiingia katika sunagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri, na akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri, na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, je! hamkufanya ihtilafu mioyoni mwenu mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu? Sikihzeni, ndugu niwapendao, Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao? Bali ninyi mmemvunjia heshima maskini. Je! matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya viti vya hukumu? Hawalitukani jina lile zuri mliloitwa? Illakini mkiitimiza sharia ya kifalme kama ilivyoandikwa. Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vyema. Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sharia kama wakosaji. Maana mtu awae yote atakaeishika sharia yote, na pamoja na hayo, akijikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, alisema, Usiue, pia. Bassi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sharia. Semeni ninyi, katendeni kama watu watakaohukumiwa kwa sharia ya uhuru. Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Na huruma hujitukuza juu ya hukumu. Yafaa nini, ndugu zangu, mtu akisema ana imani, nae hana matendo? Je! ile imani yaweza kumwokoa? Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa riziki, mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, illakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini? Vivyo hivyo na imani, isipokuwa na matendo, imekufa nafsini mwake. Lakini mtu atasema, Wewe una imani, nami nina matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo yako, nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu. Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vyema. Mashetani nao waamini na kutetemeka. Lakini wataka kujua, wewe mwana Adamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? Je! baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaak mwanawe juu ya madhbahu? Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na imani ile ilikamilishwa kwa matendo yale. Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu ikahesabiwa kwake kuwa ni haki: nae aliitwa raliki wa Mungu. Mwaona kwamba mwana Adamu ahesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa iinaui peke yake. Na Rahab, yule kahaba nae, je! hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine? Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa. MSIWE waalimu wengi, ndugu zangu, mkijua ya kuwa tutapata hukumu kubwa zaidi. Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezae kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu. Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, illi watutii, na twageuza mwili wao wote. Kaziangalieni merikebu; ingawa ni kubwua namna gani, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote aazimuko kwenda yule aongozae. Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, na hujivuna majivuno makuu. Kaangalieni jinsi moto mdogo uwasbavyo kuni nyingi sana. Nao ulimi ni moto, ulimwengu wa uovu. Ndio khabari ya ulimi katika viungo vyetu, huutia najis mwili wote, huliwasha moto gurudumu la maumbile, nao huwashwa moto na jehannum. Maana killa aina ya nyama, na ya ndege, na ya nyama watambaao, na ya vitu vilivyo baharini vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wana Adamu. Bali ulimi hapana mwana Adamu awezae kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti. Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wana Adamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, mambo haya hayapasi kuwa hivyo. Je! chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu? Ndugu zangu, mtini waweza kuzaa mazeituni au mzabibu tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na niaji matamu. Nani aliye na hekima na fahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima. Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na magomvi mioyoni mwenu msijisifu, wala msiseme nwongo juu ya kweli. Hekima hii siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, na ya tabia ya kibinadamu, na ya Shetani, maana hapo palipo wivu na magomvi, ndipo palipo machafuko, na killa tendo la aibu. Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina wala unafiki; na tunda la baki hupandwa katika amani kwa wale wafanyao amani. VITA na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humo, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? Mwatamani, wala hanma kitu; mwana na kuona wivu, na hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi. Mwaomba wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, illi mvilumie kwa tamaa zenu. Enyi wazinzi, wanaume na wanawake, hamjui ya kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? bassi killa atakae kuwa rafiki wa dunia ajifanya kuwa adui wa Mungu. Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema burre? Roho ikaayo ndani yetu hutamani kiasi cha kuona wivu? Lakini atupa sisi neema nyingi zaidi; kwa hiyo asema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neemi wanyenyekevu. Bassi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, nae atawakimbia. Mkaribieni Mungu, nae atsiwakaribieni ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, kaisafisheni mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Jihuzunisheni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu kugeuzwe kuwa kuomboleza na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za Bwana, nae atawakuzeni. Msisingiziane, ndugu; amsingiziae ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, aisingizia sharia na kuihukumu sharia. Lakini ukiihukumu sharia, huwi mtenda sharia, bali mhukumu. Mtoa sharia na mbukumu ni mmoja tu, awezae kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umbukumuye mwenzako? Haya bassi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia mji fullani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; nanyi hamjui yatakayokuwa kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi moshi uonekanao kwa kitambo, kiisha hutoweka. Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hayi na kufanya hivi au hivi. Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kwote kwa namna hii ni kubaya. Bassi yeye ajuae kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyu ni dhambi. HAYA bassi, enyi matajiri! lieni yowe kwa sababu ya mashaka yanayokujieni. Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itakushuhudieni, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku hizi za mwisho. Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, uliozuiliwa nanyi kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa Sabaoth. Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. Mmemhukumu mwenye haki mkamwua: nae hashindani nanyi. Bassi vumilieni, ndugu, hatta kuja kwake Bwana. Mwangalieni mkulima; hungoja mazao ya inchi yaliyo ya thamani, husubiri kwa ajili yake hatta yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. Bassi, na ninyi subirini, jithubutisheni mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. Msinungʼunikiane, ndugu, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango. Watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu. Angalieni, twawaita wenye kheri wao waliovumilia. Mmesikia khabari ya uvumilivu wa Ayub, mmenona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwenye rehema nyingi, mwenye huruma. Lakini zaidi ya yote, ndugu, msiape kiapo cho chote, kwa mbingu wala kwa inchi; bali ndio yenu iwe ndio, na sio yenu iwe sio, msije mkaangukia hukumu. Mtu wa kwenn amepatikana na mabaya? na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? na aimbe zaburi. Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? na awaite wazee wa kanisa wakamwombee, wakimpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; na kama amefanya dhambi, atasamehewa. Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. Eliya alikuwa mwana Adamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinye: na mvua haikunya juu ya inchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, inchi ikazaa matunda yake. Ndugu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali ya kweli, na mtu mwingine akamrejeza; ajue va kuwa veve amrejezae mwenye dhambi, atoke katika njia ya upotovu, ataiokoa roho ya mtu yule na mauti, na kufunika wingi wa dhambi. PETRO, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Mtawanyiko, wakaao bali ya wageni katika Ponto, Galatia, Kappadokia, Asia na Bithunia, kama vile Mungu alivyotangulia kuwajua tangu milele katika utakaso wa Roho, hatta wakapata kutii na kunyunyizwa damu ya Yesu Kristo; Neema na amani ziongezwe kwenu. Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambae kwa rehema zake nyingi alituzaa marra ya pili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuliwa kwake Yesu Kristo, tupate urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu, mnaolindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani mpate wokofu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho. Mnafurahi sana kwa ajili yake, ijapokuwa sasa kwa kitambo, ikiwa ni lazima, mmchuzunishwa kwa majaribu ya namna mbali mbali, illi kujaribiwa kwake imani yenu, ambako kuna thamani kuu kuliko dbahabu ipoteayo, ijapokuwa imejaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo: ambae mwampenda, ijapokuwa hamkumwona: ambae ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini, na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, iliyotukuzwa, mkiupokea mwisho wa imani yenu, wokofu wa roho zenu. Katika khabari ya wokofu huo walitafutatafuta na kuchunguzachunguza manabii waliotabiri khabari va neema itakayowafikia, wakitafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho ya Kristo iliyokuwa ndaui yao, aliyetangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwa baada ya hayo. Waliofunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yetu walitumika katika mambo hayo, ambayo sasa yamekhubiriwa kwenu na wale waliowakhubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hiayo malaika wanatamani kuyachuugulia. Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, mwe na kiasi, kwa utimilifu mkiitumainia ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza, za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi mwe watakatifu katika mwenendo wenu wote; maana imeandikwa, Mwe watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Na ikiwa mnamwita Baba yeye ahukumuye killa mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa khofu kafika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni; mkijua kwamba hamkukombolewa kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu, mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlionpokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana kondoo asio na ila, na asio na waa, ya Kristo, aliyejuliwa tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifimuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu, ambae kwa yeye mlimwamini Mungu, aliyemfufua akampa utukufu; hatta imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu. Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo; kwa kuwa mmezaliwa marra ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali isiyoharibika, kwa neno la Mungu lenye uzima, na lidumulo hatta milele. Maana, Mwili wote kama majani, Na utukufu wake wote kama ua la majaui. Majani hukauka na ua lake huanguka; Bali Neno la Bwana hudumu hatta milele. Na neno bilo ni neno lile jema lililokhubiriwa kwenu. BASSI, mkiwekea mbali uovu wote na hila yote na unafiki na husuda na niasingizio yote, kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, illi kwa hayo mpate kunkulia wokofu; ikiwa mmeonja kwamba Bwana ni mwenye fadhili. Mkimwendea yeye, jiwe lililo hayi, lililokataliwa na wana Adamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye thamani, ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hayi, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani utakatifu, mtoe dhabibu za roho, zipatazo kibali kwa Mungu, kwa Yesu Kristo. Kwa kuwa ndiyo yaliyomo katika maandiko, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye thamani, Na killa amwaminiye hatatabayarika. Bassi, thamani hii ni kwenu ninyi mnaoamini, bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni; tena, Jiwe lakujikwaza mguu, na mwamba wa kujiangusha; maana hujikwaza kwa neno lile, wakiliasi, nao waliwekwa wapate hayo. Bali ninyi m mzao mteule, ukubani wa kifaume, taifa takatifu, watu wa milki, mpate kutangaza fadhili zake aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. Mapenzi, nakusihini kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho; mwe na maongezi mazuri kati ya Mataifa, illi, iwapo huwasingizia kuwa mnatenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa nae. Tumikieni killa kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa mfalme, kama mwenye cheo kikuliwa; ikiwa wakubwa, kama wanaotumwa nae kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema; kwa sababu ndio mapenzi ya Mungu, kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu; kama huru, na wasiontumia uhuru kwa kusetiri ubaya, bali kaina watumwa wa Mungu. Heshimuni walu wote. Upendeni udugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme. Enyi watumishi, watiini bwana zenu kwa khofu nyingi; sio wao walio wema na wenye upole fu, bali nao walio wakali. Maana huu ndio wema khassa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, ateswapo isivyo baki. Kwa maana ni sifa gani kuvumilia, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kuvumilia, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema khassa mbele za Mungu. Kwa sababu ndio mlioitiwa: maana Kristo nae aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachieni mfano, mfuate nyayo zake; yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake; yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki; yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, illi, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe bayi kwa mambo ya haki; kwa kuchubuka kwake mliponywa. Kwa maana mlikuwa kama kondoo wanaopotea; lakini sasa mmemrudia Mchunga na Askofu wa roho zenu. KADHALIKA ninyi wake, watumikieni waume o zenu; kusudi, ikiwa wako waume wasioliamini Neno, kwa mwenendo wa wake zao, pasipo Neno lile, wavutwe; wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa khofu. Kujipamba kwao, kusiwe kujipamba kwa nje, ndio kusuka nywele, na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali mtu wa moyoni asiyeonekana, katika jambo lisiloharibika; ni roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana bivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumainia Mungu, wakiwatumikia waume zao; kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; ninyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala kushitushwa kwa khofu yo yote. Ninyi wanme kadhalika, kaeni na wake zenu kwa akili; mkimpa mke heshima, kama chombo kisieho nguvu, na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi sala zenu zisizuiliwe. Neno la mwisbo ni hili; mwe na nia moja, wahurumianao, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; watu wasiolipa baya badala ya baya, au laumu badala ya laumu; bali wabarikio; kwa sababu ndiyo mlioitiwa illi mrithi baraka. Kwa maana, Atakae kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie nlimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila: Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana. Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombo yao: Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya. Na ni nani atakaewadhuru, mkiwa waigaji wa wema? Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki, in kheri; msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu; mwe tayari siku zote kumjibu killa mtu akuulizae khabari za tumaini lililo ndani yenu; kwa upole na kwa khofu, mkiwa na dhamiri njema, illi katika neno lile mnalosingiziwa kwamba m watenda mabaya, wataha yarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo. Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndio mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya. Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa. Kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawakhubiri watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ndani yake watu wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji. Mfano wa mambo haya ni ubatizo, nnaowaokoa na ninyi siku hizi; (sio kuwekea, mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo; alioko mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zimetiishwa chini yake. BASSI kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake kwa ajili yenu, ninyi nanyi jivikeni nia ile ile kama silaha; kwa maana yeye allyeteswa katika mwili, ameachana na dhambi; kuanzia sasa tusiendelee kuishi katika tamaa za wana Adamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wetu wa kukaa hapa duniani uliobakia. Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda wayapendayo mataifa, kuenenda katika uasharati, ua tamaa, na ulevi, ua karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali: mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao hatta ufisadi usio kiasi, wakiwatukaneni; watakaotoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hayi na waliokufa. Maana kwa ajili hiyo na wao waliokufa walikhubiriwa Injili, illi waluikumiwe katika mwili wahukumiwavyo wana Adamu; bali wawe hayi katika roho kwa kumtii Mungu. Mwisho wa mamho yote umekaribia; bassi, mwe na akili, mkakeshe katika sala: zaidi ya yote mwe na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husetiri wingi wa dhambi; mwe wakaribishaji ninyi kwa ninyi, pasipo kunnngʼunika; killa mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kukhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu. Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin. Wapenzi, msione kuwa ni ajahu ule msiba unaowapata kama moto illi mjaribiwe, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho; lakini kama mnavyoyashiriki mateso va Kristo furahini; illi na katika ufimuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni kheri yenu, kwa kuwa Roho ya utukufu na ya Mungu unawakalia; kwa hawo anatukanwa, bali kwenu ninyi anatukuzwa. Maana mtu wa kwenu asiteswe kama muuaji, au mwizi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishae na mambo ya watu wengine. Illakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hili. Kwa maana wakati umefika hukumu ianzie nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu, nini mwisho wao wasioitu Injili ya Mungu? Na mwenye haki akiokoka kwa shidda, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi? Bassi wao wateswao apendavyo Mungu na wamwekee roho zao kama amana, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu. NAWASIHI wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadae; lichungeni kundi la Kristo lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa khiari; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo; wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya mfano kwa lile kundi. Na mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka. Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu kama mshipi, mpate kukhudumiana; kwa sababu Mungu hushindana na wenye kiburi, huwapa wanyenyekevu neema. Bassi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, awakweze kwa wakati wake; mkimtwika yeye taabu zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana katika mambo yenu. Erevukeni, kesheni; kwa kuwa mshitaki wenu Shetani, kama simba angurumae, huzungukazunguka, akitafuta mtu amle; mpingeni, mkiwa imara katika imani, mkijua ya kuwa mateso yaleyale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani. Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu. Uweza una yeye hatta milele na milele. Amin. Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nionavyo, nimewaandikieni kwa maneno machache, nikionya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli va Mungu. Simameni imara katika hiyo. Bibi mteule, mwenzi wenu aliye katika Babeli, awasalimu, na Marko mwanangu. Salimianeni kwa busu la upendo. Amani na iwe kwenu nyote, katika Kristo Yesu. Amin. SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu; kwa kuwa uweza wa Mungu umetukarimia vitu vyote vyenye uzima na utawa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe; kwa hizo tumekarimiwa ahadi kubwa, za thamani, illi kwa hizo mpate kuwa washirika wa sifa za Mungu, mkiokolewa na ubaribifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. Naam, na kwa sababu hiyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenn tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu uvumilivu, na katika uvumilivu wenu utawa, na katika utawa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo. Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo. Maana yeye asiyekuwa na haya ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani. Kwa hivo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara wito wenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuuingia ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo. Kwa hiyo sitakosa kuwakumbusheni hayo siku zote, ijapokuwa mnayajua na kuthubutishwa katika kweli iliyowatikia. Nami naona ni haki, maadam nipo mimi katika maskani hii, kuwaamsheni kwa kuwakumhusheni. Nikijua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionyesha kwa wazi. Walakini nitajitahidi, illi killa wakati baada ya kufariki kwangu mpate kuyakumbuka mambo haya. Maana hatukufuata hadithi zilozotungwa kwa werevu, tulipowajulislia ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa mashahidi wa ukuu wake. Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, ya kama, Huyu ndiye mwanangu nimpendae, amhae nimependezwa nae. Na santi hii ndiyo tuliyoisikia tulipokuwa pamoja uae katika mlima ule mtakatifu. Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ingʼaayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya assubuhi kuzuka mioyoni mwenu. Mkijua neno hili ya kwamba hapana unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fullani tu. Maana unabii haukuletwa zamani kwa mapenzi ya mwana Adamu; hali wana Adamu, watakatifu wa Mungu, walinena, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. LAKINI kuliondoka manabii wa uwongo katika watu, kama vile kwenu kutakavyokuwa waalimu wa uwongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hatta Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu nsiokawia. Na wengi watafuata jeuri zao; kwa hawo njia ya kweli itanenwa unajisi. Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa: hukumu yao tangu zamani haikawii, wala upotevu wao hausinzii. Kwa maana kama vile Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika mafungo ya giza, walindwe hatta ije hukumu; wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa wasiomeha Mungu, akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipiudua ua kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya; akamwokoa Lut, aliyehuzunishwa na mwenendo wa uasharati wa hawo wakhalifu; maaua mtu huyu mwenye haki akikaa kwao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sharia: Bwana ajua kuwaokoa wamchao na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hatta siku ya hukumu; na khassa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu, na kudharau mamlaka. Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu; ijapokuwa malaika, walio wakuu zaidi kwa uwezo na nguvu, hawaleti mashitaka mabaya juu yao mbele ya Bwana. Lakini hawo kama nyama wasio na akili, kwa asili yao watu wa kukamatwa kama nyama na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao; wakipatwa na madhara, ujira wa udhalimu wao, wakidhani kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; ni mawaa na aibu, wakifuata anasa katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi; wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kukhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo ilivozoezwa kutamani, wana wa laana; walioiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaam, mwana wa Bosor, aliyependa ujira wa ndhalimu: lakini alikaripiwa kwa ukhalifu wake mwenyewe; punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia wazimu wa nabii yule. Hawa ni visiwa visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa: wakinena maneno ya kiburi makuu mno, kwa tamaaza mwili na kwa uasharati huwakhadaa watu waliokwisha kuwakimbia wao waishio katika udanganyifu: wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu. Maana mtu akishindwa na mtu, huwa mtumwa wa mtu yule. Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua sana Bwana, Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Maana ingekuwa kheri kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua ile amri takatifu waliyopewa na kuiacha. Lakini lile onyo la ile methali ya kweli limewapata: Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa kujifingirisha matopeni. WAPENZI, waraka huu ndio wa pili niwaandikiao ninyi; katika hizo naziamsha nia zenu sali kwa kuwakumbusheni, mpate kuyakumbuka maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana Mwokozi iliyoletwa na mitume wake. Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, na kusema, iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali hiyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa. Maana hufumba macho yao wasione neno hili, ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na inchi pia, imefanyizwa kwa maji ikatoka katika maji, kwa neno la Mungu; kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. Lakini mbingu za sasa na inchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hatta siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wana Adamn wasiomcha Mungu. Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu kama siku moja. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wahesabuvyo kukawia, bali huvumilia kwenu, hapendi mtu aliye yote apotee, bali wote wafikilie toba. Maana siku ya Bwana itakuja kama mwizi usiku; katika siku biyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na inchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. Bassi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na ntawa, mkitazamia hatta ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka. Lakini, kwa sababu ya ahadi yake tunatazamia mbingu mpya na inchi mpya, ambayo haki itakaa ndani yake. Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia hayo, fanyeni bidii illi muonekane kuwa hamna mawaa au aibu mbele yake, katika amani. Na ubasibuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa wokofu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paolo alivyowaandlkieni kwa hekima aliyopewa; vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa khabari za mambo hayo mumo humo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa upotevu wao wenyewe. Bassi, wapenzi, mkitangulla kujua haya, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hawo wakhalifu, mkaanguka na kuuacha uthubutifu wenu. Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin. ILIYOKUWA tangu mwanzo, tuliyoisikia, tuliyoiona kwa macho yetu, tuliyoitazama, na mikono yetu ikaipapasa, kwa khabari ya Neno la uzima, (na uzima buo ulidhihirika, nasi tumeona, na twashuhudu, na twawakhubirini ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); tuliyoiona na kuisikia, twawakhubiri ninyi; ninyi nanyi mpate kushirikiana na sisi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. Na haya twawaandikieni, illi furaha yenu itimizwe. Na hii ndiyo khabari tuliyoisikia kwake, na kuikhubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza yo yote hamna ndani yake. Tukisema twashirikiana nae, tena tukienenda gizani, twasema uwongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwana wake, yatusafisha dhambi zote. Tukisema hatuna dhambi, twajidanganya, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, yu amini na wa haki atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha udhalimu wote. Tukisema hatukutenda dhambi, twamfanya mwongo wala neno lake halimo mwetu. WATOTO wangu wadogo, nawaandikia haya illi msitende dhambi. Na ijapo mtu akatenda dhambi tuna Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, nae ni kipatanisho kwa dhambi zetu: wala si kwa dhambi zetu tu, bali kwa dhambi za ulimwengu wote. Na hivi twajua ya kuwa tumemjua, ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemae, Nimemjua, nae hazishiki amri zake, ni mwongo, na kweli haimo ndani yake. Lakiui yeye alishikae neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Ilivi twajua ya kuwa tumo ndani yake. Yeye asemae ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vilevile kama yeye alivyoenenda. Ndugu, siwaandikii amri mpya, illa amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Na ile amri ya zamani ndiyo ile mliyosikia tangu mwanzo. Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu, kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kungʼaa. Yeye asemae kwamba yumo katika nuru, nae amchukia ndugu yake, yumo gizani hatta sasa. Yeye ampendae ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo. Bali yeye amchukiae ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho. Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. Nawaandikia, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nawaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba. Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu m hodari, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, na mmemshinda yule mwovu. Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana killa kilichomo duniani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, hazitokani na Baba, bali zatokana ua dunia. Na dunia inapita, na tamaa yake, bali yeye afanyae mapenzi ya Mungu adumu hatta milele. Watoto, ni wakati wa mwisho: na kama vile mlivyosikia kwamba adui wa Kristo yuaja, hatta sasa adui wengi wa Kristo wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. Walitoka kwetu, bali hawukuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka illi wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu. Na ninyi mmepakwa mafuta nae aliye Mtakatifu na mnajua yote. Sikuwaandikia ninyi, kwa sababu hamwijui kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uwongo wo wote utokao katika kweli. Naui aliye mwongo illa yeye akanae ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye adui wa Kristo, amkanae Baba na Mwana. Killa anikanae Mwana, amkana Baba pia. Bassi, na yakae ndani yenu maneno yale mliyoyasikia tangu mwanzo. Neno lile mlilolisikia tangu mwanzo likikaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba. Na hii ndiyo ahadi alivyowaahidia ninyi, uzima wa milele. Nimewaandikia haya katika khabari za watu wale wanaotaka kuwapoteza. Na ninyi, mafuta, yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, nanyi hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama yale mafuta yanavyokufundisheni khabari za mambo yote, tena ni kweli wala si uwongo, na kama yalivyokufundisheni, mnakaa ndani yake. Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, illi, atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibishwe mbele zake katika kuja kwake. Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa killa atendae haki amezaliwa nae. FAHAMUNI, ni pendo la nanma gani alilotupa Baba, kuitwa wana wa Mungu. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. Wapenzi, sasa tu wana wti Mungu, wala haijadhihirika bado tutakidokuwa: lakini twajua ya kuwa akidhihiri, tutafanana nae; kwa maana tutamwona kama alivyo. Na killa mwenye kunitumainia hivi hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu. Killa afanyae dhambi, afanya nasi; kwa kuwa dhambi ni nasi. Na mnajua ya kuwa yeye alidhihiri, illi aziondoe dhambi zetu; na dhambi haimo ndani yake. Killa akaae ndani yake batendi dhambi; killa atendae dhambi bakumwona, wala hakumtambua. Wanangu, mtu asikudanganyeni; afanyae haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; afanyae dhambi yu wa Shetani: kwa kuwa Shetani hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihiri, illi azivunje kazi za Shetani. Killa mtu aliyezaliwa na Mungu hafanyi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kufanya dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Hivi watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Shetani. Mtu aliye yote asiyefanya haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake. Maana hii ndiyo khabari tuliyosikia tangu mwanzo, tupendane sisi kwa sisi; si kama Kain alivyokuwa wa yule Mwovu, akamwua ndugu yake. Nae alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake ya haki. Msistaajabu, ndugu, ulimwengu ukiwachukia. Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mauti hatta uzima, kwa maana twawapenda ndugu. Asiyependa, akaa katika mauti. Killa amchukiae ndugu yake ni mwuaji: nti mnajua ya kuwa mwuaji bana uzima wa milele ukikaa ndani yake. Hivi tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliweka maisha yake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuweka maisha yetu kwa ajili ya ndugu. Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia hii, akamwona ndugu yake yu muhitaji, akamzuilia huruma zake, je! huko ndiko kumpenda Mungu? Watoto, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, biali kwa tendo na kweli. Hivi tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, na mbele zake tutatuliza mioyo yetu katika neno lo lote inalotuhukumu mioyo yetu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu nae anajua yote. Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu; na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake. Na hii ndiyo amri yake, tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana, kama alivyotupa amri. Nae azishikae amri zake hukaa ndani yake, nae ndani yake. Na hivi tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa Roho aliyotupa. WAPENZI, msiamini kiila rolio, bali zijaribuni roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uwongo wengi wametokea duniani. Hivi mwaijua Roho ya Mungu; killa roho iungamayo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Na killa roho isiyoungama kwamba Yesu Kristo amekujii katika mwili, haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya adui wa Kristo ambae mmesikia kwamba yuaja; na sasa amekwisha kuwamo duniani. Ninyi, watoto wangu, mwatokana na Mungu: nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. Hawo ni wa dunia; kwa biyo wanena ya dunia, dunia ikawasikia. Sisi twatokana na Mungu. Yeye anijuae Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Hivi twaijua Roho ya kweli, na roho ya upotevu. Wapenzi, tupendane: kwa kuwa pendo ni la Mungu, na killa apendae amezaliwa na Mungu, nae anamjua Mungu. Asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni pendo. Hivi pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwa kuwa Mungu amempeleka Mwana wake pekee ulimwenguni, tupate uzima kwa yeye. Hili ndilo pendo, si kwamba sisi twalimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akampeleka Mwana wake kuwa kipatanislio kwa dhambi zetu. Wapenzi, ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo limekamilishwa ndani yetu. Hivi tunafahamu ya kuwa tunakaa ndaui yake, nae ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho yake. Na sisi tumeona na kushuhudu ya kuwa Baba amempeleka Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu. Killa aungamae ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, nae ndani ya Mungu. Na sisi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu ndani yetu na kuliamini. Mungu ni pendo, nae akaae katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. Hivi pendo limekamilishwa kwetu, tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu. Katika pendo hamua khofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje khofu, kwa maana khofu ina adhabu; na mwenye khofu hakukamilishwa katika pendo. Sisi twapenda kwa maana yeye kwanza alitupenda sisi. Mtu akisema, Nampenda Mungu, nae anamchukia ndugu yake, yu mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambae amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambae hakumwona. Na amri hii tumepewa nae, ya kwamba yeye ampendae Mungu, ampende na ndugu yake. KILLA mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na killa mtu ampendae mwenye kuzaa ampenda na yeye mwenye kuzaliwa nae. Hivi twajua kwamba twawapencla watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kuzisinka amri zake: na amri zake si nzito. Kwa maana killa kitu kilihozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, imani yetu. Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa yeye aaminiye ya kwamba Yesu yu Mwana wa Mungu? Huyu ndiye ajae kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Na Roho ndiyo ishuhuduyo, kwa sababu Roho ndiyo iliyo kweli. Kwa maana watatu ni mashahidi mbinguni, Baba, Neno, na Robo Mtakatifu, ua watatu hawa ni umoja. Maana watatu ndio washuhuduo duniani, roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupataua kwa khabari moja. Tukiupokea ushuliuda wa wana Adamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, amemshuhudia Mwana wake. Amwaminiye Mwana wa Mungu anao ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini ushuhuda ambao Mungu amemsbuhudia Mwana wake. Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwana wake. Aliye nae Mwana, ana uzima; asiye nae Mwana wa Mungu hana uzima. Nimewaandikia mambo haya, illi mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu. Na huu ndio njasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu kama vile apendavyo, atusikia: Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombapo cho chote, twajua kwamba tunazo zile dua tulizomwomba. Mtu akimwona ndugu yake anakosa kosa lisilo la mauti, ataomba, nae atampa uzima kwa ajili ya hawo wakosao kosa lisilo la mauti. Liko kosa lililo la mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hilo. Killa lisilo la haki ni kosa, na kosa liko lisilo la mauti. Twajua ya kuwa killa mtu aliyezaliwa na Mungu hakosi: bali yeye aliyezaliwa na Mungu ajilinda, na yule mwovu hamgusi. Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu. Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele. Watoto wangu wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu. MZEE kwa bibi mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na ndugu wote waijuao ile kweli; kwa ajili ya ile kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hatta milele. Neema, na rehema, na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana wetu Yesu Kristo zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo. Nalifurahi mno kwa kuwa naliwaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba. Na sasa, Bibi, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane. Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Illi ndiyo ile amri, kama ulivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo. Kwa maana wadanganyifu wengi wameingia katika dunia, wasio-ungama ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na adui wa Kristo. Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu. Killa aendeleae mbele, asidumu katika ma-fundisho ya Kristo, hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho ya Kristo, mtu huyu ana Baba na Mwana pia. Mtu akija kwenu, nae haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu. Maana ampae salamu azishirika kazi zake mbovu. Kwa kuwa nina maneno mengi ya kuwa-andikia, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraja kuja kwenu, na kusema nanyi mdo-mo kwa mdomo, illi furaha yenu itimizwe. Wa-toto wa ndugu yako aliye mteule, wakusalimu. MZEE kwa Gaio mpenzi, nimpendae katika kweli. Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama nendavyo katika kweli. Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli. Mpenzi, kazi ile ni ya naminifu uwatendeayo ndugu na wageni, waliokushuhudia upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha kam a ilivyo wajibu wako kwa Mungu. Kwa maana, kwa ajili ya Jina hilo, walitoka, wasipokee kilu kwa mataifa. Bassi imetupasa sisi kuwakaribisha watu kama hawo, illi tuwe watendaji wa kazi pamoja na kweli. Naliliandikia kanisa, lakini Diotrefe apendae kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali. Kwa hiyo, nikija, nitamkumbusha matendo yake ate-ndayo, akitoa upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, yeye mwenyewe hawakaribishi ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa. Mpenzi, usiuige ubaya, bali wema. Yeye atendae mema ni wa Mungu, bali yeye atendae mabaya hakumwona Mungu. Demetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Na sisi pia twashuhudu, nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli. Nalikuwa na maneno mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalanm. Lakini nataraja kukuona karibu na kusema nawe mdomo kwa mdonm. Amani kwako. Rafiki zetu wakusalimu. Wasalimu rafiki, killa mtu kwa jina lake. YUDA, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu wa Yakobo, kwao waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo baada ya kuitwa; Rehemana amani na upendano muongezewe. Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia khabari ya wokofu wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikieni, illi niwaonye mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu marra moja tu. Kwa maana kuna watu wamejiingiza kwa siri, watu walioandikiwa zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufasiki, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo. Tena napenda kuwakumbusha, ijapo mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, baada ya kuwaokoa watu katika inchi ya Misri, aliwaharibu wasioamini. Na malaika wasioilinda enzi yao, wakayaacha makao yao, amewaweka kwa hukumu ile kuu katika vifungo vya milele chini ya giza. Kama vile bodoma na Gomora, na miji iliyozunguka, waliofuata uasharati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wamepasiwa hukumu yamoto wa milele. Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, hukataa kutawaliwa, hutukana matukufu. Lakini Mikael, malaika mkuu, aliposhindana na Shetani, na kuhujiana nae kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana akukemee. Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyoyajua, na mambo wayatambuayo kwa asili wajiharibu kwayo kama nyama wasio na akili. Ole wao! kwa sababu walikwenda katika njia ya Kain, na kulifuata kosa la Balaam pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora. Watu hawa ni miamba yenye khatari katika karamu zenu za upendo wafanyapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo khofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa marra mbili, na kungʼolewa kabisa; ni mawimbi ya bahari vasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu, ni nyota zipoteazo, ambao giza ndio akiba yao waliowekewa milele. Na Enok, wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hawo, akisema, Angalia, Bwana alikuja na elfu kumi za watakatifu wake, illi afanye hukumu juu ya waiu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote walizoziteuda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hawo wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake. Watu hawa ni wenye kunungʼunika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno ya kiburi makuu mno, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida. Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo, ya kwamba waliwaambia ya kuwa wakati wa mwisho watakuwuko watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe zilizo kinyume cha mapenzi ya Mungu. Watu hawo ndio wajitengao, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho. Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imaui yenu iliyo takatifu, na kuomba katika Roho Mtakatifu, jilindeni katika upendo wa Mungu, mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Krislo, hatta mpate uzima wa milele. Wahurumiane wengine walio na mashaka; bali wengine waokoeni kwa khofu, mkiwanyakua katika moto, mkilichukia hatta vazi lililotiwa takataka na mwili. Kwake Yeye awezae kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu, Yeye aliye Mungu pekee, mwenye hekima, Mwokozi wetu: kwake yeye utukufu, na ukuu, na uwezo, na nguvu kwa Yesu Kristo, tangu milele, na sasa, na hatta milele. Amin. UFUNUO wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo kwamba hayana buddi kuwa upesi: akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumishi wake Yohana; aliyeshuhudia Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo, mambo yote aliyoyaona. Yu kheri asomae, nao wayasikiao maneno ya unabii huu na kuyafanya yaliyoandikwa humo: maana wakati ni karibu. Yohana kwa makanisa saba yaliyo katika Asia: Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwake yeye alioko na aliyekuwako nii atakaekuwako: na zitokazo kwa roho saba zilizo mbele ya kiti chake cha enzi: na zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi alive mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Kwake yeye aliyetupeuda na kutuosha dhambi zetu kwa damu yake, na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, Baba yake: utukufu na ukuu una Yeye hatta milele na milele. Amin. Tazama yuaja na mawingu: na killa jicho litamwona, na hawo waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amin. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisiio, asema Bwana Mungu, alioko, aliyekuwako, na atakaekuwako, Mwenyiezi. Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu. Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu, ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia. Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, nikaona vinara saba vya dhahabu; na kati kati ya vile vinara nikaona mtu kwa mfano wa Mwana Adamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini. Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama thuluji; na macho yake kama mwako wa moto: na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi. Nae alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume: na upanga mkali, mkali kuwili, watoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua likingʼaa kwa nguvu zake. Na nilipomwona nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akiniambia, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. Bassi, yaandike mambo uliyoyaona, nayo yatakayokuwa baada ya hayo. Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhababu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, na vile vinara saba ulivyoviona ni makanisa saba. KWA malaika wa kanisa lililo katika Efeso andika; Haya ayanena yeye azishikae nyota saba katika mkono wake wa kuume, aendae kati kati ya vile vinara saba vya dhahabu. Najua matendo yako, na taabu yako, na uvumilivu wako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa wawongo; tena ulistahimili na kuwa na uvumilivu, na kwa ajili yangu umejitaabisha wala hukuchoka. Lakini nina neno jun yako, kwa sababu umeacha npendo wako wa kwanza. Bassi, kumbuka ulikoanguka, nkatubu, ukayatende matendo ya kwanza. Lakini, usipotenda hivyo, naja kwako upesi, nitaondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. Lakmi unalo neno hili kwamba wayachukia matendo ya Wanikolaiti, niyachukiayo na mimi. Yeye alive na sikio, na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae, nitampa kula matunda ya mti wa uzima ulio kati kati va bustani ya Mungu. Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Smurna andika; Haya ayanena yeye aliye wa kwanza na wa mwisbo, aliyekuwa amekufa, akawa hayi. Najua matendo yako na mateso yako na umaskini wako (lakini u tajiri), na matukano yao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sunagogi la Shetani. Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima. Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Pergamo, andika; Haya ayanena yeye aliye na upanga mkali, mkali kuwili; Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha Shetani: nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hatta katika siku za Antipa shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani. Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaam, yeye aliyemfundisha Balak atie ukwazo mbele ya wana wa Israeli, wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolaiti, niyachukiayo. Tubu; na usipotubu naja kwako upesi, nitafanya vita juu yako kwa upanga wa kinywa changu. Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae nitampa kula baadhi ya ile manna iliyofiehwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina, jina asilolijua mtu illa yeye aliyepewa. Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Thuatera andika, Haya ayanena Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho kama mwako wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana. Najua matendo yako na upendo wako na khuduma yako na uaminifu wako na uvumilivu wako na matendo yako; tena matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza. Lakini nina maneno machache juu yako, ya kwamba wamwacha yule mwanamke Yezebel, yeye ajiitae nabii, nae awafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, illi wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. Nami nimempa muda illi atubu uzinzi wake, nae bataki kutubu. Tazama, nitumtupa juu ya kitanda, na hawo wazinio pamoja nae, wapate mateso makubwa wasipotubu matendo yao; nami nitawaua watoto wake kwa manti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzae viuno na mioyo. Nami nitampa killa mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yenu. Lakini nawaambia ninyi, nao wengine walio katika Thuatera, wo wote wasio na mafundisho haya, wasiozijua fumbo za Shetani kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yen umzigo mwungine. Illa mlicho nacho kishikeni, hatta nitakapokuja. Na yeye ashindae na kuyatunza matendo yangu hatta mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa, nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyangi visetwavyo, kama mimi nilivyopokea kwa Baba yangu. Nami nitampa nyota ya assubuhi. Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. NA kwa malaika wa kanisa lililo katika Sardi, andika; Haya ayanena yeye aliye nazo roho saba za Mungu na zile nyota saba: Najua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hayi, nawe umekufa. Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe manibo yaliyosalia, yaliyo tayari kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu. Bassi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Illakini usipokesha nitakuja kwako kama mwizi, nawe hutaijua saa nitakayokuja kwako. Lakini unayo majina machache, hatta katika Sardi, watu wasioyatia uchafu mavazi yao. Nao watakwenda pamoja nami katika mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili. Yeye ashindae atavikwa mavazi meupe, wala sitalifuta jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitaliungama jina lake mbele za Baba yaugu, na mbele ya malaika zake. Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Filadelfia andika; Haya ayanena yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daud, mwenye kufungua wala hapana afungae, nae afunga wala hapana afuuguae. Najua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, wala hapana awezae kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe ulilitunza neno langu, wala hukulikana jina langu. Tazama, nakupa walio wa sunagogi la Shetani, wasemao kwamba wao ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uwongo. Tazama, nitawafanya waje wasujudu mbele ya miguu yako na kujua ya kuwa nimekupeuda. Kwa kuwa ulilishika neno la uvumilivu wangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya inchi. Tazama, naja upesi. Shika sana ulicho nacho asije mtu akaitwaa taji yako. Yeye ashindae, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, Yerusalemi ulio mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya. Yeye aliye na sikio na asikie neno bili ambalo Roho ayaambia makanisa. Na kwa Kanisa lililo katika Laodikia andika; Haya ayanena yeye aliye Amin, Shahidi aliye mwaminifu, mwanzo wa viumbe vya Mungu. Najua matendo yako, ya kuwa huwi baridi wala hu moto; ingekuwa kheri kama ungekuwa baridi au moto. Bassi, kwa sababu una uvuguvugu, wala huwi baridi wala moto, nitakutema kama mate katika kinywa changu. Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u maskini, na mtu wa kuhurumiwa, na mhitaji, na kipofu, na nchi. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya nchi wako isionekane; na dawa ya macho ya kujipaka macho yako upate kuona, Mimi nawakemea wote niwapendao, na kuwarudi: bassi uwe na bidii, ukatubu. Tazama, nasimama mlangoni, nabisha: mtu akiisikia sauti yangu na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nitakula pamoja nae, na yeye pamoja nami. Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. BAADA ya haya naliona, na tazama mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hatta huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana buddi kuwa baada ya bayo. Na marra nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na juu ya kile kiti ameketi mmoja: na yeye aliyeketi alikuwa mithili ya jiwe la yaspi na sardio, na upinde wa mvua nlikizunguka kiti kile cha enzi, mithili ya zumaridi. Na viti ishirini na vine vilikizuniguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wane, wamekeli, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu. Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na ngurumo na sauti. Na taa saha za moto zikiwaka mbele ya kiti kile cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu. Na mliele ya kile kiti cha enzi, mfano wa bahari ya kioo eheupe, kama krustallo, na kati kati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, nyama wane, wamejaa macho mbele na nyuma. Na nyama wa kwanza alikuwa mfano wa simba, na nyama wa pili mfano wa ndama, na nyama wa tatu mwenye nso kama uso wa Mwana Adamu, na nyama wa nne mfano wa tai arukae. Na hawa nyama wane, wenye uhayi, killa mmoja alikuwa na mabawa sita: pande zote na ndani wamejaa macho, nao hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyiezi, aliyekuwako, nae yuko, nae anakuja. Na hawa nyama wenye uhayi watakapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi yeye aliye hayi hatta milele na milele ntukufu na heshima na shukrani, ndipo hawa wazee ishirini na wane watakapoanguka mbele zake aketiye juu ya kiti cha enzi, nao watamsujudu veye aliye hayi hatta milele na milele, nao watatupa taji zao mbele ya kiti eha enzi, wakisema, Umestahili, Bwana, Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na nweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, vikaumbwa. NIKAONA katika mkono wa kuume wa aliyeketi juu ya kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba. Nikaona malaika mwenye nguvu akikhubiri kwa santi kuu, Nani astahiliye kukifungua kitabu na kuzivunja muhuri zake? Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya inchi, wala chini ya inchi, aliyeweza kukifunua kitabu wala kukitazama. Nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifuugua kitabu na kukisoma, wala kukitazama. Na mmoja wa wale wazee akaniambia, Usilie, tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, shina la Daud, yeye amepata uwezo wa kukifunua kitabu na kuzivunja zile muhuri saba. Nikaona, na tazama, kati kati ya kiti cha enzi na ya nyama wane wenye uhayi, na kati kati ya wale wazee, Mwana Kondoo, amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote. Akaja, akakitwaa kitabu katika mkono wa kuume wake aliyeketi juu ya kiti kile cha enzi. Hatta alipokitwaa kile kitabu, nyama wane wenye uhayi na wale wazee ishirini na wane wakaanguka mbele ya Mwana Kondoo, killa mmoja wao ana kinubi, na vitupa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambavyo ni maombi ya watakatifu. Nao waimba uimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulicbinjwa ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa killa kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu: nao wanamiliki juu ya inchi. Nikaona, nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale nyama wenye uhayi, na za wale wazee, na hesabu yao, elfu kumi marra elfu kumi, na elfu marra elfu, wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana Kondoo aliyechinjwa kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka. Na killa kiumbe kilicho mbinguni na juu ya inchi na chini ya inchi na juu ya bahari, na vitu vyote vilivyo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na una Mwana Kondoo hatta milele na milele. Na wale nyama wane wenye uhayi wakasema, Amin. Na wale wazee ishirini na wane wakaanguka wakamsujudu yeye aliye hayi milele na milele. NIKAONA hapo Mwana Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri, nikasikia mmoja wa wale nyama wenye uhayi akisema, kama sauti ya ngurumo, Njoo! uone. Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana upinde, akapewa taji, akatoka, akishinda na apate kushinda. Na alipofungua muhuri ya pili, nikamsikia nyama wa pili akisema, Njoo uone. Akatoka farasi mwingine mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katikii inchi, watu wauawe, akapewa upanga mkubwa. Na alipoifungua muhuri ya tatu nikamsikia nyama wa tatu mwenye uhayi akisema, Njoo, none. Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia sauti kati kati ya nyama wane wenye uhayi, ikisema, Kibaba cha nganu kwa nussu rupia, na vibaba vitatu vya shairi kwa nussu rupia, wala usiyadhuru mafuta na mvinyo. Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya nyama wa nne akisema, Njoo uone. Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Manti, na Kuzimu akafuatana nae. Wakapewa mamlaka juu ya robo ya inchi wane kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa nyama mwitu wa inchi. Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhbahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakiseina, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hatta lini huhukumu na kuipatia haki damu yetu kwao wakaao juu ya inchi? Wakapewa killa mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hatta itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao watakaouawa vile vile kama wao. Nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, tazama, palikuwa tetemeko kuu la inchi, jua likawa jeusi kama gunia la nywele, mwezi ukawa kama damu, nyota zikaanguka juu ya inchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. Mbingu zikaondolewa kaina ukarasa uliokunjwa, na killa mlima na kisiwa vikahamishwa katika mahali pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu, na matajiri, na majemadari, na wenye nguvu, na killa mtumwa, na mungwana, wakajificha katika pango za chini ya miamba ya milima, wakaiambia milima na miamba, Tuangukieni, katusetirini, tusione uso wake aketiye juu ya kiti cha enzi wala hasira ya Mwana Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yake, imekuja: na nani awezae kusimama? BAADA ya haya nikaona malaika wane wamesimama katika pembe nne za inchi, wakizizuia pepo nne za inchi, upepo usivume juu ya inchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote. Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hayi: akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wane waliopewa kuidhuru inchi na bahari, akisema, Msiidhuru inchi wala bahari wala miti hatta tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mwenyiezi Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao. Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika killa kabila ya wana wa Israeli, watu mia na arubaini na nne elfu. Wa kabila ya Yuda thenashara elfu waliotiwra muhuri. Wa kabila ya Reuben thenashara elfu. Wa kabila ya Gad thenashara elfu. Wa kablia ya Asher thenashara elfu. Wa kabila ya Naftali thenashara elfu. Wa kaliila ya Manasse thenashara elfu. Wa kabila ya Sumeon thenashara elfu. Wa kabila ya Lawi thenashara elfu. Wa kabila ya Issakar thenashara elfu. Wa kabila ya Zabulon thenashara elfu. Wa kabila ya Yusuf thenashara elfu. Wa kabila ya Benyamin thenashara elfu waliotiwa muhuri. Baada ya haya nikaona, na tazama mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezae kuuhesabu, watu wa killa taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kiti kile cha enzi, na mbele za Mwana Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokofu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana Kondoo. Na malaika wote wamesimama pande zote za kiti cha enzi na za wazee na za vile viumbe vine vyenye uhayi, wakaanguka kifudifudi mbele ya kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu, wakisema, Amin: Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu milele na milele. Amin. Akajibu mmoja wa wale wazee akaniambia, Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni nani? na walikotoka wapi? Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hawo ndio wanaotoka katika shidda ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao wakayafanya meupe katika damu ya Mwana Kondoo. Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda khema yake juu yao. Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote. Kwa maana Mwana Kondoo aliye kati kati ya kiti cha enzi atawachunga, nae atawaongoza kwenye chemcheni za inaji yenye uhayi, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao. HATTA alipofungua muhuri ya saba kukawa kimya mbinguni kama muda wa nussu ya saa. Nikawaona malaika saba wasimamao mbele za Mungu, wakapewa baragumu saba. Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhbahu, mwenye cheteso cha dhahabu, akapewa manukato mengi illi ayatie pamoja na sala za watakatifu juu ya madhbahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi. Na moshi wa yale manukato ukapanda pamoja na sala za watakatifu, katika mkono wa malaika, mbele za Mungu. Malaika akakitwaa cheteso akakijaza moto wa madhbahu, akautupa juu ya inchi, kukawa sauti na radi na umeme na tetemeko la inchi. Na wale malaika saba wenye baragumu saba wakajifanya tayari illi wazipige. Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya inchi: thuluth ya miti ikateketea, majani mabichi yote yakateketea. Malaika wa pili akapiga baragumu, na kitu, mfano wa mlima mkubwa uwakao moto, kikatupwa katika bahari, thuluth ya bahari ikawa damu. Wakafa thuluth ya viumbe vilivyo katika bahari, vyenye uhayi: thuluth ya merikebu zikaharibiwa. Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, iliyokuwa ikiwaka kama taa, ikaanguka juu ya thuluth ya mito, na juu ya chemchemi za maji. Na jina lake, ile nyota yaitwa Absintho, thuluth ya maji ikawa absintho, na wana Adamu wengi wakafa kwa maji hayo kwa kuwa yalitiwa uchungu. Malaika wa nne akapiga baragumu, thuluth ya jua ikapigwa, na thuluth ya mwezi, na thuluth ya nyota, illi ile thuluth itiwe giza, mchana usiangaze thuluth yake wala usiku vivyo hivyo. Nikaona, nikasikia tai akiruka kati kati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya inchi, kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu ya malaika watatu, walio tayari kupiga. MALAIKA wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya inchi; akapewa ufunguo wa shimo la abuso. Akalifungua shimo la abuso; moshi ukapanda kutoka lile shimo kama moshi wa tanuru kubwa: juu na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimo. Nzige wakatoka katika lile shimo, wakaenda juu ya inchi, wakapewa nguvu kama nguvu za nge wa inchi. Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya inchi wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, illa wale watu wasio ua muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao. Wakapewa amri wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na kuumwa kwao kulikuwa kama kuumwa na uge, aumapo mwana Adamu. Na katika siku zile wana Adamu watatafuta mauti, nao hawataiona. Na watatamaui kufa, na mauti itawakimbia. Na maumbo ya zile nzige kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao kama nyuso za wana Adamu. Na walikuwa mi nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba. Na walikuwa na mabamba kifuani kama mabamba ya chuma. Na sauti ya mabawa yao kama sauti ya magari ya farasi wengi waendao kassi vitani. Na wana mikia kama ya nge, na palikuwa kama viumo katika mikia yao. Na nguvu yao kuwadhuru wana Adamu miezi mitano. Na juu yao wana mfalme, malaika wa abuso, jina lake kwa Kiebrania Abaddon, na kwa Kiyunani jina lake Apollion. Ole wa kwanza umekwisha pita. Tazama, bado ziko ole mbili, zinakuja baadae. Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka mbele za Mungu, ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue malaika wane waliofungwa kwenye mto mkubwa Eufrati. Wale malaika wane wakafunguliwa, waliowekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka illi waue thuluth ya wana Adamu. Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi elfu ishirini marra elfu kumi; nikasikia hesabu vao. Ndivyo nilivyowaona farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana mabamba kifuani, ya moto, na ya samawati, na ya kiberiti; na vichwa vya farasi hawo kama vichwa vya simba, kukatoka katika vinywa vyao moto na moshi na kiberiti. Thuluth ya wana Adamu wakauawa kwa matatu bayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho kilichotoka katika vinywa vyao. Kwa maana nguvu zao ni katika vinywa vyao; maana mikia vao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, na kwa mikia hiyo wanadhuru. Na wana Adamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia kazi za mikono yao hatta wasiwasujudu mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za mili, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda. Wala hawakutubia mauaji yao, wala uchawi wao, wala uasharati wao, wala kuiba kwao. NIKAONA malaika mwingine hodari akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake: na uso wake kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto. Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunuliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, na wa kushoto juu ya inchi, Akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia ugurumo saba zikatoa sauti zao. Hatta ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Na yule malaika niliyemwona akisimama juu ya bahari na juu ya inchi akainua mkono wake kuelekea mbinguni, akaapa kwa yeye aliye bayi hatta milele na milele, aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na inchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na muhulla baada ya haya, isipokuwa katika siku zile za malaika wa saba, atakapokuwa tayari kupiga: hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowakhubiri watumishi wake manabii. Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena, ikisema, Enenda, kitwae kile kitabu kidogo kilichofunuliwa katika mkono wa yule malaika aliyesimama juu ya bahari na juu ya inchi. Nikamwendea malaika yule nikamwambia, Nipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, Kitwae, ukile, nacho kitakutia uchungu tumboni mwako, bali katika kinywa chako kitakuwa kitamu kama asali. Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali katika kinywa changu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu. Akaniambia, Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi. NIKAPEWA mwanzi kama ufito mmoja, akaniambia, Inuka, ukaipime hekalu ya Mungu, na madhbabu, nao wasujuduo humo. Na behewa iliyo nje ya hekalu uitupe nje wala usiipime, kwa maana mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arubaini na miwili. Nami nitawarukhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na miateen na sittini, wamevikwa mavazi ya kigunia. Hawo ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele ya Mungu wa inchi. Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa. Hawa wana mamlaka kuzifunga mbingu, illi mvua isinye katika siku za unabii wao. Na wana mamlaka juu ya maji kuyagenza kuwa damu, na kuipiga inchi kwa killa pigo, killa watakapo. Hatta watakapoumaliza ushuhuda wao yule nyama atokae katika abuso atafanya vifa nao, nae atawashinda na kuwaua. Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wetu aliposulibiwa. Na watu wa hawo jamaa na kabila na lugha na taifa wataitazama mizoga yao siku tatu u nussu, wala hawataiacha mizoga yao kuwekwa kaburini. Nao wakaao juu ya inchi watafanya furaha juu yao ua kushangilia. Na watapelekeana zawadi kwa kuwa manabii hawo wawili waliwatesa wao wakaao juu ya inchi. Na baada ya siku tatu u nussu roho ya uhayi itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama, khofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama. Nikasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hatta huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama. Na katika saa ile palikuwa na tetemeko la inchi, nalo kubwa, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka, wana Adamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na khofu wakamtukuza Mungu wa mbingu. Ole wa pili umekwisha pita, tazama ole wa tatu anakuja upesi. Malaika wa saha akapiga baragumu, pakawa sauti kuu katika mbingu, zikisema, Falme za dunia zimekwisha kuwa ufalme na Mungu na wa Kristo wake, nae atamiliki hatta milele na milele. Na wale wazee ishirini na wane waketio mbele ya Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifudifudi, wakamsujudu Mungu, wakisema, Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyiezi, ulioko, na nliyekuwako, kwa sababu umetwaa uweza wako ulio mkuu, ukamiliki. Na mataifa walighadhabika, ghadhabu yako ikaja, na wakati wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, nao walichao jina lako, wadogo na wakubwa, na wa kuwaharibu hawo waiharibuo inchi. Hekalu ya Mungu ikafunguliwa mbinguni na sanduku la agano likaonekana ndani ya hekalu yake. Kukawa umeme, na sauti, na radi, na tetemeko, na mvua ya mawe uyingi sana. NA ishara kuu ilionekana mbiuguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota thenashara. Nae alikuwa ana mimba, akilia, akiwa ana utungu na kuumwa katika kuzaa. Ishara nyingine ikaonekana mbinguni; joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. Na mkia wake wakokota thuluth ya nyota za mbinguni na kuziangusha katika inchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, illi azaapo, amle mtoto wake. Akazaa mtoto mwanamume, atakaewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hatta kwa Mungu na kwa kiti cbake cha enzi. Yule mwanamke akakimbilia nyikani ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, illi wamlishe huku siku elfu na miateen na sittini. Kulikuwa na vita mbinguni: Mikael na malaika zake wakipigana na joka, joka akapigana nao pamoja na malaika zake; nao bawakushinda wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae. Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikinena, Sasa kumekuwa wokofu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake: kwa maana ametupwa mshitaki wa ndugu zetu, awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchaua na nsiku. Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; wala hawakupenda maisha yao hatta wakati wa kufa. Kwa hiyo shangilieni, mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa inchi na bahari: kwa maana yule msingiziaji ameshuka kwao mwenye hasira nyingi, akijua ya kuwa ana wakati si mwingi. Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika inchi alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume. Mwanamke yule akapewa mabawa mawili kama ya tai yule mkubwa, illi aruke, aende zake nyikani hatta mahali pake, bapo alishwapo wakati na nyakati na nussu ya wakati, mbali ya nyoka huyo. Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyunia ya mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule. Inchi ikamsaidia mwanamke, inchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake. Joka akamkasirikia mwanamke akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo. NIKASIMAMA juu ya mchanga wa bahari. Nikaona nyama akitoka katika bahari niwenye vichwa saba, na pembe kumi, na juu ya pembe zile vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya ukafiri. Na yule nyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubba, na kinywa chake kama kinywa cha simba; yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimejeruhi jeraha ya mauti. Pigo lake la mauti likaponywa, dunia yote ikastaajabu nyama ya nyama yule. Wakamsujudu yule joka aliyempa nyama uwezo, wakamsujudu yule nyama, wakisema, Nani afananae na nyama? Nani awezae kufanya vita nae? Akapewa kinywa kunena maneno makuu, ya ukafiri. Akapewa uwezo kufanya kazi yake miezi arubaini na miwili. Akafunna kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya killa kabila na lugba na taifa. Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia. Mtu akiwa na sikio na asikie. Mtu akichukua mateka achukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hivyo ndivyo uvumilivu na imani ya watakatifu. Nikaona nyama mwingine akipanda juu kutoka inchi, nae alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana Kondoo, akanena kama joka. Atumia uweza wote wa nyama yule wa kwanza mbele yake, na kuifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie nyama wa kwanza, ambae jeraha yake ya mauti iliponywa. Nae afanya ishara kubwa, hatta afanye moto kushunka kutoka mbinguni juu ya inchi mbele ya wana Adamu. Nae awakosesha wakaao juu ya inchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya nyama, akiwaambia wakaao juu ya inchi kumfanyia sanamu yule nyama aliyekuwa na jeraha ya mauti akaishi. Akapewa kutia pumzi katika sanamu ya nyama, hatta ile sanamu ya nyama inene, na kufanya wo wote wasioisujudu sanamu ya nyama wanawe. Nae awahinya wote, wadogo na wakuu na matajiri na maskini na walio huru na watumwa, watiwe alama katika mkono wao wa kuume au katika vipaji vya nyuso zao: tena kwamba mtu aliye yote asimmne wala kuuza, isipokuwa ana alama ile au jimi la nyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapo udipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya nyama huyo: maana ni hesabu ya mwana Adamu; na hesabu yake ni Sita mia, sittini na sita. NIKAONA, na tazama, Mwana kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arubaini na nne elfu pamoja nae, wenye jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao. Nikasikia sauti kutoka mbinguni kama santi ya maji mengi na kama sauti ya radi kuu. Nikasikia sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao: nao waimba wimbo niliouona kuwa mpya mbele ya kili cha enzi, na mbele ya wale nyama wane wenye uhayi, na wale wazee; na hapana mtu aliyeweza kujifunza uimbo ule illa wale mia na arubaini na nne elfu walionunuliwa katika inchi. Hawa udio wasiotiwa najis pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana kondoo killa aendako. Hawa walinunuliwa katika inchi, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana kondoo. Na katika vinywa vyao haikuonwa bila. Maana hawana mawaa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Nikaona malaika niwingine akiruka kati kati ya mbingu, mwenye injili ya milele, awakhubiri wakaao juu ya inchi na killa taifa na kabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, kamtukuzeni, maana saa ya hukumu yake imekuja. Kamsujuduni yeye aliyezifanya mbingu na inchi na bahari na chemchemi za maji. Malaika mwingine akamfuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya hasira ya uasharati wake. Malaika wa tatu akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu akimsujudu nyama na sanamu yake, na kupokea alama katika kipaji cha uso wake au katika mkono wake, yeye nae atakunywa mvinyo ya hasira ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji katika kikombe cha ghadhabu yake, nae ataumwa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika walakalifu na mbele za Mwana kondoo. Na moshi wa maumivu yao wapanda juu hatta milele na milele, nao bawana raha mchana na usiku, bao wamsujuduo nyama na sanamu yake, na killa aipokeae alama ya jina lake. Hapo ndipo penye uvumilivu wa watakatifu wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu. Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Wa kheri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; na matendo yao yafuatana nao. Nikaona, na tazama, wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa Mwana Adamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa chake, na katika mkono wake mundu mkali. Malaika mwingine akatoka katika hekalu, kwa santi kuu akimlilia yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu wako, ukavune; kwa kuwa saa ya kuvima imekuja; kwa kuwa mavimo ya inchi yamekomaa. Na yeye aliyeketi juu ya wingu akautupa mundu wake juu ya inchi, inchi ikavunwa. Malaika mwingine akatoka katika hekalu iliyo mbinguni, yeye nae ana mundu mkali. Na malaika mwingine akatoka katika ile madhbabu, mwenye mamlaka juu ya moto; kwa sauti kuu akamlilia yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume matawi va mzabibu wa inchi, maana zabibu zake zimewiva sana. Malaika yule akautupa mundu wake hatta inchi, akauchuma mzabibu wa inchi, akatupa katika shinikizo la hasira ya Mungu, lile kubwa. Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka khatamu za farasi, mwendo wa mastadio elfu na sita mia. NIKAONA ishara nyingine katika mbingu, kubwa, ya ajabu, malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo hasira ya Mungu imetimia. Nikaona kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, nao wenye kushinda, na kujiepusha na yule nyama na sanamu yake na alama yake, na hesabu ya jina lake, wamesimama juu ya bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu. Nao wauimba uimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na uimbo wa Mwana kondoo, wakisema, Makuu, ya ajabu, matendo yako, ee Bwana Mungu Mwenyiezi; za haki, za kweli njia zako, ee Mfalme wa watakatifu. Ni nani asiyekucha, Bwana, na kulitukuza jina lako? kwa kuwa wewe peke yako Mtakatifu: kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele yako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa. Na baada ya haya nikaona, na, tazama, hekalu ya khema ya ushuhuda katika mbingu ilifunguliwa; na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakaloka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, kingʼaacho, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu. Na mmoja wa wale nyama wane wenye uliayi akawapa vichupa saba vya dhahabu, vimejaa ghadhabu ya Mungu aliye hayi hatta milele na milele. Hekalu ikajazwa moshi uliotoka kwa utukufu wa Mungu na uweza wake. Na hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu hatta yatakapotimizwa mapigo saba ya wale malaika saba. NIKASIKIA sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vichupa vya ghadhabu ya Mungu juu ya inchi. Akaenda wa kwanza, akakimimina kichupa chake juu ya inchi, pakawa jipu baya, ovu, juu ya wale watu wenye alama ya nyama, na wale wenye kuisujudu sanamu yake. Malaika wa pili akakimimina kichupa chake juu ya bahari, pakawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho va uhayi vikafa katika bahari. Malaika wa tatu akakimimina kichupa chake juu mito, na chemchemi za maji, zikawa damu. Nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, ee Bwana, ulioko, uliyekuwako, mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivu; kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na manabii, nawe umewapa damu, wainywe; nao wamestahili. Nikaisikia madhbahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyiezi, za kweli, za haki hukumu zako. Malaika wa nne akakimimina kichupa chake juu ya jua; likapewa kuwaunguza wana Adamu kwa moto. Wana Adamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo yote, wala hawtikutubu na kumpa utukufu. Malaika wa tano akakimimina kichupa chake juu ya kiti cha enzi cha yule nyama, ufalme wake ukatiwa giza, wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu yao, wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao, wala hawakuyatubia matendo yao. Malaika wa sita akakimimina kichupa chake juu ya mto ule mkubwa Eufrate, maji yake yakakauka illi njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua. Nikaona roho tatu za uchafu kama vyura zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule nyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uwongo. Maana udizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa inchi na wa ulimwengu wofe, kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyiezi. Tazama, naja kama mwizi. Yu kheri akeshae, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi wakaone aibu yake. Akawakusanya hatta maliali paitwapo kwa Kiebrania, Armageddon. Malaika wa saba akakimimina kichupa chake katika hewa. Sauti kuu ikatoka katika hekalu ya mbinguni, kalika kiti kile cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa. Pakawa sauti na radi na umeme, na palikuwa tetemeko la inchi, kubwa, ambalo tangu wana Adamu kuwako juu ya inchi halikuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo. Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ilianguka: na Babeli ule mkuu nkakumbukwa mbele za Mungu, ampe kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake. Killa kisiwa kikakimbia, na milima haikuonekana tena. Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kuloka mbinguni juu ya wana Adamu. Wana Adamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe. Maana pigo lake kubwa mno. AKAJA mmoja wa malaika wale saba wenye vile vichupa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi, ambae wafaime wa inchi walizini nae, nao wakaao katika inchi wakalevywa kwa mvinyo ya uasharati wake. Akanichukua katika Roho hatta jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu va nyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya ukafiri, mwefiye vichwa saba na pembe kumi. Na mwanamke yule alikuwa ameliwa nguo ya porfuro, na nyekuudu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, mwenye kikombe cha dhahabu mkononi mwake kilichojawa na machukizo na machafu ya uasharati wake, Na katiksi kipaji cha uso wake alikuwa na jina, limeandikwa, SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAILABA NA MACHUKIZO YA INCHI. Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu. Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya nyama amehukuae, mwenye vile vichwa saba na zile pemhe kumi. Yule nyama uliyemwona alikuwako, nae hayuko, nae yu tayari kupanda katika abuso na kwenda kwenye uharibifu. Nao wakaao juu ya inchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watataajabu wamwonapo yule nyama, ya kwamba alikuwako, nae hayuko, nae atakuwako. Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke yule. Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Nae atakapokuja imempasa kukaa muda mchache. Na yule nyama aliyekuwako nae hayuko, yeye ndiye wa nane, nae ni mmoja wa wale saba, nae aenenda kwenye uharibifu. Na zile pemlbe kumi ulizoziona ni wafalme, ambao hawajaupokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme kwa saa moja pamoja na yule nyama. Hawa wana shauri amoj, nao wampa yule nyama nguvu zao na mamlaka yao. Hawa watafanya vita na Mwana kondoo, na Mwana kondoo atawashinda, kwa maana ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; nao walioitwa wateule, waaminifu, watashinda pamoja nae. Akaniambia, Yale maji uliyoyaona, aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha. Na zile pembe kumi ulizoziona juu ya nyama, hao watamchukia yule kahaba, na watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kahisa kwa moto. Maana Muugu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule nyama ufalme hatta maneno ya Mungu yatimizwe. Na yule mwanamke uliyemwona, ndiye mji ule mkubwa, mwenye ufalme juu ya wafalme wa inchi. BAADA ya haya nalioua malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu, inchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa nguvu, kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu, umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya killa roho mchafu, na ngome ya killa ndege mchafu mwenye kuchukiza; kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasharati wake, na wafalme wa inchi wamezini nae, na matajiri ya inchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake. Nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hatta mbinguni, na Mungu amekumhuka dhuluma zake. Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mardufu kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikomhe kile alichokichanganisha, mchanganishieni mardufu. Kwa kadiri aliyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri hiyo hiyo. Kwa kuwa alisema moyoni mwake, Nimeketi malkiya, nami si mjane, wala sitaona huzuni kamwe. Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, manti, na huzuni, na njaa, nae atateketezwa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni hodari. Na wafalme wa inchii waliozini nae na kufanya anasa pamoja nae, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuumgua kwake, wakisimama mbali kwa khofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole wake mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio hodari kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja. Na matajiri wa inchi walia na kumwombolezea kwa sababu hapana mtu anunuae bidhaa yake tena, bidhaa ya dhahahu, na fedha, na jito lenye thamani, na lulu, na katani, na porfuro, na hariri, na nguo nyekundu; na killa mti wa uudi, na killa chombo cha pembe, na killa chombo cha mti wa thamani nyingi na cha shaba na cha chuma na cha marimari: na mdalasini, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na nganu, na ngʼombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wana Adamu. Na matunda yaliyotamaniwa na roho yako yamekuondokea; na vitu vyote vilivyo laini na vitu vya fakhari vimekuondokea; wala hulaviona tena kamwe. Na wafanyi biashara ya vitu hivyo, waliopata mali kwsike, watasimama mbali, kwa khofu yii maumivu yako, wakilia na kuomboleza, wakisema, Ole, ole wake mji ule mkuu uliovikwa katani, na porfuro, na nguo nyekundu, na kupambwa kwa dhahabu na kito cha thamani na lulu; kwa kuwa katika saa moja utajiri mwingi namna hii umekuwa ukiwa. Na killa mshika msukani na killa aendae mahali kwa matanga, mi baharia, nao wote watendao kazi baharini wakasimama mbali, wakalia sana, walipouona moshi wa kuungua kwake, wakisema, Ni mji upi ulio mfano wa mji huu mkubwa! Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitoka machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole wake mji ule ulio mkuu, ambao ndani yake wote wenye merikebu katika bahari walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa. Furahini juu yake, enyi mbingu, na ninyi watakatifu na mitume na manabii, kwa maana Mungu amehukumu hukumu yenu juu yake. Na malaika mmoja hodari akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Hivi kwa nguvu nyingi utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana kabisa. Wala sauti ya wapiga vinanda na ya wapiga mazumari na ya wapiga filimbi na ya wapiga baragumu haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wala fundi aliye yote wa kazi iliyo yote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa, wala sauti ya bwana arusi na bibi arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana wafanyi biashara wako walikuwa wakuu wa inchi, kwa kuwa mataifa yote wamedanganywa kwa uchawi wako. Na ndani yake ilionekana damu ya manabii na ya watakatifu na ya wale wote waliouawa juu ya inchi. BAADA ya baya nikasikia sauti ya makutano mengi, sauti kubwa katika mbingu, ikisema, Halleluya; Wokofu na utukufu na nguvu zina Bwana Mungu wetu; kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki: maana amemhukumu yule kahabu mkuu aliyeiharibu inchi kwa uasharati wake, na kumpatiliza kwa ajili va damu ya watumwa wake mkononi mwake. Wakasema marra ya pili, Halleluya. Na moshi wake hupaa juu hatta milele na milele, Na wale wazee ishirini na wane, na wale nyama wane wenye uhayi wakasujudu na kumwabudu Mungu aketiye katika kiti cha enzi, wakisema, Amin, Halleluya. Sauti ikatoka katika kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumishi wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo na wakuu. Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Halleluya; kwa kuwa Bwana Mungu Mwenyiezi amemiliki. Na tufurahi tukashangilie tukampe ulukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Nae alipewa kuvikwa kwa katani safi, ya fakhari, kwa maana katani hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. Akaniambia, Andika, Wa kheri walioitwa kwa karamu ya arusi ya Mwana Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu. Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii. Nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama farasi mweupe, nae aliyempanda, aitwae Mwaminifu na wa kweli, nae kwa haki ahukumu na kufanya vita. Na macho yake yalikuwa kama mwako wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi, nae ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu illa yeye mwenyewe. Nae amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na, jina lake, aitwa, Neno la Mungu. Na majeslii yaliyo mbinguni yakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa katani safi, nyeupe. Na upanga mkali hutoka kinywani mwake awapige mataifa kwa huo. Nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, nae anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ukali wa ghadhabu ya Mungu Mwenyiezi. Nae ana jina limeandikwa katika vazi lake mi paja vake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA. Nikaona malaika mmoja amesimama katika jua, akilia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao kati kati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu, mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya maakida, na nyama ya watu hodari na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana na watumwa, wadogo na wakubwa. Nikamwonu nyama, na wafalme wa inchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, na na majeshi yake. Yule nyama akakamatwa, na nabii wa uwongo aliye pamoja nae, yeye aliyezifanya ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile alama ya nyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa hayi katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya farasi yule, utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao. NIKAONA malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa abuso, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika joka, yule nyoka wa zamani, aliye msingiziaji, Shetani, akamfunga miaka elfu, akamtupa katika abuso, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hatta ile miaka elfu itimie; na baada ya haya imepasa afunguliwe muaa mchache. Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu. Na wafu waliosalia hawakuwa hayi, hatta ikatimia ile miaka elfu. Huo ndio ufufuo wa kwanza. Yu kheri, mtakatifu, aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watamiliki pamoja nae miaka elfu. Na ile miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa atoke kifungoni mwake: nae atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za inchi, Gog na Magog, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. Wakapanda juu ya upana wa inchi, wakazinga kituo chta watakatifu, na mji uliopendwa. Moto ukashuka katika mbingu kutoka kwa Mungu, ukawala. Na yule Msingiziaji, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule nyama na yule nabii wa nwongo. Na wataumwa mchana na usiku hatta milele na milele. Nikaona kiti eba enzi, cheupe, kikubwa, nae aketiye juu yake; inchi na mbingu zikakimbia nso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa na wadogo, wamesimama mbele za Mungu; vitabu vikafunuliwa. Kitabu kingine kikafunuliwa, kilicho eha uzima, wafu wakahukumiwa kwa mambo ya matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliomo ndani yake. Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu walio ndani yake. Wakahukumiwa killa mtu kwa kadiri ya matendo yao. Mauti na Kuzimu wakatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili. Na ikiwa mtu hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. NIKAONA mbingu mpya na inchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na inchi za kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. Nami Yohana nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemi mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wana Adamu, nae atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, Mungu wao. Nae atafuta killa chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena: wala maombolezo, wala kilio, wala taabu haitakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Na yeye aketiye juu ya kiti cha enzi akasema, Tazama, nafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika, kwa maana haya ni maneno ya kweli, na ya uaminifu. Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa mwenye kin maji ya chemchemi ya maji ya uzima, burre. Yeye ashindae atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, nae atakuwa Mwana wangu. Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili. Akaja mmoja wa wale malaika saba walio na vichupa vile saba vijaavyo yale mapigo saba ya mwisho, akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi arusi, mke wa Mwana kondoo. Akanichukua katika Roho hatta mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemi, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyiezi Mungu, wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi safi, kama bilauri: ulikuwa ua ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango thenashara, na katika ile milango malaika thenashara, na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila thenashara za wana wa Israeli. Upande wa mashariki milango mitatu: na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu: na upande wa magharibi milango mitatu. Na ukuta wa mji una misingi thenashara, na katika ile misingi majina theriashara ya mitume wa Mwana kondoo. Na yeye aliyenena nami alikuwa na mwanzi wa dhababu apate kuupima mji na milango yake na ukuta wake. Na ule mji ni wa mrabba, na marefu yake sawa sawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi, hatta stadio thenashara elfu. Marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake mamoja. Akaupima ukuta wake, ni dhiraa misi na arubaini na nne, kwa kipimo cha mwana Adamu, maana yake, cha malaika, Na majenzi ya nle ukuta ya yaspi, na mji ule dhahabu safi, mfano wa kioo safi. Na misingi ya ukuta wa mji imepambwa kwa killa jito la thamani. Msingi wa kwanza yaspi; wa pili sapfiro; wa tatu kalkedo; wa nne smaragdo; wa tano surdonuksi; wa sita sardio; wa saba krusolitho; wa nane berullo; wa tissa topazio; wa kumi, krusopraso; wa edashara huakintho; wa thenashara amathusto. Na milango thenashara, lulu thenashara: killa mlango ni lulu moja. Na njia ya mji dhahabu safi kama kioo kisichoizuia nuru. Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyiezi ni hekalu lake, na Mwana kondoo. Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi uuangaze, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana kondoo. Na mataifa wa hao wanaookolewa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa inchi wataleta utukufu wao na heshima yao ndani yake. Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku. Na wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake. Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyae machukizo na uwongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo. AKANIONYESHA mto wa maji ya uzima, wenye kungʼaa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana kondoo. Kati ya njia kuu yake na ule mto, upande huu na upande huu, mti wa uzima, uzaao matunda thenashara, mwenye kutoa matunda yake killa mwezi, na majani ya mti huo ya kuwaponya mataifa. Wala hapatakuwa laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana kondoo kitakuwa ndani yake. Na watumishi wake watamtumikia; nao watamwona uso wake, na jina lake katika vipaji vya nyuso zao. Wala hapatakuwa usiku huko; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu awatia nuru, nao watamiliki milele hatta milele. Akaniambia, Haya ni maneno ya uaminifu na ya kweli. Na Bwana Mungu wa manabii watakatifu alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumishi wake mambo ambayo hayana buddi kuwa upesi. Tazama, naja upesi; yu kheri yeye ayashikae maneno ya unabii wa kitabu hiki. Na mimi Yohana ndimi niliye mwenye kuona haya na kuyasikia. Na niliposikia na kuyaona nalianguka nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha haya. Akaniambia, Angalia, usifanye hivyo; mimi mjoli wako, na wa ndugu zako manabii na wa wale washikao maneno ya kitabu hiki. Msujuduni Mungu. Akaniambia, Msiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia. Mwenye kudhulumu na atende dhuluma tena; na mwenye uchafu na awe mchafu tena, na mwenye haki na afanye haki tena, na mtakatifu na atakaswe tena. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami kumlipa killa mtu kama itakavyokuwa kazi yake. Mimi Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Wa kheri wazifuazo nguo zao, wawe na amri kuuendea mti wa uzima, na kuuingia mji kwa milango yake. Bali nje wako mbwa na wachawi na wazinzi na wauaji nao waabuduo sanamu, na killa mtu apendae uwongo na kuufanya. Mimi Yesu nalimtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daud, ile nyota yenye kungʼaa ya assubuhi. Na Roho na Bibi arusi wasema, Njoo. Nae asikiae aseme, Njoo. Nae aliye na kiu, na aje: na apendae ayatwae maji ya uzima burre. Namshuhudia killa mtu ayasikiae maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu aliye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu aliye yote akiondoa baadhi ya maaeno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika kile kitabu cha uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao khabari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; Naja upesi. Amin: na uje Bwana Yesu. Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. Amin.